Sunday, April 15, 2012

BREAKING NEWS - KATAVI ya TANZANIA

TTCL WON A 6.7 US DOLLARS CONTRACT TO SUPPLY 1.244 GIGABYTES OF INTERNET BANDWIDTH TO RWANDA FOR 10 YEARS

Kwsho tutawaletea changamoto za TTCL hapa mjini Mpanda  



TTCL’s CEO Mr. Said Amir Said (left) and the Head of Information and Communication Technology department at the Rwanda Development Board (RDB) Patrick Nyirishema signing the contract.
TTCL’s Chief Marketing and Sales Officer Mr. Ernest Nangi (Left), TTCL’s Company Secretary Mrs. Gilder Kibola and Head Products Development Mr. Ernest Isaya.
TTCL’s Chief Executive Officer Mr. Said Amir Said speaking with Journalist in Rwanda after signings business Contract.

MASHIMO HAYA KWELI HALMASHAURI WAPO????

AFISA MAZINGIRA AMEUGUA TANGU LINI????? 







APRIL 18, 2012


MWANAHABARI SYROSE BHANJI AULA UBUNGE BUNGE LA AFRIKA MASHARIKI

Shy-Rose Bhanji
Mwandishi wa habari mwandamizi wa siku nyingi, Shyrose Bhanji amekuwa miongoni mwa wagombea ubunge wa Bunge la Afrika Mashariki ambao waliibuka kidedea katika uchaguzi uliofanyika jana mjini Dodoma.

Katika uchaguzi huo wagombea tisa kati ya 32 waliowania nafasi hiyo, walifamikiwa kuibuka kidedea na kupata tiketi ya kuwakilisha Tanzania katika bunge hilo.


Wagombea walioshinda nafasi kwa wanaume Tanzania Bara na idadi ya kura kwenye mabano ni Adam Kimbisa (210), Benard Murunya (135) na Makongoro Nyerere (123), na walioanguka ni Lifa Chipaka (8), William Melecela (42), Dk. Evans Rweikiza.


Upande wa wanawake, walioshinda ni Angela Kizigha (166), Shyrose Bhanji (120), ambao ndiyo watakaiwakilisha Tanzania katika Bunge la Afrika Mashariki, na walioshindwa ni Janeth Mbene, Fancy Nkuhi, Janeth Mmari na Dk. Godbertha Kinyondo.

Kundi la wagombea kutoka Zanzibar, walioshinda ni Abdalah Ali Mwinyi (237), Maria Yahya Ussi (91). Walioanguka ni Ahmada Hamad Khatib, Dk. Haji Mwita Haji, Khamis Jabir Makame, Dk. Said Gharib Bilal na Zubeir Ali Maulid.

Kwa upande wa kundi la upinzani, walioshinda ni Nderakindo Kessy (NCCR-Mageuzi) na Twaha Issa Taslima (CUF). Mgombea wa CHADEMA Antony Komu aliangushwa vibaya kwenye kinyang’anyiro hicho. Wengine walioshindwa ni Dk. Fortunatus Masha (UDP), Anthony Komu (CHADEMA), Juju Danda (NCCR-MAGEUZI), Michael Mrindoko (TLP), Mwaiseje Polisya (NCCR-MAGEUZI).

Wabunge wa CHADEMA ambao awali walitangaza kususia uchaguzi huo, walishiriki ikiwa ni pamoja na kusimamisha mgombea wake Anton Komu, ambaye alibwagwa vibaya.

Akizungumza na waandishi wa habari juzi, Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bunge, Freeman Mbowe, alisema hawatashiriki uchaguzi kwa madai ya kutokuwa huru na haki.


Mbowe, ambaye ni Mwenyekiti wa Taifa wa CHADEMA, alisema wabunge wa chama hicho watatoka nje na hawatakuwa tayari kuwasikiliza wagombea wala kupiga kura na kwamba CHADEMA kushiriki uchaguzi huo ni kutowatendea haki Watanzania, lakini katika hali ya kushangaza wabunge hao wakiongozwa na Mbowe walishiriki uchaguzi huo na hawakutoka ukumbini.

Awali, CHADEMA lilitaka kupewa nafasi moja kwa ajili ya chama hicho pekee badala ya kushindaniwa na wapinzani wote kama kanuni inavyoelekeza.

‘Sisi kama Chadema hatutashiriki katika uchaguzi huo wala hatutashiriki kupiga kura wala kusikiliza tutatoka nje tuache waendelee,’ alisema.

Hata hivyo, Naibu Spika Job Ndugai, alisema hoja hiyo ya CHADEMA haina msingi na kwamba, nafasi mbili walizopewa wapinzani zitahusisha vyama vyote vya upinzani.
Awali, wagombea waliingia katika nafasi hiyo ni Bernard Murunya, Adam Kimbisa, Makongoro Nyerere, Mrisho Gambo, Siraju Kaboyonga, William Malecela, Dk. Evans Rweikiza, Elibariki Kingu na Dk. Edmund Mndolwa wote kutoka Chama Cha Mapinduzi (CCM). Pia, yumo John Lifa-Chipaka wa TADEA.
Kwa upande wa wanawake mchuano kuwania nafasi hiyo ulikuwa kwa Engela Kizigha, Fancy Nkuhi, Dk. Godbertha Kinyondo, Janet Mmari, Janeth Mbene, Mariam Ussi Yahya na Sebtuu Mohamed Nassor, Shyrose Bhanji, Sofia Ali Rijaal wote kutoka CCM wakati mgombea kutoka upinzani ni Rose Mwalusamba (CUF).
Waliowania nafasi ya kuwakilisha Zanzibar katika Bunge la Afrika Mashariki walikuwa ni Abdullah Ali Hassan Mwinyi, Dk. Ahmada Hamad Khatib, Dk. Haji Mwita Haji, Khamis Jabir Makame, Dk. Said Gharib Bilal na Zubeir Ali Maulid wote kutoka CCM.


Kwa upande wa wagombea wa vyama vya upinzani, walikuwemo Dk. Fortunatus Masha (UDP), Anthony Komu (CHADEMA), Juju Danda (NCCR-MAGEUZI), Micah Mrindoko (TLP), Mwaiseje Polisya (NCCR-MAGEUZI), Nderakindo Kessy na Twaha Issa Taslima (CUF).
Adamu Kimbisa

Angela Kizigha

Makongoro Nyerere(picha na habari kwa hisani Nkoromo Daily Blog)

 NG'OMBE WANAVOIVAMIA KATAVI KWA SPEED

SASA BASI - RC KATAVI

 PICHA JUU: Lori lenye namba T847ANJ na Teller lake lenye namba T122AHH likiwa na ng'ombe katika kituo cha polisi Mpanda baada ya kukamatwa Aprili 16, 2012.

Mawaziri wamjibu Mbowe

Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman
 Mbowe, akizungumza na Waziri Mkuu aliyejiuzulu, Edward Lowassa, wakati 
wa kumbukumbu ya hayati Edward Moringe Sokoine, nje ya Kigango cha 
Sokoine, Parokia ya Dakawa mjini Morogoro juzi. Picha na Merina Robert.
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe, akizungumza na Waziri Mkuu aliyejiuzulu, Edward Lowassa, wakati wa kumbukumbu ya hayati Edward Moringe Sokoine, nje ya Kigango cha Sokoine, Parokia ya Dakawa mjini Morogoro juzi. Picha na Merina Robert.
Dk. Nagu, Ole Medeye wamtaka atoe ushahidi Magufuli ataka akamuulize Waziri Mkuu SIKU moja baada ya Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe, kumwambia Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, kwamba baadhi ya mawaziri wanawatisha wananchi ili wasiwachague wagombea wa upinzani, mawaziri hao wameamua kujibu mapigo. Wakizungumza kwa nyakati tofauti mjini hapa jana, mawaziri hao wameonyesha kutoridhishwa na kauli ya Mbowe, kwa kuwa hakuna ushahidi dhidi ya maneno yaliyosemwa. Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Uwekezaji na Uwezeshaji, Dk. Mary Nagu, alisema hakumbuki alichozungumza wakati wa kampeni za uchaguzi mdogo wa Jimbo la Arumeru Mashariki, uliomalizika hivi karibuni. “Sikumbuki kama alichosema Mbowe ni sahihi, kwa sababu kule tulikuwa kwenye kampeni, kila mmoja alikuwa akitumia silaha zake. “Katika kipindi cha miaka 10 ambayo nilikuwa Mbunge wa Viti Maalum, Mkoa wa Arusha, Jimbo la Arumeru Mashariki lilikuwa kwenye himaya yangu, ndiyo maana nilikwenda kupiga kampeni kukisaidia chama changu. “Pamoja na hayo, Mbowe wakati mwingine aachane na maneno ya kwenye kampeni kwa sababu katika kipindi hicho kunakuwa na mambo mengi sana na kama mtu ukitaka kufuata mambo ya kampeni unaweza kusababisha mambo mengine yasiyofaa,” alisema Dk. Nagu. Wakati Dk. Nagu akisema hayo, Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Goodluck ole Medeye, ambaye ni mmoja wa walioshutumiwa na Mbowe, alisema hakumbuki na wala hajui kama alisema maneno hayo. Kutokana na hali hiyo, alimtaka Mbowe awasilishe bungeni ushahidi wa alichokisema ili kuondoa utata. “Hilo suala silikumbuki kwa sababu ninachojua hayo mambo yaliripotiwa na magazeti tu. Lakini kama Mbowe ana uhakika na anachokisema, alete bungeni mikanda ya mikutano hiyo, ikiwa ni pamoja na ya upande wake ili ukweli ujulikane,” alisema ole Medeye. Kwa mujibu wa Naibu Waziri huyo, yeye binafsi amekuwa akifanya kazi bila upendeleo, ikiwa ni pamoja na kutembelea majimbo yote, yakiwamo yanayoongozwa na vyama vya upinzani. Waziri wa Ujenzi, Dk. John Magufuli, aling’aka na kukataa kuzungumzia tuhuma hizo. Badala yake alitaka akaulizwe Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, kwa vile ndiye aliyeulizwa na Mbowe. Juzi wakati wa kipindi cha maswali ya papo kwa papo kwa Waziri Mkuu, Mbowe aliwashitaki mawaziri hao, kwamba wanawatisha wananchi ili wasichague wapinzani. Akizungumza wakati akiuliza swali lake, Mbowe alisema, Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza nitoe pole kwa misiba iliyolipata taifa kwa siku za hivi karibuni. “Kwa muda mrefu kumekuwapo na matamko ya viongozi wa Serikali na wakati mwingine matamko ya viongozi wa CCM kwa wananchi, kwamba maeneo yatakayochagua wapinzani hayatapelekewa fedha za maendeleo na Serikali. “Sasa tunaomba utuambie kama suala hili lipo, ili tuweze kujua ukweli halisi,” alihoji Mbowe. Akijibu swali hilo, Waziri Mkuu alisema suala hilo halipo kwa kuwa Serikali imekuwa ikipeleka fedha za maendeleo katika maeneo yote bila kujali yanaongozwa na chama gani cha upinzani. “Mheshimiwa Naibu Spika, swali hili limeulizwa kwa ujumla sana ingawa muulizaji anajua siyo kweli. Hakuna mahali popote ambapo tumeshindwa kupeleka fedha za maendeleo kwa sababu yanaongozwa na Chadema, CUF au chama chochote. “Kwa maana hiyo, naomba Watanzania tuendelee kutimiza demokrasia, kama kuna kauli zingine katika chaguzi, hizo zinatoka kwa bahati mbaya, sisi tutaendelea kutii sheria na kanuni za kazi,” alisema Waziri Mkuu. Pamoja na kutoa majibu hayo, Mbowe alisimama tena na kuuliza swali la nyongeza, huku akisema ushahidi wa kauli za vitisho za mawaziri hao anazo na kutoa mfano kwa baadhi ya chaguzi zilikotolewa. “Mheshimiwa Waziri Mkuu, pamoja na masikitiko yako, kauli hizo zipo na zimekuwa zikitolewa mara kwa mara na baadhi ya mawaziri. “Kwa mfano, hivi karibuni Waziri Nagu (Mary Nagu, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Uwekezaji na Uwezeshaji), alitoa kauli hizo wakati wa kampeni za uchaguzi mdogo Jimbo la Arumeru Mashariki, mwingine ni Waziri Magufuli (John Magufuli, Waziri wa Ujenzi) alitoa kauli kama hizo wakati wa kampeni za uchaguzi mdogo kule Igunga. “Mwingine ni Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi (Goodluck ole Medeye) ambaye alitoa kauli hiyo kule Arusha,” alisema Mbowe.

