Tuesday, August 20, 2013

POLISI KATAVI INFO

MATAPELI WA NDUMBA MBARONI




 

Na Geofrey Chaka, Katavi
JESHI la polisi mkoani Katavi linawashikilia watu wanne kwa tuhuma za utapeli wa kutumia dawa za kienyeji

    Kwa mujibu wa taarifa ya Kamanda wa jeshi la polisi mkoani Katavi, Dhahir Kidavashari wanaoshikiliwa na jeshi hilo ni Charles Mwelela (38),mkulima mkazi wa Edeni katika Manispa ya Sumbawanga Mkoa wa Rukwa, Issa Hasan maarufu kwa jina la  Senga (42), mklima mkazi wa Kona ya Bwiru jijini Mwanza,  Hussein Hassan, (38), mkulima mkazi wa jijini Mwanza na Magreth Bakari,(45), mkulima mkazi wa Nsemulwa mjini Mpanda

  Akitoa taarifa kwa wananhabari ofisini kwake jana  Kamanda Kidavashari alisema kuwa tukio hilo lilitokea tarehe Agosti 26, 2013 majira ya saa tano usku katika mtaa wa mji Mwema katika nyumba ya kulala wageni ya Vatcan iliyopo kata ya Kashaulili, Wilaya ya Mpanda, Mkoa wa Katavi ambapo watuhumiwa hao walikamatwa kwa tuhuma za kujifanya waganga wa jadi kwa kuwatapeli wananchi mbalimbali mjini hapo.

      Alisema  watu hao walikutwa na vifaa vinavyoashiria kuwa wao ni waganga wa jadi pamoja na pasi ya kijerumani feki ambayo huitumia katika shughuli za kuwatapeli wananchi baada ya kuwahadaa kuwa watapata dawa za kienyeji za kuwasaidia katika matatizo waliyonayo licha ya kuwa siyo kweli na wala watuhumiwa hao hawana vyeti vya kuonesha kuwa ni waganga wa jadi.

       Kamanda wa polisi Mkoa wa Katavi alisema kuwa, Agosti 26, 2013 saa tano usiku jeshi la polisi lilipata taarifa toka kwa raia wema kwamba katika nyumba ya  kulala wageni ya VATCAN iliyoko mji mwema mjini Mpanda kuna watu katika chumba namba 8 na namba 11  wanajifanya waganga wa jadi na kutoa tiba ya asili pasipo na kibali cha kazi hiyo.

       Kamanda  alisema kuwa uchunguzi wa awali umebaini kuwa watu hao ni matapeli na huwatapeli watu kwa mtindo wa kuwapa madawa ya kienyeji kwa lengo la kuwalevya na muda mwingine huwatapeli watu kwa kuwadanganya watu kuwa  wanapasi ambayo wakipewa huwa na mvuto wa pesa daima na hivyo kuwataka watu hao kutoa pesa ili wapewe pasi hiyo bila wao kujua kuwa  wanatapeliwa.

      Kamanda wa polisi alisema kwamba tukio hilo lilikuwa likifanikishwa na watu hao kwa kumtumia mwanamke aitwaye MAGRETH BAKARI kwa kuwatafuta wateje sehemu mbalimbali za mji na kuwapeleka katika nyumba hiyo ya kulala wageni na kuwatapeli kwa mtindo huo, kwani mwanamke huaminika kuwa hawezi kuwatapeli kwa vile ni mwanamke.

   Kamanda wa polisi mkoa wa Katavi ametoa rai kwa wananchi kwamba wananchi wawe makini na waangalifu sana wanapokuta na watu kama hao,na kutoa taarifa kama kuna shaka na watu kama hao katika kituo cha polisi kilichopo karibu.

