Saturday, September 15, 2012

LEO MATUKIO

ZIARA YA MBUNGE AMOS MAKALLA JIMBONI MVOMERO


 Mbunge Amos Makalla, ambaye ni Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, kusikiliza kero za wananchi , Kijiji cha Kibagara 
 Kukata utepe ikiwa ni ishara ya kuzinduzi wa Ofisi ndogo ya Mbunge wa Jimbo la Mvomero

 Wananchi wa Kijiji cha Kibagara, Kata ya Tchenzema ,Wilaya ya Mvomero, wakimkabidhi zawadi ya mbuzi 'nyama' Mbunge wao Amos Makalla ( mwenye suti kulia
Wananchi wa Kijiji cha Kibagara, Kata ya Tchenzema , Wilaya ya Mvomero wakimsikiliza Mbunge wa Jimbo hiyo, Amos Makalla ( hayupo pichani) Septemba 22, mwaka huu.
Mbunge wa Jimbo la Mvomero, Amos Makalla, ambaye pia ni Naibu Waziri wa Habari, Vijana , Utamaduni na Michezo, Septemba 22, mwaka huu, alifanya ziara katika Kata ya Langali pamoja na Tchenzema, zilizopo Tarafa ya Mgeta, Wilayani Mvomero.
Akiwa katika Kijiji cha Kibagara, Kata ya Tchenzema, Mbunge huyo pamoja na kusikiliza kero mbalimbali za wananchi na kujitolea majawabu na ufafanuzi , pia aliahidi kutoa mifuko 50 ya safuji kwa ajili ya ujenzi wa Zahanati ya Kijiji hicho ili itakapokalimika iwezekuwaondolea tatizo la kusafiri umbali mrefu kwenda kupata tiba.
Katika Kata ya Langali, Mbunge huyo alishiriki hafla ya uzinduzi wa Ofisi ndogo ya Mbunge wa Jimbo hilo baada ya kukotisha Nyumba na kuifanyia utarabati mkubwa na kulipoia karo ya kipindi cha miaka mitano , ili iwezekutumika kuwahudumia wananchi wa Tarafa ya Mgeta , kufikisha kero zao kwa Katibu wa Mbunge wa Tarafa na baadaye kuzifikisha kwa Mbunge.
Pia Ofisi hiyo itakuwa ni sehemu ya uratibu wa ziara ya Mbunge wa Jimbo wakati wa kutembelea Vijiji vya Kata zilizopo kwenye Tarafa ya Mgeta.
Akizundua Ofisi ndogo hiyo, Mkuu wa Wilaya ya Mvomero, Anthony Mtaka ,alimpongeza Mbunge huyo juu uamuzi wake wa kufungua Ofisi katika Tarafa hiyo akionesha mfano wa kuingwa na Wabunge wengine , kuwasongezea huduma ya karibu wananchi , ambapo Ofisi hiyo mbali na kutumiwa na Mbunge , Serikali ya Wilaya itakuwa bega kwa bega kuwez kupata maoni ya wananchi na kero zao zitakazofanyiwa kazi kwa haraka kupitia Ofisi hiyo
Wabunge wengi wamekuwa wakilalamikiwa na wapiga kura wao kuwa hawaonekani jimboni baada ya uchaguzi mpaka kipindi cha ziara za Rais, Makamu wa Rais au Waziri Mkuu katika majimbo yao.

MPANDA KUMEKUCHA SASA....

98.5 iko hewani na 97.0 iko mbioni kuruka hewani katika mkoa wa Katavi







 SAFARI : Vijana wakisaka noti katika eneo la Tambukareli mjini Mpanda kwa kubeba pumba za kuchomea matofali
 UJUMBE PINDA kwa mkuu wa mkoa wa Katavi Dr Rajabu M. Rutengwe

 Nyumba ya Mapadre katika parokia ya Karema na majengo mengine ya watawa na ofisi za parokia

KUMBU KUMBU YA ASKOFU KIKOTI IKO HAPA






















 













UNAMAONI GANI ? 


MSIMAMO WA LIGI KUU TANZANIA LEO

Emanuel Okwi akisakata kabumbu
SIMBA SC imeanza vema kutetea ubingwa wake wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, jioni hii baada ya kuichapa mabao 3-0 African Lyon katika mchezo wa ufunguzi wa ligi hiyo, kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Hadi mapumziko, tayari Simba SC walikuwa mbele kwa mabao 2-0 yaliyotiwa kimiani na Emanuel Okwi dakika ya 33 baada ya kuwatoka mabeki wa Lyon na Mrisho Ngassa dakika ya 36 akiunganisha krosi ya Nassor Masoud ‘Chollo’, ambayo tayari ilikuwa na mwelekeo wa kutinga nyavuni.
Lyon walikosa penalti dakika ya 35, baada ya mkwaju wa Sunday Bakari kupanguliwa na Juma Kaseja, kufuatia Mwinyi Kazimoto kuunawa mpira kwenye eneo la hatari.
Kipindi cha pili, Lyon kidogo walirekebisha makosa yao, lakini bado Simba iliendelea kutawala mchezo na dakika ya 56, Danniel Akuffo aliifungia timu yake bao la kuhitimisha ushindi kwa mkwaju wa penalti, baada ya Emmanuel Okwi kuangushwa kwenye eneo la hatari.
Simba SC; Juma Kaseja, Nassor Masoud ‘Chollo’, Amir Maftah, Shomary Kapombe, Juma Nyosso, Mwinyi Kazimoto, Amri Kiemba, Haruna Moshi ‘Boban’, Daniel Akuffo/Ramadhan Chombo, Mrisho Ngassa/Abdallah Juma na Emanuel Okwi.
African Lyon; Abdul Seif, Johanes Kajuna, Hamadi Manzi, Sunday Bakari, Benedictor Mwamlangala, Sunday Hinju, Obina Salamusasa, Semmy Kessy, Iddi Mbaga, Jacob massawe na Yussuf Mlipili.
Katika mechi nyingine za ligi hiyo, Yanga imelazimishwa sare ya bila kufungana na Prisons kwenye Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya.
Yanga SC; Ally Mustafa ‘Barthez’, Juma Abdul, Oscar Joshua, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Kevin Yondan, Mbuyu Twite, Nizar Khalfan, Haruna Niyonzima, Said Bahanuzi, Didier Kavumbangu na Stefano Mwasyika.
Kwenye Uwanja wa Kaitaba, Bukoba, bao pekee la Abdulhalim Humud liliipa Azam FC ushindi wa 1-0 dhidi ya wenyeji Kagera Sugar.
Azam FC; Deo Munishi ‘Dida’, Ibrahim Shikanda, Erasto Nyoni, Said Mourad, Aggrey Morris, Abdulhalim Humud, Ibrahim Mwaipopo, Himid Mao/Jabir Aziz, John Bocco, Abdi Kassim/Kipre Balou na Kipre Herman Tchetche.

Kwenye Uwanja wa Mkwakwani Tanga, bao pekee la kiungo Mkenya, Jerry Santo dakika ya 41 liliipa Coastal Union ushindi wa 1-0 dhidi ya Mgambo FC.
Uwanja wa Jamhuri, Morogoro, wenyeji Polisi wamelazimishwa sare ya bila kufungana na Mtibwa Sugar ya Turiani, Manungu.
Uwanja wa CCM Kirumba mjini Mwanza, Toto Africans imelazimishwa sare ya 1-1 na JKT Oljoro, wakati Uwanja wa Chamazi, Mbagala, JKT Ruvu imeifunga Ruvu Shooting mabao 2-1.

MATOKEO MECHI ZOTE LIGI KUU LEO

Simba 3-0 African Lyon

Kagera Sugar 0-1 Azam FC

Prisons 0-0 Yanga

Coastal Union 1-0 Mgambo JKT

Toto African 1-1 JKT Oljoro

Polisi Moro 0-0 Mtibwa Sugar
JKT Ruvu 2-1 Ruvu Shooting






 Zahanati ya Kanisa Katoliki Karema ni sehemu ya huduma kwa jamii




 Nyumba ya watawa "masister" karema iliyojengwa na marehemu Mhasham Askofu Kikoti



 Karema ni nyumbani kwa wazazi wa askofu wa kwanza wa jimbo la Sumbawanga Mhasham Askofu Charles Msakila, pichani akibadilishana mawazo na Baba Mtakatifu John paul wa 25.




 Mungu ailaze roho ya marehemu askofu pascal Williamu Mwakikoti mahala pema peponi. Amina





 VG wa jimbo Katoliki la Mpanda ameonesha njia na changamoto kwa mapadre wenzake kuwa wa kwanza kuleta mabadiliko katika jamii kwa kuanzisha miradi inayoweza kuongeza kipato na fursa kwa wananchi, Fr. Patrick Kasomo umetuonesha njia, asante baba.

 Karema Beach' ni eneo la uwekezaji la paroko wa Karema na Vica General Fr Kasomo.








 Ujenzi unaendelea katika Karema Beach



TUME YA KATIBA IKIWA KATIKA MKOA WA KATAVI KUKUSANYA MAONI

 Dk. Sengondo Mvungi akielezea wananchi wa kijiji cha Vikonge wilayani Mpanda utaratibu mzuri wa kutoa maoni ya Katiba kabla ya kuanza mkutano wa tume ya kukusanya maoni juzi



 MAONI KATIBA: nafasi kwa jinsia zote na rika zote inazingatiwa sana katika kukusanya maoni ya katiba mpya, hakuna kundi linalobaguliwa wala kujengewa mazingira magumu katika kutoa maoni, msichana akitoa maoni ya katiba katika kijiji cha Majalila wilayani Mpanda katika mkoa wa Katavi.
 MAONI YA KATIBA TZ: Jamaa mmoja aliyefika katika mkutano wa kukusanya maoni ya Katiba katika kijiji cha Vikonge wilayani Mpanda akiwa CHAKALI lakini alipewa nafasi na kutaka Rais asiwe mmiliki wa ardhi na pia safari za Rais zipunguzwe. (PICHA NA SHADRACK SAGATI)





UNAPOWEKA REHANI MWILI WAKO, 

Usafiri ni tatizo au tatizo ni wasafiri??

 Abiria wawili wakiwa wamepakiwa katika pikipiki maarufu kwa jina la Boda boda katika barabara ya Buzogwe Mpandahoteli mjini Mpanda, upakiaji huu ni hatari kwa watumiaji wa pikipiki abiria na mwendesha piki piki mwenyewe.

UCHAGUZI UVCCM WILAYA YA MPANDA MKOA WA KATAVI



 Katibu wa Umoja wa Vijana Mkoa wa Katavi akiwaasa viajana kuwa makini katika uchaguzi









 Katibu wa Umoja wa Vijana wa Mkoa wa Katavi akiwaasa vijana kuchagua mchapakazi na siyo mtoa rushwa, pembeni yake ni katibu wa UVCCM Wilaya ya Mpanda, Tungulu



 Katibu Msaidizi wa CCM mkoa wa Katavi akiwasalimia vijana mkutanoni hapo














 Mwenyekiti wa UVCCM wilaya ya Mpanda anayemaliza muda wake, Haidary Sumry











 Mkuu wa wilaya ya Mpanda, Paza Tusamale Mwamlima akifungua mkutano wa uchaguzi leo alasiri

























































HIVI NDIVYO MWANAHABARI DAUD MWANGOSI ALIVYOPOTEZA MAISHA LEO KTK VURUGU ZA CHADEMA NA POLISI


Hapa polisi wakiwataka wafuasi wa Chadema kutawanyika eneo la tukio ofisi za Chadema Nyololo Mufindi

                                      Mwili wa mwanahabari Daud Mwangosi ukiwa chini


                                Daud Mwangosi kulia enzi za uhai dakika 20 kabla ya kuuwawa kwake
Mwandishi wa habari wa Chanel Ten mkoa wa Iringa na Mwenyekiti wa chaa chama cha waandishi wa habari mkoa wa Iringa Daud Mwangosi ameuwawa jana katika vurugu za Polisui i na wafuasi wa Chadema katika kijiji cha Nyololo wilaya ya Mufindi mkoani Iringa

Mwanahabari huyo Daud Mwangosi aliuwawa majira ya saa 10 jioni jana katika ofisi za Chadema Nyololo huku askari mmoja akijeruhiwa vibaya kwa risasi .

Kabla ya kuuwawa kwa mwanahabari huyo mabomu yaliweza kupigwa eneo hilo kuwatawanya wafuasi hao wa Chadema ambao walikuwa wakigoma kutawanyika eneo hilo na kuamua kukaa chini kuwa haapo tayari kuondoka katika ofisi yao.

Chanzo cha mwanahabari Mwangosi kuuwawa klitokana na kukamatwa kwa mwandishi wa habari wa gazeti la Nipashe mkoa wa Iringa Godfrey Mushi na hivyo mwanahabari huyo kkutaka kuhoji polisi sababu ya kukamatwa kwa mwanahabari huyo ndipo askari hao walipoanza kumshambulia kwa kichapo na baadae mlio kama wa bomu ulisikika eneo hilo na mwandishi huyo na askari mmoja waliaguka chini .

Ndani ya dakika tano ilisikika sauti kutoka kwa askari huyo kuwa afande nimekufa ndipo walipomchukua na kumpeleka Hospitali ya wilaya ya Mufindi huku mwili wa mwanahabari huyo ukipelekwa chumba cha kuhifadhia maiti .

Katika vurugu hizo zilizodumu kwa takribani dakika 30 kwa askari na wafuasi wa Chadema kurushiana mawe kwa mabomu zaidi ya magari matano ya Chadema na ya wananchi yameharibiwa huku watu kadhaa wamejeruhiwa na mwanahabari mmoja Godfrey Mushi akijeruhiwa vibaya.

Hii ni taarifa ya Jeshi la polisi kabla ya tukio kwa vyombo vya habari


JESHI la polisi mkoa wa Iringa limesema limezuia mikutano ya vyama vya siasa kwa vyama vyote na sio kwa chama cha Demokrasia na maendeleo (CHADEMA) pekee hivyo laonya vyama vyote kutii sheria bila shuruti.

Hata hivyo jeshi hilo la Polisi limesema kuwa halifanyi kazi kwa matakwa ya chama chochote cha siasa na kuwa si kweli kama wanavyodai viongozi wa Chadema kuwa jeshi la polisi linatumiwa na chama cha mapinduzi (CCM) kuzuia mikutano hiyo.

Kamanda wa polisi wa mkoa wa Iringa Michael Kamuanda ametoa kauli hiyo leo ofisini kwake alipozungumza na waandisha wa habari kuhusu zuio la mkutano wa Chadema uliopangwa kuanza jana katika wilaya ya Mufindi.

" Nawatangazia wanasiasa na vyama vyote vya siasa pamoja na wananchi wa mkoa wa Iringa kuwa hakutakuwa na mikutano ya kisiasa kutokana na shughuli za sensa zinazoendelea ....hivyo basi nawaomba wananchi wote kutoshiriki mikutano yoyote ya kisiasa itakayoitishwa na wanasiasa "alisisitiza

Kuwa mikutano hiyo imezuiliwa kwa kipindi hiki cha sensa kilichoongezwa hadi hapo tamko litakapotolewa tena na msajili wa vyama vya siasa John Tendwa kama alivyokwisha kutoa tamko la kuzuia shughuli hizo za vyama vya siasa kwa kipindi hiki cha sensa.

"Wananchi wote wa mkoa wa Iringa mnaombwa kutii sheria bila shuruti hii ni amri ....nawaombeni sana wananchi kutodanganywa na wanasiasa kwa kuvunja sheria "aliongeza kamanda huyo wa polisi.

Hata hivyo alisema kuwa kimsingi zoezi la sensa lilipaswa kuhitimishwa Septemba mosi mwaka huu ila kutokana na serikali kuongeza muda wa zoezi hilo bado jeshi hilo la polisi linazingatia maagizo ya Msajili wa vyama vya siasa kama alivyoyatoa kwa jeshi hilo.

Kamanda Kamuanda alisema kuwa jeshi hilo la polisi wala msajili wa vyama vya siasa hajazuia vyama vya siasa kuendelea na vikao vyao vya ndani kwa kipindi hiki na kuwa hata Chadema wakiwa mkoani Iringa wameendelea kufanya vikao vyao vya ndani katika kata mbali mbali za mkoa wa Iringa na hakuna mtu aliyewazuia kuendelea kufanya hivyo.
Majibu ya Dkt Slaa
Wakati jeshi la polisi likipinga shughuli hizo za vyama vya siasa kufanya mikutano ya hadhara katibu mkuu wa Chadema Taifa Dkt Willbroad Slaa ameibuka na kusema kuwa chama chake kitaendelea na mikutano kama kilivyojipangia na kuwa wapo tayari kwa lolote litakalojitokeza .

Dkt Slaa alisema kuwa walivumilia mara ya kwanza walipozuiwa mikutano hiyo mkoani Iringa na kuvuta subira hadi jumamosi zoezi hilo lilipomalizika sasa anashangazwa kuona jeshi hilo likiendelea kuzuia mikutano hiyo tena.

"Tumemsikiliza kamishina wa sensa Hajati Amina Mrisho Said kuwa hadi sasa watu asilimia 95 wameandikishwa huku akiwata wale ambao bado kuwapigia simu wenyeviti wa mitaaa na vijiji ili wakaandikishwe na makarani wa sensa ....sasa jeshi la polisi linataka kutuambia kuwa hao watu asilimia 5 waliobaki wapo Iringa peke yake hadi wakazuia mikutano yetu? tunasema hatutakubali tutaendelea na mikutano yetu kama kawaida hatupotayari kabisa kusubiri hadi tarehe nane" alisema Dkt Slaa.

Pia alisema kuwa kama ni uzalendo sasa umefika kikomo na kuwa wataendelea na ratiba zao za mikutano kama ilivyopangwa na watapambana kwa lolote .

CHADEMA +POLISI = LUGHA GONGANA

Kamanda wa polisi mkoa wa Iringa Michael Kamuhanda akizungumza na wanahabari leo kuhusu sababu za kuzuia mkutano wa Chadema leo Mufindi
Tumejinga kwa lolote asema kamanda wa polisi kuwa si Chadema pekee hata CCM na vyama vyote marufuku mikutano wanaruhusiwa kufanya vikao vya ndani ili kupisha zoezi la sensa hadi jumamosi litakapomalizika


Katibu wa Chadema Dkt Willbroad Slaa akitanza msimamo wa chama hicho kuwa mkutano upo pale pale.habari kamili utazipata baada ya kutoka Mufindi

MAZISHI YA MHASHAM ASKOFU PASCAL WILLIAM KIKOTI

SEPTEMBER 1, 2012; KANISA LA MTAKATIFU MARIA IMAKULATA


















































































































































































































SERIKALI imeelezea pengo lililoachwa na aliyekuwa askofu wa kanisa Katoliki jimbo la Mpanda, Marehem Askofu Paschal William Kikoti kufuatia kifo cha askofu huyo kilichotokea Agosti Ishirini na nane mwaka huu

Hayo yamebainishwa na Waziri mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Mizengo Kayanza Peter Pinda Septemba mosi (jana) alipokuwa kiwasilisha salamu za serikali katika ibada ya mazishi ya askofu huyo katika kanisa katoliki la Mpanda mkoa wa Katavi.
Waziri Mkuu alisema kuwa katika utume wake wa kuliongoza kanisa katoliki jimbo la Mpanda askofu Kikoti alikuwa na mchango mkubwa katika jamii ya wakristo wa Mpanda na kwa wasio wakristo waishio katika wilaya ya Mpanda kwa kutoa huduma za kiroho na za kijamii
Alisema yeye binafsi alifanya kazi kwa karibu sana na Mhashamu askofu Kikoti tangu alipowekwa wakfu na kusimikwa kuwa askofu wa jimbo la Mpanda mwaka 2001 na hata kabla ya hapo na kubaini kuwa alikuwa na shauku ya kutoa huduma za kiroho na za kijamii kwa ujumla hivyo kifo cha askofu huyo kimesababisha pengo kubwa kwa familia yake, wakatoliki, wanampanda na hata wananchi wa Tanzania kwa ujumla
Mhe. Pinda alionesha kusikitishwa kwake na kifo cha askofu Kikoti kuwa kimemfika akiwa na umri mdogo sana wa utumishi uliotukuka wa miaka hamsini na tano ambao bado alikuwa anahitajika sana kuendelea kutoa huduma kwa miaka mingine zaidi.
Alisema kabla ya kifo chake askofu Kikoti alikuwa na malengo mengi mazuri yakiwemo kufungua seminarfi ndogo ya jimbo, kujenga kituo cha kichungaji na kijamii na kupanua shule ya sekondari ya Mtakatifu Maria ya Mpanda, lakini Mungu ameamua amchukue sasa
Mhe Pinda alisema pamoja na kutambua machungu waliyo nayo wana Mpanda kwa kumpoteza kiongozi na nguzo ya jimbo la Mpanda aliwasihi kumuenzi marehemu kwa kuendeleza mazuri aliyoyaanzisha marehemu Kikoti kwani kufanya hivyo ni kuendeleza kaulimbiu ya marehemu askofu kikoti inayosema “katika Imani na Upendo”
“hata hivyo, ni imani yangu kwamba Mwenyezi Mungu atawaongoza katika kumpata mrithi wake ambaye ataendeleza kauli mbiu hiyo pamoja na kukamilisha malengo aliyokuwa nayo, muhimu ni kumuombea kwa Mwenyezi Mungu aipumzishe Roho ya Marehemu mahali pema peponi. Amina” alisema mhe. Pinda
Kufuatia kifo cha askofu Paschal Kikoti kanisa limemteua askofu wa jimbo katoliki la Sumbawanga, Damian Kyaruzi kusimamia jimbo la Mpanda kwa muda jimbo hilo hadi atakapoteuliwa askofu mwingine wa kuliongoza ambapo askofu Kyaruzi alimteua Padre Patrick Kasomo kuwa msaidizi wake wa jimbo Vicar general.