JAMBO UNALOWEZA KULISHANGAA

APRIL 15, 2012 SUNDAY
VIGOGO WAASISI WA FREEMASONS NCHINI TANZANIA NA KUENEA KWA U FREEMASONS KATIKA UKANDA WA AFRIKA MASHARIKI...2
Januari 2005 nchini Isarel ‘walipata’ kiongozi mpya wa Freemasons, Chaim Henry Gehl, ambapo sherehe yao ilifanywa katika Hoteli ya Sheraton iliyopo Herzlia. 
Wageni walitokana Uingereza, Ujerumani,Uholanzi, Austria, Luxemborg,Romania,Italia,Bulgaria na China. Kiongozi huyo alikuwa akikabidhiwa madaraka kutoka kwa Sami Raphaeli, mhasibu mstaafu wa benki mstaafu wa hekalu la Caspi lenye namba 56 lililopo mjini Haifa. Huyu cheo chake cha utendaji mkubwa katika freemasons ni 33rd degree alichotunukiwa mwaka 2003. Naam katika kuselebuka huko ndipo wakajigamba kwamba mnamo Oktoba 9, 2004 kulifanywa sherehe ya kutimiza miaka 100 ya Freemasons katika eneo la afrika mashariki. 
 Hapa kwetu Tanzania haikusemwa sana, ingawaje Jayantilal Kashavji Chande , au Sir Andy Chande katika mahojiano yake na mwandishi wa Ernest C. Ambali(The Guardian, Oktoba 8, 2004) haikuelezwa mahali patakapofanyiwa sherehe hizo. Katika mahojiano yale Sir Andy Chande alieleza kuwa mgeni rasmi alikuwa Rais Benjamini Mkapa na mkewe Mama Anna Mkapa. Pia kulikuwapo na wafanyabiashara wakubwa,wanadiplomasia,mawaziri n.k 
Sir Andy Chande akiwa nchini India katika mji wa Chennai kuzindia hekalu lao East Star alieleza  kwamba ‘marais wawili wa kwanza wa Tanzania (hawakuwa freemasons) lakini walifahamu ni nini’. Je unahitaji akili gani kuwatambua marais wako? Unahitaji Mungu akuongezee ubongo gani ili utambue kuwa ni akina nani wanaozungumziwa? Ndiyo maana nasema tatizo siyo kasi uliyonayo bali kule uendako!
Tukubaliane, kuwa kwa kiasi Fulani inajionyesha ikulu zetu zimezingirwa na Freemasons. Na katika mahojiano hayo hakusemwi ni Dar es Salaam eneo gani ambao sherehe hiyo ilifanywa, lakini katika kumsimika Chaim Henry Gehl (kule Israel)ilitajwa Hoteli ya Royal Palm ambapo wageni 350 walihudhuria.
 Katika miaka hii 100(108) ikaelezwa kuwa Freemasons walianza kujenga hekalu lao la kwanza la Harmony namba 3084 mwaka 1904 mjini Zanzibar. Katika uzinduzi wa jengo hilo Zanzibar inaelezwa Rais Theodore Roosecelt alikuwapo, Duke of York(ambaye baadaye alikuja kufahamika kama Mfalme George VI)na Duke of Connaugh na Strathean walikuwepo pia. 
Ukimsoma mwanahistoria Robert Muchembled(katika; A History of the Devil) ameorodhesha majina yenye kuabudiwa kwa ibada za kishetani lakini tunayathamini na kupofushwa nayo. Nami kwa matendo wanayoyatenda hapa duniani sina soni kusimamia hoja yangu kuwa ni ubatili mtupu waufanyao).
Naweka orodha ya mambo wanayojigamba Freemasons kujinasibu kwa miaka yao 100(108) ndani ya afrika mashariki huku wakibainisha kuwa makao makuu ya eneo zima ni barabara ya Nyerere, jijini Nairobi(soma;The Guardian, 0ktoba 8, 2004). Katika mahojiano hayo ndipo kukaorodheshwa ‘misaada’(ibilisi?), eti Kindwitwi Leprosy Centre(Utete), Mama Theresa Home for the children, shule ya vipofu(Pongwe, jijini Tanga), na Leprosy Projects (jijini Arusha). Montessori School (jijini Mwanza), Mnazi Mmoja Hospitali (iliyopo Zanzibar), Missionaries of Charity, shule ya walemavu (Buguruni, jijini Dar es salaam), wamejenga madarasa shule ya msingi Kinondoni(Dar es salaam) na kutoa pauni za Uingereza 15,000 mnamo mwaka 1996 katika ajali ya Mv Bukoba. Ukiangalia ‘misaada’ yao unapumbazika kuwa ni hisani ya hali juu Na tatizo kubwa linalotukabili, ni utegemezi ambao huzaa utumwa na kukengeuka akili zetu. Tunaishi huru mitaani lakini tupo gerezani, tunakwenda kasi sana lakini hatuangalii tunakokwenda, hatutaki kujua nini hiki tunachosaidiwa? Ni mungu gani aliruhusu mashoga na wasagaji wasimame madhabauni/altareni? Naam ndivyo tunavyouvaa uovu, ndivyo yanakotakiwa Uganda Museven aliruhusu hali hiyo. Na wenyewe husingizia haki za kiraia au dini za kiraia, inaeleweka kuwa Marekani imejngwa na Freemasons kwani wanajieleza kwa mengi tu. Je nasi tuwe na akina Jack Straw wetu bungeni? Tuvuje jasho kwa kupitisha sheria za kuruhusu mashoga, wasagaji halafu tuseme mungu anaruhusu hayo?
VIGOGO  WA FREEMASONS  KATIKA  UKANDA  WA AFRIKA MASHARIKI  NA AFRIKA  KWA UJUMLA
Sir.Andy chande ajitokeza na kusema kuwa yeye ni mmoja wa freemason afrika mashariki .Pia hakuwa nyuma kuwataja viongozi wanaohusika kwenye chama hicho akiwemo rais mstaafu wa awamu ya tatu Mh.Benjamin Mkapa .
Pia alimtaja steven kanumba, msanii nguli hapa Tanzania,Baba Riz raisi wa Tz,lowassa,AY,Mr. Blue,na wengineo wengi. Pia hakusita kumtaja yoweri museveni raisi wa uganda,Obama raisi wa marekani,George Bush,Bill Clinton,George washington,Elizabeth malkia wa uingereza na wengineo wengi.
 Sir.Andy Chande alitaja yeye kwenye chama hicho ni Grand District Master akiwa amebobea kwa miaka 18 iliyopita. 
Alipoulizwa makao yao makuu hapa Tanzania yapo wapi alijibu bila kusita "we are located at sokoine Drive behind kilimanjaro hotel here in Dar es salaam" (tunapatikana barabara ya sokoine nyuma ya hoteli ya kilimanjaro). 
Pia Sir. Andy alisema wananyaraka zote za kumiliki jengo hilo toka serikalini. Aliongezea kuwa vikao vyao hufanyika kwa siri nyakati za usiku na mtu akishaingia kwenye chama hiko hatotoka tena
HUU NI MUHTASARI TU TULIOFANIKIWA KUUPATA KUTOKA KWA MPEKUZI BLOGER KAMA ALIVYONUKUU KIPINDI CHA RADIO YA CLOUDS FM CHA NJIA PANDA MACHI 11, 2012 .
BLOGER
UNAIKUMBUKA HABARI HII???

Edward Lowasa, atabiriwa na TB Joshua?

Pichani Lowasa akiwa kanisani kwa TB Joshua kama anavyoonekana kwenye Emmanuel TV, 12 June 2011
MBINU za Edward Lowassa kutaka kurejea kileleni katika ulingo wa kisiasa zimemnasa mbunge wa Kilindi (CCM), Beatrice Shelukindo, imefahamika.
Beatrice ambaye alikuwa akijitambulisha kuwa mmoja wa “wapambanaji dhidi ya ufisadi,” waliopachikwa jina la “Mitume kumi na miwili,” sasa anatajwa kuhamia rasmi mtandao wa Lowassa.
Gazeti hili limepata ushahidi wa maandishi ya mkono wa Beatrice mwenyewe yanayoonyesha kuwa amekuwa mfuasi muhimu wa Lowassa kiasi cha kushawishi wengine kujiunga katika mtandao wake.
Akiandika kwa Pindi Chana, mbunge wa Viti Maalum (CCM), tarehe 14 Februari mwaka huu, Beatrice alieleza mambo matatu katika ujumbe wake kwa Chana.
Kwanza, kumshukuru Chana kwa kukubali kulinda kura zake. Pili,  kumshawishi kumuunga mkono Lowassa. Tatu, kumweleza juu ya ulokole wake na “mtumishi aliyepakwa mafuta” kutoka Nigeria.
Beatrice anamwambia Chana kuwa Lowassa ndiye kampeni meneja wake. Hii ilikuwa katika uchaguzi wa makamishina wa Bunge; nafasi aliyogombea na kushinda.
“Mungu ni wa ajabu, (Lowassa) ameniombea kura pasipo maelezo. Ameandaa lunch na dinner (vyakula vya mchana na usiku) ambako amekuwa akiniombea kura. Ana njia za ajabu za kufanya mambo. Ahsante kwa kukubali kuhesabu kura,” inasema sehemu ya ujumbe huo.
Chana, ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu (CC) na Halmashauri Kuu (NEC) ya CCM, ndiye alihesabu kura za Beatrice kwenye uchaguzi wa kutafuta makamishina wa Bunge.
Ni kwenye ujumbe huo ambamo Beatrice anatoboa kuwa siri ya ushindi wake ni Lowassa aliyekuwa kampeni meneja wake.
Katika kusisitiza hoja yake, Beatrice anasema, “Nimezungumza na TB Joshua wa Emmanuel TV Nigeria aliyenipa unabii kuwa rais ajaye Tanzania ni Edward Lowassa, nikamuambia haiwezekani kwani amechafuka sana.”
Anasema Joshua alimjibu, “…alikuwa amechafuka sasa amesafishwa kwani katubu. Akaniambia his past is over (maisha yake ya nyuma si kitu). Akaongeza kwa kusema, wewe Beatrice ningeangalia your past (maisha yako ya nyuma) pengine nisingekuombea kabisa. Akasema my past is over (hajali maisha yangu ya nyuma),” inasema sehemu ya ujumbe huo wa Beatrice.
Hata hivyo, Beatrice hakueleza katika waraka wake kwa Chana maisha yake ya nyuma yalikuwa vipi. Wala hajaeleza alifanya nini, hadi kuamini kuwa kama Nabii Emmanuel angeyatazama, basi asingemuombea.
Kuvuja kwa taarifa hizi kumekuja wiki tatu baada ya Lowassa kuchaguliwa kuwa mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge, Ulinzi, Usalama na Mambo ya Nje.
Mume wa Beatrice, William Shelukindo alikuwa mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini ambayo iliongoza harakati za kuundwa Kamati Teule ya Bunge iliyochunguza mkataba tata wa Richmond.
Ni taarifa ya kamati hiyo iliyosababisha Lowassa kujiuzulu wadhifa wake wa waziri mkuu, Februari 2008.
Kwa mujibu wa watu waliokaribu na Beatrice na kwa ushuhuda wake mwenyewe, mwanasiasa huyo ameamua kujisalimisha kwa Lowassa kwa kile kinachoelezwa kuwa “Lowassa ndiye rais ajaye wa Tanzania.”
Aidha, kupatikana kwa taarifa hizi kumekuja huku kukiwa na juhudi kubwa zinazofanywa na Lowassa na kundi lake kutaka kujisafisha kwa lengo la kujitosa katika kinyang’anyiro cha urais mwaka 2015.
Miongoni mwa mikakati aliyojiwekea Lowassa na kundi lake ni kujitokeza katika maeneo yote muhimu na kutoa kauli ambazo zitafanya wananchi waanze kumkubali kuwa ni kiongozi anayefaa.
Katika kutekeleza mkakati huo, Januari mwaka huu, Lowassa alijitokeza kuzungumzia vurugu zilizotokea mkoani Arusha zilizotokana na mvutano katika uchaguzi wa meya wa jiji hilo kati ya CCM na CHADEMA.
Katika mnyukano huo, watu watatu walipigwa risasi na polisi na kufariki dunia baada ya polisi kutumia nguvu isiyo ya kawaida kuzima maandamano ya CHADEMA.
Kauli hiyo ya Lowassa ilikuwa tofauti na msimamo wa Katibu Mkuu wa CCM, Yusuf Makamba aliyemtaka kuwasilisha maoni yake katika vikao vya chama badala ya kutumia vyombo vya habari.
Kauli nyingine ya Lowassa ilihusu nyongeza ya viwango vya mishahara kwa wafanyakazi, kutokana na kile alichoita mfumuko wa bei kuwa mkubwa.
Bali wiki moja iliyopita, Naibu Katibu Mkuu wa vyama vya wafanyakazi nchini (TUCTA), Nicholas Mganya alimtuhumu Lowassa kwa kutoa kauli hiyo akisema ana ajenda ya siri nyuma yake.
Mgaya alisema TUCTA haihitaji msaada wa Lowassa katika kusimamia madai yao. Alisema “mbunge huyo wa Monduli inaonekana ana ajenda yake mgongoni.”
Hatua nyingine ya Lowassa katika kujikarabati kisiasa ni kugombea na kupata nafasi ya Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama.
Lowassa amekuwa pia akihudhuria hafla nyingi, hasa za madhehebu ya Kikiristo (KKKT) ambao anaonekana akitoa maoni mbalimbali kama ilivyokuwa Jumapili iliyopita ukumbi wa Dimaond Jubilee kwenye uzinduzi wea albamu ya moja ya kwaya za injili.
Kwenye kusanyiko hilo, Beatrice naye alikuwepo. Lowassa alimtaka asome maoni ya gazeti la The Citizen juu ya ushirikina uliokithiri nchini; jambo ambalo Lowassa alizungumzia kwa urefu.
MwanaHALISI lilipowasiliana na Beatrice ili kupata maoni yake juu ya ushwahiba wake mpya na Lowassa, mahojiano yalikuwa kama ifuatavyo:
Mwandishi: Tusaidie maelezo kidogo juu ya ujumbe uliomwandikia Mheshimiwa Pindi Chana kumjulisha kuwa uliambiwa Edward Lowassa atakuwa rais. Ni kweli?
Beatrice: Barua ameandika nani na umeipata wapi?
Mwandishi: Hii barua fupi – memo ndani ya Bunge, uliposema Mheshimiwa Lowassa ambaye amesimamia vizuri kura zako za ukamishna wa Bunge.
Beatrice: Sina taarifa hiyo. Wala siikumbuki. Unajua ndani ya Bunge tunaandikiana mambo mengi, tena mengine ya utani tu. Na mimi na Mheshimiwa Chana sote ni “walokole,” tunafanyiana utani sana.
Mwandishi: Kwani mheshimiwa Shelukindo, mkiwa ndani ya bunge kuna utani mwingi, kwamba huwa mnaandikiana utani sana?
Beatrice: Kabisa, unajua tunaandika mambo mengi. Na kama unaandika kwa utani kwa mwenzako inabaki hivyo ni utani tu. Sasa tatizo hao wanaowaletea mambo haya wanatumia mambo haya kutafuta mipango yao ya kufikia mwaka 2015.
Alisema, “Mimi najua hakuna anayenibeba ndugu yangu. Mimi ni very solid (ngangari), sibebeki. Nakwambia, mbona mimi nina nguvu nyingi mimi mwenyewe; sihitaji kubebwa. Najua wanajaribu kuonyesha tunabebwa, lakini huo ni ujinga wao wa kufikiri.
Mwandishi: Mheshimiwa Shelukindo, kwani nyie waheshimiwa huwa mnatafutana (kufitiniana)?
Beatrice: Hiyo inafanyika sana, watu wakishakuwa na mambo yao wanatumia wengine kutimiza dhamira zao. Lakini mimi ninafikiria wananchi. Nimeshaamua kwamba Beatrice nashughulikia shida za wananchi jimboni. Ninatafuta njia za kuwaondolea umasikini, njaa na mambo kama hayo. Sasa wengine wanatafuta tu pa kunishika.
Mwandishi: Kwa hiyo Mh. Lowassa ndiye alikuwa kampeni meneja wako katika kutafuta ukamishna pale bungeni, au siyo Mheshimiwa?
Beatrice: Lakini kama anafanya kazi ya kampeni vizuri; ni vizuri tu. Isipokuwa kila mtu anajichukulia mwenyewe alivyo. Mimi ni mtu wa kazi sihitaji kusimamiwa hivyo. Na hebu tujadili hili; unajua kaka nyinyi mnafanya kazi kubwa. Sasa hii kusikia, sijui MwanaHALISI hivi, sijui hivi, pengine kuna watu wanachomekea vitu vyao. Tunapenda kazi yenu.
Mwandishi: Mheshimiwa nakushukuru sana.
Beatrice: Karibu sana tutafanya kazi pamoja.
Akiwa Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini, mume wa Beatrice, William Shellukindo, alikuwa na msimamo mkali dhidi ya watuhumiwa wakuu wa ufisadi nchini na hiyo ndiyo inayoelezwa kuwa sababu ya kushindwa kwake ubunge katika mchakato wa ndani ya CCM.
Shellukindo alikuwa mbunge wa jimbo la Bumbuli mkoani Tanga kwa zaidi ya miaka 20, alishindwa katika kura za maoni na January Makamba, mtoto wa katibu mkuu wa CCM anayetajwa kuwa mfuasi wa mtandao wa Lowassa.
S0urce by Mwanahalisi – 9 March 2011

