Sunday, April 14, 2013

MAKUBWA MENGINE HAYA HAPA



JELA MIAKA 10 KWA KOSA LA KUNYONYA ULIMI MWANAFUNZI WA KIKE
Mahakama ya Hakimu ya   mkazi  ya   Wilaya ya Mpanda  mkoani Katavi imemhukumu Kassim  Lugendo  (41) Mkazi wa Kijiji cha Kambanga Tarafa ya  Kabungu  kifungo  cha miaka  kumi  jela kwa kosa la  kumnyonya  ulimi  mwanafunzi mwenye umri wa miaka 13

Hukumu  hiyo  ilitolewa  na  Hakimu mkazi  mfawidhi  wa   mahama  ya wilaya  ya Mpanda  Chiganga Tengwa  baada ya ushahidi uliotolewa kumtia hatiani mtuhumiwa kuwa alimnyonya ulimi mwanafunzi wa darasa la tano katika  shule ya msingi Igalula bila ridhaa yake

Awali  akitoa maelezo ya upande wa mashitaka katika  kesi  hiyo   mwendesha  mashita  kutoka jeshi la polisi mkoani hapo, Ally Mbwijo  aliileza mahakama kuwa mshitakiwa    Kassimu Lugendo  alitenda kosa hilo    machi 30 mwaka jana  majira ya saa   6  mchana  akiwa nyumbani kwake katika kijiji cha Kambanga.

Ilidaiwa  kuwa siku   hiyo   mwanafunzi  huyo  alikuwa akitoka  shuleni  akielekea  nyumbani  kwao   alipopita  karibu  na  nyumba  ya mshitakiwa aliitwa na mwenye nyumba ambaye  alikuwa katika nyumba hiyo na kusogea mlangoni lakini alipokuwa mlangoni kabla ya kuingia ndani mtuhumiwa alimwingiza   ndani ya  nyumba kwa nguvu.

Mbwijo  aliiambia mahakama  kuwa  baada ya mshitakiwa    kumwingiza  ndani ya nyumba yake mwanafunzi  huyo alianza kumnyonya  ulimi  (Denda) mwanafunzi huyo  na kisha  alimwingiza   vidole   vyake  katika  sehemu  za siri   za mwanafunzi huyo

Ilielezwa mahakamani hapo kuwa wakati tukio hilo likiendelea kufanyika  mwanafunzi   huyo  alikuwa  akipiga  mayowe muda  akiomba  msaada  kutoka kwa majirani ambao kwa bahati nzuri walisikia na kuingia ndani ya nyumba hiyo  na kumkuta mshitakiwa akiwa na mwanafunzi  huyo  huku sehemu  ya siketi  yake   ikiwa imefunuliwa nusu

Hakimu mkazi  mfawidhi  Chiganga Tengwa  baada ya  kusikiliza  maelezo  ya pande zote alisema ushaidi uliotolewa na upende wa mashitaka umethibitisha bila shaka kuwa mshitakiwa  alitenda kosa hilo kinyume cha sheria za nchi na maadili ya Mtanzania na kumpa mshitakiwa nafasi ya kujitetea kabla mahakama haijatoa adhabu.

Katika utetezi wake   mshitakiwa  Kassimu  Lugendo  aliiomba  mahakama  isimpe adhabu kwa kile alicho kieleza kuwa  yeye  anafamilia ya watoto  saba   na wazazi  wake wote wawili   ni walemavu na wanamtegemea yeye

Pamoja na kujitetea kwa mshitakiwa huyo, Hakimu Chiganga  alisema  kitendo alicho kifanya mshitakiwa  ni cha  hatari  kwani kina  weza  kikamsababishia   msichana  huyo  ugojwa  wa  ukimwi na maradhi mengine ya kuambukiza  ambapo  mshitakiwa  amevunja  sheria  kifungu  namba  235  cha sheria   ya   marekebisho  ya mwaka  2002  ambapo  mahakama imetia hatiani mshitakiwa Kassimu Lugendo  na  imemuhukumu kwenda  kutumikia jela kifungo  cha  miaka  kumi jela