Hotuba ya mwisho w amwezi ya Rais Kikwete AGOSTI 31, 2012


HOTUBA YA MHESHIMIWA DKT. JAKAYA MRISHO KIKWETE, RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, KWA WANANCHI, TAREHE 31 AGOSTI, 2012
Utangulizi
Ndugu Wananchi;
            Kila mwisho wa mwezi nimekuwa nazungumza na taifa kuhusu masuala mbalimbali muhimu kwa taifa letu na watu wake.  Leo nina mambo mawili ya kuzungumza nanyi.  Lakini, kama ilivyo mazoea yetu hatuna budi kwanza tumshukuru Mwenyezi Mungu, muumba wetu, kwa kutujaalia baraka zake, za uhai na uzima na kutuwezesha kuwasiliana leo tarehe 31 Agosti, 2012.
Ndugu Wananchi;
            Jambo la kwanza ninalotaka kuzungumzia leo ni zoezi la Sensa ya Watu na Makazi lililoanza tarehe 26 Agosti, 2012 ambalo linatarajiwa kumalizika tarehe 01 Septemba, 2012.  Mtakumbuka kuwa tarehe 25 Agosti, 2012 nilizungumza nanyi na kuwaomba mjitokeze kwa wingi na muwape ushirikiano unaostahili Makarani wa Sensa watakapopita majumbani mwenu kutekekeza wajibu wao.  Tumebakisha siku moja kufikia kilele cha sehemu ya kwanza ya Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2012.
             Napenda kuwashukuru kwa dhati Watanzania wenzangu wote kwa kujitokeza kwa wingi kuhesabiwa.  Mpaka sasa mwelekeo ni mzuri na ugumu ulioonekana kuwepo pale mwanzoni uliendelea kupungua siku hadi siku kadri utekelezaji wa zoezi ulivyokuwa unaendelea.  Kwa mwenendo huu nina matumaini makubwa kuwa Sensa ya mwaka huu itakuwa na mafanikio mazuri.
Ndugu Wananchi; 
            Napenda kutumia nafasi hii kutoa wito kwa wale wote ambao hawajahesabiwa wafanye hivyo. Naomba waitumie siku moja iliyosalia yaani tarehe 1 Septemba, 2012 kufanya hivyo.  Aidha, namuomba Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi Kuu ya Takwimu ya Serikali ya Muungano na Mtakwimu Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kuhakikisha kuwa kasoro zo zote zilizopo mahali po pote zinatafutiwa ufumbuzi ili mambo yakamilike bila upungufu wowote.
Ndugu Wananchi;
        Baada ya kazi ya Makarani wa Sensa kuhesabu watu kufikia kilele chake, tarehe 2 Septemba, 2012, linaanza zoezi la kuwashughulikia wale ndugu zetu ambao watakuwa bado hawajahesabiwa.  Itakuwepo fursa ya siku saba kwa watu hao kuhesabiwa.  Watatakiwa wao wenyewe kupeleka taarifa zao kwa Wenyeviti wao wa Serikali za Mitaa au Vijiji.  Taarifa hizo zitafikishwa kwa Kamishna wa Sensa kwa ajili ya kujumuishwa.  Baada ya muda huo kwisha, zoezi la kuhesabu watu litakuwa limefika mwisho.  Yule ambaye atakuwa hakutumia fursa hizo mbili atakuwa amekosa kuingizwa katika hesabu ya Watanzania ya mwaka 2012.  Napenda kuwasihi ndugu zangu, Watanzania wenzangu kutumia siku ya tarehe 1 Septemba, 2012  kuhesabiwa na kama hapana budi basi tumia fursa ya kupeleka taarifa zako kwa Mwenyekiti wako wa Mtaa au Kijiji katika siku saba zinazofuatia siku hiyo ili nawe ujumuishwe.
Ndugu Wananchi;
            Baada ya kazi ya kuhesabu watu kwa namna zote mbili kufikia mwisho, itaanza kazi ya uchambuzi na kuunganisha takwimu na taarifa zilizokusanywa.  Kazi hiyo ni muhimu na ni kubwa hivyo inahitaji umakini na uangalifu wa hali ya juu sana, kwani ikikosewa zoezi zima la Sensa litaingia dosari.  Nafarijika kuhakikishiwa na Viongozi wa Sensa na Wakuu wa Idara za Takwimu za Serikali zetu mbili, kwamba wanatambua ukweli huo na wajibu wao.  Wameniarifu kwamba kama mambo yatakwenda kama ilivyopangwa, matokeo ya awali ya Sensa ya Watu na Makazi kuhusu idadi ya watu na jinsia zao yatatolewa mwishoni mwa mwaka huu. Taarifa nyingine zitafuata baadaye.  Narejea kuwasihi Watanzania wenzangu kuwapa nafasi wataalamu wetu wafanye kazi yao kwa ufanisi ili tupate matokeo yaliyo sahihi.
Mpaka na Malawi
Ndugu Wananchi;
            Jambo la pili ninalotaka kuzungumza nanyi leo ni kuhusu mpaka baina ya Tanzania na Malawi katika Ziwa Nyasa.  Kama mjuavyo, kwa miaka mingi nchi zetu mbili zinatofautiana kuhusu wapi hasa mpaka uwe.  Sisi, Tanzania, tunasema mpaka upo katikati ya ziwa wakati wenzetu wa Malawi wanasema upo kwenye ufukwe wa ziwa upande wa Tanzania.  Kwa maneno mengine wanasema ziwa lote ni mali ya nchi yao. 
Utata kuhusu mpaka wetu katika Ziwa Nyasa haujaanza leo.  Ulikuwepo tangu wakati nchi zetu mbili zikiwa bado zinatawaliwa na wakoloni na kuendelea baada ya Uhuru wa nchi zetu mpaka sasa.  Jambo kubwa lililo tofauti na jipya ni kwamba hivi sasa, nchi zetu mbili zimeamua kukaa mezani na tunalizungumza suala hilo.
Chimbuko la Mzozo
Ndugu Wananchi;
Chimbuko la mzozo wa mpaka uliopo sasa, baina ya nchi zetu mbili jirani, rafiki na ambazo watu wake ni ndugu, ni makubaliano baina ya Waingereza na Wajerumani kuhusu mpaka baina ya nchi zetu yaliyofanywa tarehe 1 Julai, 1890.  Makubaliano hayo yajulikanayo kama Mkataba wa Heligoland, (The Anglo-Germany Heligoland Treaty) yalitiwa saini kule Berlin, nchini Ujerumani baina ya Waingereza na Wajerumani.  Wakoloni hao walikubaliana kuhusu mipaka baina ya makoloni yao na baina yao na wakoloni wengine waliopakana nao.  Kwetu sisi hayo ndiyo makubaliano yaliyoweka mipaka ya Tanganyika na ile ya Zanzibar na majirani zake.  Kwa upande wa Ziwa Nyasa, Waingereza na Wajerumani walikubaliana kuwa mpaka uwe kwenye ufukwe wa nchi yetu.  Kwa maana hiyo ziwa lote likapewa nchi ya Malawi.  Kwa upande wa Mto Songwe mpaka ulikuwa ufukweni upande wa Malawi kwa maana hiyo mto wote ukawa upande wa Tanzania.
Ndugu Wananchi;
Katika kipengele cha Sita (Article VI) cha Mkataba huo, wakoloni hao walikubaliana kufanya marekebisho ya mpaka mahali po pote kama itakuwa ni lazima kufanya hivyo, kulingana na mazingira na hali halisi ya mahali hapo.  Kwa mujibu wa kutekeleza matakwa ya kipengele hicho mwaka 1898 Tume ya Mipaka iliundwa.  Ilianzia kazi katika Mto Songwe kuhakiki mpaka baina ya nchi yetu na Malawi. Tume ilikubaliana kuhamisha mpaka kutoka ufukweni mwa Mto Songwe upande wa Malawi na kuwa katikati ya mto.  Baada ya uhakiki katika eneo hilo kukamilika, mwaka 1901 mkataba mpya ulisainiwa kuhusu mpaka huo.
 Tume iliendelea na kazi yake katika Ziwa Tanganyika na kuhamisha mpaka kutoka ufukweni hadi katikati ya ziwa na mkataba mpya kusainiwa mwaka 1910.  Tume iliendelea katika ziwa Jipe ambapo mpaka ulihamishwa pia hadi katikati ya ziwa.
Ndugu Wananchi;
Bahati mbaya Tume hiyo haikufanikiwa kufanya uhakiki wa mpaka katika Ziwa Nyasa kutokana na kutokea kwa Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia kati ya mwaka 1914 - 1918.  Kama tunavyokumbuka, Waingereza na Wajerumani waligeuka kuwa maadui na kupigana hata hapa nchini.  Baada ya vita hivyo na Ujerumani kushindwa, Baraza la Umoja wa Mataifa (The League of Nations) liliikabidhi Uingereza udhamini wa Tanganyika. Hivyo, Uingereza ikawa inatawala Malawi na Tanganyika. 
Ndugu Wananchi; 
Wakati Tume ya Uingereza na Ujerumani ilipokuwa imekufa, Tume ya Mipaka kati ya Uingereza na Ureno iliendelea na kazi.  Matokeo yake, mwaka 1954, Uingereza na Ureno zilitengua mkataba wao wa mwaka 1891 ulioweka mpaka wa Ziwa Nyasa katika ufukwe wa mashariki ya Ziwa, yaani kwenye ufukwe wa Msumbiji, na kuuhamishia katikati ya ziwa.
Ndugu Wananchi;
Jambo la kustaajabisha ni kuwa, Waingereza walioona umuhimu na busara ya kurekebisha mpaka kati ya Malawi na Msumbiji, hawakuona umuhimu wa kufanya hivyo kati ya nchi yetu na Malawi.  Inashangaza, kwa sababu wakati huo Uingereza ilikuwa mtawala wa nchi zetu mbili hivyo kazi ya marekebisho ingekuwa rahisi, lakini hawakufanya hivyo.  Na, baya zaidi ni kuwa  hata pale watu wa nchi yetu walipotaka kupatiwa ufafanuzi na kutaka ukweli uwekwe wazi kuhusu mpaka hawakusikilizwa.  Watu walitaka ufafanuzi kwa sababu inasemekana kati ya mwaka 1925 na 1938, taarifa ya Uingereza kwa Umoja wa Mataifa ziliweka mpaka katikati ya ziwa.  Lakini, kuanzia mwaka 1948 mpaka ukawekwa tena ufukweni. 
Ndugu Wananchi;
Mwaka 1959, 1960 na 1962, suala la mpaka wa Malawi lilijitokeza tena na kujadiliwa na Bunge la Tanganyika, wakati ule lilijulikana kuwa Baraza la Kutunga Sheria, (Legislative Council – LEGCO).  Hoja ya Wabunge wa Tanganyika ilikuwa kwamba mpaka kuwekwa kwenye ufukwe wetu kunawanyima wananchi wa Tanganyika wanaoishi kando kando ya ziwa haki yao ya msingi ya kutumia maji kwa kunywa, kuoga, kuvua samaki na kupata manufaa mengine yatokanayo na ziwa bila ya kuomba ridhaa ya Serikali ya Koloni la Nyasaland kama Malawi ilivyokuwa inajulikana wakati ule.  Hoja iliyotolewa ilikuwa kwamba Serikali ya Tanganyika ijadiliane na Serikali ya Nyasaland kupitia Serikali ya Malkia wa Uingereza ili ufumbuzi upatikane.  Wakoloni hawakujali na wala hakuna hatua zilizochukuliwa mpaka Tanganyika ikapata uhuru wake tarehe 9 Desemba, 1961 na Malawi kupata uhuru wake mwaka 1964.
Juhudi za Kubadili Mpaka wa Ziwa Nyasa Baada ya Uhuru
Ndugu Wananchi;
            Wakati tulipopata Uhuru mwaka 1961, mjadala kuhusu mpaka wa Tanganyika na Malawi uliendelea Bungeni, ambapo ilitolewa hoja kwamba zifanyike juhudi za makusudi za kuanzisha na kuendeleza mazungumzo ya kurekebisha mpaka huo kwa manufaa ya wananchi wote wanaoishi pembezoni mwa ziwa.  Iliamuliwa kwamba tusubiri mpaka wenzetu wa Malawi wapate uhuru ili yafanyike mazungumzo baina ya nchi mbili huru.  Kulijengeka matumaini kuwa mambo yangekuwa rahisi.  Bahati mbaya haikuwa hivyo na kwamba mambo yakageuka na kuwa magumu na ya uhasama.  Miaka mitatu baada ya Malawi kupata Uhuru wake (1964), kunako tarehe 3 Januari 1967, Serikali ya Tanzania iliandika barua kwa Serikali ya Malawi kuelezea tatizo la mpaka wa ziwani na kupendekeza nchi zetu mbili zizungumze na kulitafutia ufumbuzi. 
Ndugu Wananchi;
Bahati nzuri tarehe 24 Januari, 1967, Serikali ya Malawi ikajibu kukiri kupokea barua hiyo na kuahidi kuwa itatoa majibu baada ya muda si mrefu.  Hata hivyo, tarehe 27 Juni, 1967, Rais Kamuzu Banda akilihutubia Bunge la Malawi, alikataa maombi ya Tanzania.  Alisema hayana msingi na alidai kuwa kihistoria Songea, Mbeya na Njombe ni sehemu ya Malawi.  Hivyo basi, mazungumzo yakafa. 
Tanzania haikukata tamaa.  Alipochaguliwa Rais wa Pili wa Malawi, Mheshimiwa Bakili Muluzi, juhudi zilifanyika lakini nazo hazikufika mbali. Bahati nzuri tarehe 9 Juni, 2005, Rais wa Tatu wa Malawi, Mheshimiwa Bingu Wa Mutharika, ambaye sasa ni marehemu, alimuandikia barua aliyekuwa Rais wa nchi yetu wakati ule, Mheshimiwa Benjamin William Mkapa, kushauri nchi zetu zifanye mazungumzo kuhusu mpaka wa ziwani.  Alipendekeza iundwe Tume ya Pamoja itakayojumuisha Mawaziri na Wataalamu kutoka nchi zetu mbili.  Tume hiyo itatoa mapendekezo kwa Marais wa nchi zetu mbili ambayo yatakuwa msingi wa majadiliano baina yao.  Alisisitiza umuhimu wa kulipatia ufumbuzi suala hilo. 
Ndugu Wananchi;
Kwa kuwa ilikuwa kipindi cha mpito kuelekea kuchaguliwa Serikali ya Awamu ya Nne, Rais Benjamin Mkapa hakuwahi kuishughulikia barua hiyo. Nilipoletewa barua hiyo nikaijibu kukubali ushauri na mapendekezo yake.  Aidha, nilipendekeza Wizara na Idara zipi za Serikali zetu zishirikishwe katika Tume hiyo.  Bahati nzuri Rais wa Malawi alikubali mapendekezo yangu pamoja na lile la kwamba Malawi waitishe mkutano wa kwanza wa Tume hiyo.
Ndugu Wananchi;
Mpaka sasa mikutano mitatu ya Tume ya Pamoja imeshafanyika, wa kwanza ulifanyika tarehe 8 – 10 Septemba, 2010.  Mkutano wa pili ukafanyika tarehe 27 – 28 Julai, 2012 hapa Dar es Salaam na wa tatu ukafanyika Mzuzu na Lilongwe tarehe 20 – 27 Agosti, 2012. Hatua kadhaa zimepigwa lakini bado muafaka haujapatikana kwa maana ya madai yetu ya kutaka mpaka uwe katikati ya ziwa na madai yao kuwa mpaka ubaki ufukweni kwetu kama  ilivyo kwenye Mkataba wa Heligoland wa Julai 1, 1890.  Hoja ya wenzetu ni kuwa huo ndiyo mpaka tuliorithi wakati wa uhuru.  Wanataka tuthibitishe hivyo na kwamba tuzingatie kauli ya OAU ya kuheshimu mipaka tuliyorithi kwa wakoloni. Wananukuu kauli ya Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere akisisitiza hoja hiyo katika mkutano wa OAU mwaka 1963. 
Hoja za Msingi za Kutaka Mpaka Uwe Katikati ya Ziwa
Ndugu Wananchi;
Kwa upande wetu tumekuwa na hoja kadhaa za kutaka mpaka uwe katikati ya ziwa.  Ya msingi kabisa ni ukweli kwamba Mkataba wa Heligoland umekosewa kwa kuamua kuwanyima wananchi wa Tanzania wanaoishi ufukweni mwa ziwa haki yao ya msingi ya kutumia maji na rasilimali zilizomo katika Ziwa Nyasa.  Zipo sababu kadhaa kwa upande wetu kudai hivyo.  Mojawapo ni sheria ya kimataifa inayoelekeza kwamba po pote kwenye maji ya asili kama vile ziwa na mito iliyopo kati ya nchi mbili mpaka huwa katikati.  Ndiyo utaratibu unaotumika duniani kote, na mifano iko tele.  Kwa nini iwe tofauti katika ziwa Nyasa na kwa upande wa Tanzania tu wakati kwa upande wa Msumbiji mpaka upo katikati ya ziwa?
Ndugu Wananchi; 
Kwa upande wa Mto Songwe, mpaka baina ya nchi zetu mbili upo katikati.  Iweje hapa kanuni hiyo itambulike na kuheshimiwa lakini isiwe hivyo ziwani?  Kama nilivyoeleza awali, mwanzoni Mto Songwe wote ulikuwa umewekwa upande wetu, lakini Tume ya Mipaka iliyoundwa mwaka 1898 ilifanya marekebisho na kuweka mpaka katikati ya mto.  Kama nilivyokwishagusia kwenye ziwa hilo hilo la Nyasa kwa upande wa Msumbiji mwaka 1954 mkataba wa mwaka 1891 ulioipa Malawi ziwa lote ulirekebishwa na mpaka kuwekwa katikati.  Kwa nini isifanyike hivyo hivyo kwa upande wa Tanzania?  Hivi hasa ni kipi ambacho wenzetu wa Msumbiji walichotuzidi na kustahili kupata haki yao ya msingi ya kumiliki na kutumia maji ya Ziwa Nyasa ambacho sisi Tanzania tumepungukiwa?
Ndugu Wananchi;
Maji ni zawadi ya Mwenyezi Mungu kwa wanadamu wake, waitumie kwa uhai na maendeleo yao.  Iweje leo, kwa watu wanaoishi pembeni mwa ziwa hilo hilo wengine wapewe na wengine wanyimwe haki ya kulimiliki na kulitumia? Kwa nini wanyimwe haki ya kunufaika na zawadi hiyo? Hivi kauli ya wakoloni waliokaa Berlin ya kusema fulani apate na fulani asipate inatosha?  Hivi kweli ni rahisi kiasi hicho? 
Mpaka wa kwenye maji ni tofauti na ule wa nchi kavu.  Huu una rasilimali ambayo huwezi kuamua kumnyima mwanadamu mwingine anayeishi pembeni yake kwa vile haina badala yake.  Unapowaambia watu wa Mbamba Bay, Liuli, Lituhi, Manda, Ngonga, Matema, Mwaya, Itungi na wengineo waishio kando ya ziwa kuwa maji hayo si yao bali ni mali ya Malawi hawakuelewi na watakushangaa sana.  Watadhani umechanganyikiwa kwani tangu waumbwe wamekuwepo hapo wanamiliki na kutumia maji ya Ziwa.  Unataka wafanyeje?  Waende Malawi kuomba kibali cha kuyatumia?   Wao watakuuliza swali moja tu “hivi hao wenzao wanaoishi ng’ambo ya pili wamewazidi nini katika ubinadamu wao hata wapewe maji yote na wao wanyimwe?”
Ndugu Wananchi;
Kwa maana halisi ya Mkataba wa Heligoland tangu tarehe 1 Julai, 1890, wananchi wa upande wa Tanzania wamekuwa wanakunywa, kuoga, kuvua samaki na kusafiri katika maji ya Ziwa yasiyokuwa yao bali ya nchi nyingine.  Na kwa kuwa wamekuwa wanafanya hivyo bila ya kupata kibali cha Malawi wamekuwa wanaiba maji na samaki wa Malawi na kusafiri isivyo halali katika nchi ya watu.  Jambo hili haliingii akilini hata kidogo.  Ndiyo maana tunadai haki yetu stahili.
Ndugu Wananchi;
 Na hiyo pia, ndiyo maana,  busara na hekima ya Sheria ya Kimataifa kuhusu mpaka   wa kwenye maji kuwa katikati.  Sheria hii inazingatia hali halisi ya maisha ya jamii inayozunguka ziwa ambayo imekuwa inalitegemea maisha yao yote kwa shughuli zao za kuwapatia uhai na maendeleo yao.  Haiwezekani kuwatenganisha watu waishio kando ya Ziwa Nyasa kumiliki na kutumia maji hayo na rasilimali zake.  Hawataelewa wala kukubali kuambiwa kuwa wanatumia maji na rasilimali za ziwani  kwa hisani ya nchi ya Malawi. 
Kwa watu waliokuwepo tangu Mungu anawaumba wao na wenzao wa ng’ambo ya pili, siyo sawa na siyo haki hata kidogo kuwafanyia hivyo.  Kwe kweli ni unyanyasaji wa hali ya juu.  Ndiyo maana wazee wetu walidai suala hili liwekwe sawa wakati wa ukoloni, kabla na baada ya Uhuru.  Na ndiyo maana na sisi tunafuata nyayo zao katika madai haya ya haki.
Ndugu Wananchi; 
Kuna mambo mengine mawili ambayo yanatufanya tudai haki ya kumiliki na kutumia Ziwa Nyasa.  La kwanza ni ule ukweli kwamba mito mingi ya Tanzania nayo inachangia kujaza maji katika ziwa.  Iweje leo maji yanayojaza ziwa ni jambo jema, lakini yakishaingia ziwani, ziwa hilo si mali yao wenye mito hiyo tena na wakiyatumia wanaiba mali ya watu wengine.    Hivi kweli ndivyo wanavyostahili kufanyiwa watu wanaotunza vyanzo vya mito hiyo na kuruhusu maji yake kutiririka na kuingia ziwani? 
Ndugu Wananchi;
Jambo la pili ni kwamba mpaka wa Tanzania na Malawi kuwa ufukweni kunafanya ukubwa wa nchi zetu kuwa haujulikani kwa uhakika.  Unategemea mabadiliko kutokana na  kujaa na kupungua kwa maji ziwani.  Kunafanya mpaka wa nchi kuwa hautabiriki na unaweza kuwa tatizo siku moja mbele ya safari.  Isitoshe kuwa na nchi isiyojulikana ukubwa wake nalo ni tatizo la aina yake.  Ndiyo maana mpaka kuwa katikati ya ziwa ni bora zaidi.
Ndugu Wananchi;
Kama nilivyokwishasema, chimbuko la mzozo huu ni mkataba wa Heligoland ambao umepanda mbegu ya fitina baina ya nchi zetu.  Bahati mbaya sana Tume ya Mipaka haikumaliza kazi ya kuhakiki mipaka yote ya nchi yetu na majirani zake kufuatia kuzuka kwa Vita Kuu ya Kwanza mwaka 1914.  Ujerumani ikashindwa vita na koloni lake kuwa sehemu ya himaya ya Uingereza.  Bahati mbaya kwetu Waingereza waliotawala nchi zetu mbili tangu 1918 hawakuchukua hatua za kurekebisha mpaka kabla ya uhuru wa nchi zetu.  Ni maoni yetu kuwa nchi zetu sasa zifanye kile ambacho hakikufanywa na Tume ya Mipaka ya wakoloni – Waingereza na Wajerumani.  Tukifanye sisi wenyewe kama nchi mbili huru kwa njia ya mazungumzo. 
Bahati mbaya majaribio ya mwaka 1967 hayakufanikiwa.  Bahati nzuri kufuatia uamuzi wa kijasiri wa marehemu Rais Bingu wa Mutharika nchi zetu sasa zinazungumza.  Bado hatujafikia muafaka kuhusu kurekebisha mpaka na huenda ikatuwia vigumu kufikia muafaka.  Jambo linaloleta faraja, hata hivyo, ni kuwa sote wawili tumekubaliana kuwa tutafute mtu wa kutusuluhisha. 
Ndugu Wananchi;
Hayo ndiyo matokeo ya mazungumzo ya Tume yetu ya pamoja tangu ngazi ya Wataalamu, Makatibu Wakuu mpaka kwa Mawaziri, katika vikao vya Mzuzu na Lilongwe kati ya tarehe 20 – 27 Agosti, 2012.  Katika mkutano wao wa tarehe 27 Agosti, 2012 Mawaziri husika wa nchi zetu chini ya uongozi wa pamoja wa Waziri wa Mambo ya Nje wa Malawi, Mheshimiwa Ephraim Chiume na mwenzake wa Tanzania, Mheshimiwa Bernard Membe, wameafiki mapendekezo hayo.  Aidha, wamekubaliana kuwa pande zote mbili wakutane tena Dar es Salaam kati ya tarehe 10 – 15 Septemba, 2012 kukubaliana juu ya usuluhishi wa aina gani unafaa.
Ndugu Wananchi;
 Mtakubaliana nami kuwa tumepiga hatua muhimu kuelekea kwenye kupata ufumbuzi wa kudumu wa suala hili.  Hata hivyo, bado safari ni ndefu na huenda ikawa na magumu mengi.  Maombi yangu kwa viongozi na wananchi wa Tanzania na Malawi ni kuendelea kuunga mkono jitihada hizi.  Tuwaunge mkono wataalamu na Mawaziri wetu ili wafanikishe vizuri jukumu lao.  Tuzingatie na kuheshimu walichokubaliana Lilongwe kuwa viongozi na wananchi wa nchi zetu wajiepushe na kutoa kauli au kufanya vitendo vinavyoweza kuchafua hali ya hewa, kuleta uchochezi na kuathiri majadiliano yanayoendelea. 
Nawasihi Watanzania wenzangu kuzingatia ushauri na rai hiyo ya Mawaziri na wataalamu wetu, ili kuwe na mazingira mazuri ya mazungumzo na kuwezesha mzozo huu kuisha kwa amani na kirafiki. 
Hitimisho
Ndugu Wananchi;
Kabla ya kumaliza hotuba yangu, napenda kusisitiza kuwa si makusudio yangu wala ya Serikali yetu kutafuta suluhisho la suala hili kwa nguvu ya kijeshi.  Nawahakikishia Watanzania wenzangu kuwa hatuko vitani na Malawi na wala hakuna maandalizi ya vita dhidi ya jirani zetu hawa kwa sababu ya mzozo wetu wa mpaka katika Ziwa.  Ondoeni hofu na endeleeni na shughuli zenu za ujenzi wa taifa letu kama kawaida. 
Nilimhakikishia hivyo Rais wa Malawi, Mheshimiwa Joyce Banda nilipokutana naye Maputo, Msumbiji tarehe 18 Agosti, 2012.  Tanzania haina mpango wa kuingia vitani na Malawi.  Mimi na wenzangu Serikalini tunaona kuwa fursa tuliyoitafuta miaka mingi ya kukaa na ndugu zetu Malawi kuzungumzia suala hili lenye maslahi kwetu sote sasa tumeipata.  Hatuna budi kuitumia ipasavyo.  Naamini, tukifanya hivyo, inaweza kutufikisha pale tunapopataka. Ni muhimu, kwa ajili hiyo kwa pande zetu mbili, kuipa fursa ya mazungumzo nafasi ya kuendelea bila ya vikwazo visivyokuwa vya lazima. 
Ndugu Wananchi;
            Kwa sababu hiyo basi , napenda kutumia nafasi hii kuwasihi ndugu zetu wa vyombo vya habari na wanasiasa wenzangu tuepuke kauli au matendo yatakayovuruga mazungumzo na kuchochea uhasama kati ya nchi zetu mbili jirani na rafiki.  Kuna manufaa makubwa ya kumaliza mzozo wetu kwa njia ya mazungumzo kuliko kwa njia ya vita.  Kufikiria sasa kutumia njia nyinginezo hasa za nguvu za kujeshi, si wakati wake muafaka.  Aidha, tukitumia njia ya vita, badala ya kuwa tumepata suluhisho inaweza kuwa ndiyo mwanzo wa mgogoro mpana zaidi.  Tuendelee kuwaunga mkono wawakilishi wetu katika Tume yetu ya pamoja.  Naahidi, Serikali itakuwa inawapa taarifa kadri mazungumzo yetu na wenzetu wa Malawi yatakavyokuwa yanaendelea.  Nina hakika tutamaliza salama.
Mungu Ibariki Tanzania!
Mungu Ibariki Afrika!
Asanteni kwa Kunisikiliza