  MUNGU AKUPE PUMZIKO LA AMANI STEVEN KANUMBA

Jeneza lenye Mwili wa Marehemu,Steven Kanumba likiwasili kwenye Viwanja vya Leaders Club, jijini Dar es Salaam siku ya mazishi yake

(Rest In Peace) RIP - STEVEN KANUPA

MAREHEMU STEVEN KANUMBA ENZI ZA UHAI WAKE

 Marehemu Steven Kanumba akiwa na Pacho Mwamba.
 Steven Kanumba''The great'' with the greatest Nigeria musician 2Face Idibia.
 Ama K.Abebrese and Steven Kanumba ''The great'' smilling for a camera.
 Marehemu Steven Kanumba akiwa na Jackline Walper katika moja ya filamu.
 Marehemu Steven Kanumba akiwa ofisini kwa mkurugenzi Myamba na Nteze.
Mtangazaji na mwandishi wa TBC1 Jane John akifanya mahojiano na Marehemu Steve Kanumba enzi za uhai wake.

MAGAZETI YA LEO;

----PINDA AMZIMA FREEMAN MBOWE, 

---ULAJI WAKITHIRI SERIKALINI-CAG, 

----BABA MZAZI WA LULU AIBUA MAZITO

BABA YAKE ELIZABETH MICHAEL 'LULU' ATAKA JAMII ISIMHUKUMU MWANAWE, HAKI ITENDEKE, AELEZA USHIRIKA WA LULU NA KANUMBA
 Imeandikwa na Daniel Mjema wa Gazeti la Mwananchi.
BABA mzazi wa msanii wa filamu, Elizabeth Michael 'Lulu,' ameitaka jamii kutomhukumu mwanawe kutokana na kifo cha msanii mwenzake marehemu Steven Kanumba, badala yake iache vyombo vya sheria vifanye kazi yake.
Mzazi huyo, Michael Edward Kimemeta anayeishi mjini Moshi, amewaomba Watanzania kuiachia Mahakama iamue kama mtoto wao anahusika katika kifo hicho ama la.
Kimemeta, ameeleza kuwa binti yake ana umri wa miaka 16 tofauti na inavyoelezwa kuwa ana miaka 18.
Juzi Lulu alifikishwa katika Mahakama ya Kisutu jijini Dar es Salaam na kusomewa mashtaka ya mauaji ya msanii mwenzake, Kanumba.
Kumekuwa na utata uliojitokeza kuhusu umri wa Lulu. Wakati mwenyewe akieleza kuwa ana miaka 17, Jeshi la Polisi lilieleza kuwa umri wake ni miaka 18 na juzi Mahakama iliambiwa kuwa msanii huyo ana umri wa miaka 17 na baba yake akisema ana miaka 16.
Kwa upande wake, mama mzazi wa Lulu Lucresia Karugila, alisema tukio la kifo cha Kanumba na kukamatwa kwa binti yake  Lulu, limempa mshituko mkubwa na kumsababishia maradhi ya kisaikolojia na kimwili.
“Hayo yaliyotokea kwa kweli yamenifanya niumwe kabisa hapa sasa hivi nimelala naumwa…nimempa go ahead (ruksa), baba yake azungumze kwa sababu taarifa zote anazo. Naomba mimi mniache kwa sasa,”alisema.
Kimemeta aliliambia Mwananchi jana kuwa mwanawe huyo alizaliwa Aprili 17 mwaka 1995 katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH).
“Nataka nikuambie (mwandishi) mwanangu atatimiza umri wa miaka 17 ifikapo Aprili 17 mwaka huu. Sasa ana umri wa miaka 16 na ni mtoto. Tunavyosikia Kanumba alikuwa mpenzi wake inatuuma sana,” alisema.
Baba huyo alisema alizaa na mama yake Lulu lakini hawakuwahi kuishi pamoja. "Mwanamke huyo alikuwa akifanya kazi Shirika la Ndege Tanzania (ATC) na muda wote Lulu alikuwa akiishi na mama yake jijini Dar es Salaam,"alisema Kimemeta.
Ameomba familia ya marehemu Kanumba ikubali kupokea pole ya familia ya Lulu kupitia gazeti hili kutokana na mazingira kutoruhusu familia hizo kukutana.
“Nasikitika mazingira ya tukio lenyewe mpaka sasa hayaruhusu familia yetu kwenda kutoa pole na kuifariji familia ya Kanumba kulingana na utamaduni wa mwafrika…tunaomba wapokee pole zetu kupitia njia hii,” alisema.
Kwa mujibu wa Kimemeta, hivi sasa wanahofia maisha yao kutokana na jamii kujenga mtazamo hasi juu ya tukio hilo hata bila ya kusubiri vyombo vya sheria kusikiliza ushahidi wa tukio hilo na kutoa hukumu yake.
Alisema kuwa jamii inapaswa ifahamu kuwa, kikatiba mtu yeyote anayeshitakiwa kwa kosa lolote haimaanishi tayari ni mkosaji, bali atahesabiwa kuwa mtuhumiwa hadi pale Mahakama itakapomtia hatiani.
“Yanasemwa mengi mara ooh Kanumba ndio alianza kumpiga mwanangu mara ooh Kanumba alisukumwa …mimi nasema tuiache Mahakama hata sisi hatupendi mtu auawe, lakini Mahakama iachwe itende haki,”alisisitiza.
Akizungumzia maisha ya mwanawe Lulu, Kimemeta alisema alipokuwa akitangaza Kipindi cha Watoto Televisheni ya ITV, walifarijika sana, lakini alipoanza kuingia kwenye sanaa ya filamu, walijua sasa wamempoteza.
“Baada ya kuingia kwenye sanaa ya maigizo niliona kabisa tumempoteza mtoto na nilimweleza mama yake kuwa wale aliokuwa nao katika maigizo akiwamo Kanumba mwenyewe, nilikuwa siwaamini hata kidogo,” alisema.
Kimemeta alidai kuwa siku moja mwanawe alimpigia simu akimwarifu kuwa alikuwa anakwenda jijini Arusha kurekodi filamu na Kanumba, yeye alipinga safari hiyo akitaka Kanumba amthibitishie usalama wa binti yake.
“Kwa sababu nilikuwa sipendezwi na hayo mambo nilimwambia mama yake azungumze na Kanumba na akatuhakikishia atamlinda na kambi yake ina maadili, lakini kumbe huo ndio ukawa mwanzo wa mwanaye kugeuzwa mpenzi wa msanii huyo,” Alidai Elizabeth Michael 'Lulu,'
Baba huyo mzazi alidai kutofanya vizuri darasani kwa mtoto wake huyo, kulichangiwa na hatua ya kuingia katika sanaa ya uigizaji.
“Lulu alikuwa mtoto mwenye tabia nzuri sana hata alipokuwa ITV kwa kweli alitutia moyo wazazi wake kwa jinsi ITV walivyokuwa wakimlea, lakini alipojiingiza tu kwenye uingizaji hapo ndipo mambo yalipoharibika,” alisema.
Alikanusha madai kuwa mwanawe hakumaliza kidato cha nne na kusisitiza kuwa Lulu alisoma Shule ya Kimataifa ya St Mary's na baadaye alihamia Shule ya Sekondari ya Midway High School na kumaliza kidato cha nne mwaka jana.
Alisisitiza kuwa katika mambo yaliyokuwa yakiwaumiza mioyo, ni namna mtoto huyo alivyozidi kuharibika kwa kuingia katika fani ya uigizaji filamu.
Alisema angependa kukutana na Rais Jakaya Kikwete ili azungumze naye kama rafiki yake na watafute suluhisho la maadili kwa kizazi cha sasa na cha baadaye.
Alisema tayari ameanza mchakato wa kuonana na Rais Kikwete ili amweleze siri aliyodai ni ‘nzito’ na kudai tayari ametafuta wazee watatu wenye busara wa kumsindikiza, endapo Rais atakubali ombi lake.
Pia ameziomba taasisi zinazojishughulisha na masuala ya haki za binadamu na msaada wa kisheria, kujitokeza na kumsaidia mwanawe.
Lulu alifikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam juzi na kusomewa shitaka la kumuua Kanumba, tukio lililotokea Aprili 7 mwaka huu eneo la Sinza Vatican.
Msanii huyo hakutakiwa kujibu lolote kwa kuwa Mahakama hiyo haina
mamlaka ya kusikiliza mashauri ya mauaji na hivyo alipelekwa rumande Gegeza la Segerea hadi Aprili 23 mwaka wakati kesi hiyo itakapotajwa.
Kifo cha msanii huyo kimetikisa nchi  kutokana na umaarufu wake, akiwa ameigiza filamu 40 zilikuwa zikirushwa katika vituo mbalimbali vya televisheni ndani na nje ya nchi.

Kanumba alipanga kujenga shule

Katika hatua nyingine, Fidelis Butahe na Pamela Chilongola wanaripoti kuwa mchaguaji maeneo ya kupigia picha za filamu za msanii Kanumba, Rahim Khatib alisema marehemu Kanumba alinunua eneo la ekari 15 huko Mpiji mkoani Pwani kwa ajili ya ujenzi wa shule yake ya sekondari.
Khatib alisema Kanumba alikuwa na mpango huo muda mrefu na kwamba lengo lake lilikuwa kuwasaidia wanafunzi wa eneo hilo ambao hutembea muda mrefu kutokana na shule kuwa mbali na eneo hilo.
 “Kanumba alikuwa na mipango mizuri katika maisha yake, kuna eneo kubwa alilonunua Mpiji ili ajenge shule ya sekondari,” alisema Khatib.
Alifafanua kuwa hadi anafariki dunia, aliacha kiasi cha fedha zaidi ya Sh 40 milioni katika Kampuni yake ya Kanumba The Great.
“Marehemu ameacha fedha zaidi ya Sh 40 katika kampuni yake, magari matatu na hivi karibuni alinunua jingine aina ya Toyota Land Cruiser, ”alisema Khatib.
Katika hatua nyingine Khatib alisema kifo cha Kanumba ni pigo kwa watu waliokuwa wakifanya naye kazi akiwemo yeye mwenyewe kwa kuwa walikuwa wakimtegemea kwa kiwango kikubwa.
Jeneza lenye Mwili wa Marehemu,Steven Kanumba likiwasili kwenye Viwanja vya Leaders Club,jijini Dar es Salaam siku ya mazishi ya msanii huyo wa filamu nchini.

Sintah naye alonga

Kwa upande wake msanii maarufu wa filamu nchini, Christina Manongi maarufu kama Sintah ambaye alikuwa mmoja wa wasanii wa kwanza kufika nyumbani kwa marehemu Kanumba muda mfupi baada ya msanii huyo kuanguka, alisema kuwa siku tano kabla ya Kanumba kufariki, alikuwa na hasira tofauti na alivyomzoea.
Sintah ambaye alikuwa na msanii huyo katika Viwanja vya Leaders Club jijini Dar es Salaam Jumapili ya Aprili mosi pamoja na mwigizaji mwingine, Steve Nyerere alisema kuwa kila alichokuwa akimuuliza Kanumba, alimjibu kwa ukali.
“Ni tofauti na nilivyomzoea, siku ile ya Jumapili tulikaa pale Leaders Club mpaka usiku sana na kila jambo nililokuwa nikizungumza naye alinijibu kwa mkato na ukali kweli, ilinishangaza,” alisema Sintah
Alifafanua kuwa moja ya mambo waliyokuwa wakizungumza na Kanumba ni pamoja na yeye kutaka kuacha uigizaji, suala ambalo marehemu Kanumba hakuliunga mkono na kumjibu kwa ukali kuwa asijitoe katika uigizaji.

JUMAPILI APRIL 15, 2012

Sunday, April 15, 2012

DIAMOND ASHINDA TUZO TATU KWA MPIGO KILIMANJARO MUSIC AWARD 2012

 Mwanamuziki Diamond (kulia)akipokea tuzo yake kutoka kwa George Kavishe meneja wa bia ya Kilimanjaro mara baada ya kutangazwa mshindi wa utunzi bora wa nyimbo katika hafla ya kukabidhi tuzo kwa wanamuziki bora  Kilimanjaro Music Award 2012 zinazofanyika kwenye ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es salaam na kuhudhuria na waalikwa mbalimbali pamoja na wadau wa muziki kutoka ndani ya Tanzania  na nje ya nchi.
Msanii  Nassib Abdul ‘Diamond’ usiku huu ameng’ara kwenye tuzo za Kilimanjaro Music Award, baada ya kujinyakulia tuzo tatu.
“Namshukuru Mungu, wakati mwingine uvumilivu na subira ni mzuri. Mwaka jana sikupata tuzo, nikamshukuru Mungu, nikaongeza bidii, nikafanya kazi nzuri, leo ninachukua tuzo ya tatu sasa hivi, alisema Diamond baada ya kushinda tuzo ya Video Bora ya Mwaka, kupitia wimbo Moyo Wangu, ambayo ilikuwa ya tatu usiku huu.
Diamond alizishinda nyimbo za Hakunaga ya Suma Lee, Wangu ya Jay Dee, Ndoa Ndoana ya Kassim na Bongo Fleva ya Dully Sykes.
 Mwanamuziki Diamond akipiga picha na mama yake wa pili kutoka kushoto na Mkurugenzi wa ASET Asha Baraka kutoka kulia pamona na wanenguaji wake mara baada ya kupokea tuzo yake ya utuzni bora wa nyimbo.
 Mwimbaji wa muziki wa Taarab ambaye ameshinda tuzo ya mburudishaji bora kwa wanawake Malkia Khadija Omar Kopa akitumbuiza katika hafla hiyo usiku huu.
 Malkia Khadija Omar Kopa akishukuru wapenzi wake mara baada ya kushinda tuzo ya mburudishaji bora, wa pili kutoka kushoto ni mume wake na wengine ni watoto wake.
 Watoto wa Malkia wa Mipasho Khadija Omar Kopa wakishuka jukwaani mara baada ya kumtunza mama yao wakati alipokuwa akitumbuiza katika hafla hiyo.
 Kulia ni Msanii Profesa Jay na kushoto ni Mkubwa Fella meneja wa kundi la TMK Family wakimkabidhi tuzo Roma Msanii wa muziki wa Hiphop aliyejishindia tuzo ya msanii bora wa Hiphop.
 Burudani kutoka THT zikiendelea
 Burudani zikiendelea kwa nguzu zote.
 

