Thursday, March 8, 2012

MAISHA YA MASIKINI KILA SIKU

APRIL 18, 2012 , KATAVI MPANDA  

MAFUTA NI ISSUE??????????????

 MATATIZO YA UHABA WA MAFUTA BADO YANAENDELEA KATIKA MKOA WA KATAVI HAPA CHINI TUMEKUWEKEA PICHA ZILIZOPIGWA JANA KATIKA KITUO KIMOJA CHA MAFUTA KATIKA MAKAO MAKUU YA MKOA WA KATAVI MPANDA MJINI.










HAPA CHINI NI GARI LILILOKUWA LIKIELEKEA MISHAMO LIKIENDESHWA NA DEREVA AKIWA AMELEWA CHAKARI NA KUSABABISHA AJALI NYUMA YA UKUTA WA KANISA KATOLIKI MPANDA ENEO LA SHULE YA MSINGI MSAKILA JUZI MAJIRA YA SAA SITA MCHANA, MADEREVA WALEVI TUWAPIGE VITA 




mkurugenzi wa blog hii Wilbroard Sumia, anawapongeza wale wote walioingia katika bunge la Afrika Mashariki katika kipindi kijacho

    POSHO IMEISHA SAFARI BADO


DC MPANDA AWAFUNDA WATENDAJI WA KATA NA VIJIJI
 MKUU WA WILAYA YA MPANDA MKOA WA KATAVI, DR RAJABU RUTENGWE 
Na  Willy Sumia, Mpanda
SERIKALI wilaya ya Mpanda mkoa wa Katavi imewaagiza watendaji wa kata na vijiji kuwajibika katika maeneo yao ya kazi ili kuleta ufanisi katika utendaji wa kazi
Agizo hilo limetolewa na mkuu wa wilaya ya Mpanda, Dr Rajabu Rutengwe Machi 9, 2012 katika ukumbi wa halmashauri ya wilaya ya Mpanda wakati akifunga kikao cha ushauri cha wilaya ya Mpanda DCC
Mkuu huyo wa wilaya amesema hivi sasa watendaji wengi wamekuwa wakisubiria maagizo katika utendaji kazi wao bila kujali kuwa kutenda kazi zao bila maagizo ni nguzo ya utendaji kazi  wao
Amesema katika miji mingi wilayani Mpanda uchafu umeendelea kuchukua nafasi kubwa kuliko hali inayotakiwa kwani katika hali halisi hakuna haja ya kuwa na miji michafu wakati kila mji una watendaji wa serikali wanaotakiwa kuwajibika
Ametoa mfano wa mji wa Ikola kuwa kituo kikuu cha magonjwa wa kuhara na kutapika ugonjwa ambao kimsingi unasababishwa na uchafu hivyo endapo watendaji wataweza kuwajibika na kufanya kazi ipasavyo uchafu ungeondoka wenyewe hata hao wagonjwa wangeeleweka kuwa wametoka mbali
Ameziagiza serikali za vijiji na kata kuwajibika katika suala la mifugo iliyoingia kiholela katika maeneo yao kwani amesema kuwa taarifa za uhakika zinaelekeza kuwa upo ushahidi wa kutosha kuwa wapo baadhi ya watendaji wa kata na vijiji wamekuwa wakichukua pesa ili kuruhusu mifugo kuingia katika maeneo yao
“ ndugu zangu nawaeleza kitu kimoja kikubwa ni kuwa waliokula pesa watazitapika maana naagiza au ng’ombe waondoke wewe ubaki au wewe uondoke  ng’ombe wabaki, sina namna lazima uwajibike kwa ng’ombe uliowapokea” amesema mkuu wa wilaya
Kwa upande mwingine mkuu wa wilaya ameshukuru maafisa mipango wa halmashauri ya wilaya ya Mpanda kwa kufanya vema katika maandalizi ya miradi ya maendeleo inayoleta mafanikio makubwa katika vijiji na kuweza kuondoa kero mbalimbali kwa wananchi wa wilaya yake
Mkuu wa wilaya ametoa taarifa katika kikao hiki kuwa kuanzia Machi 12, 2012 ataanza ziara ya kukagua miradi ya maendeleo katika kila kata ambapo ataweza kupokea taarifa za miradi, taarifa ya kazi, kukagua miradi na kuzungumza na wananchi katika mikutano ya hadhara katika kila palipo na mradi wa maendeleo
Mada zilizojadiliwa katika kikao cha leo cha DCC ni pamoja na kupitia mpango na bajeti ya halmashauri ya wilaya ya Mpanda ya mwaka 2012/2013, kupitia mpango wa bajeti ya halmashauri ya wilaya ya Mlele kwa mwaka 2012/2013 pamoja na uzoefu wa nchi ya Japan katika ugatuaji wa madaraka.
mwisho
HAPA KAZI TU!!!! Mmoja wa madaktari akitoa huduma ya kinywa na meno kwa mwanafunzi wa shule ya msingi Msakila mjini Mpanda katika mkoa wa Katavi, Katavi ni miongoni mwa mikoa ambayo haijaguswa na mgomo wa madaktari uliotokea mwezi uliopita na mwezi huu.
MKOA WA KATAVI NA FURSA ZINAZOPATIKANA: MKUU WA WILAYA ATEMBELEA KATA ZA H/MJI - 

