MKOA wa Katavi umedhamiria kuondoa kero ya ukosefu wa maji
katika maeneo ya vijijini ifikapo juni 2014.
Hayo yalibainishwa na mkuu wa mkoa huo Dr Rajabu Rutengwe
katika kilele cha wiki ya maji mkoani humo katika kijiji cha Ikola wilaya ya
Mpanda mwishoni mwa wiki
Alisema kila siku ofisi yake imekuwa ikihangaika na miradi
ya maji katika vijiji mbali mbali na mijini ili kukamilisha miradi hiyo kwa
ufanisi mkubwa na kuondoa kero ya maji
Katika kufanikisha azima hiyo mkuu wa mkoa aliwataka
wananchi kuacha kabisa kharibu vyanzo vya maji na uharibifu wa mazingira katika
meneo yao
Aidha aliziagiza mamlaka za serikali za mitaa na ofisi ya
Katibu tawala wa mkoa huo kusimamia kwa karibu suala la utunzaji wa mazingira
na kuzuia shughuli za binadamu zinazopelekea uharibifu wa mazingira
Amepiga marufuku shughuli za uharibifu wa mazingira kama
vile uingizaji haramu wa mifugo, ukataji mkaa, kilimo cha bila utaalamu na kazi
zingine zenye nasaba na uharibifu wa mazingira.