Sunday, January 20, 2013

ZIARA YA NAIBU WAZIRI TAMISEMI MKOANI KATAVI

MWANZA SI SHWARI


JIJI LA MWANZA

Hali ya  jiji  la Mwanza  kwa  sasa  ni tete  baada ya  kuzuka  kwa  vurugu kubwa kati ya jeshi la polisi na  waendesha boda  boda  katika  jiji  hilo ambapo kwa  sasa  kila kona  ya jiji  wananchi  wametaharuki na  kukimbizana  kuhofia usalama  wao.

Mwandishi  wa mtandao huu  wa www.sumiampanda.blogspot.com  kutoka  Jijini Mwanza ameripoti kuwa vurugu hizo  zimesababishwa na  polisi ambao  wamekuwa  wakiwafukuza vijana hao katika vijiwe vyao  .

Hivyo kutokana na mvutano  huo  jeshi la  polisi  limelazimika  kutumia risasi  za moto  kuwafukuza  waendesha boda  boda  hao ni kuna taarifa   kuwa baadhi yao  wamejeruhiwa vibaya katika  vurugu  hizo .

Kutokana na vurugu  hizo kwa sasa  jiji la Mwanza  huduma  za  usafiri  zimesimama kwa muda  ili  kuepuka madhara  zaidi .
Habari zaidi  zitakujia hivi punde

Habari tulizozipata toka ofisi ya IGP Said Mwema ni kuwa kuanzia jana jeshi la polisi nchini limeanza operesheni maalumu ya kukagua vyombo vyote vya moto ili kubaini mapungufu na kuhakikisha yanarekebishwa ikiwa ni juhudi za kukabiliana na wimbi la ajali nchini.

MIMBA SHULENI ZIKOMESHWE- MWANRI


MHE. AGGREY MWANRI, Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa nchini akiwa katika kiti alipokuwa akisomewa Taarifa ya Mradi wa Maji ya kutega katika kijiji cha Kilida wilaya ya Mlele mkoani Katavi

 UMENIKOSHA POKEA ZAWADI; Mkuu wa wilaya ya Mpanda, Paza Mwamlima akimpa zawadi kijana aliyekuwa akicheza ngoma ya kisukuma katika mkutano wa hadhara kijiji cha Kilida wilaya ya Mlele












  SERIKALI YABADILI UTARATIBU WA MICHANGO MASHULENI, YAPIGA MARUFUKU KURUDISHA WANAFUNZI KUFUATA MICHANGO NYUMBANI





 Naibu Waziri akikwa ameketi katika kiti akipokea taarifa ya mradi wa Maji ya kutega mlimani katika kijiji cha Kilida wilaya ya Mlele mkoani Katavi

















 MWENYEKITI wa kijiji cha Kilida akifungua mkutano wa hadhara ambao mgeni rasmi ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu TAMISEMI , Aggrey Mwanri




 TUNASIKILIZA KWA MAKINI




 BURUDANI TAMU KABISA



 MBINU MBADALA KATIKA KUSHIRIKI MIKUTANO







 NAWASALIMIA NDUGU ZANGU








 Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu TAMISEMI, Aggrey Mwanri akiweka jiwe la msingi katika mradi wa Maji ya kutega katika kijiji cha Kilida wilaya ya Mlele mkoani Katavi,
 Mhe. Mwanri akifungua maji baada ya kufungua mradi wa Maji wilaya ya mlele mkoani Katavi


 POKEA TAARIFA MKUU.

 MKAO WA KUSIKILIZA TAARIFA YA WANANCHI






BURUDANI; Hii unaweza kuiita Sabuwufa ya Kifipa, wananchi wakitumbuiza katika mkutano wa hadhara katika kijiji cha Kilida

Na Willy Sumia, Mpanda
SERIKALI imepiga marufuku tabia ya baadhi ya walimu kuwarudisha
wanafunzi nyumbani kwa sababu ya kutolipia michango mbali mbali ya
shule na kwa kukosa sare za masomo.

Hayo yalibainishwa jana na Naibu Waziri kutoka ofisi ya Waziri Mkuu
Tawala za Mikoa Serikali za Mitaa, Mhe Aggrey Mwanri alipokuwa
akihutubia mamia ya wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika
katika uwanja wa Kashaulili mjini Mpanda akihitimisha ziara yake
katika halmashauri ya mji wa Mpanda.

Alisema kumekuwa na mtindo kwa baadhi ya shule kuwarudisha wanafunzi
nyumbani kwa kisingizio cha kukusanya michango lakini wanasahau kuwa
muda ule ni muda wa masomo kwani siku na saa za masomo zimehesabiwa na
inapopotea dakika moja kwa mwanafunzi kukaa bila kusoma haiwezi
kufidiwa tena hivyo serikali imeliona na kuamua kuchukua hatua.

Alisema kuanzia jana (Januari 20,2013) hakuna kumrudisha mwanafunzi wa
shule ya msingi na sekondari kwa sababu hajamalizia michango ya shule
na wala eti kwa sababu hana sare za shule husika, badala yake walimu
washirikiane na uongozi wa kata kuwawajibisha wazazi wasiokamilisha
michango shuleni na kuwanunulia wanafunzi sare za masomo.

'' Walimu nisikilizeni, kuanzia leo hakuna ruhusa kwa mwalimu
kumrudisha mwanafunzi nyumbani eti kutafuta michango, mnataka
wakafanye vibarua huko? Mzigo wa michango ya shule na sare ni wa
wazazi na walezi wao siyo wa mtoto tena msiwape barua watoto
kuwapelekea wazazi wao, pelekeni katika ofisi za kata kuna kamati ya
maendeleo ya Kata WDC" alisema Mhe. Mwanri

Alisema unapomrudisha mwanafunzi nyumbani akachukue mchango wa shule
maana yake ni kwamba asirudi shule kama hajapewa mchango na hapo ndipo
unadhoofisha maendeleo ya mwanafunzi kitaaluma hivyo kama umeajiriwa
na serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania huruhusiwi kuwarudisha
wanafunzi wakatafute michango

Akizungumzia michango mingi mashuleni Mwanri alisema hivi sasa
serikali imebadili utaratibu wa kurasimisha michango kwa kupitia ofisi
ya Katibu Tawala wa Mkoa husika na hivyo kila shule itakayokaa na
wazazi na kupanga michango yao ya shule kwa maendeleo ya shule yao
lazima kwanza mapendekezo hayo yapelekwe kwa Katibu Tawala wa Mkoa huo
ili ayapitie mapendekezo hayo na kujiridhisha ndipo atoe kibali cha
kuanza kutoza michango hiyo

Alisema hivi sasa kila shule ianze utaratibu wa kuita wazazi na
kuangalia ichakavu wa madawati yaliyopo na kutolea mapendekezo ya
ukarabati wake ili yaweze kutumika badala ya kuendelea na mtindo wa
kila mwaka wanafunzi kudaiwa kwenda na madawati shuleni kwani kila mtu
anajiuliza madawati hayo hayajai shuleni huko, ni bora uwepo utaratibu
wa kuangalia mapungufu ndiyo yachangiwe na wazazi

Aliwaagiza wakurugenzi watendaji katika halmashauri kukagua na
kujiridhisha namna majembe, mapanga na madawati yanavyotumika
mashuleni kwani kuna baadhi ya sehemu wanafunzi wanaagizwa kuwenda na
majembe mapya yenye mpini lakini wakifika shuleni majembe mapya
yanakusanywa na kuwekwa badala yake siku ya kulima ikifika wanafunzi
wanagawiwa majembe ya zamani.

