Na Willy Sumia, Mpanda
Machi 20,2011
HALMASHAURI ya Mji wa Mpanda mkoa wa katavi imeweza kukusanya mapato kwa asimia 110 kutokana na majaribio ya mabadiliko ya utaratibu wa ukusanyaji mapato ya Halmashauri hiyo.
Kaimu Mkurugenzi wa Mji ndugu Joseph Simon Mchina aliliambia JamboLeo juzi kuwa katika kipindi cha mwezi Februari halmashauri yake iliamua kufanya utafiti wa namna ya kuborsha mapato ya halmashauri hiyo kutokana na vyanzo vyake viwili vya mapato kati ya vilivyopo katika halmashauri yake.
Alisema kuwa maeneo ambayo waliamua kuyafanyia utafiti na katika ushuru wa masoko ili kuwa njia bora ya ukusanaji ushuru wa masoko manne yaliyoko Mpanda mjini ambapo kwa kuanzia Mchina alisema halmashauri yake iliamua kufanyia utafiti soko kuu la wilaya ya Mpanda lililoko chini ya halmashauri yake.
Alisema katika utafiti huo ulikuja baada ya halmashauri kunekana haipati mapato ya kutosha kutoka katika vyanzo vyake vya mapato licha ya kuwa na vyanzo vingi hali iliyopelekea kuongeza ushuru kwa wafanyabiashara wa masoko ya mjini hapa hali iliyozua kukuelewana baina ya halmashauri na wafanyabiashara hao hadi suluhu ilipopatikana ya kushusha ushuru huo.
Alisema kimsingi lengo la kutafuta namna ya kuongeza mapato iliendelea kubaki pale pale na hivyo kuipelekea halmashauri kuamua kutafuta namna bora ya ukusanyaji ushuru ili kuziba mianya ambayo ingebainika kukosesha mapato halmashauri.
Kaimu mkurugenzi Mchina alisema kuwa halmashauri iliwahamasisha wafanyabiashara wenyewe kulipia ushuru wa biashara zao katika ofisi za halmashauri bila kupitia kwa mzabuni na watendaji wa soko ambapo kabla ya kuendesha zoezi hilo halmashauri ilikuwa ikikusanya asilimia 30-40 kwa mwezi lakini baada ya kukusanya kwa wafanyabiashara katika kipindi cha mwezi februari halmashauri imeweza kukusanya kwa asilimia 110.
Alisema hapo awali halmashauri ilikuwa ikikusanya kiasi cha shilingi milioni 2.2 – milioni 2.5 kwa mwezi katika soko kuu lakini kwa kubadili mfumo wa ulipaji ushuru moja kwa moja kwa wafanyabiashara hao katika mwezi februari halmashauri iliweza kukusanya shilingi milioni 4.8 katika makusanyo lengwa ya shilingi milioni 4 kwa mwezi.
Kufuatia mafanikio hayo kaimu mkurugenzi huyo alidai kuwa hivi sasa halmashauri yake inaangalia uwezekano wa kuwa na utaratibu mpya wa ukusanyaji mapato ya ushuru wa masoko baada ya kubaini kuwa mzabuni anayepewa jukumu la kukusanya mapato anapata pesa nyingi lakini anawasilisha kidogo katika halmashauri.
Alisema endapo wataamua kubakiza wazabuni katika ukusanyaji mapato ya halmashauri atapendekeza iwe ni kwa baadhi ya mapato yasiyohesabika tu na kuwa uzoefu umeoneka kwa mamlaka ya mapato nchini kupokea mapato yak e moja kwa moja toka kwa wafanyabiashara na kufanikiwa bila kupitia kwa mzabuni isipokuwa kwa baadhi ya mapato kama vile kodi za vyombo vya moto.
Kwa muda mrefu halmashauri ya mji wa Mpanda imekuwa ikikabiliwa na ukata kutokana na makusanyo duni ya mapato ya halmashauri hali inayopelekea kushindwa kukabiliana na baadhi ya kero za mji huo ikiwa ni pamoja na changamoto ya mifereji kukosekana katika barabara nzuri za mji huo.
Mwisho.
POLISI
JESHI la polisi mkoani Rukwa linawashikilia watu wawili kwa tuhuma za kukutwa na meno 147 ya kiboko na tembo yenye thamani ya Tshs 6,580,000 katika wilaya ya Mpanda mkoa wa Katavi.
Tukio hili limetokea Januari 23 mwaka huu majira ya sa saa 5:00 usiku baada ya jeshi la polisi pamoja na askari wa wanyama pori wa mbuga ya Taifa ya Katavi kuweka mtego nje kidogo ya kijiji cha Stalike Wilayani Mpanda.
Wananchi baada ya kubaini kuwepo kwa njama za kusafirisha meno ya kiboko na Tembo akiyatoa katika Hifadhi ya Taifa ya katavi walitoa taarifa kwa Askari wa wanyamapori na kuandaliwa mtego ulifanikisha kunasa meno 146 ya tembo na kiboko na Risasi tisa za bunduki mbili za aina ya SMG na SAR.
Aliyekamatwa na men ohayo ni ndugu Mussa David (35) mkazi wa kijiji cha Muze Wilayani Sumbawanga mkoa wa Rukwa kati ya hayo meno 74 ya Kiboko yalikuwa yamehifadhiwa ndani ya begi la nguo pamoja na jino moja la tembo.
Mbali na meno aliyokutwa nayo aliweza kueleza kinaga ubaga kuwa mengine yapo nyumbani kwake katika kijiji cha Muze ambako askari hao walipofika nyumbani kwake aliwaonesha shehena ya meno 72 ya kiboko hivyo kufanya idadi ya meno kuongezeka na kufikia 146 yenye thamani ya shilingi milioni 2,500,000 na jino moja la Tembo lenye thamani ya shilingi milioni 4,080,000.
