Tuesday, April 30, 2013

MTOTO MIGUU SENTIMITA TANO

Mpanda
MTOTO wa ajabu alizaliwa jana mchana katika hospitali ya wilaya ya Mpanda mkoa wa Katavi akiwa na uzito wa kilogramu  nne, miguu na mikono yenye urefu wa sentimita tano tu na kichwa kikubwa
Taarifa zilizopatikana mara baada ya kuzaliwa mtoto huyo zilidai kuwa mtoto huyo alizaliwa akiwa hai lakini baada ya dakika tano akafariki dunia alikuwa na uzito wa kilogramu nne, miguu yenye urefu wa sentimita tano, mikono ina urefu wa sentimita tano na kichwa kikubwa
Akizungumza hospitalini hapo muuguzi mkuu wa hospitali ya wilaya ya Mpanda, Alexander Gervas Kasagula alisema mama wa mtoto huyo anaitwa Johari Rafaeli (35) mkazi wa mtaa wa Makanyagio mjini Mpanda ambaye alijifungua kwa njia ya upasuaji April 30, 2013 majira ya saa sita na robo mchana.
Kasagula alisema mama huyo alikuwa akipata huduma ya upimaji (kliniki) katika zahanati ya Afya Dispensary iliyoko katika eneo la Makanyagio hadi miezi tisa ilipotimia wakamuelekeza akajifungulie hospitali ya wilaya ingawa hawakuweza kubainisha kama mama huyo alikuwa na tatizo lolote
Alisema baada ya kumpokea mama huyo April 29, 2013 waganga walimpangia kuwa afanyiwe upasuaji mkubwa baada ya kubaini kuwa huyo mama alikuwa na mtoto mkubwa (big baby) hivyo asingeweza kujifungua kwa uwezo wake mwenyewe
Alifafanua kuwa majira ya saa tatu walimuandaa na kumpeleka chumba cha upasuaji na kumfanyia upasuaji ambao ulikamilika majira ya saa sita mchana na kubaini kuwa kiumbe aliyekuwa tumboni alikuwa na hali ya kimaumbile isiyo ya kawaida
Akizungumzia hali ya mama mwenye huyo Kasagula alisema kuwa baada ya upasuaji mama anaendelea vema chini ya uangalizi wa wauguzi katika wodi ya tatu ambayo ni wodi ya wazazi ingawa kiumbe kilifariki dakika tano baada ya kuzaliwa
Ndugu anayemuuguza mama huyo katika hospitali ya wilaya alipoulizwa juu ya maisha ya mgonjwa wake nyumbani licha ya kuomba jina lake lihifadhiwe alisema kuwa mama huyo ana vizazi vitano lakini watoto walio hai wako watatu na wawili wamefariki akiwemo wa jana
Alisema mtoto wa kwanza ni wa kike yupo hai na wa pili ni wa kike na wa tatu ni wa kiume ambapo mama huyo aliweza kupoteza kizazi chake cha nne na cha tano kwani wote walifariki baada ya upasuaji na wote walikuwa wa kiume