Naibu Waziri Mwanri anatarajia kukamilisha ziara yake katika mkoa wa
Katavi Jumatano na kurejea mjini Dodoma kwa ajili ya kikao kijacho cha
bunge.

 KAZI IPO NZITO; Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu TAMISEMI, Aggrey Mwanri akikagua bati katika ghala la Mazao kijiji cha Mirumba kama ni Geji 28 wilaya ya Mlele Januari 16, 2013.

 Baadhi ya wataalamu wa mkoa wa Katavi wakijipatia picha za ukumbusho katika hoteli ya kitalii ya Katuma Lodge iliyopo katika Hifadhi ya Wanyama ya Taifa ya Katavi mkoani Katavi kabla ya kuwasilisha taarifa ya serikali ya mkoa na wilaya kwa Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali na Mitaa, Mhe Aggrey Mwanri kabla kuanza ziara.




 Naibu Waziri TAMISEMI akisikiliza Taarifa ya Mkoa wa Katavi

 Kaimu Katibu Tawala mkoa wa Katavi, Lauteri Kanoni akiwasilisha Taarifa ya mkoa kwa Naibu Waziri TAMISEMI, Mhe Aggrey Mwanri



 Baadhi ya wataalamu wa mkoa wa Katavi wakipokea maelekezo kutoka kwa Mhe Mwanri

 Mhe Mwanri akipokea taarifa ya wilaya ya Mpanda kutoka kwa Kaimu Katibu Tawala wa wilaya hiyo, Kenneth Simuyemba

 Mhe Mwanri akipokea taarifa kutoka kwa Kaimu Katibu tawala mkoa wa Katavi, Lauteri Kanoni, kushoto kwake ni mke wake, Grace Mwanri
 Mhe Mwanri akipokea taarifa ya wilaya ya Mlele kutoka kwa Kaimu Katibu tawala wa wilaya hiyo, Epafrace Tenganamba. waliosimama meza kuu ni Mkuu wa wilaya ya Mpanda (suti ya bluu), Paza Mwamlima, mwenyekiti wa halmashauri ya mji Mpanda, Enock Gwambasa, mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Mpanda, Wilbroad Mayala na Kaimu katibu Tawala wa mkoa wa Katavi, Lauteri Kanoni


 Kaimu Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Mpanda, Patrick Mwakyusa akikabidhi taarifa ya halmashauri yake kwa naibu waziri

 Naibu Waziri OW-TAMISEMI Mhe. Aggrey Mwanri akitoa nasaha kwa watendaji wa mkoa wa Katavi baada ya kupokea taarifa ya mkoa huo.



 TUKO MAKINI MKUU; Baadhi ya wataalamu wa mkoa wa Katavi wakisikiliza maagizo na maelekezo ya wizara katika hoteli ya Katuma iliyopo Katavi National Park


 ASANTENI KWA UKARIMU WENU; Naibu waziri akiuaga uongozi wa Katuma Lodge baada ya mapumziko ya siku moja hotelini hapo


 Naibu Waziri akiwasili kijiji cha Mirumba kuweka jiwe la msingi mradi wa ghala la Mazao





 Taarifa ya Mradi wa Ghala Mirumba



 Naibu Waziri akipokea taarifa ya mradi wa ghala Mirumba



 Hakuna Mzaha; Naibu Waziri, Mhe Mwanri akikagua bati la kuezekea ghala kama kweli ni vipimo vinavyotakiwa kwa ajili ya majengo ya serikali geji 28.

 Naibu Waziri akibadilishana mawazo na mwenyekiti wa kijiji cha Mirumba wilaya ya Mlele


 Mhandisi kitimoto, kwa nini hamjaweka conduit pipe katika ukuta huu?


 Shangilia; Jiwe la msingi limewekwa katika mradi wa ghala la mazao Mirumba




 Mhandisi na mkandarasi mmmefanya kazi nzuri katika jengo hili, pongezi sana, ndivyo anavyosema Naibu Waziri wa TAMISEMI, Aggrey Mwanri



 Mhe Mwanri ni mwanamazingira mzuri, anapanda mti wa kumbu kumbu katika kijiji cha Mirumba


kazi inaendelea


Na Willy Sumia, Katavi
Naibu  Waziri wa nchi  Ofisi ya waziri mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi)  Mhe Aggrey Mwanri amewaagiza viongozi na Watendaji wa serikali kuhakikisha wanakomesha suala la mimba mashuleni.
Waziri Mwanri ametoa agizo hilo katika mkutano wa hadhara katika vijiji vya  Kilida Kata ya Mamba na Inyonga wilayani Mlele Mkoani Katavi katika ziara yake ya kukagua na kuhimiza shughuli za maendeleo katika mkoa wa ikiwa ni pamoja na kuangalia Halmashauri zinavyosimamia fedha za serikali zinazoletwa  kwa ajili ya shughuli za miradi mbali mbali ya maendeleo
 Amesema  katika taarifa ya mkoa imeelezwa kuwa asilimia ya wanafunzi wanaopata mimba imepungua kutoka asilimia sitini na tisa hadi sitini na saba hali inayoashiria kuwa tatizo linaendelea kwa kasi sana na kuwa endapo hatua za makusudi hazitachukuliwa suala la elimu kwa watoto wa kike itaendelea kudumazwa
Amesema kila mkoa na wilaya nchini zipo taarifa za tatizo la mimba kwa wanafunzi hivyo ipo haja ya watu kuwajibika katika kuhakikishani tatizo hili linaondoka kabisa na ni wajibu wa viongozi kuhakikisha suala la mimba linakomeshwa kabisa mashuleni na haitoshi kila mara viongozi kuripoti tu suala la mimba mashuleni bila kuchukua hatua kuchukuliwa kwa wale wahusika wanaofanya vitendo hivyo vya kuwapa mimba watoto wa kike.
“Haitakiwi kuripoti tu, pia inatakiwa kueleza ni hatua gani zimechukuliwa  kuhakikisha hao wanofanya vitendo hivyo wamechukuliwa hatua zipi za kisheria ili kukomesha vitendo hivyo, ukisikia mimba, kamata binti mwenye mimba, kamata wazazi wake weka msukosuko watakueleza mwenye mimba” Alisema Mhe. Mwanri.
Aidha katika taarifa ya mkoa wa Katavi kwa Mhe. Mwanri imeelezwa kuwa mimba kwa mkoa wa katavi zimepungua kutoa wasichana waliopata ujauzito mwaka 2011 walikua 63  na  mwaka 2012  mimba zilikuwa  61   sawa na upungufu wa asilimia tano taarifa ambayo haikueleza namna wanavyolishughulikia tatizo la mimba na kueleza wangapi walichukuliwa hatua za kisheria kulingana na makosa hayo.
Akiwasilisha taarifa hiyo Kaimu Katibu Tawala wa mkoa huo, Lauteri Kanoni amesema kuwa juhudi za kuwabana wanaotenda vitendo vya kuwapa ujauzito wanafunzi zinakwama kutokana na changamoto ya baadhi ya wazazi wa mwanafunzi mwenye ujauzito kushiriki katika mikakati ya kuficha ushahidi wakati wa kumtafuta mhalifu






























