JELA MIAKA 30 KWA KUMBAKA KIKONGWE WA MIAKA 90
wacha Mungu wasema tuombe na kufunga
MAHAKAMA ya hakimu mkazi wilaya ya Mpanda mkoani Katavi
imemuhukumu kifungo cha miaka thelathini jela Sindembela Msagi (26) baada ya
kupatikana na hatia ya kumbaka kikongwe mwenye umri wa miaka tisini mwenye
ugonjwa wa kupooza
Hukumu hiyo iliyotolewa Ijumaa Aprili 19, 2013 na hakimu
mfawidhi mkazi wa mahakama hiyo Chiganga Tengwa kufuatia tukio la ubakaji
lilitokea Desemba 22, 2012 katika kijiji cha Bulembo katika makazi ya wakambizi
ya Katumba wilaya ya Mlele
Awali akitoa maelezo mahakamani hapo mwendesha mashitaka wa
jeshi la polisi, Ally Bwijo alisema kuwa mtuhumiwa alifanya kosa hilo Desemba
22, 2012 majira ya usiku baada ya kumuingilia kikongwe huyo ambaye ni mgonjwa
wa kupooza kwa muda mrefu
Aliiambia mahakama kuwa baada ya kumbaka kikongwe huyo
mtuhumiwa aliweza kukimbia lakini baada ya wananchi kumuhoji kikongwe huyo
aliweza kumtambua kwa sura na jina kwani alikuwa anamfahamu kabla ya tukio hilo
la kinyama
Alisema kufuatia maelekezo ya kikongwe aliyefanyiwa unyama
huo wananchi kwa kushirikiana na jeshi la polisi waliweza kumkamata mtuhumiwa
na kumfikisha katika vyombo vya sheria kwa hatua zaidi
Akitoa utetezi wake mahakamani hapo Sindembelea Msagi
aliiambia mahakama kuwa imuonee huruma kwani alifanya kosa hilo kwa mara ya
kwanza na kuwa alishawishiwa na tama ya pesa kutokana na kuwa na anawategemezi wengi wanaohitaji pesa za kuwahudumia
Baada ya kupata maelezo ya pande zote hakimu Chiganga Tengwa
alisema mahakama yake imeridhishwa bila shaka yoyote na ushahidi uliotolewa na
upande wa mashitaka na hivyo mtuhumiwa anastahili adhabu
Chiganga alisema kwa kutumia kifungu sha sheria Namba 154
cha makosa ya ubakaji iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2002 mtuhumiwa atatumikia
kifungo cha miaka thelathini jela ili iwe fundisho kwa wengine wenye tabia ya
ubakaji