Monday, December 10, 2012

MIAKA 51 YA UHURU WA TANGANYIKA

Miaka 51 yawatoa jela wafungwa 3,814,sherehe uwanja wa taifa nazo zanoga


Baraza la mawaziri na wawakilishi wa mataifa ya nje nchini


Wale wanaokumbukaSharo milionea katika mkasa wa kukabidhiwa mikoba aliona mkia wakerewe hawa walifanya  mambo

Warembo kutoka nchi jirani ya Rwanda walifika kuwakilisha  uzuri katikia maonesho ya miaka 51 ya Uhuru

Hata kama uko jukwaani na jana uliwaona lazima uwasalimie:Jk akisalimiana na baadhi ya wakuu na wageni wengine waliofika kutupa tafu miaka 51
RAIS Jakaya Kikwete na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama nchini, ametoa msamaha kwa wafungwa 3,814 wakiwemo wenye magonjwa yasiopona na wanawake wajawazito.
Hata hivyo msamaha huo uliotolewa kuadhimisha Miaka 51 ya Uhuru wa Tanzania, hauwahusu wafungwa wenye makosa ya ubakaji, ulawiti, kuwapa wanafunzi mimba, waliotumia madaraka vibaya na wala rushwa.
Taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa leo na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi imeeleza kuwa, Rais Kikwete ametekeleza hilo kwa kutumia madaraka aliyonayo chini ya Ibara ya 45 (1) (d) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, wafungwa waliohusika na msamaha huo ni waliothibitika kuwa na ugonjwa wa Ukimwi, Kifua Kikuu (TB) na saratani ambao wako katika hali mbaya, wazee wenye umri wa miaka 70 na kuendelea.
“Wamo waliopatikana na hatia na kuhukumiwa kuwepo gerezani kwa ridhaa ya Rais wa Tanzania chini ya kifungu cha 26 cha Kanuni ya Adhabu, ambao hadi Desemba 9, mwaka huu wamekaa gerezani si chini ya miaka mitano na wamekuwa na tabia njema,” alisema Dk Nchimbi.
Wengine ni wafungwa wanawake walioingia na mimba au na watoto wadogo gerezani, wenye ulemavu wa mwili na akili, wanaotumikia kifungo kisichozidi miaka mitano na ambao walishatumikia robo ya kifungo chao.
Dk Nchimbi alisema kuwa, kutokana na madaraka hayo, Rais Kikwete ametoa msamaha huo kwa wafungwa 3,814 na kwamba wafungwa wenye matatizo maalum kati ya waliosamehewa, wamethibitishwa na jopo la madaktari chini ya Uenyekiti wa Mganga Mkuu wa Mkoa au Wilaya husika.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, msamaha huo hauwahusu wafungwa waliohukumiwa kunyongwa, kifungo cha maisha, waliofungwa kwa kujihusisha na dawa za kulevya, waliotoa au kupokea rushwa na wenye makosa ya unyang’anyi wa kutumia silaha na wizi wa magari kwa silaha.
Pia hauwahusu waliopatikana na makosa ya kunajisi, kubaka na kulawiti, waliowapa wanafunzi mimba, walioharibu miundombinu kama kuiba nyaya za simu, umeme au mafuta ya transformer na waliokutwa na silaha au risasi.
Dk Nchimbi alisema wengine wasiohusika ni wafungwa wazoefu wanaotumikia kifungo cha pili na kuendelea, waliowahi kupewa msamaha lakini wanatumikia sehemu ya kifungo kilichobaki, waliowahi au kujaribu kutoroka na waliotumia madaraka vibaya.
Wengine ni waliohukumiwa kwa kosa la kuzuia watoto kusoma na wale wanaotumikia kifungo chini ya Sheria namba 25 ya mwaka 1994 ya Bodi ya Parole na  Sheria ya Huduma kwa Jamii namba 6 ya mwaka 2002.
Katika maadhimisho ya Miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania mwaka jana, Rais Kikwete alitoa msamaha kwa wafungwa 3,803 na mwaka 2010 katika shehere kama hizi alisamehe wafungwa 3563.
Mwisho.

Saturday, December 8, 2012

MTUHUMIWA WA MAUAJI YA MWANGOSI MBADO

MTUHUMIWA WA MAUWAJI YA MWANGOSI AKWAMA MAHABUSU TENA

Huyu ndie mtuhumiwa wa mauwaji ya Daudi Mwangosi


MTUHUMIWA wa mauaji ya aliyekuwa mwandishi wa habari wa kituo cha runinga cha Channel Ten Daud Mwangosi aliyetakiwa kufikishwa mahakamani kwa mara nyingine kutokana na sababu ya magari ya kubebea mahabusu kukosa mafuta.

Mwandishi  wa mtandao huu  kutoka  Iringa  Gustav Chahe anaripoti kuwa ,Askari wa kikosi cha kuzuia ghasia wengine waliokuwa na silaha mbalimbali huku wengine wakivaa kiraia waliweka ulinzi mkali kuhakikisha waandishi wa habari hawapati mwanya wa kupiga picha.

Mwendesha mashtaka wa serikali Adolf Maganda aliambia mahakama mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi Dyness Lyimo kuwa mtuhumiwa hakufikishwa mahakamani kutokana na magari ya kuwabeba mahabusu yamekosa mafuta.

Hata hivyo Maganda alisema upelelezi haujakamilika na kesi imeahilishwa hadi 19 Desemba mwaka huu.

Pasificus Cleophace Simon (23) alifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi kwa tuhuma ya kumuua kwa makusudi mwandishi huyo katika ufunguzi wa matawi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA katika kijiji cha Nyololo Wilaya ya Mufindi Mkoa wa Iringa uliofanyika Septemba 2 mwaka huu.

Siku ya kwanza mtuhumiwa huyo alifikishwa mahakamani hapo kwa gari la kifahari lenye namba za kiraia T 320 ARC linalosadikiwa kuwa ni la RCO huku kwa mara ya pili akifikishwa kwa miguu na kuondolewa mahakamani hapo kwa gari namba DFP 2175 pick up akiwa katika ulinzi mkali huku waandishi wa habari wakidhibitiwa na polisi na mmoja wao kunusurika kupigwa jambo lililozusha hisia tofauti miongoni mwa wananchi wengi mkoani hapa.

Hii ni mara ya pili kwa mtuhumiwa huyo kutokufikishwa mahakamani kutokana na sababu ya magari kukosa mafuta japo kuwa kwa wakati huu hakuna tatizo la mafuta kama kipindi cha mwanzo.

Mwangosi aliuawa kwa bomu Septemba 2 mwaka huu katika kijiji cha Nyololo yo alipokuwa akiwajibika kwa kazi za kihabari wakati wa ufunguzi wa matawi hayo.