Mara baada ya kukamatwa na nyara hizo aliweza kukiri kuwa amekuwa kinara wa biashara haramu ya meno ya tembo nay a kiboko na kuwa soko lake kubwa liko nchini za Burundi na Congo DRC.
Akithibitisha tukio hilo Kamanda wa Polisi mkoani Rukwa Isuto Mantage amesema meno, hayo yalikutwa yamefukiwa chini ya ardhi pamoja na risasi Tisa za bunduki aina ya SMG na SAR shambani kwa ndugu Romwadi Isobila(46) na kwamba watuhumiwa wote watafikishwa mahakamani mara baada ya upelelezi wa awali kukamilika.
MWISHO
January 15, 2011
WANAFUNZI 2136 wa Kata ya Kibaoni wilaya ya Mpanda mkoani Katavi watanufaika na msaada wa Kilogramu 450 za sukari zilizotolewa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni mbunge wa Jimbo la Katavi.
Sukari hiyo iliyokabidhiwa juzi Januari 14,2011 na Msaidizi wake katika jimbo la Katavi Charles Kanyanda imegawiwa kwa shule za kata ya Kibaoni za Msingi na shule ya sekondari ya kata hiyo iitwayo Mizengo Pinda sekondari itawasaidia wanafunzi kupata uji wakati wa masomo katika shule hizo.
Akikabidhi sukari hiyo ndugu Kanyanda ambaye ni msaidizi wa Mheshimiwa Pinda katika jimbo la Katavi ambalo kata ya Kibaoni ni mojawapo katika ya kata zinazounda jimbo hilo alisema kuwa sukari hiyo imetolewa na mbunge wao Mheshimiwa Pinda kwa lengo la kuanzisha utaratibu wa kutoa
chakula cha mchana kwa wanafunzi kama ambavyo serikali imekuwa ikisisitiza kuwepo kwa utaratibu huo mashuleni.
Alisema serikali za vijiji zitambue kuwa shule zilizoko katika maeneo yao ni mali ya serikali ya kijiji na hivyo ziatakiwa kuanza kuwajibika kwa masuala yote ya uendeshaji wa shule hizo hasa katika kuhakikisha wanafunzi wanaanza kupata mlo wa mchana mashuleni ili kupunguza utoro na kuongeza ufanisi mashuleni
Mheshimiwa Waziri Mkuu ametoa sukari kiasi cha mifuko 45 ya kilogramu hamsini kila mmoja kwa shule ya msingi Kakuni iliyoko kijijini kwao
Kibaoni, mifuko 15 yenye uzito wa kilogramu 50 kila mmoja kwa shule ya sekondari ya Mizengo Pinda na shule za msingi za Ilalangulu na Mirumba kiasi cha mifuko 15 kila moja mifuko yenye uzito wa kilogramu hamsini kila mfuko.
Afisa kutoka idara ya Elimu ya Halmashauri ya wilaya ya Mpanda ndugu Venance Tesha akitoa shukrani kwa niaba ya Halmashauri alisema kuwa sukari iliyotolewa na Mheshimiwa Waziri Mkuu kwa shule za Kata ya Kibaoni ni changamoto kwa wazazi wa kata hiyo kuanza kujipanga ili kuuendeleza utaratibu wa utoaji uji na chakula mashuleni mara baada ya sukari hiyo kuisha.
“Wazazi na walezi wa kata hii mnatakiwa kuanza kujipanga sasa ili kuendesha michango itakayoendeleza utaratibu wa utoaji chakula mashuleni pindi sukari hii itakapoisha!!” alisema Tesha
Alisema licha ya kuwa Halmashauri inamshukuru Mheshimiwa Pinda bali inatoa shukrani za dhati na pongezi nyingi kwake kwa kutoa sukari ambayo imewapa changamoto halmashauri kuhakikisha utaratibu huo wa kutoa chakula mashuleni hasa katika shule za msingi unaendeshwa katika shule zote wilayani Mpanda.
“Labda niseme kwamba kitendo alichokifanya Mheshimiwa Pinda ni kutupatia shughuli ya kufanya kwakuwa kama bosi wako kaanzisha uji shuleni katika kata zilizoko jimboni kwake wewe unangoja nini
kuanzisha huo utaratibu katika maeneo mengine, lazioma kama halmashauri tumshukuru Mheshimiwa Waziri Mkuu kwa kutuamsha” Alisema Tesha.
Baadhi ya walimu wa shule za msingi katika kata ya kibaoni wakizungumza katika hafla fupi ya makabidhiano hayo walisema kuwa mpango wa utoaji uji shuleni utapunguza utoro na kuongeza ufanisi kwa wanafunzi katika kujifunza.
“Unajua mwanafunzi wakati wa mchana huwa hawasomi hata kama wako darasani kwa sababu ya njaa! Hata kama mwalimu ukiingia unagundua kuwa humu darasani wanaonisikiliza ni wachache wengine wanakuwa wameshabanwa na njaa na hivo kumbu kumbu inakuwa imepungua sana” alisema mwalimu Mwakifuna wa shule ya msingi Kakuni
Alifafanua kuwa licha ya kuwa uji utapunguza utoro mashuleni lakini pia utajenga mazingira bora ya kujifunza katika vipindi vya mchana na kujenga hamasa ya kuanza shule kwa watoto wanaokwepa kuanza shule katika jamii.
Walimu hao walimuomba Mheshimiwa Waziri Mkuu siku moja afike shuleni hapo kushuhudia namna wanafunzi wanavyoufurahia uji wakiwa shuleni na kushirikiana nao japo siku moja.
MWISHO.