MAMBO YA TUZO ZA KILIMANJARO MUSIC AWARD 2012 MLIMANI CITY USIKU JANA

 Mwanamuziki Diamond katikati akiwa jukwaani na wenzake kabla ya kuimba wimbo wa msondo katika hafla ya kukabidhi tuzo za wanamuzikii bora za Kilimanjaro Music Award zainazofanyika usiku huu kwenye ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es salaam kulia ni Khalid Chokoraa wa bendi ya mapacha watatu.
 Msanii HBaba akiwa amezungukwa na vimwana katika hafla hiyo
 Mtayarishaji wa muziki P. Funk kulia akiwa na msanii wa muziki wa Hiphop Jay Moo.
 Wakurugenzi wa ASET kutoka kulia ni Asha Baraka akiwa na kaka yake Baraka pamoja na mdau mwingine katika hafla hiyo.
 Kulia ni Dina Marios wa Clouds akiwa na Asma Makau kutoka Clouds pia.
 Makamu Mwenyekiti wa klabu ya Simba Geofrey Nyange Kaburu kulia akibadilishana mawazo na Mulamu Ghambi katika hafla hiyo.
Mohamed Nasor kushoto akiwa na Evance Aveva wakifuatilia matukio mbalimbali katika hafla hiyo usiku huu.

ORODHA YA WALIOTEULIWA KUGOMBEA UBUNGE WA BUNGE LA AFRIKA MASHARIKI

(Inatolewa kwa mujibu wa Kanuni ya 5(3) ya Nyongeza ya Pili ya Kanuni za Bunge Toleo la 2007)
_______________________________
1.0 Tarehe 9 Machi, 2012 nilitoa Tangazo kwa vyombo
vya habari na gazeti la Serikali juu ya kuwepo kwa nafasi Tisa wazi za Ubunge wa Bunge la Afrika Mashariki kufuatia kufikia ukomo wa maisha ya Bunge la sasa hapo 04 Juni, 2012.
Katika Tangazo hilo niliwaomba wananchi wenye sifa za kugombea nafasi hizo wafanye mchakato wa kugombea kupitia vyama vyao vya Siasa na fomu za wagombea waliopendekezwa zirejeshwe Ofisi ya Bunge kabla ya saa 10.00 jioni tarehe 10 Aprili, 2012 ambayo ndiyo siku ya uteuzi. Jumla ya Wagombea 34 kutoka Vyama vya Siasa vya CCM, CHADEMA, CUF, NCCR-MAGEUZI, TLP, UDP na TADEA wamerudisha Fomu.
2.0 Zoezi la uteuzi limekamilika, Wajumbe 33 wametimiza masharti ya uchaguzi kwa mujibu wa Mkataba wa kuanzisha Jumuiya ya Afrika Mashariki na Kanuni za Bunge, hivyo, wameteuliwa kugombea nafasi hizo. Aidha, Mgombea mmoja hakutimiza masharti ya uchaguzi ya kuthibitisha uraia wake na kulipa ada ya uchaguzi kwa mujibu wa Kanuni 5(3) na 6 ya Nyongeza ya Tatu ya Kanuni za Bunge, hivyo hakuteuliwa kugombea.
Ifuatayo ni Orodha ya Wagombea walioteuliwa na wasioteuliwa kugombea nafasi za Ubunge wa Afrika Mashariki:-
1. WAGOMBEA WALIOTEULIWA
KUNDI A: WAGOMBEA WANAWAKE
S/NO.
JINA
CHAMA
1.
Nd. Angela Charles Kizigha
CCM
2.
Nd. Fancy Haji Nkuhi
CCM
3.
Dkt. Godbertha Kokubanza Kinyondo
CCM
4.
Nd. Janet Deo Mmari
CCM
5.
Nd. Janet Zebedayo Mbene
CCM
6.
Nd. Maryam Ussi Yahya
CCM
7.
Nd. Rose Daudi Mwalusamba
CUF
8.
Nd. Sebtuu Mohamed Nassor
CCM
9.
Nd. Shy-Rose Sadruddin Bhanji
CCM
10.
Nd. Sofia Ali Rijaal
CCM
KUNDI B: WAGOMBEA WA ZANZIBAR
S/NO.
JINA
CHAMA
1.
Nd. Abdullah Ali Hassan Mwinyi
CCM
2.
Dkt. Ahmada Hamad Khatib
CCM
3.
Dkt. Haji Mwita Haji
CCM
4.
Nd. Khamis Jabir Makame
CCM
5.
Dkt. Said Gharib Bilal
CCM
6.
Nd. Zubeir Ali Maulid
CCM
KUNDI C: WAGOMBEA WA VYAMA VYA UPINZANI
S/NO.
JINA
CHAMA
1.
Nd. Antony Calist Komu
CHADEMA
2.
Dkt. Fortunatus Lwanyantika Masha
UDP
4.
Nd. Juju Martin Danda
NCCR-MAGEUZI
5.
Nd. Micah Elifuraha Mrindoko
TLP
6.
Nd. Mwaiseje S. Polisya
NCCR-MAGEUZI
7.
Nd. Nderakindo Perpetua Kessy
NCCR- MAGEUZI
8.
Nd. Twaha Issa Taslima
CUF

Thursday, March 8, 2012

MAISHA YA MASIKINI KILA SIKU

APRIL 18, 2012 , KATAVI MPANDA  

MAFUTA NI ISSUE??????????????

 MATATIZO YA UHABA WA MAFUTA BADO YANAENDELEA KATIKA MKOA WA KATAVI HAPA CHINI TUMEKUWEKEA PICHA ZILIZOPIGWA JANA KATIKA KITUO KIMOJA CHA MAFUTA KATIKA MAKAO MAKUU YA MKOA WA KATAVI MPANDA MJINI.










HAPA CHINI NI GARI LILILOKUWA LIKIELEKEA MISHAMO LIKIENDESHWA NA DEREVA AKIWA AMELEWA CHAKARI NA KUSABABISHA AJALI NYUMA YA UKUTA WA KANISA KATOLIKI MPANDA ENEO LA SHULE YA MSINGI MSAKILA JUZI MAJIRA YA SAA SITA MCHANA, MADEREVA WALEVI TUWAPIGE VITA 




mkurugenzi wa blog hii Wilbroard Sumia, anawapongeza wale wote walioingia katika bunge la Afrika Mashariki katika kipindi kijacho

    POSHO IMEISHA SAFARI BADO


DC MPANDA AWAFUNDA WATENDAJI WA KATA NA VIJIJI
 MKUU WA WILAYA YA MPANDA MKOA WA KATAVI, DR RAJABU RUTENGWE 
Na  Willy Sumia, Mpanda
SERIKALI wilaya ya Mpanda mkoa wa Katavi imewaagiza watendaji wa kata na vijiji kuwajibika katika maeneo yao ya kazi ili kuleta ufanisi katika utendaji wa kazi
Agizo hilo limetolewa na mkuu wa wilaya ya Mpanda, Dr Rajabu Rutengwe Machi 9, 2012 katika ukumbi wa halmashauri ya wilaya ya Mpanda wakati akifunga kikao cha ushauri cha wilaya ya Mpanda DCC
Mkuu huyo wa wilaya amesema hivi sasa watendaji wengi wamekuwa wakisubiria maagizo katika utendaji kazi wao bila kujali kuwa kutenda kazi zao bila maagizo ni nguzo ya utendaji kazi  wao
Amesema katika miji mingi wilayani Mpanda uchafu umeendelea kuchukua nafasi kubwa kuliko hali inayotakiwa kwani katika hali halisi hakuna haja ya kuwa na miji michafu wakati kila mji una watendaji wa serikali wanaotakiwa kuwajibika
Ametoa mfano wa mji wa Ikola kuwa kituo kikuu cha magonjwa wa kuhara na kutapika ugonjwa ambao kimsingi unasababishwa na uchafu hivyo endapo watendaji wataweza kuwajibika na kufanya kazi ipasavyo uchafu ungeondoka wenyewe hata hao wagonjwa wangeeleweka kuwa wametoka mbali
Ameziagiza serikali za vijiji na kata kuwajibika katika suala la mifugo iliyoingia kiholela katika maeneo yao kwani amesema kuwa taarifa za uhakika zinaelekeza kuwa upo ushahidi wa kutosha kuwa wapo baadhi ya watendaji wa kata na vijiji wamekuwa wakichukua pesa ili kuruhusu mifugo kuingia katika maeneo yao
“ ndugu zangu nawaeleza kitu kimoja kikubwa ni kuwa waliokula pesa watazitapika maana naagiza au ng’ombe waondoke wewe ubaki au wewe uondoke  ng’ombe wabaki, sina namna lazima uwajibike kwa ng’ombe uliowapokea” amesema mkuu wa wilaya
Kwa upande mwingine mkuu wa wilaya ameshukuru maafisa mipango wa halmashauri ya wilaya ya Mpanda kwa kufanya vema katika maandalizi ya miradi ya maendeleo inayoleta mafanikio makubwa katika vijiji na kuweza kuondoa kero mbalimbali kwa wananchi wa wilaya yake
Mkuu wa wilaya ametoa taarifa katika kikao hiki kuwa kuanzia Machi 12, 2012 ataanza ziara ya kukagua miradi ya maendeleo katika kila kata ambapo ataweza kupokea taarifa za miradi, taarifa ya kazi, kukagua miradi na kuzungumza na wananchi katika mikutano ya hadhara katika kila palipo na mradi wa maendeleo
Mada zilizojadiliwa katika kikao cha leo cha DCC ni pamoja na kupitia mpango na bajeti ya halmashauri ya wilaya ya Mpanda ya mwaka 2012/2013, kupitia mpango wa bajeti ya halmashauri ya wilaya ya Mlele kwa mwaka 2012/2013 pamoja na uzoefu wa nchi ya Japan katika ugatuaji wa madaraka.
mwisho
HAPA KAZI TU!!!! Mmoja wa madaktari akitoa huduma ya kinywa na meno kwa mwanafunzi wa shule ya msingi Msakila mjini Mpanda katika mkoa wa Katavi, Katavi ni miongoni mwa mikoa ambayo haijaguswa na mgomo wa madaktari uliotokea mwezi uliopita na mwezi huu.
MKOA WA KATAVI NA FURSA ZINAZOPATIKANA: MKUU WA WILAYA ATEMBELEA KATA ZA H/MJI - 

UNAMAONI GANI ?  tuandikie kwa email willysumia@gmail.com

BARAZA LA MADIWANI LARIDHIA BAJETI YA BIL. 14
BARAZA la madiwani la halmashauri ya mji Mpanda katika mkoa wa Katavi limepitisha mapendekezo ya bajeti ya hamashauri hiyo kwa kipindi cha mwaka 2012/2013 kwa ajili  ya shughuli za maendeleo
Baraza hilo lilioketi leo Machi 9, 2012 limekubali kuyapitisha makadirio na makisio ya bajeti ya halmashauri hiyo ambapo mweka hazina wa Halmashauri hiyo Tatu Kisori amesema katika kipindi cha 2012/13 halmashauri imepanga kukusanya kiasi cha shilingi 606,847,000 kutoka katika vyanzo vya ndani ambapo pia halmashauri yake inatarajia kupokea ruzuku toka serikali kuu kiasi cha shilingi 6,441,517,240.
Amesema katika ruzuku ya serikali kiasi cha shilingi 5,338,014,240/= ni malipo ya mishahara kwa watumishi wa kada mbali mbali na shilingi 1,103,503,000/= ni za matumizi ya kawaida na kufafanua kuwa katika bajeti hiyo mishahara ni ongezeko la asilimia 20 kutoka shilingi 4,265,057,000/= hadi 5,338,014,240/=
Akizungumzia miradi ya maendeleo mweka hazina huyo alisema katika bajeti ya maendeleo halmashauri yake inatarajia kutumia shilingi 3,870,010,627/= kutoka serikali kuu, katika fedha hizo miradi ya maji imepewa kipaumbele kikubwa kwa kutengewa asilimia 34 ambayo ni shilingi 1,300,288,600/= ikifuatiwa na idara ya utawala kwa asilimia 26 sawa na shilingi 1,027,733,000/= pamoja na elimu ya sekondari iliyopewa shilingi 614,474,000/= sawa na asilimia 16.
Tatu Kisori pia amewasilisha bajeti ndogo ya maombi maalum ya nje ya ukomo wa bajeti kutokana na baadhi ya shughuli muhimu kushindwa kuingia katika bajeti kutokana na viwango vidogo vya bajeti vilivyowekwa na TAMISEMI na hivyo kuathiri bajeti kushindwa kuingizwa vitu muhimu ili kufikia malengo na kuondoa kero zilizoko katika jamii
Kisori amesema kutokana na hali hiyo halmashauri imelazimika kuomba fedha nje ya bajeti ya kawaida kiasi cha shilingi 3,558,000,000/= kwa ajili ya kununulia gari la kuzoa taka ngumu mjini Mpanda, kununulia gari la kunyonya maji machafu mjini, matengenezo ya gari la zimamoto na ujenzi wa sekondari ya Kata ya Kakese pamoja na kuweka miundombinu ya umeme katika shule za sekondari zote.
Aidha baraza la madiwani la halmashauri ya mji Mpanda limeridhia na kupitisha makisio ya bajeti ya hamashauri hiyo katika kipindi cha Julai 2012 hadi juni 2013 kiasi cha shilingi 14,688,051,240/= ikiwa ni mapato ya ndani na ruzuku ya serikali kwa ajili ya maendeleo ya halmashauri ya Mji Mpanda
Awali akiwasilisha mapitio ya bajeti ya 2011/2012 Kisori amesema halmashauri yake ilipanga kukusanya kiasi cha shilingi 823,164,000/= kutoka katika vyanzo vya ndani na kuweza kukusanya kiasi cha shilingi 241,873,480/= katika kipindi cha Julai 2012 hadi januari 2012 sawa na asilimia 29.38 ya makisio ambapo kiasi hicho kimefikiwa kwa kutumia mawakala wa ukusanyaji wa ushuru.
Amesema katika kipindi cha bajeti 2011/12 halmashauri ilipanga kuingiza mapato ya shilingi 70,350,000/= kutokana na vyanzo vya mapato vilivyofutwa na kuweza kukusanya shilingi 42,028,500/= sawa na asilimia 60 ya makisio.
Katika hatua nyingine baraza hilo limetoa Baraka zote kwa shirika la nyumba la Taifa kuenza ujenzi wa majengo katika mji wa Mpanda baada ya kuridhia malipo ya shilingi milioni 100 ikiwa ni kwa ajili ya eneo la jingo la starehe maarufu kwa jina la jengo la Paradise eneo litakalojengwa gorofa nne kwa ajili ya matumizi ya kibenki, ofisi na maduka ya biashara
Aidha baraza hilo limepokea na kuridhia maombi ya mamlaka ya viwanja vya ndege nchini juu ya kuomba upanuzi wa uwanja wa ndege wa Mpanda utakaopelekea kuhamishwa kwa baadhi ya wakazi wa eneo la Nsemulwa Uwanja wa ndege ili kupisha upanuzi huo.
Imeelezwa katika baraza hilo kuwa upanuzi huo taathiri baadhi ya wananchi watakaotakiwa kipisha upanuzi huo baada ya kulipwa fidia na mamlaka husika katika kipindi kifupi kijacho kwani ujenzi unatarajia kuanza katika kipindi kifupi kijacho.\\
MAAFISA WATENDAJI WAAGIZWA KUSHUGHULIKIA MIFUGO HARAMU

