Thursday, September 17, 2009

KAMA VILEEEEEEEEEE

Na Willy Sumia, Mpanda
SHULE ya Msingi Kivukoni iliyoko katika Kata ya Ikolongo wilaya ya Mpanda mkoani Rukwa haina vyumba vya madarasa licha ya kuwa na wanafunzi wa darasa la kwanza hadi la saba.

Uchunguzi uliofanywa na waandishi wa habari shuleni hapo umebaini kuwa shule hiyo iliyoanza mwaka 2003 ina jumla ya wanafunzi 265 wa darasa la kwanza hadi la saba na walimu watatu ambao nao hukaa katika majengo ya kanisa.

Wanafunzi waliokutwa shuleni hapo na waandishi waliofika shuleni hapo wakiongozana na Mbunge wa Jimbo la Mpanda Kati Said Arfi walisema kuwa wamekuwa wakisomea katika vibanda vya miti na udongo vya zamani vilivyojengelewa miaka kumi iliyopita lakini uongozi wa Halmashauri ya wilaya ya Mpanda haujawahi kuwajengea hata darasa moja.

Walisema kuwa nyakati za masika masomo yao huendeshwa kimachale huku wakichungulia angani kama kuna mawingi ya mvua ili waweze kukimbilia katika majengo ya kanisa yaliyoko kaijijini hapo

Walipoulizwa na waandishi kama walimu huwa wanakaa wapi wanafunzi hao walidai kuwa kawaida walimu huwa wanakaa katika madawati kusahihisha madaftari na huwa wanawachanganya darasa la tatu na la nne katika kuwafundisha pamoja ambapo hawakusita kueleza kuwa hawajui meza ya mwalimu na kiti chake kwani hawajawahi kuviona shuleni hapo.

Baadhi ya walimu walioongea na waandishi walisema kuwa wamekuwa wanapata shida katika ufundishaji kutokana na mazingira yanayowakabili katika shule hiyo kwani hakuna ofisi ya walimu, madarasa wanayotumia ni chini ya mti na katika vibanda vya udongo ambavyo navyo havijulikani mlango wala dirisha lake kutokana na kuanguka kwa maudongo.

Walimu hao walithibitisha kuwa hakuna meza za walimu wala viti vyake kutokana na shule hiyo kutokujulikana licha ya kuwa imesajiriwa na kupewa namba ya usaliri namba 168 na kuwa hata mazingira wanayoishi ni magumu sana kutokana na eneo hilo kuwa mbali na zahanati umbali wa kilometa 25 toka shuleni hapo na kuwa wanapata shida pindi wanapougua au kuuguliwa.

Mama mzazi mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Zaingiye Ndikumana alisema kuwa vibanda hivyo vya udongo vilijengwa na wanakijiji kwa ajili ya kukaushia tumbaku lakini wakawa wanahitaji shule ndipo wakaamua kuwa watoto wao waanze kusomea katika vibanda hivyo na tangu 2003 tayari wameshamaliza wanafunzi wa darasa la saba mwaka jana na kufdaulu wanafunzi wane kuingia kidato cha kwanza.

Alisema katika kipindi cha kiangazi watoto wanaugua sana mafua kutokana na vumbi la chini ya mti wanaposomea na vibandani kukosekana sakafu ya kuzuia vumbi lakini wafanyaje na wanahitaji watoto wao wasome shule wapate elimu.

Taarifa za shule hiyo zinaonesha shule hiyo ilikuwa na wanafunzi mia nane lakini kutokana na mazingira kutokuboreshwa wanafunzi wameacha shule na kubaki 265 sawa na muanguko (drop out) wa 302% (aslimia 302) ambapo wanafunzi wa darasa la saba waliomaliza mwaka 2008 walikuwa 54 na wanafunzi wanaotarajiwa kumaliza mwaka huu wako 40 licha ya kuwa utoro kwa wanafunzi wa darasa la saba kwa mwezi Julai ni 75%.