Monday, January 31, 2011
FOCUS 2011 - KATAVI REGION ISSUES
Na Willy Sumia, Katavi
ASKARI wa jeshi la mgambo katika Halmashauri ya Mji wa Mpanda Mkoa mpya wa Katavi wamenusurika kipigo kutoka kwa wafanya biashara wa masoko matatu tofauti kufuatia kupandishwa kwa ushuru wa masoko hayo.
Vurugu zilianza mara baada ya askari hao kufika katika masoko yaliyoko mjini hapa kukusanya ushuru ambao umegomewa na wafanya biashara hao kwa madai ya ongezeko kubwa la ushuru kuliko hali halisi ya kipato cha biashara zao sokono hapo.
Tukio hilo limetokea jana katika muda tofauti mara baada ya askari wa mgambo hao pamoja na wakala wa kukusanya ushuru wa masoko ya mji kufika katika maeneo yao kwa lengo la kukusanya ushuru ambao unapingwa na wafanya biashara hao kwa kile kinachodaiwa na wafanya biashara hao kuwa ni ongezeko kubwa la ushuru.
Akizungumzia matukio hayo katibu wa wafanyabiashara wa Mji huo Amani Mahela ametoa wito kwa Mkurugenzi wa Mji kufika kwenye masoko hayo na kufanya mazungumzo na wafanya biashara badala ya utaratibu anaoutumia sasa wa kutoa matangazo kwenye vyombo vya habari akiwataka walipe ongezeko hilo la ushuru kabla ya kufanya mazungumzo nao.
Diwani wa kata ya Kashaulili John Matongo amesema kuwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji ameitisha kikao cha Madiwani wa kata tatu na viongozi wa wafanyabishara toka katika masoko yaliyo na mgogoro wa
ushuru ili kujadili namna ya kutatua tatizo hilo
Halmashauri ya Mji wa Mpanda imebandika matangazo katika masoko hayo matatu akiwaeleza wafanya biashara kuwa wale ambao hawatakuwa tayari
kulipa ongezeko la ushuru waondoke katika maeneo ya masoko hayo Kaimu mkurugenzi wa Mji Mpanda Josefu Mchina aliwaeleza waandishi wa habari ofisini kwake kuwa ushuru ni suala la kisheria na huwa lina
mchakato wake katika kuuanzisha, kuongeza au kuupunguza kabla ya kuanza utekelezaji hivyo ushuru unaolalamikiwa ni halali kisheria na pia umezingatia hali halisi ya bishara na mahitaji ya maendeleo katika
masoko na mji kwa ujumla.
Na WALTER Mguluchuma
Mpanda
Madiwani wa chama cha mapinduzi (CCM) katika Halmashauri ya Mji wa Mpanda wamesusia sherehe ya kumuaga Mkurugenzi wao kutokana na itikadi za siasa
Tukio hilo limetokea hapo jana ambapo Halmashauri ya Mji wa Mpanda iliandaa sherehe ya kumuaga Mkurugenzi wao ambaye alikuwa anastaafu utumishi Bwana Henry Haule
Sherehe za kumuaga Mkurugenzi huyo zilifanyika katika Ukumbi wa Katavi Resort mali ya Abrahamu Kombe ambaye anadaiwa na Madiwani hao kuwa aliwasariti kwenye uchaguzi Mkuu na kuisaidia Chadema
Madiwani hao baada ya kupata taarifa za sherehe za kumuaga mkurugenzi wao kweny Ukumbi wa Katavi walianza kupinga na kutaka sherehe hizo zifanyike kwenye Ukumbi wa Idara ya Mji ambao hata hivyo ulikuwa umeandaliwa kwa shughuli za Mkutano wa wawekezaji na Waziri Mkuu
Sherehe hizo zilianza huku ndani ya Ukumbi kukiwa na madiwani wawili wa kata za kashaulili na makanyagio ambao ni wa Chadema
Wakati sherehe zikiendelea madiwani hao waliendelea na kikao chao nje ya Ukumbi huo kwa lengo la kuendelea na msimamo wao huo Hata hivyo wakati sherehe zikienda mwisho waliingia madiwani wawili wa Chama hicho ambao ni Enock Gwambasa ambaye pia ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji huo pamoja na diwani Willy Mbogo

Walipo hojiwa Madiwani hao sababu iliowafanya waingie mwishoni mwa sherehe walisema tulikuwa na mvutano na wenzetu ila sisi tumeamua kuingia kwenye sherehe
Na Peti Siyame umbawanga
MWENDESHA pikipiki aitwaye Ramadhani Sood (25) amefariki dunia baada ya kugongwa na gari katika kijiji cha Makanyagio katika barabara ya Mpanda –Shanwe iliyopo wilayani Mpanda katika mkoa wa Rukwa.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Rukwa , Isuto Mantage alisema kuwa ajali hiyo ililihusisha basi la abiria aina ya scania yenye namba za usajili T 519 ACV iliyokuwa ikiendeshwa na dereva aitwaye Masoud
Musa (32) mkazi wa Makanyagio mjini Mpanda

Kwa mujibu wa Kamanda huyo wa Polisi gari hilo la abiria lilimgonga mwendesha pikipiki Ramadhani mkazi wa Makanyagio aliyekuwa akiendesha pikipiki aina ya Honda yenye namba za
usajiri T. 612 ANT na kumsababishia majeraha makubwa .
“Ramadhani aliyekuwa mahututi ambapo alikuwa na majeraha makubwa mwilini alifariki muda mfupi baada ya kufikishwa kwenye hospitali ya wilaya ya Mpanda kwa matibabu” alisema Mantage .
