Monday, August 12, 2013

KATALA BEACH HOTEL SINGIDA YAZINDULIWA RASMI

IPO KATIKA MANISPAA YA SINGIDA PEMBEZONI MWA ZIWA SINGIDANI




VYUMBA VYA KULALA VYA AINA ZOTE KWA BEI NAFUU

SINGIDA MANISPAA
Wasanii wakitumbuiza katika viwanja vya hoteli ya Katala Beach Singida wakati wa uzinduzi wa hoteli hiyo uliofanywa na kiongozi wa Mbio za Mwenge 2013 ndugu Juma Ali Simai Agosti 11, 2013







JIKONI

MALIWATO / VYOO VYA NJE


FLAMINGO HALL NA UTEMINI HALL, JENGO LILILOZINDULIWA NA MWENGE

TAYARI WAZUNGU WAMEANZA KUHOTELI YA KBH YA SINGIDANI

MMILIKI WA KATALA HOTELI , KITILA MKUMBO AKIFURAHIA UZINDUZI WA HOTELI YAKE


MMILIKI NDUGU KITILA MKUMBO AKITAFAKARI JAMBO SIKU YA MWENGE 2013

TAARIFA YA UJENZI WA KATALA BEACH HOTELI






TUNAZINDUA KAMA IFUATAVYO



WATANZANIA MSIICHAFUE TANZANIA NJE

WATANZANIA wameaswa kuepuka vitendo vinavyoitangaza Tanzania vibaya nje ya mipaka  vinavyofanywa na baadhi ya wananchi wanapokuwa nje ya nchi yetu na kuharibu taswira ya Tanzania katika ramani ya dunia

Wito huo ulitolewa jana na kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka huu 2013, Juma Ali Simai katika kituo kikuu cha mabasi mjini Singida Agosti 11, 2013 mara baada ya kumaliza mbio za Mwenge wa Uhuru katika Manispaa ya Singida wilaya ya Singida mkoani hapo

Simai alisema hivi sasa kumeibuka tabia ya kuharibu sifa ya Tanzania kitaifa na kimataifa inayofanywa na baadhi ya wananchi wanapokuwa ndani au nje ya nchi kwa vitendo vyao vya kuitangaza vibaya Tanzania kinyume na hali halisi ya Watanzani na mambo yanavyokwenda hapa nchini

Alisema hivi sasa kumekuwa na tabia ya kuilaumu serikali kila kukicha licha ya kuwa serikali imekuwa ikifanya mambo makubwa na ya maana kabisa kwa wananchi kwa lengo la kuwaondoa katika lindi la umasikini na kuhakikisha kuwa lengo la maisha bora kwa kila Mtanzania linafikiwa na kuondoa changamoto zinazowakabili wananchi

Alisema kuna baadhi ya watu wakisafiri kwenda nje kwenye mikutano ya kimataifa wanatumia mwanya huo kuitangaza Tanzania vibaya kwa maslahi yao binafsi bila kujali kuwa kufanya hivyo ni kujiaibisha mwenyewe pia ni kosa mbele ya Mwenyezi Mungu kusema uongo

Alisema wananchi wawe macho na watu hao ambao wamekuwa wakipita huku nakule nchini wakieneza propaganda zisizofaa tena zenye ubaguzi ambapo alisema wengine wamefikia hata kudai kuwa Mwenge wa Uhuru hauna maana kwa nchi yetu ya Tanzania

Mwenge wa Uhuru uko mkoani Singida ambako tayari umemaliza ziara katika wilaya za Iramba na Singida


