Thursday, March 8, 2012

MKOA WA KATAVI NA FURSA ZINAZOPATIKANA: MKUU WA WILAYA ATEMBELEA KATA ZA H/MJI

DC MPANDA ATOA SIKU KUMI NA NNE WALOFAULU KURIPOTI SHULENI
SERIKALI ya wilaya ya Mpanda mkoa tarajiwa wa Katavi imeuagiza uongozi wa Kata ya Ilembo mjini Mpanda kuwasilisha kwake majina ya wahamiaji haramu walioingia katika kata hiyo ili waweze kushughulikiwa mapema iwezekanavyo
Agizo hilo limetolewa na mkuu wa wilaya hiyo Dr Rajabu Rutengwe katika mkutano wa hadhara mara baada ya kuelezwa kero kubwa ya wakulima na wafugaji iliyopo katika kata hiyo iliyodumu kwa takribani miaka mine sasa.
Awali akitoa ufafanuzi wa kaero hiyo afisa mtendaji wa kata ya Ilembo Marry Ngomarufu amesema kuwa ofisi ya kata imeweza kutumia ofisi ya polisi na mahakama kushughulikia migogoro hiyo ingawa bado hali haijaweza kutengamaa kiasi cha kutosha
Mkuu wa wilaya ya Mpanda amesema migogoro mingi ya wahamiaji haramu hasa wafugaji toka mikoa ya kanda ya Ziwa kutokana na baadhi ya wananchi kuuziana maeneo na wafugaji kwa tamaa ya pesa kwa wenye mashamba na badala yake wameuza fursa zao na kuleta migogoro kwa sababu majirani na eneo lililonunuliwa na wafugajia au mfugaji mmoja wao wakauwa wanaendelea kulima na hiyo inakuwa ni sehemu ya chakula cha mifugo na ng’ombe hawana mipaka kama binadamu
Akihutubia wananchi katika mkutano wa hadhara Ilembo mkuu wa wilaya amesema urithi pekee kwa motto ni elimu na siyo majumba na magari hivyo amewataka wananchi mahala popote wasimamie watoto kusoma kwa bidii na kuzitumia kwa uhakika fursa za kupata elimu zilizopo b ila kujali kipato cha mzazi au mlezi kwani ni hazina ya baadae kwa wilaya, mkoa na hata taifa kwa ujumla
Amesema hivi sasa serikali imeweka mazingira ya kuhakikisha kuwa watoto wote wanapata elimu ya msingi na sekondari hata kama hawana uwezo kifedha kwani hivi sasa kila kata ina sekondari yake inayotoa fursa kwa watoto wote walioko katika kata kuendelea na masomo ya sekondari pindi wanapofaulu mtihani wa darasa la saba.
Pia mkuu wa wilaya hiyo Dr Rajabu ameagiza watoto wa kike kumi na mmoja waliofaulu kuingia kidato cha kwanza hawajaripoti shuleni wafike shuleni ndani ya kipindi cha siku kumi na nne kuanzia Machi 6, 2012 wawe wamshaanza masomo na taarifa toka kwa mkuu wa shule iwasilishwe kwake baada ya siku kumi na nne kabla serikali ya wilaya haijaanza kuwafuatilia kisheria kwa nini hawajaripoti shuleni kuanza na masomo ya sekondari.
Amewasihi wananchi kuanza kujenga majengo yanayoendana na hadhi ya manispaa kwani muda wa miezi michache ijayo halmashauri ya mji Mpanda utakuwa na hadhi ya manispaa baada ya mkoa wa Katavi kuanza ili kuanza na kasi ya maendeleo ya mkoa wa Katavi ambao umenza kukimbia kimaendeleo kabla ya kuanza kazi rasmi.
Amewahimiza wananchi wa Ilembo kuanza kufanya miradi ya ufugaji kuku hasa akina mama ambao wanaweza kuwa karibu na mifugo hiyo kwani hivi sasa kuku mmoja anauzwa kwa bei ya shilingi elfu kumi na mbili kwa kuku mmoja mdogo na hivyo ukianza kufuga makoo mmmoja akapewa pumba anaweza kuzaa vifaranga mia moja na arobaini kwa mwaka sawa na kuingiza kipato cha shilingi milioni mbili na laki nne kwa mwaka kutoka kwenye kuku mmoja.
Amesema mkoa utakapoanza wageni wanaohitaji kula kuku wataongezeka mara dufu ya sasa na bei itaongezeka mara mbili ya sasa,
“Mnapopita mjini fikeni nyumbani kwangu muone kuku ninaofuga ni wakubwa na ni wengi na nikiwaingiza sokoni sikosi shilingi elfu kumi na tano taslimu” alisema mkuu wa wilaya
Ametoa mfano wa mhe. Waziri Mkuu Mhe. Pinda ambaye anafuga nyuki ambao ni wadudu lakini wana faida kubwa kwa mfugaji na mlaji wa asali kwani hivi sasa bei ya lita moja ya asali ni shilingi elfu kumi wakati mzinga mmoja unaweza kutoa lita arobaini za asli kwa msimu mmoja tu sawa na kuwa utaweza kuvuna shilingi laki nne za mauzo ya asali kwa msimu mmoja, je kwa mwenye mizinga kumi atapata kiasi gani kwa msimu ihali hana gharama ya kuwalishia wala kuweka dawa
Ametoa wito mkwa wananchi kuanza kuzitumia fursa zilizopo za shughuli za kiuchumi ili kusaidia kuwa na miradi inayoweza kusaidia kuondokana na kero za ukosefu wa kipato
Aidha amewasihi wananchi kuanza kujiandaa kwa sense ya watu na makazi itakayofanyika mwezi Agosti mwaka huu kwani tayari maandali yameanza kufanyika na shughuli za msingi za maandalizi ya sense zimekamilika bado mambo machache.


