MARTIN DESTIO (27) anaishi kwa mateso makali kutokana na mguu wake wa kushoto kuharibika vibaya kwa vidonda viwili vinavyomsumbua kwa muda wa miaka nane sasa.
Kijana huyo mkazi wa Mjimwema mjini Mpanda anawaomba wasamalia wema wenye mapenzi mema kumchangia gharama za matibabu ili aweze kupona na kurejea katika hali yake ya kawaida
Akizungumza na mwandishi wa habari hizi jana Jumamosi April 21, 2012 alisema kuwa alipata jeraha la kidonda mwaka 2004 asubuhi alipokuwa akiwahi ibada ya kanisani kutumikia kama alivyokuwa amezoea akiwa njiani alijikwaa kwa kijiti kilichomkwangua na kumchubua kasha damu ikatoka kiasi
Alisema siku hiyo aliona kama kijidonda cha kawaida lakini siku zilivyozidi kusonga mbele ndivyo na kidonda kilivyozikdi kukua huku akiendelea kupata matibabu katika hospitali ya wilaya ya Mpanda
Alisema hali ilipozidi kuwa mbaya alipata msaada kutoka kwa Mhe. Pinda, Waziri Mkuu akaenda kutibiwa hospitali ya Muhimbili jijini DSM lakini haikusaidia akapewa rufaa ya kwenda kutibiwa nchini India
Wakati akitafuta ufadhiri wa kwenda India alisema alijitokeza msamaria mmoja aliyemtaja kwa jina la Raju na kumpeleka hospitali ya CCBRT DSM ambako waliweza kukata sehemu ya mwili wake na kuuotesha katika kidonda akaanza kupata nafuu
Alisema baada ya muda mfupi alianza kuona mabadiliko ya kidonda kuanza kuongezeka akarejea hospitali ya CCBRT akapewa rufaa ya kwenda India ambapo alipopigiwa hesabu ya gharama akaambiwa inatakiwa shilingi milioni kumi na nne (14,000,000/=) kwa safari na matibabu
Alisema amejaribu kuomba wahisani na kufanikiwa kupata shilingi milioni nne (4,000,000/=) bado milioni kumi (10,000,000/=) hivyo wewe msomaji tunakuomba utoe msaada kwa kuchangia japo kiasi chochote ulichonacho.
Mchango wako wasilisha kwa njia utakayoona inafaa, piga simu namba 0767 519989 au 0784 519988 au fika ofisi ya Waziri Mkuu wasilisha mchango wako au wasiliana na mbunge wa jimbo la Mpanda mjini Mhe. Said Amour Arfi 0786001122 au mbunge wa viti maalumu mkoa wa Katavi mhe Pudensiana Kikwembe 0759457879
Taarifa za hivi punde kutoka Bungeni Mjini Dodoma,zinaeleza kuwa Kusudio la Mbunge wa Jimbo la Kigoma Kaskazini,Mh. Zitto Kabwe la kutaka kupiga kura za kuanzishwa kwa mjadala wa kutokuwa na imani na Waziri Mkuu,Mh. Mizengo Pinda,limepigwa chini na Spika wa Bunge,Mh. Anne Makinda.
Akisoma kanuni za Bunge,Mh. Spika alisema kwa mujibu wa kanuni za Bunge na Katiba ya Nchi,kusudio la kutaka kumuondoa Madarakani Waziri Mkuu kwa kupiga kura ya kutokuwa na Imani nae ambayo ni taarifa ya maandishi inapaswa kuwasilishwa kwake siku 14 kabla ya siku husika.
Hivyo kwakuwa ofisi yake haijapata taarifa ya maandishi ju ya zoezi hilo,basi zoezi hilo moja kwa moja litakuwa ni batili, na kwasababu kikao hicho cha Bunge kinatarajiwa kufungwa siku ya jumatatu,basi hakutakuwa na uwezekano wa zoezi hilo kukamilika.
Awali Mbunge wa Jimbo la Bumbuli,Mh. January Makamab aliomba muongozo wa Spika kuhusu jambo hilo ndipo Spika,Mh. Anne Makinda akasimama na kutoa ufafanuzi huo.Na www.issamichuzi.blogspot.com
WAKUVANGA WA ORIJINO KOMEDY APAGAWISHWA NA ULANZI IRINGA msanii wa Orijino Komedy Bw.Wakuvanga akinywa pombe ya asili ya mkoa wa Iringa Ulanzi eneo la Kihesa mjini Iringa jioni hii Jasiri haachi asili ama mdharau kwao ni mtumwa ni vigumu sasa na wasanii kupenda pombe za asili kama hivi Hapa wakipokezana lita ya ulanzi Wakuvanga akiwa na wadau eneo la Kihesa mjini Iringa huku gari lao likiwa limechafuliwa kwa kuchorwa kwa tope Wakuvanga akionyesha gari lake lilivyochafuliwa kwa tope
Kocha
Kim Poulsen anayeinoa timu ya vijana wenye umri chini ya miaka 20 cha
Tanzania (Ngorongoro Heroes) ameahidi kikosi chake kufanya vizuri kwenye
mechi dhidi ya Sudan.
Akizungumza
jana (Aprili 20 mwaka huu) kwenye mkutano na Waandishi wa Habari,
Poulsen amesema timu yake imejiandaa vizuri kwa mechi hiyo na kiu yao ni
kushinda.
Kwa
upande wake Kocha wa Sudan, Azhari Osman El Tahir amesema ingawa
haifahamu vizuri timu ya Tanzania, lakini wamejiandaa kushinda kwani kwa
muda mrefu walikuwa hawajashiriki mashindano ya vijana ya kimataifa.
Mechi
hiyo ya michuano ya Afrika kwa vijana wenye umri huo itachezwa kesho
(Aprili 21 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kuanzia saa 10
kamili jioni kwa viingilio vya sh. 3,000, sh. 5,000, sh. 10,000 na sh.
15,000.
Sudan
iliwasili nchini jana (Aprili 19 mwaka huu) ikiwa na kikosi cha
wachezaji 20, viongozi kumi na mwandishi wa habari mmoja kwa ajili ya
mechi hiyo ya kwanza kabla ya timu hizo kurudiana jijini Khartoum kati
ya Mei 4, 5 na 6 mwaka huu.
Mechi
hiyo itachezeshwa na mwamuzi Brian Miiro atakayesaidiwa na Mark Ssonko,
Lee Patabali na Denis Batte wote kutoka Uganda. Ejigu Ashenafi wa
Ethiopia ndiye atakayekuwa Kamishna wa mechi hiyo namba 15.
Fainali
za Afrika kwa michuano hiyo zitafanyika Machi mwakani nchini Algeria
wakati za Dunia zitafanyika nchini Uturuki kuanzia Juni hadi Julai
mwakani. Katika fainali za Dunia, Afrika itawakilishwa na timu nne za
kwanza kwenye fainali za Algeria.
MALINZI MGENI RASMI MKUTANO MKUU TFF
Mwenyekiti
wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT), Dioniz Malinzi anatarajia kuwa
mgeni rasmi kwenye ufunguzi Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Shirikisho la Mpira
wa Miguu Tanzania (TFF) utakaofanyika kwa siku mbili (Aprili 21 na 22
mwaka huu) kwenye ukumbi wa NSSF Waterfront jijini Dar es Salaam.
Wajumbe
wa mkutano huo watawasili jijini kesho (Aprili 20 mwaka huu) na
watafikia kwenye hoteli ya Royal Valentino. Wajumbe wanatoka katika
vyama vya mpira wa miguu vya mikoa, vyama shiriki na klabu za Ligi Kuu
ya Vodacom.
Mkutano
huo utakaoanza saa 3 asubuhi utakuwa na ajenda kumi na moja. Baadhi ya
ajenda hizo ni hotuba ya Rais wa TFF, taarifa ya utendaji ya mwaka 2011,
bajeti ya mwaka 2012 na taarifa ya ukaguzi wa hesabu (audited
accounts).
MECHI ZA VPL WIKIENDI HII, MAREKEBISHO
Ligi
Kuu ya Vodacom inaingia raundi ya 24 wikiendi hii kwa mechi mbili
zitakazochezwa Aprili 22 jijini Dar es Salaam. Villa Squad itaumana na
African Lyon kwenye Uwanja wa Chamazi wakati Yanga itakuwa mwenyeji wa
Polisi Dodoma katika Uwanja wa Taifa.
Azam
na Mtibwa Sugar zilizokuwa zicheze Aprili 21 mwaka huu sasa zitacheza
Aprili 23 mwaka huu kwenye Uwanja wa Chamazi, Dar es Salaam wakati siku
hiyo hiyo jioni kutakuwa na mechi kati ya Simba na Moro United. Mechi
zote zitaanza saa 10.30 jioni.
