RC Katavi anena, SUMATRA yawa mbogo
Wananchi wasema tumeumizwa sanaaaa
basi likopolewa mtoni na mtambo |
Basi la Sumry lenye namba T909AZT mara baada ya kuondolewa mtoni Sitalike maarufu kama nyumba ya VibokoJulai 5, 2013 |
Kijidaraja chembamba kinachodaiwa kusababisha ajali tisa tangu Januari 2013 hadi Juni 2013 |
Baadhi ya majeruhi wahanga wa ajali ya Basi la Sumry iliyotokea Sitalike katika mto Iku Julai 5, 2013 majira ya saa 7:30 usiku |
KATIKA hali isiyo ya kawaida basi la kampuni ya Sumry
limetumbukia mtoni na kuuwa watu tisa na kujeruhi abiria wapatao hamsini na
tatu katika mto Iku uliopo katika kijiji cha Sitalike wilaya ya Mlele mkoani
Katavi
Tukio hilo la kusikitisha lilitokea saa sita usiku
kuamkia Julai 5, 2013 basi hilo lilipokuwa likitokea mjini Sumbawanga kuelekea
Mpanda mkoani Katavi likiwa na abiri waliokuwa wametoka Mbeya
Kaimu Kamanda wa Polisi mkoani Katavi Emanuely Nnley
alisema jana kuwa ajali hiyo ilihusisha basi aina ya Nissan Diesel lenye namba
T909 AZT mali ya kampuni ya Sumry lililokuwa likiendesha na dereva aliyetajwa
kwa jina na Stephano Chimane maarufu kwa jina la Ntungu
Alisema basi hilo lilipofika katika daraja hilo lenye
kona kali na mteremko dereva wake alishindwa kulimudu na kulenga daraja hali
iliyosababisha tairi za nyuma kupanda juu ya ukingo na kudumbukia mtoni ambapo
dereva wa basi hilo aliweza kutoka na kukimbilia kusikojulikana
Alifafanua kuwa juhudi za uokoaji zilianza kufanyika
usiku huo huo ambapo majeruhi 53 waliokolewa na maiti tisa za wanaume watatu na
wanawake watano na motto mmoja wa kike ziliopolewa katika maji
Alisema hali ya majeruhi inaendelea vizuri isipokuwa
majeruhi watatu walikimbizwa katika hospitali ya mkoa wa Rukwa kwa matibabu
zaidi na kufafanua kuwa chanzo cha ajali hiyo ni uzembe wa dereva kushindwa
kuliongoza gari, ubovu wa gari na wembamba wa daraja
Akizungumza na gazeti hili Afisa Mwandamizi wa SUMATRA
mikoa ya Rukwa na Katavi, David Chiragi alisema basi hilo lilikuwa limeiba njia
kwani leseni yake inaliruhusu basi hilo kufanya safari za Sumbawanga Kirando na
siyo Sumbawanga Mpanda kwa mujibu wa leseni iliyotolewa mwezi Juni mwaka huu
Alisema hata upana wa daraja ilipotkea ajali hiyo ni
mdogo sana ambapo vipimo vinaonesha daraja hilo lina upana wa mita 3.5 (tatu na
nusu) tu wakati basi lina upana wa mita nne na nusu hivyo kujenga mazingira ya
ugumu wa dereva kulenga daraja inapotokea msukosuko wa aina yoyote hasa wakati
wa usiku na hivyo kuwataka wakala wa barabara mkoani Katavi kuangalia namna ya
kupanua daraja hilo na kuboresha eneo hilo
Alisema katika kipindi cha Januari hadi July 2013 zaidi
ya ajali tisa zimetokea katika daraja hilo zikihusisha magari makubwa saba na
madogo mawili kutokana na madereva kushindwa
kumudu magari yao na kulenga daraja hilo
Alisema pia basi hilo lina makosa ya kutembea nje ya
ratiba, kuiba njia na kuzidisha abiria hivyo ofisi yake imechukua hatua ya
kuvunja safari za mabasi ya kampuni ya Sumry za mchana na badala yake mabasi
yote yataondoka Sumbawanga na Mpanda majira ya asubuhi pekee
Baadhi ya majeruhi wa ajali hiyo wakiongea kwa tabu
katika hospitali ya wilaya ya Mpanda jana walisema kuwa dereva wa basi hilo
alikuwa akiendesha kwa mwendo wa taratibu sana tangu mwanzo wa safari hali
iliyowapa shaka kuwa huenda alikuwa hajui kueondesha magari au basi hilo
lilikuwa na hitilafu kwani waliondoka mjini sumbawanga majira ya saa kumi na
moja jioni na kufika eneo hilo saa saba na nusu usiku tofauti na mwendo wa
kawaida ambapo walitakiwa kufika saa nne usiku eneo hilo.
Kondakta wa basi lililopata ajali alisema kuwa dereva
huyo alikuwa mgeni wa njia pia alikuwa hajazoea kuendesha mabasi aina ya Nissan
Diesel hali iliyomlazimu kumuelekeza njia wakati wote wa safari lakini
ilipofika eneo la mteremko wa mto Sitalike Iku alimueleza kuwa mbele kuna
daraja jembamba na kona kali dereva huyo alibadili gia ikagoma na kuanza
kuporomoka hadi mtoni.
Mkuu wa mkoa wa Katavi Dr Rajabu Rutengwe alitoa rambi
rambi kwa wafiwa wote na kuwapa pole wahanga wa ajali hiyo mbaya kutokea tangu
mkoa huo uanze.
Mganga mkuu wa wilaya ya Mpanda Mkoani Katavi, Dr Emanuely Kamgobe akifafanua jinsi walivyoweza kumudu kuwahudumia wahanga wa ajali |