MKE WA MTU SUMU

WIVU wa mapenzi umepoteza maisha ya ndugu Juma Moshi mkazi wa kijiji cha Kamsanga kata ya Kabungu wilaya ya Mpanda mkoani Katavi baada ya kupigwa na kufariki dunia kwa fimbo katika sehemu za mwili na watu wasiofahamika

Tukio hilo lilitokea Agosti 16, 2013 majira ya saa nane mchana katika kijiji anachoishi marehemu ambapo marehemu Juma Moshi (30) alikamatwa na watu wasiofahamika alipokuwa katika kilabu cha pombe za kienyeji kilichopo kijijini hapo wakimtuhumu kuwa anatembea na mke wa mtu aliyefahamika kwa jina la Peter Makenzi

Taarifa toka eneo la tukio na kuthibitishwa na jeshi la polisi zilidai kuwa marehemu baada ya kukamatwa na watu hao walimuhoji maswali kuhusiana na tuhuma hizo ambapo iansemekana marehemu alikiri na mbele yao na kuanza kumuadhibu marehemu kwa kumchapa  viboko kuanza saa tano asubuhi hadi saa nane mchana marehemu aliweza kupoteza maisha akila kichapo

Kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Katavi, Dhahir Kidavashari alisema uchunguzi wa awali umebaini chanzo cha mgogoro huu uliopelekea mauaji umetokana na wivu wa kimapenzi kati ya marehemu dhidi ya Peter Makenzi ambaye inasemekana ni mume wa mwanamke aliyesemekana kutembea na marehemu

Alisema baada ya kutokea mauaji hayo ndugu Peter Makenzi aliweza kutoweka hajulikani aliko ambapo jeshi la polisi linaendelea na juhudi za kumtafuta ili aweze kupatikana na kufikishwa kwenye mahakamani kujibu tuhuma za kupanga mauaji hayo pamoja na kuwasaka aliowapa ujira wa kufanya mauaji ya marehemu kwa tuhuma za kutembea na mke wake

Katika tukio lingine Sele Njija mwanamke mwenye umri wa miaka 60 aliuwawa kwa kukatwa katwa kichwani na kitu kinachosadikiwa kuwa ni shoka na watu wasiofahamika Agosti 14, 2013 majira ya saa moja jioni katika kitongoji cha Mboge-Kalila kata ya Kabungu wilaya ya Mpanda mkoani Katavi

Kamanda wa polisi mkoani Katavi, Dhahir Kidavashari alisema jana ofisini kwake alisema katika tukio hilo watu watatu wasiofahamika walifika nyumbani kwa marehemu na kumkuta akiwa na mwanae aliyetajwa kwa jina la Ng’walu Lukulaga na kuomba maji ya kunywa ndipo motto huyo alipoinuka na kwenda ndani kuwachukulia maji ya kunywa

Alisema motto huyo akiwa ndani kuchota maji mtungini watu hao walimvamia mama yake na kumkatakata kwa shoka kichwani hadi kufariki dunia papo hapo kisha watu hao wakatokomea kusikojulikana

Alisema uchunguzi wa awali umebaini kuwa chanzo cha mauaji hayo ni migogoro ya kifamilia na kiukoo kwani takribani miaka miwili iliyopita mume wa marehemu aliuwawa kwa kukatwa katwa kwa mapanga na watu wasiojulikana katika kijiji cha Kasisi eneo la Mpanda ndogo

Alisema hakuna mtu yeyote aliyekamatwa kwa tuhuma za mauaji hayo ambapo kamanda huyo aliwasihi wananchi kuacha kujichukulia sheria mkononi badala yake watoe taarifa katika vyombo vya dola ili hatua ziweze kuchukuliwa kwa kufuata utaratibu wa kisheria.