Aprili
25 mwaka huu Oljoro JKT itaikaribisha Yanga kwenye Uwanja wa Kumbukumbu
ya Sheikh Kaluta Amri Abeid jijini Arusha wakati JKT Ruvu itakuwa
mwenyeji wa Ruvu Shooting kwenye Uwanja wa Chamazi, Dar es Salaam.
Raundi
ya 25 itakamilika kwa mechi nne; Aprili 28 mwaka huu Coastal Union
itakuwa mwenyeji wa Kagera Sugar kwenye Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga
huku Mtibwa Sugar ikiwa mgeni wa African Lyon kwenye Uwanja wa Chamazi.
Azam na Toto African zitacheza Chamazi, Aprili 30 mwaka huu wakati Mei 1
mwaka huu Villa Squad itaumana na Oljoro JKT kwenye Uwanja wa Chamazi.
Ligi
hiyo itafunga msimu wa 2011/2012, Mei 5 mwaka huu ambapo timu zote 14
zitakuwa uwanjani. Simba vs Yanga (Uwanja wa Taifa), Oljoro JKT vs
Polisi Dodoma (Sheikh Kaluta Amri Abeid, Arusha), Ruvu Shooting vs Villa
Squad (Mabatini, Mlandizi), Coastal Union vs Toto African (Mkwakwani,
Tanga), African Lyon vs JKT Ruvu (Manungu, Morogoro), Azam vs Kagera
Sugar (Chamazi, Dar es Salaam) na Moro United vs Mtibwa Sugar (Jamhuri,
Morogoro).
WASWAZI KUCHEZESHA SIMBA, AL AHLY SHANDY
Shirikisho
la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) limeteua waamuzi kutoka Swaziland
kuchezesha mechi ya kwanza ya 16 bora ya Kombe la Shirikisho kati ya
Simba na Al Ahly Shandy ya Sudan itakayochezwa Aprili 29 mwaka huu
Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Waamuzi
hao wa mechi hiyo namba 71 ni Nhleko Simanga Pritchard atakayepuliza
filimbi wakati wasaidizi wake ni Mbingo Petros Mzikayifani na Sibandze
Thulani. Mwamuzi wa mezani atakuwa Fakudze Mbongiseni Elliot.
CAF pia imemteua Kayijuga Gaspard wa Rwanda kuwa Kamishna wa mechi hiyo.
KAMPUNI NNE ZAPITA TENDA YA TIKETI
Kampuni
nne kati ya sita zimepita hatua ya kwanza ya mchakato wa kupata moja
itakayofanya kazi ya kutengeneza tiketi za elektroniki kwa ajili ya
mechi za Ligi Kuu ya Vodacom na nyingine zinazosimamiwa na Shirikisho la
Kimataifa la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF).
Shughuli
ya ufunguzi wa maombi ya hatua ya awali ya kuonesha nia (Expression of
Interest) kwa ajili ya tenda hiyo ilifanywa jana (Aprili 19 mwaka huu)
na Kamati ya Mipango na Fedha ya TFF ambayo ndiyo Bodi ya Tenda ya
shirikisho.
Kampuni
ambazo zimepita hatua hiyo ya kwanza sasa zinatakiwa kuwasilisha rasmi
tenda zao kwa ajili ya shughuli hiyo ndani ya kipindi cha wiki tatu
tangu ulipofanyika ufunguzi wa hatua ya kwanza.
Baadaye
Bodi ya Tenda itakutana tena kupitia tenda zitakazokuwa zimewasilishwa
na kufanya uteuzi wa kampuni moja itakayofanya kazi hiyo.
Kampuni
ambazo zimefanikiwa kuingia katika hatua hiyo ya pili ni CRDB Bank PLC,
SKIDATA People Access Inc., Prime Time Promotions na Punchlines (T)
Limited.
MATATANI KWA KUKUTWA NA NOTI BANDIA ZA SHILINGI MILIONI MOJA ZA TANZANIA
JESHI la polisi wilaya ya Mpanda mkoa wa Katavi
linamshikilia mtu mmoja kwa tuhuma za kukutwa na noti bandia zenye thamani ya
shilingi milioni moja.
Tukio hilo la aina yake limetokea katika kijiji cha
Kakese Mbugani nje kidogo ya mji wa Mpanda majira ya saa tisa alasiri ambapo
aliyekamatwa ametajwa kuwa ni Gwisu Jishosha Bunhyawandama (38) mkazi wa kijiji
cha Kashishi tarafa ya mpimbwe wilaya ya Mlele.
Taarifa kutoka kwa diwani wa kata ya Kakese, Mhe.
Maganga Mussa Katambi imesema kuwa mtuhumiwa alifika kijijini hapo alhamisi
Aprili 19, 2012 kwa lengo la kununua ng’ombe katika mnada uliofanyika leo
Aprili 20, 2012 na ilipofika majira ya mchana mtuhumiwa alinunua ng’ombe mmoja
kwa bei ya shilingi laki tatu na sabini elfu na kasha kumuuza papo hapo kwa bei
ya shilingi laki tatu na nusu.
Diwani Maganga amesema kuwa baada ya kuuza huyo ng’ombe
watu walianza kuchunguza sababu za kumuuza huyo ng’ombe ndipo walipobaini kuwa
pesa alizonazo ni za bandia ndipo walimkamata kwa kutumia mgambo na kuanza
kumshambulia hali iliyotishia maisha yake kwani walitaka kumchoma kwa moto.
Amesema kuwa viongozi wa kijiji waliamua kuingilia kati
na kumkamata kisha wakamfikisha kituo cha polisi ambapo alikuwa na noti za
shilingi elfu kumi kumi zikiwa katika mafungu kwa nambari BT 2145563, BH 4262398, BK 3272328, BE
9452918 na BF 2131869 shilingi za Tanzania
Akizungumza na mwandishi wa habari hizi mtuhumiwa alidai
kupewa pesa hizo na mfanyabiashara wa ng’ombe aliyemtaja kwa jina la Yenze
Bundala mkazi wa Kijiji cha Kashishi wilaya ya Mlele mkoa wa Katavi.
Mwisho.
FUSO LAUA WATATU, TISA WAJERUHIWA
WATU watatu wamefariki dunia katika ajali ya gari aina
ya fuso iliyotokea katika mlima Lyamba mpakani mwa mkoa wa Rukwa na Katavi
Kamanda wa jeshi la polisi mkoani Rukwa Isuto Mantage
amesema ajali hiyo ilihusisha lori aina ya Fuso lenye namba ya usajiri T620ABA
mali ya Eliud Sanga mkazi wa kijiji cha Laela mkoani Rukwa
Amesema katika ajali hiyo watu watatu wamefariki dunia
na wengine tisa wamejeruhiwa na kulazwa katika hospitali ya wilaya yam panda mkoa
wa katavi na wengine katika hospitali ya wilaya ya Nkasi mjini Namanyere
Amewataja waliofariki dunia kuwa ni Maha Lukwetula (51)
mkazi wa shankala wilaya ya Mpanda, Kanwa (36) mkazi wa kijiji cha Itenka
wilaya ya Mpanda na mtoto wake mwenye umri wa miaka mine (4) ambaye jina lake
halikuweza kupatikana
Amewataja waliojeruhiwa kuwa ni Jeshi Charles (33) mkazi
wa Namanyere, Juma Lukwetula (40) mkazi wa Shankala, Thomas Simwinga (25) mkazi
wa Laela, Sailas Kuzenza (30) mkazi wa Mpalamawe na Linusi Kidomu (36)
Amewataja waliojeruhiwa wengine kuwa ni Shukuru Rafael
(9) mkazi wa Laela, Francis Kidomu (24) mkazi wa Londokazi wilaya ya Nkasi na
mmoja wao hajafahamika kwani hajitambui hawezi kuongea ambapo wote wamelazwa
katika hospitali ya wilaya ya Mpanda
Amesema majeruhi Saidi (25) ambaye amekatika miguu yote
miwili amelazwa katika hospitali ya wilaya ya Nkasi kutokana na hali yake kuwa
mbaya
Kamanda Mantage amesema chanzo cha ajali ni kukatika kwa
breki za lori hilo lilipokuwa likiteremka mlima Lyamba Lyamfipa Aprili 19, 2012
majira ya saa 8:30 mchana na dereva wa lori hilo anatafutwa na jeshi la polisi
baada ya kukimbia mara baada ya ajali kutokea.
Mpaka sasa wabinge waliosaini kura ya kutokuwa
na imani na Waziri Mkuu Pinda, kati ya majina 54 hapo chini ni wawili tu kutoka
CCM ndiyo wamesaini. Majina ya Wabunge walio-sign Vote of No Confidence hadi
sasa hivi 1.Rashid Ali Abdallah CUF 2.Chiku Aflah Abwao CDM 3.Salum Ali Mbarouk
CUF 4.Salum Khalfam Barwany CUF 5.Deo H Filikuchombe- CCM 6.Pauline P.
Gekul-CDM 7. Asaa O Hamad-CUF 8.Prof.Kuliyokela Kahigi- CDM 9.Naomi M Kaihula –
CDM 10.Sylvester Kasulumbayi- CDM 11. Raya Ibrahim Khamis - CDM 12.Mkiwa H. Kiwanga
CUF 13.Susan L Kiwanga-CDM 14.Grace S Kiwelu CDM 15. Kombo Khamis Kombo – CUF
16. Joshua S Nassari –CDM 17. Tundu A Lissu- CDM 18. Aphaxar K Lugola- CCM 19.
Susan A Lyimo- CDM 20. Moses Machali – NCCR 21. John Shibuda Magalle CDM 22.
Faki Haji Makame-CUF 23. Esther N Matiko-CDM 24. Joseph Mbilinyi- CDM
25.Freeman Mbowe- CDM 26. Kurudhum J. Mchuchuli – CDM 27.Halima Mdee-CDM
28.John Mnyika- CDM 29. Augustino L Mrema- TLP 30. Maryam S Msabaha- CDM 31.
Peter Msingwa-CDM 32. Christowaja G Mtinda CDM 33. Philipa G Mturano- CDM 34.
Christina L Mughwai- CDM 35.Joyce Mukya – CDM 36.Israel Y Natse – CDM 37.
Philemon Ndesamburo- CDM 38.Ahmed Juma Ngwali-CUF 39. Vincent Nyerere- CDM
40.Rashid Ali Omar-CUF 41.Meshack J Opulukwa- CDM 42. Lucy Owenya- CDM
43.Rachel Mashishanga- CDM 44. Mhonga Ruhwanya – CDM 45.Conchesta Rwamlaza –
CDM 46. Moza Abedi Saidy-CUF 47. Joseph R Selasini – CDM 48.David E Silinde-CDM
49.Rose Kamili - CDM 50. Cecilia Paresso- CDM 51.Kabwe Zuberi Zitto- CDM 52.
Magdalena Sakaya – CUF 53. Rebecca Mngodo- CDM 54. Sabreena Sungura -CDM
KAULI mbili zinazotofautiana zilizotolewa na mawaziri wa Wizara ya Viwanda na Biashara juu ya tuhuma zinazomkabili bosi wa Shirika la Viwango (TBS), Charles Ekerege, zimewakera wabunge ambao wameitaka Serikali itoe tamko ni kauli ya waziri upi ni ya kweli.
Hatua hiyo ilijitokeza jana baada ya Mbunge wa Mwibara, Alphaxard Lugora, kuomba Mwongozo wa Spika kutokana na Waziri wa Viwanda na Biashara, Dk. Cyril Chami na Naibu wake, Lazaro Nyalandu kutofautiana juu ya uchunguzi dhidi ya bosi wa TBS.
Wakati Nyalandu anajibu swali juzi alisema uchunguzi wa CAG umekamilika na ameshawasilisha ripoti serikalini, bosi wake, Dk. Chami alisema jana uchunguzi huo haujakamilika na unaendelea kufanywa na CAG.
Ekerege anatuhumiwa na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mashirika ya Umma (POAC) na ile ya Hesabu za Serikali (PAC) kuweka kampuni hewa za kukagua magari nje ya nchi na hivyo kuingizia hasara ya Sh bilioni 30 ambazo zimeainishwa katika ripoti ya CAG.
Baada ya Lugora kumaliza kuomba mwongozo, alisimama Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), William Lukuvi aliyesema ni kweli majibu ya mawaziri hayo hayafanani na Serikali imeliona hilo, na Ofisi ya Waziri Mkuu itakusanya ushahidi wote juu ya jambo hilo na itatoa taarifa bungeni.
Lakini Mbunge wa Kigoma Mjini, Peter Serukamba (CCM) alihoji kwa nini Serikali inashindwa kutoa majibu ya uhakika juu ya suala hilo wakati wabunge wanachotaka kufahamu ni kauli ipi yenye ukweli.
Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Kabwe Zitto (Chadema) alisema kamati yake anayoiongoza ya Mashirika ya Umma iliunda kamati ndogo kushughulikia tuhuma zinazomkabili Ekerege na tayari wameshawasilisha taarifa kwa spika ambaye anatakiwa aipeleke Ofisi ya Waziri Mkuu ili walete taarifa ya utekelezaji bungeni.
Kwa upande wake, Naibu Spika Job Ndugai alikiri kuwa jambo hilo ni la muda mrefu umefika wakati liishie kwa kupatiwa ufumbuzi kwani linawapaka matope wabunge bila sababu za msingi. Chanzo: Habari Leo
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na baadhi ya viongozi wa dini alipowasili kwenye Hoteli ya White Sands jijini Dar es Salaam,kwa ajili ya kufungua Kongamano la Dini la Waislam na Wakristo, lililoanza jana Aprili 18, 2012
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisoma hotuba yake wakati akifungua rasmi Kongamano la Dini la Waislam na Wakristo lililoanza jana Aprili 18, kwenye Hoteli ya White Sands jijini Dar es Salaam. Picha na Muhidin Sufiani-OMR
HALMASHAURI YA MJI MPANDA KUJENGA CHUO KIKUU CHA KILIMO
HALMASHAURI ya Mji Mpanda mkoani Rukwa, ipo katika mchakato wa ujenzi wa Chuo Kikuu cha Kilimo (KUA) ili kuboresha huduma muhimu kwa maendeleo ya jamii na uchumi.
Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Mpanda, Nzori Kinero alisema hayo jana katika kikao maalumu cha Baraza la Madiwani cha kupitisha mpango wa bajeti kwa mwaka wa fedha wa 2012/2013.
Alisema katika hatua za awali, halmashauri hiyo imeomba zaidi ya Sh bilioni tatu kutoka taasisi za kifedha ili kuanzia shughuli za uanzishwaji wa chuo hicho kinachotarajiwa kujengwa mwaka huu.
“Hata hivyo, Commercial Bank of Africa (T) Ltd wako tayari kutoa kiasi hicho cha fedha kwa ajili ya uanzishwaji wa chuo hicho kwa sharti kwamba dhamana ya Serikali Kuu ipatikane kama mdhamini mkuu na Halmashauri ya Mji Mpanda ambaye ni mmiliki wa chuo hicho iwe mdhamini wa pili.
“Mchakato wa kupata udhamini wa Serikali Kuu kupitia Wizara ya Fedha unaendelea vizuri na uko katika hatua za mwisho,” alisema Kinero.
Alisema halmashauri hiyo imeruhusiwa kufanya hivyo kwa mujibu wa Sheria ya Serikali za Mitaa nambari nane ya mwaka 1982 na lengo ni kuiwezesha kutekeleza malengo na majukumu yake makuu.
Ili kutekeleza mradi huo, Kinero alisema halmashauri hiyo ya Mji itaongeza na kuboresha huduma za jamii na kiuchumi si kwa wakazi wa Mpanda pekee, bali Taifa kwa ujumla. Tayari halmashauri hiyo imeshapata usajili wa muda na kutambuliwa na Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania.
Kwsho tutawaletea changamoto za TTCL hapa mjini Mpanda
TTCL’s CEO Mr. Said Amir Said (left) and the Head of Information and Communication Technology department at the Rwanda Development Board (RDB) Patrick Nyirishema signing the contract.
TTCL’s Chief Marketing and Sales Officer Mr. Ernest Nangi (Left), TTCL’s Company Secretary Mrs. Gilder Kibola and Head Products Development Mr. Ernest Isaya.
TTCL’s Chief Executive Officer Mr. Said Amir Said speaking with Journalist in Rwanda after signings business Contract.
Mwandishi wa habari mwandamizi wa siku nyingi, Shyrose Bhanji amekuwa miongoni mwa wagombea ubunge wa Bunge la Afrika Mashariki ambao waliibuka kidedea katika uchaguzi uliofanyika jana mjini Dodoma.
Katika uchaguzi huo wagombea tisa kati ya 32 waliowania nafasi hiyo, walifamikiwa kuibuka kidedea na kupata tiketi ya kuwakilisha Tanzania katika bunge hilo.
Wagombea walioshinda nafasi kwa wanaume Tanzania Bara na idadi ya kura kwenye mabano ni Adam Kimbisa (210), Benard Murunya (135) na Makongoro Nyerere (123), na walioanguka ni Lifa Chipaka (8), William Melecela (42), Dk. Evans Rweikiza.
Upande wa wanawake, walioshinda ni Angela Kizigha (166), Shyrose Bhanji (120), ambao ndiyo watakaiwakilisha Tanzania katika Bunge la Afrika Mashariki, na walioshindwa ni Janeth Mbene, Fancy Nkuhi, Janeth Mmari na Dk. Godbertha Kinyondo.
Kundi la wagombea kutoka Zanzibar, walioshinda ni Abdalah Ali Mwinyi (237), Maria Yahya Ussi (91). Walioanguka ni Ahmada Hamad Khatib, Dk. Haji Mwita Haji, Khamis Jabir Makame, Dk. Said Gharib Bilal na Zubeir Ali Maulid.
Kwa upande wa kundi la upinzani, walioshinda ni Nderakindo Kessy (NCCR-Mageuzi) na Twaha Issa Taslima (CUF). Mgombea wa CHADEMA Antony Komu aliangushwa vibaya kwenye kinyang’anyiro hicho. Wengine walioshindwa ni Dk. Fortunatus Masha (UDP), Anthony Komu (CHADEMA), Juju Danda (NCCR-MAGEUZI), Michael Mrindoko (TLP), Mwaiseje Polisya (NCCR-MAGEUZI).
Wabunge wa CHADEMA ambao awali walitangaza kususia uchaguzi huo, walishiriki ikiwa ni pamoja na kusimamisha mgombea wake Anton Komu, ambaye alibwagwa vibaya.
Akizungumza na waandishi wa habari juzi, Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bunge, Freeman Mbowe, alisema hawatashiriki uchaguzi kwa madai ya kutokuwa huru na haki.
Mbowe, ambaye ni Mwenyekiti wa Taifa wa CHADEMA, alisema wabunge wa chama hicho watatoka nje na hawatakuwa tayari kuwasikiliza wagombea wala kupiga kura na kwamba CHADEMA kushiriki uchaguzi huo ni kutowatendea haki Watanzania, lakini katika hali ya kushangaza wabunge hao wakiongozwa na Mbowe walishiriki uchaguzi huo na hawakutoka ukumbini.
Awali, CHADEMA lilitaka kupewa nafasi moja kwa ajili ya chama hicho pekee badala ya kushindaniwa na wapinzani wote kama kanuni inavyoelekeza.
‘Sisi kama Chadema hatutashiriki katika uchaguzi huo wala hatutashiriki kupiga kura wala kusikiliza tutatoka nje tuache waendelee,’ alisema. Hata hivyo, Naibu Spika Job Ndugai, alisema hoja hiyo ya CHADEMA haina msingi na kwamba, nafasi mbili walizopewa wapinzani zitahusisha vyama vyote vya upinzani. Awali, wagombea waliingia katika nafasi hiyo ni Bernard Murunya, Adam Kimbisa, Makongoro Nyerere, Mrisho Gambo, Siraju Kaboyonga, William Malecela, Dk. Evans Rweikiza, Elibariki Kingu na Dk. Edmund Mndolwa wote kutoka Chama Cha Mapinduzi (CCM). Pia, yumo John Lifa-Chipaka wa TADEA. Kwa upande wa wanawake mchuano kuwania nafasi hiyo ulikuwa kwa Engela Kizigha, Fancy Nkuhi, Dk. Godbertha Kinyondo, Janet Mmari, Janeth Mbene, Mariam Ussi Yahya na Sebtuu Mohamed Nassor, Shyrose Bhanji, Sofia Ali Rijaal wote kutoka CCM wakati mgombea kutoka upinzani ni Rose Mwalusamba (CUF). Waliowania nafasi ya kuwakilisha Zanzibar katika Bunge la Afrika Mashariki walikuwa ni Abdullah Ali Hassan Mwinyi, Dk. Ahmada Hamad Khatib, Dk. Haji Mwita Haji, Khamis Jabir Makame, Dk. Said Gharib Bilal na Zubeir Ali Maulid wote kutoka CCM.
Kwa upande wa wagombea wa vyama vya upinzani, walikuwemo Dk. Fortunatus Masha (UDP), Anthony Komu (CHADEMA), Juju Danda (NCCR-MAGEUZI), Micah Mrindoko (TLP), Mwaiseje Polisya (NCCR-MAGEUZI), Nderakindo Kessy na Twaha Issa Taslima (CUF).
PICHA JUU: Lori lenye namba T847ANJ na Teller lake lenye namba T122AHH likiwa na ng'ombe katika kituo cha polisi Mpanda baada ya kukamatwa Aprili 16, 2012.
Jumamosi, Aprili 14, 2012 09:46 Na Maregesi Paul, Dodoma
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe, akizungumza na Waziri Mkuu aliyejiuzulu, Edward Lowassa, wakati wa kumbukumbu ya hayati Edward Moringe Sokoine, nje ya Kigango cha Sokoine, Parokia ya Dakawa mjini Morogoro juzi. Picha na Merina Robert.
Dk. Nagu, Ole Medeye wamtaka atoe ushahidi
Magufuli ataka akamuulize Waziri Mkuu
SIKU moja baada ya Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe, kumwambia Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, kwamba baadhi ya mawaziri wanawatisha wananchi ili wasiwachague wagombea wa upinzani, mawaziri hao wameamua kujibu mapigo.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti mjini hapa jana, mawaziri hao wameonyesha kutoridhishwa na kauli ya Mbowe, kwa kuwa hakuna ushahidi dhidi ya maneno yaliyosemwa.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Uwekezaji na Uwezeshaji, Dk. Mary Nagu, alisema hakumbuki alichozungumza wakati wa kampeni za uchaguzi mdogo wa Jimbo la Arumeru Mashariki, uliomalizika hivi karibuni.
“Sikumbuki kama alichosema Mbowe ni sahihi, kwa sababu kule tulikuwa kwenye kampeni, kila mmoja alikuwa akitumia silaha zake.
“Katika kipindi cha miaka 10 ambayo nilikuwa Mbunge wa Viti Maalum, Mkoa wa Arusha, Jimbo la Arumeru Mashariki lilikuwa kwenye himaya yangu, ndiyo maana nilikwenda kupiga kampeni kukisaidia chama changu.
“Pamoja na hayo, Mbowe wakati mwingine aachane na maneno ya kwenye kampeni kwa sababu katika kipindi hicho kunakuwa na mambo mengi sana na kama mtu ukitaka kufuata mambo ya kampeni unaweza kusababisha mambo mengine yasiyofaa,” alisema Dk. Nagu.
Wakati Dk. Nagu akisema hayo, Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Goodluck ole Medeye, ambaye ni mmoja wa walioshutumiwa na Mbowe, alisema hakumbuki na wala hajui kama alisema maneno hayo.
Kutokana na hali hiyo, alimtaka Mbowe awasilishe bungeni ushahidi wa alichokisema ili kuondoa utata.
“Hilo suala silikumbuki kwa sababu ninachojua hayo mambo yaliripotiwa na magazeti tu. Lakini kama Mbowe ana uhakika na anachokisema, alete bungeni mikanda ya mikutano hiyo, ikiwa ni pamoja na ya upande wake ili ukweli ujulikane,” alisema ole Medeye.
Kwa mujibu wa Naibu Waziri huyo, yeye binafsi amekuwa akifanya kazi bila upendeleo, ikiwa ni pamoja na kutembelea majimbo yote, yakiwamo yanayoongozwa na vyama vya upinzani.
Waziri wa Ujenzi, Dk. John Magufuli, aling’aka na kukataa kuzungumzia tuhuma hizo. Badala yake alitaka akaulizwe Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, kwa vile ndiye aliyeulizwa na Mbowe.
Juzi wakati wa kipindi cha maswali ya papo kwa papo kwa Waziri Mkuu, Mbowe aliwashitaki mawaziri hao, kwamba wanawatisha wananchi ili wasichague wapinzani.
Akizungumza wakati akiuliza swali lake, Mbowe alisema, Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza nitoe pole kwa misiba iliyolipata taifa kwa siku za hivi karibuni.
“Kwa muda mrefu kumekuwapo na matamko ya viongozi wa Serikali na wakati mwingine matamko ya viongozi wa CCM kwa wananchi, kwamba maeneo yatakayochagua wapinzani hayatapelekewa fedha za maendeleo na Serikali.
“Sasa tunaomba utuambie kama suala hili lipo, ili tuweze kujua ukweli halisi,” alihoji Mbowe.
Akijibu swali hilo, Waziri Mkuu alisema suala hilo halipo kwa kuwa Serikali imekuwa ikipeleka fedha za maendeleo katika maeneo yote bila kujali yanaongozwa na chama gani cha upinzani.
“Mheshimiwa Naibu Spika, swali hili limeulizwa kwa ujumla sana ingawa muulizaji anajua siyo kweli. Hakuna mahali popote ambapo tumeshindwa kupeleka fedha za maendeleo kwa sababu yanaongozwa na Chadema, CUF au chama chochote.
“Kwa maana hiyo, naomba Watanzania tuendelee kutimiza demokrasia, kama kuna kauli zingine katika chaguzi, hizo zinatoka kwa bahati mbaya, sisi tutaendelea kutii sheria na kanuni za kazi,” alisema Waziri Mkuu.
Pamoja na kutoa majibu hayo, Mbowe alisimama tena na kuuliza swali la nyongeza, huku akisema ushahidi wa kauli za vitisho za mawaziri hao anazo na kutoa mfano kwa baadhi ya chaguzi zilikotolewa.
“Mheshimiwa Waziri Mkuu, pamoja na masikitiko yako, kauli hizo zipo na zimekuwa zikitolewa mara kwa mara na baadhi ya mawaziri.
“Kwa mfano, hivi karibuni Waziri Nagu (Mary Nagu, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Uwekezaji na Uwezeshaji), alitoa kauli hizo wakati wa kampeni za uchaguzi mdogo Jimbo la Arumeru Mashariki, mwingine ni Waziri Magufuli (John Magufuli, Waziri wa Ujenzi) alitoa kauli kama hizo wakati wa kampeni za uchaguzi mdogo kule Igunga.
“Mwingine ni Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi (Goodluck ole Medeye) ambaye alitoa kauli hiyo kule Arusha,” alisema Mbowe.
JAMBO UNALOWEZA KULISHANGAA
APRIL 15, 2012 SUNDAY
VIGOGO WAASISI WA FREEMASONS NCHINI TANZANIA NA KUENEA KWA U FREEMASONS KATIKA UKANDA WA AFRIKA MASHARIKI...2
Januari 2005 nchini Isarel ‘walipata’ kiongozi mpya wa Freemasons, Chaim Henry Gehl, ambapo sherehe yao ilifanywa katika Hoteli ya Sheraton iliyopo Herzlia.
Wageni walitokana Uingereza, Ujerumani,Uholanzi, Austria, Luxemborg,Romania,Italia,Bulgaria na China. Kiongozi huyo alikuwa akikabidhiwa madaraka kutoka kwa Sami Raphaeli, mhasibu mstaafu wa benki mstaafu wa hekalu la Caspi lenye namba 56 lililopo mjini Haifa. Huyu cheo chake cha utendaji mkubwa katika freemasons ni 33rd degree alichotunukiwa mwaka 2003.Naam katika kuselebuka huko ndipo wakajigamba kwamba mnamo Oktoba 9, 2004 kulifanywa sherehe ya kutimiza miaka 100 ya Freemasons katika eneo la afrika mashariki.
Hapa kwetu Tanzania haikusemwa sana, ingawaje Jayantilal Kashavji Chande , au Sir Andy Chande katika mahojiano yake na mwandishi wa Ernest C. Ambali(The Guardian, Oktoba 8, 2004) haikuelezwa mahali patakapofanyiwa sherehe hizo.Katika mahojiano yale Sir Andy Chande alieleza kuwa mgeni rasmi alikuwa Rais Benjamini Mkapa na mkewe Mama Anna Mkapa. Pia kulikuwapo na wafanyabiashara wakubwa,wanadiplomasia,mawaziri n.k
Sir Andy Chande akiwa nchini India katika mji wa Chennai kuzindia hekalu lao East Star alieleza kwamba ‘marais wawili wa kwanza wa Tanzania (hawakuwa freemasons) lakini walifahamu ni nini’. Je unahitaji akili gani kuwatambua marais wako? Unahitaji Mungu akuongezee ubongo gani ili utambue kuwa ni akina nani wanaozungumziwa? Ndiyo maana nasema tatizo siyo kasi uliyonayo bali kule uendako!
Tukubaliane, kuwa kwa kiasi Fulani inajionyesha ikulu zetu zimezingirwa na Freemasons. Na katika mahojiano hayo hakusemwi ni Dar es Salaam eneo gani ambao sherehe hiyo ilifanywa, lakini katika kumsimika Chaim Henry Gehl (kule Israel)ilitajwa Hoteli ya Royal Palm ambapo wageni 350 walihudhuria.
Katika miaka hii 100(108) ikaelezwa kuwa Freemasons walianza kujenga hekalu lao la kwanza la Harmony namba 3084 mwaka 1904 mjini Zanzibar.Katika uzinduzi wa jengo hilo Zanzibar inaelezwa Rais Theodore Roosecelt alikuwapo, Duke of York(ambaye baadaye alikuja kufahamika kama Mfalme George VI)na Duke of Connaugh na Strathean walikuwepo pia.
Ukimsoma mwanahistoria Robert Muchembled(katika; A History of the Devil) ameorodhesha majina yenye kuabudiwa kwa ibada za kishetani lakini tunayathamini na kupofushwa nayo. Nami kwa matendo wanayoyatenda hapa duniani sina soni kusimamia hoja yangu kuwa ni ubatili mtupu waufanyao).
Naweka orodha ya mambo wanayojigamba Freemasons kujinasibu kwa miaka yao 100(108) ndani ya afrika mashariki huku wakibainisha kuwa makao makuu ya eneo zima ni barabara ya Nyerere, jijini Nairobi(soma;The Guardian, 0ktoba 8, 2004). Katika mahojiano hayo ndipo kukaorodheshwa ‘misaada’(ibilisi?), eti Kindwitwi Leprosy Centre(Utete), Mama Theresa Home for the children, shule ya vipofu(Pongwe, jijini Tanga), na Leprosy Projects (jijini Arusha).Montessori School (jijini Mwanza), Mnazi Mmoja Hospitali (iliyopo Zanzibar), Missionaries of Charity, shule ya walemavu (Buguruni, jijini Dar es salaam), wamejenga madarasa shule ya msingi Kinondoni(Dar es salaam) na kutoa pauni za Uingereza 15,000 mnamo mwaka 1996 katika ajali ya Mv Bukoba. Ukiangalia ‘misaada’ yao unapumbazika kuwa ni hisani ya hali juuNa tatizo kubwa linalotukabili, ni utegemezi ambao huzaa utumwa na kukengeuka akili zetu. Tunaishi huru mitaani lakini tupo gerezani, tunakwenda kasi sana lakini hatuangalii tunakokwenda, hatutaki kujua nini hiki tunachosaidiwa? Ni mungu gani aliruhusu mashoga na wasagaji wasimame madhabauni/altareni? Naam ndivyo tunavyouvaa uovu, ndivyo yanakotakiwa Uganda Museven aliruhusu hali hiyo. Na wenyewe husingizia haki za kiraia au dini za kiraia, inaeleweka kuwa Marekani imejngwa na Freemasons kwani wanajieleza kwa mengi tu. Je nasi tuwe na akina Jack Straw wetu bungeni? Tuvuje jasho kwa kupitisha sheria za kuruhusu mashoga, wasagaji halafu tuseme mungu anaruhusu hayo?
VIGOGO WA FREEMASONS KATIKA UKANDA WA AFRIKA MASHARIKI NA AFRIKA KWA UJUMLA
Sir.Andy chande ajitokeza na kusema kuwa yeye ni mmoja wa freemason afrika mashariki .Pia hakuwa nyuma kuwataja viongozi wanaohusika kwenye chama hicho akiwemo rais mstaafu wa awamu ya tatu Mh.Benjamin Mkapa .
Pia alimtaja steven kanumba, msanii nguli hapa Tanzania,Baba Riz raisi wa Tz,lowassa,AY,Mr. Blue,na wengineo wengi. Pia hakusita kumtaja yoweri museveni raisi wa uganda,Obama raisi wa marekani,George Bush,Bill Clinton,George washington,Elizabeth malkia wa uingereza na wengineo wengi.
Sir.Andy Chande alitaja yeye kwenye chama hicho ni Grand District Master akiwa amebobea kwa miaka 18 iliyopita.
Alipoulizwa makao yao makuu hapa Tanzania yapo wapi alijibu bila kusita "we are located at sokoine Drive behind kilimanjaro hotel here in Dar es salaam" (tunapatikana barabara ya sokoine nyuma ya hoteli ya kilimanjaro).
Pia Sir. Andy alisema wananyaraka zote za kumiliki jengo hilo toka serikalini. Aliongezea kuwa vikao vyao hufanyika kwa siri nyakati za usiku na mtu akishaingia kwenye chama hiko hatotoka tena
HUU NI MUHTASARI TU TULIOFANIKIWA KUUPATA KUTOKA KWA MPEKUZI BLOGER KAMA ALIVYONUKUU KIPINDI CHA RADIO YA CLOUDS FM CHA NJIA PANDA MACHI 11, 2012 .
Pichani Lowasa akiwa kanisani kwa TB Joshua kama anavyoonekana kwenye Emmanuel TV, 12 June 2011
MBINU za Edward Lowassa kutaka kurejea kileleni katika ulingo wa kisiasa zimemnasa mbunge wa Kilindi (CCM), Beatrice Shelukindo, imefahamika.
Beatrice ambaye alikuwa akijitambulisha kuwa mmoja wa “wapambanaji dhidi ya ufisadi,” waliopachikwa jina la “Mitume kumi na miwili,” sasa anatajwa kuhamia rasmi mtandao wa Lowassa.
Gazeti hili limepata ushahidi wa maandishi ya mkono wa Beatrice mwenyewe yanayoonyesha kuwa amekuwa mfuasi muhimu wa Lowassa kiasi cha kushawishi wengine kujiunga katika mtandao wake.
Akiandika kwa Pindi Chana, mbunge wa Viti Maalum (CCM), tarehe 14 Februari mwaka huu, Beatrice alieleza mambo matatu katika ujumbe wake kwa Chana.
Kwanza, kumshukuru Chana kwa kukubali kulinda kura zake. Pili, kumshawishi kumuunga mkono Lowassa. Tatu, kumweleza juu ya ulokole wake na “mtumishi aliyepakwa mafuta” kutoka Nigeria.
Beatrice anamwambia Chana kuwa Lowassa ndiye kampeni meneja wake. Hii ilikuwa katika uchaguzi wa makamishina wa Bunge; nafasi aliyogombea na kushinda.
“Mungu ni wa ajabu, (Lowassa) ameniombea kura pasipo maelezo. Ameandaa lunch na dinner (vyakula vya mchana na usiku) ambako amekuwa akiniombea kura. Ana njia za ajabu za kufanya mambo. Ahsante kwa kukubali kuhesabu kura,” inasema sehemu ya ujumbe huo.
Chana, ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu (CC) na Halmashauri Kuu (NEC) ya CCM, ndiye alihesabu kura za Beatrice kwenye uchaguzi wa kutafuta makamishina wa Bunge.
Ni kwenye ujumbe huo ambamo Beatrice anatoboa kuwa siri ya ushindi wake ni Lowassa aliyekuwa kampeni meneja wake.
Katika kusisitiza hoja yake, Beatrice anasema, “Nimezungumza na TB Joshua wa Emmanuel TV Nigeria aliyenipa unabii kuwa rais ajaye Tanzania ni Edward Lowassa, nikamuambia haiwezekani kwani amechafuka sana.”
Anasema Joshua alimjibu, “…alikuwa amechafuka sasa amesafishwa kwani katubu. Akaniambia his past is over (maisha yake ya nyuma si kitu). Akaongeza kwa kusema, wewe Beatrice ningeangalia your past (maisha yako ya nyuma) pengine nisingekuombea kabisa. Akasema my past is over (hajali maisha yangu ya nyuma),” inasema sehemu ya ujumbe huo wa Beatrice.
Hata hivyo, Beatrice hakueleza katika waraka wake kwa Chana maisha yake ya nyuma yalikuwa vipi. Wala hajaeleza alifanya nini, hadi kuamini kuwa kama Nabii Emmanuel angeyatazama, basi asingemuombea.
Kuvuja kwa taarifa hizi kumekuja wiki tatu baada ya Lowassa kuchaguliwa kuwa mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge, Ulinzi, Usalama na Mambo ya Nje.
Mume wa Beatrice, William Shelukindo alikuwa mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini ambayo iliongoza harakati za kuundwa Kamati Teule ya Bunge iliyochunguza mkataba tata wa Richmond.
Ni taarifa ya kamati hiyo iliyosababisha Lowassa kujiuzulu wadhifa wake wa waziri mkuu, Februari 2008.
Kwa mujibu wa watu waliokaribu na Beatrice na kwa ushuhuda wake mwenyewe, mwanasiasa huyo ameamua kujisalimisha kwa Lowassa kwa kile kinachoelezwa kuwa “Lowassa ndiye rais ajaye wa Tanzania.”
Aidha, kupatikana kwa taarifa hizi kumekuja huku kukiwa na juhudi kubwa zinazofanywa na Lowassa na kundi lake kutaka kujisafisha kwa lengo la kujitosa katika kinyang’anyiro cha urais mwaka 2015.
Miongoni mwa mikakati aliyojiwekea Lowassa na kundi lake ni kujitokeza katika maeneo yote muhimu na kutoa kauli ambazo zitafanya wananchi waanze kumkubali kuwa ni kiongozi anayefaa.
Katika kutekeleza mkakati huo, Januari mwaka huu, Lowassa alijitokeza kuzungumzia vurugu zilizotokea mkoani Arusha zilizotokana na mvutano katika uchaguzi wa meya wa jiji hilo kati ya CCM na CHADEMA.
Katika mnyukano huo, watu watatu walipigwa risasi na polisi na kufariki dunia baada ya polisi kutumia nguvu isiyo ya kawaida kuzima maandamano ya CHADEMA.
Kauli hiyo ya Lowassa ilikuwa tofauti na msimamo wa Katibu Mkuu wa CCM, Yusuf Makamba aliyemtaka kuwasilisha maoni yake katika vikao vya chama badala ya kutumia vyombo vya habari.
Kauli nyingine ya Lowassa ilihusu nyongeza ya viwango vya mishahara kwa wafanyakazi, kutokana na kile alichoita mfumuko wa bei kuwa mkubwa.
Bali wiki moja iliyopita, Naibu Katibu Mkuu wa vyama vya wafanyakazi nchini (TUCTA), Nicholas Mganya alimtuhumu Lowassa kwa kutoa kauli hiyo akisema ana ajenda ya siri nyuma yake.
Mgaya alisema TUCTA haihitaji msaada wa Lowassa katika kusimamia madai yao. Alisema “mbunge huyo wa Monduli inaonekana ana ajenda yake mgongoni.”
Hatua nyingine ya Lowassa katika kujikarabati kisiasa ni kugombea na kupata nafasi ya Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama.
Lowassa amekuwa pia akihudhuria hafla nyingi, hasa za madhehebu ya Kikiristo (KKKT) ambao anaonekana akitoa maoni mbalimbali kama ilivyokuwa Jumapili iliyopita ukumbi wa Dimaond Jubilee kwenye uzinduzi wea albamu ya moja ya kwaya za injili.
Kwenye kusanyiko hilo, Beatrice naye alikuwepo. Lowassa alimtaka asome maoni ya gazeti la The Citizen juu ya ushirikina uliokithiri nchini; jambo ambalo Lowassa alizungumzia kwa urefu.
MwanaHALISI lilipowasiliana na Beatrice ili kupata maoni yake juu ya ushwahiba wake mpya na Lowassa, mahojiano yalikuwa kama ifuatavyo:
Mwandishi: Tusaidie maelezo kidogo juu ya ujumbe uliomwandikia Mheshimiwa Pindi Chana kumjulisha kuwa uliambiwa Edward Lowassa atakuwa rais. Ni kweli?
Beatrice: Barua ameandika nani na umeipata wapi?
Mwandishi: Hii barua fupi – memo ndani ya Bunge, uliposema Mheshimiwa Lowassa ambaye amesimamia vizuri kura zako za ukamishna wa Bunge.
Beatrice: Sina taarifa hiyo. Wala siikumbuki. Unajua ndani ya Bunge tunaandikiana mambo mengi, tena mengine ya utani tu. Na mimi na Mheshimiwa Chana sote ni “walokole,” tunafanyiana utani sana.
Mwandishi: Kwani mheshimiwa Shelukindo, mkiwa ndani ya bunge kuna utani mwingi, kwamba huwa mnaandikiana utani sana?
Beatrice: Kabisa, unajua tunaandika mambo mengi. Na kama unaandika kwa utani kwa mwenzako inabaki hivyo ni utani tu. Sasa tatizo hao wanaowaletea mambo haya wanatumia mambo haya kutafuta mipango yao ya kufikia mwaka 2015.
Alisema, “Mimi najua hakuna anayenibeba ndugu yangu. Mimi ni very solid (ngangari), sibebeki. Nakwambia, mbona mimi nina nguvu nyingi mimi mwenyewe; sihitaji kubebwa. Najua wanajaribu kuonyesha tunabebwa, lakini huo ni ujinga wao wa kufikiri.
Mwandishi: Mheshimiwa Shelukindo, kwani nyie waheshimiwa huwa mnatafutana (kufitiniana)?
Beatrice: Hiyo inafanyika sana, watu wakishakuwa na mambo yao wanatumia wengine kutimiza dhamira zao. Lakini mimi ninafikiria wananchi. Nimeshaamua kwamba Beatrice nashughulikia shida za wananchi jimboni. Ninatafuta njia za kuwaondolea umasikini, njaa na mambo kama hayo. Sasa wengine wanatafuta tu pa kunishika.
Mwandishi: Kwa hiyo Mh. Lowassa ndiye alikuwa kampeni meneja wako katika kutafuta ukamishna pale bungeni, au siyo Mheshimiwa?
Beatrice: Lakini kama anafanya kazi ya kampeni vizuri; ni vizuri tu. Isipokuwa kila mtu anajichukulia mwenyewe alivyo. Mimi ni mtu wa kazi sihitaji kusimamiwa hivyo. Na hebu tujadili hili; unajua kaka nyinyi mnafanya kazi kubwa. Sasa hii kusikia, sijui MwanaHALISI hivi, sijui hivi, pengine kuna watu wanachomekea vitu vyao. Tunapenda kazi yenu.
Mwandishi: Mheshimiwa nakushukuru sana.
Beatrice: Karibu sana tutafanya kazi pamoja.
Akiwa Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini, mume wa Beatrice, William Shellukindo, alikuwa na msimamo mkali dhidi ya watuhumiwa wakuu wa ufisadi nchini na hiyo ndiyo inayoelezwa kuwa sababu ya kushindwa kwake ubunge katika mchakato wa ndani ya CCM.
Shellukindo alikuwa mbunge wa jimbo la Bumbuli mkoani Tanga kwa zaidi ya miaka 20, alishindwa katika kura za maoni na January Makamba, mtoto wa katibu mkuu wa CCM anayetajwa kuwa mfuasi wa mtandao wa Lowassa.
S0urce by Mwanahalisi – 9 March 2011
MUNGU AKUPE PUMZIKO LA AMANI STEVEN KANUMBA
Jeneza lenye Mwili wa Marehemu,Steven Kanumba likiwasili kwenye Viwanja vya Leaders Club, jijini Dar es Salaam siku ya mazishi yake
BABA YAKE ELIZABETH MICHAEL 'LULU' ATAKA JAMII ISIMHUKUMU MWANAWE, HAKI ITENDEKE, AELEZA USHIRIKA WA LULU NA KANUMBA
Imeandikwa na Daniel Mjema wa Gazeti la Mwananchi.
BABA mzazi wa msanii wa filamu, Elizabeth Michael 'Lulu,' ameitaka jamii kutomhukumu mwanawe kutokana na kifo cha msanii mwenzake marehemu Steven Kanumba, badala yake iache vyombo vya sheria vifanye kazi yake.
Mzazi huyo, Michael Edward Kimemeta anayeishi mjini Moshi, amewaomba Watanzania kuiachia Mahakama iamue kama mtoto wao anahusika katika kifo hicho ama la.
Kimemeta, ameeleza kuwa binti yake ana umri wa miaka 16 tofauti na inavyoelezwa kuwa ana miaka 18.
Juzi Lulu alifikishwa katika Mahakama ya Kisutu jijini Dar es Salaam na kusomewa mashtaka ya mauaji ya msanii mwenzake, Kanumba.
Kumekuwa na utata uliojitokeza kuhusu umri wa Lulu. Wakati mwenyewe akieleza kuwa ana miaka 17, Jeshi la Polisi lilieleza kuwa umri wake ni miaka 18 na juzi Mahakama iliambiwa kuwa msanii huyo ana umri wa miaka 17 na baba yake akisema ana miaka 16.
Kwa upande wake, mama mzazi wa Lulu Lucresia Karugila, alisema tukio la kifo cha Kanumba na kukamatwa kwa binti yake Lulu, limempa mshituko mkubwa na kumsababishia maradhi ya kisaikolojia na kimwili.
“Hayo yaliyotokea kwa kweli yamenifanya niumwe kabisa hapa sasa hivi nimelala naumwa…nimempa go ahead (ruksa), baba yake azungumze kwa sababu taarifa zote anazo. Naomba mimi mniache kwa sasa,”alisema.
Kimemeta aliliambia Mwananchi jana kuwa mwanawe huyo alizaliwa Aprili 17 mwaka 1995 katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH).
“Nataka nikuambie (mwandishi) mwanangu atatimiza umri wa miaka 17 ifikapo Aprili 17 mwaka huu. Sasa ana umri wa miaka 16 na ni mtoto. Tunavyosikia Kanumba alikuwa mpenzi wake inatuuma sana,” alisema.
Baba huyo alisema alizaa na mama yake Lulu lakini hawakuwahi kuishi pamoja. "Mwanamke huyo alikuwa akifanya kazi Shirika la Ndege Tanzania (ATC) na muda wote Lulu alikuwa akiishi na mama yake jijini Dar es Salaam,"alisema Kimemeta.
Ameomba familia ya marehemu Kanumba ikubali kupokea pole ya familia ya Lulu kupitia gazeti hili kutokana na mazingira kutoruhusu familia hizo kukutana.
“Nasikitika mazingira ya tukio lenyewe mpaka sasa hayaruhusu familia yetu kwenda kutoa pole na kuifariji familia ya Kanumba kulingana na utamaduni wa mwafrika…tunaomba wapokee pole zetu kupitia njia hii,” alisema.
Kwa mujibu wa Kimemeta, hivi sasa wanahofia maisha yao kutokana na jamii kujenga mtazamo hasi juu ya tukio hilo hata bila ya kusubiri vyombo vya sheria kusikiliza ushahidi wa tukio hilo na kutoa hukumu yake.
Alisema kuwa jamii inapaswa ifahamu kuwa, kikatiba mtu yeyote anayeshitakiwa kwa kosa lolote haimaanishi tayari ni mkosaji, bali atahesabiwa kuwa mtuhumiwa hadi pale Mahakama itakapomtia hatiani.
“Yanasemwa mengi mara ooh Kanumba ndio alianza kumpiga mwanangu mara ooh Kanumba alisukumwa …mimi nasema tuiache Mahakama hata sisi hatupendi mtu auawe, lakini Mahakama iachwe itende haki,”alisisitiza.
Akizungumzia maisha ya mwanawe Lulu, Kimemeta alisema alipokuwa akitangaza Kipindi cha Watoto Televisheni ya ITV, walifarijika sana, lakini alipoanza kuingia kwenye sanaa ya filamu, walijua sasa wamempoteza.
“Baada ya kuingia kwenye sanaa ya maigizo niliona kabisa tumempoteza mtoto na nilimweleza mama yake kuwa wale aliokuwa nao katika maigizo akiwamo Kanumba mwenyewe, nilikuwa siwaamini hata kidogo,” alisema.
Kimemeta alidai kuwa siku moja mwanawe alimpigia simu akimwarifu kuwa alikuwa anakwenda jijini Arusha kurekodi filamu na Kanumba, yeye alipinga safari hiyo akitaka Kanumba amthibitishie usalama wa binti yake.
“Kwa sababu nilikuwa sipendezwi na hayo mambo nilimwambia mama yake azungumze na Kanumba na akatuhakikishia atamlinda na kambi yake ina maadili, lakini kumbe huo ndio ukawa mwanzo wa mwanaye kugeuzwa mpenzi wa msanii huyo,” Alidai Elizabeth Michael 'Lulu,'
Baba huyo mzazi alidai kutofanya vizuri darasani kwa mtoto wake huyo, kulichangiwa na hatua ya kuingia katika sanaa ya uigizaji.
“Lulu alikuwa mtoto mwenye tabia nzuri sana hata alipokuwa ITV kwa kweli alitutia moyo wazazi wake kwa jinsi ITV walivyokuwa wakimlea, lakini alipojiingiza tu kwenye uingizaji hapo ndipo mambo yalipoharibika,” alisema.
Alikanusha madai kuwa mwanawe hakumaliza kidato cha nne na kusisitiza kuwa Lulu alisoma Shule ya Kimataifa ya St Mary's na baadaye alihamia Shule ya Sekondari ya Midway High School na kumaliza kidato cha nne mwaka jana.
Alisisitiza kuwa katika mambo yaliyokuwa yakiwaumiza mioyo, ni namna mtoto huyo alivyozidi kuharibika kwa kuingia katika fani ya uigizaji filamu.
Alisema angependa kukutana na Rais Jakaya Kikwete ili azungumze naye kama rafiki yake na watafute suluhisho la maadili kwa kizazi cha sasa na cha baadaye.
Alisema tayari ameanza mchakato wa kuonana na Rais Kikwete ili amweleze siri aliyodai ni ‘nzito’ na kudai tayari ametafuta wazee watatu wenye busara wa kumsindikiza, endapo Rais atakubali ombi lake.
Pia ameziomba taasisi zinazojishughulisha na masuala ya haki za binadamu na msaada wa kisheria, kujitokeza na kumsaidia mwanawe.
Lulu alifikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam juzi na kusomewa shitaka la kumuua Kanumba, tukio lililotokea Aprili 7 mwaka huu eneo la Sinza Vatican.
Msanii huyo hakutakiwa kujibu lolote kwa kuwa Mahakama hiyo haina
mamlaka ya kusikiliza mashauri ya mauaji na hivyo alipelekwa rumande Gegeza la Segerea hadi Aprili 23 mwaka wakati kesi hiyo itakapotajwa.
