Na,Elizabeth Ntambala , Katavi
Watendaji wa halmashauri katika mikoa
ya Rukwa na Katavi wametakiwa kuhakikisha wanakutana na wananchi wa
maeneo yanayohitajika kuchukuliwa kwa ardhi yao kabla ya kuanzisha
miradi ili kuepukana na uwezekano wa kuingia katika migogoro ya ardhi.
Ushauri
umetolewa na wajumbe wa Jumuiya ya serikali za Mitaa (ALAT )katika
mikoa ya Rukwa na Katavi ambao wako mjini Mpanda mkoani Katavi kwaajili
ya kikao chao na kukagua shughuli mbalimbali za maendeleo katika
halmashauri .
Akizungumza mara baada ya kukagua mradi wa jengo la
ofisi ya Afisa Mtendaji wa kata ya Ilembo iliyojengwa kwenye eneo la
Kasimba mjini Mpanda, Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Nkasi Bw.
Kimulika Galikunda amesema miradi mingi ya ya halmashauri imekuwa
ikichelewa kukamilika kutokana na wananchi wa maeneo husika
kutoshirikishwa katika mchakato wake.
Galikunda amesema matokeo
ya kupuuzwa kwa wananchi yamekuwa yakileta madhara kwa wananchi hao
kuiwekea pingamizi miradi hiyo, hali ambayo inachangiwa na baadhi yao
kutolipwa fidia kwa haraka na kuzua malalamiko mengi kwa serikali yao.
Amesema
ipo haya kwa viongozi wa halmashauri kuzingatia mambo hayo ili kuleta
wepesi katika kufanikisha miradi yao huku wananchi pia wakiwaunga mkono
baada ya kuridhika kuwa watendewa haki katika fidia za ardhi yao
iliyochukuliwa.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa ALAT katika mikoa
ya Rukwa na Katavi Bw. Godfrey Sichona amewataka Watendaji wa
halmashauri hizo kuwa makini katika ujenzi wa miradi hiyo ikiwa ni
pamoja na kuzingatia miundo mbinu muhimu inayohitajika katika majengo
yao.
Mwisho.
RUKWA HAWAAMINI HOMA YA NGURUWE
Na Elizabeth Ntambala ,Rukwa
IMEELEZWA KUWA kutokana na ugonjwa wa homa ya nguruwe iliyojitokeza katika baadhi ya mikoa ikiwa pamoja na Rukwa kuwa ni athali kwa matumizi ya binadamu japo wao hawaamini
Akizungumza kwa njia ya simu leo , Ofisa Mifugo na Uvuvi wa Halmashauri ya Sumbawanga , Denis Magala ameleza kuwa tarafa tano zimeshambuliwa vibaya na homa hiyo ya nguruwe ambazo amezitaja kuwa ni pamoja na Laela na Mpui zilizopo wilayani Sumbawanga , Matai , Mwimbi Kasanga mwambao mwa Ziwa Tanganyika wilaya mpya ya Kalambo mkoani Rukwa.
Huku mjini Sumbawanga biashara ya nyama ya nguruwe maarufu kama kitimoto imepigwa marufuku.
Amesema kuwa licha ya homa hiyo ya nguruwe inapomshambulia nguruwe huwa aina tiba wala chanjo hadi sasa isitoshe unasababisha hasara kubwa kwa mfugaji kwani unaenea kwa kasi na kuua nguruwe wote walioshambuliwa na ugonjwa huo.
Aidha kwa upande wa binadamu kudaiwa kuwa licha ya kwamba hausababishi maradha yoyote kiafya lakini wanazuiliwa kula nyama ya nguruwe kwa kuwa nao watasababisha kuueneza ugonjwa huo kutoka eneo moja hadi lingine.
“Ndiyo maana biashara yoyote ya nguruwe na mazao yake ikiwemo nyama , mbolea , manyoya , mifupa , ngozi na vyakula vya kusindikwa imepigwa marufuku ili ikiwa ni jitihada za makusudi za kukabiliana na ugonjwa huo “ alisisitiza.
Kwa mujibu wa Ofisa huyo wa Mifugo na Uvuvi katika tarafa hizo tano zilizokumbwa na mlipuko wa homa hiyo, kuanzia Januari mwaka huu hadi sasa tayari nguruwe 4,884 wamekufa kwamba kabla ya ugonjwa huo, kulikuwa na nguruwe 28,630 na sasa wamebaki 24,449.
Kwa upande wa wafanyabiashara wa nyama hiyo maarufu kama kitimoto wamesema kumekuwepo na ugumu wa maisha kwa upande wao kwani'ilikuwa ikiwapatia kipato kwa kikubwa kwa ajili ya kusaidia kusukuma gurudumu la maisha yao kutokana na watu wengi kupenda kutumia kitoweo hicho.