Sunday, February 24, 2013

SABABU 17 ZA KUFELI F. II NA F. IV 2012

SAKATA LA MITIHANI KIDATO CHA NNE TAHOSA YAIBUKA NA SABABU 17.
Mwalimu Maria Rustus, mkuu wa shule ya sekondari Kwela
akichangia mada katika mkutano wa TAHOSA Rukwa na Katavi mjini Mpanda
kikao kilichoibuka na sababu 17 za kufeli wanafunzi 2012
Mwenyekiti wa TAHOSA mkoa wa Rukwa ambaye ni mkuu wa
Shule ya sekondari Milala, Augustino Chasilla akisoma tamko la kikao
cha TAHOSA Rukwa na Katavi kulia ni Afisa elimu wa Mkoa wa Katavi
Ernesti Hinju


Mwenyekiti wa TAHOSA mwalimu Augustino Chasilla akihitimisha
kikao cha siku mbili cha TAHOSA kilichoketi Februari 22 na 23, 2013
katika ukumbi wa Idara ya maji mjini Mpanda katika mkoa wa Katavi

Taarifa ya sababu za kufeli wanafunzi wa kidato cha pili na cha
nne mwaka 2012, waraka uliotolewa na TAHOSA


Tamko la TAHOSA Rukwa na Katavi kuhusu kufeli kwa wanafunzi
katika mitihani ya kidato cha pili na cha nne 2012 lililotolewa na
wakuu wa shule Rukwa na Katavi mjini Mpanda


Umoja wa wakuu wa shule za Sekondari nchini katika mikoa ya Rukwa na Katavi umetoa sababu kumi na saba za kufeli kwa wanafunzi wa kidato cha nne nchini katika mtihani wa mwaka jana pamoja na kulaani ujumbe wa maandishi katika simu za mikononi unaowapongeza walimu kwa kufanikisha azima yao

Hayo yamebainishwa katika kikao cha wakuu hao wa shule za sekondari nchini TAHOSA wanaotoka katika mikoa ya Rukwa na Katavi kilichofanyika kwa siku mbili februari 22 na 23 kwenye ukumbi wa Idara ya Maji mjini Mpanda katika mkoa wa Katavi uliopelekea wakuu hao wa shule kuibuka na sababu 17 za kufeli wanafunzi wa kidato cha nne nchini.

Katika kikao hicho cha kikatiba wakuu wa shule waliorodhesha orodha ya mambo ambayo wanaona ni sababu za kufanya vibaya katika mitihani yao wanafunzi waliomaliza kidato cha nne mwaka jana 

Baadhi ya mambo yaliyoko katika muhtasari wa kikao chao uliopatikana jumamosi usiku februari 23, 2013 mjini Mpanda chini ya kichwa cha habari “Sababu zilizosababisha kufeli wanafunzi wa kidato cha pili na cha nne mwaka 2012” ni haya hapa

Imeelezwa kuwa sababu mojawapo ni mwamko mdogo wa elimu kwa baadhi ya wazazi na walezi hali inayopelekea ufuatiliaji finyu wa maendeleo ya watoto wao, kutochangia michango na kutotoa mahitaji muhimu kwa wanafunzi hasa mahitaji ya shule

Muhtasari huo umeelezwa kuwa nidhamu mbaya ya wanafunzi inachangia kwa kiwango kikubwa kufeli kwa wanafunzi hasa katika utoro wa reja reja na wa kudumu pamoja na upungufu wa walimu mashuleni unapelekea mada za masomo mengi kutoisha na wakati mwingine baadhi ya masomo hayakufundishwa miaka yote mine

Wakuu hao wa shule waliitaja tabia ya siasa kuingilia taalumu ya elimu kuwa kikwazo pia kilichochangia ufaulu duni wa wanafunzi ambapo wamelalamikia tabia ya baadhi ya wanasiasa wanaotoa maagizo ya vitisho kwa walimu na watendaji wa elimu na hivyo kupunguza ari na moyo wa kufanya kazi kwa ufanisi

