Thursday, January 31, 2013

PINDA AWATAKA WABUNGE MTWARA KUSHIRIKIANA

WAZIRI Mkuu, Mizengo Pinda amefanikiwa kutuliza jazba za wakazi wa Mkoa wa Mtwara baada ya kueleza jinsi watakavyonufaika na gesi itakayozalishwa mkoani humo kabla ya kusafirishwa kwa bomba hadi Dar es Salaam.
Aidha, Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Joseph Simbakalia amewaomba radhi wananchi wa mkoa huo kutokana na kauli Desemba 21, mwaka jana akiwakebehi baada ya kumwomba apokee maandamano yao ya kupinga mpango wa kusafirisha gesi hiyo.
Akizungumza katika mkutano wa majumuisho uliofanyika jana baada ya kusikiliza madai ya wananchi hao kwa siku mbili mfululizo, Pinda alisema hakuna tone la gesi ghafi itakayosafirisha kwa njia ya bomba na kusema kiwanda cha kusindika gesi ghafi kitajengwa katika Kijiji cha Madimba, mkoani humo ili mabaki yatokanayo na gesi hiyo yatumike kuvutia uwekezaji wa viwanda.
“Wataalamu wanasema gesi haiwezi kwa namna yoyote ile kusafirishwa kama ilivyo, lazima ibadilishwe kuwa hewa au barafu… kiwanda cha kusafisha gesi kitajengwa Madimba. Gesi yote itakayotoka Mnazi Bay itasafishwa hapo na masalia yote yatabaki huku ili kuvutia viwanda vya mbolea na vingine vinavyotumia malighafi hizo,” alisema Pinda na kuongeza:
“Kama tungekuwa tunasafirisha gesi ghafi basi hata kiwanda cha Dangote kisingejengwa hapa… gesi itakayopelekwa Dar es Salaam ni ile iliyosafishwa kwa ajili ya matumizi ya kuzalisha umeme… tusaidieni wenzetu kuliokoa Taifa na tatizo la umeme.”
“Gesi lazima isindikwe Mtwara, haitoki hadi viwanda vije… nadhani hili ni jambo jema lazima tuliwekee utaratibu. Nikawauliza wataalamu wangu kwani kiwanda cha kusafisha gesi kinajengwa wapi, wakanijibu Madimba… nikasema kumbe tatizo kubwa ni kutowaeleza vya kutosha wananchi suala la gesi.” alisema Waziri Mkuu huku akipigiwa makofi... “Nafikiri tatizo ni sisi Serikali hatukuwa na mpango mzuri wa kuwaelimisha wananchi.”
Awali, madai ya wakazi wa Mkoa wa Mtwara yalikuwa ku pinga usafirishaji wa gesi ghafi kwenda Dar es Salaam wakieleza kuwa mpango huo utafukuza uwekezaji wa viwanda mkoani humo ambao ungechochewa na upatikanaji wa malighafi baada ya kusafishwa kwa gesi.
Pia wananchi walipinga uje nzi wa mitambo ya kuzalisha umeme Kinyerezi, Dar es Salaam wakiitaka Serikali kujenga mitambo hiyo mkoani Mtwara.
Alitoa wito kwa wabunge wa Mkoa wa Mtwara kufuta tofauti zao za kisiasa ili waweze kuharakisha maendeleo ya mkoa huo... “Purukushani hizi ndani ya chama hazina tija, tuseme basi… wabunge hawaelewani, sasa bungeni wanakwendaje... kila mtu na lake … hebu tuseme watu kwanza mimi badaaye,” alisema Pinda huku akishangiliwa.
Katika siku hizo mbili mkoani Mtwara, Waziri Mkuu alikutana na viongozi wa vyama vya siasa, dini, wafanyabiashara, madiwani na wenyeviti wa mitaa na wanaharakati mbalimbali.
 
