Friday, April 12, 2013

AMINI USIAMINI



BABA AUWA WANAE WATATU NA KUDUMBUKIZA MAITI ZAO NA MAMA YAO KISIMANI
KISA - Ni Wivu wa Mapenzi
Na Willy Sumia, Mpanda
Jeshi la polsi   Mkoa wa  Katavi  lina mshikilia  mkazi wa kijiji cha  Majimoto   kwa tuhuma    za kuwauwa   watoto   wake  watatu  na kuwatumbukiza  wawili ndani  ya kisima  cha  maji kutokana  na   ugomvi wa mapenzi

Kamanda wa polisi mkoani katavi amemtaja anayeshikiliwa kuwa ni Yustini  Albati  (24)  kutokana na mauwaji ya kusikitisha    ya  watoto  wa familia moja  lilitokea    majira ya saa 11 alfajiri   katika kijiji cha  Majimoto   wilaya ya mlele
Aliwataja watoto  walio uwawa  kuwa ni  Frenk Yustini (6),  Eliza  Yustini  (4) na  Maria Yustini  mwenye umri wa miezi 4 .
Alisema   katika tukio hilo  mama  mzazi wa watoto  hao Jackilini Luvike (21)  aliokolewa   na wananchi   akiwa   ametumbukizwa  ndani ya kisima hicho  pamoja na watoto wake akiwa mahututi na kukimbizwa hospitali ya wilaya yam panda kwa matibabu.
Alisema  wananchi hao waliweza kuokoa mwili  wa  mtoto Maria  iliokutwa  kando ya barabara  walioweza kuutambua kuwa  ni  mototo wa  mwanakijiji  mwenzao anayeitwa  Yustini
Kamanda Kidavashari alifafanua kuwa Wanakijiji waliamua kwenda  nyumbani  kwa  baba wa mtoto huyo  ambaye alikutwa akiwa na hofu akitaka kukimbia  mazingira yaliyopelekea  wanakijiji kumuuliza waliko mtoto wake Yustini  na mke wake  lakini mtuhumiwa huyo aliwajibu  kuwa mkewe  toka asubuhi na mapema  alitoroka  na watoto.
Kidavashari alieza  kuwa baada ya majibu hayo   wanakijiji wenzake  waliamua kwenda kutoa taarifa kwenye  kituo cha polisi  cha Maji moto kilichopo kijijini hapo
Baada ya kupata taarifa kamanda wa polisi alisema askari Polisi walifika  katika  eneo la tukio kuuangalia mwili wa marehemu Maria  ambao   ulikuwa  na damu ukiwa umelowana   matapishi kukiwa na  alama za kuburuzwa  jirani na mwili wa kichanga hicho
Kamanda Kidavashari  alieleza kuwa askari polisi kwa kushirikiana  na wananchi hao  waliamua kuufuata alama hizo za kuburuzwa hadi   kwenye  nyumba ya ndugu Kawaida  Jonas  ambapo palikuwa na kisima cha maji kilichofunikwa
Alisema kufuatia mazingira yaliyoonekana kisimani hapo Polisi na wanajiji  waliamua kufunua   mfuniko  wa kisima hicho na kukuta  miili ya watoto wawili  wakiwa na mama yao   wakieleea ndani ya kisima hicho huku mama yao akiwa hajafariki bado.
Alisema watoto  tolewa nje  ya kisima  tayari watoto hao walikuwa wamwesha  kufa  huku mama yao hakiwa mahututi  sana   na  ililazimika kumkimbiza   katika kichuo  cha afya  cha  Mamba ambako  amelazwa  huku  akiwa mahututi
Alisema askari polisi walishirikiana na wananchi kumfuata baba wa watoto hao na walipomkuta nyumbani kwake alitaka kukimbia  lakini akadhibitiwa na wananchi waliokuwa wamemzunguka  ambapo alifikishwa kituo cha polisi cha Majimoto.
Kamanda wa polisi wa Mkoa wa Katavi, Dhahiri Kidavashari alisema uchunguzi wa awali  wa mauwaji  ya watoto hao umebaini kuwa mauaji hayo yanatokana  na ugomvi wa  muda mrefu  baina ya wazazi wao  kutokana na  wivu  wa mapenzi
Alisema mtuhumiwa Yustini alikuwa akimshutumu  mkewe kuwa na mausiano ya kimapenzi na  mwaume mwingine jirani yao ingawa alisema kuwa maelezo  zaidi yatapatikana   pale  mama wa  marehemu wa  watoto hao  atakapo  pata fahamu  na kuweza kuongea  ili hatua za kisheria zichukue nafasi yake.
mwisho