Kamanda Mantage alisema kuwa chanjo cha ajali hiyo bado hakijajulikana na kwamba dereva wa gari alikamatwa na atafikishwa mahakamani mara baada ya uchunguzi wa awali kukamilika

Saturday, November 20, 2010
Monday, September 13, 2010
GAZETI LA LEO - MPANDA
NKASI - WAMPEMBE - 17 MBARONI KWA KUVAMIA KITUO CHA POLISI
WATU kumi na saba wanashikiliwa na jeshi la polisi mkoani Rukwa kwa tuhuma za kuvamia kituo cha polisi kwa lengo la kutaka kukiteketeza kituo hicho kwa moto.
Kamanda wa polisi mkoani Rukwa Isuto Mantage amesema Novemba 30,2010 ofisini kwake kuwa wanaoshikiliwa ni wanakijiji wa kijiji cha Wampembe wilaya ya Nkasi mkoani Rukwa baada ya jaribio la kutaka kukitekeza kwa moto kituo kidogo cha polisi cha Wampembe kwa lengo la kumuua mtu mmoja waliyekuwa wanadai kuwa ni mchawi.
Amesema kuwa awali katika kijiji hicho kulitokea msiba wa kijana aliyetajwa kwa jina la Joseph Kapelo (19) baada ya kuugua muda mfupi mnamo Novemba 22, 2010 ambapo kijana huyo aligua majira ya saa mbili asubuhi nakufariki saa tano mchana kifo kilichozua mijadala kijijini hapo wakazi wengi wakidai kuwa marehemu alikuwa amefariki kutokana na imani za kishirikina.
Amefafanua kuwa baada ya kupata taarifa za kifo hicho wananchi walianza kukusanyika katika msiba na kuanza kupanga mikakati ya kummaliza baba wa marehemu aliyetajwa kwa jina la ndugu Daudi Kapelo (76) kwa madai kuwa ndiye aliyamuua mwanae huyo kwani ni miezi miwili tu tangu kijana mwingine mtoto wa huyo mzee alifariki katika mazingira ya kutatanisha kama ilivyotokea katika huo msiba.
Amesema kuwa wakati wananchi hao wakipanga mikakati hiyo taarifa zilifika kituo kidogo cha polisi Wampembe ambapo polisi wa kituo hicho waliweza kuchukua hatua ya kumuokoa Mzee huyo lakini kabla hawajafika msibani tayari Mzee huyo alikuwa ameshaanza kushambuliwa na wananchi na kuokolewa na polisi na mgambo na kasha kuchukuliwa na kwenda kuhifadhiwa kituo cha polisi kwa usalama wake.
Amesema wakati wananchi hai wakielekea kuzika walichukua jeneza la marehemu na kwenda nalo hadi kituo cha polisi ambapo waliliweka jeneza hilo hapo kituoni na kudai wanataka Mzee Daudi Kapelo atolewe humo ndani wammalize naye akazikwe na mwanae na kuanza kushambulia kituo hicho kwa mawe hali iliyopelekea askari kupiga risasi hewani lakini wananchi hao hawakuweza kuogopa na kuanza kumshambulia askari huyo na kuibua mapigano baina ya askari na wananchi wapatao 300.
Amesema kuwa wananchi hao baada ya kutawanyika walikimbia wote wakiwa tayari wameshawasha moto kituo cha polisi kikiungua ambapo askari polisi na mgambo kwa kusaidiana na viongozi wa kijiji walifanikiwa kuuzima moto huo na wananchi hao waliweza kurudi usiku wakachukua maiti ya merehemu na kwenda kuzika usiku huo huo.
Amesema mapambano hayo yaliendelea ambapo mwananchi mmoja Imelda Kayanda (46) alipigwa risasi na kufariki na Agnes Kisori(21) alijeruhiwa mguuni huku vitu vilivyoharibiwa vikiwa ni pamoja na solar panel ya kituo, vioo vya kituo vyote kwa pamoja vikiwa na thamani ya shilingi laki tano.
Amesema majeruhi walipelekwa kituo cha afya Wampembe na baadae hospitali ya wilaya ya Nkasi kupata matibabu ambapo hali zao zimeelezewa kuwa zinaendelea vema.
Amesema tayari jeshi la polisi limewakamata ndugu Zakaria Francis (28), Ikombe Yustini (39), Stephano Kambe (18), Benard Kabeja (16) na John Kapandila (22).
Wengine waliokamatwa amewataja kuwa ni ndugu Said Diwali (36), Vido Tuwakazi (21), Abdalah Vicent (19), Sylveter Kapala (17), Richad Bushota (19), John Mathias (58), Wilbroad Chambi (16) na Kapondo Anatoli (23) na wengine wane wote wakazi wa kijiji cha Wampembe wilaya ya Nkasi.
Kamanda wa Polisi amesema wakati watuhumiwa hao wote watafikishwa mahakamani mara baada ya upelelezi kukamilika na kuwa wengine waliokimbia watafuatiliwa hadi wakamatwe ili sheria ichukue mkondo wake.
Aidha kamanda Mantage ametoa wito kwa wananchi kuacha tabia ya kujichukulia sheria mkononi na tabia mbaya ya kuvamia vituo vya polisi nchini hapa nchini kuwa vinalipeleka taifa kusikojulikana kutokana na ukweli kuwa hizo ni dalili za kuondoa misingi ya amani na utulivu katika jamii.
MWISHO
MBUNGE mmoja wa Chama Cha Mapinduzi wilayani Mpanda amelalamikiwa kuwafanyia kitu mbaya vijana watatu akiwemo mlemavu asiyekuwa na uwezo wa kutembea.
Taarifa zilizolifikia gazeti hili zimeeleza kuwa mbunge huyo mwenye sifa ya kuitwa Mbuyu mdogo amewadhulumu vijana watatu waliokuwa watumishi wa ofisi yake ya bunge katika jimbo lake ofisi zilizoko mjini Mpanda baada ya kuwatumikisha bila kuwalipa mishahara yao halali.