WANAFUNZI LAZIMA WAPATE CHAKULA CHA MCHANA SHULENI - MWANRI


Na Kibada Kibada –Katavi
 Viongozi wa Serikali wa Mkoa wa Katavi wametakitakiwa  kuhakikisha wanaweka utaratibu  wa wanafunzi wote wa shule za sekondari wanapatiwa chakula cha mchana kwenye shule zao.
Agizo hilo limelitolewaa leo(jana) na Naibu Waziri wa TAMISEMI Aggri Mwanri wakati  akiongea na viongozi wa serikali mkoani humo kwenye hoteli ya Katuma iliyoko katika hifadhi ya Taifa ya Katavi mara baada ya kusomewa Taarifa ya utekelezaji wa shughuli za maendeleo za Mkoa huo.
Mwaniri alisema kuwa ni vizuri viongozi  washirikiane na bodi za shule  zasekonari kukaa na wazazi wa wanafunzi wanaosoma kwenye shule za sekondari katika mkoa huo kupanga namna ya  kuhakikisha wanafunzi wanapata chakula cha mchana hapohapo shuleni kwao.
Kauli hiyo aliitoa kufuatia taarifa iliyosomwa mbele yake na Kaimu Katibu tawala wa Mkoa wa Katavi Lauteri Kanoni ambayo ilieleza kuwa ni wanafunzi asilimia 60 tu wanaosoma katika shule za sekondari za kata ndio wanaopata chakula katika mkoa wa katavi.
Alieleza kuwa ameshitushwa na taarifa hiyo ya baadhi ya shule wanafunzi kutopata chakula cha mchana ukizingatia mkoa wa katavi ni miongoni mwa mikoa inayozalisha chakula kwa wingi hapa nchini likiwemo na zao la mahindi
“Inawezekana kabisa wazazi wakawa hawajapewa elimu ya kutosha  juu ya namna  ya uchangia wa chakula cha wanafunzi mashuleni sasa ni juu yenu viongozi kuwaelimisha”alisema Mwaniri.
Akifafanua zaidi alieleza kuwa endapo mzazi wa mwanafunzi akishakuwa na elimu ya uelewa wa kuchangia chakula tatizo hilo halitakuwapo tena.
Naibu Waziri Mwanri ameanza ziara ya siku saba mkoani katavi yenye lengo la kukagua shughuli za Miradi ya maendeleo ili kuona fedha inayotolewa na serikali kama zinatumika ipasavyo kwa lengo lililokusudiwa na  miradi inayotekelezwa inalingana na thamani ya fedha iliyotolewa na serikali
Lengo linguine la ziara hiyo ni kuangalia namna halmashauri za mkoa huo zinavyoweza kukusanya mapato ya ndani na jinsi zinavyotumia kwa ajili ya kuwaletea maendeleo.
Miradi aliyoikagua kwa siku ya kwanza ya ziara yake hapo jana aliweka jiwe la msingi katika la kuhifadhia mazo ya chakula mbalimbali katika kijiji cha mirumba Kata ya Kibaoni Wilayani Mlele,kutembele a mradi wa ghala, mashine ya kusindika mpunga na kituo cha Habari cha Kilimo katika ya Mwamapuli.
Miradi mingine atakayotembelea katika ziara yake hiyo ni kuweka jiwe la msingi katika jingo la utawala Nsimbo Kata ya Nsimbo,kutembelea shamba darasa la miembe Nsimbo  pamoja na kuangalia ujenzi wa kituo cha Afya cha Inyonga ambacho kiombwa kigezwa kuwa hospitali ya wilaya ya Mlele pindi kitakapokamilika na huo utakuwa mradi wake wa mwisho katika wilaya ya Mlele.

Tuesday, January 15, 2013

HABARI ZA MICHEZO

MECHI YA YANGA, AZAM YAINGIZA MIL 240/- FEB 22, 2013

 Kikosi cha Yanga
 Kocha wa Yanga
 Kikosi cha Azamu
Mechi namba 120 ya Ligi Kuu ya Vodacom iliyochezwa jana (Februari 23 mwaka huu) kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na kumalizika kwa Yanga kuibuka ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Azam imeingiza sh. 239,686,000.
Watazamaji 39,315 walikata tiketi kushuhudia mechi hiyo ambayo viingilio vilikuwa sh. 5,000, sh. 8,000, sh. 15,000 na sh. 20,000 huku kila klabu ikipata mgawo wa sh. 58,794,927.45 wakati Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) iliyolipwa ni sh. 36,562,271.19.
Kiingilio cha sh. 5,000 ndicho kilichovutia watazamaji wengi ambapo waliokata tiketi hizo walikuwa 33,315 na kuingiza sh. 165,655,000 wakati idadi ndogo ya washabiki ilikuwa ya kiingilio cha sh. 20,000 kilichovutia washabiki 485 na kuingiza sh. 9,700,000.
Mgawo mwingine wa mapato hayo ni asilimia 15 ya uwanja sh. 29,895,725.82, tiketi sh. 3,183,890, gharama za mechi sh. 17,937,435.49, Kamati ya Ligi sh. 17,937,435.49, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh. 8,968,717.75 na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) sh. 6,975,669.36.
Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)

KLABU YA SIMBA YATAJA KAMATI YA UFUNDI



Hawa ndiyo wajumbe wapya wa kamati za Simba.
KAMATI YA UFUNDI
  1. DAMIAN MANEMBE-MWENYEKITI
  2. IBRAHIM MASOUD-MAKAMU MWENYEKITI
  3. CRESCENCIUS MAGORI
  4. KHALID ABEID
  5. SAID TULLY
  6. DR. KATEGILE
  7. ZAMOYONI MOGELA
  8. JOHN WILLIAM (DEL PIERO)
  9. YUSUFU MACHO
  10. JEFF LEA
  11. BITA JOHN
  12. SHABAAN BARAZA
 