RC aomba radhi

Katika hatua nyingine, Mkuu wa Mkoa, Simbakalia aliwaomba radhi wakazi wa Mkoa wa Mtwara akisema alipotoka kuwaita wananchi hao wapuuzi na baadaye wahaini kauli ambazo ziliwaudhi wengi
“Kupitia hadhara hii nawaomba radhi kwa kuwakwaza, nimesikitishwa kwa kauli yangu ambayo imepokewa kwa hisia kwamba niliwadharau,” alisema Simbakalia.
Baadaye Waziri Mkuu aliwasihi wananchi wa Mtwara kumsamehe Mkuu wao wa Mkoa wa Mtwara kwa kauli hiyo aliyoitoa 21 Desemba, mwaka jana katika kikao cha Kamati ya Ushauri Mkoa, (RCC), pale alipoombwa kuyapokea maandamano ya wakazi wa mkoa huo Desemba, 27, mwaka jana.

ZIARA YA NAPE KIGOMA

4. Makamu Mwenyekiti wa CCM-Bara, Ndugu philip Mangula akiteremka kutoka kwenye ndege ya shirika la ndege la Tanzania (Air Tanzania) ,kwenye uwanja wa ndege wa Kigoma  asubuhi tarehe 1/2/2013.

5. Makamu Mwenyekiti CCM Bara Philip Mangula  akipokelewa na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Moses Nnauye mara baada ya kuwasili Kigoma asubuhi ya leo kwa ndege ya shirika la ndege la Tanzania (Air Tanzania)

14. Makamu Mwenyekiti wa CCM-Bara,Ndugu Philip Mangula akisalimiana na baadhi ya viongozi wa CCM mkoani Kigoma mara tu alipowasili katika uwanja wa ndege wa Kigoma, uwanja ambao umefanyiwa maboresh makubwa ikiwa na kuongezwa sehemu ya kurushia ndege.

18.Makamu Mwenyekiti wa CCM-Bara ,Ndugu Philip Mangulaakitoa salaam za shukrani kwa mapokezi mazuri pia alitoa pongezi kwa maboresho ya uwanja wa ndege ambao alisema ni mzuri kulinganisha na miaka ya nyuma na amekiri kumekuwa na mabadiliko makubwa ya kimaendeleo katika mji wa Kigoma. Makamu Mwenyekiti amewasili rasmi kwa ajili ya sherehe za miaka 36 ya kuzaliwa kwa Chama Cha Mapinduzi ambazo kitaifa mwaka huu zitafanyika tarehe 3/2/2013 mkoani kigoma kwenye Uwanja wa Lake Tanganyika.
Picha na Adam H. Mzee
Kigoma ,Tanzania.

 Katibu waItikadi na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi Nape Nnauye ametembelea Kijiji chaRungwe Mpya kilichopo kata ya Rungwe Mpya Wilayani Kasulu Mkoani Kigoma na kufanya shughuli mbalimbali za Chama ikiwa ni pamoja na Kuweka jiwe la Msingila Ofisi ya CCM kijijini hapo na kuhutubia mkutano wa hadhara wa wananchi wa Kata hiyo pamoja na Kata ya Asante Nyerere.
 Baada yakuweka Jiwe hilo la Msingi, Nnauye alikabidhi kadi kwa wanachama wapya wa Chama hicho kutoka katika kata za Asante Nyerere pamoja na Rugwe Mpya, wanachama ambao wamerejea CCM kutoka vyama vya upinzani hasa NCCR Mageuzi na Chadema kabla ya kuzungumza na Wajumbe wa Nyumba Kumi wa chama hicho, Wazee pamoja na Vijana waendesha Bodaboda mjini Kasulu.

 Nape akikabidhi kadi kwa wanachama wapya.
 Baadhi ya Kadi zilizorejeshwa katika mkutano wa hadhara.
Mkuu wa Wilaya Kasulu, Danny Makanga akicheza ngoma wakati wa mapokezi hayo ya Nape Kijijini hapo.
 Katibu
wa Itikadi na Uenezi wa CCM Taifa, Nape Nnauye akiweka jiwe la Msingi la
Ujenzi wa Ofisi ya CCM ikiwa ni moja kati ya miradi aliyoitembelea wilayani Kasulu.