AJALI YA LORI LA MAGOGO ASUBUHI NA MAPEMA KATI KATI YA MJI WA MPANDA



 LORI lenye namba za usajiri T901AJJ mali Soud Abdalah mkazi wa madukani mjini Mpanda likiwa limeanguka jirani na Hoteli ya Bismilah njiapanda ya barabara ya Buzogwe na NMB Tawi la Mpanda


 Wananchi wakiangalia magogo yaliyokuwa yamepakiwa katika lori hilo na kusababisha ajali, taarifa za mashuhuda zinadai kuwa chanzo cha ajali ni mwendo mkali uliosababisha dereva kushindwa kumudu kona kali zilizo karibu, kona ya Katavi Resort na kona ya Bismilah hoteli.


























BARABARA CHINI YA KIWANGO MANISPAA YA SUMBAWANGA

 Mfanyakazi wa kampuni ya ujenzi wa barabara ya KMM, Doris Kayanda ya mjini Sumbawanga mkoani Rukwa akifanya usafi katika barabara inayojengwa na kampuni hiyo kwa kiwango cha lami mjini Sumbawanga, bara bara hiyo ipo mtaa wa Stoo ya Samaki imeshaanza kubomoka mifereji kabla ya kukamilika ujenzi wake.

WAWEKEZAJI EPUKENI MIGOGORO NA WAKULIMA - RC



Na Willy Sumia, Sumbawanga
MKOA wa Rukwa umewataka wawekezaji wanaokwenda kuwekeza mkoani humo kuhakikisha wanaepuka migogoro ya ardhi baina yao na wananchi wanaowakuta katika maeneo husika.
Agizo hilo lilitolewa jana na mkuu wa mkoa huo Mhandisi Stella Martini Manyanya alipokuwa akizungumza na wawekezaji wa shayiri kutoka kampuni ya bia ya TBL ofisini kwake.
Alisema mkoa wa Rukwa unawakaribisha wawekezaji hao na wengine waje kuwekeza kama walivoonesha nia lakini msimamo wa mkoa wake ni kuhakikisha mwekezaji hachukui mashamba ya wananchi na kuleta migogoro mikubwa isiyo takiwa kwa sababu tegemeo la wananchi wa mkoa huo kujipatia kilimo ni kwa njia ya kilimo
Alisema makampuni kadhaa yanataka kuwekeza katika kilimo mkoani mwake hivyo mkoa unawashauri kuwa waanze kuwaimarisha wakulima katika kilimo cha mazao wanayotaka kuyatumia kama malighafi ili waweze kupata malighafi hiyo kutoka kwa wakulima  na kuinua kipato cha wananchi badala ya kuwapora wananchi ardhi yao na kuibua migogoro ya ardhi
Alisema kampuni inayotaka kuwa na mashamba yake iombe kwenye ofisi yake ili itafutiwe mashamba katika maeneo ambayo hayamilikiwi na mtu yeyote lakini kabla ya kufanya hivyo lazima mwekezaji ahakikishe anawawezesha na wakulima watakaopakana naye katika eneo husika
Kwa upande wake meneja shayiri wa kampuni ya bia Tanzania, Bennie Basson alisema kampuni yake inataka kuwawezesha wakulima wa mkoa wa Rukwa kuanzisha kilimo cha shayiri ili waweze kuuza shayiri hiyo kwenye kampuni yao na kuwa na zao la biashara kwani mkoa huo wakulima wake wanalima mazao ya chakula yanayowapa chakula na mahitaji ya kujikimu
Aliahidi kuwa kampuni ya bia Tanzania itakuwa inawawezesha wakulima elimu ya kilimo cha shayiri, utayarishaji wa shamba, mbegu, pembejeo, na usafirishaji wa mazao kutoka shambani mpaka ghalani ambapo kampuni ya bia imeandaa maafisa ugani wa zao la shayiri kuja kufanya kazi na wakulima wa Rukwa
Meneja huyo aliaomba serikali iwape eneo la kulima kama shamba darasa kwa wakulima mkoani Rukwa ili iwe rahisi kujifunza na kuendesha kilimo cha shayiri kutokana na hali ya hewa ya mkoa huo kukubali kilimo cha shayiri vizuri.
Gerry Van Deu kutoka kampuni mama ya TBL, kampuni ya bia ya Afrika ya kusini alisema maeneo mengi wamekuwa wakiwajengea uwezo wakulima na kushirikiana nao tangu maandalizi ya shamba utunzaji na uvunaji kasha wao wananunua kwa bei ya soko la dunia na wala hawamkati mkulima gharama alizosaidiwa wakati wa uzalishaji na kulifanya zao la shayiri kuwa zao la biashara kwa wakulima wengi.
Mkulima wa shayiri mkoani humo, Mohamedi Rashidi Mdangwa alisema kuwa tangu aanze kilimo cha shayiri amekuwa akipata mavuno mazuri yaliyomuinua kipato kutokana na uzalishaji mzuri ambapo katika msimu wa 2009/10 alilima ekari mia moja ishirini na tano za shayiri na kuvuna takribani tani kumi na nane za shayiri iliyompatia zaidi ya shilingi milioni arobaini na tano.
Mdangwa alisema TBL ilimuwezesha kuanzia maandalizi ya shamba, kulima, pembejeo na hata uvunaji na baada ya mauzo hakukatwa hata senti ya marejesho kwa huduma alizopata wakati wa msimu wote wa kilimo.
Kampuni ya bia Tanzania imefungua tawi lake jijini Mbeya katika kanda ya Nyanda za juu Kusini na kuanzisha uzalishaji wa shayiri katika mikoa ya Mbeya, Iringa, Njombe na Rukwa ili kuongeza uzalishaji na kupunguza gharama uendeshaji kwani hivi sasa shayiri inayotumika kutengenezea bia Tanzania ni asilimia ishirini t undo inayolimwa hapa nchini na asilimia themanini inazalishwa nje ya nchi licha ya kuwa na hali ya hewa inayofaa kwa zao hilo.















MKOA wa Rukwa umewataka wawekezaji wanaokwenda kuwekeza mkoani humo kuhakikisha wanaepuka migogoro ya ardhi baina yao na wananchi wanaowakuta katika maeneo husika.
Agizo hilo lilitolewa jana na mkuu wa mkoa huo Mhandisi Stella Martini Manyanya alipokuwa akizungumza na wawekezaji wa shayiri kutoka kampuni ya bia ya TBL ofisini kwake.
Alisema mkoa wa Rukwa unawakaribisha wawekezaji hao na wengine waje kuwekeza kama walivoonesha nia lakini msimamo wa mkoa wake ni kuhakikisha mwekezaji hachukui mashamba ya wananchi na kuleta migogoro mikubwa isiyo takiwa kwa sababu tegemeo la wananchi wa mkoa huo kujipatia kilimo ni kwa njia ya kilimo
Alisema makampuni kadhaa yanataka kuwekeza katika kilimo mkoani mwake hivyo mkoa unawashauri kuwa waanze kuwaimarisha wakulima katika kilimo cha mazao wanayotaka kuyatumia kama malighafi ili waweze kupata malighafi hiyo kutoka kwa wakulima  na kuinua kipato cha wananchi badala ya kuwapora wananchi ardhi yao na kuibua migogoro ya ardhi
Alisema kampuni inayotaka kuwa na mashamba yake iombe kwenye ofisi yake ili itafutiwe mashamba katika maeneo ambayo hayamilikiwi na mtu yeyote lakini kabla ya kufanya hivyo lazima mwekezaji ahakikishe anawawezesha na wakulima watakaopakana naye katika eneo husika
Kwa upande wake meneja shayiri wa kampuni ya bia Tanzania, Bennie Basson alisema kampuni yake inataka kuwawezesha wakulima wa mkoa wa Rukwa kuanzisha kilimo cha shayiri ili waweze kuuza shayiri hiyo kwenye kampuni yao na kuwa na zao la biashara kwani mkoa huo wakulima wake wanalima mazao ya chakula yanayowapa chakula na mahitaji ya kujikimu
Aliahidi kuwa kampuni ya bia Tanzania itakuwa inawawezesha wakulima elimu ya kilimo cha shayiri, utayarishaji wa shamba, mbegu, pembejeo, na usafirishaji wa mazao kutoka shambani mpaka ghalani ambapo kampuni ya bia imeandaa maafisa ugani wa zao la shayiri kuja kufanya kazi na wakulima wa Rukwa
Meneja huyo aliaomba serikali iwape eneo la kulima kama shamba darasa kwa wakulima mkoani Rukwa ili iwe rahisi kujifunza na kuendesha kilimo cha shayiri kutokana na hali ya hewa ya mkoa huo kukubali kilimo cha shayiri vizuri.
Gerry Van Deu kutoka kampuni mama ya TBL, kampuni ya bia ya Afrika ya kusini alisema maeneo mengi wamekuwa wakiwajengea uwezo wakulima na kushirikiana nao tangu maandalizi ya shamba utunzaji na uvunaji kasha wao wananunua kwa bei ya soko la dunia na wala hawamkati mkulima gharama alizosaidiwa wakati wa uzalishaji na kulifanya zao la shayiri kuwa zao la biashara kwa wakulima wengi.
Mkulima wa shayiri mkoani humo, Mohamedi Rashidi Mdangwa alisema kuwa tangua aanze kilimo cha shayiri amekuwa akipata mavuno mazuri yaliyomuinua kipato kutokana na uzalishaji mzuri ambapo katika msimu wa 2009/10 alilima ekari mia moja ishirini na tano za shayiri na kuvuna takribani tani kumi na nane za shayiri iliyompatia zaidi ya shilingi milioni arobaini na tano.
Mdangwa alisema TBL ilimuwezesha kuanzia maandalizi ya shamba, kulima, pembejeo na hata uvunaji na baada ya mauzo hakukatwa hata senti ya marejesho kwa huduma alizopata wakati wa msimu wote wa kilimo.
Kampuni ya bia Tanzania imefungua tawi lake jijini Mbeya katika kanda ya Nyanda za juu Kusini na kuanzisha uzalishaji wa shayiri katika mikoa ya Mbeya, Iringa, Njombe na Rukwa ili kuongeza uzalishaji na kupunguza gharama uendeshaji kwani hivi sasa shayiri inayotumika kutengenezea bia Tanzania ni asilimia ishirini t undo inayolimwa hapa nchini na asilimia themanini inazalishwa nje ya nchi licha ya kuwa na hali ya hewa inayofaa kwa zao hilo.

ASKOFU KIKOTI AFARIKI DUNIA
ASKOFU wa kanisa katoliki jimbo la Mpanda Mkoa wa Katavi, Mhashamu askofu Paschal William Kikoti amefariki dunia katika hospitali ya Bugando jijini Mwanza Agosti 28, 2012 alikokuwa amepelekwa kutibiwa.
Taarifa iliyotolewa na kanisa katoliki jimbo la Mpanda imeeleza kuwa mwili wa marahemu utawasili Mpanda kwa ndege siku ya alhamisi Agosti 30, 2012 saa tisa alasiri na kupokelewa na waumini  na wananchi wengine katika uwanja wa ndege wa Kashaulili mjini humo.
Mara baada ya kuwasili mwili waumini wataandamana na mwili hadi kanisa kuu Katoliki la Mpanda mjini kwa ibada ya mfululizo kumuombea askofu wao ambapo ibada zitaendelea usiku na mchana hadi siku ya Jumamosi .
Taarifa hiyo imeeleza kuwa ibada ya mazishi itakuwa siku ya Jumamosi katika kanisa kuu katoliki la Mpanda ambapo ratiba ya mazishi hayo itatolewa baadaye na kanisa hilo.
Taarifa za kuumwa Mhasham Askofu Kikoti zilipatikana siku ya jumapili baada ya kuelezwa kuwa aliteleza na kuanguka ghafla alipokuwa akioga na baadae alielezewa kuwa anasumbuliwa na ugonjwa wa moyo hali iliyopelekea kuita ndege kwa ajili ya kumuwahisha katika hospitali ya Bugando jijini Mwanza kwa matibabu ambako aliendelea na matibabu hadi mauti yanamfikia.
Askofu Paschal William Kikoti alizaliwa mnamo Machi 3, 1957 katikia kijiji cha Ilimo mkoani Iringa na kupata upadrisho mnamo Juni 29, 1988 na baadaye alipewa daraja la Uaskofu Januari 14, 2001 baada ya kuteuliwa kuliongoza jimbo la Katoliki la Mpanda enzi hizo ikiwa mkoani Rukwa na baadaye mkoa wa Katavi hadi mauti yalipofika Agosti 28, 2012.
Hii  ni mara ya pili kwa askofu huyo kuanguka kwa ugonjwa wa moyo ambapo awali alianguka siku anasimikwa  kuwa askofu wa kanisa katoliki la Mpanda katika kanisa kuu la mtakatifu Maria Immaculata mjini Mpanda.