Na  Willy Sumia, Mpanda
SERIKALI wilaya ya Mpanda mkoa wa Katavi imewaagiza watendaji wa kata na vijiji kuwajibika katika maeneo yao ya kazi ili kuleta ufanisi katika utendaji wa kazi
Agizo hilo limetolewa na mkuu wa wilaya ya Mpanda, Dr Rajabu Rutengwe Machi 9, 2012 katika ukumbi wa halmashauri ya wilaya ya Mpanda wakati akifunga kikao cha ushauri cha wilaya ya Mpanda DCC
Mkuu huyo wa wilaya amesema hivi sasa watendaji wengi wamekuwa wakisubiria maagizo katika utendaji kazi wao bila kujali kuwa kutenda kazi zao bila maagizo ni nguzo ya utendaji kazi  wao
Amesema katika miji mingi wilayani Mpanda uchafu umeendelea kuchukua nafasi kubwa kuliko hali inayotakiwa kwani katika hali halisi hakuna haja ya kuwa na miji michafu wakati kila mji una watendaji wa serikali wanaotakiwa kuwajibika
Ametoa mfano wa mji wa Ikola kuwa kituo kikuu cha magonjwa wa kuhara na kutapika ugonjwa ambao kimsingi unasababishwa na uchafu hivyo endapo watendaji wataweza kuwajibika na kufanya kazi ipasavyo uchafu ungeondoka wenyewe hata hao wagonjwa wangeeleweka kuwa wametoka mbali
Ameziagiza serikali za vijiji na kata kuwajibika katika suala la mifugo iliyoingia kiholela katika maeneo yao kwani amesema kuwa taarifa za uhakika zinaelekeza kuwa upo ushahidi wa kutosha kuwa wapo baadhi ya watendaji wa kata na vijiji wamekuwa wakichukua pesa ili kuruhusu mifugo kuingia katika maeneo yao
“ ndugu zangu nawaeleza kitu kimoja kikubwa ni kuwa waliokula pesa watazitapika maana naagiza au ng’ombe waondoke wewe ubaki au wewe uondoke  ng’ombe wabaki, sina namna lazima uwajibike kwa ng’ombe uliowapokea” amesema mkuu wa wilaya
Kwa upande mwingine mkuu wa wilaya ameshukuru maafisa mipango wa halmashauri ya wilaya ya Mpanda kwa kufanya vema katika maandalizi ya miradi ya maendeleo inayoleta mafanikio makubwa katika vijiji na kuweza kuondoa kero mbalimbali kwa wananchi wa wilaya yake
Mkuu wa wilaya ametoa taarifa katika kikao hiki kuwa kuanzia Machi 12, 2012 ataanza ziara ya kukagua miradi ya maendeleo katika kila kata ambapo ataweza kupokea taarifa za miradi, taarifa ya kazi, kukagua miradi na kuzungumza na wananchi katika mikutano ya hadhara katika kila palipo na mradi wa maendeleo
Mada zilizojadiliwa katika kikao cha leo cha DCC ni pamoja na kupitia mpango na bajeti ya halmashauri ya wilaya ya Mpanda ya mwaka 2012/2013, kupitia mpango wa bajeti ya halmashauri ya wilaya ya Mlele kwa mwaka 2012/2013 pamoja na uzoefu wa nchi ya Japan katika ugatuaji wa madaraka.
mwisho

RAIS JAKAYA KIKWETE KESHO KULIHUTUBIA TAIFA ,MGOMO WA MADAKTARI WAWEZA KUZUNGUMZIWA

Taarifa zilizotua hivi punde kupitia mwanahabari wa mtandao huu wa www.sumiampanda.blogspot.com kutoka chumba cha habari cha radio Uhuru zinadai kuwa Rais Jakaya Kikwete kesho ijumaa saa 10 jioni atalihutubia Taifa kupitia wazee wa mkoa wa Dar es Salaam katika ukumbi wa Diamond Jubilee na hutuba yake kurushwa moja kwa moja (live) na TV na radio nchini.


SERIKALI YATANGAZA RASMI MIKOA MIPYA MINNE NA WILAYA 19

Waziri mkuu Mizengo Pinda

Habari ambayo imetua hivi punde katika mtandao huu wa www.sumiampanda.blogspot.com inadai kuwa serikali imetoa matangazo rasmi ya Serikali (Government Notices) kuhusu uanzishaji wa mikoa mipya minne na wilaya mpya 19 ambayo yamechapishwa tangu Machi 2, mwaka huu.
Waziri Mkuu Mizengo Pinda amesema matangazo hayo ambayo yalisainiwa na Rais Jakaya Kikwete tangu Machi mosi, 2012, yanabainisha mikoa mipya kuwa ni Geita, Katavi, Njombe na Simiyu. Mikoa hii imechapishwa katika Tangazo la Serikali Na. 72.
Wilaya 19 ambazo zimeanzishwa na kuchapishwa katika Tangazo la Serikali Na.73 ni Buhigwe, Busega, Butiama, Chemba, Gairo, Ikungi na Itilima. Wilaya nyingine ni Kakonko, Kalambo, Kaliua, Kyerwa, Mbogwe, Mkalama na Mlele. Nyingine ni Momba, Nyang’hwale, Nyasa, Uvinza na Wanging’ombe.
Kwa mujibu wa matangazo hayo makao makuu ya mikoa hiyo mipya minne yatakuwa kama ifuatavyo: Geita (Geita), Simiyu (Bariadi) Njombe (Njombe) na Katavi (Mpanda).
Mikoa hiyo itakuwa na wilaya zifuatazo; Geita utakuwa na wilaya tano za Bukombe, Chato, Geita, Mbongwe na Nyang’hwale. Mkoa wa Katavi utakuwa na wilaya mbili za Mlele na Mpanda. Mkoa wa Njombe utakuwa na wilaya nne za Makete, Njombe, Ludewa na Wanging’ombe wakati mkoa wa Simiyu utakuwa na wilaya tano za Bariadi, Busega, Maswa, Meatu na Itilima.
Makao makuu ya wilaya mpya zilizoanzishwa ni kama ifuatavyo: Buhigwe (Buhigwe); Busega (Nyashimo); Butiama (Butiama); Chemba (Chemba); Gairo (Gairo); Ikungi (Ikungi) Itilima (Lagangabilili); Kakonko (Kakonko); Kalambo (Matai) na Kaliua (Kaliua).
Nyingine ni Kyerwa (Rubwera); Mbogwe (Mbogwe); Mkalama (Nduguti); Mlele (Inyonga); Momba (Chitete); Nyang’hwale (Kharumwa); Nyasa (Mbamba Bay); Uvinza (Lugufu) na Igwachanya (Wanging’ombe).
Julai 2010, kabla Rais Kikwete hajatoa hotuba ya kulivunja Bunge, Serikali ilitoa uamuzi wa kuunda mikoa mipya minne na wilaya mpya 21. Hata hivyo, baada ya kuhakiki mipaka ya maeneo hayo yote na kuandaa maelezo ya mipaka hiyo vizuri (boundary descriptions), wilaya zilipunguzwa na kubakia 19.
(mwisho)
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
S. L. P. 3021,
DAR ES SALAAM.
ALHAMISI, MACHI 8, 2012.
www.katavim.blogspot.com

MKOA WA KATAVI NA FURSA ZINAZOPATIKANA: MKUU WA WILAYA ATEMBELEA KATA ZA H/MJI

DC MPANDA ATOA SIKU KUMI NA NNE WALOFAULU KURIPOTI SHULENI
SERIKALI ya wilaya ya Mpanda mkoa tarajiwa wa Katavi imeuagiza uongozi wa Kata ya Ilembo mjini Mpanda kuwasilisha kwake majina ya wahamiaji haramu walioingia katika kata hiyo ili waweze kushughulikiwa mapema iwezekanavyo
Agizo hilo limetolewa na mkuu wa wilaya hiyo Dr Rajabu Rutengwe katika mkutano wa hadhara mara baada ya kuelezwa kero kubwa ya wakulima na wafugaji iliyopo katika kata hiyo iliyodumu kwa takribani miaka mine sasa.
Awali akitoa ufafanuzi wa kaero hiyo afisa mtendaji wa kata ya Ilembo Marry Ngomarufu amesema kuwa ofisi ya kata imeweza kutumia ofisi ya polisi na mahakama kushughulikia migogoro hiyo ingawa bado hali haijaweza kutengamaa kiasi cha kutosha
Mkuu wa wilaya ya Mpanda amesema migogoro mingi ya wahamiaji haramu hasa wafugaji toka mikoa ya kanda ya Ziwa kutokana na baadhi ya wananchi kuuziana maeneo na wafugaji kwa tamaa ya pesa kwa wenye mashamba na badala yake wameuza fursa zao na kuleta migogoro kwa sababu majirani na eneo lililonunuliwa na wafugajia au mfugaji mmoja wao wakauwa wanaendelea kulima na hiyo inakuwa ni sehemu ya chakula cha mifugo na ng’ombe hawana mipaka kama binadamu
Akihutubia wananchi katika mkutano wa hadhara Ilembo mkuu wa wilaya amesema urithi pekee kwa motto ni elimu na siyo majumba na magari hivyo amewataka wananchi mahala popote wasimamie watoto kusoma kwa bidii na kuzitumia kwa uhakika fursa za kupata elimu zilizopo b ila kujali kipato cha mzazi au mlezi kwani ni hazina ya baadae kwa wilaya, mkoa na hata taifa kwa ujumla
Amesema hivi sasa serikali imeweka mazingira ya kuhakikisha kuwa watoto wote wanapata elimu ya msingi na sekondari hata kama hawana uwezo kifedha kwani hivi sasa kila kata ina sekondari yake inayotoa fursa kwa watoto wote walioko katika kata kuendelea na masomo ya sekondari pindi wanapofaulu mtihani wa darasa la saba.
Pia mkuu wa wilaya hiyo Dr Rajabu ameagiza watoto wa kike kumi na mmoja waliofaulu kuingia kidato cha kwanza hawajaripoti shuleni wafike shuleni ndani ya kipindi cha siku kumi na nne kuanzia Machi 6, 2012 wawe wamshaanza masomo na taarifa toka kwa mkuu wa shule iwasilishwe kwake baada ya siku kumi na nne kabla serikali ya wilaya haijaanza kuwafuatilia kisheria kwa nini hawajaripoti shuleni kuanza na masomo ya sekondari.
Amewasihi wananchi kuanza kujenga majengo yanayoendana na hadhi ya manispaa kwani muda wa miezi michache ijayo halmashauri ya mji Mpanda utakuwa na hadhi ya manispaa baada ya mkoa wa Katavi kuanza ili kuanza na kasi ya maendeleo ya mkoa wa Katavi ambao umenza kukimbia kimaendeleo kabla ya kuanza kazi rasmi.
Amewahimiza wananchi wa Ilembo kuanza kufanya miradi ya ufugaji kuku hasa akina mama ambao wanaweza kuwa karibu na mifugo hiyo kwani hivi sasa kuku mmoja anauzwa kwa bei ya shilingi elfu kumi na mbili kwa kuku mmoja mdogo na hivyo ukianza kufuga makoo mmmoja akapewa pumba anaweza kuzaa vifaranga mia moja na arobaini kwa mwaka sawa na kuingiza kipato cha shilingi milioni mbili na laki nne kwa mwaka kutoka kwenye kuku mmoja.
Amesema mkoa utakapoanza wageni wanaohitaji kula kuku wataongezeka mara dufu ya sasa na bei itaongezeka mara mbili ya sasa,
“Mnapopita mjini fikeni nyumbani kwangu muone kuku ninaofuga ni wakubwa na ni wengi na nikiwaingiza sokoni sikosi shilingi elfu kumi na tano taslimu” alisema mkuu wa wilaya
Ametoa mfano wa mhe. Waziri Mkuu Mhe. Pinda ambaye anafuga nyuki ambao ni wadudu lakini wana faida kubwa kwa mfugaji na mlaji wa asali kwani hivi sasa bei ya lita moja ya asali ni shilingi elfu kumi wakati mzinga mmoja unaweza kutoa lita arobaini za asli kwa msimu mmoja tu sawa na kuwa utaweza kuvuna shilingi laki nne za mauzo ya asali kwa msimu mmoja, je kwa mwenye mizinga kumi atapata kiasi gani kwa msimu ihali hana gharama ya kuwalishia wala kuweka dawa
Ametoa wito mkwa wananchi kuanza kuzitumia fursa zilizopo za shughuli za kiuchumi ili kusaidia kuwa na miradi inayoweza kusaidia kuondokana na kero za ukosefu wa kipato
Aidha amewasihi wananchi kuanza kujiandaa kwa sense ya watu na makazi itakayofanyika mwezi Agosti mwaka huu kwani tayari maandali yameanza kufanyika na shughuli za msingi za maandalizi ya sense zimekamilika bado mambo machache.