Thursday, August 15, 2013

ALIYEACHA MIHADARATI APEWE AJIRA - DC

MKUU WA WILAYA YA SINGIDA MWL QUEEN M. MLOZI AKISALIMIANA NA KIJANA YUSUFU SAIMON SHUMBI BAADA YA KUTANGAZA KUWA AMEACHANA NA MIHADARATI KATIKA ENEO LA MKESHA WA MWENGE WA UHURU 2013 KATIKA UWANJA WA KITUO CHA MABASI KIPYA CHA MJINI SINGIDA
HONGERA mwanangu kwa kuamua kuachana na madawa ya Kulevya - DC Mlozi, aliyeshika kismeo ni mganga wa Manispaa ya Singida, ilikuwa Agosti 09, 2013 kituo kipya cha mabasi mjini Singida katika wiki ya Mwenge wa Uhuru



Mganga mkuu wa Manisaa, nakuagiza umpe kazi kijana huyu kwa kuamua kuachana na madawa ya kulevya na taarifa hiyo niipate mezani kwangu kuwa umempa kazi huyu kijana - DC

Singida
MKUU wa wilaya ya Singida mkoani Singida, Mwalimu Queen Mlozi amemuagiza mganga mkuu wa Manispaa ya Singida kumuajiri kijana aliyekuwa anatumia madawa ya kulevya na kuamua kuachana nayo

Agizo hilo lilitolewa na Mkuu huyo wa wilaya kufuatia ushuhuda uliotolewa na kijana Yusufu Saimoni Shumbi mbele ya wananchi katika viwanja vya stendi kuu ya mabasi Singida jana katika ukaguzi wa mabanda ya Mwenge yaliyopo eneo hilouliofanywa na Mkuu wa wilaya

Alisema maelezo ya kijana huyo yanaonesha kuwa miongoni mwa kilichosababisha Yusufu kuanza kutumia madawa ya kulevya ni kukosekana kwa kazi ya kufanya na kumpa vishawishi vya kujiunga na makundi ya madawa ya kulevya hivyo uamuzi wa kwanza wa serikali ni kumpa shughuli ya kufanya kijana

Alisema vijana wanaotumia madawa ya kuelvya wako wengi na wanahitaji kuwafuatilia kwa karibu ili kuwarejeha katika hali ya kawaida na kuokoa nguvukazi ya Taifa hivyo Manispaa ya Singida itafute mbinu za kuwaweka karibu vijana walioko katika janga la madawa ya kulevya waachane na madawa hayo

“Mganga nakupa kazi moja kubwa, kuanzia leo tafuta namna ya kumpa kazi ya kufanya kijana huyu ili asije akarejea katika madawa ya kulevya na taarifa niipate haraka sana” alisema mkuu wa wilaya

Awali akitoa ushuhuda wake Yusufu Saimoni Shumbi amesema alianza kutumia madawa ya kulevya alipokuwa kidato cha pili katika shule ya Sekondari Kikatiti ambako alikuwa na rafiki zake wengine ambao walikuwa wanasoma naye na baada ya kumaliza na kufeli mtihani aligundua kuwa alijipotezea muda shuleni

Alisema kutokana na kutumia madawa hayo alibadilika afya yake akawa anaugua mara kwa mara kichwa, mwili kulegea na kukosa kumbu kumbu pamoja na kukosa uwezo wa kujimudu katika baadhi ya matendo kutokana na mwili wake kulegea mikono na mikono

Alisema hivi sasa ameamua kurudia mtihani wa kidato cha nne kwani awali alifanya mtihani huo na kufeli mwaka 2011 lakini kutokana na uwezo mdogo aliokuwa nao kutokana na kutumia madawa ya kulevya alipata daraja la nne alama 30

Kwa upande wake mama mzazi wa Yusufu, Grace Shumbi (50) amesema mwanae ni kitinda mimba katika familia yake ya watoto tisa ambapo wamekuwa wakiishi kwa kutegemea kodi ya nyumba kwani alikuwa akifanya kazi ya kuhubiri neon la Mungu katika shirika la Life Ministry na kustaafu miaka kadhaa iliyopita

Amesema mwanae licha ya kuwa na hali hiyo amekuwa mwaminifu sana nyumbani kwani hata ujenzi wa nyumba kubwa wanayokaa hivi sasa aliisimamia Yusufu wakati huo mama yake akiwa anatibiwa hospitali