MTOTO MIGUU SENTIMITA TANO

Mpanda
MTOTO wa ajabu alizaliwa jana mchana katika hospitali ya wilaya ya Mpanda mkoa wa Katavi akiwa na uzito wa kilogramu  nne, miguu na mikono yenye urefu wa sentimita tano tu na kichwa kikubwa
Taarifa zilizopatikana mara baada ya kuzaliwa mtoto huyo zilidai kuwa mtoto huyo alizaliwa akiwa hai lakini baada ya dakika tano akafariki dunia alikuwa na uzito wa kilogramu nne, miguu yenye urefu wa sentimita tano, mikono ina urefu wa sentimita tano na kichwa kikubwa
Akizungumza hospitalini hapo muuguzi mkuu wa hospitali ya wilaya ya Mpanda, Alexander Gervas Kasagula alisema mama wa mtoto huyo anaitwa Johari Rafaeli (35) mkazi wa mtaa wa Makanyagio mjini Mpanda ambaye alijifungua kwa njia ya upasuaji April 30, 2013 majira ya saa sita na robo mchana.
Kasagula alisema mama huyo alikuwa akipata huduma ya upimaji (kliniki) katika zahanati ya Afya Dispensary iliyoko katika eneo la Makanyagio hadi miezi tisa ilipotimia wakamuelekeza akajifungulie hospitali ya wilaya ingawa hawakuweza kubainisha kama mama huyo alikuwa na tatizo lolote
Alisema baada ya kumpokea mama huyo April 29, 2013 waganga walimpangia kuwa afanyiwe upasuaji mkubwa baada ya kubaini kuwa huyo mama alikuwa na mtoto mkubwa (big baby) hivyo asingeweza kujifungua kwa uwezo wake mwenyewe
Alifafanua kuwa majira ya saa tatu walimuandaa na kumpeleka chumba cha upasuaji na kumfanyia upasuaji ambao ulikamilika majira ya saa sita mchana na kubaini kuwa kiumbe aliyekuwa tumboni alikuwa na hali ya kimaumbile isiyo ya kawaida
Akizungumzia hali ya mama mwenye huyo Kasagula alisema kuwa baada ya upasuaji mama anaendelea vema chini ya uangalizi wa wauguzi katika wodi ya tatu ambayo ni wodi ya wazazi ingawa kiumbe kilifariki dakika tano baada ya kuzaliwa
Ndugu anayemuuguza mama huyo katika hospitali ya wilaya alipoulizwa juu ya maisha ya mgonjwa wake nyumbani licha ya kuomba jina lake lihifadhiwe alisema kuwa mama huyo ana vizazi vitano lakini watoto walio hai wako watatu na wawili wamefariki akiwemo wa jana
Alisema mtoto wa kwanza ni wa kike yupo hai na wa pili ni wa kike na wa tatu ni wa kiume ambapo mama huyo aliweza kupoteza kizazi chake cha nne na cha tano kwani wote walifariki baada ya upasuaji na wote walikuwa wa kiume



Sunday, April 21, 2013

JELA MIAKA 30 KWA KUMBAKA KIKONGWE WA MIAKA 90


JELA MIAKA 30 KWA KUMBAKA KIKONGWE WA MIAKA 90
wacha Mungu wasema tuombe na kufunga
MAHAKAMA ya hakimu mkazi wilaya ya Mpanda mkoani Katavi imemuhukumu kifungo cha miaka thelathini jela Sindembela Msagi (26) baada ya kupatikana na hatia ya kumbaka kikongwe mwenye umri wa miaka tisini mwenye ugonjwa wa kupooza
Hukumu hiyo iliyotolewa Ijumaa Aprili 19, 2013 na hakimu mfawidhi mkazi wa mahakama hiyo Chiganga Tengwa kufuatia tukio la ubakaji lilitokea Desemba 22, 2012 katika kijiji cha Bulembo katika makazi ya wakambizi ya Katumba wilaya ya Mlele
Awali akitoa maelezo mahakamani hapo mwendesha mashitaka wa jeshi la polisi, Ally Bwijo alisema kuwa mtuhumiwa alifanya kosa hilo Desemba 22, 2012 majira ya usiku baada ya kumuingilia kikongwe huyo ambaye ni mgonjwa wa kupooza kwa muda mrefu
Aliiambia mahakama kuwa baada ya kumbaka kikongwe huyo mtuhumiwa aliweza kukimbia lakini baada ya wananchi kumuhoji kikongwe huyo aliweza kumtambua kwa sura na jina kwani alikuwa anamfahamu kabla ya tukio hilo la kinyama
Alisema kufuatia maelekezo ya kikongwe aliyefanyiwa unyama huo wananchi kwa kushirikiana na jeshi la polisi waliweza kumkamata mtuhumiwa na kumfikisha katika vyombo vya sheria kwa hatua zaidi
Akitoa utetezi wake mahakamani hapo Sindembelea Msagi aliiambia mahakama kuwa imuonee huruma kwani alifanya kosa hilo kwa mara ya kwanza na kuwa alishawishiwa na tama ya pesa kutokana na kuwa na  anawategemezi wengi  wanaohitaji pesa za kuwahudumia
Baada ya kupata maelezo ya pande zote hakimu Chiganga Tengwa alisema mahakama yake imeridhishwa bila shaka yoyote na ushahidi uliotolewa na upande wa mashitaka na hivyo mtuhumiwa anastahili adhabu
Chiganga alisema kwa kutumia kifungu sha sheria Namba 154 cha makosa ya ubakaji iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2002 mtuhumiwa atatumikia kifungo cha miaka thelathini jela ili iwe fundisho kwa wengine wenye tabia ya ubakaji