TUMIENI MAJIKO RAFIKI WA MAZINGIRA - MAKAMU WA RAIS
WAKAZI wa mkoa wa Rukwa wametakiwa kutumia majiko yanayotumia kuni na mkaa kidogo ili kupunguza uharibifu wa mazingira katika mkoa huo
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr Mohamed Gharib Bilal, alitoa rai hiyo jana katika mkutano wa Hadhara katika uwanja wa kumbu kumbu ya Nelson Mandela mjini Sumbawanga
Alisema hivi sasa mkoa wa Rukwa umeanza kupoteza misitu mingi kutokana na kushamiri kwa vitengo vya uharibifu wa mazingira katika maeneo mengi ya mkoa huo vinavyochangiwa na shughuli mbali mbali za binadamu
Alisema kuchoma moto kiholela kunachangia sana kuua mbegu za miti na misitu mingi kuendelea kuteketea kwani miti iliyopo nayo inaendelea kuteketezwa na wachoma mkaa pamoja na matumizi ya kuni kwa ajili ya kupikia.
“hivi sasa ukipita katika maeneo karibu yote vijijini hasa vijiji vya wilaya ya Sumbawanga kumebaki upara licha ya kuwa maeneo hayo yalikuwa na misitu minene tena ya kutisha” alisema Dr Bilali
Alisema umefika wakati wananchi wa Rukwa waanze kubadili tabia na kuona suala la uharibifu wa mazingira kuwa ni sawa na janga la mkoa mzima na lianze kushughulikiwa kwa mikakati maalumu itakayosimamiwa vema na kupunguza uharibifu uliopo sasa.
Alisema kuwa moto kichaa ni moto ambao unachomwa pasipo misingi ya kiutaalamu kwani hata wanaosafisha mashamba wanatumia kuchoma moto na kuuacha unaendelea kuangamiza misitu mingine
Katika mkoa wa Rukwa kumekuwa na utamaduni wa kuchoma moto hasa nyakati za kiangazi kwa lengo la kuwinda, kuchimba panya, kusafisha mashamba baada ya kuvuna mazao pamoja na kutenga maeneo ya kuchungia mifugo yao.
Maeneo yaliyoathirika na uharibifu wa mazingira kwa kiwango kikubwa ni pamoja na wilaya ya Nkasi, Sumbawanga vijijini , wilaya ya kalambo na kata za Inyonga, Kasokola, Mpanda mjini, Magamba, Nsimbo, Uruila na Mtapenda katika wilaya ya Mpanda.
MWISHO
MKOA WA KATAVI NA FURSA ZINAZOPATIKANA: MKUU WA WILAYA ATEMBELEA KATA ZA H/MJI
 Pia fungua www.sumiampanda.blogspot.com

Monday, February 21, 2011

HABARI ZA MICHEZO

April 19, 2012
TAARIFA TOKA TFF LEO ,25 TWIGA STARS KAMBINI APRILI 20
Kocha Mkuu wa Twiga Stars, Charles Boniface Mkwasa ameita wachezaji 25 watakaoingia kambini kesho (Aprili 20 mwaka huu) kwa ajili ya mechi ya kirafiki dhidi ya Zimbabwe inayotarajiwa kuchezwa Aprili 28 mwaka huu jijini Dar es Salaam.
Mechi hiyo ni sehemu ya maandalizi ya Twiga Stars kabla ya mechi ya mashindano ya Afrika kwa Wanawake (AWC) dhidi ya Ethiopia itakayochezwa Mei 26 mwaka huu jijini Addis Ababa kabla ya timu hizo kurudiana jijini Dar es Salaam wiki mbili baadaye.
Baada ya kuripoti kambini jioni, wachezaji hao watafanyiwa vipimo vya afya (medical examination) siku inayofuata (Aprili 21 mwaka huu) na kuanza mazoezi Aprili 22 mwaka huu. Kambi ya timu hizo itakuwa kwenye hosteli za Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) ya Ruvu mkoani Pwani.
Wachezaji walioitwa ni Amina Ally kutoka Sekondari ya Lord Baden, Asha Rashid, Aziza Mwadini (New Generation, Zanzibar), Etoe Mlenzi (JKT Mbweni), Evelyne Sekikuto (Mburahati Queens), Fadhila Hamad (Uzuri Queens), Fatuma Bashiri (Simba Queens), Fatuma Khatib (Mburahati Queens) na Fatuma Mustafa (Sayari).
Wengine ni Fatuma Omari (Sayari), Hanifa Idd (Uzuri Queens), Maimuna Said (JKT Mbweni), Mariam Aziz (Tanzanite), Mwajuma Abdallah (Tanzanite), Mwanahamisi Omari (Mburahati Queens), Mwanaidi Tamba (Mburahati Queens), Mwapewa Mtumwa (Sayari) na Rehema Abdul (Lord Baden).
Kikosi hicho pia kina akina Rukia Khamis (Sayari), Semeni Abeid (Tanzanite), Siajabu Hassan (Evergreen), Sophia Mwasikili (Luleburgaz Spor Kulubu, Uturuki), Veneranda Mtamo (Tanzanite), Zena Khamis (Mburahati Queens) na Zena Said (Uzuri Queens).
KUONA NGORONGORO HEROES, SUDAN 3,000/-
Kiingilio cha chini cha mechi ya kuwania kucheza Fainali za Afrika kwa vijana chini ya miaka 20 kati ya Tanzania (Ngorongoro Heroes) na Sudan itakayochezwa Jumamosi (Aprili 21 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam ni sh. 3,000.
Mechi hiyo itaanza saa 10 kamili jioni, na viingilio vingine vitakuwa sh. 5,000 kwa viti vya rangi ya chungwa, sh. 10,000 kwa VIP C na B wakati VIP itakuwa ni sh. 15,000.
Sudan inatarajia kuwasili leo mchana kwa ndege ya Ethiopian Airlines ikiwa na msafara wa watu 30 na itafikia hoteli ya Rungwe iliyoko maeneo ya Kariakoo jijini Dar es Salaam. Jioni itafanya mazoezi Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume.
Ngorongoro Heroes tayari iko kambini chini ya Kocha Kim Poulsen, na leo inaendelea na mazoezi kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Sudan yenyewe itafanya mazoezi kwenye uwanja huo kesho.
Kesho (Aprili 20 mwaka huu) saa 4 asubuhi kwenye ofisi za Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kutakuwa na mkutano kati ya makocha wa timu zote mbili na Waandishi wa Habari.
MKUTANO MKUU TFF APRILI 21, 22
Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) utafanyika kwa siku mbili (Aprili 21 na 22 mwaka huu) kwenye ukumbi wa NSSF Waterfront jijini Dar es Salaam.
Wajumbe wa mkutano huo watawasili jijini kesho (Aprili 20 mwaka huu) na watafikia kwenye hoteli ya Royal Valentino. Wajumbe wanatoka katika vyama vya mpira wa miguu vya mikoa, vyama shiriki na klabu za Ligi Kuu ya Vodacom.
Mkutano huo utakaoanza saa 3 asubuhi utakuwa na ajenda kumi na moja. Baadhi ya ajenda hizo ni hotuba ya Rais wa TFF, taarifa ya utendaji ya mwaka 2011, bajeti ya mwaka 2012 na taarifa ya ukaguzi wa hesabu (audited accounts).
JKT RUVU, SIMBA ZAINGIZA MIL 30/-
Pambano la Ligi Kuu ya Vodacom kati ya JKT Ruvu na Simba lililochezwa jana (Aprili 18 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam limeingiza sh. 30,095,000.
Jumla ya watazamaji 8,362 walikata tiketi kushuhudia mechi hiyo kwa viingilio vya sh. 3,000, sh. 5,000, sh. 10,000 na sh. 15,000. Watazamaji 7,310 kati ya hao walishuhudia mechi hiyo kwa kiingilio cha sh. 3,000.
Baada ya kuondoa gharama za awali za mchezo na asilimia 18 ya Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) ambayo ni sh. 4,590,762.71 kila klabu ilipata sh. 4,455,551.19, uwanja sh. 1,485,183.73.
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) sh. 1,485,183.73, Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) sh. 297,036.75 na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Pwani (COREFA) sh. 297,036.75.
Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh. 742,591.86, Baraza la Michezo la Taifa (BMT) sh. 148,518.37 na asilimia 10 ya gharama za mechi ni sh. 1,485,183.73.
Gharama za awali za mechi zilikuwa nauli ya ndani kwa waamuzi sh. 10,000, nauli ya ndani kwa kamishna wa mchezo sh. 10,000 na nauli ya ndani kwa mtathmini wa waamuzi sh. 10,000.
Mwamuzi wa akiba sh. 30,000, posho ya kujikimu kwa kamishna, mtathmini wa waamuzi na waamuzi sh. 120,000, gharama ya tiketi sh. 3,750,000, maandalizi ya uwanja (pitch) sh. 400,000, umeme sh. 300,000, usafi na ulinzi kwa uwanja sh. 2,350,000 na Wachina (Beijing Construction) sh. 2,000,000.
Gharama nyingine ni Jichangie ambayo ni sh. 200 kwa kila tiketi; kila klabu ilipata sh. 585,340 wakati Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) kilipata sh. 510,720.
SIMBA, MORO UNITED KUCHEZA USIKU
Mechi ya Ligi ya Vodacom kati ya Simba na Moro United iliyokuwa ichezwe Aprili 5 mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam imerudishwa nyuma hadi Jumatatu ya Aprili 23 mwaka huu kwenye uwanja huo huo na itaanza saa 1 kamili usiku.
Mabadiliko hayo yamefanyika ili kuipa Simba fursa ya kujiandaa vizuri kwa mechi yao ya Kombe la Shirikisho la Afrika dhidi ya Al Ahly Shandy ya Sudan itakayochezwa Aprili 29 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kuanzia saa 10 kamili jioni.
Pia mechi kati ya Azam na Mtibwa Sugar iliyokuwa ichezwe Aprili 21 mwaka huu kwenye Uwanja wa Chamazi, Dar es Salaam imesogezwa mbele hadi Aprili 22 mwaka huu kupisha mechi ya U20 kati ya Tanzania na Sudan itakayochezwa Aprili 21 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Mechi nyingine mbili zimefanyiwa marekebisho; Coastal Union na Kagera Sugar zilizokuwa zicheze jijini Tanga, Aprili 29 mwaka huu, mechi yao imesogezwa hadi Aprili 30 mwaka huu ili kupisha shughuli za Mei Mosi kwenye Uwanja wa Mkwakwani. Nazo Azam na Toto Africans zilizokuwa zicheze Aprili 26 mwaka huu Uwanja wa Chamazi, sasa zitacheza Aprili 28 mwaka huu.
Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
Imewekwa na Francis Godwin ni Iringa na matukio 0



Monday, January 31, 2011

FOCUS 2011 - KATAVI REGION ISSUES

Na Willy Sumia, Mpanda
Machi 20,2011
HALMASHAURI ya Mji wa Mpanda mkoa wa katavi imeweza kukusanya mapato kwa asimia 110 kutokana na majaribio ya mabadiliko ya utaratibu wa ukusanyaji mapato ya Halmashauri hiyo.
Kaimu Mkurugenzi wa Mji ndugu Joseph Simon Mchina aliliambia JamboLeo juzi kuwa katika kipindi cha mwezi Februari halmashauri yake iliamua kufanya utafiti wa namna ya kuborsha mapato ya halmashauri hiyo kutokana na vyanzo vyake viwili vya mapato kati ya vilivyopo katika halmashauri yake.
Alisema kuwa maeneo ambayo waliamua kuyafanyia utafiti na katika ushuru wa masoko ili kuwa njia bora ya ukusanaji ushuru wa masoko manne yaliyoko Mpanda mjini ambapo kwa kuanzia Mchina alisema halmashauri yake iliamua kufanyia utafiti soko kuu la wilaya ya Mpanda lililoko chini ya halmashauri yake.
Alisema katika utafiti huo ulikuja baada ya halmashauri kunekana haipati mapato ya kutosha kutoka katika vyanzo vyake vya mapato licha ya kuwa na vyanzo vingi hali iliyopelekea kuongeza ushuru kwa wafanyabiashara wa masoko ya mjini hapa hali iliyozua kukuelewana baina ya halmashauri na wafanyabiashara hao hadi suluhu ilipopatikana ya kushusha ushuru huo.
Alisema kimsingi lengo la kutafuta namna ya kuongeza mapato iliendelea kubaki pale pale na hivyo kuipelekea halmashauri kuamua kutafuta namna bora ya ukusanyaji ushuru ili kuziba mianya ambayo ingebainika kukosesha mapato halmashauri.
Kaimu mkurugenzi Mchina alisema kuwa halmashauri iliwahamasisha wafanyabiashara wenyewe kulipia ushuru wa biashara zao katika ofisi za halmashauri bila kupitia kwa mzabuni na watendaji wa soko ambapo kabla ya kuendesha zoezi hilo halmashauri ilikuwa ikikusanya asilimia 30-40 kwa mwezi lakini baada ya kukusanya kwa wafanyabiashara katika kipindi cha mwezi februari halmashauri imeweza kukusanya kwa asilimia 110.
Alisema hapo awali halmashauri ilikuwa ikikusanya kiasi cha shilingi milioni 2.2 – milioni 2.5 kwa mwezi katika soko kuu lakini kwa kubadili mfumo wa ulipaji ushuru moja kwa moja kwa wafanyabiashara hao katika mwezi februari halmashauri iliweza kukusanya shilingi milioni 4.8 katika makusanyo lengwa ya shilingi milioni 4 kwa mwezi.
Kufuatia mafanikio hayo kaimu mkurugenzi huyo alidai kuwa hivi sasa halmashauri yake inaangalia uwezekano wa kuwa na utaratibu mpya wa ukusanyaji mapato ya ushuru wa masoko baada ya kubaini kuwa mzabuni anayepewa jukumu la kukusanya mapato anapata pesa nyingi lakini anawasilisha kidogo katika halmashauri.
Alisema endapo wataamua kubakiza wazabuni katika ukusanyaji mapato ya halmashauri atapendekeza iwe ni kwa baadhi ya mapato yasiyohesabika tu na kuwa uzoefu umeoneka kwa mamlaka ya mapato nchini kupokea mapato yak e moja kwa moja toka kwa wafanyabiashara na kufanikiwa bila kupitia kwa mzabuni isipokuwa kwa baadhi ya mapato kama vile kodi za vyombo vya moto.
Kwa muda mrefu halmashauri ya mji wa Mpanda imekuwa ikikabiliwa na ukata kutokana na makusanyo duni ya mapato ya halmashauri hali inayopelekea kushindwa kukabiliana na baadhi ya kero za mji huo ikiwa ni pamoja na changamoto ya mifereji kukosekana katika barabara nzuri za mji huo.
Mwisho.
POLISI
JESHI la polisi mkoani Rukwa linawashikilia watu wawili kwa tuhuma za kukutwa na meno 147 ya kiboko na tembo yenye thamani ya Tshs 6,580,000 katika wilaya ya Mpanda mkoa wa Katavi.