UNAMAONI GANI ?  tuandikie kwa email willysumia@gmail.com

BARAZA LA MADIWANI LARIDHIA BAJETI YA BIL. 14
BARAZA la madiwani la halmashauri ya mji Mpanda katika mkoa wa Katavi limepitisha mapendekezo ya bajeti ya hamashauri hiyo kwa kipindi cha mwaka 2012/2013 kwa ajili  ya shughuli za maendeleo
Baraza hilo lilioketi leo Machi 9, 2012 limekubali kuyapitisha makadirio na makisio ya bajeti ya halmashauri hiyo ambapo mweka hazina wa Halmashauri hiyo Tatu Kisori amesema katika kipindi cha 2012/13 halmashauri imepanga kukusanya kiasi cha shilingi 606,847,000 kutoka katika vyanzo vya ndani ambapo pia halmashauri yake inatarajia kupokea ruzuku toka serikali kuu kiasi cha shilingi 6,441,517,240.
Amesema katika ruzuku ya serikali kiasi cha shilingi 5,338,014,240/= ni malipo ya mishahara kwa watumishi wa kada mbali mbali na shilingi 1,103,503,000/= ni za matumizi ya kawaida na kufafanua kuwa katika bajeti hiyo mishahara ni ongezeko la asilimia 20 kutoka shilingi 4,265,057,000/= hadi 5,338,014,240/=
Akizungumzia miradi ya maendeleo mweka hazina huyo alisema katika bajeti ya maendeleo halmashauri yake inatarajia kutumia shilingi 3,870,010,627/= kutoka serikali kuu, katika fedha hizo miradi ya maji imepewa kipaumbele kikubwa kwa kutengewa asilimia 34 ambayo ni shilingi 1,300,288,600/= ikifuatiwa na idara ya utawala kwa asilimia 26 sawa na shilingi 1,027,733,000/= pamoja na elimu ya sekondari iliyopewa shilingi 614,474,000/= sawa na asilimia 16.
Tatu Kisori pia amewasilisha bajeti ndogo ya maombi maalum ya nje ya ukomo wa bajeti kutokana na baadhi ya shughuli muhimu kushindwa kuingia katika bajeti kutokana na viwango vidogo vya bajeti vilivyowekwa na TAMISEMI na hivyo kuathiri bajeti kushindwa kuingizwa vitu muhimu ili kufikia malengo na kuondoa kero zilizoko katika jamii
Kisori amesema kutokana na hali hiyo halmashauri imelazimika kuomba fedha nje ya bajeti ya kawaida kiasi cha shilingi 3,558,000,000/= kwa ajili ya kununulia gari la kuzoa taka ngumu mjini Mpanda, kununulia gari la kunyonya maji machafu mjini, matengenezo ya gari la zimamoto na ujenzi wa sekondari ya Kata ya Kakese pamoja na kuweka miundombinu ya umeme katika shule za sekondari zote.
Aidha baraza la madiwani la halmashauri ya mji Mpanda limeridhia na kupitisha makisio ya bajeti ya hamashauri hiyo katika kipindi cha Julai 2012 hadi juni 2013 kiasi cha shilingi 14,688,051,240/= ikiwa ni mapato ya ndani na ruzuku ya serikali kwa ajili ya maendeleo ya halmashauri ya Mji Mpanda
Awali akiwasilisha mapitio ya bajeti ya 2011/2012 Kisori amesema halmashauri yake ilipanga kukusanya kiasi cha shilingi 823,164,000/= kutoka katika vyanzo vya ndani na kuweza kukusanya kiasi cha shilingi 241,873,480/= katika kipindi cha Julai 2012 hadi januari 2012 sawa na asilimia 29.38 ya makisio ambapo kiasi hicho kimefikiwa kwa kutumia mawakala wa ukusanyaji wa ushuru.
Amesema katika kipindi cha bajeti 2011/12 halmashauri ilipanga kuingiza mapato ya shilingi 70,350,000/= kutokana na vyanzo vya mapato vilivyofutwa na kuweza kukusanya shilingi 42,028,500/= sawa na asilimia 60 ya makisio.
Katika hatua nyingine baraza hilo limetoa Baraka zote kwa shirika la nyumba la Taifa kuenza ujenzi wa majengo katika mji wa Mpanda baada ya kuridhia malipo ya shilingi milioni 100 ikiwa ni kwa ajili ya eneo la jingo la starehe maarufu kwa jina la jengo la Paradise eneo litakalojengwa gorofa nne kwa ajili ya matumizi ya kibenki, ofisi na maduka ya biashara
Aidha baraza hilo limepokea na kuridhia maombi ya mamlaka ya viwanja vya ndege nchini juu ya kuomba upanuzi wa uwanja wa ndege wa Mpanda utakaopelekea kuhamishwa kwa baadhi ya wakazi wa eneo la Nsemulwa Uwanja wa ndege ili kupisha upanuzi huo.
Imeelezwa katika baraza hilo kuwa upanuzi huo taathiri baadhi ya wananchi watakaotakiwa kipisha upanuzi huo baada ya kulipwa fidia na mamlaka husika katika kipindi kifupi kijacho kwani ujenzi unatarajia kuanza katika kipindi kifupi kijacho.\\
MAAFISA WATENDAJI WAAGIZWA KUSHUGHULIKIA MIFUGO HARAMU