Wakiongea kwa uchungu vijana hao pamoja na binti mmoja mlemavu wa miguu aisyeweza kutembea kwa miguu ya kawaida walidai kuwa mbunge huyo amewadhulumu zaidi ya shilingi miliono moja na laki nane zikiwa ni mishahara na posho za kazi zaidi ya shilingi milioni moja na laki mbili.
Kijana mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Peter Pulwila Panta aliyekuwa ameajiriwa kwa kazi ya udereva na kupewa kitambulisho chenye nambari 001 alisema wamekuwa wakimdai mbunge huyo mishahara yao lakini cha kusikitisha amekuwa akidai kuwa hizo pesa hajaletewa kutoka ofisi ya bunge kitu ambacho si kweli kutokana na maelezo yaliyoko katika barua yenye kumb namba FA.155/2006/01/70.
Alisema licha ya kuwa barua inaagiza kuwalipa mshahara wa kiasi cha shilingi 150,000 kwa mwezi lakini yeye aliwaeleza kuwa watakuwa wanalipwa shilingi laki moja kila mwezi na kuwa alikuwa anakidai kuwa anawalipa kutokana na mshahara wake wa ubunge ihali barua inaonesha kuwa fedha hizo zinatumwa kila mwezi katika akaunti ya mbunge huyo kwa ajili ya mishahara na posho.
Naye binti mwenye ulemavu aliyekuwa akifanya kazi kama mhudumu wa ofisi ya mbunge huyo alisema kuwa tangu mwaka 2005 alikuwa akifanya kazi na kupewa hela ya soda tu shilingi 20,000/= tu kila anapodai mshara wake na kuwa ukosefu wa mshahara kumepelekea mwanaye anayesoma katika shule ya sekondari Mwese kuzuia kuendelea masomo kutokana na madeni ya ada.
Alipofuatwa na mwandishi wa habari ofisini kwake kujua kulikoni anadaiwa na watumishi wake akiwemo mlemavu wa miguu lakini mbunge huyo hakuweza kupatikana badala yake alikuwepo mtu aliyejieleza kuwa ni katibu wa mbunge huyo ingawa alikataa ktaja jina lake aliyeeleza kuwa mbunge wake yuko katika kikao CCM
Juhudi za kumtafuta kwa simu mbunge huyo zilifanikiwa ambapo mbunge huyo alijibu katika simu kuwa anahitaji kuonana na mwandishi wa habari.
Cha kushangaza ni kuwa alikwenda mwandishi ofisini kwake kuzungumzia suala la madeni na kuzomewa alikozomewa wakati wa mkutano wa hadhara katika kijiji kimoja mbunge huyo alimsihi mwandishi huyo asiandike taarifa yoyote mbaya kumhusu na kumpatia kiasi cha shilingi elfu ishirini kwa ajili ya kumziba mdomo pesa ambazo mwandishi alizikataa na kuondoka
Uchunguzi umebaini kuwa madai hayo na mengine mengi yalishawahi kufikishwa katika ofisi za CCM wilaya ya Mpanda na kukosa suluhu ambapo mbunge huyo amekuwa akijinadi kuwa ni mtaalamu wa propaganda, mbuyu mdogo anataka kugombea mwakani kutetea kiti cha ubunge hivyo wasimjadili kuhusu madeni yake.
Mbunge huyo alijikuta akitemwa katika kura ya maoni ndani ya chama chake katika uchaguzi mkuu wa 2010 nchini Tanzania
MWISHO
MILIONI KUMI HIZI ZIMETUMIKA KWELI NAMNA HII
ZAIDI ya shilingi milini 10.1 zimetumika kwa ajili ya kuwanunulia sare za shule na kuwalipia ada na chakula watoto yatima na wanaoishi katika mazingira magumu wilaya ya Mpanda mkoani Rukwa
Mratibu wa asasi isiyokuwa ya kiserikali ya SHDEPHA + tawi la Mpanda Mwalimu Euzebius Ngulusha alisema hayo jana (Novemba 3, 2009) wakati wa hafla fupi ya kuwakabidhi sare, chakula na mahitaji ya shuleni watoto yatima na wanaoishi katika mazingira hatarishi wapatao 54 iliyofanyika katika ukumbi wa SHDEPHA + mjini Mpanda.
Alisema katika kipindi cha Januari hadi Oktoba mwaka huu zaidi ya shilingi milini 10.1 zimetumika kuwahudumia watoto 204 wanaoishi katika mazingira hatarishi, yatima na watoto wanaoishi na Virusi vya UKIMWI wilayani Mpanda fedha ambazo zimetoka kwa wafadhili mbalimbali ikiwa ni pamoja na shirika la Kimarekani la WALTER REED la nchini Marekani.
Alisema shirika lake limelipia ada za sekondari na kuwanunulia sare za shule watoto wanaosoma katika shule za sekondari wapatao 150 kwa gharama ya shilingi 8,304,300/= na watoto wanaosoma shule za Msingi wapatao 35 na wachache wanaotoka katika mazingira hatarishi.
Alisema kiasi cha shilingi 1,800,000 zimetumika kuwanunulia mahitaji ya shuleni kama vile daftari, kalamu, vihifadhio, mifuko ya shule na vifaa vya kuchorea vya wanafunzi hao ili nao wajisikie kama sehemu ya jamii.
Akiongea kwa niaba ya Mkurugenzi wa Mji wa Mpanda afisaelimu wa sekondari wa Halmashauri ya Mji wa Mpanda Said Mwapongo aliwashukuru viongozi wa asasi hiyo ya SHDEPHA + kwa kufanya kazi ya kuwasaidia wanaohitaji katika jamii na kuvishinda vishawishi wanavyokumbana navyo vishawishi ambavyo amesema vinawapelekea kushikwa na tamaa ya kutumia fedha hizo bila kujali ni za nani.