Amesema hivi sasa Yusufu anamdai ada akalipe shule ili asome upya aweze kurudia mtihani wa kidato cha nne ili aweze kuendelea na masomo kwani anaelewa kuwa ana uwezo wa kuendelea kusoma shule na kufaulu hadi chuo kikuu bila shida ikiwa tu atapata ada

MANISPAA KUBORESHA MAZINGIRA YA SHULE

Baraza la Madiwani linaendelea Agosti 14/15, 2013 Chuo cha Maendeleo ya wananchi Singida


NAKIRI kuupokea Mwenge 2013, ukiwa unapendeza, unang'aa
 
MANISPAA ya Singida mkoni Singida imejipanga kuboresha mazingira ya
shule za msingi na Sekondari ikiwa ni katika juhudi za kuboresha
mazingira ya kujifunzia na kufundishia kwa lengo la kuinua taaluma
mshuleni

Hayo yalibainishwa jana na Mkurugenzi wa Manispaa hiyo, Joseph Mchina
mara baada ya kumalizika kwa baraza la madiwani la manispaa hiyo
lililofanyika Agosti 14, 2013 katika ukumbi wa  chuo cha Maendeleo ya
wananchi Singida mjini Singida na kupitisha maazimio hayo

Mchina alisema katika baraza hilo walikubaliana kuanza kutenga bajeti
ya kupima maeneo yote ya shule za Sekondari na Msingi ili kuzuia
uvamizi unafanywa na baadhi ya watu hasa matajiri wenye fedha kwa
kulipia gharama za upimaji katika viwanja vinavyzunguka mashule ili
kuweza kumega maeneo ya shule n kujitwalia kwa kiggezo cha kupimiwa

Alisema kufuatia kuibuka kwa migogoro mingi ya kugombania maeneo baina
ya watu binafsi na taasisi za shule katika manispaa baraza liliazimia
kutenga pesa kwa ajili ya kupima maeneo yote ya taasisi za shule mjini
hapa ikiwa ni pamoja na kushawishi wamiliki wa shule binafsi kukubali
kuingia katika mpango ili shule zao nazo ziweze kupimiwa

Mkurugenzi huyo wa Manispaa ya Singida alifafanua kuwa katika
kupunguza kero ya migogoro ya kugombania maeneo baina ya taasisi na
wananchi pia ofisi yake imeamua kusimamia migogoro hiyo ili kuitafutia
ufumbuzi na kuwapa walimu muda wa kutosha kutimiza wajibu wao na kwa
kuanzia Manispaa imeamua kuyapima maeneo yote yanayomilikiwa na
taasisi za shule ziliz chini ya Manispaa

Aidha alisema kuwa katika kuboresha mazingira ya kujifunza na
kufundishia mashuleni Manispaa kupitia baraza la madiwani imepanga
kupeleka nishati ya umeme katika taasisi zote za shule zilizoko katika
Manispaa hiyo ambazo ni shule za Msingi na Sekondari

Alisema kutokuwapo kwa nishati ya umeme mashuleni kunaweza kutengeneza
mazingira kuzurura ovyo usiku badala ya kujisomea hivyo baraza la
madiwani la Manispaa limeona umuhimu wa kupeleka nishati ya umeme
katika shule za Sekondari na Msingi ili wanafunzi waweze kutumia muda
wa jioni kujisomea masmo ya ziada

Alisema anaamini uwepo wa nishati hiyo kutainua ari ya kujisomea kwa
wanafunzi pamoja na walimu kupanga program maalumu ya kuwafundisha
wanafunzi nyakati za jinni  na hivyo kuweza kuinua taaluma mashuleni

Manispaa ya Singida ina jumla ya shule za Msingi 51 kati ya hizo 47
zinamilikiwa na Manispaa na 4 ni za binafsi ambapo pia shule za
sekndari katika Manispaa hiyo ziko 21, kati ya hizo 17 zinamilikiwa na
Manispaa na 4 ni za binafsi




Mkuu wa wilaya ya Singida Queen Mlozi akimkabidhi Mwenge wa Uhuru mkurugenzi wa Manispaa ya Singida(hayupo pichani)  Agosti 11, 2013