Wednesday, December 5, 2012

TAFAKURI KATIKA JAMII




MAWAZIRI NA SEMI ZAO NCHINI

WAZIRI MWAKYEMBE AWAFUKUZA KAZI VIONGOZI TPA


                                                       Dr Mwakyembe


Waziri wa Uchukuzi Dr Harrison Mwakyembe  amewaafukuza kazi  EPHRAIM MGAWE, na Naibu wake Bwana JULIUS MFUKO kufuatia ripoti iliyotolewa na tume maalum ya kuchunguza hali ya uendeshwaji wa bandari hiyo na kuonyesha kuwa watendaji hao wamekosa umakini pamoja na kufanya uzembe uliopitiliza.


Akisoma ripoti hiyo Dokta MWAKYEMBE amesema kuwa Viongozi hao wameshindwa kuonyesha umaridadi wa kuisimamia bandari hiyo, hali iliyopelekea kuisababishia Hasara kubwa Serikali sambamba na kushusha hadhi ya Bandari ya Dar es Salaam, hadi kufikia hatua ya kutajwa kama Bandari isiyoingiza faida yoyote miongoni mwa Bandari 36 za barani Afrka.

Katika Hatua nyingine Dokta MWAKYEMBE ametangaza kuwafukuza kazi Meneja Mkuu wa Bandari hiyo KASSIAN NGAMILO pamoja na Meneja wa kitengo cha Mafuta CAPTAIN TUMAINI MASSAWE, kufuatia kushindwa kusimamia ipasavyo mikataba mbalimbali ya uondoshaji wa mafuta machafu bandari hapo sambamba na uzembe uliopitiliza.

Hata hivyo Dokta MWAKYEMBE amebainisha kuwa Wizara yake haitamvumilia mtendaji yeyote kutoka idara ama taasisi iliyo chini ya Wizara hiyo ambaye utendaji wake utaonekana kulega lega, na kusabaisha Serikali kupata hasara pasipo sababu za Msingi.

Kufukuzwa kwa Viongozi hao ni miongoni mwa utekeleza wa uboreshaji wa Bandari ya Dar es Salaam ambayo imeshika nafasi ya Mwisho kwa uingizaji faida katika Bandari 36 za Bara la Afrika hii ni ikiwa ni Ripoti iliyotolewa hivi karibuni.
HABARI HII NI KUTOKA MTANDAO WA www.francisgodwin.blogspot.com

NAIBU WAZIRI ALIYETIKISA RUKWA KESHO KUANZA ZIARA KATAVI KESHO




NAIBU waziri wa Tawala za Mikoa na serikali za Mitaa nchini, Aggrey Mwanri baada ya kufanya ziara na kuibua mambo mazito ikiwa ni pamoja na kigugumizi ya Manispaa ya Sumbawanga kuwasha umeme katika stendi kuu ya mabasi mjini humo anatarajia kuanza ziara kama hiyo mkoani Katavi ambako atatembelea, kukagua na kuweka mawe ya msingi katika miradi mbalimbali ya maendeleo.

Taarifa zinasema kuwa waziri huyo ambaye amefanya ziara ya siku tisa mkoani Rukwa atafanya ziara mkoani kKatavi katika Halmashauri zote kuanzia Januari 16, 2013 hadi Januari 21, 2013 ambapo atafanya kazi kubwa ya kukagua miradi, kuweka mawe ya msingi katika miradi kuzindua na hatimaye atakuwa anafanya mikutano ya hadhara.

Naibu Waziri Mwanri amekuwa na tabia ya kukagua miradi kwa vitendo ambapo akiwa mjini Sumbawanga aliweza kukagua upana wa barabara kwa kutumia tepu ya kupimia na kukagua uimara wa sakafu na kuta za majengo aliyoakagua kwa kutindua na tindo kwa kutumia tindo na nyundo vitendo ambavyo vimejenga dhana ya uwajibikaji kwa watendaji wa halmashauri na manispaa

Akiwa katika mkoa wa Katavi Mhe. Mwanri atatembelea wilaya mbili za Mlele na Mpanda zinazounda halmashauri nne ambazo ni Halmashauri ya wilaya ya Mlele, halmashauri ya wilaya ya Mpanda, Halmashauri ya Nsimbo na halmashauri ya mji Mpanda.

Katika blog hii tutajitahidi kukuletea yatakayojiri katika ziara hiyo kwa wakati ili uweze kuelewa nini kimefanyika.

WASIRA: KILIMO KWANZA KUUFIKISHA UCHUMI MIFUKONI MWA WANANCHI

 

                                                              Waziri Wasira

 NA MWANDISHI WETU
UHALISIA wa kukua kwa uchumi hadi mifukoni mwa wananchi walio wengi una matumaini ya kufikiwa kutokana na
utekelezwaji  madhubuti wa kuinua Kilimo kupitia mpango wa Kilimo Kwanza unayotekelezwa na serikali.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Sera na Uratibu, Steven Wasira alipokuwa akizungumza kwenye
kipindi cha 'Tuongee Asubuhi' cha kituo cha televisheni cha Star Tv, leo, Januari 15, 2013.

Katika kipindi hicho, kilichokuwa na mada ya 'Uhalisia na Kukua kwa Uchumi' pamoja na Wasira wazungumzaji wengine
walikuwa, Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba na Mtaalam wa Uchumi kutoka Chuo cha SAUTI cha Mwanza, Odas Bilame.

Wasira alisema, kwa sasa wananchi wengi hawaoni uhalisia wanapoambiwa kwamba uchumi wa nchi unakuwa, kwa
sababu, hali ya kukuwa kwa uchumi kwa sasa hakujawagusa waajiriwa katika sekta ya kilimo ambao ndio wengi kiasi
cha asilimia 80.

Alisema, katika kipindi cha kati ya mwaka juzi na mwaka jana uchumi wa Tanzania ulionyesha kuwa umekuwa kwa kati
ya asilimia 6.5 na 6.7, lakini kukua huku kuliwagusa zaidi watumishi waliopo katika sekta nyingine kama za viwanda na
watumishi wa umma.

"Katika hali hii ambayo watumishi wa sekta zote wanategemea lazima wapate chakula na mazao mengine kutoka kwa
wakulima, ambao hawajanufaika vya kutosha na mafanikio ya kukua wa uchumi huu, ni lazima, athari za kutoonekana
ukuaji uchumi katika jamii utakuwepo", alisema, Wasira.

Alisema, kutokana na kutambua kwamba ni lazima sekta ya Kilimo iboreshwe vya kutosha ndipo ukuaji wa uchumi utadhihirika kwa uhakika miongoni mwa wengi, Serikali imeelekeza nguvu zake kuhakikisha mpango wa Kilimo Kwanza unazaa matunda.

Alisema, katika jitihada za kufikia lengo hilo, Serikali imetenga sh. bilioni 300 kwa ajili ya kuwekeza kwenye utafiti katika kilimo, ambapo katika uwekezaji huo, sasa wapo wataalam wengi na maofisa ugani vijijini kwa ajili ya kuwezesha wakulima kufanya kilimo bora na cha kisasa.

Wasira alisema, pia kiwanda cha mbolea cha Minjingu kimejengwa ili kuongeza upatikanaji wa mbolea ili kuhakikisha kwamba kila mkulima anapata mbolea ya kutosha na kuongeza kuwa  pamoja na kiwanda hicho Serikali inao mpango wa kujenga vingine vya mbolea ili kuongeza wigo wa upatikanaji wa pembejeo hiyo.