CHUMBA KIMOJAWAPO KILIVYOPANGWA KWA NADHIFU

WAHUDUMU WAPO FIT


HONGERA KAKA YANGU MAMBO MAKUBWA HAYA

MANDHARI INAVUTA USIKIVU


SIYO ULAYA NI SINGIDA



KITANDA NDANI YA CHUMBA CHA SUIT



SIYO AFRIKA YA KUSINI NI BONGO TENA SINGIDA




PICHA YA PAMOJA

NIMEONA MAMBO MAZURI NDANI MZEE






 ALIYEACHA KUTUMIA MADAWA YA KULEVYA APEWE AJIRA - DC

Singida
MKUU wa wilaya ya Singida mkoani Singida, Mwalimu Queen Mlozi amemuagiza mganga mkuu wa Manispaa ya Singida kumuajiri kijana aliyekuwa anatumia madawa ya kulevya na kuamua kuachana nayo

Agizo hilo lilitolewa na Mkuu huyo wa wilaya kufuatia ushuhuda uliotolewa na kijana Yusufu Saimoni Shumbi mbele ya wananchi katika viwanja vya stendi kuu ya mabasi Singida jana katika ukaguzi wa mabanda ya Mwenge yaliyopo eneo hilouliofanywa na Mkuu wa wilaya

Alisema maelezo ya kijana huyo yanaonesha kuwa miongoni mwa kilichosababisha Yusufu kuanza kutumia madawa ya kulevya ni kukosekana kwa kazi ya kufanya na kumpa vishawishi vya kujiunga na makundi ya madawa ya kulevya hivyo uamuzi wa kwanza wa serikali ni kumpa shughuli ya kufanya kijana

Alisema vijana wanaotumia madawa ya kuelvya wako wengi na wanahitaji kuwafuatilia kwa karibu ili kuwarejeha katika hali ya kawaida na kuokoa nguvukazi ya Taifa hivyo Manispaa ya Singida itafute mbinu za kuwaweka karibu vijana walioko katika janga la madawa ya kulevya waachane na madawa hayo

“Mganga nakupa kazi moja kubwa, kuanzia leo tafuta namna ya kumpa kazi ya kufanya kijana huyu ili asije akarejea katika madawa ya kulevya na taarifa niipate haraka sana” alisema mkuu wa wilaya

Awali akitoa ushuhuda wake Yusufu Saimoni Shumbi amesema alianza kutumia madawa ya kulevya alipokuwa kidato cha pili katika shule ya Sekondari Kikatiti ambako alikuwa na rafiki zake wengine ambao walikuwa wanasoma naye na baada ya kumaliza na kufeli mtihani aligundua kuwa alijipotezea muda shuleni

Alisema kutokana na kutumia madawa hayo alibadilika afya yake akawa anaugua mara kwa mara kichwa, mwili kulegea na kukosa kumbu kumbu pamoja na kukosa uwezo wa kujimudu katika baadhi ya matendo kutokana na mwili wake kulegea mikono na mikono

Alisema hivi sasa ameamua kurudia mtihani wa kidato cha nne kwani awali alifanya mtihani huo na kufeli mwaka 2011 lakini kutokana na uwezo mdogo aliokuwa nao kutokana na kutumia madawa ya kulevya alipata daraja la nne alama 30

Kwa upande wake mama mzazi wa Yusufu, Grace Shumbi (50) amesema mwanae ni kitinda mimba katika familia yake ya watoto tisa ambapo wamekuwa wakiishi kwa kutegemea kodi ya nyumba kwani alikuwa akifanya kazi ya kuhubiri neon la Mungu katika shirika la Life Ministry na kustaafu miaka kadhaa iliyopita

Amesema mwanae licha ya kuwa na hali hiyo amekuwa mwaminifu sana nyumbani kwani hata ujenzi wa nyumba kubwa wanayokaa hivi sasa aliisimamia Yusufu wakati huo mama yake akiwa anatibiwa hospitali

Amesema hivi sasa Yusufu anamdai ada akalipe shule ili asome upya aweze kurudia mtihani wa kidato cha nne ili aweze kuendelea na masomo kwani anaelewa kuwa ana uwezo wa kuendelea kusoma shule na kufaulu hadi chuo kikuu bila shida ikiwa tu atapata ada