Mkurugenzi wa Manispaa ya Singida, Joseph S. Mchina akipokea Mwenge wa Uhuru kutoka kwa Mkuu wa wilaya ya Singida Mwl Queen Mlozi (hayupo pichani) Agosti 11, 2013

Kushoto ni mkimbiza Mwenge Kitaifa Seperatus Ngemela Lubinga akimuangalia mkurugenzi wa Manispaa ya Singida, Joseph Mchina alipokuwa akipokea Mwenge huo kutoka kwa Mkuu wa wilaya ya Singida Agosti 11, 2013

MAZINGIRA: Tunatunza mazingira kwa kupanda miti katika miradiyetu

Huku hata wazungu wanafurahia Mwenge wa Uhuru wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kama walivyonaswa na kamera yetu kwenye eneo la mkesha wa Mwenge katika Manispaa ya Singida 2013

WACHUUZI; Tunauza mafuta ya alizeti sh 14,000 kwa lita 5, vitunguu pia vipo

Wednesday, August 14, 2013

REFA ALAMBWA KIPIGO AVULIWA NGUO UWANJANI



Na Ernest Simya, Sumbawanga
Mwamuzi na wachezaji watatu wa timu ya Serengeti SC ya wilayani Sumbawanga mkoani  Rukwa wamelazwa kwenye kituo cha Afya cha Laela baada kushambuliwa na kwa kupigwa sehemu mbalimbali za miili yao katika mchezo wa Ligi ya ujirani mwema.



Katika mchezo huo uliopigwa katika uwanja wa shule ya msingi Kisalala kata ya Laela Mwamuzi wa mchezo huo Eliaza Simsokwe ilipofika dk ya 75 alishambuliwa  na kundi la mashabiki na kumvua nguo zake wakiendelea kumpa kipigo

Kipigo hicho kilisababisha mwamuzi huyo kujisaidia haja kubwa kipigo kinachodaiwa kutolewa na wapenzi wa timu ya Serengeti FC wakipinga bao lililofungwa na mchezaji wa timu pinzani ya Muchiza FC, Siyaye Mgonde wakidai alikuwa ameotea kabla ya kufunga.

Meneja wa Timu ya Serengeti FC ya Kisalala , Andrew William alisema kuwa baada ya mwamuzi huyo kuvuliwa nguo na kupata kipigo hicho ilibidi baadhi ya wananchi kuingilia kati na kumwokoa hatimaye mwanamke mmoja alimsaidia kwa kumfunga khanga  ya kumsitili kabla ya  kukimbizwa kituo cha Afya cha Laela kwa ajili ya matibabu.

 Katika vurugu hizo pia wachezaji wawili na kocha watimu ya Serengeti walijeruhiwa na kulazwa kwenye kituo hicho cha Afya pamoja na uharibifu mkubwa wa pikipiki na baiskeli 10 zilizokuwapo uwanjani hapo

Aidha ugomvi huo uliibuka tena majira ya usiku nje ya uwanja ambako watu wanaodaiwa kuwa ni wakazi wa kijiji cha Kisalala walivamia tena wachezaji wa timu ya Serengeti FC na kumjeruhi Peter Willy alijeruhiwa kwa kupigwa panga kichwani na kusababishiwa jeraha kubwa.

Kufuatia hali hiyo uongozi wa Chama cha soka wilayani Sumbawanga (SURUFA) kupitia kwa katibu wake, Kanyiki Nsokolo kimewatahadharisha washabiki wa mchezo huo kuachana na vitendo vya vurugu kwenye michezo mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuwashambulia waamuzi wa mchezo kwa kuwapiga pale wanapochezesha michezo mbalimbali.

Alisema kufanyika kwa vitendo hivyo ni matokeo ya kuendesha masuala ya soka kienyeji pasipo kufuata taratibu ikiwa ni pamoja mashindano hayo kufanywa pasipo kukishirikisha chama cha soka cha wilaya sanjari na kutokuwapo kwa makocha  na waamuzi wenye sifa kwa ajili ya kuchezesha michezo mbalimbali ya soka.