Alisema, wakati jitihada zimewekwa kwenye uinuaji sekta ya kilimo, ujenzi na uboreshaji miundombinu ya usafiri ikiwemo barabara na reli, utafungua milango ya mazao kutoka vijijini kwenda maeneo mbalimbali nchini hata nje ya nchi kwa urahisi, hatua ambayo itachochea kukua kwa kasi zaidi kwa uchumi.

Akielezea historia ya Uchumi wa Tanzania, Wasira alisema, awali hali ya uchumi ilikuwa ikienda vizuri, lakini ilianza kuathiriwa na uhaba wa mafuta miaka uliojitokeza miaka ya 1977 lakini ukaendelea kuathiriwa zaidi na vita vya Kagera, mwaka 1978 na hadi sasa zimeendelea kuwepo changangamoto za kidunia ambapo Tanzania kama moja ya nchi zilizomo haiwezi kuzikwepa.

Kwa upande wake Profesa Lipumba, alikiri kwamba Kilimo Kwanza ni 'muarobaini' wa kukua kwa uchumi wa nchi, lakini akaonya kwamba ni lazima juhudi za makusudi zifanyike kuhakikisha kuwa uhalisia wa kukua wa uchumi ni kuigusa mifuko ya wananchi.

Pamoja na kukiri umuhimu wa mpango wa kilimo kwanza, Profesa Lipumba aliponda kwamba, licha ya mikakati mizuri  kuwepo lakini mingi ipo katika makatarasi tu, haitekelezwi kwa vitendo.

"Sasa kama dhamira ipo, umefika wakati wa watekelezaji kuacha maneno na badala yake kufanya kazi kwa vitendo zaidi", alisema Lipumba.

Kwa upande wa nafasi ya wasomi wanavyoisadifu hali ya kukua kwa uchumi Tanzania, Odax alisema, wasomi wanakubalina kwamba juhudi zikiwekezwa kwenye kilimo uchumi utakuwa.

MAHANGA ATAKA MABADILIKO YA MITAALA ELIMU YA JUU KUKAZANIA HISABATI NA SAYANSI ZAIDI



Dr Makongolo Mahanga, Naibu Waziri wa Kazi na Ajira Tanzania

NAIBU Waziri wa Kazi na Ajira, Dr. Makongoro Mahanga ameshauri vyuo vya elimu ya juu kurekebisha mitaala yao ili kukazania zaidi masomo ya hisibati na sayansi, na pia kuhakikisha kwamba kwenye kila fani au program katika vyuo hivyo, kunakuwepo na masomo ya ujasiriamali na stadi za maisha ili kuwaandaa wahitimu kujiajiri kama hawatapata kazi za kuajiriwa. Aidha ameshauri  kwamba, kama ilivyofanywa kwa fani ya ualimu, kuwepo na program au shahada mahsusi ya ujasiriamali katika kila chuo cha elimu ya juu.

 Dr. Mahanga ametoa ushauri huo jana mjini Mtwara alipokuwa akiwahutubia wananchi wa Mtwara, viongozi na wahitimu katika chuo kishiriki cha Stella Maris kilichoko Mtwara na kinachomilikiwa na Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania. Alisema sababu kubwa ya baadhi ya wahitimu wa vyuo vikuu kukosa ajira ni pamoja na vijana hao kutotaka au kuweza kuchukua masomo ya sayansi na hisibati na pia kutotaka kuchukua fani kama ya ualimu ambazo zina fursa za uhakika za ajira. Aidha, alisema sera na mitaala ya elimu haijazingatia sawasawa mahitaji ya soko la ajira. Alisema sababu nyingine ni ukosefu wa nafasi za kujifunza elimu ya ufundi, ujasiriamali na stadi za kazi au kufanya mazoezi ya stadi za kazi ili kupata ujuzi wa aina ya ajira nzuri kwenye soko la ajira. Hivyo kuanzisha masomo au shahada ya ujasiriamali kwenye vyuo vikuu vyote ingeweza kuwa suluhisho la wahitimu wengi kukosa ajira. Alisema kwa sasa kati ya vijana zaidi ya 800,000 wanaoingia kwenye soko la ajira kila mwaka baada ya kumaliza elimu ya msingi, sekondari na vyuo vya elimu ya juu, vijana 240,000 hawapati ajira kabisa na baadhi yao ni wahitimu wa vyuo vya elimu ya juu.
> >>
> >> Dr. Mahanga, aliyekuwa mgeni rasmi kwenye mahafali hayo ya kwanza ya chuo hicho ambacho ni chuo kishiriki cha Chuo Kikuu cha St. Augustine cha Mwanza, aliwataka pia wahitimu wanaokopeshwa na Bodi ya Mikopo ya wanafunzi kurejesha mikopo hiyo wakishaanza kufanya kazi. Akitoa takwimu za mikopo ya wanafunzi, alisema kwa miaka 18 kuanzia mwaka 1994/95 ambapo mikopo hiyo ilianza kutolewa kwa wanafunzi hadi Juni 2012, Serikali imeshatoa mikopo ya shs. 1.184 trilioni kwa wanafunzi 593,712. Hata hivyo alisema kati ya mikopo ilioiva na kustahili iwe imesharudishwa na wahitimu waliokopa ni asilimia 49% tu imeshalipwa kwa Bodi.

HOTUBA CHINI

HOTUBA YA MHE. DKT. MILTON MAKONGORO MAHANGA (MB), NAIBU WAZIRI WA KAZI NA AJIRA KWENYE MAHAFALI YA KWANZA YA CHUO KIKUU CHA STELLA MARIS MTWARA (STEMMUCO), TANZANIA TAREHE 5 DESEMBA, 2012

    Mhashamu Baba Askofu Mkuu, Norbet Mtega – Mkuu wa Chuo,
  Mhashamu Baba Askofu Gabriel Mmole, Askofu wa Jimbo la Mtwara na Mwenyekiti wa Bodi ya Chuo,
    Mhashamu Baba Askofu John Ndimbo, Askofu wa Jimbo la Mbinga na Mwenyekiti wa Baraza la Chuo,
    Mhashamu Baba Askofu Bruno Ngonyani, Askofu wa Jimbo la Lindi,
    Mhashamu Baba Askofu Castor Msemwa, Askofu wa Jimbo la Tunduru Masasi,
    Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa wa Mtwara,
    Mheshimiwa Mkuu wa Wilaya ya Mtwara,
    Waheshimwa Wakuu wa Vyuo na Taasisi za Elimu,
    Mabibi na Mabwana.

Tumsifu Yesu Kristu!

Ni heshima kubwa kwangu binafsi na kwa Serikali kwa ujumla kunipa mwaliko wa kuwa Mgeni Rasmi katika tukio hili la kihistoria, tukio la mahafali ya kwanza ya Chuo hiki Kishiriki cha Stella Maris hapa Mtwara.