Alisema moyo wa kuwafikishia walengwa ambao hawakujua kama wanaletewa nini ni moyo wa kipekee na wa kiungwana ambapo amewasihi kutokukata tamaa na kuwa Mungu peke yake ndiye atakayewalipa kwa kazi njema hiyo.
Mwapongo aliwasihi wanafunzi hao kuitumia misaada waliyoipata na wanayoendelea kuipata kwa kusoma kwa bidii, kuwa na heshima katika jamii ili kuwawezesha kufikia malengo yao ambayo ni kuwaondoa katika lindi la maisha ya masikitiko na umasikini uliopindukia.
MWISHO
WANANCHI HAWA WAMECHUKIA DILI ZA POLISI AU NI HASIRA KWELI?
WANANCHI wenye hasira wamefanikiwa kuliua jambazi lililokuwa likitafutwa na jeshi la polisi mkoani Rukwa baada ya kumkuta akiiba magunia ya mpunga
Akiyeuwawa ametajwa kwa jina la Revocatus Benedicto Katunga mwenye umri wa miaka 33 mkazi wa Nsemulwa mjini mpanda ambaye aliuwawa na wananchi Septemba 23,2009 saa kumi na mbili asubuhi mara baada ya kukutwa akiiba magunia ya mpunga katika mashine ya kusaga ya mfanyabiashara anayejulikana kwa jina la Kasimu lyanga maarufu kwa jina la Usayi.
Kamanda wa polisi mkoani Rukwa Isuto Mantage aliwaeleza waandishi wa habari kuwa siku ya tukio marehemu anayesadikiwa kuwa ni jambazi sugu aliyekuwa anatafutwa na jeshi hilo alikutwa na wananchi akiwa katika harakati za kuiba magunia ya mpunga ambapo alikuwa ameshaiba magunia manne ya kuyatoa nje ya jingo hilo .
Alisema baada ya kumkuta marehemu huyo wananchi hao walianza kumhoji lakini akawa anawajibu maneno ya jeuri kwa sauti kubwa iliyowaamusha majirani wengine waliofika hapo na kumkuta jambazi huyo aliyekuwa akitafutwa na jeshi la polisi mkoani Rukwa kwa tuhuma za kushiriki katika matukio kadhaa ya uhalifu walianza kumpa kipigo hadi akapoteza fahamu ndipo wakawaita polisi kituo cha Mpanda.
Alisema kamanda Mantage kuwa polisi walipofika eneo la tukio walimchukua marehemu na kumwahisha hospitali ambako kabla ya kupewa huduma yoyote alifariki akiwa eneo la hospitali.
Kamanda alisema hakuna aliyekamatwa kuhusiana na tukio hilo ambapo alieleza kuwa marehemu alikuwa akitafutwa kwa kosa la kuvunja na kuiba vitabu katika shule ya msingi Katavi iliyoko mjini Mpanda na pia alikuwa na kesi mahakani ya kuiba kwa kutumia silaha
Kwa upande wao wananchi wa eneo la Mpanda Hoteli mjini Mpanda walionesha kusikitishwa kwao na mwenendo wa utendaji kazi wa jeshi la polisi wilayani Mpanda kwani jambazi huyo alikuwa ameshikana kukamatwa na jeshi hilo hadi walipomkamata wananchi wenyewe na kumpa hukumu ya kifo licha ya kuwa alikuwa na matukio mengi ya kutafutwa.
the end

Sunday, August 22, 2010
CHAKACHUA YA PINDA YAISUMBUA CHADEMA
Na Willy Sumia, Mpanda
WAZIRI mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mizengo Pinda ambaye amepita bila kupingwa katika kinyang’anyiro cha ubunge katika jimbo la Katavi mkoa wa Katavi kumeelezewa na wananchi wa jimbo lake kuwa ni uamuzi wa siku nyingi kabla hajateuliwa kuwa Waziri Mkuu.
Hayo yalielezwa na baadhi ya wananchi wa jimbo hilo katika mahojiano ya hivi karibuni na waandishi wa Habari mara baada ya tume ya uchaguzi jimbo la Katavi kutangaza kuwa Pinda amepita bila kupingwa kutokana na wagombea wane wa CUF, CHADEMA, NLD na CHADEMA kujitoa katika kinyang’anyiro hicho kwa barua.
Wananchi hao wanaotoka katika vijiji vya Ilunde, Ilela, Majimoto, Kasansa na Kilida walidai kuwa tangu Pinda awe mbunge wa jimbo lao lililokuwa awali likiitwa jimbo la Mpanda Mashariki kumekuwa na maendeleo makubwa pamoja na mabadiliko ya kiuchumi kwa wananchi hao.
Ndugu Hussein Omari mkazi wa kijiji cha Inyonga alisema kuwa wananchi wa tarafa ya Inyonga walikuwa wakiteseka sana kutokana na kukosekana kwa barabara ya uhakika na mawasiliano ya simu lakini tangu Pinda awe mbunge wao wameweza kupata miundombinu hiyo kwa kasi ya ajabu.
Mmoja wa wagombea waliokuwa wametangaza nia ya kugombea katika jimbo hilo ndugu Sebastiani Kasinge alisema kuwa mara baada ya kuchukua fomu ya kugombea ubunge jimbo la Katavi kwa Pinda alipata upinzani mkubwa sana toka kwa wananchi wa jimbo hilo, ndugu zake na hata ndani ya Chama chake cha CHADEMA.