Na  Willy Sumia, Mpanda
SERIKALI wilaya ya Mpanda mkoa wa Katavi imewaagiza watendaji wa kata na vijiji kuwajibika katika maeneo yao ya kazi ili kuleta ufanisi katika utendaji wa kazi
Agizo hilo limetolewa na mkuu wa wilaya ya Mpanda, Dr Rajabu Rutengwe Machi 9, 2012 katika ukumbi wa halmashauri ya wilaya ya Mpanda wakati akifunga kikao cha ushauri cha wilaya ya Mpanda DCC
Mkuu huyo wa wilaya amesema hivi sasa watendaji wengi wamekuwa wakisubiria maagizo katika utendaji kazi wao bila kujali kuwa kutenda kazi zao bila maagizo ni nguzo ya utendaji kazi  wao
Amesema katika miji mingi wilayani Mpanda uchafu umeendelea kuchukua nafasi kubwa kuliko hali inayotakiwa kwani katika hali halisi hakuna haja ya kuwa na miji michafu wakati kila mji una watendaji wa serikali wanaotakiwa kuwajibika
Ametoa mfano wa mji wa Ikola kuwa kituo kikuu cha magonjwa wa kuhara na kutapika ugonjwa ambao kimsingi unasababishwa na uchafu hivyo endapo watendaji wataweza kuwajibika na kufanya kazi ipasavyo uchafu ungeondoka wenyewe hata hao wagonjwa wangeeleweka kuwa wametoka mbali
Ameziagiza serikali za vijiji na kata kuwajibika katika suala la mifugo iliyoingia kiholela katika maeneo yao kwani amesema kuwa taarifa za uhakika zinaelekeza kuwa upo ushahidi wa kutosha kuwa wapo baadhi ya watendaji wa kata na vijiji wamekuwa wakichukua pesa ili kuruhusu mifugo kuingia katika maeneo yao
“ ndugu zangu nawaeleza kitu kimoja kikubwa ni kuwa waliokula pesa watazitapika maana naagiza au ng’ombe waondoke wewe ubaki au wewe uondoke  ng’ombe wabaki, sina namna lazima uwajibike kwa ng’ombe uliowapokea” amesema mkuu wa wilaya
Kwa upande mwingine mkuu wa wilaya ameshukuru maafisa mipango wa halmashauri ya wilaya ya Mpanda kwa kufanya vema katika maandalizi ya miradi ya maendeleo inayoleta mafanikio makubwa katika vijiji na kuweza kuondoa kero mbalimbali kwa wananchi wa wilaya yake
Mkuu wa wilaya ametoa taarifa katika kikao hiki kuwa kuanzia Machi 12, 2012 ataanza ziara ya kukagua miradi ya maendeleo katika kila kata ambapo ataweza kupokea taarifa za miradi, taarifa ya kazi, kukagua miradi na kuzungumza na wananchi katika mikutano ya hadhara katika kila palipo na mradi wa maendeleo
Mada zilizojadiliwa katika kikao cha leo cha DCC ni pamoja na kupitia mpango na bajeti ya halmashauri ya wilaya ya Mpanda ya mwaka 2012/2013, kupitia mpango wa bajeti ya halmashauri ya wilaya ya Mlele kwa mwaka 2012/2013 pamoja na uzoefu wa nchi ya Japan katika ugatuaji wa madaraka.
mwisho