KAMATI YA FEDHA
  1. GEOFREY IRICK NYANGE (MWENYEKITI)
  2. RAHMA AL KHALOOS-MAKAMU MWENYEKITI
  3. FRANCIS WAYA
  4. ZITTO KABWE
  5. JUMA NKAMIA
  6. RUGE MUTAHABA
 
KAMATI YA MASHINDANO
  1. SWEDY MKWABI-MWENYEKITI
  2. SAID PAMBA-MAKAMU MWENYEKITI
  3. SELEMANI ZEDDY. (MB)
  4. JERRY YAMBI
  5. IDDI KAJUNA
  6. CHAUREMBO
  7. GERLAD LUKUMAY
  8. HABBIB NASSA
  9. BUNDALA KABULWA
  10. CHARLES HAMKAH
  11. SAID RUBEYA
  12. ABDULFATAH SALUM (SAPHIRE)
  13. HATIBU MWINYI (BUSTA)
  14. ABDUL  MSHANGAMA
  15. HUMPHREY ZEBEDAYO
  16. MAJALIWA MBASSA
  17. SULEIMAN ZAKAZAKA
  18. KESI MOHAMED RASHID
  19. MOHAMED ISSA MBENA
 
KAMATI YA PROGRAMU ZA VIJANA
  1. IBARHIM MASOUD –MWENYEKITI
  2. RUGE MUTAHABA-MAKAMU MWENYEKITI
  3. JOSEPH ITANG’ARE-MJUMBE/MLEZI
  4. WILFRED KIDAU
  5. MOHAMED ABDALLAH
  6. SAID TULLY
  7. CANISIUS MASOMBOLA
  8. HAMIS MRISHO
  9. DAMAS NDUMBARO
  10. TALIB HILAL
 Imetolewa na,
Ezekiel Kamwaga
Ofisa Habari
Simba SC

MZUNGUKO WA PILI VPL JUMAMOSI FEB 2, 2013, DARAJA LA KWANZA  TANZANIA

Wakati mzunguko wa pili wa Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kuwania ubingwa wa Tanzania Bara unaanza Jumamosi (Januari 22 mwaka huu), mzunguko wa pili wa Ligi Daraja la Kwanza (FDL) umesogezwa mbele kwa wiki moja ambapo sasa utaanza Februari 2 mwaka huu.
Uamuzi wa VPL kuendelea Januari 26 mwaka huu ulifikiwa katika kikao cha Kamati ya Ligi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) na klabu za ligi hiyo kilichofanyika jana (Januari 21 mwaka huu) jijini Dar es Salaam.
Hata hivyo, uamuzi huo umefikiwa huku yakiwepo masharti kadhaa kutokana na uamuzi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kukamata sh. milioni 157 kwenye akaunti za TFF, fedha ambazo zilitoka kwa mdhamini wa VPL (Kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom) kwa ajili ya timu zinazoshiriki ligi hiyo.
Masharti hayo yatawasilishwa na Kamati ya Ligi kwa maandishi kwa Katibu Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), nakala kwa Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo. Awali klabu kupitia Kamati ya Ligi zilisisitiza zisingecheza ligi hadi fedha hizo zitakaporejeshwa.
Kwa upande wa FDL itaanza bila timu ya Small Kids ya Rukwa ambayo imeshushwa daraja kwa mujibu wa kanuni baada ya kushindwa kucheza mechi mbili katika mzunguko wa kwanza.
Kwa mujibu wa kanuni za ligi hiyo, matokeo yote ya mechi ambazo Small Kids ilicheza katika mzunguko huo wa kwanza yamefutwa. (Ratiba ya VPL imeambatanishwa).
OCHIENG, AKUFFO WAFIKIA MUAFAKA SIMBA
Kamati ya Sheria, Maadili na Hadhi za Wachezaji iliyokutana Januari 19 mwaka huu chini ya Mwenyekiti wake Alex Mgongolwa imeliondoa shauri lililokuwa mbele yake dhidi ya klabu ya Simba lililowasilishwa na wachezaji Pascal Ochieng na Daniel Akuffo baada ya pande hizo kufikia makubaliano.
Wachezaji hao kutoka Kenya na Uganda waliwasilisha malalamiko mbele ya kamati wakipinga kukatizwa mikataba yao bila kulipwa stahili zao. Hata hivyo, pande zimefikia makubaliano ya kuvunja mikataba nje ya kamati, na wachezaji hao kulipwa stahili zao.
Pia Simba imekiri kudaiwa na wachezaji Shija Mkina, Swalehe Kabali, Victor Costa na Rajab Isiaka na kuahidi kuwalipa wachezaji hao wakati Coastal Union na mchezaji wake Mohamed Issa wamefikia makubaliano ya malipo, hivyo kuvunja mkataba kati ya pande hizo mbili.
SHABANI KADO AIDHINISHWA COASTAL UNION
Kamati ya Sheria, Maadili na Hadhi za Wachezaji ilikutana Januari 19 mwaka huu kupitia maombi ya usajili wa dirisha dogo kwa klabu za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) na Ligi Daraja la Kwanza (FDL) ambapo kipa Shabani Kado ameidhinishwa kuidakia timu ya Coastal Union ya Tanga.
 Wachezaji wengine waliodhinishwa kwenye dirisha dogo na klabu zao kwenye mabano ni Humphrey Mieno, Brian Umony, Jockins Atudo, David Mwantika, Abdallah Seif, Malika Ndeule na Uhuru Selemani- kwa mkopo (Azam), Juma Mdindi, Njaidi Mohamed na Mahmoud Mbulu (Ruvu Shooting), Mohamed kayi na Emmanuel Gabriel (Tanzania Prisons).
Nurdin Selemani, Shaibu Nayopa, Hamidu Hassan, Paul Malipesa, Josephat Moses, Muharami Mnyangamala, Majaliwa Mbaga na Alphonce Peter (Oljoro JKT), Shukuru Kassim, Chacha Marwa, Salum Machaku, Mzamiru Said, Victor Bundala, Delta Thomas, Edward Mzeru na Tizzo Chomba (Polisi Morogoro), Edmund Kashamila na Julius Mrope (Kagera Sugar).
Rajab Mohamed, Zakayo Joseph, Baraka Anthony na Mussa Chambo (Mtibwa Sugar), Zahoro Pazi- kwa mkopo, Emmanuel Linjechele, Kisimba Luambano na Nashon Naftali (JKT Ruvu), Moaka Shabani, Ismail Mkaima na Damas Milanzi (Mgambo Shooting), Donald Obimma, Exavery Muhollery, Mohamed Hussein na Ulugbe Odia (Toto Africans).
Obadi Mungusa, Juma Seif, Yusuf Mgwao, Ibrahim Job- kwa mkopo, Shamte Ally- kwa mkopo, Buya Jamwaka, Takang Valentine, Nurdin Mussa, Salvatory Jackson, Mohamed Athuman, Athuman Kajembe na Jarufu Kizombi (African Lyon), Mussa Mudde na Abel Dhaila (Simba).
Rashid Simba, Zuberi Hamisi, Shaongwe Ramadhan, Castory Mumbara, Tinashe Machemedze na Shabani Kado (Coastal Union).
Mchezaji Martin Mlolere aliyeombewa usajili Mgambo Shooting kutoka Majimaji amekataliwa kwa vile taratibu za uhamisho hazijakamilika, hivyo anabaki kwenye timu yake ya Majimaji.
Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)

