|
Meza kuu ikiwa na
bango lenye ujumbe mzito kutoka katika nukuu za Mheshimiwa Rais na
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete. |
|
Katibu wa
Halmashauri kuu Taifa (NEC) Siasa na Mahusiano ya Kimataifa Mhe. January
Makamba akisalimiana na wageni waalikwa kutoka katika jumuiya za vijana
vyama mbalimbali kusini na afrika ya kati. |
|
Makatibu wa
halmashauri kuu (NEC) kutoka Kulia Uchumi na Fedha Mhe. Mwigulu Nchemba,
Siasa na Mahusiano ya Kimataifa Mhe. January Makamba na Itikadi na
Uenezi Ndugu. Nape Nnauye. |
|
Vijana wa Chama Cha Mapinduzi ambao pia ni wajumbe wa Mkutano Mkuu wa nane wa Umoja wa Vijana wa CCM. |
|
Vijana mbalimbali ambao wanawakilisha mikoa wakiwa na mabango ambayo yanaonyesha Mikoa wanayotoka. |
|
Mheshimiwa Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambae pia ni Mwenyekiti wa Chama Cha
Mapinduzi akisalimiana na viongozi mbalimbali wa chama hicho ambao
walimpokea akiwa anaingia katika ukumbi wa mkutano wa nane wa vijana wa
chama cha mapinduzi. |
|
Kaimu Mwenyekiti
wa Umoja wa Vijana Ndugu Benno Malisa akimueleza jambo Mwenyekiti wa
Chama cha Mapinduzi Mhe. Jakaya Kikwete katika Mkutano huo. |
MWENYEKITI CCM TAIFA AWAPA UKWELI UVCCM
Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) wanaendelea na
Mkutano Mkuu wa Taifa ambapo wanatarajia kuchagua viongozi mbalimbali
katika ngazi ya Taifa ya jumuiya hiyo, ambapo jumla ya wagombea 133
wamejitokeza kuwania nafasi hizo ambazo ni nafasi ya Mwnyekiti, Makamo
Mwenyekiti, Wajumbe wa Halmashauri kuu ya Chama cha Mapinduzi (NEC)
kupitia jumuiya ya vijana, ambapo nafasi (6) zinatoka bara na (4)
zinatoka Tanzania Visiwani, nafasi nyingine ni Baraza Kuu Taifa, Viti 5
Bara na 5 Zanzibarm Nafasi ya Uwakilishi WAZAZI Taifa na mwisho ni
nafasi ya uwakilishi UWT Taifa.
Mkutano Mkuu huo wa UVCCM umefunguliwa Na Mwenyekiti wa Chama cha
Mapinduzi ambae pia ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.
Jakaya Mrisho Kikwete, ulianza Rasmi, saa 4 asubuhi, ambapo Mhe. Rais
alifanya ufunguzi kwa Hotuba makini, iliyoeleza mambo makubwa na ya
msingi juu ya Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM).
Mhe. Jakaya Kikwete alisisitiza na kukumbusha juu ya Lengo kuu na
Dhumuni Kuu la Chama Cha Mapinduzi lililotajwa katika katiba yake Ibara
ya 5 ambayo inaeleza bayana kuwa ni kushinda uchaguzi na kushika dola.
Lakini pia akaeleza kuwa CCM kinategemea jumuiya yake hiyo kufanya kazi
ya siasa miongoni mwa vijana wa Tanzania na kushawishi wakubali kuwa
wanachama na wapenzi wa CCM. Akasisitiza kuwa matumaini makubwa ya
msingi kuliko yote ya Chama Cha Mapinduzi ni kuona jumuiya yake hiyo
inakuwa MKOMBOZI wa vijana.
Mhe. Kikwete akawataka wahakikishe kuwa wanapata Viongozi
ambaowataongoza vyema, watakaoongoza juhudi za kuendeleza, kutetea na
kulinda maslahi ya CCM. Viongozi wanaoijua na kuipenda jumuiya ya
Vijana.