Kwa kunialika kushiriki tukio hili, ni ishara wazi inayoonyesha ushirikiano uliopo kati ya Serikali na Taasisi hii katika suala zima la kutoa elimu kwa Watanzania – elimu inayowajengea wahitimu uwezo kiujuzi, kiuelewa, kiutaalam, kimitazamo na kimaamuzi ili waweze kushiriki kwa vitendo kuleta maendeleo halisi ya Taifa letu.

Waheshimiwa Maaskofu, Mabibi na Mabwana,

Umuhimu wa elimu katika maendeleo ya taifa lolote haliwezi kusisitizwa zaidi.  Nchi zote ambazo zimeendelea kwa haraka duniani zimewekeza katika elimu ya watoto na vijana wake.  Tanzania vile vile imekuwa ikiwekeza kiasi kikubwa cha bajeti yake katika sekta ya elimu na kuipa kipaumbele cha kwanza kila mwaka.  Kwa mfano, katika mwaka 2010/11 Serikali ya Tanzania ilitenga shs. 2.195 trilioni kwa ajili ya sekta ya elimu, hii ikiwa ni asilimia 18.9% ya bajeti nzima ya Serikali.  Kwa mwaka 2011/12, Serikali ilitenga shs. 2.415 trilioni kwa ajili ya sekta ya elimu (asilimia 17.86%).

Kwa kushirikiana na watu binafsi na Taasisi mbalimbali likiwemo Kanisa Katoliki, Serikali inatilia maanani umuhimu wa kutoa elimu bora kwa raia. Serikali imekuwa inafuatilia kwa makini kupitia Tume na vyombo vyake vingine, utoaji wa elimu iliyo bora, elimu yenye kumkomboa mwanadamu na kumpa uwezo wa kuyatawala na kuyaboresha mazingira yake. Kwa misingi hiyo, kwa niaba ya Serikali, natoa shukrani zangu za dhati kwa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania kwa ushiriki wake wa kutoa elimu bora ya ngazi zote tangu elimu ya awali hadi elimu ya juu. Ushiriki wa Kanisa katoliki na taasisi zingine za kidini na watu binafsi katika fani ya elimu umechangia kwa kiasi kikubwa kuleta maendeleo ya Taifa letu.

Wakati ambapo kufikia mwisho wa mwaka 2010/11 vyuo vya elimu ya juu vilikuwa na jumla ya wanafunzi 139,638, vyuo vya Serikali vilikuwa na wanafunzi 104,129 huku vyuo binafsi vikiwa na wanafunzi 35,509. Hata hivyo vyuo vya elimu ya juu vya Serikali vilikuwa 11 tu kulinganisha na 21 vya binafsi. Hii ina maana kwamba vyuo binafsi vilikuwa vingi (65.6%) kulinganisha na vya Serikali (34.4%) lakini viliweza kudahili wanafunzi asilimia 25.4% tu. Kwa maana hiyo kuna haja ya vyuo binafsi kupanua miundombinu ya vyuo vyake na udahili ili viweze kuchukua wanafunzi wengi zaidi.

Maaskofu, Mabibi na Mabwana,
Ikijua na kujali umuhimu na mchango wa vyuo binafsi, Serikali, kupitia Tume yake ya Vyuo Vikuu (TCU), mnamo Desemba 2009, iliruhusu Taasisi hii ianze kutoa elimu ya juu kama kituo cha chuo kikuu cha SAUT. Miaka miwili baadaye, yaani Julai, 2011 Serikali iliipandisha hadhi Taasisi hii na kuifanya Chuo Kikuu Kishiriki.

Ikitambua uwezo mdogo wa kiuchumi wa Watanzania, Serikali kupitia Bodi yake ya mikopo imekuwa ikitoa mikopo kwa wanafunzi wa vyuo vya elimu ya juu wenye vigezo vinavyotakiwa. Kwa miaka 11 toka mikopo hii ianze kutolewa mwaka 1994/95 hadi 2004/2005, jumla ya wanafunzi 113,240 waliweza kukopeshwa jumla ya shilingi 51,103,687,000.  Lakini kwa miaka saba ya awamu ya nne ya Serikali ya Rais Jakaya Kikwete, kutoka mwaka 2005/06 hadi 2011/12, Serikali, kupitia Bodi ya Mikopo iliyoundwa mwaka 2005, ilikopesha wanafunzi 480,472 jumla ya shs. 1,133,386,869,000.

Mabibi na Mabwana,

Kama ilivyoelezwa hapa leo, chuo hiki pia kilifaidika na mikopo hii ambapo asilimia 94% ya wahitimu wake wamewezeshwa kwa njia ya mikopo hiyo. Aidha kupitia Serikali za Mitaa hapa Mtwara-Mikindani, Serikali imetoa ardhi takribani ekari 140 kwa ajili ya maendeleo ya chuo hiki. Haya yote yanaonyesha jinsi Serikali yetu inavyojali watu wake katika masuala ya elimu. Kwa niaba ya Serikali nawaahidi kwamba ushirikiano huu utaendelea kudumishwa.  

Inafurahisha na kutia moyo kuwa Chuo hiki kiliona ni vema kuanza kazi yake Mkoani Mtwara kwa kuandaa walimu wa sekondari. Tunda la kwanza la chuo ni walimu walioandaliwa kutoa elimu ya Sekondari. Elimu hii itachangia kwa kiasi kikubwa katika kuleta maendeleo ya watanzania tukizingatia kuwa zipo shule nyingi za sekondari zenye idadi ndogo ya walimu. Tukianzia na Mikoa ya Kusini, mmejionea wenyewe uhaba wa walimu uliopo. Ninawahimiza wahitimu wa leo wawe tayari kuitumia elimu yao kuchangia kuleta maendeleo ya watanzania.

Mabibi na Mabwana,

Ukosefu wa ajira bado ni tatizo kubwa nchini, hasa kwa vijana. Kati ya vijana wapatao 800,000 wanaoingia kwenye soko la ajira kila mwaka baada ya kumaliza masomo ya msingi, sekondari na vyuo vya juu, ni asilimia kama 5 tu (au vijana 40,000) ndio wanapata ajira kwenye sekta rasmi isiyo ya kilimo.  Waliobaki wanaingia kwenye ajira kwenye sekta ya kilimo, ufugaji na uvuvi (asilimia 35) na sekta isiyo rasmi (aslimia 30), huku asilimia 30 waliobaki (vijana 240,000) wakikosa kazi. Kati ya vijana wanaoingia kwenye soko la ajira na kukosa kazi, wako pia wahitimu wa vyuo vikuu. 

Sababu kubwa ya baadhi ya wahitimu wa vyuo vikuu kukosa ajira ni pamoja na vijana hao kutotaka au kuweza kuchukua masomo ya sayansi na hisibati na pia kutotaka kuchukua fani kama ya ualimu ambazo zina fursa za uhakika za ajira. Aidha, sera na mitaala ya elimu haijazingatia sawasawa mahitaji ya soko la ajira. Na pia kuna ukosefu wa nafasi za kujifunza elimu ya ufundi, ujasiriamali na stadi za kazi au kufanya mazoezi ya stadi za kazi ili kupata ujuzi wa aina ya ajira nzuri kwenye soko la ajira.