WADAU WAONGEZEKA UCHAGUZI WA TFF


Idadi ya wadau waliojitokeza kuchukua fomu za kuwania uongozi katika Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imeongezeka ambapo wengine saba wamechukua leo (Januari 15 mwaka huu) na kufanya idadi yao kufikia 26.
Hata hivyo, idadi hiyo ni kwa wale wanaochukua fomu hizo katika ofisi za TFF, kwani vilevile zinapatikana kupitia tovuti ya TFF ya www.tff.or.tz ambapo mwisho wa kuchukua na kurejesha ni saa 10 kamili alasiri Januari 18 mwaka huu.
Waliochukua leo ni Michael Wambura anayewania umakamu wa rais wakati kwa wajumbe wa Kamati ya Utendaji ni Mbasha Matutu, Muhsin Balhabou, Salum Chama, Titus Osoro na Zafarani Damoder.
Idadi kamili ya waliochukua Michael Wambura, Ramadhan Nassib na Wallace Karia (Makamu wa Rais). Kwa upande wa wajumbe na kanda zao kwenye mabano ni Salum Chama (Kagera na Geita), Mugisha Galibona, Samuel Nyalla, Titus Osoro na Vedastus Lufano (Mara na Mwanza).
Epaphra Swai na Mbasha Matutu (Shinyanga na Simiyu), Charles Mugondo, Elly Mbise na Twahili Njoki (Arusha na Manyara), Yusuph Kitumbo (Kigoma na Tabora), Ayubu Nyaulingo, Nazarius Kilungeja na Selemani Kameya (Katavi na Rukwa) na James Mhagama (Njombe na Ruvuma).
Athuman Kambi (Lindi na Mtwara), Hussein Mwamba na Stewart Masima (Dodoma na Singida), Farid Nahdi (Morogoro na Pwani), Khalid Mohamed (Kilimanjaro na Tanga) na Muhsin Balhabou, Shaffih Dauda na Zafarani Damoder (Dar es Salaam).
Naye Said Mohamed amechukua fomu ya kuwania umakamu mwenyekiti wa Bodi ya Ligi Kuu (TPL Board).
UCHAGUZI TAIFA KUFANYIKA DAR ES SALAAM
Uchaguzi wa viongozi wa Chama cha Makocha wa Mpira wa Miguu Tanzania (TAFCA) utafanyika Jumamosi (Januari 19 mwaka huu) kwenye ukumbi wa mikutano wa Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa Katibu Mkuu wa TAFCA, Eugene Mwasamaki, mikoa ambayo tayari imefanya uchaguzi wa viongozi inatakiwa kuwasilisha muhtasari wa mkutano uliowaingiza madarakani. Muhtasari huo uwasilishwe TAFCA kabla ya keshokutwa (Januari 17 mwaka huu).
Mkoa utakaoshindwa kutuma muhtasari ndani ya muda uliotolewa utakosa haki ya kushiriki katika uchaguzi huo uliovutia wagombea watano. Wagombea hao ni Oscar Korosso (Mwenyekiti), Lister Manyara (Makamu Mwenyekiti), Michael Bundala (Katibu Mkuu) na Magoma Rugora na Wilfred Kidao wanaowania ujumbe wa Mkutano Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF).
Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)

Wednesday, January 9, 2013

KATIBU KOTINI KWA KUTISHIA KUUA

KATIBU WA CCM MUFINDI AFIKISHWA MAHAKAMANI AKITUHUMIWA KUTISHIA KUUA



 .

KATIBU  wa chama  cha mapinduzi (CCM) wilaya ya Mufindi Jackob Nkomola leo amefiishwa mahakamani akituhumiwa  kuua kwa maneno .
Akisoma shtaka hilo  linalomkabili katibu  huyo  mahakamani hapo hakimu  wa mahakama ya mwanzo Mafinga wilayani Mufindi Zakaria Mushi alisema  mtuhumiwa Jackob Nkomola anashtakiwa kwa kosa la kumtishia kumuua  kwa maneno, Alexandel Tweve  kinyume na  sheria kifungu namba 89 kifungu kidogo “A”.

Aidha hakimu huyo alisema mshitakiwa alitenda kosa hilo, Octoba 3 mwaka 2012 katika eneo la Mkombwe, ambapo alimtishia mkazi huyo wa mji  wa Mafinga  wilaya ya Mufindi..

Mtuhumiwa alikana shtaka hilo na hakimu kutoa masharti ya dhamana ya ahadi
ambayo inathamani ya shilingi  200,000 na adhaminiwe na mtu mmoja
atakayetambulishwa kwa barua kutoka katika ofisi ya serikali ya kijiji au
Kata masharti ambayo yalitimizwa na mshitakiwa na kesi hiyo itafikishwa  tena mahakamani hapo Januari 30 mwaka huu.

Hakimu alimtaka mlalamikaji   wa kesi hiyo kufika na mashahidi wake
aliowaorodhesha.
Wakati  huo  huo mwandishi  wa habari  wa gazeti la mtanzania  mkoani Iringa Oliver Moto amenusurika  kupigwa na mtuhumiwa  huyo  wakati akitimiza wajibu  wake kwa  kumpiga picha mtuhumiwa  huyo .
Tukio hilo lilitokea muda mfupi baada ya mtuhumiwa huyo  kusomewa mashtaka yake na kusubiri kutimiza masharti ya dhamana na akiwa chini ya ulinzi  ya ulinzi  wa  polisi mahakamani hapo

Hatua hiyo iliwashangaza watu waliohudhuria kesi hiyo katika mahakama hiyo huku  wakihoji mamlaka ya mtuhumiwa kumfuata umbali wa hatua zaidi  ya tano mwandishi, huku mtuhumiwa akiwa chini ya ulinzi kwa kuwa bado alikuwa naashikiriwa na Mahakama hiyo kwa kutokidhi vigezo vya dhamana yake.

