Dkt.Bilal Azindua Mkoa Wa Katavi
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungao ya Tanzania Dkt Mohamed Gharib Bilal akizindua rasmi mkoa wa Katavi kwa kuweka jiwe la msingi katika kilima cha kijiji cha Kabungu kwa ajili ya kujenga kituo cha kumbukumbu ya historia ya mkoa wa Katavi, kulia kwake ni mkuu wa mkoa hu Dr Rajabu M. Rutengwe akishuhudia jana Novemba 25, 2012
Mkuu wa wilaya ya mpanda, Paza Tusamale Mwamlima akimkaribisha makamu wa Rais wilayani kwake katika hafla ya uzinduzi wa mkoa wa Katavi na Tathmini ya uwekezaji kwa mwaka mmoja.
Kijiji Cha Kabungu ndipo palipozaliwa Wilaya ya Mpanda Mwaka 1947 na Boma la mtawala wa kwanza wa kikoloni Mpanda lilijengwa hapo
Makamu
wa Rais Akizungumza na wafanyakazi wa benki ya NMB wakati alipotembelea
katika banda hilo leo njini Mpanda Kushoto ni Mkuu wa mkoa wa Katavi
Dkt. Rajab Rutengwe.
Waziri
Mkuu wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Mh. Mizengo Pinda akizungumza
na wana Katavi wakati wa uzinduzi wa mkoa wa mpya wa Katavi kwenye
viwanja vya Kashaulili mjini Mpanda leo.
Wananchi wa Mkoa wa Katavi wakishangilia
Baada ya uwekaji
wa jiwe la msingi kijijini Kabungu, Makamu wa Rais alirejea mjini mpanda
katika viwanja vya Kashaulili ambapo kumefanyika shughuli mbalimbali
za uzinduzi rasmi wa mkoa huo na hotuba mbalimbali zikiendana na
sherehe za ngoma za makabila mbalimbali ya asili ya mkoa wa KataviMakamu wa Rais Dkt. Gharib Bilal akizungumza na wananchi wa kijiji cha Kabungu wakati wa uwekaji wa jiwe la msingi kuzindua mkoa wa Katavi, kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Katavi Dkt Rajab Rutengwe na kutoka kulia ni Mke wa Makamu wa Rais Mama Zakia Bilal na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Katavi Bw. Abdallah Mselem Said
Makamu wa Rais Dkt. Gharib Bilal, Waziri Mkuu Mizengo Pinda, Waziri wa Uwezeshaji na Uwekezaji Dkt Mary Nagu, Mke wa Makamu wa Rais mama Zakia Bilal na Mke wa Waziri Mkuu mama Tunu Pinda wakiimba wimbo mara baada ya kuwasili kwenye viwanja vya Kashaulili mjini Mpanda tayari kwa Sherehe za uzinduzi wa mkoa wa Katavi
Baadhi ya wawekezaji waliohudhuria katika uzinduzi huo uliofanyika kwenye viwanja vya Kashaulili.
Mkuu
wa mkoa wa Katavi akiongea na kukaribisha viongozi mbalimbali kutoka
salam zao kutoka mikoa waliyotoka na wizara mbalimbali.
Waziri
wa Ardhi na makazi Goodluck Ole Medeye akizungumza na wana Katavi na
kuwaasa mambo mbalimbali kuhusu ardhi yao hasa katika suala zima la
uwekezaji, ambapo amewaambia wasiuze ardhi bali waingie ubia na
wawekezaji ili kunufaisha vizazi vyao pia.
Mke wa Waziri Mkuu Mama Tunu Pinda akiwasalimia wananchi wa Katavi na kuwapongeza kwa kupata mkoa mpya wa Katavi.
Mama Aisha Bilal akisalimia wananchi wa katavi katika sherehe hizo.
Kwaya
ya Vijana ya Moravian mjini Mpanda wakitumbuiza katika uzinduai huo
uliofanyika kwenye viwanja vya Kashaulili mjini Mpanda.
Martha
Mbogo mwimbaji wa kundi la Katavi Curture Group akiimba wakati kundi
hilo lilipokuwa likitumbuiza katika uzinduzi huo mjini Mpanda.
Watoto Daniel Ntwangile na Christina Benedicto wakitunzwa na Waziri Mkuu Mizengo Pinda mara baada ya kuimba na kucheza vizuri na Kwaya ya Vijana Moravian Mjini Mpanda wanaofuatia ni Waziri wa Uwezeshaji na Uwekezaji Dkt Mary Nagu, Mke wa Makamu wa Rais mama Zakia Bilal na Mke wa Waziri Mkuu mama Tunu Pinda wakijiandaa na wao kuwatunza