Tatizo sugu la maslahi ya walimu na stahili limeelezewa kwa kina kuchangia katika matokeo duni ya mitihani hiyo ambapo imeelezwa stahili za walimu aidha zinacheleweshwa kupatikana au kutolewa kwa upendeleo na hivyo kupunguza morali wa kazi na kujenga makundi ya wenye uswahiba na wakubwa na wasiona na uswahiba nao

Uandaaji wa mitihani nao umetajwa katika mkutano huo kuwa ulichangia kwa kiwango kikubwa kufelisha wanafunzi mwaka jana hasa katika matumizi ya “Table of Specification” katika maandalizi ya mitihani ambapo wamebainisha kuwa walimu waliopo kazini hivi sasa hawakuiva ipasavyo katika matumizi ya jedwali hilo kutokana na mhamo wa ruwaza (paradigm shift)

Uwezo mdogo wa baadhi ya walimu katika ufundishaji umetajwa kuchangia kufeli kwa wanafunzi mwaka jana na hivyo wakuu hao kupitia TAHOSA walipendekeza walimu wapiti stashada kabla ya kuanza masomo ya shahada ya ualimu ambapo sababu nyingine imetajwa kuwa ni ufahamu mdogo wa lugha ya kiingereza katika ufundishaji na ujifunzaji ambapo walipendekeza kuwepo kwa vitabu vya kutosha vya kiingereza kama ilivyokuwa wakati wa British Council.

Ongezeko la wanafunzi na kupelekea madarasa kuwa na idadi kubwa ya wanafunzi kuliko inavyopaswa kuwa ni chagizo la kufeli kwa wanafunzi mwaka 2012 ambapo wakuu hao walipendekeza kuwa ifuatwe miongozo inayoelekeza kuwa idadi ya wanafunzi katika darasa moja iwe ni wanafunzi 40 tu ili kurahisisha ufuatliaji wa maendeleo ya mwanafunzi kwa walimu darasani.

Alama za ufaulu wa kuingia kidato cha kwanza kushushwa sana kunasababisha udahiri wa wanafunzi walio na uwezo mdogo kiakili na hivyo kusababisha ufaulu wa kidato cha pili na nne kushuka sana ambapo waliainisha alama za sasa kuwa ni 70/250 ni sawa na 28%,  au alama 100/250 ni sawa na 40% hivyo walipendekeza alama ya ufaulu iwe 125/250 ambayo ni sawa na 50%

Wingi wa vitabu vya kiada ambavyo wakuu hao wa shule za sekondari waliuita “Utitiri” unapelekea kutofautiana katika upokeaji wa maarifa mapya na hivyo ufaulu kubaki duni tu ambapo walipendekeza kuwa uteuzi wa vitabu vya kiada ufanywe na vitumike nchi nzima vitabu teule vya kiada.

Aidha wakuu hao wa shule walibainisha kuwa madhara ya Sayansi na Teknolojia kwa wanafunzi ni makubwa na yanapelekea ufaulu duni kwa wanafunzi ambapo wanafunzi wamekuwa wakitumia muda mwingi kutizama runinga, internet na matumizi ya simu na hivyo TAHOSA ilipendekeza kuundwa kwa sheria ya kusimamia mambo hayo hata kama ni nyumbani kwao

Katika kikao hicho wakuu walieleza kuwa mfumo wa elimu ya shule za kata unachangia kwa kiasi kikubwa kuwa na matokeo duni ya mitihani kwani hivi sasa wanafunzi wa shule moja ya msingi wanatumika kujaza shule moja ya sekondari na kupelekea ushindani duni wa kitaaluma hivyo walipendekeza kuwepo na utaratibu wa kuwachanganya wanafunzi kutoka kata moja na nyingine 