Ningependa kutoa wito kwa vyuo vya elimu ya juu kurekebisha kasoro hizi kwa kutilia maanani masomo ya hisibati na sayansi, na pia kuhakikisha kwamba kwenye kila fani au program katika vyuo vikuu vyote, kunakuwepo na masomo ya ujasiriamali na stadi za maisha ili kuwaandaa wahitimu kujiajiri kama hawatapata kazi za kuajiriwa. Aidha ningeshauri kwamba, kama ilivyofanywa kwa fani ya ualimu, kuwepo na program au shahada mahsusi ya ujasiriamali (Bachalor of Business Administration/Management in Entreprenuership) katika kila chuo cha elimu ya juu. Nimeona kwamba ingawa leo wahitimu wa chuo hiki ni wa fani ya ualimu mlioanza nayo, lakini kwa sasa mmeshaanzisha program za shahada zingine hapa chuoni.  Angalieni pia uwezekano wa kuanzisha shahada ya ujasiriamali katika mipango yenu ya baadaye.

Waheshimiwa Maaskofu, Mabibi na Mabwana,

Kabla sijamaliza hotuba yangu, nitoe wito kwa wenzetu 1,100 wanaohitimu leo katika chuo hiki cha Stella Maris kama ifuatavyo:-
•    Uadilifu kazini: Wahitimu mmefundishwa sio tu kuwa walimu bali walimu-walezi. Serikali inawatazamia kuwa mifano bora kazini kwa kuyaishi maadili ya kazi yenu. Epukeni upendeleo, rushwa na unyanyasaji. Fanyeni kazi kwa haki na ueledi wa hali ya juu.

•    Utayari wa kurudisha pesa ya mikopo: Mmesoma kwa pesa ya mikopo. Kumbukeni kulipa madeni ili wakopeshwe wengine. Tatizo la wahitimu wa vyuo vikuu kurudisha mikopo waliokopeshwa bado ni kubwa. Kwa mfano, kufikia Juni 2012, madeni ya wahitimu wa vyuo vya juu yaliyokuwa yameiva yalikuwa Tshs. bilioni 160.7 na kati yake, shs. 39.5 bilioni zilitakiwa ziwe zimeshakusanywa kutoka kwa waliokopa, lakini ni asilimia 49% tu kati ya hizo zilikuwa zimekusanywa na Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi

•    Maslahi Binafsi: Katika kazi zenu za ualimu lazima mtangulize maslahi ya wengi na wala si maslahi binafasi

•    Migomo na Vurugu: Ni muhimu mkaepuka migomo na vurugu kazini. Pale migogoro inapotokea, ni lazima mtafute suluhisho za migogoro kwa mazungumzo na pande zote zinazohusika.

•    Utayari wa kufanya kazi popote bila kubagua maeneo: Fanyeni kazi popote nchini bila kupendelea mijini au maeneo ya nyumbani kwenu. Katika risala ya chuo mmeeleza jinsi imekuwa vigumu wahitimu kufanya kazi kwenye maeneo fulani ya nchi, kwa mfano katika mikoa hii ya kusini ikiwemo Mtwara na Lindi. Kwanza sitegemei wahitimu wa chuo hiki hapa Mtwara baada ya kuzoea mazingira ya mkoa huu na ya jirani walipokuwa wakisoma, wakashindwa kufanya kazi huku baada ya kumaliza masomo yao. Lakini pia nyie wenyewe ni mashahidi kwamba Serikali imekuwa ikichukua hatua za makusudi kuboresha hali ya maisha na miundombinu ya mikoa iliyokuwa inaonekana iko nyuma kimaendeleo kama Mtwara ili wananchi wa mikoa hii na watanzania wengine wanaopangwa kufanya kazi kwenye mikoa hii wasione tofauti kubwa na mikoa mingine.

Kwa upande wa Mtwara na mikoa mingine ya kusini, ukiacha uboreshaji mkubwa wa miundombinu ya barabara, umeme na bandari, kumekuwepo vile vile uwekezaji kwenye miradi ya kiuchumi kama utafiti na uchimbaji wa gesi asilia, utafiti wa mafuta na viwanda kadhaa kama vya saruji na mbolea vinavyotarajiwa kuanza kujengwa karibuni. Yote haya yamefanya mikoa hii ianze kuwavutia hata wananchi wengine kupenda kuishi, kufanya kazi, kuwekeza na kufanya biashara katika mikoa hii.

Hapa ningependa kuwapongeza Baraza la Maaskofu Katoliki kwa kuanzisha chuo hiki hapa Mtwara na kukipa jina la Stella Maris linaloendana na maendeleo yanayoendelea kuwepo katika mkoa huu wa Mtwara. Jina hili nimeambiwa maana yake ikitafsiriwa kwa kilatini ni “Nyota ya Bahari”.  Jina hili linabeba dhana nzima ya uwepo wa chuo hiki mkoani Mtwara, kwa maana ya kuwa chimbuko la mwanga na matumaini katika misukosuko ya kimaisha, kielimu, kitaaluma na  kiuchumi. Jina hilo pia linaendana na maendeleo na uwekezaji unaoanza kuonekana hapa mkoani Mtwara kama nilivyoeleza hapo juu.
  
Waheshimiwa Maaskofu, Mabibi na Mabwana

Kwa upande wa Serikali ningependa kuahidi yafuatayo:-
   Ajira kwa walimu: Kwa kuzingatia uhitaji uliopo, Serikali inawaahidi wahitimu wa chuo hiki kupewa ajira katika fani ya ualimu, kama ambavyo imekuwa ikifanya kila mwaka kwa wahitimu wa fani hii. Kwa mfano katika mwaka 2011, Serikali ilitoa ajira 11,629 kwa walimu wa shule za sekondari kote nchini na kufanya shule hizo kuwa na walimu 52,146 mwaka 2011 kulinganisha na walimu 40,516 waliokuwepo mwaka 2010 katika shule zote za sekondari za Serikali na binafsi nchini.
  Sera nzuri kwa kazi ya ualimu: Serikali inaahidi kuendelea kuweka sera nzuri kwa kazi ya ualimu ili kuondoa kero za walimu zinazowapelekea kugoma na kuona kwamba taaluma yao haithaminiwi na Serikali.

Mwisho kabisa, niwaombe wananchi na wakazi wa Mtwara, mpokee taasisi zilizo Mtwara kama baraka na wadau wa kuleta maendeleo. Kwa misingi hiyo wapokeeni wanafunzi wasomao vyuoni Mtwara kama watoto wenu. Wapokeeni kama wapangaji kwenye nyumba zenu kwa gharama za kiungwana bila kuwadai pesa nyingi kupita uwezo wao. Wenye vyombo vya usafiri tozeni gharama za haki.

Nimalizie kwa kuwashukuru tena Baraza la Maaskofu Katoliki na uongozi wa chuo kwa kunialika kujumuika nanyi katika mahafali ya kwanza ya chuo hiki kikuu kishiriki cha Stella Maris, na niwatakie kila la heri kwenye kazi zao wahitimu wetu wa leo.