Monday, August 12, 2013

KATALA BEACH HOTEL SINGIDA YAZINDULIWA RASMI

IPO KATIKA MANISPAA YA SINGIDA PEMBEZONI MWA ZIWA SINGIDANI




VYUMBA VYA KULALA VYA AINA ZOTE KWA BEI NAFUU

SINGIDA MANISPAA
Wasanii wakitumbuiza katika viwanja vya hoteli ya Katala Beach Singida wakati wa uzinduzi wa hoteli hiyo uliofanywa na kiongozi wa Mbio za Mwenge 2013 ndugu Juma Ali Simai Agosti 11, 2013







JIKONI

MALIWATO / VYOO VYA NJE


FLAMINGO HALL NA UTEMINI HALL, JENGO LILILOZINDULIWA NA MWENGE

TAYARI WAZUNGU WAMEANZA KUHOTELI YA KBH YA SINGIDANI

MMILIKI WA KATALA HOTELI , KITILA MKUMBO AKIFURAHIA UZINDUZI WA HOTELI YAKE


MMILIKI NDUGU KITILA MKUMBO AKITAFAKARI JAMBO SIKU YA MWENGE 2013

TAARIFA YA UJENZI WA KATALA BEACH HOTELI






TUNAZINDUA KAMA IFUATAVYO



WATANZANIA MSIICHAFUE TANZANIA NJE

WATANZANIA wameaswa kuepuka vitendo vinavyoitangaza Tanzania vibaya nje ya mipaka  vinavyofanywa na baadhi ya wananchi wanapokuwa nje ya nchi yetu na kuharibu taswira ya Tanzania katika ramani ya dunia

Wito huo ulitolewa jana na kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka huu 2013, Juma Ali Simai katika kituo kikuu cha mabasi mjini Singida Agosti 11, 2013 mara baada ya kumaliza mbio za Mwenge wa Uhuru katika Manispaa ya Singida wilaya ya Singida mkoani hapo

Simai alisema hivi sasa kumeibuka tabia ya kuharibu sifa ya Tanzania kitaifa na kimataifa inayofanywa na baadhi ya wananchi wanapokuwa ndani au nje ya nchi kwa vitendo vyao vya kuitangaza vibaya Tanzania kinyume na hali halisi ya Watanzani na mambo yanavyokwenda hapa nchini

Alisema hivi sasa kumekuwa na tabia ya kuilaumu serikali kila kukicha licha ya kuwa serikali imekuwa ikifanya mambo makubwa na ya maana kabisa kwa wananchi kwa lengo la kuwaondoa katika lindi la umasikini na kuhakikisha kuwa lengo la maisha bora kwa kila Mtanzania linafikiwa na kuondoa changamoto zinazowakabili wananchi

Alisema kuna baadhi ya watu wakisafiri kwenda nje kwenye mikutano ya kimataifa wanatumia mwanya huo kuitangaza Tanzania vibaya kwa maslahi yao binafsi bila kujali kuwa kufanya hivyo ni kujiaibisha mwenyewe pia ni kosa mbele ya Mwenyezi Mungu kusema uongo

Alisema wananchi wawe macho na watu hao ambao wamekuwa wakipita huku nakule nchini wakieneza propaganda zisizofaa tena zenye ubaguzi ambapo alisema wengine wamefikia hata kudai kuwa Mwenge wa Uhuru hauna maana kwa nchi yetu ya Tanzania

Mwenge wa Uhuru uko mkoani Singida ambako tayari umemaliza ziara katika wilaya za Iramba na Singida