MSIBA MZITO KANISA KATOLIKI MPANDA

ASKOFU wa kanisa katoliki jimbo la Mpanda Mkoa wa Katavi, Mhashamu askofu Paschal William Kikoti amefariki dunia katika hospitali ya Bugando jijini Mwanza Agosti 28, 2012 alikokuwa amepelekwa kutibiwa.
Taarifa iliyotolewa na kanisa katoliki jimbo la Mpanda imeeleza kuwa mwili wa marahemu utawasili Mpanda kwa ndege siku ya alhamisi Agosti 30, 2012 saa tisa alasiri na kupokelewa na waumini  na wananchi wengine katika uwanja wa ndege wa Kashaulili mjini humo.
Mara baada ya kuwasili mwili waumini wataandamana na mwili hadi kanisa kuu Katoliki la Mpanda mjini kwa ibada ya mfululizo kumuombea askofu wao ambapo ibada zitaendelea usiku na mchana hadi siku ya Jumamosi .
Taarifa hiyo imeeleza kuwa ibada ya mazishi itakuwa siku ya Jumamosi katika kanisa kuu katoliki la Mpanda ambapo ratiba ya mazishi hayo itatolewa baadaye na kanisa hilo.
Taarifa za kuumwa Mhasham Askofu Kikoti zilipatikana siku ya jumapili baada ya kuelezwa kuwa aliteleza na kuanguka ghafla alipokuwa akioga na baadae alielezewa kuwa anasumbuliwa na ugonjwa wa moyo hali iliyopelekea kuita ndege kwa ajili ya kumuwahisha katika hospitali ya Bugando jijini Mwanza kwa matibabu ambako aliendelea na matibabu hadi mauti yanamfikia.
Hii  ni mara ya pili kwa askofu huyo kuanguka kwa ugonjwa wa moyo ambapo awali alianguka siku anasimikwa  kuwa askofu wa kanisa katoliki la Mpanda katika kanisa kuu la mtakatifu Maria Immaculata mjini Mpanda.
Source:www.willysumiampanda.blogspot.com





August 27, 2012

SEMINA YA MAADILI YA UANDISHI WA HABARI RUKWA PRESS CLUB UKUMBI WA CWT-SUMBAWANGA

 Wanachama wa RPC wakiwa katika ukumbi wa semina mjini Sumbawanga siku ya kwanza ya semina

 Makamu mwenyekiti wa RPC akifungua mkutano wa semina ya waandishi wa habari leo mjini Sumbawanga katika ukumbi wa Chama cha walimu Rukwa.
 Mwezeshaji kiuchumi wa MCT, Jackline Shirima akisikiliza somo la maadili ya uandishi wa habari mjini Sumbawanga katika ukumbi wa Chama cha walimu

 Mkufunzi wa maadili kutoka MCT, Beda Msimbe akifafanua umuhimu wa uandishi wa kufuata maadili wakati wa kuandaa habari kwa mwandishi wa habari katika ukumbi wa CWT Rukwa mjini Sumbawanga leo.



 Umakini huongezeka somo linapokolea kwa  wahusika, wanasemina wakiwa busy" wakati wa somo




 Mwenyekiti wa Rukwa Press Club (RPC), Peti Siyame akifafanua maslahi kwa wanasemina

 


NAPE AIKOMALIA CHADEMA

Nape Nnauye

KATIBU wa Halmashauri Kuu ya Taifa Itikadi na Uenezi CCM, Nape Nnauye amewataka Chadema kwenda mahakamani haraka badala ya kusubiri kuombwa radhi kama walivyotaka ili kusafishwa dhidi ya madai ya chama chao kupewa mabilioni ya fedha na mataifa tajiri.

Aidha amemtaka Katibu Mkuu wa chama hicho Dk. Wilbrod Slaa kuiomba radhi CCM la sivyo itamburuza mahakamani kudai fidia ya sh. bilioni 3 na shilingi moja, kwa kuituhumu uongo kwamba imeingiza silaha kutoka nje ya nchi tena bila kulipia ushuru.

Nape alisema hayo leo Agosti 27, 2012, kweneye mkutano wake na waandishi wa habari, uliofanyika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, mtaa wa Lumumba mjini Dar es Salaam.

"Bila shaka mmesikia jana Chadema wakinitaka niombe radhi au wananipeleka mahakamani kudai fidia ya sh. bilioni 3, kwa madai eti nimesema Chama hicho kinapata mabilioni ya fedha kutoka kwa mataifa tajiri. Mkubwa hatishiwi nyau, nawataka waende haraka mahakamani wala wasisubiri hizo siku saba", alisema Nape.

Alisema, CCM inao ushahidi wa kutosha kuhusu madai aliyotoa Nape dhidi ya Chadema na kwamba huyo tayari kutoa uthibitisho huo mahakamani badala ya kuomba radhi.

"Nadhani wakienda mahakani itapendeza zaidi maana huko ndiko pazuri kutoa uthibitisho kuhusu tuliyosema, na ninawahakikishieni tukishathibitisha na Msajili wa Vyama akaupata uthibitisho huo chama chao kinafutwa", alisema.

Kuhusu CCM kumburuza Dk. Slaa mahakamani, Nape alisema, ameshawaagiza wanasheria wa Chama, kuandaa barua ya kusudio la mashitaka hayo, na Dk. Slaa atapelekewa ili aamue kama ataomba radhi au atakuwa tayari kwenda mahakamani.

"Wakati wanakwenda mahakamani, Chadema wamwambie babu yao ajiandae kuomba radhi au kuburuzwa mahakamani kuilipa CCM fidia ya sh. bilioni 3 na shilingi moja kwa kuizushia CCM uongo kwamba inaingiza silaha nchini tena", alisema Nape.

JESHI LA POLISI  KATAVI LAWAHAKIKISHIA USALAMA WANANCHI KIPINDI CHA SENSA

Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Katavi, Dhahiri A. Kidavashari (ACP)
 
JESHI la polisi mkoa wa Katavi limewahakikishia wananchi kuwa hakuna tatizo la usalama wao na mali zao katika kipindi chote cha Sensa ya watu na makazi na hata baada ya sense
Akizungumza na blog hii kamanda wa jeshi la polisi mkoani humo, Dhahiri Kidavashari amesema wananchi wasiwe na wasi wasi juu ya kutokea tatizo lolote la kiusalama wakati wa zoezi la sense ya watu na makazi na hata baada ya sense kutokana na mikakati ya kuimarisha utendaji kazi wa jeshi lake mkoani humo
Kidavashari amesema leo uwanja wa ndege wa Mpanda kuwa kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa imefanya ziara katika maeneo yote yaliyokuwa na dalili za utata kuhusu sense na kujiridhisha juu ya usalama wa makarani, wananchi na mali za wananchi na kujipanga vema kukabili tishio lolote la kiusalama
Amesema polisi wako tayari kukabiliana na dalili zozote za kiuhalifu katika mkoa mzima na wananchi wasisite kutoa taarifa pale watakapobaini uwepo wa watu wasi na nia njema katika eneo lolote wakati wowote ili jeshi lake liweze kuchukua hatua stahili kwa wakati na kuzuia uhalifu na ikiwezekana kuwatia nguvuni wahalifu watakaokuwa wamebainika
Amesema jeshi lake limekuwa likifanya kazi usiku na mchana kukabiliana na njama za uhalifu kuliko kukabiliana na uhalifu uliotokea tayari kwa kushirikiana na wananchi wema pindi tu wanapotoa taarifa kwa wakati
Amewaomba wananchi kuendelea kutoa taarifa za uwepo wa dalili za kiuhalifu ili kuzuia vifo, uharibifu wa mali na hata madhara yanayotokea pindi uhalifu unapotokea eneo Fulani na kuwa jeshi lake liko tayari masaa ishirini na nne
Amewatahadharisha wananchi watakaodanganyika kugomea zoezi la sense kuwa jeshi la polisi halitasita kuwachukulia hatua kwani sense ipo kisheria na sheria inapendeza sana kama wananchi wataitii bila shuruti  lakini wanapotokea wasiopenda kutii sheria lazima kutatokea nguvu ya jeshi la polisi hivyo amewasihi wananchi kuepuka kabisa vitendo vitakavyoashiria uvunjifu wa sheria ya sense kipindi cha sense.













SENSA YA WATU NA MAKAZI 2012; 

WAZIRI MKUU PINDA AREJEA KUHESABIWA KWAO
 Ndege aliyotumia Waziri Mkuu Mhe Pinda akitokea jijini DSM kwenda Mpanda leo ikitua uwanja wa ndege wa kashaulili mjini hapo
 Waziri Mkuu akiwaaga wafanya kazi wa kwenye ndege aliyoitumia kusafiria kwenda kushiriki sensa kwao kijiji cha  Kibaoni
 Waziri Mkuu Mhe. Pinda akisalimiana na Viongozi wa Mkoa wa Katavi katika uwanja wa ndege wa Kashaulili Mjini Mpanda mara baada ya kuwasili uwanjani hapo kwa lengo la kwenda kushiriki katika sensa kijijini kwao Kibaoni wilaya ya Mlele mkoa wa Katavi.










 Waziri Mkuu Mhe Pinda akisalimiana na Mwenyekiti wa UVCCM (W) Mpanda Haidary Sumry mara baada ya kuwasili uwanja wa ndege mjini Mpanda Leo Agosti 24, 2012 akitokea jijini DSM.
 Mkuu wa mkoa wa Katavi Dr Rajabu Rutengwe( kushoto) akimuongoza Waziri Mkuu katika chumba cha Mapumziko ya viongozi wanapowasili uwanjani hapo
Baadhi ya wananchi wakiingia katika ndege iliyomleta waziri mkuu wakipanda ndege tayari kwa safari ya kuelekea jijini DSM

August 23, 2012


WAZIRI DKT MWAKYEMBE AMSIMAMISHA KAZI MKURUGENZI MKUU WA TPA

Waziri wa Uchukuzi Dokta HARRISON MWAKYEMBE amemsimamisha kazi Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari-TPA-Ndugu EPHRAIM MGAWE-TPA pamoja na wasaidizi wake wawili ili kupisha uchunguzi wa tuhuma zinazowakabili.

Wengine waliosimamishwa ni Meneja wa Mafuta ya Ndege Kurasini, Meneja wa JET na Meneja wa Oil Terminal kutokana na tuhuma za kupotea kwa mafuta na kuidanganya serikali kuhusu mafuta masafi na machafu.

Kutokana na kuwasimamisha kazi Wakurugenzi hao Dokta MWAKYEMBE amemteua Injinia MADENI KIPANGE kukaimu nafasi ya Mkurugenzi Mkuu wa TPA.

Kufuatia tuhuma hizo zinazofanywa Bandarini Dokta MWAKYEMBE ameunda Tume wa ya watu saba kufanya uchunguzi kwa wiki mbili na kumpelekea taarifa ofisini kwake ili kubaini ukweli wa tuhuma hizo zikiwemo za wizi.

Pia ameagiaza kufikia Septemba Mosi mwaka huu malipo yote yafanyike benki ili kuondoa rushwa na wizi unaofanyika ndani ya Mamlaka hiyo.

Waziri MWAKYEMBE anachukua hatua hizo kutokana na wwadao wengi sasa hawaitumii Bandari ya Dar es salaam kupitisha mizigo yao kutokana na kutokuwa na inami na watumishi wake hatua inayoifanya serikali kukosa mapato.

Pia ameagiza kusimamishwa mara moja kwa Kampuni ya Singilimo ambayo inajihusisha na kazi ya kubeba mafuta machafu na badala yake itafutwe Kampuni nyingine.






August 20, 2012


HALMASHAURI ZA MKOA WA LINDI ZAAGIZWA KUTENGA MAENEO YA VIWANJA VYA MICHEZO

Mkuu wa Mkoa wa Lindi,Ludovick Mwananzira
akikabidhi kikombe cha IMRAN Kwa Nahodha wa Timu ya Lunduno Fc baada
ya kuibugiza Timu ya Nachingwea kwa mikwaju ya penalti na kupata
jumla ya mabao 6 kwa 5

SERIKALI mkoani Lindi imeziagiza Halmashauri za Wilaya Na Manispaa katika Mkoa wa Lindi kutenga bajeti ya kutosha ya kuhudumia michezo hasa ujenzi wa viwanja vya michezo ili kukabiliana na tatizo la upungufu wa viwanja hivyo.

Akifunga rasmi mashindano ya Imran cup yaliyomalizika jana na
kushirikisha timu 7 za Manispaa ya Lindi,Mkuu wa Mkoa wa
Lindi,Ludovick Mwananzila alizitaka Halmashauri hizo kuthamini Michezo
ikiwa pamoja na utengaji na Ujenzi wa Viwanja vya Michezo ili kuibua
vipaji vya Wanamichezo

Ili kuinua sekta ya michezo katika ngazi yoyote kama hutakuwa na
viwanja vya kutosha na vilivyo katika ubora unaostahili kwa michezo
husika. Ikiwa pamoja na uwepo wa ufinyu wa bajeti ya michezo

‘’Wakurugenzi kupitia maafisa michezo nawaomba kupanga bajeti za
michezo na pia lazima mtenge maeneo ya viwanja na huu wa Ilulu
uboreshwe kwa kuwa ndio kioo cha Mkoa katika viwanja;;;Alisisitiza
Mwananzila

Awali akitoa taarifa ya Mashindano hayo kwa Mgeni rasmi,Mratibu wa
Mashindano hayo ambae pia ni Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa
Habari Mkoa wa Lindi,Abdulaziz Ahmeid alimuomba mkuu wa Mkoa wa Lindi
kuangalia Uwezekano wa kuunda Mfuko wa kusaidia Michezo Lindi kwa
kuchangisha kupitia Mazao,Mafuta na Vinywaji ikiwa Pamoja na Kuona
umuhimu wa kutenga maeneo ya Ujenzi wa Viwanja

Katika Fainali hiyo Timu ya Lunduno Fc Ya Kata ya Mikumbi iliibuka
kidedea na kutwaa kikombe cha Ligi hiyo pamoja na seti ya jezi baada
ya Kuifunga Timu ya Kata ya Nachingwea .Manispaa ya Lindi kwa mabao 6
kwa 5 baada ya kupigiana Mikwaju ya penalty baada ya Kumalizika kwa
dakika 90 mabao yakiwa bila kwa bila
Timu zilizoshiriki ligi hiyo ni Nachingwea fc,Brazil Fc,Makavu
Fc,Kusini Soccer,Lunduno sc,Mtanda Fc na Lindi Sports zote toka
Manispaa ya Lindi

Fainali za ligi iliyokuwa katika sikukuu za Idd el fitr ziliendana na
michezo ya kukimbia,kufukuza kuku,kukimbia na magunia pamoja na mbio
za baiskeli kuzunguka uwanja wa Ilulu

BONDIA MANENO OSWARD AMTWANGA RASHIDI MATUMLA KWA POINT


MANENO OSWARD AKIJARIBU KUTUPIANA NGUMI ZA MABISHANO NA RASHIDI MATUMLA YANI NIPE NIKUPE MPAKA MWISHO WA MCHEZO MANENO ALIBUKA MSHINDI KWA POINT
Bondia Rashidi Matumla kushoto akioneshana umwamba wa kutupa masumbwi na Maneno Osward wakati wa mpambano wao uliofanyika jana katika ukumbi wa Dar live Maneno alishinda kwa point
Bondia Rashidi Matumla kushoto akioneshana umwamba wa kutupa masumbwi na Maneno Osward wakati wa mpambano wao uliofanyika jana katika ukumbi wa Dar live Maneno alishinda kwa point.

SENSA  YA  WATU  NA  MAKAZI 2012


Makarani wa sensa katika halmashauri ya Mji Mpanda mkoa wa Katavi wakinolewa tayari kwa ajili ya zoezi la sensa katika ukumbi wa shule ya sekondari Mwangaza


Hakimu mkazi wa wilaya ya Mpanda, Mhe. Richard Robert Kasele akifafanua utaratibu wa Kiapo kwa makarani wa sensa ya watu na makazi 2012 katika ukumbi wa shule ya sekondari ya Mwangaza mjini Mpanda katika mkoa wa Katavi leo alasiri.


KIAPO KWA MAKARANI WA SENSA 2012





Mhe Richard Robert Kasele, Hakimu mkazi akisaini kiapo cha karani wa sensa leo alasiri mara baada ya kuwaapisha makarani wa sensa mjini Mpanda.

Mmoja wa makarani akisaini kiapo mara baada ya kuapishwa na Hakimu mkazi wa wilaya ya Mpanda



























WAZIRI MKUU PINDA AWASILI MKOA MPYA WA KATAVI AGOSTI 19, 2012, AENDA MOJA KWA MOJA KIJIJINI KWAO KIBAONI TARAFA YA MPIMWE WILAYA YA MLELE



















































Kamanda wa polisi Mkoa wa Katavi ACP Dhahir Kidavashari




Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na Rais wa Malawi Mhe.Joyce Banda mjini Maputo Msumbiji walipokutana leo asubuhi kuzungumzia kutafuta suluhu katika mgogoro wa mpaka kati nchi hizo uliopo kwenye ziwa Nyasa.Wakati wa mazungumzo hayo Marais hao wawili wameelezea nia ya nchi zao kufikia suluhu kwa njia za kidiplomasia kupititia kamati maalumu iliyoundwa kushughulikia mgogoro huo (picha na Freddy Maro).
Rais wa Malawi Mhe.Joyce Banda akisalimiana na Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete mapema leo asubuhi mjini Maputo Msumbiji,walipokutana kuzungumzia kutafuta suluhu katika mgogoro wa mpaka kati nchi hizo uliopo kwenye ziwa Nyasa.Wakati wa mazungumzo hayo Marais hao wawili wameelezea nia ya nchi zao kufikia suluhu kwa njia za kidiplomasia kupititia kamati maalumu iliyoundwa kushughulikia mgogoro huo.
Marais wakizungumza kwa furaha kabisa.
Rais Dkt.Jakaya Kikwete akifafanua jambo mbele ya Wanahabari mapema leo asubuhi mjini Msumbiji,ambapo Rais Kikwete amekutana na Rais wa Malawi Mhe.Joyce Banda kuzungumzia kutafuta suluhu katika mgogoro wa mpaka kati nchi hizo uliopo kwenye ziwa Nyasa.Wakati wa mazungumzo hayo Marais hao wawili wameelezea nia ya nchi zao kufikia suluhu kwa njia za kidiplomasia kupititia kamati maalumu iliyoundwa kushughulikia mgogoro huo.


August 19, 2012


SHEKHE MKUU WA WAISLAM MKOA WA IRINGA AZUNGUMZIA MGOGORO WA MPAKA KATI YA MALAWI NA TANZANIA

Waumini wa dini ya Kiislam mjini Iringa wakipongezana baada ya ibada ya sikukuu ya Idd El Fitri iliyofanyika uwanja wa samora leo
Kamanda wa UV CCM Iringa vijijini Arif Abri akipongezana na muumini mwenzake mara baada ya ibada kumalizika
Ibada ikiendelea uwanja wa samora leo
Mwenyekiti wa CCM Iringa mjini Abed Kiponza (kulia) akiwa katika ibada hiyo
Shekhe mkuu wa Waislam mkoa wa Iringa Ally Juma Tagalile ( wa pili kushoto ) akiwa katika ibada
Furaha za Idd toka kwa kamanda wa UVCCM Iringa vijijini Arif Abri
Picha ya kumbukumbu kwa waislam kusali pamoja leo Iringa
Wadau wa mtandao hu kutoka Famari Store wakiwa katika ibada hiyo


SHEKHE mkuu wa waislam mkoani Iringa Ally Juma Tagalile amempongeza Rais Jakaya Kikwete kwa hatua yake ya kuanza kulitafutia ufumbuzi bila mapingano suala la mgogoro wa mpaka kati ya Tanzania na Malawi.
Huku akiwataka watanzania pamoja na viongozi wa dini zote hapa nchini kuendelea kuliombea Taifa ili lisiingie katika machafuko ya vita baina ya nchi na nchi .

Kuhusu zoezi la sensa ya watu na kamazi inayotaraji kufanyika kote nchini usiku wa jumamosi Agosti 25 kuamkia Agosti 26 siku ya jumapili ijayo , Tagalile amewahimiza waislam mkoani Iringa kushiriki katika zoezi hilo bila kurubuniwa na mtu yeyote .
Alisema kuwa zoezi hilo la sensa ya watu na makazi ni zoezi mhimu kwa watanzani wote bila kujali itikadi za dini ,vyama wala rangi na hivyo kuwataka waumini wa dini hiyo kupuuza maneno ya mitaani dhidi ya sensa na badala yake kutoa ushirikiano wao kwa makalani wa sensa watakaofika katika maeneo yao kwa ajili ya kukamilisha zoezi hilo.

WAZIRI MKUU PINDA KUWASILI KATAVI LEO HII ASUBUHI 

Taarifa zilizopatikana kutoka ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Katavi zinasema kuwa mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Kashaulili mjini Mpanda, Mhe. Waziri Mkuu atapokea taarifa ya utekelezaji wa shughuli za serikali za mkoa na wilaya mbili za Mlele na Mpanda kisha baadaye ataelekea kijijini kwao Kibaoni Tarafa ya Mpimbwe kwa mapumziko ya kifamilia.

WASHINDI WA MASHINDANO YA KUSOMA QURAAN TAKATIFU IRINGA WAPATIKANA USIKU HUU

Mmoja kati ya majaji na walimu waliowanoa watoto hao Masoud Salim(kushoto) akizungumza kwa niaba ya majaji wenzake
Waumini wa msikiti wa Ijumaa Iringa wakifuatilia mashindano hayo









Timu ya waratibu wakijiandaa kwa kutoa zawadi chini ya mgeni rasmi mstahiki meya wa Iringa Aman Mwamwindi (kulia)


Mgeni rasmi Mshtahiki meya wa manispaa ya Iringa Aman Mwamwindi akikabidhi zawadi kwa washindi

















Jopo la majaji


mmoja kati ya washiriki















Changamoto imetolewa kwa waumini wa dini ya Kiislam mkoani Iringa pindi wanapoanzisha mashindano mbali mbali kwa ajili ya watoto pia kukumbuka kuwatazama walimu ambao wamewawezesha watoto hao kufanya vema.