MAAJABU YA MPANDA

Details
Published on Wednesday, 17 April 2013 00:46
Written by PETI SIYAME in Mpanda, DAILY NEWS
Hits: 178
MPANDA District Council in Katavi Region plans to transform the area into a satellite town, a business hub and centre of learning by constructing four ambitious projects worth over 660bn/-.
The projects include construction of Katavi University of Agriculture (KUA), modern shopping mall, market, bus terminal and upgrading of eight kilometres of roads within the town to tarmac level.
Mpanda Town Council Executive Director, Mr Joseph Mchina told the ‘Daily News’ on Tuesday that the funds are expected to come from various development partners including the World Bank and the Commercial Bank of Africa (CBA) as loans.
According to Mr Mchina, three years ago the council envisioned to build the university at Kazima area in Mpanda town at a cost of 650bn/-, where more than 500 acres of land have been allocated to that effect. Mr Mchina said that thus far CBA has already accepted to disbursed over 4.5bn/- as a loan for feasibility studies, curriculum development, project writeup and some of the funds would be spent on compensating people to pave way for the construction of the university.
The bank has agreed to finance the project after being satisfied with several guarantees by the council, including evaluation of the 500 acres of land set aside by the council for construction of KUA which is worth 3.6bn/-. Mr Mchina mentioned other guarantees as the acceptance by African Trade Insurance Agency (ATIA) to insure CBA’s loan.
Upon completion of the university, he said, apart from teaching modern farming techniques, it will also offer a special programme on bee-keeping. Other three planned projects will be financed by the World Bank which include construction of a modern bus terminal at the cost of 4.2bn/-, with eight companies already having expressed interest in undertaking the project.
“The other project is construction of a shopping mall that will cost 4.9bn/- from the same financier,” hinted Mr Mchina. He also revealed that the town council in collaboration with the National Housing Corporation (NHC) would jointly construct a five storey building that will have a conference hall at Paradise area and it is expected to cost 2.5bn/-. The project has been scheduled to start on May 12, this year

Thursday, April 18, 2013

ALAT RUKWA YASHAURI WATENDAJI

Na,Elizabeth Ntambala  , Katavi

Watendaji wa halmashauri katika mikoa ya Rukwa na Katavi wametakiwa kuhakikisha wanakutana na wananchi wa maeneo yanayohitajika kuchukuliwa kwa ardhi yao kabla ya kuanzisha miradi ili kuepukana na uwezekano wa kuingia katika migogoro ya ardhi.

Ushauri umetolewa na wajumbe wa Jumuiya ya serikali za Mitaa  (ALAT )katika mikoa ya Rukwa na Katavi ambao wako mjini Mpanda mkoani Katavi  kwaajili ya kikao chao na   kukagua shughuli mbalimbali za maendeleo katika halmashauri .

Akizungumza mara baada ya kukagua mradi wa jengo la ofisi ya Afisa Mtendaji wa kata ya Ilembo iliyojengwa kwenye eneo la Kasimba mjini Mpanda, Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Nkasi  Bw. Kimulika Galikunda amesema miradi mingi ya ya halmashauri imekuwa ikichelewa kukamilika kutokana na wananchi wa maeneo husika kutoshirikishwa  katika mchakato wake.