RAIS JAKAYA KIKWETE KESHO KULIHUTUBIA TAIFA ,MGOMO WA MADAKTARI WAWEZA KUZUNGUMZIWA

Taarifa zilizotua hivi punde kupitia mwanahabari wa mtandao huu wa www.sumiampanda.blogspot.com kutoka chumba cha habari cha radio Uhuru zinadai kuwa Rais Jakaya Kikwete kesho ijumaa saa 10 jioni atalihutubia Taifa kupitia wazee wa mkoa wa Dar es Salaam katika ukumbi wa Diamond Jubilee na hutuba yake kurushwa moja kwa moja (live) na TV na radio nchini.


SERIKALI YATANGAZA RASMI MIKOA MIPYA MINNE NA WILAYA 19

Waziri mkuu Mizengo Pinda

Habari ambayo imetua hivi punde katika mtandao huu wa www.sumiampanda.blogspot.com inadai kuwa serikali imetoa matangazo rasmi ya Serikali (Government Notices) kuhusu uanzishaji wa mikoa mipya minne na wilaya mpya 19 ambayo yamechapishwa tangu Machi 2, mwaka huu.
Waziri Mkuu Mizengo Pinda amesema matangazo hayo ambayo yalisainiwa na Rais Jakaya Kikwete tangu Machi mosi, 2012, yanabainisha mikoa mipya kuwa ni Geita, Katavi, Njombe na Simiyu. Mikoa hii imechapishwa katika Tangazo la Serikali Na. 72.
Wilaya 19 ambazo zimeanzishwa na kuchapishwa katika Tangazo la Serikali Na.73 ni Buhigwe, Busega, Butiama, Chemba, Gairo, Ikungi na Itilima. Wilaya nyingine ni Kakonko, Kalambo, Kaliua, Kyerwa, Mbogwe, Mkalama na Mlele. Nyingine ni Momba, Nyang’hwale, Nyasa, Uvinza na Wanging’ombe.
Kwa mujibu wa matangazo hayo makao makuu ya mikoa hiyo mipya minne yatakuwa kama ifuatavyo: Geita (Geita), Simiyu (Bariadi) Njombe (Njombe) na Katavi (Mpanda).
Mikoa hiyo itakuwa na wilaya zifuatazo; Geita utakuwa na wilaya tano za Bukombe, Chato, Geita, Mbongwe na Nyang’hwale. Mkoa wa Katavi utakuwa na wilaya mbili za Mlele na Mpanda. Mkoa wa Njombe utakuwa na wilaya nne za Makete, Njombe, Ludewa na Wanging’ombe wakati mkoa wa Simiyu utakuwa na wilaya tano za Bariadi, Busega, Maswa, Meatu na Itilima.
Makao makuu ya wilaya mpya zilizoanzishwa ni kama ifuatavyo: Buhigwe (Buhigwe); Busega (Nyashimo); Butiama (Butiama); Chemba (Chemba); Gairo (Gairo); Ikungi (Ikungi) Itilima (Lagangabilili); Kakonko (Kakonko); Kalambo (Matai) na Kaliua (Kaliua).
Nyingine ni Kyerwa (Rubwera); Mbogwe (Mbogwe); Mkalama (Nduguti); Mlele (Inyonga); Momba (Chitete); Nyang’hwale (Kharumwa); Nyasa (Mbamba Bay); Uvinza (Lugufu) na Igwachanya (Wanging’ombe).
Julai 2010, kabla Rais Kikwete hajatoa hotuba ya kulivunja Bunge, Serikali ilitoa uamuzi wa kuunda mikoa mipya minne na wilaya mpya 21. Hata hivyo, baada ya kuhakiki mipaka ya maeneo hayo yote na kuandaa maelezo ya mipaka hiyo vizuri (boundary descriptions), wilaya zilipunguzwa na kubakia 19.
(mwisho)
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
S. L. P. 3021,
DAR ES SALAAM.
ALHAMISI, MACHI 8, 2012.
www.katavim.blogspot.com