ASANTENI KWA KUNISIKILIZA

MAPAMBANO: POLISI Vs WANAHABARI TZ

POLISI WAMPIGA RISASI MWANDISHI WA HABARI MWINGINE TENA

                                                                    IGP MWEMA



Shaban Matutu
Mwanahabari mwingine  mkoani Dar es Salaam apigwa  risasi na askari  polisi ambao  wanadaiwa  kuwa  walikuwa  wakimsaka mtuhumiwa  wa ujambazi  mwanamke na kuishia kumpiga mwanahabari  huyo mwanaume  Bw  Shaban Matutu wa gazeti la Tanzania  Daima.
Tukio  hilo limetokea jana majira  ya saa 2 usiku  jijini  Dar es Salaam ambapo askari  hao walipofika  nyumbani  kwa  mwanahabari  huyo na  kumgongea mlango na  wakati akifungua mlango ndipo

 Matutu amepigwa risasi na Polisi, ambao wanadaiwa walikuwa wanamtafuta mhalifu ambapo katika zoezi hilo, walienda na kugonga chumbani kwa Mwandishi huyo, kabla ya kutwanga kwa risasi.
Taarifa zaidi zinaeleza kuwa, mara baada ya tukio hilo, mwandishi huyo amekimbizwa hospitali ya Mwananyamala ambako anaendelea kupatiwa huduma ya haraka na inaelezwa kuwa, amejeruhiwa lakini hali yake si mbaya sana
Habari zaidi zitakujieni

Taarifa za uhakika na ambazo zimethibitishwa­ zinaeleza kuwa jana usiku polisi mwenye silaha, aina ya bastola alimjeruhi begani kwa risasi, mwandishi wa habari wa Tanzania Daima, Shaaban Matutu.

Risasi bado imenasa kwenye bega lake hadi sasa Matutu alipigwa risasi nyumbani kwake Kunduchi, Dar es Salaam wakati askari walipovamia nyumba yake kwa madai kwamba kuna kibaka aliingia kujificha nyumbani hapo. Hivi sasa Matutu anatibiwa Mwananyamala hospitali, lakini amepewa rufaa kwenda Muhimbili.

Mwenyekiti  wa  jukwaa la wahariri Tanzania Bw Absalom Kibanda, ambaye amefanya jitihada za kumuhamishia Matutu Muhimbili, anasema hali ya Matutu siyo nzuri na kwamba wanajipanga kwenda Muhimbili kuona iwapo risasi hiyo itaondolewa mwilini.

Hata  hivyo  Kibanda ameeleza  kusikitishwa kwake ni  vitendo vya uvunjifu wa amani dhidi ya  wanahabari nchini Tanzania ambavyo  vimeendelea kufanywa na jeshi la  Polisi nchini na kutaka polisi  waliofanya  hivyo  kuchukuliwa hatua  kali.

Alisema wakati Taifa likiwa bado katika majonzi ya  mauwaji ya  kinyama ya Mwandishi wa Chanel Ten mkoa wa Iringa Daudi Mwangosi leo  tunashudia tena unyama mwingine dhidi ya  mwanahabari  huyo.

Hivyo  iwapo jeshi la  polisi litakosa majibu juu ya sababu ya  kumpiga risasi mwanahabari  huyo ambaye hata  hivyo hakuwa mlengwa katika msako wao  wa kumsaka mtuhumiwa wa ujambazi ambae ni mwanamke basi itafika  sehemu  wanahabari nchini  watalichukulia jeshi la polisi ni maeneo ya hatari kwao

Tuesday, December 4, 2012

DAR HAKUKALIKI WAZIRI AKIMBILIA KATAVI

Naibu Waziri wa Uchukuzi Dr. Charles Tizeba
Naibu Waziri wa Uchukuzi Dkt. Charles Tizeba amerejea mkoani Katavi siku chache tangu ashiriki katika uzinduzi wa mkoa wa Katavi na tathmini ya kongamano la uwekezaji la Oktoba 17, 2011 tathmini iliyofanyika mwezi Novemba kuanzia 19-25, 2012

Taarifa zinaeleza kuwa Naibu waziri huyo amerejea Katavi baada ya kutoridhishwa na majibu ya hoja yaliyotolewa katika kikao cha tahmnini hiyo alipokuwa jijini DSM kwani hakushiriki kikao hicho hadi mwisho hivyo amerejea kuweka mambo sawa ili kukidhi mahitaji ya wawekezaji.

Naibu Waziri huyo aliwasili mkoani Katavi Desemba 2, 2012 ambapo jumatatu desemba 3, alifanya kikao cha ndani baina ya viongozi wa mkoa wa Katavi na wadau wa sekta ya uchukuzi ambapo baadaye mchana alifika katika kituo cha reli cha Mpanda kutembelea eneo hilo

Akiwa katika stesheni ya reli ya Mpanda Naibu waziri wa uchukuzi alipiga marufuku tabia ya makarani wa treni kuwatoza faini wananchi wanaokosa tiketi na kuingia ndani ya behewa ili kusafiri kutokana na kuwepo kwa tatizo la ukosefu wa tiketi za kusafiria za treni kutoka Mpanda hadi mikoa ya Mwanza, Tabora, Dodoma na DSM.

Alisema kuanzia jana hakuna karani yeyote kumlipisha faini abiria aliyepanda treni bila tiketi na badala yake walipe nauli ya kawaida au waangalie utaratibu wa kuwapunguzia nauli kwani wanapata shida ya kusafiri wakiwa wamesimama hadi Tabora.

Leo Naibu Waziri ametembelea ujenzi wa gati la meli Kasanga mkoani Rukwa na kesho atatembelea ujenzi wa gati la meli Karema mkoani Katavi.

HII NDIO AJALI MBAYA ILIYOUA WATANO WA FAMILIA MOJA IRINGA LEO

: GARI LILILOPATA AJALI TOYOTA RAV 4 T 770 BMP ENEO LA TANANGOZI -IRINGA LILILOKUWA LIKIENDESHWA NA  BWANA EZEKIEL MWAITELEKE  (MAREHEMU)  MAJIRA YA SAA SITA NA NUSU MCHANA NA KUSABABISHA VIFO VYA WATU WATANO WA FAMILIA MOJA PAPO HAPO DESEMBA 4, 2012  

BAADHI YA AKINA MAMA WASAMARIA WEMA WA TANANGOZI  IRINGA WAKIJARIBU KUMPEPELEA MMOJA WA MAJERUHI WA AJALI ILIYOTOKEA DESEMBA 4,2012 HUKO TANANGOZI IRINGA LIKIHUSISHA TOYOTA RAV 4 T 770 BMP LILILOINGIA NYUMA YA TRAILER  T 566 BNQ AMBAPO WATU WATANO WA FAMILIA MOJA WALIOKUWA WAKITOKEA DAR KWENDA MBEYA WALIFARIKI PAPO HAPO
6:BAADHI YA WASAMARIA WEMA WAKITOA MOJA YA  MAITI  KUTOKA KATIKA GARI TOYOTA RAV 4 T 770 BMP HUKO TANANGOZI IRINGA DESEMBA 4,2012 WATU WATANO WA FAMILIA MOJA WALIOKUWEMO KATIKA GARI HILO WALIFARIKI PAPO HAPO(PICHA ZOTE NA MISANJO LIVIGHA (MLALAHOI ALWATAN WWW.FRANCISGODWIN.BLOGSPOT.COM

 GARI AINA YA SCANIA LENYE CABIN NA. T 840 BST LIKIWA NA TRAILER NAMBA  T 566 BNQ LILIGONGWA KWA NYUMA NA TOYOTA RAV 4 T 770 BMP HUKO TANANGOZI IRINGA NA KUSABABISHA VIFO VYA WATU WA TANO WA FAMILIA MOJA PAPO HAPO  WALIOKUWA KATIKA GARI HILO RAV 4
Ajali  mbaya  imetokea  mkoani Iringa mchana  wa  leo na kusababisha  vifo  vya  watu  wanne  wa familia  moja  pamoja na mfanyakazi  wa ndani mmoja.