Galikunda amesema matokeo ya kupuuzwa kwa wananchi yamekuwa yakileta madhara kwa wananchi hao kuiwekea pingamizi miradi hiyo, hali ambayo inachangiwa na baadhi yao kutolipwa fidia kwa haraka na kuzua malalamiko mengi kwa serikali yao.

Amesema ipo haya kwa viongozi wa halmashauri kuzingatia mambo hayo ili kuleta wepesi katika kufanikisha miradi yao huku wananchi pia wakiwaunga mkono baada ya kuridhika kuwa watendewa haki katika fidia za ardhi yao iliyochukuliwa.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa ALAT katika mikoa ya Rukwa na Katavi Bw. Godfrey Sichona amewataka Watendaji wa halmashauri hizo kuwa makini katika ujenzi wa miradi hiyo ikiwa ni pamoja na kuzingatia miundo mbinu muhimu inayohitajika katika majengo yao.
Mwisho.

RUKWA HAWAAMINI HOMA YA NGURUWE

 
Na Elizabeth Ntambala  ,Rukwa

IMEELEZWA KUWA kutokana na ugonjwa wa homa ya nguruwe iliyojitokeza katika baadhi ya mikoa ikiwa pamoja na Rukwa kuwa ni athali kwa matumizi ya binadamu japo wao hawaamini

Akizungumza   kwa njia ya simu leo , Ofisa Mifugo na Uvuvi  wa  Halmashauri ya Sumbawanga , Denis Magala  ameleza kuwa  tarafa tano  zimeshambuliwa vibaya na  homa  hiyo  ya nguruwe  ambazo  amezitaja kuwa ni  pamoja na Laela  na Mpui  zilizopo  wilayani  Sumbawanga , Matai , Mwimbi  Kasanga  mwambao  mwa Ziwa Tanganyika  wilaya mpya  ya Kalambo  mkoani Rukwa.

Huku mjini Sumbawanga biashara ya nyama ya nguruwe maarufu kama kitimoto imepigwa marufuku.

Amesema kuwa  licha ya homa  hiyo  ya  nguruwe  inapomshambulia  nguruwe  huwa  aina  tiba wala  chanjo  hadi sasa  isitoshe   unasababisha  hasara kubwa kwa mfugaji kwani  unaenea kwa  kasi  na kuua  nguruwe  wote walioshambuliwa  na  ugonjwa huo.

Aidha kwa upande wa  binadamu kudaiwa kuwa licha  ya kwamba hausababishi  maradha yoyote kiafya lakini  wanazuiliwa kula nyama  ya  nguruwe  kwa  kuwa nao  watasababisha  kuueneza  ugonjwa  huo  kutoka  eneo  moja hadi  lingine.

“Ndiyo  maana biashara yoyote ya nguruwe na mazao yake ikiwemo nyama , mbolea , manyoya , mifupa , ngozi na vyakula vya kusindikwa imepigwa marufuku ili  ikiwa  ni jitihada  za makusudi za  kukabiliana  na  ugonjwa  huo “ alisisitiza.

Kwa  mujibu  wa Ofisa huyo  wa Mifugo na Uvuvi   katika  tarafa hizo tano  zilizokumbwa na mlipuko wa homa hiyo, kuanzia Januari  mwaka  huu  hadi  sasa  tayari  nguruwe 4,884 wamekufa kwamba kabla ya ugonjwa huo, kulikuwa na nguruwe 28,630 na sasa wamebaki 24,449.

Kwa upande wa wafanyabiashara wa nyama hiyo maarufu kama kitimoto wamesema kumekuwepo na ugumu wa maisha kwa upande wao kwani'ilikuwa ikiwapatia kipato kwa kikubwa kwa ajili ya kusaidia kusukuma gurudumu la maisha yao kutokana na watu wengi kupenda kutumia kitoweo hicho.

