Monday, March 25, 2013

ZAWADI YA SIKU KUU YA MATAWI 2013

AIFA STARS YAICHAPA MOROCCO BAO 3-1

 Ubao wa Matokeo unavyosomeka mara baada ya kumalizika kwa mechi kati ya Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) dhidi ya Timu ya Taifa ya Morocco uliochezwa jioni hii kwenye uwanja wa Taifa wa Jijini Dar es Salaam.
 Mshambuliaji wa Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars),Thomas Ulimwengu akiwatoka Golikipa na Beki wa Timu ya Taifa ya Morocco wakati wa Mchezo wa kuwania tiketi ya kufuzu kucheza Kombe ya Dunia Mwaka 2014 kule nchini Brazil,uliochezwa jioni hii kwenye uwanja wa Taifa wa Jijini Dar es Salaam.Taifa Stars imeshinda Bao 3 - 1,mabao mawili yaliyotiwa kimiani na Mshambuliaji Machachari,Mbwana Samatha huku moja likifungwa na Thomas Ulimwengu.
Kiungo Mshambuliaji wa Timu ya Taifa (Taifa Stars),Shomari Kapombe akichuana vikali na Beki wa timu ya Morocco wakati wa Mchezo wa kuwania tiketi ya kufuzu kucheza Kombe ya Dunia Mwaka 2014 kule nchini Brazil,uliochezwa jioni hii kwenye uwanja wa Taifa wa Jijini Dar es Salaam.
Lango la timu ya Morocco ilikuwa ni hatari muda wote wa mchezo.
 Kipa wa Timu ya Morocco akiusindikiza kwa Macho mpira ulioingia wavuni,baada ta kuigwa na Mchezaji Mbwana Samatta wa Taifa Stars.

WAKRISTO WAFANYA KUMBUKUMBU YA MATAWI

Baadhi ya Wakristo wakatoliki wakiwa na matawi ya mizeituni kufunya kumbukumbu ya kumpokea mwokozi wao kama walivyofanya wana wa Yerusalemu.

Waamini wakiwa na matawi mbele ya jukwa la Kichangani wakisubiri Padre ayabariki ili kuanza maandamano kuelekea kanisani.


Waamini wakiwa kwenye maandamamo yaliyoanzia Kichangani kuelekea Kanisa Kuu la Kiaskofu Kihesa.

Wanakwaya wa Kwaya ya Mt. Cecilia Parokia ya Kihesa wakiwa kwenye maandamamo kuingia Kanisani.

Sunday, March 24, 2013

NMB YAKABIDHI DAWATI MIA SHULENI KAKESE



HALMASHAURI ya mji wa Mpanda imeishukuru benki ya NMB Tawi la Mpanda kwa kukabidhi madawati mia moja katika shule ya Msingi Kakese Mbugani yenye thamani ya shilingi milioni tisa na nusu na kupunguza kero ya uhaba wa madawati shuleni hapo

Akizungumza mara baada ya kupokea madawati hayo kutoka kwa benki hiyo Mkurugenzi wa mji wa Mpanda Joseph Mchina alisema mchango wa madawati mia kwa ajili ya shule ya Msingi Kakese mbugani kunasaidia juhudi za serikali za kuondoa kero ya uhaba wa madawati hapa nchini

Alisema katika halmashauri yake kuna uhitaji wa madawati 6313 wakati yaliyopo ni madawati 3213 na hivyo kuwa na upungufu wa madawati 3100 na kutokana na msaada wa benki wa madawati mia upungufu unabaki dawati 3000

Alitoa wito kwa taasisi zingine kurejesha sehemu fa faida yake kwa kusaidia jamii katika sekta ya elimu, afya na maendeleo ya wanawake na watoto

Akizungumza katika hafla hiyo mkuu wa kitengo cha wajasiliamali wadogo na wa kati wa NMB, Filbert Mponzi alisema hivi sasa benki yake imeanzisha utaratibu wa kutoa huduma ya elimu ya fedha mashuleni ili kuwajenga wanafunzi kukua katika elimu ya fedha

“Tunataka kuhakikisha tunajenga kizazi chenye uelewa na taaluma ya fedha kutoka shuleni hadi katik jamii’’
alisema afisa huyo wa benki
 



KATAVI NA MAJI KWA WANANCHI





MKOA wa Katavi umedhamiria kuondoa kero ya ukosefu wa maji katika maeneo ya vijijini ifikapo juni 2014.
Hayo yalibainishwa na mkuu wa mkoa huo Dr Rajabu Rutengwe katika kilele cha wiki ya maji mkoani humo katika kijiji cha Ikola wilaya ya Mpanda mwishoni mwa wiki

Alisema kila siku ofisi yake imekuwa ikihangaika na miradi ya maji katika vijiji mbali mbali na mijini ili kukamilisha miradi hiyo kwa ufanisi mkubwa na kuondoa kero ya maji

Katika kufanikisha azima hiyo mkuu wa mkoa aliwataka wananchi kuacha kabisa kharibu vyanzo vya maji na uharibifu wa mazingira katika meneo yao

Aidha aliziagiza mamlaka za serikali za mitaa na ofisi ya Katibu tawala wa mkoa huo kusimamia kwa karibu suala la utunzaji wa mazingira na kuzuia shughuli za binadamu zinazopelekea uharibifu wa mazingira

Amepiga marufuku shughuli za uharibifu wa mazingira kama vile uingizaji haramu wa mifugo, ukataji mkaa, kilimo cha bila utaalamu na kazi zingine zenye nasaba na uharibifu wa mazingira.