Afisa Elimu wa Halmashauri ya wilaya ya Mpanda Labani Bitulo alipotafutwa ofisini kwake ilielezwa kuwa yupo katika ziara ya Naibu waziri wa Elimu na alipopigiwa simu yake ya mkononi na kuuulizwa na waandishi wa habari juu ya hali ya shule ya msingi Kivukoni alijibu kuwa suala hilo inabidi kuongea ana kwa ana na kisha akakata simu yake ya mkononi

Baadhi ya wananchi walipoulizwa juu ya hali ya shule walieleza kuwa hiyo inatokana na tabia ya viongozi wa ngazi ya wilaya pindi wanapotembelewa na mawaziri au viongozi wa kitaifa kuwatembeza sehemu nzuri na kuficha matatizo yaliyoko katika jamii kwani hakuna kiongozi aliyewahi kufanya ziara katika kijiji hicho licha ya kuwa kijiji hicho ni sehemu ya jimbo la Mpanda Mashariki ambapo mbunge wake ni Mheshimiwa Mizengo Kayanza Piter Pinda Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
MWISHO.

HABARI

HALMASHAURI YA MJI NA NDOTO

HALMASHAURI ya Mji wa Mpanda imeweza kutoa elimu ya ujasiliamali kwa wakulima 55 kupitia maonesho ya wakulima nane nane yaliyofanyika katika uwanja wa maonesho wa John Mwakangale.

Waliofaidika na elimu hiyo ni wakulima 30, wafugaji 10, wajasilaiamali 11, na wanamazingira 4 ambao licha ya kujionea namna ya kulima, kufuga na kufanya shughuli zao kitaalamu kwa wenzao wa mikoa mingine ya kanda ya Nyanda za Juuu pia nao walipata fursa ya kuonyesha bidhaa wanzaozalisha kwa wenzao.

Mkurugnezi wa Mji wa Mpanda Simon Mayeye alisema kuwa lengo ni kuwapa fursa zote za kuwawezesha kuongeza kipato chao kwa kuongeza uzalshaji wa bidhaa mbalimbali katika maeneo ya mjini kwa gharama nafuu kwakutumia teknolojia rahisi.

Mayeye alisema kuwa endapo wakulima hao watatekeleza kwa vitendo waliyojifunza basi matokeo ya kazi zao yataleta maendeleo makubwa sana katika familia zao na jamii kwa ujumla kwani wamejifunza mambo mengi kuanzia darasani hadi Uwanjani.

Alisema awali walipata mafunzo katika chuo cha Maendeleo Msaginya na baadaye katika Chuo cha Kilimo Laela wilaya ya Sumbawanga kisha kuhudhuria katika maonesho ya nane nane katika uwanja wa John Mwakangale jijini Mbeya .

Mkurugenzi huo alisema kuwa hivi sasa Halmashauri yake imejikita katika kilimo licha ya kuwa wakazi wake ni wa mjini lakini wanajishughulisha na kilimo katika vijiji vya pembezoni mwa mji wa Mpanda na ndio wakulima wanaotegemewa katika vijiji husika kutokana na ukweli kwamba ndio pekee wanaolima kilimo cha biashara huko vijijini.

Alisema tayari mpango wa kuhakikisha pembejeo ya ruzuku inapatikana kwa wakati umeshaanza kwa kutengeneza daftari la wakulima linaloonesha idadi ya ekari, aina ya mazao na maeneo wanakolima kwa kila mkulima aliyeko katika eneo la Halmashaufri ya Mji Mpanda.

Alisema kuwa katika bajeti ya 2009/10 Halmashauri yake imetenga kununua matrekta madogo 50 kwa ajili ya kilimo na kuwapa mafunzo wakulima ya ugani ili waweze kukabiliana na changamoto ya upungufu wa maafisa ugani katika Halmashauri yake ambayo inahitaji maafisa ugani kwa 75%.

Halmashauri ya Mji wa Mpanda ina eneo la kilometa za mraba 90.4 na wakazi wapatao 61,000 kwa mujibu wa takwimu za 2008 na inaundwa na kata sita za Kawajense, Kashaulili, Misunkumilo, Nsemulwa, Shanwe na kata ya Ilembo.
MWISHO.