Kutokana na tukio  hilo lilimlazimu mwandishi  huyo kukimbilia kwa hakimu wa mahakama hiyo akitaka msaada  wake katika  hilo   huku hakimu Mushi akimtaka  mwandishi huyo kufika kituo chapolisi kutoa taarifa ya tukio hilo ushauri ambao hakuufanyia kazi .

Akiwa njiani Mwandishi alimpigia simu Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Mufindi
Cosmas Kaguo ambaye alimuomba mwandishi kuonana naye kabla ya kufika katika
kituo cha Polisi cha Mafinga.

Hatua ya mwenyekiti wa CCM Kaguao, - aliitisha kikao cha dharua cha kamati
ya siasa na kuomba radhi juu ya tukio lililotokea, na baada ya muda dakika
20 Katibu wa CCM (Mtuhumiwa) aliingia katika moja ya ofisi ya Halmashauri
ya Wilaya ya Mufindi, iliyopo katika ukumbi wa mikutano na kuomba radhi juu
ya kile alichokifanya kwa  mwanahabari huyo  mahakama.

Ombi la mwenyekiti wa CCM Wilaya, lilikubaliwa na mwandishi huyo kwa
kusitisha hatua yake ya kufungua kesi katika kituo cha polisi Mafinga.

Akitoa utetezi wake, mtuhuimiwa huyo alisema “Ninaomba unisamehe sana
Oliver, unajua kesi yangu hii niya kisiasa, na kukufanyia hivyo ni hasira
baada ya mtu anayenituhumu kutumia njia mbalimbali za kuniangamiza, ninajua
nimekukwaza wewe, lakini pia nimeidhalilisha taaluma yako, ninakuomba
unisamehe,” Alisema Nkomola.

WASIRA: KILIMO KWANZA KUUFIKISHA UCHUMI MIFUKONI MWA WANANCHI

 

                                                              Waziri Wasira

 NA MWANDISHI WETU
UHALISIA wa kukua kwa uchumi hadi mifukoni mwa wananchi walio wengi una matumaini ya kufikiwa kutokana na
utekelezwaji  madhubuti wa kuinua Kilimo kupitia mpango wa Kilimo Kwanza unayotekelezwa na serikali.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Sera na Uratibu, Steven Wasira alipokuwa akizungumza kwenye
kipindi cha 'Tuongee Asubuhi' cha kituo cha televisheni cha Star Tv, leo, Januari 15, 2013.

Katika kipindi hicho, kilichokuwa na mada ya 'Uhalisia na Kukua kwa Uchumi' pamoja na Wasira wazungumzaji wengine
walikuwa, Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba na Mtaalam wa Uchumi kutoka Chuo cha SAUTI cha Mwanza, Odas Bilame.

Wasira alisema, kwa sasa wananchi wengi hawaoni uhalisia wanapoambiwa kwamba uchumi wa nchi unakuwa, kwa
sababu, hali ya kukuwa kwa uchumi kwa sasa hakujawagusa waajiriwa katika sekta ya kilimo ambao ndio wengi kiasi
cha asilimia 80.

Alisema, katika kipindi cha kati ya mwaka juzi na mwaka jana uchumi wa Tanzania ulionyesha kuwa umekuwa kwa kati
ya asilimia 6.5 na 6.7, lakini kukua huku kuliwagusa zaidi watumishi waliopo katika sekta nyingine kama za viwanda na
watumishi wa umma.

"Katika hali hii ambayo watumishi wa sekta zote wanategemea lazima wapate chakula na mazao mengine kutoka kwa
wakulima, ambao hawajanufaika vya kutosha na mafanikio ya kukua wa uchumi huu, ni lazima, athari za kutoonekana
ukuaji uchumi katika jamii utakuwepo", alisema, Wasira.

Alisema, kutokana na kutambua kwamba ni lazima sekta ya Kilimo iboreshwe vya kutosha ndipo ukuaji wa uchumi utadhihirika kwa uhakika miongoni mwa wengi, Serikali imeelekeza nguvu zake kuhakikisha mpango wa Kilimo Kwanza unazaa matunda.

Alisema, katika jitihada za kufikia lengo hilo, Serikali imetenga sh. bilioni 300 kwa ajili ya kuwekeza kwenye utafiti katika kilimo, ambapo katika uwekezaji huo, sasa wapo wataalam wengi na maofisa ugani vijijini kwa ajili ya kuwezesha wakulima kufanya kilimo bora na cha kisasa.

Wasira alisema, pia kiwanda cha mbolea cha Minjingu kimejengwa ili kuongeza upatikanaji wa mbolea ili kuhakikisha kwamba kila mkulima anapata mbolea ya kutosha na kuongeza kuwa  pamoja na kiwanda hicho Serikali inao mpango wa kujenga vingine vya mbolea ili kuongeza wigo wa upatikanaji wa pembejeo hiyo.

Alisema, wakati jitihada zimewekwa kwenye uinuaji sekta ya kilimo, ujenzi na uboreshaji miundombinu ya usafiri ikiwemo barabara na reli, utafungua milango ya mazao kutoka vijijini kwenda maeneo mbalimbali nchini hata nje ya nchi kwa urahisi, hatua ambayo itachochea kukua kwa kasi zaidi kwa uchumi.

Akielezea historia ya Uchumi wa Tanzania, Wasira alisema, awali hali ya uchumi ilikuwa ikienda vizuri, lakini ilianza kuathiriwa na uhaba wa mafuta miaka uliojitokeza miaka ya 1977 lakini ukaendelea kuathiriwa zaidi na vita vya Kagera, mwaka 1978 na hadi sasa zimeendelea kuwepo changangamoto za kidunia ambapo Tanzania kama moja ya nchi zilizomo haiwezi kuzikwepa.

Kwa upande wake Profesa Lipumba, alikiri kwamba Kilimo Kwanza ni 'muarobaini' wa kukua kwa uchumi wa nchi, lakini akaonya kwamba ni lazima juhudi za makusudi zifanyike kuhakikisha kuwa uhalisia wa kukua wa uchumi ni kuigusa mifuko ya wananchi.

Pamoja na kukiri umuhimu wa mpango wa kilimo kwanza, Profesa Lipumba aliponda kwamba, licha ya mikakati mizuri  kuwepo lakini mingi ipo katika makatarasi tu, haitekelezwi kwa vitendo.

"Sasa kama dhamira ipo, umefika wakati wa watekelezaji kuacha maneno na badala yake kufanya kazi kwa vitendo zaidi", alisema Lipumba.