Ajali  hiyo  imetokea katika  eneo la Tanangozi  wilaya ya  Iringa kwenye kizuizi cha barabara  cha mafundi wa kutengeneza barabara  kuu ya Iringa -Mafinga  mkoani Iringa mida ya saa nane mchana

Kwa mujibu  wa mashuda  wa  tukio   hilo  wameueleza  mtandao  huu  wa  www.francisgodwin.blogspot.com  kuwa  chanzo  cha ajali  hiyo ni dereva wa gari dogo aina ya Rav 4  lenye namba  za usajili T 770 BMP kulipalamia lori  lenye tela kwa nyuma. 
 
Huku  chanzo kikitajwa  kuwa ni kuendesha  kwa mwendo kasi  wa  dereva  wa gari ndogo marehemu Ezekiel Mwaiteleke  na kushindwa  kulimudu na kulipalamia lori kwa nyuma.
 
Kwa mujibu  wa mashuda  wa  tukio   hilo  wameueleza    kuwa  chanzo  cha ajali  hiyo ni dereva wa gari dogo aina ya Rav 4 kuendesha  kwa mwendo kasi na kushindwa  kulimudu na kulipalamia lori kwa nyuma na kuwa  gari hiyo ilikuwa ikitokea  jijini Dar es Salaam kwenda Kyela mkoani Mbeya.

Hivyo katika ajali  hiyo  abiria  wote  wanne akiwemo baba na mama  wa  watoto  wawili  waliokuwemo katika gari  hiyo pamoja na  watoto hao  kufa papo hapo na maiti  zote  kupelekwa katika Hospitali ya mkoa wa Iringa.

 Majina ya  waliokufa  ni pamoja  na Ezekiel Mwaiteleke ambaye ni dereva  wa gari hilo na baba  wa familia  hiyo ,mkewe Grace Mwaiteleke ,mtoto Kelvin Mwaiteleke (2),Happy Mwandike na mfanyakazi  wao  wa ndani aliyefahamika kwa jina la Linda Ezekiel  huku majeruhi katika ajali  hiyo ni mmoja na amekimbizwa  Hospital ya mkoa  wa Iringa.

BREAKINGNEWz  RAV 4 YAUA WANNE WA FAMILIA MOJA IRINGA


    Mkuu  wa Jeshi la Polisi Tanzania (IGP) Said Mwema
Ajali  mbaya  imetokea  mkoani Iringa mchana  wa  leo na kusababisha  vifo  vya  watu  wanne  wa familia  moja .


Ajali  hiyo  imetokea katika  eneo la geti la mafundi wa kutengeneza barabara  kuu ya Iringa -Mafinga  mkoani Iringa.

Kwa mujibu  wa mashuda  wa  tukio   hilo  wameueleza  mtandao   wa  www.francisgodwin.blogspot.com  kuwa  chanzo  cha ajali  hiyo ni dereva wa gari dogo aina ya Rav 4 kuendesha  kwa mwendo mkali na kushindwa  kulimudu na kulipalamia lori kwa nyuma.

Hivyo katika ajali  hiyo  abiria  wote  wanne akiwemo baba na mama  wa  watoto  wawili  waliokuwemo katika gari  hiyo pamoja na  watoto hao  kufa papo hapo na maiti  zote  kupelekwa katika Hospitali ya mkoa wa Iringa.
EWURA YAFUNGUKA YATANGAZA BEI YA MAFUTA TENA

TAARIFA KWA UMMA KUHUSU BEI KIKOMO ZA MAFUTA AINA YA PETROLI KUANZIA
JUMATANO, TAREHE 5 DISEMBA 2012

Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) inatangaza bei kikomo za bidhaa za mafuta ya petroli hapa nchini. Bei hizi zitaanza kutumika kuanzia Jumatano, Tarehe 5 Disemba 2012. Pamoja na kutambua bei kikomo za bidhaa mbalimbali za petroli nchi nzima, ni muhimu kuzingatia yafuatayo.

(a) Bei za jumla na rejareja kwa mafuta aina zote ya Petroli, Dizeli na Mafuta ya Taa zimeongezeka ikilinganishwa na toleo lililopita la tarehe 07 Novemba 2012. 
Katika toleo hili, bei za rejareja kwa Petroli na Dizeli zimeongezeka kwa viwango vifuatavyo: Petroli Sh 70/lita sawa na asilimia 3.4; Dizeli Sh 10/lita sawa na asilimia 0.53. 
Bei ya Mafuta ya Taa imepungua kwa Sh 3/lita sawa na asilimia 0.1. Bei za jumla kwa kulinganisha matoleo haya mawili zimeongezeka kama ifuatavyo: Petroli kwa Sh 69.56/lita sawa na asilimia 3.52; Dizeli kwa Sh 10.04/lita sawa na asilimia 0.52. 
Bei ya Mafuta ya Taa imepungua kwa Sh 3/lita sawa na asilimia 0.15. Mabadiliko haya ya bei yametokana na ongezeko la bei ya mafuta katika soko la dunia na kushuka kidogo kwa thamani ya Shilingi ya Tanzania dhidi ya Dola ya Marekani.

(b) Kwa mujibu wa Sheria ya Mafuta ya mwaka 2008, bei za bidhaa za mafuta ya petroli zitaendelea kupangwa na soko. EWURA itaendelea kuhamasisha ushindani kwa kutoa taarifa za bei kikomo za bidhaa za mafuta. Taarifa hizi zina lengo la kuwasaidia wadau kufanya maamuzi stahiki kuhusu manunuzi ya bidhaa za mafuta.

(c) Kampuni za mafuta zipo huru kuuza bidhaa za mafuta ya petroli kwa bei ya ushindani ilimradi bei hizo ziko chini ya bei kikomo (price cap) kama ilivyokokotolewa na fomula mpya iliyopitishwa na EWURA na ambayo ilichapwa kwenye Gazeti la Serikali Na. 454 la tarehe 23 Desemba 2011.