Tukio hili limetokea Januari 23 mwaka huu majira ya sa saa 5:00 usiku baada ya jeshi la polisi pamoja na askari wa wanyama pori wa mbuga ya Taifa ya Katavi kuweka mtego nje kidogo ya kijiji cha Stalike Wilayani Mpanda.

Wananchi baada ya kubaini kuwepo kwa njama za kusafirisha meno ya kiboko na Tembo akiyatoa katika Hifadhi ya Taifa ya katavi walitoa taarifa kwa Askari wa wanyamapori na kuandaliwa mtego ulifanikisha kunasa meno 146 ya tembo na kiboko na Risasi tisa za bunduki mbili za aina ya SMG na SAR.

Aliyekamatwa na men ohayo ni ndugu Mussa David (35) mkazi wa kijiji cha Muze Wilayani Sumbawanga mkoa wa Rukwa kati ya hayo meno 74 ya Kiboko yalikuwa yamehifadhiwa ndani ya begi la nguo pamoja na jino moja la tembo.

Mbali na meno aliyokutwa nayo aliweza kueleza kinaga ubaga kuwa mengine yapo nyumbani kwake katika kijiji cha Muze ambako askari hao walipofika nyumbani kwake aliwaonesha shehena ya meno 72 ya kiboko hivyo kufanya idadi ya meno kuongezeka na kufikia 146 yenye thamani ya shilingi milioni 2,500,000 na jino moja la Tembo lenye thamani ya shilingi milioni 4,080,000.

Mara baada ya kukamatwa na nyara hizo aliweza kukiri kuwa amekuwa kinara wa biashara haramu ya meno ya tembo nay a kiboko na kuwa soko lake kubwa liko nchini za Burundi na Congo DRC.

Akithibitisha tukio hilo Kamanda wa Polisi mkoani Rukwa Isuto Mantage amesema meno, hayo yalikutwa yamefukiwa chini ya ardhi pamoja na risasi Tisa za bunduki aina ya SMG na SAR shambani kwa ndugu Romwadi Isobila(46) na kwamba watuhumiwa wote watafikishwa mahakamani mara baada ya upelelezi wa awali kukamilika.

MWISHO


January 15, 2011
WANAFUNZI  2136 wa Kata ya Kibaoni wilaya ya Mpanda mkoani Katavi watanufaika na msaada wa Kilogramu 450 za sukari zilizotolewa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni mbunge wa Jimbo la Katavi.
Sukari hiyo iliyokabidhiwa juzi Januari 14,2011 na Msaidizi wake katika jimbo la Katavi Charles Kanyanda imegawiwa kwa shule za kata ya Kibaoni za Msingi na shule ya sekondari ya kata hiyo iitwayo Mizengo Pinda sekondari itawasaidia wanafunzi kupata uji wakati wa masomo katika shule hizo.
Akikabidhi sukari hiyo ndugu Kanyanda ambaye ni msaidizi wa Mheshimiwa Pinda katika jimbo la Katavi ambalo kata ya Kibaoni ni mojawapo katika ya kata zinazounda jimbo hilo alisema kuwa sukari hiyo imetolewa na mbunge wao Mheshimiwa Pinda kwa lengo la kuanzisha utaratibu wa kutoa
chakula cha mchana kwa wanafunzi kama ambavyo serikali imekuwa ikisisitiza kuwepo kwa utaratibu huo mashuleni.
Alisema serikali za vijiji zitambue kuwa shule zilizoko katika maeneo yao ni mali ya serikali ya kijiji na hivyo ziatakiwa kuanza kuwajibika kwa masuala yote ya uendeshaji wa shule hizo hasa katika kuhakikisha wanafunzi wanaanza kupata mlo wa mchana mashuleni ili kupunguza utoro na kuongeza ufanisi mashuleni
Mheshimiwa Waziri Mkuu ametoa sukari kiasi cha mifuko 45 ya kilogramu hamsini kila mmoja kwa shule ya msingi Kakuni iliyoko kijijini kwao
Kibaoni, mifuko 15 yenye uzito wa kilogramu 50 kila mmoja kwa shule ya sekondari ya Mizengo Pinda na shule za msingi za Ilalangulu na Mirumba kiasi cha mifuko 15 kila moja mifuko yenye uzito wa kilogramu hamsini kila mfuko.
Afisa kutoka idara ya Elimu ya Halmashauri ya wilaya ya Mpanda ndugu Venance Tesha akitoa shukrani kwa niaba ya Halmashauri alisema kuwa sukari iliyotolewa na Mheshimiwa Waziri Mkuu kwa shule za Kata ya Kibaoni ni changamoto kwa wazazi wa kata hiyo kuanza kujipanga ili kuuendeleza utaratibu wa utoaji uji na chakula mashuleni mara baada ya sukari hiyo kuisha.
“Wazazi na walezi wa kata hii mnatakiwa kuanza kujipanga sasa ili kuendesha michango itakayoendeleza utaratibu wa utoaji chakula mashuleni pindi sukari hii itakapoisha!!” alisema Tesha
Alisema licha ya kuwa Halmashauri inamshukuru Mheshimiwa Pinda bali inatoa shukrani za dhati na  pongezi nyingi kwake kwa kutoa sukari ambayo imewapa changamoto halmashauri kuhakikisha utaratibu huo wa kutoa chakula mashuleni hasa katika shule za msingi unaendeshwa katika shule zote wilayani Mpanda.
“Labda niseme kwamba kitendo alichokifanya Mheshimiwa Pinda ni kutupatia shughuli ya kufanya kwakuwa kama bosi wako kaanzisha uji shuleni katika kata zilizoko jimboni kwake wewe unangoja nini
kuanzisha huo utaratibu katika maeneo mengine, lazioma kama halmashauri tumshukuru Mheshimiwa Waziri Mkuu kwa kutuamsha” Alisema Tesha.
Baadhi ya walimu wa shule za msingi katika kata ya kibaoni wakizungumza katika hafla fupi ya makabidhiano hayo walisema kuwa mpango wa utoaji uji shuleni utapunguza utoro na kuongeza ufanisi kwa wanafunzi katika kujifunza.
“Unajua mwanafunzi wakati wa mchana huwa hawasomi hata kama wako darasani kwa sababu ya njaa! Hata kama mwalimu ukiingia unagundua kuwa humu darasani wanaonisikiliza ni wachache wengine wanakuwa wameshabanwa na njaa na hivo kumbu kumbu inakuwa imepungua sana” alisema mwalimu Mwakifuna wa shule ya msingi Kakuni
Alifafanua kuwa licha ya kuwa uji utapunguza utoro mashuleni lakini pia utajenga mazingira bora ya kujifunza katika vipindi vya mchana na kujenga hamasa ya kuanza shule  kwa watoto wanaokwepa kuanza shule katika jamii.
Walimu hao walimuomba Mheshimiwa Waziri Mkuu siku moja afike shuleni hapo kushuhudia namna wanafunzi wanavyoufurahia uji wakiwa shuleni na kushirikiana nao japo siku moja.
MWISHO.
Na Willy Sumia, Katavi
ASKARI wa jeshi la mgambo katika Halmashauri ya Mji wa Mpanda Mkoa mpya wa Katavi wamenusurika kipigo kutoka kwa wafanya biashara wa masoko matatu tofauti  kufuatia kupandishwa kwa ushuru wa masoko hayo.
Vurugu zilianza mara baada ya askari hao kufika katika masoko yaliyoko mjini hapa  kukusanya ushuru ambao umegomewa na wafanya biashara hao kwa madai ya ongezeko kubwa la ushuru kuliko hali halisi ya kipato cha biashara zao sokono hapo.
Tukio hilo limetokea jana katika muda tofauti mara baada ya askari wa mgambo hao pamoja na wakala wa kukusanya ushuru wa masoko ya mji kufika katika maeneo yao kwa lengo la kukusanya ushuru ambao unapingwa na wafanya biashara hao kwa kile kinachodaiwa na wafanya biashara hao kuwa ni ongezeko kubwa la ushuru.
Akizungumzia matukio hayo katibu wa wafanyabiashara wa Mji huo Amani Mahela ametoa wito kwa Mkurugenzi wa Mji kufika kwenye masoko hayo na kufanya mazungumzo na wafanya biashara badala ya utaratibu anaoutumia sasa wa kutoa matangazo kwenye vyombo vya habari akiwataka walipe ongezeko hilo la ushuru kabla ya kufanya mazungumzo nao.
Diwani wa kata ya Kashaulili John Matongo  amesema kuwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji ameitisha kikao cha Madiwani wa kata tatu na viongozi wa wafanyabishara toka katika masoko yaliyo na mgogoro wa
ushuru  ili kujadili namna ya kutatua tatizo hilo
Halmashauri ya Mji wa Mpanda imebandika matangazo katika masoko hayo matatu akiwaeleza wafanya biashara kuwa wale ambao hawatakuwa tayari
kulipa ongezeko la ushuru waondoke katika maeneo ya masoko hayo Kaimu mkurugenzi wa Mji Mpanda Josefu Mchina aliwaeleza waandishi wa habari ofisini kwake kuwa ushuru ni suala la kisheria na huwa lina
mchakato wake katika kuuanzisha, kuongeza  au kuupunguza kabla ya kuanza utekelezaji hivyo ushuru unaolalamikiwa ni halali kisheria na pia umezingatia hali halisi ya bishara na mahitaji ya maendeleo katika
masoko na mji kwa ujumla.


Na WALTER  Mguluchuma
Mpanda
Madiwani wa chama cha mapinduzi (CCM) katika Halmashauri ya Mji wa Mpanda wamesusia sherehe ya kumuaga Mkurugenzi wao kutokana na itikadi za siasa
Tukio hilo limetokea hapo jana ambapo Halmashauri ya Mji wa Mpanda iliandaa sherehe ya kumuaga Mkurugenzi wao ambaye alikuwa anastaafu utumishi Bwana Henry Haule
Sherehe za kumuaga Mkurugenzi huyo zilifanyika katika Ukumbi wa Katavi Resort mali ya Abrahamu Kombe ambaye anadaiwa na Madiwani hao kuwa aliwasariti kwenye uchaguzi Mkuu na kuisaidia Chadema
Madiwani hao baada ya kupata taarifa za sherehe za kumuaga mkurugenzi wao kweny Ukumbi wa Katavi walianza kupinga na kutaka sherehe hizo zifanyike kwenye Ukumbi wa Idara ya Mji ambao hata hivyo ulikuwa umeandaliwa kwa shughuli za Mkutano wa wawekezaji na Waziri Mkuu
Sherehe hizo zilianza huku ndani ya Ukumbi kukiwa na madiwani wawili wa kata za kashaulili na makanyagio ambao ni wa Chadema
Wakati sherehe zikiendelea madiwani hao waliendelea na kikao chao nje ya Ukumbi huo kwa lengo la kuendelea na msimamo wao huo Hata hivyo wakati sherehe zikienda mwisho waliingia madiwani wawili wa Chama hicho ambao ni Enock Gwambasa ambaye pia ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji huo pamoja na diwani Willy Mbogo
Walipo hojiwa Madiwani hao sababu iliowafanya waingie mwishoni mwa sherehe walisema tulikuwa na mvutano na wenzetu ila sisi tumeamua kuingia kwenye sherehe
Na Peti Siyame umbawanga
MWENDESHA  pikipiki  aitwaye Ramadhani  Sood (25)  amefariki  dunia baada ya kugongwa na  gari  katika kijiji cha  Makanyagio  katika barabara  ya Mpanda –Shanwe iliyopo  wilayani Mpanda katika mkoa wa Rukwa.
Kamanda  wa Polisi Mkoa wa Rukwa , Isuto Mantage  alisema  kuwa  ajali hiyo  ililihusisha   basi la abiria aina  ya scania  yenye  namba  za usajili  T 519  ACV iliyokuwa ikiendeshwa  na dereva  aitwaye Masoud
Musa (32) mkazi wa  Makanyagio  mjini Mpanda
Kwa mujibu wa Kamanda huyo wa Polisi  gari  hilo  la  abiria lilimgonga  mwendesha pikipiki  Ramadhani  mkazi wa Makanyagio aliyekuwa  akiendesha pikipiki aina ya  Honda  yenye  namba  za
usajiri  T. 612 ANT na kumsababishia  majeraha  makubwa .
“Ramadhani  aliyekuwa  mahututi  ambapo  alikuwa na  majeraha makubwa mwilini  alifariki  muda mfupi  baada ya kufikishwa  kwenye  hospitali  ya  wilaya ya Mpanda  kwa matibabu” alisema  Mantage .
Kamanda Mantage  alisema kuwa  chanjo  cha  ajali  hiyo  bado hakijajulikana  na kwamba  dereva  wa  gari  alikamatwa  na atafikishwa  mahakamani  mara  baada ya  uchunguzi  wa awali kukamilika