Kwa upande wa nafasi ya wasomi wanavyoisadifu hali ya kukua kwa uchumi Tanzania, Odax alisema, wasomi wanakubalina kwamba juhudi zikiwekezwa kwenye kilimo uchumi utakuwa.
Waziri mkuu Mizengo Pinda amemtunuku Rpc wa mkoa wa katavi acp Dhahiri Kidavashari Tuzo ya heshima ya mkoa wa katavi ya mwaka 2012 kutokana na uhamasishaji wa jamii kushirikiana na jeshi la polisi katika kupambana na uhalifu yani polisi jamii kulia kwa waziri mkuu ni mkuu wa mkoa wa wakatavi Dr Rajabu Rutengwe na kulia kwa mkuu wa mkoa ni Mbunge wa mpanda mh Saidi Arifi sherehe hiyo ilifanyika usiku wa mkesha wa kukaribisha mwaka mpya mkoani katavi picha na chris mfinanga

WAZIRI MKUU PINDA AZINDUA KITABU CHA WAPIMBWE

WAZIRI MKUU Mizengo Pinda amezindua kitabu cha historia ya kabila la Wapimbwe lililoko mkoani Katavi na kutayataka makabila mengine kuandika historia zao ili waweze kutunza kumbukumbu kwa ajili ya vizazi vijavyo.

Akizindua kitabu hicho hivi karibuni mjini Mpanda, Waziri Mkuu aliwataka watu wa makabila mengine ya mkoa wa Katavi ambayo ni Waruira, Wabende, Wakonongo na Warungwa wafanye tafiti kuhusu mila na tamaduni zao na kisha waandike vitabu vyao.

Kabla ya uzinduzi huo, mtunzi wa kitabu hicho, Bw. Peter Mgawe alisema kitabu hicho kimetokana na utafiti uliofanywa tangu mwaka 2007 ambao ulilenga kukusanya  taarifa na masimulizi mbalimbali kutoka kwa wazee wa Kipimbwe ambao wameishi miaka mingi huku wakiwa na hazina ya mila na tamaduni za kabila hilo ambalo pia ni kabila lake Waziri Mkuu Pinda.

“Hili ni kabila dogo lisilofahamika na wengi, nimekuwa nikitafuta taarifa na machapisho (literature) mbalimbali kuhusu kabila hili lakini sikuwahi kupata chochote… ndipo nikamshirikisha Mheshimiwa Waziri Mkuu juuya kufanya utafiti na kuandika historia yetu naye akalikubali wazo langu,” alisema Bw. Mgawe ambaye pia ni
Mhadhiri wa Chuo cha Ustawi wa Jamii, Kijitonyama, Dar es Salaam.

Akizungumza na wakazi waliohudhuria uzinduzi huo, Waziri Mkuu alisema utafiti huo usiishie hapo tu, bali wafanye tafiti nyingine kuhusu mavazi, vyakula, ndege, wanyama waliokuwa wakipendelewa na mababu zao ili kuongeza hazina ya taarifa ya kabila hilo.

“Lengo la kitabu hiki lilikuwa ni kuhifadhi katika maandishi historia ambayo ilikuwa imefichika ndani ya vichwa vya wazee wetu kutoka vijiji mbalimbali vya Mpimbwe… nafurahi kwamba tunao wazee watatu waliokuwa katika warsha ya kwanza kabisa iliyofanyika mwaka 2008. Leo hii wako hapa na wanashuhudia matunda ya kazi yao,” Alisema Waziri Mkuu.

Wazee hao ni Mzee Simba Pangani Kalulu (76) kutoka kijiji cha Mamba, Mzee Valeri Kipande (76)  kutoka kijiji cha Lyangalile na Mzee Moses Kasalani (67) kutoka kijiji cha Mirumba. Vijiji vyote hivyo viko wilaya ya Mlele, mkoani Katavi.

Waziri Mkuu amerejea jijini Dar es Salaam jana mchana (Jumanne, Januari 9, 2013) akitokea kijijini kwake Kibaoni, wilayani Mlele, Katavi ambako alifanya ziara ya siku 10 kwenye jimbo lake la Katavi na kisha kuwa na mapumziko ya Krismasi na mwisho wa mwaka.

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
JUMATANO, JANUARI 09, 2013.
Itatoka katika Radio; Uhuru Fm DSM saa 21:00 USIKU leo Januri 10, 2013 kipindi cha Habari na Matukio

OMBA OMBA ALIYEJIFANYA MLEMAVU ......

OMBA OMBA ALIYEIGIZA MLEMAVU WA MIGUU NA MIKONO ATIMUA MBIO

 Huyu  ni omba omba anayeigiza  kutokuwa na mkono mmoja na mguu akiwa ameka eneo la M.R akisubiri kupewa msaada na wapita njia "saidia baba, saidia mama nikale chakula" 

MTI WAANGUKA MLIMA IPOGOLO MAGARI YAKWAMA KUPITA

 Wananchi wakisubiri mti  kutolewa barabarani  baada ya  kuanguka na kuziba barabara ya mlima wa Ipogolo mjini Iringa leo jioni
 Hapa  wananchi  wakihangaika kukata mti huo kwa shoka  ili  kupata nafasi ya  kupita
Abiria  zaidi ya  500 leo  wamekwama katika  mlima wa Ipogolo mjini Iringa  baada ya mti mkubwa  uliokuwepo kandokando ya barabara  ya Ipogolo -Iringa mjini  kuanguka na  kunusuru  kulifunika basi la abiria  leo kabla ya  kuziba barabara  hiyo.

Tukio  hilo  limetokea mida ya saa 8 mchana  katika  eneo hilo ambapo moja kati ya daladala  lililokuwa  likipandisha eneo hilo  likiwa na abiria  zaidi ya 50  limenusurika  kufunikwa na mti huo.

Baadhi ya abiria  na mashuhuda wa  tukio  hilo waliozungumza na mtandao  wa www.francisgodwin.blogspot.com eneo la  tukio  wamedai kuwa hakuna mtu aliyejeruhiwa  japo  wameomba wasimamizi  wa barabara   hiyo wakala  wa barabara  mkoa  wa Iringa (TANROADS) kuangalia  uwezekano  wa  kukata  miti mikubwa  iliyopo eneo hilo ili kuepusha maafa makubwa  zaidi ya hayo.

Kwani  wamesema tatizo la mti huo na mawe  kuanza  kuporomoka katika mlima   huo  limetokana na baruti ambazo zilikuwa  zikitumika  kupasua mawe katika mlima  huo  wakati  wa upanuzi  wa barabara  hiyo  hivyo   sasa maji yanapoingia ndani ya ardhi hiyo ndio husababisha matatizo hayo .