Changamoto hiyo imetolewa mapema leo wakati wa mashindano ya kiongozi wa majaji Masoud Salim kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi mstahiki meya wa Iringa Aman Mwamwindi kukabidhi zawadi kwa washindi wa shindano hilo


Habari kamili na picha zitakujia hapo kesho kumbuka kesho pia ni siku kuu ya

Idd El FitriMAVAZI MAFUPI YANAASHIRIA KITU KIBAYA KINAINGIA KWA ASKARI POLISI WA KIKE

Je! Mavazi ya Polisi wa Kike yanakidhi matakwa ya Waraka Na 3 wa Mavazi ya Watumishi wa Umma?


Baadhi ya wadau wamehoji mavazi ya namna hii kwa Asakri Polisi wa Kike kama yanakidhi matakwa na kuweza kumsitiri Askari wa kike wa Jeshi la Polisi awapo katika Utekelezaji wa Kazi zake za kila siku kwa kuwahudumia wananchi.

Pia wadau wanahoji kuwa Waraka wa Utumishi wa Umma na 3 wa mwaka 2007 kuhusu mavazi kwa watumishi wa umma kama unatekelezwa na Jeshi jeshi hilo ama au wahusu.

Aidha wadau hao wamesema ipo haja kwa Jeshi la Polisi hapa nchini kubadili mavazi hayo kwa Wanawake na kuamuru zivaliwe surwale wakati wote wawapo kazini maana wapo askari wa kikle wanaoenda doria na sketi hizo jambo ambalo ni rahisi kutokea vitendo vya uzalilishaji kwao, na badala yake wameshauri zivaliwe wakati wa shughuli maalum tu kama vile sherehe za kijeshi na Kitaifa ambapo hakuihitaji pilika pilika za hapa na pale ndio wavae Sketi huku pia wakidai sketi hizo ziwe ndefu kiasi cha kuvuka magati.

Hata hivyo Sketi fupi mfano wa hiyo iliyovaliwa na Askari hiyo ambaye Blog hii imemhifadhi haiendani na sheria za mavazi ya Mtumishi wa Umma ambayo hapaswi kuvaa nguo fupi kwa Mujibu wa waraka wa Utumishi wa Umma.
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA OFISI YA RAIS
Kumb. Na. EG.45/86/01/”A”/2 12/9/2007
WARAKA WA UTUMISHI WA UMMA NA 3 WA MWAKA
2007 KUHUSU MAVAZI KWA WATUMISHI WA UMMA
Utangulizi:
Waraka wa Utumishi Na. 1 wa mwaka 1971 unaohusu mavazi ulitokana na mwongozo uliotolewa na Chama cha TANU kuhusu mavazi. Madhumuni ya waraka huo ilikuwa kuimarisha heshima ya Taifa kwa kuhakikisha kuwa watumishi wa Serikali wanavaa mavazi ya heshima wanapowahudumia wananchi. Waraka huo uliainisha baadhi ya mifano ya mavazi ambayo yalionekana hayafai na yale yanayofaa kwa wanawake na wanaume, utengenezaji wa nywele unaofaa na usiofaa na vipodozi visivyokubalika.

Hali ilivyo sasa:

2. Tangu waraka huo ulipotolewa kumekuwepo na mabadiliko makubwa ya mitindo ya mavazi, nywele na vipodozi. Mabadiliko ya mitindo ya mavazi ni jambo lisiloepukika. Hata hivyo baadhi ya mitindo hiyo ya mavazi inashusha heshima na hadhi ya utumishi wa umma kama itaendelea
kuvaliwa na ni kinyume na kifungu cha 2 (e) cha kanuni za Maadili ya utendaji katika utumishi wa umma za mwaka 2005 Hata hivyo kumekuwepo na tatizo la kutokuwepo na tafsiri inayoeleweka juu ya mavazi gani ni ya heshima au yanayokubalika na yasiyokubalika mahali pa kazi.

2
Uamuzi wa Serikali:
Tafsiri ya mavazi ya heshima hutegemea mila na desturi ya jamii husika. Katika utumishi wa umma mavazi ya heshima kwa mtumishi wa umma ni yale ambayo yanazingatia mila na desturi za taifa letu ambayo yanapovaliwa hayaonyeshi sehemu ya maungo ya mwili ambayo hayakuzoeleka kuachwa wazi, hayabani na ambayo hayana michoro au maandishi ya kudhalilisha wengine au yanayoonyesha ushabiki wa kitu fulani. Kwa hiyo waraka huu unatoa ufafanuzi kuhusu mavazi nadhifu yanayopaswa kuvaliwa kazini kwa kutoa mifano michache ya mavazi ambayo siyo ya heshima na ambayo hayakubaliki katika utumishi wa umma kwa jinsi zote mbili.

Utekelezaji:
3. Ufuatao ni ufafanuzi wa mavazi yasiyokubalika mahali pa kazi ambayo pia yameonyeshwa kwa picha kwenye kiambatisho A na B. Nguo kama “Jeans” na fulana zinaweza kuvaliwa na watumishi ambao wanalazimika kufanya kazi za nje ya ofisi.

3.1 Kwa Wanawake
(i) Baadhi ya mavazi yasiyofaa:
• Nguo zinazobana,
• Nguo fupi ambazo zinaacha magoti wazi.
• Nguo ambazo zinaacha sehemu ya mwili wazi kama
vile kitovu na kifua,
• Nguo ambazo zina picha, michoro, na maandishi ambayo hayaendani na shughuli za serikali,
• Kaptura aina yoyote ile kama vile pedo na pensi,
• Nguo zinazoonyesha maungo ya mwili (transparent).
• Suruali za “Jeans”,
• Suruali yoyote iliyoachwa bila kupindwa,
• Fulana – “T-Shirts” (Hizi zivaliwe tu wakati wa shughuli maalum inayotambulika),
• Nguo ambazo ni za kazi maalum – michezo, kazi za nje au burudani. Hizi zivaliwe mahususi wakati wa utekelezaji wa shughuli hizo,
• Nguo yenye maandishi ya chama chochote cha siasa au ushabiki wa kitu fulani,
• Nguo yeyote inayopingana na maadili ya utumishi wa umma.
(ii) Nywele zisizofaa:
• Nywele chafu na ambazo hazikutengenezwa vizuri.
(iv) Viatu visivyofaa
• Kandambili,
• Viatu vya michezo (isipokuwa wakati wa shughuli
maalum za michezo),

3.2. Kwa Wanaume
(i) Baadhi ya mavazi yasiyofaa:
• Nguo ambazo ni za kazi maalum kama vile michezo (Hizi zivaliwe wakati wa shughuli hiyo tu).
• Nguo ambazo zina michoro, maandishi na picha ambazo haziendani na shughuli za serikali.
• Nguo zinazobana,
• Kaptura ya aina yoyote.
• Suruali yoyote inayoachwa bila kupindwa.
• Suruali za “Jeans” na Fulana “T-shirts” (Hizi zivaliwe tu wakati wa shughuli maalum inayotambulika).
• Kikoi au msuli
• Nguo zenye maandishi ya chama chochote cha siasa na yenye kuonyesha ushabiki wa kitu fulani.
• Nguo yeyote inayopingana na maadili ya utumishi wa
umma.
(iii) Nywele zisizofaa:
• Nywele chafu na ambazo hazikutengenezwa vizuri.
• Nywele zilizosukwa mitindo ya aina yoyote ile
• Ndevu zisizotunzwa vizuri.
(iv) Viatu visivyofaa:
• Kandambili,
• Viatu vya michezo( Labda wakati wa shughuli maalum
za michezo).

Mwisho:
4. Kwa waraka huu waajiri wote wanapaswa kuwaelimisha watumishi kuhusu mavazi yasiyokubalika na kusimamia kikamilifu suala la mavazi kwa watumishi wa umma .
5. Waraka huu unafuta Waraka wa Utumishi Na.1 wa mwaka 1971 na unaanza kutumika mara moja.
George D. Yambesi
KATIBU MKUU
(MENEJIMENTI YA UTUMISHI WA UMMA)






















WANASWA KWA WIZI WA UMEME SUMBAWANGA
 WATU wawili wakazi wa manispaa ya Sumbawanga mkoani Rukwa wametiwa nguvuni na jeshi la polisi kwa tuhuma za kubainika kuliibia shirika la umeme nchini TANESCO mkoa wa Rukwa kwa kujiunganishia umeme bila kupitia kwenye mita
WATUHUMIWA hao wawili Elizabeth Mhando na Mwandele investment wamefunguliwa mashtaka ya wizi wa udanganyifu na upelelezi unaendelea kujua kiasi halisi cha fedha wanazodaiwa na  TANESCO katika kipindi cha miezi kumi na mbili iliyopita
KAIMU meneja wa TANESCO mkoa wa Rukwa Emmanuel Kachewa amesema mikakati ya shirika kitaifa kupitia operesheni iitwayo-KAWEU-kamata wezi wa umeme ni kutaka kukabiliana na udanganyifu unaofanywa na baadhi ya wateja
HATA hivyo bw. Kachewe amekiri kuwapo kwa tuhuma kuwa baadhi ya wafanyakazi wa shirika la TANESCO wanashirikiana na baadhi ya wateja wasiokuwa waaminifu kuliibia shirika umeme na kuwa mteja baada ya kukatwa kwa tuhuma hizi hurudishiwa umeme baada ya kufanyiwa tathimini ya matumizi ya vifaa vyake kwa mwezi
JESHI la polisi mkoa wa Rukwa nalo limeshirikishwa na TANESCO katika operesheni hii ya kuwabaini wateja wasiokuwa waaminifu ambapo kamanda wa jeshi hilo Jacob Mwaruanda amesema zoezi hilo litakuwa endelevu ili kupunguza kasi ya uhujumu wa umeme wa shirika
AJALI YA FUSO YAUA KUMI NKASI

Wananachi wa Mwangata Iringa wakishuhudia ajali hiyo asubuhi ya leo
POLISI mkoani RUKWA imethibitisha kutokea vifo vya watu kumi waliokufa katika ajali iliyotokea jana asubuhi kwenye kijiji cha NTATUMBILA wilaya NKASI kwenye barabara itokayo kijiji cha KATE kwenda mjini SUMBAWANGA mkoani RUKWA

TAARIFA ya Kamanda wa polisi wa mkoa wa RUKWA JACOB MWARUANDA imeeleza kuwa waliokufa ni Martin Mpuka, Erasto Bonifas, January Kallelembe, Kabuta Bulugu, Leswida Fwamba, Gilbert Kakuwa, Ibrahimu  Mwanawima na wengine waliojulikana kwa jina moja moja Deodatus,  Skola,  na Fabora

AMEELEZA kuwa marehemu hao wanaume watano, wanawake wawili na watoto watatu wa kiume wanatoka katika vijiji vya Kitosi, Ntunchi, Ifundwa na Kalundi na kuwa hadi sasa majeruhi waliolazwa katika hospitali ya mkoa mjini Sumbawanga ni 25 na watatu kati yao hali zao sio nzuri

KAMANDA MWARUANDA amesema dreva wa gari aina ya Fuso lililosababisha ajali lenye namba za usajili T.407 AST,  GEORGE KAWITI anatafutwa na polisi baada ya kutoroka kufuatia ajali hiyo iliyosababisho vifo vya watu sita papo hapo na wengine wanne kufia hospitali na 29 kujeruhiwa

Kamanda amefafanua kuwa bado uchunguzi unafanyika kujua chanzo cha ajali hiyo licha ya kueleza kuwa gari hilo la mizigo lilikuwa na abiria wengi pamoja na mizigo kupita uwezo wa gari.


MKUU WA WILAYA YA MPANDA, PAZA MWAMLIMA AZINDUA KAMPENI YA HAMASA YA SENSA MPANDA MJINI KATIKA ENEO LA KAKESE

 Mkuu wa wilaya ya Mpanda Paza Tusamale Mwamlima akimhoji mwananchi mmoja mkazi wa kijiji cha Kakese aliyejitambulisha kuwa jina lake anaitwa SHETANI na wala hana dini
 Huyu ndo SHETANI anayeishi kijiji cha Kakese Mbugani wilaya ya Mpanda mkoa wa Katavi akizungmzia sensa katika mkutano wa hadhara uliofanyika jana kijijini hapo, mwananchi huyu alimwambia mkuu wa wilaya katika mkutano huo kuwa hana dini ila anaamini kuwa sensa ni muhimu sana kwa Watanzania.
 Baadhi ya wananchi waliojitokeza kushiriki katika uzinduzi wa kampeni ya hamasa ya sensa katika kijiji cha Kakese jana jioni, mgeni rasmi alikuwa mkuu wa wilaya ya Mpanda Paza Tusamale Mwamlima
 Mkuu wa wilaya ya Mpanda, Paza Tusamale Mwamlima akihutubia wananchi katika uzinduzi wa kampeni ya hamasa ya sensa 2012 katika kijiji cha Kakese nje kidogo ya Mji wa Mpanda katika mkoa wa Katavi

RIPOTI KAMILI YA SOKO LA MAGAZETI IRINGA, MWANANCHI , JIBU LA MAISHA , UWAZI , MWANAHALISI YAONGOZA ...

Mwakilishi msaidizi wa gazeti la Mwananchi Iringa Diana Kangusi (kulia) akiwa na mwandishi wa gazeti la The Citizen Iringa Clement Sanga wakionyesha kwa wanahabari za uchunguzi nakala ya magazeti hayo leo baada ya kufika katika ofisi za Mwananchi kwa ajili ya uchunguzi wa soko la magazeti Iringa. Wakala wa magazeti mbali mbali mjini Iringa Salum Zingilwa akiwa amebeba mzigo wa mabaki ya magazeti yaliyorudishwa na wauzaji Hapa ni kusoma bure na kuondoka hakuna mnunuzi hapa
Iimeelezwa kuwa tatizo la kushuka kwa soko la magazeti mkoani Iringa limechangiwa na baadhi ya wauza magazeti kukodisha magazeti hayo pamoja na vituo vya radio na Runginga kuendesha vipindi vyake kwa kutegemea magazeti hayo . Uchunguzi uliofanywa na wanahabari mjini Iringa umebaini hayo baada ya kuzungumza na makundi mbali mbali likiwemo kundi la wauza magazeti na wadau mbali mbali kuhusiana na hali halisi ya soko la magazeti kwa sasa. Mwenyekiti wa wauza magazeti mjini Iringa Mashaka Kayoka amesema mbali ya kuwa baadhi ya magazeti yamekuwa yakiongoza kwa mauza na kuonekana kumalizika mapema katika vibanda vya magazeti ila asubuhi wakati wa kurudisha mabaki vijana hao wanaofanya kazi ya kutembeza magazeti wamekuwa wakirudisha mabaki ambayo kimsingi ni mabaki yanayotoka kwa wateja wao ambao hukodi kwa kiasi cha shilingi 100-200 kwa kila gazeti. Kayoka alisema kuwa hadi sasa wauza magazeti hao wameonekana kuyumba kiuchumi zaidi kutokana na kufungiwa kwa gazeti la Mwanahalisi ambalo lilikuwa ni gazeti maarufu ambalo kila wiki linapotoka huchukua nakala nyingi kati ya 100 hadi 200 na kumaliza mapema na hivyo kujipatia faida zaidi tofauti na magazeti mengine ya wiki. Alisema kuwa sasa baada ya mwanahalisi kufungiwa gazeti la wiki linaloongoza ni Raia mwema na kufuatiwa na Rai ,wakati magazeti ya kila siku yanaongoza kwa kuuzwa zaidi ni Mwananchi, Tanzania daima na Nipashe huku magazeti ya dini ,Jibu la Maisha, Nyakati ,Msemakweli huku gazeti la Kiongozi AN-Nuur na Kisiwa yakichuana katika soko. Mbali ya magazeti hayo alisema magazeti ya udaku (magazeti Pendwa ) kama Uwazi, Ijumaa na kiu kwa upande wa mauzo yamekuwa yakiungoza kwa kuuzwa nakala nyingi kuliko gazeti lolote nchini. Huku wadau mbali mbali akiwemo Salim Mbata alisema kuwa bei kubwa ya magazeti imechangia kwa upande wao kushindwa kununua magazeti na kuwa kwa sasa amekuwa akilazimika kusikiliza radio na kutazama Runginga na kama kuna gazeti ambalo amevutiwa ama halijasomwa katika vyombo hivyo vya habari ndilo hununua. Meneja wa vipindi katika kituo cha Radio Nuru Fm Paulina Kuye alisema kuwa kuendesha vipindi kwa njia ya magazeti kunawezesha radio kusikilizwa zaidi ikiwa ni pamoja na kupata wazo la habari kwa siku husika. Huku akidai kuwa kwa upande wao magazeti hayo ambayo huyatumia kuendesha vipindi wamekuwa wakinunua kwa pesa za ofisi kama walivyowateja wengine. Wakala wa magazeti ya Majira, Nipashe , Jamboleo , Habari leo mkoani Iringa Salm Zingilwa amesema kuwa soko la magazeti limekuwa likiyumba kutokana na habari zinazoandikwa kwa siku husika . Akitolea mfano Habari ya Kushambuliwa kwa mwenyekiti wa chama cha madaktari nchini Stivin Ulimboka na habari za bungeni na matukio makubwa katika Taifa pamoja na habari zinazohusu mkoa wa Iringa zimekuwa na wasomaji wengi zaidi . Alisema kwa upande wake kwa gazeti la Nipashe amekuwa akipokea nakala 140 na mabaki ni kati ya 30 na 35 wakati Majira hupokea nakala 100 mabaki huwa nakala 40 ,Jamboleo nakala 60 mabaki ni kati ya 20 au 25 huku Habari leo hupokea nakala 30 hubaki 5 na gazeti la kiu nakala 400 hubaki 50 Daily News huletwa nakala 50 mabaki ni nakala 10 Mwakilishi msaidizi wa mkoa wa Iringa kwa gazeti la Mwananchi Diana Kangusi alisema kuwa kati ya nakala 900 hadi 1000 mbazo huletwa mkoani Iringa mabaki huwa nakala 150 hadi 100 wakati gazeti la Citizen kati ya nakala 70 mabaki huwa ni 29 au 30 Wakati kwa gazeti la Kwanza jamii Iringa kwa mjibu wa mhariri gazeti hilo Greyson Mgoi amedai kuwa kati ya nakala 5000 mabaki ni nakala 1000 pekee.

WAZIRI MALIMA ASEMA SIKU ZA WACHAKACHUAJI WA PEMBEJEO ZA KILIMO ZINAHESABIKA

ASHANGAA KUONA MALIPO BADO MPAKA LEO,

ASEMA LAZIMA KITAELEWEKA MWAKA HUU.

Naibu Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika Mheshimiwa ADAM MALIMA ametangaza kuwa siku za watu wenye tabia ya kuchakachua Mbolea za Kilimo kwa wakulima kwa kuchanganya Simenti na Chumvi katika Mbolea hizo zinahesabika.
Mheshimiwa MALIMA ametangaza kauli hiyo leo jijini Dar es salam wakati akizungumza katika Kipindi cha Hello Tanzania kinachorushwa na Kituo cha Uhuru FM kila siku Asubuhi, huku akisema watu hao watafikishwa Mahakamani ili iwe fundisho kwa wengine.
Naibu Waziri huyo amesema kuhesabika kwa siku za watu hao inatokana na mpango wa serikali wa kumpa mamlaka zaidi Mthibiti wa Mbolea Nchini kuwakamata na kuwakuchukuliwa hatua kali za kisheria watu hao wanaorudisha nyuma maendeleo ya mkulima nchini.
Kazi ya Mthibiti huyo wa Mbolea Nchini ni kusimamia ipasavyo masuala yote ya mbolea na kuishauri serikali njia za kukomesha mtandao unaotumiwa na watu wasiowatakia mafanikio wakulima kwa kuwachakachulia Mbolea za mazao kwa manufaa yao binafsi.
Kuhusu suala la malipo ya Korosho kwa wakulima wa Tunduru, Rufiji na Mkurunga, Mheshimiwa MALIMA amewakata kuwa wavumilivu wakati serikali ikiendelea kufuatilia malipo hayo ambapo katika Wilaya ya Mkuranga tayari pesa za wakulima zimeshapelekwa na anashangaa ni kwa nini hawajalipwa bado.

SOKO LA MPANDA HOTELI LAENDELEA KUWA KATIKA HALI TATA,

Bidhaa za vyakula zaendelea kuuzwa chini hali inayotishia afya za walaji, Afisa afya wa Mji atupia lawama kwa wafanyabiashara wenyewe kutosikia maelekezo, jukumu lake la kusimamia sheria za afya aliweka pembeni, Blog yatia timu sokoni na kulamba picha hizi

 

 Afisa afya wa Mji wa Mpanda Paschal Kwea akifafanua hatua anazozichukua kukabiliana na uuziaji biadhaa chini sakafuni katika soko la Mpanda hoteli. MAJUKUMU YA KUKABILIANA NA UUZIAJI CHAKULA KATIKA MAZINGIRA MACHAFU NI YA AFISA AFYA WA ENEO HUSIKA

ZAWADI YA KATAVI KWA MKUU WA MKOA WA RUKWA.