CHUMBA KIMOJAWAPO KILIVYOPANGWA KWA NADHIFU

WAHUDUMU WAPO FIT


HONGERA KAKA YANGU MAMBO MAKUBWA HAYA

MANDHARI INAVUTA USIKIVU


SIYO ULAYA NI SINGIDA



KITANDA NDANI YA CHUMBA CHA SUIT



SIYO AFRIKA YA KUSINI NI BONGO TENA SINGIDA




PICHA YA PAMOJA

NIMEONA MAMBO MAZURI NDANI MZEE






 ALIYEACHA KUTUMIA MADAWA YA KULEVYA APEWE AJIRA - DC

Singida
MKUU wa wilaya ya Singida mkoani Singida, Mwalimu Queen Mlozi amemuagiza mganga mkuu wa Manispaa ya Singida kumuajiri kijana aliyekuwa anatumia madawa ya kulevya na kuamua kuachana nayo

Agizo hilo lilitolewa na Mkuu huyo wa wilaya kufuatia ushuhuda uliotolewa na kijana Yusufu Saimoni Shumbi mbele ya wananchi katika viwanja vya stendi kuu ya mabasi Singida jana katika ukaguzi wa mabanda ya Mwenge yaliyopo eneo hilouliofanywa na Mkuu wa wilaya

Alisema maelezo ya kijana huyo yanaonesha kuwa miongoni mwa kilichosababisha Yusufu kuanza kutumia madawa ya kulevya ni kukosekana kwa kazi ya kufanya na kumpa vishawishi vya kujiunga na makundi ya madawa ya kulevya hivyo uamuzi wa kwanza wa serikali ni kumpa shughuli ya kufanya kijana

Alisema vijana wanaotumia madawa ya kuelvya wako wengi na wanahitaji kuwafuatilia kwa karibu ili kuwarejeha katika hali ya kawaida na kuokoa nguvukazi ya Taifa hivyo Manispaa ya Singida itafute mbinu za kuwaweka karibu vijana walioko katika janga la madawa ya kulevya waachane na madawa hayo

“Mganga nakupa kazi moja kubwa, kuanzia leo tafuta namna ya kumpa kazi ya kufanya kijana huyu ili asije akarejea katika madawa ya kulevya na taarifa niipate haraka sana” alisema mkuu wa wilaya

Awali akitoa ushuhuda wake Yusufu Saimoni Shumbi amesema alianza kutumia madawa ya kulevya alipokuwa kidato cha pili katika shule ya Sekondari Kikatiti ambako alikuwa na rafiki zake wengine ambao walikuwa wanasoma naye na baada ya kumaliza na kufeli mtihani aligundua kuwa alijipotezea muda shuleni

Alisema kutokana na kutumia madawa hayo alibadilika afya yake akawa anaugua mara kwa mara kichwa, mwili kulegea na kukosa kumbu kumbu pamoja na kukosa uwezo wa kujimudu katika baadhi ya matendo kutokana na mwili wake kulegea mikono na mikono

Alisema hivi sasa ameamua kurudia mtihani wa kidato cha nne kwani awali alifanya mtihani huo na kufeli mwaka 2011 lakini kutokana na uwezo mdogo aliokuwa nao kutokana na kutumia madawa ya kulevya alipata daraja la nne alama 30

Kwa upande wake mama mzazi wa Yusufu, Grace Shumbi (50) amesema mwanae ni kitinda mimba katika familia yake ya watoto tisa ambapo wamekuwa wakiishi kwa kutegemea kodi ya nyumba kwani alikuwa akifanya kazi ya kuhubiri neon la Mungu katika shirika la Life Ministry na kustaafu miaka kadhaa iliyopita

Amesema mwanae licha ya kuwa na hali hiyo amekuwa mwaminifu sana nyumbani kwani hata ujenzi wa nyumba kubwa wanayokaa hivi sasa aliisimamia Yusufu wakati huo mama yake akiwa anatibiwa hospitali

Amesema hivi sasa Yusufu anamdai ada akalipe shule ili asome upya aweze kurudia mtihani wa kidato cha nne ili aweze kuendelea na masomo kwani anaelewa kuwa ana uwezo wa kuendelea kusoma shule na kufaulu hadi chuo kikuu bila shida ikiwa tu atapata ada