NAPE KIJIJINI  RUNGWE MPYA

.  Katibu waItikadi na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi Nape Nnauye ametembelea Kijiji cha Rungwe Mpya kilichopo kata ya Rungwe Mpya Wilayani Kasulu Mkoani Kigoma na kufanya shughuli mbalimbali za Chama ikiwa ni pamoja na Kuweka jiwe la Msingila Ofisi ya CCM kijijini hapo na kuhutubia mkutano wa hadhara wa wananchi wa Kata  hiyo pamoja na Kata ya Asante Nyerere. Baada yakuweka Jiwe hilo la Msingi, Nnauye alikabidhi kadi kwa wanachama wapya wa Chama hicho kutyoka katika kata za Asante Nyerere pamoja na Rugwe Mpya,...

RAIS KABILA ATUA JIJINI DAR

RAIS JOSEPH KABILA WA DRC ATUA DAR  KWA ZIARA YA SIKU MOJA

 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimjpokea Rais Joseph Kabila wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) alipowasili uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam mchana wa Januari 30, 2013

 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimtambulisha maafisa mbalimbali Rais Joseph Kabila wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) alipowasili uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam mchana  Januari 30, 2013

  Rais Jakaya Mrisho Kikwete na mgteni wake  Rais Joseph Kabila wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) wakmiangalia ngoma za utamaduni alipowasili uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijijni Dar es salaam  mchana  Januari 30, 2013
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Rais Joseph Kabila wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) wakiingia hoteli ya Hyatt  Kilimanjaro jijini mchana  Januari 30, 2013
PICHA NA IKULU YA TZ.

Kimbunga Felleng Kutua Afrika Mashariki

Taarifa kwa umma: Uwezekano wa matukio ya mvua kubwa

Taarifa Na. 20130129-02

Muda wa Kutolewa Saa za Afrika Mashariki Saa 12:00 Jioni

Daraja la Taarifa:

1:Taarifa 2:Ushauri 3:Tahadhari 4:Tahadhari Kubwa:

Ushauri

Kuanzia:

Tarehe 30 Januari, 2013 Mpaka: Tarehe  01 Februari, 2013

Aina ya Tukio Linalotarajiwa

Mvua kubwa (zaidi ya milimita 50 katika kipindi cha saa 24 kilasiku)

Kiwango cha uhakika: Wastani

Maeneo yatakayoathirika Baadhi ya maeneo ya mikoa ya Rukwa, Iringa, Mbeya, Njombe,Ruvuma, Morogoro, Lindi, Pwani, Mtwara na maeneo jirani na mikoa hiyo.

Maelezo:

Kuwepo kwa kimbunga “FELLENG” kaskazini-mashariki mwa,Madagascar ambacho kinavuta upepo wenye unyevunyevu.kutoka Congo kupitia maeneo tajwa hapo juu.

Angalizo:

Wakazi wa maeneo hatarishi, watumiaji wa Bahari na nchi kavuwanashauriwa kuchukua tahadhari. Aidha taasisi zinazohusika na Maafa zinashauriwa kuchukua hatua stahiki.

Maelezo ya Ziada

Mamlaka inaendelea kufuatilia mwenendo wa kimbunga hicho,na kutoa mrejeo (updates) kila itakapobidi.

IMETOLEWA NA MAMLAKA YA HALI YA HEWA TANZANIA

MAMLAKA YA HALI YA HEWA YATOA HADHARI

Wednesday, January 23, 2013

MWANRI AKAGUA USAFI WA MAZINGIRA NA MITARO MJINI MPANDA

WAZIRI ANAYEZUNGUMZWA SANA NA WANA KATAVI KWA UWAJIBIKAJI

Hospitali kuwa sokoni ni Sawa???????? mkurugenzi wa mji, Joseph Mchina akikuna kichwa hoja nzito.

Mhe Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu TAMISEMI akimsikiliza kwa makini mama aliyemlalamikia kuishi kwa shida kutokana na kuwepo kwa Dampo jirani na nyumba yake "Wakati wa Kula tunalazimika kuingia katika chandarua kukwepa nzi"