 Mkuu wa mkoa wa Katavi, Dr Rajabu Rutengwe akimkabidhi zawadi ya Wanakatavi mkuu wa wilaya ya Kalambo mkoa wa Rukwa katika hafla ya wana Katavi jijini Mbeya
 
Msukuma mkokoteni akitafuta wateja wa maji katika mtaa wa Buzogwe mjini Mpanda katika mkoa wa Katavi kama alivyonaswa na kamera yetu, msimu wa kiangazi  huwa na soko zuri la maji kwa wauza maji hasa mjini Mpanda kutokana na uhaba wa maji kipindi hiki ambapo ndoo moja huuzwa kati ya shilingi 300-500.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akishiriki katika swala ya Magharibi kabla ya kushiriki katika futari aliyoandaliwa na wananchi wa Tanga jana Agosti 15, 2012 jijini Tanga. Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na Mkuu wa Wilaya ya Temeke Mhe Sophia Mjema katika uwanja wa ndege wa ,kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Agosti 16, 2012 muda mfupi kabla ya kuondoka kuekelea Msumbiji kuhudhuria mkutano wa SADC jijini Maputo. Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na Makamu wa Rais Dkt Mohamed Ghalib Bilali aliyemsindikiza katika uwanja wa ndege wa ,kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Agosti 16, 2012 muda mfupi kabla ya kuondoka kuekelea Msumbiji kuhudhuria mkutano wa SADC jijini Maputo Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na balozi mpya wa India hapa nchini Mhe Debnath Shaw baada ya kupokea hati zake za utambulisho leo Agosti 16, 2012 Ikulu jijini Dar es salaam

-->

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA MALIASILI NA UTALII
Description: nembo
TAARIFA KWA UMMA
KUUWAWA KWA JANGILI KATIKA PORI LA AKIBA BURIGI
Usiku wa tarehe 13 (kuamkia tarehe 14) Agosti 2012 mtu mmoja jangili ambaye jina halijapatikana aliuwawa katika Pori la Akiba la Burigi Mkoani Kagera baada ya mapambano kati ya genge la majangili na askari wa Wanyamapori waliokuwa wakifanya doria ndani ya pori hilo.
Siku hiyo mnamo saa 7 usiku askari wanyamapori walisikia milio ya risasi katika eneo la Nyungwe Kilomita 5 ndani ya Pori la Burigi. Askari walifika katika eneo la tukio maana walikuwa wakifanya doria karibu na eneo hilo na kukuta majangili ambao walikuwa wamemulika tochi zenye mwanga mkali.
Majangili walianza kurusha risasi walipobaini kuwa askari wamewakaribia. Askari Wanyamapori walijibu mapigo na mapigano hayo yaliendelea kwa muda wa takriban saa moja kabla ya majangili kukimbia.
Ilipofika saa moja asubuhi, wakati walipokuwa wanakagua eneo la tukio, askari wa Wanyamapori waligundua kuwepo kwa maiti akiwa na bunduki aina ya gobore na baruti. Askari Wanyamapori walitoa taarifa katika kituo cha Polisi Biharamulo ambapo Polisi waliuchukua mwili wa Marehemu na kuupeleka katika hospitali ya Biharamulo ambako mwili umehifadhiwa hadi sasa.
Hadi leo hakuna mtu aliyejitokeza kudai kupotelewa na ndugu. Hata hivyo uchunguzi wa awali umebaini kuwa marehemu huyo anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 20 hadi 28 anaweza akawa ni raia wa nchi jirani.
Uchunguzi unaendelea.
[MWISHO]
George Matiko
MSEMAJI
WIZARA YA MALIASILI NAUTALII
16th Agosti 2012

RAIS DKT. JAKAYA MRISHO KIKWETE AKIZINDUA AWAMU YA TATU YA MFUKO WA MAENDELEO YA JAMII (TASAF III)

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akizindua awamu ya tatu ya Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAFAIII) Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma leo Agosti 15, 20`12
-->
HOTUBA YA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, MHESHIMIWA DKT. JAKAYA MRISHO KIKWETE AKIZINDUA AWAMU YA TATU YA MFUKO WA MAENDELEO YA JAMII (TASAF III) UWANJA WA JAMHURI, DODOMA, 15 AGOSTI 2012
Mhe. Spika;
Mhe. Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar;
Mhe. Steven Wassira, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais - Uratibu na Mahusiano,;
Waheshimiwa Mawaziri;
Mhe. Daktari Rehema Nchimbi, Mheshimiwa Steven Wassira (Mb);
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma;,
Mheshimiwa Dr. Rehema Nchimbi;
Waheshimiwa Mawaziri na Wabunge;
Mhe. Katibu Mkuu Kiongozi;
Mwakilishi wa Benki ya Dunia: Tanzania, Uganda na Burundi,
Bwana Philippe Dongier;
Ndugu Peniel Lyimo, Mwenyekiti wa Kamati ya Taifa ya Uongozi wa TASAF;
Mwakilishi wa Benki ya Dunia;
Wawakilishi wa Ndugu Peniel Lyimo;
wWashirika wetu wangine wa mMaendeleo; ,
Waheshimiwa Viongozi wa Vyama vya Siasa;
Waheshimiwa Wabunge
Viongozi mbalimbali wa vyama vya siasa nawa Serikali;
Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF;
Wageni wWaalikwa;
Mabibi na Mabwana:;:
Shukrani
Ndugu Wananchi:
Namshukuru sana Mheshimiwa Waziri Steven Wassira na Nndugu Ladislaus Mwamanga, Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) na Kamati yake kwa kunialika nije kushiriki nanyi kwenye uzinduzi wa Awamu ya Tatu ya TASAF.Tarehe 30 Machi 2000 tulizindua Awamu ya Kwanza ya Mfuko wa Kwa kuwa huko tulipotoka tumepata mafanikio ya kutia moyo, naomba nianze kwa kutoa pongezi na kuwashukuru wote walioshiriki kufanikisha utekelezaji wa awamu mbili za TASAF zilizotangulia.
Pongezi
Ndugu Wananchi;
Napenda kuishukuru kwa dhati Benki ya Dunia na Mwakilishi Mkazi wa Benki hiyo wa wao hapa nchini kwa kushirikiana na sisi kutekeleza miradi mbalimbali ya TASAF tangu mwaka 2000. Siku zote Benki ya Dunia imekuwa mwenzetu muhimu na wa kutumainiwa na hii inasikiliza hoja zetu na kuzingatia vipaumbele vya sSerikali na wananchi wa Tanzania yetu katika jitihada zetu za kupambana na umaskini na kujiletea maendeleo. Tunafurahishwa sana na sera ya kusikiliza vipaumbele vyetu. Jambo hilo Hali hii ndiylo limetuwezesha sisi kushirikiana nao kubuni mpango huu wa TASAF unaofadhiliwa na ubia mzuri wa maendeleo kati yetu Serikali na Benki ya Dunia, , kwa kushirikiana na wadau wengine wa maendeleo, Serikali zetu mbili na wananchi wa nchi yetu.
Natoa ipongezai nyingi kwa sana Kamati ya Taifa ya Uongozi ya TASAF, chini ya uenyekiti imara wa Ndugu Peniel Lyimo, Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu, kwa uongozi wake thabiti wa kusimamia vizuri shughuli za TASAF. Aidha, nampongeza Katibu Mkuu, Afisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar kwa usimamizi wake thabiti. Hali kadhalika nNawapongeza pia viongozi na watendaji katika Halmashauri zote za Tanzania Bara , Afisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar kwa kazi nzuri waifanyayo ya usimamizi na utekelezaji wa miradi katika awamu iliyotangulia. Bila uongozi wao thabiti, mafanikio ya Awamu zya Kwanza na Pili yangekuwa ni ndoto. Kwa namna ya pekee nawapongeza wananchi wote walioitikia wito na kuchangia kwa hali na mali kufanikisha utekelezaji wa mpango huo wa kujiletea maendeleo yao wenyewe.
Nitakuwa mchoyo wa fadhila nisipoipongeza Kamati ya Dkt. Servacius Likwelile, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, kwa kazi nzuri ya kuandaa Awamu ya Tatu ya TASAF. Kazi hiyo wameifanya vizuri na kwa umakini mkubwa wahuku akikishirikiana na Bibi Ida Manjolo na wataalamu wengine wa Benki ya Dunia. Tunawashukuru sana.
Mabibi na Mabwana;
Kuna msemo wa Kiswahili usemao “ukiona vyaelea, ujue vimeundwa”. Na hivi ndivyo ilivyo kwa TASAF. Siri ya mafanikio yaliyopatikana katika utekelezaji wa Awamu ya Pili ni usimamizi mzuri unaofanywa na Menejimenti ya TASAF. Hivyo napenda kuchukua nafasi hii kuipongeza Menejimenti, Mkurugenzi Mtendaji, na wafanyakazi wote wa TASAF kwa kusimamia vizuri shughuli na miradi mbalimbali iliyotekelezwa katika Awamu ya Pili. Ni matumaini yangu kuwa mtafanya vizuri maradufu katika Awamu ya Tatu tunayoizindua leo.
Utekelezaji wa Awamu ya Pili ya TASAF
Ndugu Wananchi;
Utekelezaji wa Awamu ya Pili ya TASAF ulikuwa na mafanikio makubwa. Jumla ya miradi 11,572 imetekelezwa na kati ya hiyo, miradi 4,294 ilikuwa ya huduma za jamii; miradi 1,405 ya ujenzi na miradi 5,875 ya makundi maalum. Miradi hiyo imegharimiwa na serikali kwa kushirikiana na washirika wake wa maendeleo. Serikali imetoa Shillingi bilioni 32.2 na Benki ya Dunia ilitupatia mkopo wa masharti nafuu wa Shilingi bilioni 322. Washirika wetu wengine walituongezea nguvu kwa kuchangia Shillingi bilioni 72. Aidha, wananchi wametoa fedha, rasilimali na nguvu kazi ambazo thamani yake inakadiriwa kuwakwa ujumla ni zaidi ya Shilingi billioni 20.2.
Miradi ya Huduma
Miradi ya Huduma za Jamii imeongeza na/au kuboresha madarasa 5,485; ofisi za walimu 150; nyumba za walimu 152;, maabara kwenye shule za sekondari 157; majengo ya utawala katika shule za sekondari 20; mabweni ya wanafunzi 163; vyoo vya wanafunzi 705; madawati 22,946, viti 5,483, meza 4,354; vituo vya afya 63; zahanati 606, nyumba za watumishi wa zahanati 301, vyoo kwenye zahanati 339, vichomea taka 182; vituo vya maji 2,198, visima virefu 192, visima vifupi 335 na matanki ya maji 205.
Miradi ya Ujenzi
Miradi ya ujenzi, yenyewe imeongeza au kuboresha barabara za vijijini 825; mabwawa madogo 78; mifumo midogo ya umwagiliaji 289; mifumo ya kuondoa maji ya mvua barabarani mita 4,593; maghala ya kuhifadhia nafaka 113; masoko 80; makaravati 901; madaraja ya watembea kwa miguu 64; na, miradi ya mazingira 608 yenye walengwa 566,938.
Makundi Maalum
Na miradi ya makundi maalum imetoa huduma kwa yatima 32,113; wajane 15,205; wazee 17,961; watu wenye ulemavu 7,840; watu wanaoishi na virusi vya UKIMWI 52,316; na vijana wasio na ajira 36,859. Vilevile, watu 2,083 wamehamasishwa kujikinga na ugonjwa wa UKIMWI.
Mabibi na Mabwana;
Mafanikio ya utekelezaji wa Awamu ya Pili ya TASAF hayakuishia hapo. Vikundi 1,778 vyenye wanachama 22,712 vimeundwa kupitia Mpango wa Kuweka Akiba na Kuwekeza (COMSIP ) katika Halmashauri 44 zilizopo Tanzania Bara, Unguja na Pemba. Walengwa wote wamepatiwa mafunzo ya kuendesha vikundi vyao kwa ufanisi pamoja na vifaa. Vilevile, mafunzo ya usimamizi, utekelezaji bora wa miradi na fani mbalimbali katika ngazi ya vijiji, wilaya na taifa yametolewa kwa walengwa 27,373.
Serikali kupitia TASAF imefanikiwa pia kutekeleza Programu ya Kijamii ya Uhawilishaji Fedha kwa Kaya Maskini kwa majaribio katika Wilaya za Bagamoyo, Kibaha na Chamwino. Walengwa zaidi ya 13,000 kutoka kaya 6,000 maskini na zilizo katika mazingira hatarishi zilipatiwa ruzuku ya jumla ya shillingi bilioni moja na nusu. Kaya hizo zimejengewa uwezo na watoto sasa wanapelekwa kwenye zahanati na vituo vya afya kwa ajili ya chanjo na kufuatiliwa maendeleo yao.
Aidha, watoto 1,638 ambao hawakuweza kwenda shule kwa sababu ya umasikini sasa wameandikishwa na wanakwenda shule. Kati ya wanafunzi hao, 392 wamefaulu kwenda shule za sekondari za kata. Vile vile wazee 4,956 wamewezeshwa kupata huduma za afya na baadhi yao wamejiunga na bima ya afya ili kupata huduma kwa urahisi na uhakika zaidi. Kufuatia mafanikio ya haraka ya programu hii, sasa maandalizi yanafanyika ili isambazwe kwenye Halmashauri zote katika utekelezaji wa Awamu ya Tatu ya TASAF.
Ndugu Wananchi;
Inafurahisha kuona jinsi suala la jinsia lilivyozingatiwa katika utekelezaji wa programu na miradi ya TASAF. Wanaume na wanawake walishirikishwa sawa sawa katika hatua zote za utekelezaji wa miradi yao. Idadi ya wanawake katika kamati ya mradi ilipangwa makusudi ili isipungue asilimia 50 ya jumla ya wajumbe, na idadi ya walengwa wanawake katika miradi ya ujenzi nayo isipungue asilimia 50. Bahati nzuri akina mama waliokuwa wajumbe kwenye Kamati mbalimbali wameonesha uwezo mkubwa wa uongozi. Naomba ushirikishwaji huu uendelee kuimarishwa na akina mama wajitokeze kwa wingi kushiriki katika usimamizi wa miradi ya TASAF ya Awamu ya Tatu.
Ni wazi kuwa siri ya mafanikio ya Awamu ya Pili ya TASAF ni ushiriki mzuri wa wananchi, utayari wao wa kumiliki maendeleo yao wenyewe na moyo wa kujituma kwao pamoja na uongozi na usimamizi mzuri wa miradi katika ngazi zote.
Changamoto Katika Utekelezaji wa Awamu ya Pili
Maendeleo ya Jamii (TASAF I) kule Mwanhuzi, Wilayani Meatu, Mkoa wa Shinyanga.
Vile vile tarehe 23 Mei 2005, tulizindua Awamu ya Pili ya Mfuko huu (TASAF II ) kule Wilayani Magu, Mkoa wa Mwanza.
Leo hii ninayo furaha kubwa kuja hapa Dodoma kuzindua Awamu ya Tatu ya Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF III).
Tunazindua Awamu ya Tatu ya Mfuko wa Maendeleo ya Jamii kwa kuwa Awamu ya Kwanza na ya Pili zimetekelezwa kwa mafanikio makubwa. Hivyo basi, naanza kwa kutoa shukurani na pongezi zangu za dhati kwa wote walioshiriki kufanikisha Awamu mbili zilizotangulia na walioshiriki kuandaa Awamu hii ya Tatu.
Naishukuru Benki ya Dunia na ninamshukuru Mkurugenzi Mwakilishi wa Benki hii kwa nchi za Tanzania, Uganda na Burundi, Bw. Philippe Dongier. Kwa hakika Bw. Dongier anaiwakilisha vyema Benki ya Dunia ambayo siku zote inasikiliza hoja na kuzingatia vipaumbele vya vita dhidi ya umaskini vinavyowekwa na Serikali yetu. Mfano halisi ni Mfuko huu wa Maendeleo ya Jamii - TASAF. Kwa usikivu huo, tumebuni ubia mzuri wa maendeleo kati ya Serikali yetu, Benki ya Dunia, Wadau wengine wa Maendeleo na Wananchi.
Napenda pia, kuwashukuru washirika wengine wa maendeleo ambao wanashiriki Awamu hii ya Tatu ya TASAF hususan Serikali ya Uingereza kupitia Idara yake ya Maendeleo ya Kimataifa (DFID), Serikali ya Hispania na Serikali ya Watu wa Marekani kupitia Shirika lake la Maendeleo ya Kimataifa (USAID).
Ninawashukuru Wataalam wa Benki ya Dunia na Washirika wengine wa Maendeleo wakiongozwa na Bibi Ida Manjolo ambao walishirikiana nasi kwa karibu katika utekelezaji wa Awamu ya Pili ya TASAF na kuandaa Awamu ya Tatu.
Naipongeza pia Kamati ya Taifa ya Uongozi ya TASAF ambayo mwenyekiti wake ni Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu, Ndugu Peniel M. Lyimo, pamoja na Kamati ya Maandalizi ya Awamu ya Tatu ya TASAF iliyoongozwa na Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Fedha, Dkt. Servacius B. Likwelile, kwa kazi nzuri.
Nawapongeza Viongozi na Watendaji katika Halmashauri zote za Tanzania Bara, Afisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar na wananchi wote kwa jumla kwa usimamizi na utekelezaji wa miradi ya jamii katika awamu zote mbili zilizotangulia. Wananchi wote waliitikia kwa moyo mkunjufu na ari kubwa kupokea mawazo ya Serikali katika utekelezaji wa mpango huo wa kujiletea maendeleo yao wenyewe.
Naipongeza pia Menejimenti ya TASAF, ikiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji, Ndugu Ladislaus J. Mwamanga na wasaidizi wake. Nina imani kuwa wataendelea kufanya kazi nzuri katika Awamu hii ya Tatu.
Tangu mwaka 2000 TASAF imekuwa ni kichocheo katika jitihada za wananchi kujiletea maendeleo. TASAF haina miradi; miradi ni ya wananchi. Inachokifanya TASAF ni kuwawezesha tu wananchi kutekeleza vipaumbele vyao vya maendeleo.
Awamu ya Pili ya TASAF iligharimiwa kwa kiasi kikubwa na mkopo wa masharti nafuu kutoka Benki ya Dunia. Mkopo huo ni kiasi cha Shilingi 322 bilioni sawa na Dola za Kimarekani 215 milioni. Vilevile kwa utekelezaji mzuri wa TASAF, kumekuwa na Wahisani na Miradi mingine kupitishia fedha TASAF zenye jumla ya shilling 72 bilioni sawa na Dola za Kimarekani 45 milioni. Mchango wa Serikali yetu ulikuwa ni Shilingi 32.2 bilioni, na wananchi walichangia fedha rasilimali na nguvu kazi ambazo thamani yake ilifikia zaidi ya Shilingi 20.2 bilioni.
Ndugu Wananchi
Ushiriki wa wananchi, utayari wao wa kumiliki maendeleo yao na kujituma kwao pamoja na uongozi na usimamizi mzuri wa kitaifa na halmashauri husika ndio msingi wa mafanikio ya Awamu ya Pili ya TASAF.
Mafanikio hayo ni pamoja na :-
1.Jumla ya miradi 11,572 ilipitishwa na kupewa fedha; miradi 4,294 ikiwa ya Huduma za Jamii, miradi 1,405 ya Ujenzi na miradi 5,875 ni ya Makundi Maalum.
2.Miradi ya Huduma za Jamii imeongeza na/au kuboresha madarasa 5,485, ofisi za walimu 150, nyumba za walimu 152, maabara kwenye shule za sekondari 157, majengo ya utawala katika shule za sekondari 209, mabweni ya wanafunzi 163, vyoo vya wanafunzi 705, madawati 22,946, viti 5,483, meza 4,354; zahanati 606, vituo vya afya 63, nyumba za watumishi wa zahanati 301, vyoo kwenye zahanati 339, vichomea taka 182; vituo vya maji 2,198, visima virefu 192, visima vifupi 335 na matanki ya maji 205.
3.Miradi ya ujenzi imeongeza au kuboresha barabara za vijijini 825, mabwawa madogo 78, na mifumo ya kuondoa maji ya mvua barabarani mita 4,593, maghala ya kuhifadhia nafaka 113, masoko 80, mifumo midogo ya umwagiliaji 289, makaravati 901, miradi ya mazingira 608 yenye walengwa 566,938 na madaraja ya watembea kwa miguu 64.
4.Miradi ya makundi maalum imetoa huduma kwa yatima 32,113, wajane 15,205, wazee 17,961, watu wenye ulemavu 7,840, watu wanaoishi na virusi vya UKIMWI 52,316 na vijana wasio na ajira 36,859. Vilevile, uhamasishaji juu ya kudhibiti UKIMWI umetolewa kwa watu 2,083.
5.Vikundi 1,778 vyenye wanachama 22,712 vimeundwa kupitia Mpango wa Kuweka Akiba na Kuwekeza (COMSIP ) katika Halmashauri 44 na Unguja na PembaWalengwa wote wamepatiwa mafunzo ya kuendesha vikundi vyao kwa ufanisi pamoja na vifaa.
6.Mafunzo ya usimamizi, utekelezaji bora wa miradi na fani mbalimbali katika ngazi ya vijiji, wilaya na taifa yametolewa kwa walengwa mbalimbali 27,373.
Ndugu wananchi,
7.Serikali pia kupitia Awamu ya Pili ya TASAF imefanikiwa kutekeleza Programu ya Kijamii ya Uhawilishaji Fedha kwa Kaya Maskini kwa majaribio katika Wilaya za Bagamoyo, Kibaha na Chamwino. Walengwa zaidi ya 13,000 kutoka kaya 6,000 maskini na zilizo katika mazingira hatarishi zilipatiwa ruzuku ya jumla ya shillingi bilioni moja na nusu (Sh. 1,500,000,000). Kaya hizo zimejengewa uwezo na watoto ambao ndiyo walengwa wanapelekwa kwenye zahanati na vituo vya afya kwa ajili ya chanjo na kufuatilia maendeleo yao.
8.Aidha, watoto 1,638 ambao hawakuweza kwenda shule sababu ya umasikini sasa wameandikishwa na wanakwenda shule. Kati ya wanafunzi hao 392 wamefaulu kwenda shule za sekondari za kata. Vile vile wazee 4,956 ambao ni walengwa wamewezeshwa kupata huduma za afya. Pia Kaya za walengwa zimejiunga na mpango wa bima ya afya ili kupata huduma kwa urahisi na uhakika zaidi.
9.Programu hii imekuwa na mchango mkubwa katika kuboresha hali ya maisha ya kaya za walengwa kwa muda mfupi sana. Mafanikio yake yamefanya sasa programu hii kusambazwa kwenye Halmashauri zote katika utekelezaji wa TASAF Awamu ya Tatu. Haya yote yasingewezekana bila ninyi wananchi kukubali kwa pamoja kushiriki katika kurekebisha hali ya uchumi wetu, kwa kuwa muhimili mkuuwa maendeleo katika ngazi ya jamii.
Ndugu wananchi,
Kwa kuwa TASAF imepanua uwigo wa kuwafikia walengwa masikini katika makundi mbalimbali ndani ya Tanzania Bara na Zanzibar na uzoevu wao wa zaidi ya miaka kumi na mbili; ni dhahili kuwa ni chombo pekee cha serikali chenye uwezo wa kutekeleza vizuri Mpango wa Kitaifa wa Kinga ya Jamii ( National Social Protection Framework)
Awamu ya Pili ya TASAF imeimarisha uwajibikaji katika ngazi zote kwa kuhakikisha kuwa fedha zote zilizotengwa kwa ajili ya utekelezaji wa shughuli mbalimbali zinatolewa taarifa na wadau wote wanajulishwa mapato na matumizi yake. Kamati za usimamizi wa miradi ziliwajibika kutoa taarifa za utekelezaji hatua kwa hatua na matumizi ya fedha.
Suala la jinsia katika utekelezaji wa miradi lilizingatiwa, na kuonekana wazi kuwa ni jambo la haki na la manufaa kila palipokuwa na mradi unaochangiwa na TASAF. Wanaume na wanawake walishirikishwa sawa sawa katika hatua zote za utekelezaji wa miradi yao. Idadi ya wanawake katika kamati ya mradi ilipangwa kwa makusudi isipungue asilimia 50 ya jumla ya wajumbe, na idadi ya walengwa wanawake katika miradi ya ujenzi nayo isipungue asilimia 50. Lengo ni kuhakikisha kuwa kipato kisichopungua asilimia 50 kinaelekezwa kwa walengwa ambao ni wanawake. Matumaini yangu ni kuwa uwezo waliouonyesha wanawake waliokuwa kwenye kamati hizi utawasukuma wengi wao kuomba uongozi katika ngazi mbalimbali.
Ndugu wananchi;
Pamoja na mafanikio hayo ya kutia moyo, Wakati wa utekelezaji wa Awamu ya Pili ulikabiliwa na changamoto ya TASAF kumekuwepo na changamoto mbalilmbali. Changamoto hizo ni pamoja na uhaba wa fedha kutokutosheleza kukidhi wezo wa Mfuko kutokidhi mmahitaji ya wananchi; uwezo mdogo wa kusimamia miradi katika ngazi mbalimbali za uongozi; na ya wananchi ambayo ni mengi, ukosefu wa huduma kwenye baadhi ya vituo vya kutolea huduma kama zahuhaba wa watumishi katika vituo vya kutoa huduma. Bahati nzuri serikali na uongozi wa TASAF unazitambua changamoto hizo na tumejipanga vizuri kukabiliana nazo katika Awamu hii ya Tatu tunayoizindua leo.
Awamu ya Tatu ya TASAF
anati, vituo vya afya na masoko vilivyotokana na miradi kutokana na sababu mbalimbali kama vile uhaba wa watumishi.
Changamoto nyingine ni pamoja uhaba wa fedha za utekelezaji wa shughuli za kujenga uwezo, wigo mdogo wa utekelezaji wa jitihada nyingine, kama vile Mpango wa Jamii wa Uhawilishaji Fedha kwa Kaya Maskini, Mpango wa Jamii wa Kuweka Akiba na Kuwekeza, uansishwaji wa Taasisi za Maendeleo ya Jamii katika sehemu za mijini.
Kadhalika ilijitokeza changamoto ambapo baadhi ya wanasiasa walipotosha dhana ya kuanzishwa kwa TASAF na pia kutokuwepo mfumo wa uendelevu thabiti wa kutekeleza TASAF kwa kutegemea rasilimali za ndani.
Mabibi na Mabwana;Ndugu wananchi
Kufuatia mafanikio katika utekelezaji wa Awamu mbili zilizotangulia na pia katika kukabiliana na changamoto zake, Serikali imeamua kuanzisha Awamu ya Tatu ya TASAF itatekelezwa kwa miaka kumi, katika vipindi viwili vya miaka mitano mitano. ambapo Muondo wake umezingatia kupata ufumbuzi wa chanamoto zilizopatikana na hivyo ambayo itatekelezwa katika kipindi cha miaka kumi nchi nzima kwa Awamu mbili za miaka mitano mitano.
Tunategemea
Awamu hii ya Tatu ya TASAF itatoa mchango mkubwa katika kufikia nalenga kuchangania kufikiwa malengo yetu yaliyomo kwenye ya D Dira ya Maendeleo ya Taifa 2025, Mpango wa Maendeleo wa Miaka Mitano, Mkakati wa Pili wa Kukuza Uchumi na Kupunguza Umaskini (MKUKUTA II) na Mkakati wa Pili wa Kukuza Uchumi Kukuza Uchumi na Kupunguza Umaskini Zanzibar (MKUZA II) na Mpango wa Mpango wa Maendeleo wa Miaka Mita. Tutaweka mkazo zaidi katika miradi ya huduma za elimu, afya na maji nay a kuondoa umaskini wa kipato. no kwa kuwekeza katika kuendeleza rasilimali watu miongoni mwa kaya maskini na zilizo katika mazingira hatarishi. Kupitia utekelezaji wa Awamu ya Tatu ya TASAF tunatarajiainatarajiwa kuwa kaya nyingimaskini maskini zitapiga hatua na kutoka kwenyekuanza kutoka katika umaskini namaisha ya utegemezi. hatimaye kuwa na mchango katika kukuza uchumi na kuondokana na utegemezi.
Ili kutekeleza miradi ya Awamu ya Tatu ya TASAF, jumla ya Shilingi bilioni 408 zitahitajika. Fedha hizo zitatolewa na serikali yetu, Benki ya Dunia na washirika wengine wa maendeleo. Serikali itatoa Shillingi bilioni 45; Benki ya Dunia itachangia Shillingi bilioni 330; Hispania itatoa Shillingi bilioni 9; Uingereza Shillingi bilioni 24; na Marekani Shillingi bilioni 1.4. Kama ilivyokuwa kwa Awamu zilizotangulia, tunawategemea sana wananchi kutuunga mkono na kuchangia kwa hali na mali. Mafanikio ya Awamu hii yatategemea sana mchango wa wananchi katika maeneo husika.
Ahadi na Wito kwa Wananchi
Ndugu wananchi;
Tunapenda kuahidi kuwa tutaendelea kushirikiana na wananchi wote ambao wanaonesha dhamira ya dhati ya kupambana na umaskini na kujiongezea
Kwa ushirikiano wenu wananchi, TASAF imetekelezwa vizuri sana na matunda yake yapo wazi, na kwa vile mmeendelea kuiunga mkono Serikali yenu ya CCM katika kutekeleza Mwelekeo wa Sera zake za Miaka mitano (2010-2015) zinazohimiza mageuzi ya kiuchumi na uwezeshaji wananchi, serikali imetenga fedha tena na kupata mkopo wa masharti nafuu kutoka Benki ya Dunia na washirika wengine wa maendeleo ili kutekeleza Awamu ya Tatu ya TASAF.
Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya Dunia iliridhia na kupitisha utekelezaji wa Awamu ya Tatu ya TASAF tarehe 29 Machi, 2012. Mkataba kati ya Benki ya Dunia na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ulisainiwa tarehe 15 Juni 2012. Na idhini ya kuanza kutumia fedha hizo tayari imeshatolewa.
Awamu ya Tatu ya TASAF inatarajiwa kugharimu Shilingi 408 Bilioni sawa na Dola za Kimarekani 272 Milioni kwa mchanganuo ufuatao:
1.Benki ya Dunia itachangia shilingi 330 bilioni (USD 220 milioni),
2.Serikali ya Hispania itachangia Shilingi 9 bilioni (USD 6 milioni)
3.Serikali ya Uingereza kwa kupitia Idara ya Serikali ya Uingereza ya Maendeleo ya Kimataifa(DFID) itachangia Shilingi 24 bilioni (USD 16 milioni)
4.Serikali ya Watu wa Marekani kupitia Shirika la Marekani la Maendeleo ya Kimataifa (USAID) itachangia Shillingi 1.44 bilioni ( USD 900,000)
5.Serikali ya Tanzania itachangia sh.45 bilioni (USD 30 milioni)
Ndugu wananchi
Utekelezaji wa Awamu ya Tatu ya TASAF unategemewa kuwa na changamoto zifuatazo:
1.Upatikanaji wa raslimali fedha za kukidhi mahitaji halisi ya walengwa. Jitihada za kupata rasilimali zaidi ziendelee na Wadau wa Maendeleo watoe ushirikiano zaidi hasa wale ambao wameonyesha nia ya kushiriki katika kuchangia mfuko huu.
2.Kujenga uwezo mapema wa kusimamia na kutekeleza kwa wakati uhawilishaji wa fedha kwa walengwa. Mpango wa kujenga uwezo wa watekelezaji katika ngazi mbalimbali upewe kipaumbele. Ufuatiliaji na tathmini vifanyike ili kubaini mapungufu mapema iwezekanavyo.
3.Uwezo wa kusimamia utekelezaji miradi kwa ufanisi na kwa wakati. Ngazi zote zinazohusika na utekelezaji zishiriki kikamilifu katika kuhakikisha usimamizi wa utekelezaji unafanyika ipasavyo. Aidha, utekelezaji ufanyike kwa awamu kuzingatia uwezo unavyojengwa.
4.Kusimamia uendelevu wa rasilimali na vituo vya kutolea huduma vilivyotokana na miradi iliyotekelezwa na wananchi. Wataalamu kutoka halmashauri husika na Viongozi katika maeneo ya utekelezaji wawezesha jamii kuwa na mipango endelevu ya uendeshaji.
5.Usimamizi wa fedha zitakazotolewa kutekeleza miradi inayochangiwa na TASAF utahitaji uwepo wa udhibiti mkubwa katika ngazi zote. Kazi hiyo nayo ifanywe kuanzia sasa na kwa kipindi chote cha utekelezaji.
Ndugu wananchi,
Leo tunapozindua Awamu ya Tatu ya TASAF napenda tujikumbushe kuwa historia yetu ya vita dhidi ya umaskini imetufundisha mambo kadhaa:
Kwanza, sera nzuri, mipango mizuri na nia njema peke yake havileti
maendeleo.
Pili, fedha za Serikali, mikopo au wahisani peke yake hazileti
maendeleo.
Tatu, ipo tofauti kubwa kati ya kutamani maendeleo na kuwa tayari
kutoka jasho kutafuta maendeleo.
Baada ya miaka 50 ya Uhuru sasa nadhani tumeelewa kunahitajika nini ili maendeleo yaje kwa kasi ya kutosha kuweza kupunguza na hatimaye kuondoa umaskini kabisa.
Hatua ya kwanza ya maendeleo ni mtu kutoridhika na hali duni ya maisha yake; ni kujenga tamaa na wivu wa maendeleo na kuchukia hali ya umaskini.
Hatua ya pili ni mtu kuamua kwa dhati kutafuta maendeleo kwa jasho
lake, na inapobidi kwa kushirikiana na wenzake wanaochukia umaskini kama yeye.
Hatua ya tatu ni mtu kupima uwezo alionao – uwezo wa fedha na wa mali nyingine; uwezo wa akili na maarifa; na uwezo wa nguvu za kufanya kazi na kubuni mbinu za kutumia ili kuboresha hali yake ya maisha na hali ya jamii yake kwa ujumla.
Hatua ya nne ni kutekeleza kwa kadri ya uwezo wake mbinu za maendeleo alizozibuni, au zilizobuniwa na jamii yake.
Hatua ya tano ni kuomba msaada kwa yale mambo yaliyo nje ya uwezo wake, ikiwemo msaada wa fedha, msaada wa vifaa, au msaada wa elimu na utaalamu.
Mfuko huu wa Kuongeza Uwezo wa Wananchi katika Maendeleo ni jitihada nyingine ya Serikali kuwasaidia wale wananchi ambao wamepitia hatua zote hizo za kutafuta maendeleo, yaani tayari wameonyesha chuki yao dhidi ya umaskini, wameamua kwa dhati kuondokana na umaskini kwa kuongeza kkipato chao. Kipato cha mtu kinapoongezeka watoto wake watahudhuria masomo na kupata huduma bora za afya. Wazee na akina mama nao watapata huduma bora za afya. Lakini kipato hakiwezi kuongezeka kama mtu hataki kufanya kazi, hataki maendeleo, na hataki kujishughulisha na kitu chochote. Maisha bora kwa kila mMtanzania yatapatikana kama tutafanya kazi kwa bidii na maarifa. Inawezekana, kila mtu atimize wajibu wake.
kaya ili watoto wahudhurie masomo na kwenda kliniki kupata chanjo na huduma zingine za afya. Vile vile ongezeko la kipato litawezesha akina mama wajawazito na wazee kupata huduma zote muhimu za afya.
Hivyo ndugu zangu natoa wito kwa wananchi wote watumie vizuri fursa hii murua ya TASAF. Tushirikiane na uongozi wa TASAF kubuni miradi itakayotuletea maendeleo ya haraka, miradi itakayoboresha huduma za jamii. Tushirikiane nao kusimamia utekelezaji wa miradi hiyo. Tuhakikishe kuwa tunafuata maelekezo ya wataalam na viongozi wetu katika ngazi mbalimbali. Tuwafichue wabadhirifu wa fedha za miradi ya TASAF na wale wote wanaotumia vibaya rasilimali za miradi. Daima tukumbuke kuwa miradi hii ni kwa ajili yetu sisi pamoja na watoto wetu, ndugu zetu na jamaa zetu. Tukifanya hivi nina imani tutakuwa na msingi imara wa kujenga taifa linaloendelea na hatimaye kushinda vita dhidi ya adui watatu wa maendeleo: umaskini, njaa na magonjwa.
Rai kwa Washirika wa Maendeleo na Viongozi wa TASAF
Mabibi na Mabwana;
Natumaini washirika wetu wa maendeleo wataendelea kuunga mkono juhudi zetu hizi za kuondoa maadui watatu wa maendeleo. Wamekuwa wakifanya hivyo tangu tulipoanzisha Mfuko huu wa TASAF na nina imani wataendelea. Msaada wao utasaidia sana kufikia malengo yetu tuliyojiwekea katika utekelezaji wa Awamu hii.
Nawaomba pia viongozi wa TASAF, Kamati ya Taifa ya Uongozi, Menejimenti na Mkurugenzi Mtendaji waongeze ufanisi na maarifa katika utendaji wao. Waongeze usimamizi wa fedha na rasilimali, wajenge uwezo wa kusimamia utekelezaji wa miradi katika ngazi mbalimbali, na wabuni vyanzo vingine vya kupata fedha za kuendeleza miradi. Naamini wataweza.
Mwisho
Mheshimiwa Waziri;
Wageni waalikwa;
Mabibi na Mabwana;
Kabla ya kumaliza hotuba yangu naomba nitoe shukrani za dhati kwa Mhe. Benjamin William Mkapa, Rais wa Awamu ya Tatu kwa kubuni wazo hili jema ambalo manufaa yake tunayaona. Baada ya kusema hayo, sasa nipo tayari kufanya kazi iliyonileta hapa Nazindua Awamu ya Tatu ya Mfuko wa Maendeleo ya Jamii kwa matumaini makubwa kuwawamba sasa Watanzania sasa tumeupata ufunguo wa maendeleo yetu sote. Napenda kutamka kwamba Awamu ya Tatu ya Mfuko wa Maendeleo ya Jamii, (TASAF) umezinduliwa rasmi leo. Nawatakia kila la heri na mafanikio katika utekelezaji wake.
Asanteni sana kwa kunisikiliza.kwa kutumia fursa ambazo mageuzi ya uchumi, na usimamizi bora wa uchumi, umeweka mbele yetu.
Kwa pamoja tutafanya mengi. Na kwa mradi huu wa TASAF, ukichanganywa na miradi mingine, na utaratibu huu wa kushirikisha wananchi katika shughuli za kupunguza umasikini, ninaamini Watanzania wote tutakuwa na msingi imara wa kujenga taifa linaloendelea na hatimaye kushinda vita dhidi ya umaskini.
Na sasa natangaza kuwa nimezindua rasmi Awamu ya Tatu ya Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF III).
Ahsanteni sana kwa kunisikiliza.