MKOA WA KATAVI NA FURSA ZINAZOPATIKANA: MKUU WA WILAYA ATEMBELEA KATA ZA H/MJI

DC MPANDA ATOA SIKU KUMI NA NNE WALOFAULU KURIPOTI SHULENI
SERIKALI ya wilaya ya Mpanda mkoa tarajiwa wa Katavi imeuagiza uongozi wa Kata ya Ilembo mjini Mpanda kuwasilisha kwake majina ya wahamiaji haramu walioingia katika kata hiyo ili waweze kushughulikiwa mapema iwezekanavyo
Agizo hilo limetolewa na mkuu wa wilaya hiyo Dr Rajabu Rutengwe katika mkutano wa hadhara mara baada ya kuelezwa kero kubwa ya wakulima na wafugaji iliyopo katika kata hiyo iliyodumu kwa takribani miaka mine sasa.
Awali akitoa ufafanuzi wa kaero hiyo afisa mtendaji wa kata ya Ilembo Marry Ngomarufu amesema kuwa ofisi ya kata imeweza kutumia ofisi ya polisi na mahakama kushughulikia migogoro hiyo ingawa bado hali haijaweza kutengamaa kiasi cha kutosha
Mkuu wa wilaya ya Mpanda amesema migogoro mingi ya wahamiaji haramu hasa wafugaji toka mikoa ya kanda ya Ziwa kutokana na baadhi ya wananchi kuuziana maeneo na wafugaji kwa tamaa ya pesa kwa wenye mashamba na badala yake wameuza fursa zao na kuleta migogoro kwa sababu majirani na eneo lililonunuliwa na wafugajia au mfugaji mmoja wao wakauwa wanaendelea kulima na hiyo inakuwa ni sehemu ya chakula cha mifugo na ng’ombe hawana mipaka kama binadamu
Akihutubia wananchi katika mkutano wa hadhara Ilembo mkuu wa wilaya amesema urithi pekee kwa motto ni elimu na siyo majumba na magari hivyo amewataka wananchi mahala popote wasimamie watoto kusoma kwa bidii na kuzitumia kwa uhakika fursa za kupata elimu zilizopo b ila kujali kipato cha mzazi au mlezi kwani ni hazina ya baadae kwa wilaya, mkoa na hata taifa kwa ujumla
Amesema hivi sasa serikali imeweka mazingira ya kuhakikisha kuwa watoto wote wanapata elimu ya msingi na sekondari hata kama hawana uwezo kifedha kwani hivi sasa kila kata ina sekondari yake inayotoa fursa kwa watoto wote walioko katika kata kuendelea na masomo ya sekondari pindi wanapofaulu mtihani wa darasa la saba.
Pia mkuu wa wilaya hiyo Dr Rajabu ameagiza watoto wa kike kumi na mmoja waliofaulu kuingia kidato cha kwanza hawajaripoti shuleni wafike shuleni ndani ya kipindi cha siku kumi na nne kuanzia Machi 6, 2012 wawe wamshaanza masomo na taarifa toka kwa mkuu wa shule iwasilishwe kwake baada ya siku kumi na nne kabla serikali ya wilaya haijaanza kuwafuatilia kisheria kwa nini hawajaripoti shuleni kuanza na masomo ya sekondari.
Amewasihi wananchi kuanza kujenga majengo yanayoendana na hadhi ya manispaa kwani muda wa miezi michache ijayo halmashauri ya mji Mpanda utakuwa na hadhi ya manispaa baada ya mkoa wa Katavi kuanza ili kuanza na kasi ya maendeleo ya mkoa wa Katavi ambao umenza kukimbia kimaendeleo kabla ya kuanza kazi rasmi.
Amewahimiza wananchi wa Ilembo kuanza kufanya miradi ya ufugaji kuku hasa akina mama ambao wanaweza kuwa karibu na mifugo hiyo kwani hivi sasa kuku mmoja anauzwa kwa bei ya shilingi elfu kumi na mbili kwa kuku mmoja mdogo na hivyo ukianza kufuga makoo mmmoja akapewa pumba anaweza kuzaa vifaranga mia moja na arobaini kwa mwaka sawa na kuingiza kipato cha shilingi milioni mbili na laki nne kwa mwaka kutoka kwenye kuku mmoja.
Amesema mkoa utakapoanza wageni wanaohitaji kula kuku wataongezeka mara dufu ya sasa na bei itaongezeka mara mbili ya sasa,
“Mnapopita mjini fikeni nyumbani kwangu muone kuku ninaofuga ni wakubwa na ni wengi na nikiwaingiza sokoni sikosi shilingi elfu kumi na tano taslimu” alisema mkuu wa wilaya
Ametoa mfano wa mhe. Waziri Mkuu Mhe. Pinda ambaye anafuga nyuki ambao ni wadudu lakini wana faida kubwa kwa mfugaji na mlaji wa asali kwani hivi sasa bei ya lita moja ya asali ni shilingi elfu kumi wakati mzinga mmoja unaweza kutoa lita arobaini za asli kwa msimu mmoja tu sawa na kuwa utaweza kuvuna shilingi laki nne za mauzo ya asali kwa msimu mmoja, je kwa mwenye mizinga kumi atapata kiasi gani kwa msimu ihali hana gharama ya kuwalishia wala kuweka dawa
Ametoa wito mkwa wananchi kuanza kuzitumia fursa zilizopo za shughuli za kiuchumi ili kusaidia kuwa na miradi inayoweza kusaidia kuondokana na kero za ukosefu wa kipato
Aidha amewasihi wananchi kuanza kujiandaa kwa sense ya watu na makazi itakayofanyika mwezi Agosti mwaka huu kwani tayari maandali yameanza kufanyika na shughuli za msingi za maandalizi ya sense zimekamilika bado mambo machache.