Baraza la mitihani la Taifa limenyoshewa kidole nalo kwa kuteua watia alama (makers) waiostahili kwa misingi ya kujuana ambapo walipendekeza uteuzi ufuate uwezo wa mwalimu katika somo analofundisha na usiwepo upendeleo ambapo katika kushusha kiwango cha ufaulu pia Wizara ya Serikali za Mitaa nchini TAMISEMI imehusishwa na kuelezewa kuwa upo mgongano wa watunga sera hivyo TAHOSA imependekeza kuwa TAMISEMI na Baraza la Mitihani (NACTE) wakae pamoja na kurekebisha kasoro zinazojitkeza

Msukumo wa ndani wa kujifunza kwa wanafunzi siku hizi ni mdogo sana kwa hali hiyo wanafunzi wengi hawajitumi kujifunza na kujipatia maarifa wanapokuwa shuleni na hata nyumbani ndiyo maana wanakosa maarifa ya kutosha na kuwawezesha kufanya vema katika mitihani 

TAHOSA imeishauri serikali kuangali upya utaratibu wa kuvunja masomo katika kipindi cha mambo mtambuka ya Kitaifa kama sense na uchaguzi ambapo imependekeza kuwa kama ikiwezekana shughuli hizo zisivunje ratiba za masomo na inapobidi shughuli hizo zifanyike katika vipindi vya likizo za wanafunzi

TAMKO








TUKO MAKINI; Wajumbe wa TAHOSA Rukwa na Katavi
Katika kuhitimisha kikao cha TAHOSA mikoa ya Rukwa na Katavi kilichoketi kwa mjini Mpanda mkoani Katavi mkuu wa shule ya sekondari ya Milala, Augustino Chasilla alitoa tamko la pamoja na TAHOSA Rukwa na Katavi kuwa TAHOSA inatambua kuwa suala la kufeli wanafunzi mwaka jana ni suala mtambuka kwa walimu, wazazi, serikali na wadau wengine wanohusika na elimu ambapo alisema TAHOSA Rukwa na Katavi inalaani vikali ujumbe (massage) mfupi unaopongeza walimu kwa ufaulu mdogo katika matokeo ya mitihani kidato cha pili na cha nne 2012 kwa hali hiyo TAHOSA inaahidi kuendelea kuendeleza taaluma nchini na kuwa inaomba ushirikiano kutoka kwa wadau wengine wa elimu nchini ili kuboresha elimu katika kujenga jamii yenye fikra chanya nchini.










WAJUMBE








MKUU WA SHULE YA SEKONDARI MAZWAI KATIKA MANISPAA YA SUMBAWANGA, REGINALD KAUZENI, KATIBU MSAIDIZI WA TAHOSA RUKWA AKIHOJIWA NA WANAHABARI MJINI MPANDA FEBRUARI 22, 2013

MWAL MARIA RUSTUS, MKUU WA SHULE YA SEKONDARI KWELA SUMBAWANGA AKIJITAMBULISHA UKUMBINI KATIKA KIKAO CHA TAHOSA RUKWA NA KATAVI







AUGUSTINO CHASILLA, MKUU WA SHULE YA SEKONDARI MILALA, MWENYEKITI WA TAHOSA RUKWA



VENANCE NYANG'WALE, AFISA ELIMU SEKONDARI HALMASHAURI YA WILAYA YA MPANDA MKOANI KATAVI AKISALIMIA WAJUMBE WA TAHOSA RUKWA NA KATAVI


