Mpanda
MTOTO wa ajabu alizaliwa jana mchana katika hospitali ya
wilaya ya Mpanda mkoa wa Katavi akiwa na uzito wa kilogramu nne, miguu na mikono yenye urefu wa sentimita
tano tu na kichwa kikubwa
Taarifa zilizopatikana mara baada ya kuzaliwa mtoto huyo
zilidai kuwa mtoto huyo alizaliwa akiwa hai lakini baada ya dakika tano
akafariki dunia alikuwa na uzito wa kilogramu nne, miguu yenye urefu wa
sentimita tano, mikono ina urefu wa sentimita tano na kichwa kikubwa
Akizungumza hospitalini hapo muuguzi mkuu wa hospitali
ya wilaya ya Mpanda, Alexander Gervas Kasagula alisema mama wa mtoto huyo
anaitwa Johari Rafaeli (35) mkazi wa mtaa wa Makanyagio mjini Mpanda ambaye
alijifungua kwa njia ya upasuaji April 30, 2013 majira ya saa sita na robo
mchana.
Kasagula alisema mama huyo alikuwa akipata huduma ya upimaji
(kliniki) katika zahanati ya Afya Dispensary iliyoko katika eneo la Makanyagio
hadi miezi tisa ilipotimia wakamuelekeza akajifungulie hospitali ya wilaya
ingawa hawakuweza kubainisha kama mama huyo alikuwa na tatizo lolote
Alisema baada ya kumpokea mama huyo April 29, 2013
waganga walimpangia kuwa afanyiwe upasuaji mkubwa baada ya kubaini kuwa huyo
mama alikuwa na mtoto mkubwa (big baby) hivyo asingeweza kujifungua kwa uwezo
wake mwenyewe
Alifafanua kuwa majira ya saa tatu walimuandaa na
kumpeleka chumba cha upasuaji na kumfanyia upasuaji ambao ulikamilika majira ya
saa sita mchana na kubaini kuwa kiumbe aliyekuwa tumboni alikuwa na hali ya
kimaumbile isiyo ya kawaida
Akizungumzia hali ya mama mwenye huyo Kasagula alisema
kuwa baada ya upasuaji mama anaendelea vema chini ya uangalizi wa wauguzi
katika wodi ya tatu ambayo ni wodi ya wazazi ingawa kiumbe kilifariki dakika
tano baada ya kuzaliwa
Ndugu anayemuuguza mama huyo katika hospitali ya wilaya
alipoulizwa juu ya maisha ya mgonjwa wake nyumbani licha ya kuomba jina lake
lihifadhiwe alisema kuwa mama huyo ana vizazi vitano lakini watoto walio hai
wako watatu na wawili wamefariki akiwemo wa jana
Alisema mtoto wa kwanza ni wa kike yupo hai na wa pili
ni wa kike na wa tatu ni wa kiume ambapo mama huyo aliweza kupoteza kizazi
chake cha nne na cha tano kwani wote walifariki baada ya upasuaji na wote
walikuwa wa kiume