Alisema kuwa uamuzi wake wa kuchukua fomukatika jimbo hilo ulipelekea mvutano mkubwa ndani ya CHADEMA na kupelekea mbunge wa jimbo la Mpanda kati CHADEMA Said Arfi kutangaza kujitoa katika uchaguzi iwapo chama chake kingesimamisha mgombea jimbo la Pinda ambapo mwenyekiti wa CHADEMA mwasisi aliamua kujivua uanachama wa CHADEMA na kuhamia chama kingine cha siasa katika kikao kilichokuwa kikijadili wagombea.
Chanzo cha uhakika cha habari toka katika chama cha CHADEMA kimeeleza kuwa CHADEMA ndio waliokuwa wakishinikiza Pinda apite bila kupingwa katika jimbo hilo lakini baadhi ya viongozi wa CCM walikuwa wakitaka kuwepo na mgombea ili wapate mshiko wa kampeni katika jimbo hilo na kutofautiana na katibu wa CCM wa wilaya Mohamed Omary Nyawenga aliyeonekana akifanya juhudi za kweli kuhakikisha Pinda anapita bila kupingwa akishirikiana na baadhi ya wananchi wa Inyonga.

Nguruwe kunywa dawa za Kupunguza makali ya VVU ARVs inakuwajeeeeeee
Iringa
WADAU wa asasi zisizo za kiserikali nchini wametoa onyo kwa wafugaji na wakulima wanaotumia dawa za binadamu kuwapa mifugo na kupulizia kwenye mazao na kusababisha ongezeko la madhara makubwa kwa jamii.
Hayo yalizungumzwa na washiriki wa mafunzo ya uchambuzi wa Sera yaliyoandaliwa na Mwamvuli wa asasi za kiraia mkaoni Iringa na Njombe Iringa Civil Society Organizations (ICISO) katika ukumbi wa Lutherani
mjini Makambako katika mkoa mpya wa Njombe wiki iliyopita.
Wadau hao walisema kuwa tabia iliyoibuka hivi karibuni kwa baadhi ya wafugaji na wakulima kutumia dawa zitumikazo kwa ajili ya binadamu kwa kuipa Mifugo hali inayopelekea kuibuka kwa magonjwa yasiyofahamika na kusababisha madhara kwa walaji wa bidhaa zitokanazo na mifugo.
Bwana Obothe Msemakweli mmoja wa wadau kutoka asasi ya LUCAPOA ya wilayani Ludewa alisema baadhi ya wakulima wa zao la nyanya wamekuwa wakipulizia dawa ya kuua Mbu aina ya Ngao katika zao hilo kwa lengo la kuua wadudu waharibifu wa zao hilo hali inayowaletea madhara walaji.
“Unajua wakulima wanapotosha sana matumizi sahihi ya dawa ya Ngao, imefikia baadhi ya wakulima wanapulizia katika miche ya nyanya hali inayopelekea walaji kudhulika,” Alisema Msemakweli.
Walisema pia dawa za uzazi wa mpango ambazo hutumiwa na akinamama kupanga uzazi zimekuwa zikitumiwa na baadhi ya wafugaji huwapa kuku kwa lengo la kuwafanya wakue haraka ili kupata bei nzuri ya mifugo hiyo kutokana na tamaa ya pesa.
Wadau hao walisema wanyama aina ya Nguruwe nao wamekuwa wakipatiwa vidonge vya ARVs ambavyo hutolewa kwa wagonjwa wa Ukimwi ili kuwaongezea siku za kuishi na mazao ya mahindi na Maharage yamekuwa yakiwekewa dawa ya Ngao ya unga kwa imani kuwa hayatabunguliwa na Fukuzi wadudu waharibifu wa mazao.
Bi Grace Sanga wa asasi ya PROMISE ya mjini Iringa alisema upotoshwaji wa matumizi hayo ya dawa yanajengwa na uzushi ambapo wafugaji na wakulima huamini kuwa baada ya kuwapa mifugo dawa za binadamu, kuku na Nguruwe hukua haraka bila kuwa na ushauri wa kitaalamu.
Bwana Renatus Mpiluka mwanachama wa asasi ya MUNGONET ya Mufindi alifafanua kuwa hali hiyo inatokana na sera nyingi kutungwa na kuishia katika vitabu na wananchi kushindwa kuzifahamu hali inayopelekea baadhi ya wananchi kufanya mambo kinyume na utaratibu wa sera husika.
“Sera ya Kilimo, yenye kauli mbiu ya Kilimo kwanza naieleweki kwa baadhi ya wakulima ambao ndiyo walengwa wakuu wa mpango huo, kuna hajaya serikali kutoa elimu sahihi ya sera ili jamii izifahamu.” Alisema
Renatusi
Naye ndugu Leonard Kalolo mujumbe wa asasi ya LIMAU ya Mgololo wilayani Mufindi alisema wakulima na wafugaji wapatiwe elimu ili kupunguza matumizi yasiyo sahihi ya dawa hizo pamoja na udhibiti wa usambaaji wa dawa za binadamu.
“Mbolea na madawa zinatumiwa vibaya, unakuta mtu anaweka mbolea hata kwenye mazao ya muda mfupi kama mboga mboga, hii inasababisha kumfikia mlaji kemikali za madawa hayo zikiwa bado hazijaisha na
kusababisha maradhi ,” alisema ndugu Kalolo.
Wadau hao wa asasi zisizo za Serikali waliitaka serikali itoe elimu sahihi kwa wakulima juu ya Sera mbalimbali zitolewazo na serikali ikiwa ni pamoja na kuwashirikisha wananchi katika utungaji wa Sera
kwani wao ndiyo watekelezaji wakuu wa irani hizo.
