Naibu Waziri wa Uchukuzi Dr. Charles Tizeba |
Taarifa zinaeleza kuwa Naibu waziri huyo amerejea Katavi baada ya kutoridhishwa na majibu ya hoja yaliyotolewa katika kikao cha tahmnini hiyo alipokuwa jijini DSM kwani hakushiriki kikao hicho hadi mwisho hivyo amerejea kuweka mambo sawa ili kukidhi mahitaji ya wawekezaji.
Naibu Waziri huyo aliwasili mkoani Katavi Desemba 2, 2012 ambapo jumatatu desemba 3, alifanya kikao cha ndani baina ya viongozi wa mkoa wa Katavi na wadau wa sekta ya uchukuzi ambapo baadaye mchana alifika katika kituo cha reli cha Mpanda kutembelea eneo hilo
Akiwa katika stesheni ya reli ya Mpanda Naibu waziri wa uchukuzi alipiga marufuku tabia ya makarani wa treni kuwatoza faini wananchi wanaokosa tiketi na kuingia ndani ya behewa ili kusafiri kutokana na kuwepo kwa tatizo la ukosefu wa tiketi za kusafiria za treni kutoka Mpanda hadi mikoa ya Mwanza, Tabora, Dodoma na DSM.
Alisema kuanzia jana hakuna karani yeyote kumlipisha faini abiria aliyepanda treni bila tiketi na badala yake walipe nauli ya kawaida au waangalie utaratibu wa kuwapunguzia nauli kwani wanapata shida ya kusafiri wakiwa wamesimama hadi Tabora.
Leo Naibu Waziri ametembelea ujenzi wa gati la meli Kasanga mkoani Rukwa na kesho atatembelea ujenzi wa gati la meli Karema mkoani Katavi.
HII NDIO AJALI MBAYA ILIYOUA WATANO WA FAMILIA MOJA IRINGA LEO
GARI AINA YA SCANIA LENYE CABIN NA. T 840 BST LIKIWA NA TRAILER NAMBA T 566 BNQ LILIGONGWA KWA NYUMA NA TOYOTA RAV 4 T 770 BMP HUKO TANANGOZI IRINGA NA KUSABABISHA VIFO VYA WATU WA TANO WA FAMILIA MOJA PAPO HAPO WALIOKUWA KATIKA GARI HILO RAV 4
Ajali mbaya imetokea mkoani Iringa mchana wa leo na kusababisha vifo vya watu wanne wa familia moja pamoja na mfanyakazi wa ndani mmoja.
Ajali hiyo imetokea katika eneo la Tanangozi wilaya ya Iringa kwenye kizuizi cha barabara cha mafundi wa kutengeneza barabara kuu ya Iringa -Mafinga mkoani Iringa mida ya saa nane mchana
Kwa mujibu wa mashuda wa tukio hilo wameueleza mtandao huu wa www.francisgodwin.blogspot.com kuwa chanzo cha ajali hiyo ni dereva wa gari dogo aina ya Rav 4 lenye namba za usajili T 770 BMP kulipalamia lori lenye tela kwa nyuma.
Huku
chanzo kikitajwa kuwa ni kuendesha kwa mwendo kasi wa dereva wa
gari ndogo marehemu Ezekiel Mwaiteleke na kushindwa
kulimudu na kulipalamia lori kwa nyuma.
Kwa mujibu wa mashuda wa tukio hilo wameueleza kuwa chanzo cha ajali hiyo ni dereva wa gari dogo aina ya Rav 4 kuendesha kwa mwendo kasi na kushindwa kulimudu na kulipalamia lori kwa nyuma na kuwa gari hiyo ilikuwa ikitokea jijini Dar es Salaam kwenda Kyela mkoani Mbeya.
Hivyo katika ajali hiyo abiria wote wanne akiwemo baba na mama wa watoto wawili waliokuwemo katika gari hiyo pamoja na watoto hao kufa papo hapo na maiti zote kupelekwa katika Hospitali ya mkoa wa Iringa.
Majina ya waliokufa ni pamoja na Ezekiel Mwaiteleke ambaye ni dereva wa gari hilo na baba wa familia hiyo ,mkewe Grace Mwaiteleke ,mtoto Kelvin Mwaiteleke (2),Happy Mwandike na mfanyakazi wao wa ndani aliyefahamika kwa jina la Linda Ezekiel huku majeruhi katika ajali hiyo ni mmoja na amekimbizwa Hospital ya mkoa wa Iringa.
