MARTIN DESTIO (27) anaishi kwa mateso makali kutokana na mguu wake wa kushoto kuharibika vibaya kwa vidonda viwili vinavyomsumbua kwa muda wa miaka nane sasa.
Kijana huyo mkazi wa Mjimwema mjini Mpanda anawaomba wasamalia wema wenye mapenzi mema kumchangia gharama za matibabu ili aweze kupona na kurejea katika hali yake ya kawaida
Akizungumza na mwandishi wa habari hizi jana Jumamosi April 21, 2012 alisema kuwa alipata jeraha la kidonda mwaka 2004 asubuhi alipokuwa akiwahi ibada ya kanisani kutumikia kama alivyokuwa amezoea akiwa njiani alijikwaa kwa kijiti kilichomkwangua na kumchubua kasha damu ikatoka kiasi
Alisema siku hiyo aliona kama kijidonda cha kawaida lakini siku zilivyozidi kusonga mbele ndivyo na kidonda kilivyozikdi kukua huku akiendelea kupata matibabu katika hospitali ya wilaya ya Mpanda
Alisema hali ilipozidi kuwa mbaya alipata msaada kutoka kwa Mhe. Pinda, Waziri Mkuu akaenda kutibiwa hospitali ya Muhimbili jijini DSM lakini haikusaidia akapewa rufaa ya kwenda kutibiwa nchini India
Wakati akitafuta ufadhiri wa kwenda India alisema alijitokeza msamaria mmoja aliyemtaja kwa jina la Raju na kumpeleka hospitali ya CCBRT DSM ambako waliweza kukata sehemu ya mwili wake na kuuotesha katika kidonda akaanza kupata nafuu
Alisema baada ya muda mfupi alianza kuona mabadiliko ya kidonda kuanza kuongezeka akarejea hospitali ya CCBRT akapewa rufaa ya kwenda India ambapo alipopigiwa hesabu ya gharama akaambiwa inatakiwa shilingi milioni kumi na nne (14,000,000/=) kwa safari na matibabu
Alisema amejaribu kuomba wahisani na kufanikiwa kupata shilingi milioni nne (4,000,000/=) bado milioni kumi (10,000,000/=) hivyo wewe msomaji tunakuomba utoe msaada kwa kuchangia japo kiasi chochote ulichonacho.
Mchango wako wasilisha kwa njia utakayoona inafaa, piga simu namba 0767 519989 au 0784 519988 au fika ofisi ya Waziri Mkuu wasilisha mchango wako au wasiliana na mbunge wa jimbo la Mpanda mjini Mhe. Said Amour Arfi 0786001122 au mbunge wa viti maalumu mkoa wa Katavi mhe Pudensiana Kikwembe 0759457879
MUNGU AKUBARIKI SANA.
HOJA YA MH. ZITTO KABWE YA KUPIGA KURA ZA KUTOKUWA NA IMANI NA WAZIRI MKUU YAPIGWA CHINI NA KANUNI ZA BUNGE
Taarifa za hivi punde kutoka Bungeni Mjini Dodoma,zinaeleza kuwa Kusudio la Mbunge wa Jimbo la Kigoma Kaskazini,Mh. Zitto Kabwe la kutaka kupiga kura za kuanzishwa kwa mjadala wa kutokuwa na imani na Waziri Mkuu,Mh. Mizengo Pinda,limepigwa chini na Spika wa Bunge,Mh. Anne Makinda.
Akisoma kanuni za Bunge,Mh. Spika alisema kwa mujibu wa kanuni za Bunge na Katiba ya Nchi,kusudio la kutaka kumuondoa Madarakani Waziri Mkuu kwa kupiga kura ya kutokuwa na Imani nae ambayo ni taarifa ya maandishi inapaswa kuwasilishwa kwake siku 14 kabla ya siku husika.
Hivyo kwakuwa ofisi yake haijapata taarifa ya maandishi ju ya zoezi hilo,basi zoezi hilo moja kwa moja litakuwa ni batili, na kwasababu kikao hicho cha Bunge kinatarajiwa kufungwa siku ya jumatatu,basi hakutakuwa na uwezekano wa zoezi hilo kukamilika.
Awali Mbunge wa Jimbo la Bumbuli,Mh. January Makamab aliomba muongozo wa Spika kuhusu jambo hilo ndipo Spika,Mh. Anne Makinda akasimama na kutoa ufafanuzi huo.Na www.issamichuzi.blogspot.com

MAMBO YA ZE ORIJINO COMEDY
WAKUVANGA WA ORIJINO KOMEDY APAGAWISHWA NA ULANZI IRINGAmsanii wa Orijino Komedy Bw.Wakuvanga akinywa pombe ya asili ya mkoa wa Iringa Ulanzi eneo la Kihesa mjini Iringa jioni hii
Jasiri haachi asili ama mdharau kwao ni mtumwa ni vigumu sasa na wasanii kupenda pombe za asili kama hivi
Hapa wakipokezana lita ya ulanzi
Wakuvanga akiwa na wadau eneo la Kihesa mjini Iringa huku gari lao likiwa limechafuliwa kwa kuchorwa kwa tope
Wakuvanga akionyesha gari lake lilivyochafuliwa kwa tope