(d) Vituo vyote vya mafuta vinatakiwa kuchapisha bei za bidhaa za mafuta katika mabango yanayoonekana bayana na yakionyesha bei ya mafuta, punguzo, vivutio vya biashara au promosheni zinazotolewa na kituo husika.
 Pale ambapo inawezekana kuchagua, wateja wanashauriwa kununua bidhaa za mafuta kutoka kwenye vituo vinavyouza mafuta kwa bei ndogo zaidi ili kushamirisha ushindani. Ni kosa kuuza mafuta bila kuweka mabango ya bei inayoonekana vizuri kwa wateja na adhabu itatolewa kwa kituo husika.

(e) Wanunuzi wanashauriwa kuhakikisha kuwa wanapata stakabadhi ya malipo inayoonesha jina la kituo, tarehe, aina ya mafuta yaliyonunuliwa na bei kwa lita. Stakabadhi hiyo ya malipo itatumika kama kidhibiti cha mnunuzi wa mafuta endapo kutajitokeza malalamiko ya ama kuuziwa mafuta kwa bei ya juu kuliko bei kikomo; ama endapo utakuwa umeuziwa mafuta yenye kiwango cha ubora kisichofaa.

Tuesday, November 27, 2012

INVESTMENT PROFILE KATAVI REGION




Pamoja na jeshi la polisi mkoa wa Iringa kuwabana madereva wanaoruhusu abiria wao kuning'inia katika magari ila bado wanaendelea kutenda kosa sasa ni nani wa kumuwajibisha mwenzake? hili ni eneo la posta mjini Iringa, ni kazi nzuri ya www.francisgodwin.blogspot.com




Monday, November 26, 2012

CHOZI HILI LINAMAANISHA ..........

BI REHEMA MOHAMMED AKITANGAZA KUHAMA CHADEMA NA KUHAMIA CCM KATIKA MKUTANO WA CCM ARUSHA MWISHONI MWA WIKI.....



Rehema Mohammed alikuwa Diwani Chadema kabla ya kuhamia CCM kufuatia mkutano wa CCM ulioongozwa na katibu mkuu wa CCM Taifa, Abdalahman Kinana.

Sunday, November 25, 2012

MKOA WA KATAVI WAZINDULIWA RASMI

Dkt.Bilal Azindua Mkoa Wa Katavi

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungao ya Tanzania Dkt Mohamed Gharib Bilal akizindua rasmi mkoa wa Katavi kwa kuweka jiwe la msingi katika kilima cha kijiji cha Kabungu kwa ajili ya kujenga kituo cha kumbukumbu ya historia ya mkoa wa Katavi, kulia kwake ni mkuu wa mkoa hu Dr Rajabu M. Rutengwe akishuhudia jana Novemba 25, 2012
Mkuu wa wilaya ya mpanda, Paza Tusamale Mwamlima akimkaribisha makamu wa Rais wilayani kwake katika hafla ya uzinduzi wa mkoa wa Katavi na Tathmini ya uwekezaji kwa mwaka mmoja.


Kijiji Cha Kabungu ndipo palipozaliwa Wilaya ya Mpanda Mwaka 1947 na Boma la mtawala wa kwanza wa kikoloni Mpanda lilijengwa hapo
 
Makamu wa Rais Akizungumza na wafanyakazi wa benki ya NMB wakati alipotembelea katika banda hilo leo njini Mpanda Kushoto ni Mkuu wa mkoa wa Katavi Dkt. Rajab Rutengwe.
 
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Mh. Mizengo Pinda akizungumza na wana Katavi wakati wa uzinduzi wa mkoa wa mpya wa Katavi  kwenye viwanja vya Kashaulili mjini Mpanda leo.
Wananchi wa Mkoa wa Katavi wakishangilia
Baada ya uwekaji wa jiwe la msingi kijijini Kabungu, Makamu wa Rais alirejea mjini mpanda katika viwanja vya Kashaulili ambapo kumefanyika shughuli mbalimbali za  uzinduzi rasmi wa mkoa huo na hotuba mbalimbali zikiendana na sherehe za  ngoma za makabila mbalimbali  ya asili ya mkoa wa Katavi


 Makamuwa Rais Dkt. Gharib Bilal akikaribishwa na mkuu wa wilaya ya Mpanda Mh. Paza Tusamale Mwamlima huku akipungia mkono wananchi waliofika kumlaki na kushuhudia uwekaji wa jiwe la msingi katika kijiji cha Kabungu nje kidogo ya mji wa Mpanda.
 Makamu wa Rais Dkt. Gharib Bilal akizungumza na wananchi wa kijiji cha Kabungu wakati wa uwekaji wa jiwe la msingi kuzindua mkoa wa Katavi, kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Katavi Dkt Rajab Rutengwe na kutoka kulia ni Mke wa Makamu wa Rais Mama Zakia Bilal na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Katavi Bw. Abdallah Mselem Said
 Makamu wa Rais Dkt. Gharib Bilal, Waziri Mkuu Mizengo Pinda, Waziri wa Uwezeshaji na Uwekezaji Dkt Mary Nagu, Mke wa Makamu wa Rais mama Zakia Bilal na Mke wa Waziri Mkuu mama Tunu Pinda wakiimba wimbo mara baada ya kuwasili kwenye viwanja vya Kashaulili mjini Mpanda tayari kwa Sherehe za uzinduzi wa mkoa wa Katavi
 
Baadhi ya wawekezaji waliohudhuria katika uzinduzi huo uliofanyika kwenye viwanja vya Kashaulili.
 
Mkuu wa mkoa wa Katavi akiongea na kukaribisha viongozi mbalimbali kutoka salam zao kutoka mikoa waliyotoka na wizara mbalimbali.
 
Waziri wa Ardhi na makazi Goodluck Ole Medeye akizungumza na wana Katavi na kuwaasa mambo mbalimbali kuhusu ardhi yao hasa katika suala zima la uwekezaji, ambapo amewaambia wasiuze ardhi bali waingie ubia na wawekezaji ili kunufaisha vizazi vyao pia.
 
Mke wa Waziri Mkuu Mama Tunu Pinda akiwasalimia wananchi wa Katavi na kuwapongeza kwa kupata mkoa mpya wa Katavi.
 
Mama Aisha Bilal akisalimia wananchi wa katavi katika sherehe hizo.
 
Kwaya ya Vijana ya Moravian mjini Mpanda wakitumbuiza katika uzinduai huo uliofanyika kwenye viwanja vya Kashaulili mjini Mpanda.
 
Martha Mbogo mwimbaji wa kundi la Katavi Curture Group akiimba wakati kundi hilo lilipokuwa likitumbuiza katika uzinduzi huo mjini Mpanda.

 Watoto Daniel Ntwangile na Christina Benedicto wakitunzwa na Waziri Mkuu Mizengo Pinda mara baada ya kuimba na kucheza vizuri na Kwaya ya Vijana Moravian Mjini Mpanda wanaofuatia ni Waziri wa Uwezeshaji na Uwekezaji Dkt Mary Nagu, Mke wa Makamu wa Rais mama Zakia Bilal na Mke wa Waziri Mkuu mama Tunu Pinda wakijiandaa na wao kuwatunza