UMRI WAWATOA JASHO WAGOMBEA WA UVCCM MKOA WA IRINGA

Kamanda wa UVCCM mkoa wa Iringa Salim Abri Asas akiwaomba wajumbe wa kikao cha mapendekezo ya majina ya wagombea kutenda haki katika kupendekeza majina Mwanahabari na Mwanachama wa UVCCM Bi Tumain Msowoya ambaye ni mgombea nafasi ya kiti UVCCM mkoa wa Iringa
Mwanachama Geofrey Lukuvi anayegombea baraza kuu la UVCCM mkoa wa Iringa
Mwanachama Fauzia Jemedari anayegombea kiti
Mwanachama Gaudence Kabwabwalika anayegombea baraza kuu la UVCCM mkoa
Hawa ndio wagombea wa nafai ya UVCCM na ndio vijana wenyewe wa CCM SAKATA la kashfa nzito kwa wana chama wa umoja wa vijana wa chama cha mapinduzi (UVCCM) mkoa wa Iringa kutuhumiwa kudanganya umri wao wa kuzaliwa limechukua sura mpya baada ya idadi kubwa ya vijana waliojaza fomu za kuomba nafasi mbali mbali katika UVCCM kukimbia kikao cha usaili kwa wagombea hao. Huku kamanda wa umoja wa UVCCM mkoa wa Iringa Salim Abri Asas na katibu wa CCM mkoa wa Iringa Emmanuel Mteming'ombe wakipigilia msumari kwa kutaka haki itendeke katika kuchuja majina ya wagombea wa nafasi mbali mbali bila kuwepo upendeleo wowote na wale waliochakachua miaka kuwajibishwa . Hatua hiyo imekuja baada ya mtandao huu kuibua siri nzito ya robo tatu ya vijana hao kujaza umri wa uongo ikiwa ni pamoja na kurudisha nyuma miaka ya kuzaliwa ili iweze kuendena na kanuni ya UVCCM inayomtaka mgombea kuanzia miaka 14-30. Uchunguzi uliofanywa na mtandao huu juzi wakati wa kikao cha mapendekezo ya majina ya wagombea wa nafasi mbali mbali ndani ya UVCCM mkoa wa Iringa kikao kilichofanyika katika ukumbi wa CCM mkoa wa Iringa chini ya mgeni rasmi kamanda wa UVCCM mkoa wa Iringa Salim Abri Asas. Sehemu kubwa ya wanachama hao walioojaza fomu hizo kushindwa kutokea katika kikao hicho nyeti cha kuhakiki taarifa walizojaza katika fomu zao za kuomba nafasi mbali mbali. Taarifa kutoka ndani ya kikao hicho ambazo zimethibitishwa na baadhi ya wanachama zinadai kuwa walioshindwa kutokea katika kikao hicho ni baadhi ya wale wanaodaiwa kufanya uchakachuaji wa umri katika zoezi la ujazaji wa fomu hizo.