AFISA ELIMU MKOA WA KATAVI, ERNEST HINJU AKIFUNGUA KIKAO CHA SIKU MBILI CHA TAHOSA RUKWA NA KATAVI MJINI MPANDA

AJALI HII HII IRINGA USIKU WA LEO NI 

Ajali  mbaya  imetokea  mjini Iringa  eneo la Makosa ama CRDB ya  zamani kwenye barabara  kuu ya Iringa _Dodoma baada ya gari aina ya RAV 4 yenye namba T 319 AFL kuhama njia na  kuigonga  Taxi yenye namba  za usajili T 510 AYU yenye namba  za  usajiliRAV iliyokuwa  ikiendeshwa na dereva Kavin Kaduma.
Ajali  hiyo  imetokea majira ya saa 10 usiku wa  leo  wakati  dereva  wa RAV4 hiyo akitoka maeneo ya mji  wa Iringa akielekea  mwelekeo ambao wakazi  wa mji wa Iringa wamekuwa  wakipata  starehe zao eneo la  Dragon Bar na Club  Twistas  kuendelea  kumalizia starehe za mwisho  wa  wiki.
Mashuhuda  wa  tukio  hilo  wameueleza mtandao huu  wa www.francisgodwin.blogspot.com  kuwa gari hiyo aina ya  RAV 4 ilikuwa katika mwendo mkali mfano  wa gari  lililopo katika mashindano na  hivyo dereva  wake  kushindwa kukata kona ya mnala  wa Manispaa ya Iringa  na hivyo  kugonga ukuta  wa  barabara hiyo  kabla ya  kuhama na kuigonga Taxi hiyo kwa  kuipanda  juu .

Hata  hivyo  mashuhuda hao   walisema  kuwa  dereva  huyo  wa RAV 4 alikuwa anaonekana  kulewa zaidi kutokana na mazingira  ambayo alikuwa akionekana kuwa ni mtu ambae amepata pombe kiasi

Japo  baadhi yao  wakidai  kuwa yawezekana  hata  dereva Taxi iliyogongwa  pia alikuwa amelewa . 
(Habari hii ni kwa mujibu wa www.francisgodwin.blogspot.com)

  CHONDE ! CHONDE! ULEVI.......!!!? NOOOMA!!!!?

 Mwananchi  mkazi  wa Manispaa ya  Iringa  akipita  jirani na ajali mbaya ya magari kugongana eneo Makosa ama la CRDB ya  zamani katikati ya mji  wa Iringa  kwenye barabara ya Iringa -Dodoma chanzo cha ajali  hii  ni unywaji  pombe  kupita kiasi
 Naibu meya  wa Manispaa ya Iringa Gravas Ndaki akishangaa ajali ya karne yenye maajabu makubwa kwa mkoa  wa Iringa  ,ajali  iliyotokea  usiku wa leo eneo la Hoteli ya kati (makosa) au CRDB ya  zamani katika barabara ya Iringa -Dodoma,hakuna majeruhi  wala aliyepoteza maisha
 Askari  wa usalama barabara  nao  washangaa kuona ajali  kama hii katikati ya mji 

DEREVA ASIMULIA AJALI ILIVYOTOKEA IRINGA
Dereva  aliyegongwa na gari aina ya RAV 4 yenye namba T 319 AFLBw  Kalvin kaduma ambae  alikuwa akiendesha Taxi yenye namba  T 510 AYU amejitokeza kuelezea  chanzo  cha ajali  hiyo na jinsi ambavyo alivyonusurika kifo.

Kaduma anasema  kuwa alishuhudia  gari hilo RAV 4  hiyo  ikija kwa mwendo wa kasi na ndipo alipoamua  kusimama ili  kushuhudia na ghafla alijikuta akifunikwa na RAV 4 hiyo.

Alisema  kuwa  RAV 4 hiyo  iliruka  ukingo la  barabara  ambao  una michongoma na kujengwa kwa  sementi na kutua  juu ya Taxi yake na kushindwa  kuendelea na  safari na kuwa  iwapo asingesimama kuona mtiti wa gari hilo basi dereva huyo wa RAV4 angekufa kwa  kugonga nyumba iliyopo jirani ambayo ina hoteli ya Hast Tast .

Hata  hivyo amesema hana mchumbuko  wowote na kuwa  dereva huyo wa RAV 4 kwa sasa anashikiliwa na  polisi baada ya  kushindwa  kukimbia kutokana na pombe
 Gari aina ya  RAV4  ikiwa  juu ya Taxi yenye namba  za usajili T510 AYU ambayo  imefuatwa  upande  wake na  kugongwa na RAVyenye namba T 319 AFL  iliyoruka ukuta  upande  wa pili na kuigonga Taxi  hiyo
 wananchi  wakitazama ajali  hiyo ya aina  yake  kutokea  mkoani Iringa