BREAKINGNEWz RAV 4 YAUA WANNE WA FAMILIA MOJA IRINGA
Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania (IGP) Said Mwema
Ajali mbaya imetokea mkoani Iringa mchana wa leo na kusababisha vifo vya watu wanne wa familia moja .Ajali hiyo imetokea katika eneo la geti la mafundi wa kutengeneza barabara kuu ya Iringa -Mafinga mkoani Iringa.
Kwa mujibu wa mashuda wa tukio hilo wameueleza mtandao wa www.francisgodwin.blogspot.com kuwa chanzo cha ajali hiyo ni dereva wa gari dogo aina ya Rav 4 kuendesha kwa mwendo mkali na kushindwa kulimudu na kulipalamia lori kwa nyuma.
Hivyo katika ajali hiyo abiria wote wanne akiwemo baba na mama wa watoto wawili waliokuwemo katika gari hiyo pamoja na watoto hao kufa papo hapo na maiti zote kupelekwa katika Hospitali ya mkoa wa Iringa.
JUMATANO, TAREHE 5 DISEMBA 2012
Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA)
inatangaza bei kikomo za bidhaa za mafuta ya petroli hapa nchini. Bei hizi
zitaanza kutumika kuanzia Jumatano, Tarehe 5 Disemba 2012. Pamoja na kutambua
bei kikomo za bidhaa mbalimbali za petroli nchi nzima, ni muhimu kuzingatia
yafuatayo.
(a) Bei za jumla na rejareja kwa mafuta aina zote ya Petroli,
Dizeli na Mafuta ya Taa zimeongezeka ikilinganishwa na toleo lililopita la
tarehe 07 Novemba 2012.
Katika toleo hili, bei za rejareja kwa Petroli na
Dizeli zimeongezeka kwa viwango vifuatavyo: Petroli Sh 70/lita sawa na asilimia
3.4; Dizeli Sh 10/lita sawa na asilimia 0.53.
Bei ya Mafuta ya Taa imepungua
kwa Sh 3/lita sawa na asilimia 0.1. Bei za jumla kwa kulinganisha matoleo haya
mawili zimeongezeka kama ifuatavyo: Petroli kwa Sh 69.56/lita sawa na asilimia
3.52; Dizeli kwa Sh 10.04/lita sawa na asilimia 0.52.
Bei ya Mafuta ya Taa
imepungua kwa Sh 3/lita sawa na asilimia 0.15. Mabadiliko haya ya bei
yametokana na ongezeko la bei ya mafuta katika soko la dunia na kushuka kidogo
kwa thamani ya Shilingi ya Tanzania dhidi ya Dola ya Marekani.
(b) Kwa mujibu wa Sheria ya Mafuta ya mwaka 2008, bei za
bidhaa za mafuta ya petroli zitaendelea kupangwa na soko. EWURA itaendelea
kuhamasisha ushindani kwa kutoa taarifa za bei kikomo za bidhaa za mafuta.
Taarifa hizi zina lengo la kuwasaidia wadau kufanya maamuzi stahiki kuhusu manunuzi
ya bidhaa za mafuta.
(c) Kampuni za mafuta zipo huru kuuza bidhaa za mafuta ya
petroli kwa bei ya ushindani ilimradi bei hizo ziko chini ya bei kikomo (price
cap) kama ilivyokokotolewa na fomula mpya iliyopitishwa na EWURA na ambayo
ilichapwa kwenye Gazeti la Serikali Na. 454 la tarehe 23 Desemba 2011.
(d) Vituo vyote vya mafuta vinatakiwa kuchapisha bei za bidhaa
za mafuta katika mabango yanayoonekana bayana na yakionyesha bei ya mafuta,
punguzo, vivutio vya biashara au promosheni zinazotolewa na kituo husika.
Pale
ambapo inawezekana kuchagua, wateja wanashauriwa kununua bidhaa za mafuta
kutoka kwenye vituo vinavyouza mafuta kwa bei ndogo zaidi ili kushamirisha
ushindani. Ni kosa kuuza mafuta bila kuweka mabango ya bei inayoonekana vizuri
kwa wateja na adhabu itatolewa kwa kituo husika.
(e) Wanunuzi wanashauriwa kuhakikisha kuwa wanapata stakabadhi
ya malipo inayoonesha jina la kituo, tarehe, aina ya mafuta yaliyonunuliwa na
bei kwa lita. Stakabadhi hiyo ya malipo itatumika kama kidhibiti cha mnunuzi wa
mafuta endapo kutajitokeza malalamiko ya ama kuuziwa mafuta kwa bei ya juu
kuliko bei kikomo; ama endapo utakuwa umeuziwa mafuta yenye kiwango cha ubora
kisichofaa.