USIPOTEZE MUDA FUNGUA www.habarikatavi.wordpess.com
Katavi
BARAZA la madiwani la Halmashauri ya Mji wa Mpanda Mkoa wa Katavi limepitisha bajeti ya shilingi Bil 36 katika mapato yake ya 2014 na 2015
Kwa mujibu wa ndugu Suleimani Lukanga ambaye ni Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo, halmashauri yake inatarajia kujipatia kiasi cha shilingi 36, 229,866,934 katika mwaka wa fedha wa 2014/15.
Lukanga alibainisha hayo katika kikao maalumu cha Baraza la Madiwani kilichofanyika Jumatano Januari 15, 2014 katika ukumbi wa Chuo Kikuu Huria cha Mkoa wa Katavi mjini Mpanda
Alisema ofisi yake imeandaa Bajeti hiyo kwa kuzingatia mwongozo wa Bajeti ya Taifa ya kuondoa umasikini ambapo kati ya Fedha hizo Sh 8,192, 020,461 ni mishahara ya watumishi ruzuku ya kutoka Serikali kuu.
Aidha alisema matumizi mengine ya fedha za Maendeleo ni Sh 25,535,581,473 na fedha za makusanyo ya ndani na makusanyo ya huduma za afya na na ada za Sekondari halmashauri hiyo inatarajia kukusana Sh 1,285,460
Alisema pia alimashauri hiyo imeomba maombi maalumu nje ya ukomo wa Bajeti shilingi 3,302 500,000 na kufanya bajeti hiyo kufikia Sh 39,532,366,934
Alisema Bajeti ya mwaka wa 2013 na 2014 Halmashauri ya mji wa Mpanda iliidhinisha jumla ya shilingi 12,833,792,818 lakini hadi kufikia Novemba 2013 Halmashauri ilikuwa imepokea jumla ya Sh 4,165,656,732 ambazo ni sawa na asilimia 28 ya Bajeti iliyoidhinishwa kwa mwaka wa fedha wa 2013 na 2014-01-15
Aidha alieleza kuwa ongezeko hilo la Bajeti limeongezeka kutokana na ongezeko la watumishi wa ajira mpya na ongezeko la miradi ya maendeleo katika kata zote tisa za Halmashauri hiyo pamoja na huduma mbalimbali
Hata hivyo Lukanga alisema Bajeti ya msimu uliopita ya mapato ya ndani ilikuwa ni Tsh Milioni 926,422 wakati msimu wa Fedha wa mwaka huu mapato ya ndani ni Tsh Bilioni 1,285,460,000 ambalo ni sawa la ongezeko la asilimia 38.8 ya Bajeti ya Halmashauri ya msimu uliopita
mwisho