RAIS Jakaya Mrisho Kikwete amewka jiwe la Misngi katika mradi mkubwa
wa umeme wenye thamani ya shili Bilioni 12 kwa ajili ya Miji ya
Namanyere na Sumbawanga mkani Rukwa. Mradi huo uliwekewa jiwe la msingi katika eneo la Mitambo ya umeme ya shirika la umeme nchini TANESCO mjini Sumbawanga Jumamosi iliyopita unajumuisha mashine nne kubwa zenye uwezo wa kuzalisha kilowatt 5 za umeme kwa wakati mmoja zilizonunuliwa na serikali kwa gharama ya shilingi Bilioni 3.
Akitoa taarifa mbele ya Mheshimiwa Rais Waziri wa Nishati na Madini Wiliamu Ngeleja alisema kuwa mradi huo wa umeme unaanza Julai 2010 na kukamilika Juni 2011 ambapo waziri huyo alimueleza rais kuwa umeme utaanza kuwaka mjini Namanyere Machi 2011. Aidha Waziri Ngeleja alisema kuwa mradi huo utawawezesha wananchi waishio katika vijiji vinavyopitiwa na nguzo za umeme katika barabara ya kuelekea Namanyere mjini kupatiwa umeme kwa ajili ya matumizi ya majumbani na matumizi mengine kama ilivyo kwa wananchi wa mijini.Waziri Ngeleja alisema kuwa Serikali imeondoa gharama za nguzo kwa wananchi wa vijijini ili kupunguza gharama za kuingiza umeme katika nyumba zao na badala yake gharama za nguzo zitakzotumika kuingizia umeme kwa wananchi serikali ndiyo itakayogharamia kutokana na ukweli kuwa wananchi wa vijijini wana kipato kidogo ukilinganisha na waishio mijini.
Naye Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. Jakaya Mrisho Kikwete aliwataka wananchi wa vijiji husika kuanza kujiandaa kuupokea umeme pindi utakapofika ikiwa ni pamoja na kuachana na ujenzi wa nyumba za nyasi kwa rais alisema nyasi hazipatani na umeme “ Ndugu zangu wananchi wa Kipande na wengine walioko katika njia hii, changamkieni umeme huu ili mpate maendeleo ya haraka, acheni kujenga nyumba za nyasi kwa sababu umeme na nyasi haviendani, jengeni nyumba bora hivi sasa ili umeme ukifika kijijini kwenu muupokee na kuanza kuufaidi” alisema Mhe. Rais Rais Kikwete alisema hivi sasa wananchi wa Rukwa neema imewashukia kwani tayari umeme wanatarajia kuupata wa uhakika, barabara nazo zinajengwa kwa kiwango cha lami na pia kuna maboresho ya kilimo kupitia dhana ya KILIMO KWANZA.
Alifafanua kuwa kilimo kikizalisha mazao ya kutosha sasa wananchiwataweza kusafirisha mazao hadi kwenye soko bila matatizo na tena wakiuza mazao kwa bei nzuri katika soko wataweza kuutumia umeme
kujiletea maendeleo na hayo ndo maisha bora kwa kila Mtanzania.
MWISHO
No comments:
Post a Comment