MAHALI PENYEWE PAKO HIVI KATIKA PICHA TULIYOPIGA JUMAPILI JULAI 28, 2013
KIMEMO kilikutwa katika ofisi kikitoa maelekezo kampuni izuiliwe |
Tunajiandikisha mahudhurio ya mkutano wa hadhara wa Jumuiya ya Watumia maji ya Mto Katuma uliofanyika Jumapili Julai 28, 2013 katika kijiji cha Katuma |
Usingizi Ruksa si hakuna viboko wala maswali!!!!!! |
Kufunga Kikao |
Tunaagana baada ya mkutano |
Hapa siyo kwa Mzee Madiba waliko makaburu ni Ndani ya Mkoa wa Katavi katika barabara ya Sibwesa Katuma |
Kuoshea magari katika mto Mpanda imekuwa kama kawaida vile, hivi wana Mazingira toka Halmashauri ya Mji Mpanda mnasubiri Waziri wa Mazingira aje kufanya ziara ndipo muamke???? |
SAKATA la muwekezaji wa kampuni moja ya madini kudaiwa
kutumia kemikali Katika kuyeyushia mawe ili kupata madini ya dhahabu kisha
kutiririsha maji mtoni limechukua sura mpya baada ya wanakijiji kuagiza
serikali ya kijiji chao kumzuia muwekezaji huyo asiendelee na kazi Katika eneo
la kijiji chao
Barua
aliyoandikiwa muwekezaji huyo na Afisa Mtendaji wa kijiji cha Katuma inamzuia
muwekezaji huyo aliyetambulika kwa jina la LUKMAK MINING (T) LTD ya jijini
Mwanza asiendelee na kazi hadi atakapoweka wazi kazi zake ikiwa ni pamoja na
kuwasilisha nyaraka zinazotakiwa Katika ofisi yake
Katika barua
hiyo yenye kumb Na. MDC/KTM/ VC 28/ 1/64 (nakala tunayo) afisa mtendaji aliitaka
kampuni hiyo kusimamisha shughuli zote Katika eneo hilo hadi atakapokamilisha kutekeleza ushauri
wa kitaalamu kutoka ofisi ya madini kanda ya Magharibi mjini Mpanda pamoja na
kuweka wazi shughuli zake.
Kamera ya Mtandao huu lilifika Katika eneo la uwekezaji la kampuni ya Lukmak Mining (T) Ltd Katika
kijiji cha Katuma kilometa moja kutoka sekondari ya Katuma na kuwakuta
wafanyakazi watano wakiendelea na kazi ambapo walieleza kuwa wanalipwa mshahara
wa shilingi elfu nane kwa wiki na kampuni hiyo na kuwa boasi wao aliondoka wiki
mbili zilizopita kwenda jijini Mwanza
Wakifafanua namna
wanavyotumia kemikali Katika eneo hilo
walisema huku wakionesha matanki kuwa yamejengwa matanki kumi na sita yenye
ujazo wa lita elfu kumi na tatno ya maji, wakishajaza maji humwagia humo mawe
yaliyotoka kwenye mashimo ya madini ambayo wanayaita kwa jina la Kanyero ambapo
humwagia humo kemikali ya kuyeyushia
Licha ya kuomba
kuhifadhiwa majina yao
kwa usalama wa ajira zao walisema baada ya kuyeyuka na kubaki uji mchemko huo
huo hupitishwa Katika mambomba matatu yanayotoka Katika kila tanki na kuelekea
kwenye maabara ambayo imejengwa kwa bondeni ambako hutenganishwa madini ya
dhahabu na tope la takataka yenye kemikali ambalo humwagiwa Katika mashimo
yaliyoko nje ya maabara hiyo
Katika eneo hilo
kuna mwinuko ambao hutiririsha maji Katika mto Katuma na hilo ndo linaloibua
hofu kwa wanakijiji ambao ni watumiaji wakubwa wa maji ya mto Katuma kwa
shughuli za binadamu na wanyama hoja ambazo ziliibuliwa na wananchi Katika
mkutano wa hadhara wa jumuiya ya watuamiaji wa maji ya bonde dogo la mto Katuma
uliofanyika Julai 28, 2013 katika ofisi ya Kata ya Katuma mchana
Wanajumuiya hao
ambao ni wanakijiji wote walilalamikia namna serikali inavyosita kuchukua hatua
ikiwa ni pamoja na kumzuia kabisa muwekezaji huyo kufanya kazi zake Katika eneo
la kijiji chao na kuwa Baraza la Mazingira la Taifa NEMC kufika kijijini hapo
ili kujionea hali halisi kwa lengo la kuepusha madhara yanayoweza kuwakumba
wanakijiji hao.
Akizungumza na mtandao huu, Afisa Maendeleo ya Jamii Mwandamizi kutoka ofisi ya Bonde la mto
Katuma, Thadeusi Ndeseiyo alisema kumbu kumbu za ofisi yake zinaonesha kampuni
hiyo ya Lukmak (T) Ltd haina kibali cha Wizara ya Maji cha kutumia maji ya mto
Katuma kwa shughuli zake kinyume cha utaratibu uliopo ambapo makampuni yote
yanayotumia maji Katika shughuli zake hutakiwa kulipia maji hayo Wizarani na
kupewa kibali cha kutumia maji.
Ukataji miti kiholela ni tatizo linalochangia kwa kiwango kikubwa katika uharibifu wa Mazingira, hapa ni jirani na shule ya sekondari Katuma ambako msitu unaisha kwa kukatwa |
TOA MAONI YAKO KWA KUPITIA willysumia@gmail.com au 0767519989