Baadhi ya  wananchi  wamempongeza meneja  wa TANROADS mkoa  wa Iringa Paul Lwakurwa  kwa  kufika mapema  eneo hilo na kufanikisha  kutatua tatizo hilo vinginevyo hadi  kesho barabara  hiyo ingefungwa rasmi. KALI YA 2013
OMBA OMBA ALIYEIGIZA MLEMAVU WA MIGUU NA MIKONO ATIMUA MBIO

 Huyu  ni omba omba anayeigiza  kutokuwa na mkono mmoja na mguu akiwa ameka eneo la M.R akisubiri  kuomba chochote  kutoka kwa  wapita njia leo

 Hapa akisubiri msaada  kutoka kwa wasamaria  wema leo
 Hapa akitimua mbio  kukwepa kamera ya PAPARAZ mjini Iringa  leo

Ule  usemi wa  wahenga  kuwa  ukistaajabu ya mussa utayaona ya filauni leo umetimia katika  eneo la M.R mjini Iringa baada ya  wananchi  waliokuwepo eneo hilo kupigwa na butwaa baada ya mzee janja ambaye amekuwa akishindwa eneo hilo na kujifanya mlemavu asiyekuwa na mkono mmoja na mguu  mmoja kutimua mboni kukwepa kamera ya mtandao  huu.

Tukio  hilo limetokea majira ya saa 8 mchana baada ya camera ya mwandishi  kufika  eneo  hilo kushuhudia umati  wa wananchi  wakiendelea  kumpa  fedha mzee janja  huyo ambae alijifanya mlemavu  wa viongo na kuongea kwa  shida .

Hata  hivyo baada ya mmoja kati ya  wananchi kufika  eneo hilo alionyesha  kufichua mbinu hiyo chafu ya  mzee  huyo kujifanya ni mlemavu  wakati asubuhi alikutana maeneo akiwa mzima wa afya  njema na katika  kumhoji zaidi  ndipo kamera ya mtandao huu  ilipoamua  kufanya kazi yake  ya kunasa  kituko  hicho na ndipo mzee   huyo alipoanza  kuongea  kwa  sauti vizuri  tofauti na alivyokuwa akijifanya kuwa hawezi kuongea kabisa (bubu)

Wakati mabishano yakiendelea  eneo hilo ghafla  mzee  huyo alisimama kwa miguu  yake  yote  miwili pamoja na awali kujifanya ni mlemavu asiye na mguu mmoja ila baada ya  watu  kutaka  apigwe  picha ndipo mzee  huyo alipoanza  kutimua mbio  huku ulemavu aliokuwa nao akiusahau hapo  pamoja na kandambili zake na hakuna mtu  aliyeweza  kumfukuza na kufanikiwa  kumkuta.

Baadhi ya  wananchi  wameuomba uongozi  wa Manispaa ya Iringa na miji mingine  kuwabana  omba omba hao ambao  wamekuwa  wakidanganya  watu kuwa  wao ni  walemavu kumbe ni  wazima na kutaka  kuwepo kwa utaratibu maalum wa   watu kuomba misaada.Habari hii ni kwa mujibu wa Francis Gowin

Monday, December 10, 2012

MIAKA 51 YA UHURU WA TANGANYIKA

Miaka 51 yawatoa jela wafungwa 3,814,sherehe uwanja wa taifa nazo zanoga


Baraza la mawaziri na wawakilishi wa mataifa ya nje nchini


Wale wanaokumbukaSharo milionea katika mkasa wa kukabidhiwa mikoba aliona mkia wakerewe hawa walifanya  mambo

Warembo kutoka nchi jirani ya Rwanda walifika kuwakilisha  uzuri katikia maonesho ya miaka 51 ya Uhuru

Hata kama uko jukwaani na jana uliwaona lazima uwasalimie:Jk akisalimiana na baadhi ya wakuu na wageni wengine waliofika kutupa tafu miaka 51
RAIS Jakaya Kikwete na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama nchini, ametoa msamaha kwa wafungwa 3,814 wakiwemo wenye magonjwa yasiopona na wanawake wajawazito.
Hata hivyo msamaha huo uliotolewa kuadhimisha Miaka 51 ya Uhuru wa Tanzania, hauwahusu wafungwa wenye makosa ya ubakaji, ulawiti, kuwapa wanafunzi mimba, waliotumia madaraka vibaya na wala rushwa.
Taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa leo na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi imeeleza kuwa, Rais Kikwete ametekeleza hilo kwa kutumia madaraka aliyonayo chini ya Ibara ya 45 (1) (d) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, wafungwa waliohusika na msamaha huo ni waliothibitika kuwa na ugonjwa wa Ukimwi, Kifua Kikuu (TB) na saratani ambao wako katika hali mbaya, wazee wenye umri wa miaka 70 na kuendelea.
“Wamo waliopatikana na hatia na kuhukumiwa kuwepo gerezani kwa ridhaa ya Rais wa Tanzania chini ya kifungu cha 26 cha Kanuni ya Adhabu, ambao hadi Desemba 9, mwaka huu wamekaa gerezani si chini ya miaka mitano na wamekuwa na tabia njema,” alisema Dk Nchimbi.
Wengine ni wafungwa wanawake walioingia na mimba au na watoto wadogo gerezani, wenye ulemavu wa mwili na akili, wanaotumikia kifungo kisichozidi miaka mitano na ambao walishatumikia robo ya kifungo chao.
Dk Nchimbi alisema kuwa, kutokana na madaraka hayo, Rais Kikwete ametoa msamaha huo kwa wafungwa 3,814 na kwamba wafungwa wenye matatizo maalum kati ya waliosamehewa, wamethibitishwa na jopo la madaktari chini ya Uenyekiti wa Mganga Mkuu wa Mkoa au Wilaya husika.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, msamaha huo hauwahusu wafungwa waliohukumiwa kunyongwa, kifungo cha maisha, waliofungwa kwa kujihusisha na dawa za kulevya, waliotoa au kupokea rushwa na wenye makosa ya unyang’anyi wa kutumia silaha na wizi wa magari kwa silaha.
Pia hauwahusu waliopatikana na makosa ya kunajisi, kubaka na kulawiti, waliowapa wanafunzi mimba, walioharibu miundombinu kama kuiba nyaya za simu, umeme au mafuta ya transformer na waliokutwa na silaha au risasi.
Dk Nchimbi alisema wengine wasiohusika ni wafungwa wazoefu wanaotumikia kifungo cha pili na kuendelea, waliowahi kupewa msamaha lakini wanatumikia sehemu ya kifungo kilichobaki, waliowahi au kujaribu kutoroka na waliotumia madaraka vibaya.
Wengine ni waliohukumiwa kwa kosa la kuzuia watoto kusoma na wale wanaotumikia kifungo chini ya Sheria namba 25 ya mwaka 1994 ya Bodi ya Parole na  Sheria ya Huduma kwa Jamii namba 6 ya mwaka 2002.
Katika maadhimisho ya Miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania mwaka jana, Rais Kikwete alitoa msamaha kwa wafungwa 3,803 na mwaka 2010 katika shehere kama hizi alisamehe wafungwa 3563.
Mwisho.