Naye muhadhiri wa chuo kikuu cha Tumaini mkoani Iringa Lucas Mwahombela aliitaka serikali kuingilia kati ukiukwaji wa matumizi hayo ikiwa ni pamoja na kuziweka wazi sera mbalimbali hasa za Kilimo ambazo
zinawalenga watu wa hali ya chini ili wazielewe na kufanikisha sera ya Kilimo kwanza na kauli mbiu ya Mapinduzi ya Kijani.

MWENYEKITI mwasisi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo wilaya ya Mpanda mkoa wa Rukwa amekihama chama chake baada ya kunyimwa fursa ya kuwa mgombea wa Udiwani katika kata mpya ya Makanyagio mjini Mpanda katika mkoa wa Katavi.
Mwenyekiti huyo Bwana Juma Mausi alihama chama chake mara baada ya kuanza kwa mchakato wa uchaguzi mkuu wa 2010 kuanza kupamba moto kufuatia kuanza kwa mikutano ya kampeni na kujikuta akitupwa nje ya timu ya wagombea wa CHADEMA katika kinyang’anyiro cha udiwani kata ya Makanyagio baada ya nafasi hiyo kupewa mjumbe wa serikali ya mtaa wa Kachoma ndugu Nziguye Juma.
Juma Mausi ambaye ndiye aliyeipokea na kuasisi chama cha CHADEMA wilaya ya Mpanda wakati wa vuguvugu la vyama vingi nchini alijikuta akikihama chama chake baada ya kubaini kile alichokieleza yeye
mwenyewe kuwa CHADEMA imekamatwa na wageni na kukiita kitendo hicho kuwa ni Uvamizi wa kisiasa ndani ya CHADEMA yake.
Taarifa sahihi toka katika chanzo cha kuaminika ndani ya CHADEMA zimeeleza kuwa baada ya kuona haridhishwi na uamuzi aliofanyiwa ndani ya CHADEMA Mzee Mausi aliamua kujiunga na chama cha NCCR Mageuzi ambako alipewa nafasi ya kuwa mgombea wa chama hicho katika king’anyiro cha udiwani kata ya Makanyagio ili kupambana na wagombea wa CCM, CHADEMA na CUF.
Juma Mausi alikuwa mwenyekiti wa CHADEMA wilaya ya Mpanda hadi Agosti alipotangaza kuachana na chama hicho na kuhamia NCCR Mageuzi hali iliyopelekea CHADEMA wilaya ya Mpanda kutafuta mwenyekiti wa muda katika kipindi hiki cha uchaguzi ambapo chama hicho kinatetea nafasi ya ubunge jimbo la Mpanda mjini ambapo mbunge wa sasa wa jimbo hilo ni mheshimiwa Said Arfi wa CHADEMA.
mwisho

Saturday, August 14, 2010
BARABARA ZA LAMI RUKWA
RAIS Jakaya Mrisho Kikwete amewka jiwe la Misngi katika mradi mkubwa
wa umeme wenye thamani ya shili Bilioni 12 kwa ajili ya Miji ya
Namanyere na Sumbawanga mkani Rukwa. Mradi huo uliwekewa jiwe la msingi katika eneo la Mitambo ya umeme ya shirika la umeme nchini TANESCO mjini Sumbawanga Jumamosi iliyopita unajumuisha mashine nne kubwa zenye uwezo wa kuzalisha kilowatt 5 za umeme kwa wakati mmoja zilizonunuliwa na serikali kwa gharama ya shilingi Bilioni 3.
Akitoa taarifa mbele ya Mheshimiwa Rais Waziri wa Nishati na Madini Wiliamu Ngeleja alisema kuwa mradi huo wa umeme unaanza Julai 2010 na kukamilika Juni 2011 ambapo waziri huyo alimueleza rais kuwa umeme utaanza kuwaka mjini Namanyere Machi 2011. Aidha Waziri Ngeleja alisema kuwa mradi huo utawawezesha wananchi waishio katika vijiji vinavyopitiwa na nguzo za umeme katika barabara ya kuelekea Namanyere mjini kupatiwa umeme kwa ajili ya matumizi ya majumbani na matumizi mengine kama ilivyo kwa wananchi wa mijini.Waziri Ngeleja alisema kuwa Serikali imeondoa gharama za nguzo kwa wananchi wa vijijini ili kupunguza gharama za kuingiza umeme katika nyumba zao na badala yake gharama za nguzo zitakzotumika kuingizia umeme kwa wananchi serikali ndiyo itakayogharamia kutokana na ukweli kuwa wananchi wa vijijini wana kipato kidogo ukilinganisha na waishio mijini.
Naye Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. Jakaya Mrisho Kikwete aliwataka wananchi wa vijiji husika kuanza kujiandaa kuupokea umeme pindi utakapofika ikiwa ni pamoja na kuachana na ujenzi wa nyumba za nyasi kwa rais alisema nyasi hazipatani na umeme “ Ndugu zangu wananchi wa Kipande na wengine walioko katika njia hii, changamkieni umeme huu ili mpate maendeleo ya haraka, acheni kujenga nyumba za nyasi kwa sababu umeme na nyasi haviendani, jengeni nyumba bora hivi sasa ili umeme ukifika kijijini kwenu muupokee na kuanza kuufaidi” alisema Mhe. Rais Rais Kikwete alisema hivi sasa wananchi wa Rukwa neema imewashukia kwani tayari umeme wanatarajia kuupata wa uhakika, barabara nazo zinajengwa kwa kiwango cha lami na pia kuna maboresho ya kilimo kupitia dhana ya KILIMO KWANZA.
Alifafanua kuwa kilimo kikizalisha mazao ya kutosha sasa wananchiwataweza kusafirisha mazao hadi kwenye soko bila matatizo na tena wakiuza mazao kwa bei nzuri katika soko wataweza kuutumia umeme
kujiletea maendeleo na hayo ndo maisha bora kwa kila Mtanzania.

Subscribe to:
Posts (Atom)