TUMIENI MAJIKO RAFIKI WA MAZINGIRA - MAKAMU WA RAIS
WAKAZI wa mkoa wa Rukwa wametakiwa kutumia majiko yanayotumia kuni na mkaa kidogo ili kupunguza uharibifu wa mazingira katika mkoa huo
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr Mohamed Gharib Bilal, alitoa rai hiyo jana katika mkutano wa Hadhara katika uwanja wa kumbu kumbu ya Nelson Mandela mjini Sumbawanga
Alisema hivi sasa mkoa wa Rukwa umeanza kupoteza misitu mingi kutokana na kushamiri kwa vitengo vya uharibifu wa mazingira katika maeneo mengi ya mkoa huo vinavyochangiwa na shughuli mbali mbali za binadamu
Alisema kuchoma moto kiholela kunachangia sana kuua mbegu za miti na misitu mingi kuendelea kuteketea kwani miti iliyopo nayo inaendelea kuteketezwa na wachoma mkaa pamoja na matumizi ya kuni kwa ajili ya kupikia.
“hivi sasa ukipita katika maeneo karibu yote vijijini hasa vijiji vya wilaya ya Sumbawanga kumebaki upara licha ya kuwa maeneo hayo yalikuwa na misitu minene tena ya kutisha” alisema Dr Bilali
Alisema umefika wakati wananchi wa Rukwa waanze kubadili tabia na kuona suala la uharibifu wa mazingira kuwa ni sawa na janga la mkoa mzima na lianze kushughulikiwa kwa mikakati maalumu itakayosimamiwa vema na kupunguza uharibifu uliopo sasa.
Alisema kuwa moto kichaa ni moto ambao unachomwa pasipo misingi ya kiutaalamu kwani hata wanaosafisha mashamba wanatumia kuchoma moto na kuuacha unaendelea kuangamiza misitu mingine
Katika mkoa wa Rukwa kumekuwa na utamaduni wa kuchoma moto hasa nyakati za kiangazi kwa lengo la kuwinda, kuchimba panya, kusafisha mashamba baada ya kuvuna mazao pamoja na kutenga maeneo ya kuchungia mifugo yao.
Maeneo yaliyoathirika na uharibifu wa mazingira kwa kiwango kikubwa ni pamoja na wilaya ya Nkasi, Sumbawanga vijijini , wilaya ya kalambo na kata za Inyonga, Kasokola, Mpanda mjini, Magamba, Nsimbo, Uruila na Mtapenda katika wilaya ya Mpanda.
MWISHO
MKOA WA KATAVI NA FURSA ZINAZOPATIKANA: MKUU WA WILAYA ATEMBELEA KATA ZA H/MJI
 Pia fungua www.sumiampanda.blogspot.com

No comments: