April
20, 2012
MATATANI KWA KUKUTWA NA NOTI BANDIA ZA SHILINGI MILIONI MOJA ZA TANZANIA
JESHI la polisi wilaya ya Mpanda mkoa wa Katavi
linamshikilia mtu mmoja kwa tuhuma za kukutwa na noti bandia zenye thamani ya
shilingi milioni moja.
Tukio hilo la aina yake limetokea katika kijiji cha
Kakese Mbugani nje kidogo ya mji wa Mpanda majira ya saa tisa alasiri ambapo
aliyekamatwa ametajwa kuwa ni Gwisu Jishosha Bunhyawandama (38) mkazi wa kijiji
cha Kashishi tarafa ya mpimbwe wilaya ya Mlele.
Taarifa kutoka kwa diwani wa kata ya Kakese, Mhe.
Maganga Mussa Katambi imesema kuwa mtuhumiwa alifika kijijini hapo alhamisi
Aprili 19, 2012 kwa lengo la kununua ng’ombe katika mnada uliofanyika leo
Aprili 20, 2012 na ilipofika majira ya mchana mtuhumiwa alinunua ng’ombe mmoja
kwa bei ya shilingi laki tatu na sabini elfu na kasha kumuuza papo hapo kwa bei
ya shilingi laki tatu na nusu.
Diwani Maganga amesema kuwa baada ya kuuza huyo ng’ombe
watu walianza kuchunguza sababu za kumuuza huyo ng’ombe ndipo walipobaini kuwa
pesa alizonazo ni za bandia ndipo walimkamata kwa kutumia mgambo na kuanza
kumshambulia hali iliyotishia maisha yake kwani walitaka kumchoma kwa moto.
Amesema kuwa viongozi wa kijiji waliamua kuingilia kati
na kumkamata kisha wakamfikisha kituo cha polisi ambapo alikuwa na noti za
shilingi elfu kumi kumi zikiwa katika mafungu kwa nambari BT 2145563, BH 4262398, BK 3272328, BE
9452918 na BF 2131869 shilingi za Tanzania
Akizungumza na mwandishi wa habari hizi mtuhumiwa alidai
kupewa pesa hizo na mfanyabiashara wa ng’ombe aliyemtaja kwa jina la Yenze
Bundala mkazi wa Kijiji cha Kashishi wilaya ya Mlele mkoa wa Katavi.
Mwisho.
FUSO LAUA WATATU, TISA WAJERUHIWA
WATU watatu wamefariki dunia katika ajali ya gari aina
ya fuso iliyotokea katika mlima Lyamba mpakani mwa mkoa wa Rukwa na Katavi
Kamanda wa jeshi la polisi mkoani Rukwa Isuto Mantage
amesema ajali hiyo ilihusisha lori aina ya Fuso lenye namba ya usajiri T620ABA
mali ya Eliud Sanga mkazi wa kijiji cha Laela mkoani Rukwa
Amesema katika ajali hiyo watu watatu wamefariki dunia
na wengine tisa wamejeruhiwa na kulazwa katika hospitali ya wilaya yam panda mkoa
wa katavi na wengine katika hospitali ya wilaya ya Nkasi mjini Namanyere
Amewataja waliofariki dunia kuwa ni Maha Lukwetula (51)
mkazi wa shankala wilaya ya Mpanda, Kanwa (36) mkazi wa kijiji cha Itenka
wilaya ya Mpanda na mtoto wake mwenye umri wa miaka mine (4) ambaye jina lake
halikuweza kupatikana
Amewataja waliojeruhiwa kuwa ni Jeshi Charles (33) mkazi
wa Namanyere, Juma Lukwetula (40) mkazi wa Shankala, Thomas Simwinga (25) mkazi
wa Laela, Sailas Kuzenza (30) mkazi wa Mpalamawe na Linusi Kidomu (36)
Amewataja waliojeruhiwa wengine kuwa ni Shukuru Rafael
(9) mkazi wa Laela, Francis Kidomu (24) mkazi wa Londokazi wilaya ya Nkasi na
mmoja wao hajafahamika kwani hajitambui hawezi kuongea ambapo wote wamelazwa
katika hospitali ya wilaya ya Mpanda
Amesema majeruhi Saidi (25) ambaye amekatika miguu yote
miwili amelazwa katika hospitali ya wilaya ya Nkasi kutokana na hali yake kuwa
mbaya
Kamanda Mantage amesema chanzo cha ajali ni kukatika kwa
breki za lori hilo lilipokuwa likiteremka mlima Lyamba Lyamfipa Aprili 19, 2012
majira ya saa 8:30 mchana na dereva wa lori hilo anatafutwa na jeshi la polisi
baada ya kukimbia mara baada ya ajali kutokea.
Mpaka sasa wabinge waliosaini kura ya kutokuwa
na imani na Waziri Mkuu Pinda, kati ya majina 54 hapo chini ni wawili tu kutoka
CCM ndiyo wamesaini. Majina ya Wabunge walio-sign Vote of No Confidence hadi
sasa hivi 1.Rashid Ali Abdallah CUF 2.Chiku Aflah Abwao CDM 3.Salum Ali Mbarouk
CUF 4.Salum Khalfam Barwany CUF 5.Deo H Filikuchombe- CCM 6.Pauline P.
Gekul-CDM 7. Asaa O Hamad-CUF 8.Prof.Kuliyokela Kahigi- CDM 9.Naomi M Kaihula –
CDM 10.Sylvester Kasulumbayi- CDM 11. Raya Ibrahim Khamis - CDM 12.Mkiwa H. Kiwanga
CUF 13.Susan L Kiwanga-CDM 14.Grace S Kiwelu CDM 15. Kombo Khamis Kombo – CUF
16. Joshua S Nassari –CDM 17. Tundu A Lissu- CDM 18. Aphaxar K Lugola- CCM 19.
Susan A Lyimo- CDM 20. Moses Machali – NCCR 21. John Shibuda Magalle CDM 22.
Faki Haji Makame-CUF 23. Esther N Matiko-CDM 24. Joseph Mbilinyi- CDM
25.Freeman Mbowe- CDM 26. Kurudhum J. Mchuchuli – CDM 27.Halima Mdee-CDM
28.John Mnyika- CDM 29. Augustino L Mrema- TLP 30. Maryam S Msabaha- CDM 31.
Peter Msingwa-CDM 32. Christowaja G Mtinda CDM 33. Philipa G Mturano- CDM 34.
Christina L Mughwai- CDM 35.Joyce Mukya – CDM 36.Israel Y Natse – CDM 37.
Philemon Ndesamburo- CDM 38.Ahmed Juma Ngwali-CUF 39. Vincent Nyerere- CDM
40.Rashid Ali Omar-CUF 41.Meshack J Opulukwa- CDM 42. Lucy Owenya- CDM
43.Rachel Mashishanga- CDM 44. Mhonga Ruhwanya – CDM 45.Conchesta Rwamlaza –
CDM 46. Moza Abedi Saidy-CUF 47. Joseph R Selasini – CDM 48.David E Silinde-CDM
49.Rose Kamili - CDM 50. Cecilia Paresso- CDM 51.Kabwe Zuberi Zitto- CDM 52.
Magdalena Sakaya – CUF 53. Rebecca Mngodo- CDM 54. Sabreena Sungura -CDM