TUMIENI MAJIKO RAFIKI WA MAZINGIRA - MAKAMU WA RAIS
WAKAZI wa mkoa wa Rukwa wametakiwa kutumia majiko yanayotumia kuni na mkaa kidogo ili kupunguza uharibifu wa mazingira katika mkoa huo
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr Mohamed Gharib Bilal, alitoa rai hiyo jana katika mkutano wa Hadhara katika uwanja wa kumbu kumbu ya Nelson Mandela mjini Sumbawanga
Alisema hivi sasa mkoa wa Rukwa umeanza kupoteza misitu mingi kutokana na kushamiri kwa vitengo vya uharibifu wa mazingira katika maeneo mengi ya mkoa huo vinavyochangiwa na shughuli mbali mbali za binadamu
Alisema kuchoma moto kiholela kunachangia sana kuua mbegu za miti na misitu mingi kuendelea kuteketea kwani miti iliyopo nayo inaendelea kuteketezwa na wachoma mkaa pamoja na matumizi ya kuni kwa ajili ya kupikia.
“hivi sasa ukipita katika maeneo karibu yote vijijini hasa vijiji vya wilaya ya Sumbawanga kumebaki upara licha ya kuwa maeneo hayo yalikuwa na misitu minene tena ya kutisha” alisema Dr Bilali
Alisema umefika wakati wananchi wa Rukwa waanze kubadili tabia na kuona suala la uharibifu wa mazingira kuwa ni sawa na janga la mkoa mzima na lianze kushughulikiwa kwa mikakati maalumu itakayosimamiwa vema na kupunguza uharibifu uliopo sasa.
Alisema kuwa moto kichaa ni moto ambao unachomwa pasipo misingi ya kiutaalamu kwani hata wanaosafisha mashamba wanatumia kuchoma moto na kuuacha unaendelea kuangamiza misitu mingine
Katika mkoa wa Rukwa kumekuwa na utamaduni wa kuchoma moto hasa nyakati za kiangazi kwa lengo la kuwinda, kuchimba panya, kusafisha mashamba baada ya kuvuna mazao pamoja na kutenga maeneo ya kuchungia mifugo yao.
Maeneo yaliyoathirika na uharibifu wa mazingira kwa kiwango kikubwa ni pamoja na wilaya ya Nkasi, Sumbawanga vijijini , wilaya ya kalambo na kata za Inyonga, Kasokola, Mpanda mjini, Magamba, Nsimbo, Uruila na Mtapenda katika wilaya ya Mpanda.
MWISHO
MKOA WA KATAVI NA FURSA ZINAZOPATIKANA: MKUU WA WILAYA ATEMBELEA KATA ZA H/MJI
 Pia fungua www.sumiampanda.blogspot.com