Monday, September 13, 2010

GAZETI LA LEO - MPANDA

NKASI - WAMPEMBE - 17 MBARONI KWA KUVAMIA KITUO CHA POLISI
WATU kumi na saba wanashikiliwa na jeshi la polisi mkoani Rukwa kwa tuhuma za kuvamia kituo cha polisi kwa lengo la kutaka kukiteketeza kituo hicho kwa moto.
Kamanda wa polisi mkoani Rukwa Isuto Mantage amesema Novemba 30,2010 ofisini kwake kuwa wanaoshikiliwa ni wanakijiji wa kijiji cha Wampembe wilaya ya Nkasi mkoani Rukwa baada ya jaribio la kutaka kukitekeza kwa moto kituo kidogo cha polisi cha Wampembe kwa lengo la kumuua mtu mmoja waliyekuwa wanadai kuwa ni mchawi.
Amesema kuwa awali katika kijiji hicho kulitokea msiba wa kijana aliyetajwa kwa jina la Joseph Kapelo (19) baada ya kuugua muda mfupi mnamo Novemba 22, 2010 ambapo kijana huyo aligua majira ya saa mbili asubuhi nakufariki saa tano mchana kifo kilichozua mijadala kijijini hapo wakazi wengi wakidai kuwa marehemu alikuwa amefariki kutokana na imani za kishirikina.
Amefafanua kuwa baada ya kupata taarifa za kifo hicho wananchi walianza kukusanyika katika msiba na kuanza kupanga mikakati ya kummaliza baba wa marehemu aliyetajwa kwa jina la ndugu Daudi Kapelo (76) kwa madai kuwa ndiye aliyamuua mwanae huyo kwani ni miezi miwili tu tangu kijana mwingine mtoto wa huyo mzee alifariki katika mazingira ya kutatanisha kama ilivyotokea katika huo msiba.
Amesema kuwa wakati wananchi hao wakipanga mikakati hiyo taarifa zilifika kituo kidogo cha polisi Wampembe ambapo polisi wa kituo hicho waliweza kuchukua hatua ya kumuokoa Mzee huyo lakini kabla hawajafika msibani tayari Mzee huyo alikuwa ameshaanza kushambuliwa na wananchi na kuokolewa na polisi na mgambo na kasha kuchukuliwa na kwenda kuhifadhiwa kituo cha polisi kwa usalama wake.
Amesema wakati wananchi hai wakielekea kuzika walichukua jeneza la marehemu na kwenda nalo hadi kituo cha polisi ambapo waliliweka jeneza hilo hapo kituoni na kudai wanataka Mzee Daudi Kapelo atolewe humo ndani wammalize naye akazikwe na mwanae na kuanza kushambulia kituo hicho kwa mawe hali iliyopelekea askari kupiga risasi hewani lakini wananchi hao hawakuweza kuogopa na kuanza kumshambulia askari huyo na kuibua mapigano baina ya askari na wananchi wapatao 300.
Amesema kuwa wananchi hao baada ya kutawanyika walikimbia wote wakiwa tayari wameshawasha moto kituo cha polisi kikiungua ambapo askari polisi na mgambo kwa kusaidiana na viongozi wa kijiji walifanikiwa kuuzima moto huo na wananchi hao waliweza kurudi usiku wakachukua maiti ya merehemu na kwenda kuzika usiku huo huo.
Amesema mapambano hayo yaliendelea ambapo mwananchi mmoja Imelda Kayanda (46) alipigwa risasi na kufariki na Agnes Kisori(21) alijeruhiwa mguuni huku vitu vilivyoharibiwa vikiwa ni pamoja na solar panel ya kituo, vioo vya kituo vyote kwa pamoja vikiwa na thamani ya shilingi laki tano.
Amesema majeruhi walipelekwa kituo cha afya Wampembe na baadae hospitali ya wilaya ya Nkasi kupata matibabu ambapo hali zao zimeelezewa kuwa zinaendelea vema.
Amesema tayari jeshi la polisi limewakamata ndugu Zakaria Francis (28), Ikombe Yustini (39), Stephano Kambe (18), Benard Kabeja (16) na John Kapandila (22).
Wengine waliokamatwa amewataja kuwa ni ndugu Said Diwali (36), Vido Tuwakazi (21), Abdalah Vicent (19), Sylveter Kapala (17), Richad Bushota (19), John Mathias (58), Wilbroad Chambi (16) na Kapondo Anatoli (23) na wengine wane wote wakazi wa kijiji cha Wampembe wilaya ya Nkasi.
Kamanda wa Polisi amesema wakati watuhumiwa hao wote watafikishwa mahakamani mara baada ya upelelezi kukamilika na kuwa wengine waliokimbia watafuatiliwa hadi wakamatwe ili sheria ichukue mkondo wake.
Aidha kamanda Mantage ametoa wito kwa wananchi kuacha tabia ya kujichukulia sheria mkononi na tabia mbaya ya kuvamia vituo vya polisi nchini hapa nchini kuwa vinalipeleka taifa kusikojulikana kutokana na ukweli kuwa hizo ni dalili za kuondoa misingi ya amani na utulivu katika jamii.
MWISHO
MBUNGE mmoja wa Chama Cha Mapinduzi wilayani Mpanda amelalamikiwa kuwafanyia kitu mbaya vijana watatu akiwemo mlemavu asiyekuwa na uwezo wa kutembea.
Taarifa zilizolifikia gazeti hili zimeeleza kuwa mbunge huyo mwenye sifa ya kuitwa Mbuyu mdogo amewadhulumu vijana watatu waliokuwa watumishi wa ofisi yake ya bunge katika jimbo lake ofisi zilizoko mjini Mpanda baada ya kuwatumikisha bila kuwalipa mishahara yao halali.
Wakiongea kwa uchungu vijana hao pamoja na binti mmoja mlemavu wa miguu aisyeweza kutembea kwa miguu ya kawaida walidai kuwa mbunge huyo amewadhulumu zaidi ya shilingi miliono moja na laki nane zikiwa ni mishahara na posho za kazi zaidi ya shilingi milioni moja na laki mbili.
Kijana mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Peter Pulwila Panta aliyekuwa ameajiriwa kwa kazi ya udereva na kupewa kitambulisho chenye nambari 001 alisema wamekuwa wakimdai mbunge huyo mishahara yao lakini cha kusikitisha amekuwa akidai kuwa hizo pesa hajaletewa kutoka ofisi ya bunge kitu ambacho si kweli kutokana na maelezo yaliyoko katika barua yenye kumb namba FA.155/2006/01/70.
Alisema licha ya kuwa barua inaagiza kuwalipa mshahara wa kiasi cha shilingi 150,000 kwa mwezi lakini yeye aliwaeleza kuwa watakuwa wanalipwa shilingi laki moja kila mwezi na kuwa alikuwa anakidai kuwa anawalipa kutokana na mshahara wake wa ubunge ihali barua inaonesha kuwa fedha hizo zinatumwa kila mwezi katika akaunti ya mbunge huyo kwa ajili ya mishahara na posho.
Naye binti mwenye ulemavu aliyekuwa akifanya kazi kama mhudumu wa ofisi ya mbunge huyo alisema kuwa tangu mwaka 2005 alikuwa akifanya kazi na kupewa hela ya soda tu shilingi 20,000/= tu kila anapodai mshara wake na kuwa ukosefu wa mshahara kumepelekea mwanaye anayesoma katika shule ya sekondari Mwese kuzuia kuendelea masomo kutokana na madeni ya ada.
Alipofuatwa na mwandishi wa habari ofisini kwake kujua kulikoni anadaiwa na watumishi wake akiwemo mlemavu wa miguu lakini mbunge huyo hakuweza kupatikana badala yake alikuwepo mtu aliyejieleza kuwa ni katibu wa mbunge huyo ingawa alikataa ktaja jina lake aliyeeleza kuwa mbunge wake yuko katika kikao CCM
Juhudi za kumtafuta kwa simu mbunge huyo zilifanikiwa ambapo mbunge huyo alijibu katika simu kuwa anahitaji kuonana na mwandishi wa habari.
Cha kushangaza ni kuwa alikwenda mwandishi ofisini kwake kuzungumzia suala la madeni na kuzomewa alikozomewa wakati wa mkutano wa hadhara katika kijiji kimoja mbunge huyo alimsihi mwandishi huyo asiandike taarifa yoyote mbaya kumhusu na kumpatia kiasi cha shilingi elfu ishirini kwa ajili ya kumziba mdomo pesa ambazo mwandishi alizikataa na kuondoka
Uchunguzi umebaini kuwa madai hayo na mengine mengi yalishawahi kufikishwa katika ofisi za CCM wilaya ya Mpanda na kukosa suluhu ambapo mbunge huyo amekuwa akijinadi kuwa ni mtaalamu wa propaganda, mbuyu mdogo anataka kugombea mwakani kutetea kiti cha ubunge hivyo wasimjadili kuhusu madeni yake.
Mbunge huyo alijikuta akitemwa katika kura ya maoni ndani ya chama chake katika uchaguzi mkuu wa 2010 nchini Tanzania
MWISHO

MILIONI KUMI HIZI ZIMETUMIKA KWELI NAMNA HII
ZAIDI ya shilingi milini 10.1 zimetumika kwa ajili ya kuwanunulia sare za shule na kuwalipia ada na chakula watoto yatima na wanaoishi katika mazingira magumu wilaya ya Mpanda mkoani Rukwa
Mratibu wa asasi isiyokuwa ya kiserikali ya SHDEPHA + tawi la Mpanda Mwalimu Euzebius Ngulusha alisema hayo jana (Novemba 3, 2009) wakati wa hafla fupi ya kuwakabidhi sare, chakula na mahitaji ya shuleni watoto yatima na wanaoishi katika mazingira hatarishi wapatao 54 iliyofanyika katika ukumbi wa SHDEPHA + mjini Mpanda.
Alisema katika kipindi cha Januari hadi Oktoba mwaka huu zaidi ya shilingi milini 10.1 zimetumika kuwahudumia watoto 204 wanaoishi katika mazingira hatarishi, yatima na watoto wanaoishi na Virusi vya UKIMWI wilayani Mpanda fedha ambazo zimetoka kwa wafadhili mbalimbali ikiwa ni pamoja na shirika la Kimarekani la WALTER REED la nchini Marekani.
Alisema shirika lake limelipia ada za sekondari na kuwanunulia sare za shule watoto wanaosoma katika shule za sekondari wapatao 150 kwa gharama ya shilingi 8,304,300/= na watoto wanaosoma shule za Msingi wapatao 35 na wachache wanaotoka katika mazingira hatarishi.
Alisema kiasi cha shilingi 1,800,000 zimetumika kuwanunulia mahitaji ya shuleni kama vile daftari, kalamu, vihifadhio, mifuko ya shule na vifaa vya kuchorea vya wanafunzi hao ili nao wajisikie kama sehemu ya jamii.
Akiongea kwa niaba ya Mkurugenzi wa Mji wa Mpanda afisaelimu wa sekondari wa Halmashauri ya Mji wa Mpanda Said Mwapongo aliwashukuru viongozi wa asasi hiyo ya SHDEPHA + kwa kufanya kazi ya kuwasaidia wanaohitaji katika jamii na kuvishinda vishawishi wanavyokumbana navyo vishawishi ambavyo amesema vinawapelekea kushikwa na tamaa ya kutumia fedha hizo bila kujali ni za nani.
Alisema moyo wa kuwafikishia walengwa ambao hawakujua kama wanaletewa nini ni moyo wa kipekee na wa kiungwana ambapo amewasihi kutokukata tamaa na kuwa Mungu peke yake ndiye atakayewalipa kwa kazi njema hiyo.
Mwapongo aliwasihi wanafunzi hao kuitumia misaada waliyoipata na wanayoendelea kuipata kwa kusoma kwa bidii, kuwa na heshima katika jamii ili kuwawezesha kufikia malengo yao ambayo ni kuwaondoa katika lindi la maisha ya masikitiko na umasikini uliopindukia.
MWISHO

WANANCHI HAWA WAMECHUKIA DILI ZA POLISI AU NI HASIRA KWELI?
WANANCHI wenye hasira wamefanikiwa kuliua jambazi lililokuwa likitafutwa na jeshi la polisi mkoani Rukwa baada ya kumkuta akiiba magunia ya mpunga
Akiyeuwawa ametajwa kwa jina la Revocatus Benedicto Katunga mwenye umri wa miaka 33 mkazi wa Nsemulwa mjini mpanda ambaye aliuwawa na wananchi Septemba 23,2009 saa kumi na mbili asubuhi mara baada ya kukutwa akiiba magunia ya mpunga katika mashine ya kusaga ya mfanyabiashara anayejulikana kwa jina la Kasimu lyanga maarufu kwa jina la Usayi.
Kamanda wa polisi mkoani Rukwa Isuto Mantage aliwaeleza waandishi wa habari kuwa siku ya tukio marehemu anayesadikiwa kuwa ni jambazi sugu aliyekuwa anatafutwa na jeshi hilo alikutwa na wananchi akiwa katika harakati za kuiba magunia ya mpunga ambapo alikuwa ameshaiba magunia manne ya kuyatoa nje ya jingo hilo .
Alisema baada ya kumkuta marehemu huyo wananchi hao walianza kumhoji lakini akawa anawajibu maneno ya jeuri kwa sauti kubwa iliyowaamusha majirani wengine waliofika hapo na kumkuta jambazi huyo aliyekuwa akitafutwa na jeshi la polisi mkoani Rukwa kwa tuhuma za kushiriki katika matukio kadhaa ya uhalifu walianza kumpa kipigo hadi akapoteza fahamu ndipo wakawaita polisi kituo cha Mpanda.
Alisema kamanda Mantage kuwa polisi walipofika eneo la tukio walimchukua marehemu na kumwahisha hospitali ambako kabla ya kupewa huduma yoyote alifariki akiwa eneo la hospitali.
Kamanda alisema hakuna aliyekamatwa kuhusiana na tukio hilo ambapo alieleza kuwa marehemu alikuwa akitafutwa kwa kosa la kuvunja na kuiba vitabu katika shule ya msingi Katavi iliyoko mjini Mpanda na pia alikuwa na kesi mahakani ya kuiba kwa kutumia silaha
Kwa upande wao wananchi wa eneo la Mpanda Hoteli mjini Mpanda walionesha kusikitishwa kwao na mwenendo wa utendaji kazi wa jeshi la polisi wilayani Mpanda kwani jambazi huyo alikuwa ameshikana kukamatwa na jeshi hilo hadi walipomkamata wananchi wenyewe na kumpa hukumu ya kifo licha ya kuwa alikuwa na matukio mengi ya kutafutwa.
the end