WATEKAJI WA BASI LA SUMRY KATAVI MBARONI
Basi mojawapo la kampuni ya Sumry linalotoa huduma katika mikoa ya Rukwa na Katavi |
WATUHUMIWA wa utekaji wa basi la sumry katika tukio la wiki
iliyopita wanashikiliwa na jeshi la polisi mkoa wa Katavi wakiwamo wakimbizi
kutoka nchi jirani ya Burundi.
Jeshi la polisi mkoani Katavi limetoa taarifa kuwa jumla ya
watuhumiwa kumi na mbili wamekamatwa kwa tuhuma za kuliteka basi la kampuni ya
usafishaji ya Sumry High Class lenye namba T107BHT wiki iliyopita katika kijiji
cha Magamba wilaya ya Mlele mkoa wa Katavi kilometa nne toka Mpanda mjini.
Kaimu Kamanda wa polisi mkoa wa Katavi Joseph Myovella
alisema Oktoba 26, 2012 kuwa watuhumiwa hao wamekamatwa wakiuza simu za mkononi
zilizochukuliwa katika tukio la utekaji wa basi la Sumry ambapo baada ya
kuhojiwa walikiri na kuwataja waliokuwa nao.
Alisema katika upelelezi kwa kutumia tekionolojia ya
mawasiliano mtambo maalum uliweza kubaini kuwapo matumizi ya simu
zilizochukuliwa katika eneo la mkoa wa Katavi ndipo waliweza kufuatilia vipimo
na kufanikiwa kuwakamata watuhumiwa wakiziuza simu hizo licha ya kuwa zilikuwa
zimebadilishwa laini zake.
“Kwakutumia tekinolojia tumeweza kuzisoma simu
zilizochukuliwa katika tukio hilo zikisomeka katika mtandao kuwa zinatumika
katika eneo la mkoa wetu wa Katavi tukaanza kuzifuatilia hadi tukafanikiwa
kuwakamata watuhumiwa moja baada ya wmingine hadi kufikia idadi ya kumi na
mbili” alisema Myovella.
Alifafanua kuwa hivi sasa bado jeshi lake linaendelea na
uchunguzi zaidi na hivyo majina ya watuhumiwa yatawekwa wazi mara baada ya
kukamilika upelelezi ambapo silaha zilizotumika zilikuwa ni mapanga, nondo na
fimbo.
Jeshi hilo lilitoa wito kwa wananchi kutokununua simu
zinazouzwa mitaani kwani kwa kufanya hivyo wanaweza kuingia kwenye mkubo wa
utekaji basi kwa sababu sasa hivi tekinolojia inayotumika inaonesha mtumiaji wa
simu iliyochukuliwa katika utekaji wa basin a mahali alipo mtumiaji kiasi
kwamba endapo mtu atanunua simu hiyo atakamatwa na kwa utaratibu wa upelelezi
atajumuishwa katika orodha ya watuhumiwa.
Alisema kati ya watuhumiwa hao kumi ni Watanzania na wawili
ni Raia wan chi jirani ya Burundi wanaoishi kama wakimbizi katika makazi ya
wakimbizi ya Katumba.
Watu
wanane wenye silaha zikiwamo za jadi wameliteka basi la abiria la Sumry
baada ya kuweka kizuizi cha magogo na mawe katika msitu wa Msaginya
kijijini Magamba wilayani Mlele katika Mkoa wa Katavi katika barabara
kuu ya Sumbawanga – Mpanda.
Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Katavi, Dhahiri Kidavashari, uhalifu huo ulifanyika saa sita usiku wa kuamkia jana ambapo gari hilo lenye namba za usajili T107 BHT lililokuwa likisafiri kwenda mjini Mpanda likitokea mjini Sumbawanga.
Akifafanua, alisema basi hilo lilipofika eneo hilo lenye mteremko na kona kali ambalo lipo kilometa 15 kutoka Mpanda Mjini, lilikumbana na vizuizi vya mawe na magogo ndipo lilipolazimika kusimama ghafla.
Inadaiwa kuwa ndipo walipojitokeza watu wanane waliokuwa mafichoni wakiwa na silaha za jadi zikiwamo mapanga, nondo, mawe na visu na kuwalazimisha abiria wote kushuka ambapo walipekuliwa na kuporwa simu za mkononi 15 na kiwango kikubwa cha fedha, thamani halisi haijafahamika.
Kwa mujibu wa taarifa nyingine kutoka eneo hilo zinadai kuwa baadhi ya abiria walidhalilishwa kwa kuvuliwa nguo maungoni mwao wakati walipokuwa wakipekuliwa na watu hao ambao kila aliyeshuka garini, alilazimishwa kukabidhi chochote alichokuwa nacho kisha walilazimishwa kulala chini.
Kwa mujibu wa mtoa habari kutoka eneo la tukio ambaye hakuwa tayari jina lake liandikwe alisema baadhi ya abiria walikumbwa na adha hiyo walikuwa wanawake na watoto ambapo mmoja wao alikuwa mtawa wa kike ambaye inadaiwa alikuwa akisafiri kwenda Mwanza.
Hata
hivyo, Kamanda huyo alikanusha abiria yeyote aliyevuliwa nguo ila
walilazimishwa kulala chini baada ya kuamriwa kushuka garini na gari
hilo baadaye liliwafikisha abiria wake hadi Mpanda Mjini.
Kwa
mujibu wa Kidavashari kutokana na tafrani hiyo, watu wanane wakiwamo
dereva wa gari, Said Chile na utingo wake ambaye jina lake
halikufahamika mara moja walijeruhiwa na kukimbizwa katika Hospitali ya
Wilaya mjini Mpanda kwa matibabu.
Kamanda alisema Polisi inafanya msako mkali kuwasaka watu hao ambao hadi sasa hawajapatikana na haijulikani walikojificha kwani walikimbia kusikojulikana baada ya kufanya uhalifu huo. (Na Ziro99 blog)