Sunday, April 14, 2013

MAKUBWA MENGINE HAYA HAPA



JELA MIAKA 10 KWA KOSA LA KUNYONYA ULIMI MWANAFUNZI WA KIKE
Mahakama ya Hakimu ya   mkazi  ya   Wilaya ya Mpanda  mkoani Katavi imemhukumu Kassim  Lugendo  (41) Mkazi wa Kijiji cha Kambanga Tarafa ya  Kabungu  kifungo  cha miaka  kumi  jela kwa kosa la  kumnyonya  ulimi  mwanafunzi mwenye umri wa miaka 13

Hukumu  hiyo  ilitolewa  na  Hakimu mkazi  mfawidhi  wa   mahama  ya wilaya  ya Mpanda  Chiganga Tengwa  baada ya ushahidi uliotolewa kumtia hatiani mtuhumiwa kuwa alimnyonya ulimi mwanafunzi wa darasa la tano katika  shule ya msingi Igalula bila ridhaa yake

Awali  akitoa maelezo ya upande wa mashitaka katika  kesi  hiyo   mwendesha  mashita  kutoka jeshi la polisi mkoani hapo, Ally Mbwijo  aliileza mahakama kuwa mshitakiwa    Kassimu Lugendo  alitenda kosa hilo    machi 30 mwaka jana  majira ya saa   6  mchana  akiwa nyumbani kwake katika kijiji cha Kambanga.

Ilidaiwa  kuwa siku   hiyo   mwanafunzi  huyo  alikuwa akitoka  shuleni  akielekea  nyumbani  kwao   alipopita  karibu  na  nyumba  ya mshitakiwa aliitwa na mwenye nyumba ambaye  alikuwa katika nyumba hiyo na kusogea mlangoni lakini alipokuwa mlangoni kabla ya kuingia ndani mtuhumiwa alimwingiza   ndani ya  nyumba kwa nguvu.

Mbwijo  aliiambia mahakama  kuwa  baada ya mshitakiwa    kumwingiza  ndani ya nyumba yake mwanafunzi  huyo alianza kumnyonya  ulimi  (Denda) mwanafunzi huyo  na kisha  alimwingiza   vidole   vyake  katika  sehemu  za siri   za mwanafunzi huyo

Ilielezwa mahakamani hapo kuwa wakati tukio hilo likiendelea kufanyika  mwanafunzi   huyo  alikuwa  akipiga  mayowe muda  akiomba  msaada  kutoka kwa majirani ambao kwa bahati nzuri walisikia na kuingia ndani ya nyumba hiyo  na kumkuta mshitakiwa akiwa na mwanafunzi  huyo  huku sehemu  ya siketi  yake   ikiwa imefunuliwa nusu

Hakimu mkazi  mfawidhi  Chiganga Tengwa  baada ya  kusikiliza  maelezo  ya pande zote alisema ushaidi uliotolewa na upende wa mashitaka umethibitisha bila shaka kuwa mshitakiwa  alitenda kosa hilo kinyume cha sheria za nchi na maadili ya Mtanzania na kumpa mshitakiwa nafasi ya kujitetea kabla mahakama haijatoa adhabu.

Katika utetezi wake   mshitakiwa  Kassimu  Lugendo  aliiomba  mahakama  isimpe adhabu kwa kile alicho kieleza kuwa  yeye  anafamilia ya watoto  saba   na wazazi  wake wote wawili   ni walemavu na wanamtegemea yeye

Pamoja na kujitetea kwa mshitakiwa huyo, Hakimu Chiganga  alisema  kitendo alicho kifanya mshitakiwa  ni cha  hatari  kwani kina  weza  kikamsababishia   msichana  huyo  ugojwa  wa  ukimwi na maradhi mengine ya kuambukiza  ambapo  mshitakiwa  amevunja  sheria  kifungu  namba  235  cha sheria   ya   marekebisho  ya mwaka  2002  ambapo  mahakama imetia hatiani mshitakiwa Kassimu Lugendo  na  imemuhukumu kwenda  kutumikia jela kifungo  cha  miaka  kumi jela