Kifo cha msanii huyo kimetikisa nchi kutokana na umaarufu wake, akiwa ameigiza filamu 40 zilikuwa zikirushwa katika vituo mbalimbali vya televisheni ndani na nje ya nchi.
Kanumba alipanga kujenga shule
Katika hatua nyingine, Fidelis Butahe na Pamela Chilongola wanaripoti kuwa mchaguaji maeneo ya kupigia picha za filamu za msanii Kanumba, Rahim Khatib alisema marehemu Kanumba alinunua eneo la ekari 15 huko Mpiji mkoani Pwani kwa ajili ya ujenzi wa shule yake ya sekondari.
Khatib alisema Kanumba alikuwa na mpango huo muda mrefu na kwamba lengo lake lilikuwa kuwasaidia wanafunzi wa eneo hilo ambao hutembea muda mrefu kutokana na shule kuwa mbali na eneo hilo.
“Kanumba alikuwa na mipango mizuri katika maisha yake, kuna eneo kubwa alilonunua Mpiji ili ajenge shule ya sekondari,” alisema Khatib.
Alifafanua kuwa hadi anafariki dunia, aliacha kiasi cha fedha zaidi ya Sh 40 milioni katika Kampuni yake ya Kanumba The Great.
“Marehemu ameacha fedha zaidi ya Sh 40 katika kampuni yake, magari matatu na hivi karibuni alinunua jingine aina ya Toyota Land Cruiser, ”alisema Khatib.
Katika hatua nyingine Khatib alisema kifo cha Kanumba ni pigo kwa watu waliokuwa wakifanya naye kazi akiwemo yeye mwenyewe kwa kuwa walikuwa wakimtegemea kwa kiwango kikubwa.
Jeneza lenye Mwili wa Marehemu,Steven Kanumba likiwasili kwenye Viwanja vya Leaders Club,jijini Dar es Salaam siku ya mazishi ya msanii huyo wa filamu nchini.
Sintah naye alonga
Kwa upande wake msanii maarufu wa filamu nchini, Christina Manongi maarufu kama Sintah ambaye alikuwa mmoja wa wasanii wa kwanza kufika nyumbani kwa marehemu Kanumba muda mfupi baada ya msanii huyo kuanguka, alisema kuwa siku tano kabla ya Kanumba kufariki, alikuwa na hasira tofauti na alivyomzoea.
Sintah ambaye alikuwa na msanii huyo katika Viwanja vya Leaders Club jijini Dar es Salaam Jumapili ya Aprili mosi pamoja na mwigizaji mwingine, Steve Nyerere alisema kuwa kila alichokuwa akimuuliza Kanumba, alimjibu kwa ukali.
“Ni tofauti na nilivyomzoea, siku ile ya Jumapili tulikaa pale Leaders Club mpaka usiku sana na kila jambo nililokuwa nikizungumza naye alinijibu kwa mkato na ukali kweli, ilinishangaza,” alisema Sintah
Alifafanua kuwa moja ya mambo waliyokuwa wakizungumza na Kanumba ni pamoja na yeye kutaka kuacha uigizaji, suala ambalo marehemu Kanumba hakuliunga mkono na kumjibu kwa ukali kuwa asijitoe katika uigizaji.
Mwanamuziki Diamond (kulia)akipokea tuzo yake kutoka kwa George Kavishe meneja wa bia ya Kilimanjaro mara baada ya kutangazwa mshindi wa utunzi bora wa nyimbo katika hafla ya kukabidhi tuzo kwa wanamuziki bora Kilimanjaro Music Award 2012 zinazofanyika kwenye ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es salaam na kuhudhuria na waalikwa mbalimbali pamoja na wadau wa muziki kutoka ndani ya Tanzania na nje ya nchi.
Msanii Nassib Abdul ‘Diamond’ usiku huu ameng’ara kwenye tuzo za Kilimanjaro Music Award, baada ya kujinyakulia tuzo tatu.
“Namshukuru Mungu, wakati mwingine uvumilivu na subira ni mzuri. Mwaka jana sikupata tuzo, nikamshukuru Mungu, nikaongeza bidii, nikafanya kazi nzuri, leo ninachukua tuzo ya tatu sasa hivi, alisema Diamond baada ya kushinda tuzo ya Video Bora ya Mwaka, kupitia wimbo Moyo Wangu, ambayo ilikuwa ya tatu usiku huu.
Diamond alizishinda nyimbo za Hakunaga ya Suma Lee, Wangu ya Jay Dee, Ndoa Ndoana ya Kassim na Bongo Fleva ya Dully Sykes.
Mwanamuziki Diamond akipiga picha na mama yake wa pili kutoka kushoto na Mkurugenzi wa ASET Asha Baraka kutoka kulia pamona na wanenguaji wake mara baada ya kupokea tuzo yake ya utuzni bora wa nyimbo.
Mwimbaji wa muziki wa Taarab ambaye ameshinda tuzo ya mburudishaji bora kwa wanawake Malkia Khadija Omar Kopa akitumbuiza katika hafla hiyo usiku huu.
Malkia Khadija Omar Kopa akishukuru wapenzi wake mara baada ya kushinda tuzo ya mburudishaji bora, wa pili kutoka kushoto ni mume wake na wengine ni watoto wake.
Watoto wa Malkia wa Mipasho Khadija Omar Kopa wakishuka jukwaani mara baada ya kumtunza mama yao wakati alipokuwa akitumbuiza katika hafla hiyo.
Kulia ni Msanii Profesa Jay na kushoto ni Mkubwa Fella meneja wa kundi la TMK Family wakimkabidhi tuzo Roma Msanii wa muziki wa Hiphop aliyejishindia tuzo ya msanii bora wa Hiphop.
Mwanamuziki Diamond katikati akiwa jukwaani na wenzake kabla ya kuimba wimbo wa msondo katika hafla ya kukabidhi tuzo za wanamuzikii bora za Kilimanjaro Music Award zainazofanyika usiku huu kwenye ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es salaam kulia ni Khalid Chokoraa wa bendi ya mapacha watatu.
Msanii HBaba akiwa amezungukwa na vimwana katika hafla hiyo
Mtayarishaji wa muziki P. Funk kulia akiwa na msanii wa muziki wa Hiphop Jay Moo.
Wakurugenzi wa ASET kutoka kulia ni Asha Baraka akiwa na kaka yake Baraka pamoja na mdau mwingine katika hafla hiyo.
Kulia ni Dina Marios wa Clouds akiwa na Asma Makau kutoka Clouds pia.
Makamu Mwenyekiti wa klabu ya Simba Geofrey Nyange Kaburu kulia akibadilishana mawazo na Mulamu Ghambi katika hafla hiyo.
Mohamed Nasor kushoto akiwa na Evance Aveva wakifuatilia matukio mbalimbali katika hafla hiyo usiku huu.
(Inatolewa kwa mujibu wa Kanuni ya 5(3) ya Nyongeza ya Pili ya Kanuni za Bunge Toleo la 2007)
_______________________________
1.0Tarehe 9 Machi, 2012 nilitoa Tangazo kwa vyombo
vya habari na gazeti la Serikali juu ya kuwepo kwa nafasi Tisa wazi za Ubunge wa Bunge la Afrika Mashariki kufuatia kufikia ukomo wa maisha ya Bunge la sasa hapo 04 Juni, 2012.
Katika Tangazo hilo niliwaomba wananchi wenye sifa za kugombea nafasi hizo wafanye mchakato wa kugombea kupitia vyama vyao vya Siasa na fomu za wagombea waliopendekezwa zirejeshwe Ofisi ya Bunge kabla ya saa 10.00 jioni tarehe 10 Aprili, 2012 ambayo ndiyo siku ya uteuzi. Jumla ya Wagombea 34 kutoka Vyama vya Siasa vya CCM, CHADEMA, CUF, NCCR-MAGEUZI, TLP, UDP na TADEA wamerudisha Fomu.
2.0Zoezi la uteuzi limekamilika, Wajumbe 33 wametimiza masharti ya uchaguzi kwa mujibu wa Mkataba wa kuanzisha Jumuiya ya Afrika Mashariki na Kanuni za Bunge, hivyo, wameteuliwa kugombea nafasi hizo. Aidha, Mgombea mmoja hakutimiza masharti ya uchaguzi ya kuthibitisha uraia wake na kulipa ada ya uchaguzi kwa mujibu wa Kanuni 5(3) na 6 ya Nyongeza ya Tatu ya Kanuni za Bunge, hivyo hakuteuliwa kugombea.
Ifuatayo ni Orodha ya Wagombea walioteuliwa na wasioteuliwa kugombea nafasi za Ubunge wa Afrika Mashariki:-