Bodi ya Mikopo, TCU yawaengua 3074 walioomba

BODI ya Mikopo ya Elimu ya Juu nchini pamoja na Tume ya Vyuo Vikuu nchini (TCU) imewaengua zaidi ya wanafunzi 3074 walioomba vyuo na mikopo ya elimu ya juu kwa mwaka 2012/13.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na taasisi hizo kupitia mitandao yao (website) Agosti 10 na 12, 2012 zaidi ya wanafunzi 3074 wameenguliwa katika maombi yao kwa kuwa na dosari mbalimbali.
Taarifa hiyo imeeleza kuwa Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu (HESLB) pekee imeorodhesha zaidi ya wanafunzi 2,649 ambao imebaini kuwa na mapungufu kadhaa katika maombi yao ya kupewa mikopo ya vyuo.
Miongoni mwa makosa ama dosari ambazo bodi imezibaini kwa walioenguliwa kwa sasa ni pamoja kukosekana kwa vyeti vya kuzaliwa kwa muombaji, sahihi ya mdhamini/muombaji, kukosekana kwa picha ndogo ya muombaji/mdhamini, kukosekana kwa sahihi za viongozi wa Serikali za mitaa/vijiji kwa waombaji na nyaraka nyingine muhimu kwa waombaji.
Kwa upande wake TCU imewaengua jumla ya waombaji 425 kwa dosari na makosa mbalimbali, ambayo imeyabainisha katika taarifa yake.
Miongoni mwa dosari ambazo zimetajwa na TCU kwa wanafunzi hao ni pamoja na baadhi yao kukosea namba za vyeti vya masomo kwa vidato vya nne na tano (O' level na A' level Index number), miaka ya kumaliza masomo (year of completion), mawasiliano sahihi kwa muombaji (Contact information e.g. Mobile phone number, email address and postal address) pamoja na uchaguzi wa masomo (Programme selected).
Hata hivyo taasisi hizo mbili zimetoa muda kwa walioenguliwa sasa kutokana na dosari hizo kurekebisha na kutuma tena maombi yao kupitia mitandao kwa mujibu wa maelekezo waliyotoa. Kwa taarifa zaidi pia waweza kutembelea mitandao ya www.heslb.go.tz na www.tcu.go.tz

  JE? WAJUA SHERIA YA TAKWIMU NA ADHABU YAKE KWA KUKWAMISHA ZOEZI LA SENSA ?

Rais Dkt Jakaya Kikwete akipitia majarida yanayozungumzia masuala ya sheria wakati wa siku ya mahakama nchini
SHERIAYA TAKWIMU, SURA 351(THE STATTISTICS ACR, CAP.351
1.0 Utangulizi
Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) ni Wakala wa Serikali yenye mamlaka ya kisheria ya kutoa takwimu rasmi nchini.
2.0 Mjukumu ya Ofisi ya Taifa ya Takwimu yameainishwa katika Sheria yaTakwimu, 2002 (Na.1, 2002). Miongoni mwa majukumu hayo ni kuendelesha zoezi la Sensa ya Watu na Makazi katika Jamhuri ya Mungano wa Tanzania(To conduct population and Housing Census in the United Republic). Kifungu cha 5(1)(a) cha Sheria ya Takwimu, 2002.
Aidha , Sheria hiyo inaelekeza kuwa katika kutekeleza majukumu ya kitakwimu ambayo yanaihusisha Tanzania na Zanzibar, NBS itashirikiana na Ofisi ya Mtakwimu Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi ya, Zanzibar (Office oa Chief Gornment Statatician-OCGS). Kifungu cha 5(2) cha Sheria ya Takwimu, 2002.
3.0 Kiapo cha kutunza siri(Oath of secrecy)
Shughuli za NBS ni za kipekee kwa kuwa zinahusu ukusanywaji wa taarifa zinazohusu maisha ya mtu binafsi. Kwa mantiki hiyo, taarifa hizo zinahitaji usiri mkubwa. Katika kudhihirisha jambo hilo, sheria ya Takwimu inaeleza kuwa mtu atakaye husika katika zoezi la ukusanyji wa takwimu ikiwa ni pamoja na takwimu za Sensa ya Watu na Makazi, atalazimika kuapishwa (kiapo cha kutunza siri) mbele ya Kamishna wa viapo (Commissioner for Oaths) kabla ya kuanza kazi husika. Kifungu cha 11(2) cha Sheria ya Takwimu, 2002.
4.0 Maofisa walioidhinishwa (authorized Officersa
Katika kutekeleza majukumu yake, Mkurungenzi Mkuu amepewa mamlaka ya kuwaidhinisha watu wengine kwa lengo kukusanya taarifa maalum za kitakwimu kulingana na mahitaji.
Kifungu cha Sheria ya Takwimu, 2002.
5.0 Amri ya Rais kuhusu kufanyika kwa Sensa ya Watu na Makazi
Sensa ya Watu na Makazi ni shughuli ya kitaifa ambayo katika utekelezaji inahusisha maelekezo ya Rais wa Nchi. Sheria ya Takwimu inaeleza kuwa kabla zoezi la Sensa ya Watu na Makazi halijafanyika, Rais anatakiwa kutoa Amri (Presidential Order) ya kufanyika kwa Sensa. Amri hiyo inatakiwa kueleza:-
a) Tarehe ya kufanyika kwa Sensa;
b) Taarifa zitakazokusanywa katika Sensa;
c) Namna Sensa itakavyofanyika;
d) Muda na mahali Sensa itakapofanyika; na
e) Wahusika katika kukusanya taarifa za Sensa
Kifungu cha 14 cha Sheria ya Takwimu, 2002
6.0 Makosa ya Jinai na Adhabu zake
Sheria ya Takwimu inaainisha vitendo ambavyo ni makosa ya jinai na pia Sheria hiyo inaweka wazi adhabu zinazoweza kutolewa kwa yeyote ambaye atakuwa ametenda makosa hayo.
Kifungu cha 27 cha Sheria ya Takwimu, 2002 kinabainisha makundi ya aina tatu ya watu wanaoweza kushtakiwa kutokana na viten do ambavyo ni makosa kwa mujibu wa Sheria hiyo.
6.1 Waajiriwa wa NBS/ Wadadisi/ Wasimamizi(Authorized Officer)
a. Kutumia taarifa za kitakwimu kwa manufaa binafsi (use of information for personal gain);
b. Kutoa taarifa za kitakwimu bila kibali (publishing any information without authority);
c. Kutoroka/kutelekeza kazi uliyopangiwa kuifanya (desertion);
d. Kudai taarifa tofauti na zilizoruhusiwa kukusanywa (obtaining information not authorized to obtain); na
e. Kuomba malipo/ujira(asking payment or reward).
Vitendo hivyo vyote ujumla ni makosa ya jinai na mhusika akipatikana na hatia atastahili adhabu ya kifungo cha miezi 12 au kulipa faini ya shilingi milioni moja au vyote viwili. Kifungu cha 27(1) a-e) cha Sheria ya Takwimu, 2002.
6.2 Kutoa taarifa zilizopatikana isivyo halali (Mtu yeyote)
Sheria hii inabainisha kuwa ni kosa kwa mtu yeyote kukutwa au kutoa taarifa za kitakwimu zilizopatikana kwa kukika vifungu vya Sheria ya Takwimu. Adhabu kwa makosa ya kundi hili ni kifungo cha miezi 18 au faini ya shilingi milioni moja na laki tano au vyote viwili. Kifungu cha 27(2) cha Sheria ya Takwimu, 2002
6.3 Kutotoa ushirikiano katika zoezi la kitakwimu (Respondent/ Mtu yeyote)
Sheria hii pia inaainisha makosa yanayowezakufanywa na mtu yeyote au Respondent wakati wa zoezi la kitakwimu (wakati wa kukusanya takwimu). Makosa hayo ni:
a. Kumzuia Authorized Officer (Msimamizi/Mdadisi/Karani wa Sensa kutekeleza majukumu yake
b. Kukataa /kuacha kwa makusudi:
i. Kujaza fomu au nyaraka yoyote iliyokabidhiwa kwake kwa lengo maalum;
ii. Kujibu maswali aliyoulizwa;
c. Kutoa taarifa za uongo
d. Kuharibu au nyaraka yoyote
e. Kujifanya Authorized Officer kwa lengo la kujipatia taarifa ambazo hastahili kuzipata;
f. Kukataa kutoa nyaraka zozote zinazohitajika katika shughli za kitakwimu;
g. Kukiuka kifungu chochote cha Sheria hii.
Sheria inaeleza kuwa adhabu kwa kosa lolote kati ya hayo ni kifungo cha miezi 6 au faini ya shilingi laki sita. Kifungu cha 27(3) cha Sheria ya Takwimu, 2002.
7.0 Hitimisho
Sheria ya Takwimu, 2002 imeainisha majukumu ya NBS na kutamka wazi aina za makosa na adhabu zake.
Kwa mantiki hiyo ni kjukumu la kila mmoja kutimiza wajibu wake na kutoa ushirikiano unaostahili katika zoezi la Sensa ya Watu ma Makazi ya Mwaka 2012.
Kwa kufanya hivyo, kila mdau atakuwa ameisaidia Serikali kupata taarifa sahihi kwa ajili ya mipango ya maendeleo ya nchi.
Waziri Mkuu Mizengo Pinda akitoa wosia kwa wanafunzi 20 waliofanya vizuri katika mitihani ya kidato cha sita kwa mwaka 2012 bungeni leo mjini Dodoma. Wanafunzi hao 10 wasichana na 10 wavulana wamepewa cheti , kopyuta ya pakato (laptop) na fedha taslimu shilingi laki mbili kwa kila mmoja.
Wanafunzi 20 waliofanya vizuri katika mitihani wa kidato cha sita kwa mwaka 2012 wakiwa katika picha ya pamoja nje ya ukumbi wa Bunge leo mjini Dodoma. Wanafunzi hao 10 wasichana na 10 wavulana wamepewa cheti na Waziri Mkuu, kopyuta ya pakato (laptop) na fedha taslimu shilingi laki mbili kwa kila mmoja.WAZIRI Mkuu, Mizengo Pinda amewataka wanafunzi wote nchini kuwa na nidhamu , kujituma na kufuata maelekezo vizuri ya walimu wao na kuepuka makundi mabaya ili kuweza kupata mafanikio katika masomo yao. Aidha Waziri Mkuu Pinda amewaasa wanafunzi waliofanya vizuri katika mtihani wa kuhitimu kidato cha sita wa mwaka huu kutumia uhuru vizuri watakaoupata kwenye maisha ya vyuo vya elimu ya juu bila kurudi nyuma katika maendeleo ya masomo yao. Kauli hiyo ilitolewa leo na Waziri Mkuu, Pinda Bungeni mjini Dodoma kabla ya kuwatunuku vyeti vya kuwapongeza wanafunzi hao 19 kati 20 waliofanya vizuri katika mtihani huo,kutoka shule mbalimbali nchini, ambapo mmoja wao, Jamal Juma yuko nje ya nchi. Wanafunzi hao ambao wote walipata ufaulu wa daraja la kwanza katika mtihani huo, saba kati yao wanatoka katika shule ya wasichana ya Marian, watatu Mzumbe, wawili Fedha na wengine wawili Kibaha. Waliobakia mmoja mmoja anatoka Kilakala, Ufundi Ifunda, Tabora girls, Tabora boys, Minaki na Mpwapwa. Mmefanya vizuri. Mnastahili ! Hongereni Sana. Tunataka ufaulu wenu uwe mzuri zaidi kwa vile sasa ninyi mnakweda kujenga weledi. Mnakuwa wataalamu wa fani Fulani. Tumieni muda wenu kujifunza zaidi kutafuta maarifa zaidi na kuvumbua mambo makubwa zaidi yatakayowasaidia ninyi wenywe na jamii kwa ujumla kujiletea maendeleo alisema Waziri Mkuu Pinda. Aliongeza kuwa ni vizuri utaratibu huo wa kuwatambua wanafunzi bora uwe endelevu na ikiwezekana wapatiwe fursa ya kuendelezwa katika vyuo vikuu vya kipekee nje ya nchi hususan kwenye fani zitakazojenga uwezo kwa taifa Waziri Mkuu alisema kati ya shule 10 ,ambazo wanafunzi hao wanatoka, wawili ni kutoka shule za kata, ambao ni Ester Marcel toka shule ya sekondari ya wasichana ya Olele Kilimanjaro na Brighton Lema toka shule ya sekondari ya Kitangiri, Mwanza. Napenda niwape pongezi za pekee wanafunzi hawa kwa jihudi kubwa walizozionesha. Kufaulu kwao kunadhihirisha kwamba shule hizi za kata tukiweka bidii kwa kuziwezesha zaidi zitafanya vizuri zaidi kama ilivyo katika shule nyingine. Waziri Mkuu pia aliwataka walimu wote nchini kushirikiana na wazazi na serikali kwa pamoja kufundisha watoto kwa bidii ili waweze kufanya vizuri katika masomo yao kama wanafunzi hao waliotunukiwa vyeti hivyo. Kwa upande wake Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk. Shukuru Kawambwa alisema wanafunzi hao watazawadiwa pakato (laptop) na sh. 200,000, pia kila shule iliyotoa mwanafunzi bora itazawadiwa sh. milioni moja katika hafla maalum itakayofanyika jioni. Wanafunzi hao wanatoka katika mchepuo wa PCM ambao ni 16 na mmojammoja toka mchepuo wa PGM, CBA, ECA na HKL. Naye Spika wa Bunge la Jamhuri, Anna Makinda aliwataka wanafunzi hao kuwa makini na makundi kwa kuyasilikiza huku wakitumia akili zao huku akitoa changamoto shule nyingine kujitahidi kufanya vizuri.

SENSA HAIHUSIANI NA DINI WALA KABILA LOLOTE

AJIRA KWA WATOTO, kijana ambaye jina lake halikuweza kupatika anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 7-9 alinaswa na kamera yetu akiwa amebeba gunia la mahindi katika stendi kuu ya mabasi mjini Iringa hivi karibuni
WAANDISHI WA HABARI WANA HURUMA SANA; Mwenyekiti wa semina elekezi ya sensa kanda ya nyanda za juu, Nyenyembe akimkabidhi shilingi 409,800/= Mussa Chilongo mwandishi wa habari mongwe na mtangazaji wa Luangwa FM aliyepatwa na ulemavu wa macho akiwa kazini 2009 ukiwa ni mchango wa waandishi wa habari kwake.
Tushamaliza kazi hapa tukaandae vipindi, waandishi na watangazaji wa Radio Chem chem ya Sumbawanga wakibadilishana mawazo baada ya kumaliza semina elekezi mjini Iringa juu ya sensa ya watu na makazi 2012.
WAANDISHI BWANA, Mwandishi wa Habari wa TBC, Zeno lukowa akiwachukua waandishi wenzake kwa ajili ya 'Story' ya jioni; semina elekezi kwa waandishi wa habari Iringa.
Wakati mwingine waandishi walichoka baada ya muwezeshaji kushindwa kuvuta usikivu kwa wana semina
TUNASIKILIZA HOTUBA YAKO MAMA; kama anaambiwa hivo katibu tawala wa mkoa wa Iringa

BAADA YA SEMINA KUISHA SASA SAFARI KUELEKEA MAENEO

Kondakta wa waandishi hapana shaka lazima awe mwandishi mwenzao kama alivyonaswa na kamera yetu mwandishi wa Chanel Ten, Juddy Ngonyani akikatisha tiketi kwa waandishi wa habari waliokuwa wakielekea jiji Mbeya.
NJIANI NAKO KAMERA ZILIKUWA ''BUSY;''
 TUNATAFUTA RIZIKI HAKUNA KULALA
KAZI NI KAZI ALIMRADI TU IWE HALALI NAKIPATO KIWEPO
SAFARI YA JUELEKEA JIJINI MBEYA WANDISHI KUTOKA MBEYA RUKWA NA KATAVI

-->
SENSA ya watu na makazi haina uhusiano wowote na dini, kabila wala tabaka lolote katika jamii bali ni kwa ajili ya kupata takwimu zitakazotumika kuboresha utoaji huduma na kuongeza kasi ya maendeleo kwa wananchi
Hayo yalisemwa na Mratibu wa Sensa mkoa wa Iringa, Fabian Fundi katika ukumbi wa Chuo Kikuu cha Ruaha mjini Iringa alipokuwa akitoa mada juu ya umuhimu wa sensa ya watu na makazi kwa waandishi wa habari waliokuwa katika semina ya sensa ya Nyanda za juu kusini na mikoa ya Lindi na Mtwara Agosti 12, 2012
Fundi alisema katika sensa ya watu na makazi iliyoanza kuendeshwa hapa nchini mwaka 1967 haijawahi kuwekwa hoja ya swali la dodoso linalohusu dini, kabila wala tabaka lolote katika jamii kutokana na malengo ya sensa kutokuhitaji matabaka ya kijamii
Alisema kupitia sensa serikali ina lengo la kujua idadi ya watu, hali zao kimaisha, mahitaji na umiliki wa rasilimali ili kupanga mipango ya maendeleo ya eneo husika na wala haina lengo la kujua idadi ya watu  katika kabila fulani au dini fulani kwani takwimi hizo hazitaisaidia serikali wala wadau wake
Alisema serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania haipangi maendeleo kwa kigezo cha dini wala kabila bali inapanga kwa kuzingaztia mahitaji ya sehemu kutokana na takwimu zilizopo
Aidha alifafanua kuwa serikali ya Tanzania haina dini wala kabila isipokuwa imetoa ruhusa kwa wananchi wake kuwa na dini zao kwa kufuata sheria za nchi na ndiyo maana haiwezi kuweka swali la dini au kabila katika dodoso la sensa na wale wanaotaka liwepo waeleze lengo la kuweka swali hilo katika dodoso litalenga kupata takwimu zitakazotumiwa na serikali katika kuboresha nini.
Alisema kimsingi takwimu za dini zimo katika dini za wahusika na siyo nje ya dini zao kutokana na malengo yao katika kutekeleza majukumu yao kwani lengo la serikali ni kuweka mipango itakayosaidia kuboresha huduma za kijamiii kama vile upatikanaji wa huduma za afya, maji, soko, shule, umeme n.k mahitaji yasiyohusu kundi fulani tu.
Aliwataka Watanzania kuyapuuza maneno ya watu wanahamasisha kuwa wasishiriki katika sensa kwa minajiri ya makabila yao, dini zao, matabaka yao n.k kwani kufanya hivo kutadhoofisha maendeleo katika maeneo yao hadi baada ya miaka kumi tena kupita kutokana na utaratibu wa sensa kufanyika baada ya miaka kumi.
Mkuu wa mkoa wa Iringa Dr Christine Ishengoma katika picha ya pamoja na baadhi ya washiriki wa semina
Mwenyekiti wa Klabu ya waandishi wa habari mkoa wa Mbeya Chrispher Nyenyembe alipewa jukumu la kuwa mwenyekiti wa semina elekezi ya sensa Nyanda za Juu Kusini mjini Iringa
Waandishi wa habari wa mikoa ya Katavi na Rukwa wakiwa katika picha ya pamoja na mkuu wa mkoa wa Iringa Dr Christine Ishengoma
washiriki wa semina katika ukumbi wa Chuo Kikuu cha Ruaha mjini Iringa
Nauliza hivi ikiwa mtu amefariki saa sita na robo usiku wa kuamkia siku ya sensa atahesabiwa, swali la mshiriki wa semina ya sensa

TAASISI YA TAKWIMU YATOA MAFUNZO  KWA WANAHABARI JUU YA SENSA

Waandishi wa habari kutoka mkoa wa Mbeya wakiwa katika picha ya pamoja na mgeni rasmi. Mkuu wa mkoa wa Iringa Dr Christine Ishengoma akisoma risala kwa waandishi wa Habari toka katika mikoa ya Nyanda za juu kusini. Washiriki wasemina waandisho toka mkoa wa Iringa wakiwa katika picha ya pamoja na mgeni rasmi baada ya kufungua rasmi mafunzo hayo.
Waandishi toka Mkoa wa Rukwa na Katavi

Mkuu wa mkoa wa Iringa DKT Christine Ishengoma amewataka wanahabari kushirikiana na ofisi ya taifa ya takwimu kulisaidia Taifa katika zoezi la sensa ya watu na makazi kwa kuendelea kuhamasisha wananchi kujitokeza katika zoezi hilo.
Mkuu huyo wa mkoa ametoa Rai hiyo leo katika ukumbi wa Ruco mjini Iringa wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya siku mbili ya wanahabari kutoka mikoa ya nyanda za juu kusini pamoja na mkoa wa Lindi na Mtwara yalioandaliwa na ofisi ya Taifa ya Takwimu.
Alisema kuwa zoezi hilo la sensa ya watu na mkazi lina nafasi kubwa katika Taifa ili kuwezesha kupanga bajeti kulingana na mahitaji sahihi ya wananchi wake,hivyo kuwataka wanahabari hao kusaidia kutoa elimu zaidi kwa umma .
Hivyo alisema kuwa ni wajibu kwa wanahabari kuelimishwa zaidi juu ya zoezi hilo litakavyofanyika Kama njia ya kuwezesha Taifa kufanikisha zoezi hilo.
Alisema kuwa vyombo vya habari ni miongoni mwa wadau wakubwa ambavyo vinategemea zaidi Takwimu katika kufikisha ujumbe kwa Taifa hivyo ili zoezi hilo liweze kufanikiwa lazima kuwepo na ushirikiano mkubwa kutoka kwa vyombo hivyo vya habari.
DKT Ishengoma alisema kuwa hadi kufikia siku ya zoezi hilo la sensa ni siku 13 ndizo zilizosalia hivyo ni matumaini ya serikali kuona siku zilizobaki zinatumika vema katika kufikisha taarifa kwa wananchi.
Alisema kuwa sensa ya watu na makazi ni zoezi ambalo limekuwa likifanyika kila baada ya miaka 10 hivyo lazima umma kujulishwa ili kujitokeza kwa wingi katika zoezi Hilo.
Mkuu huyo wa mkoa alishauri wakuu wa kaya kuweka kumbukumbu sahihi ambazo zitawezeshwa makalani wa sensa kupata taarifa zilizo sahihi katika kufanikisha zoezi Hilo.