Wednesday, July 31, 2013

BONDE LA KATUMA WACHAGUANA

JUMUIYA YA WATUMIA MAJI YA BONDE DOGO LA MTO KATUMA IMEFANYA UCHAGUZI WA VIONGOZI WAKE JANA JULAI 30, 2013

MATOKEO NI KAMA YALIVYO HAPA CHINI

















 
JUMUIYA ya watumia maji ya bonde dogo la mto Katuma wilaya ya Mpanda mkoa wa Katavi wametakiwa kuepuka rushwa katika utendaji kazi wao

Angalizo hilo limetolewa na Kaimu Katibu Tawala wa wilaya ya Mpanda, Joseph Mzimya kwa wanajumuiya watumia maji ya bonde dogo la mto Katuma kwa Kaimu jana Julai 30,2013 katika ukumbi wa shule ya sekondari ya St. Mary’s  Mpanda kufuatia jumuiya hiyo kukamilisha mchakato wa uundaji katiba yake

amesema baada ya kujengewa uwezo na ofisi ya bonde la ziwa Rukwa wameweza kuandaa katiba yao itakayokuwa mwongozo katika kudhibiti matumizi holela ya maji ya mto Katuma pamoja na kulinda mazingira ya bonde dogo la mto huo hivyo kabla ya kuanza kazi wanapaswa kujua kuwa Rushwa kwao ni mwiko

Katibu Tawala wa wilaya ya Mpanda kuwa ofisi ya Mkuu wa wilaya inaitegemea jumuiya hiyo kumaliza migogoro iliyoko katika bonde hilo ambapo wakulima wanagombania maeneo ya kulima na wafugaji wanagombania maeneo ya kufugia na kulishia wanyama hivyo kuna kila sababu kwa jumuiya hiyo kusimama imara katika kazi zake

Alisema Miongoni mwa jukumu la jumuiya ya watumia maji ya bonde dogo la mto Katuma ni kulinda, kusimamia, kuhifadhi na kuendeleza rasilimali ya maji yaliyoko katika mto Katuma ambapo jumuiya hiyo ina uwakilishi kutoka vijiji tisa vilivyoko katika bonde la mto Katuma

Baadhi ya changamoto walizoziainisha ni pamoja na kilimo holela, matumizi ya vizibo vya maji kwa baadhi ya wakulima wa zao la mpunga katika bonde hilo, ufugaji usiozingatia hifadhi ya mazingira, uvamizi wa chanzo cha mto Katuma katika mlima Waitaba kijiji cha Bugwe unaofanywa na wafugaji pamoja na matumizi ya kemikali katika machimbo ya madini na kutiririsha maji katika mto

Akizungumza kwa niaba ya mkuu wa wilaya ya Mpanda, Kaimu Katibu Tawala wa wilaya hiyo, Joseph Mzimya amewataka wanajumuiya hiyo kufanya kazi kwa uaminifu na uadilifu mkubwa kabla ya uzinduzi ili serikali ione matunda mazuri kutoka kwenye jumuiya ambayo ni kumalizika kwa migogoro iliyopo katika bonde hilo

Amewasihi viongozi wa jumuiya kuepukana na vitendo vya Rushwa katika jumuiya yao kwani serikali inataka kuona haki inatendeka kwa misingi ya usawa bila kujali uwezo wa mtu kifedha au nafasi yake katika jamii kwani katika kazi za uzalishaji mali kila mmoja ana mchango wake kwa taifa na jamii nzima

Aidha mkuu wa wilaya ya Mpanda ameziagiza halmashauri zilizopo katika bonde hilo za Nsimbo, Halmashauri ya Mji na Halmashauri ya wilaya ya Mpanda kukamilisha haraka zoezi la mpango wa upimaji ardhi katika vijiji na kuweka mpango wa matumizi bora ya ardhi ili kuipa nafasi jumuiya kusimamia bonde dogo la mto Katuma kwa ufanisi