BREAKING NEWS ......
RAIS KIKWETE AMEKATISHA ZIARA YA KISERIKALI NCHINI KUWAIT
Taarifa ambazo zimeufikia mtandao maarufu wa www.francisgodwin.blogspot.com hivi punde zinadai kuwa Rais Dkt Jakaya Kikwete wa Tanzania amekatisha ziara yake ya kiserikali ya siku mbili nchini Kuwait kufuatia mlipuko wa bomu katika kanisa la Mt Joseph mfanyakazi Arusha ambapo katika tukio hilo watu wawili hadi sasa wanadaiwa kufa baada ya majeruhi mmoja kufariki leo .
RAIS WA BARAZA LA MAASKOFU AWATAKA WAKRISTO NCHINI KUONGEZA KASI YA SALA
=====================================
Na Gustav Chahe, Iringa
RAIS wa Baraza la Maakofu
Tanzania (TEC) Mhashamu askofu Tarcisius Ngalalekumtwa amewataka waamini
wakristo kutokuwa na moyo wa kuhamaki kutokana na kitendo kilipuliwa Kanisa
Katoliki huko Arusha.
Amezungumza hayo katika mahojiano
maalum mtandao huu wa www.sumiampanda.blogspot.com mahojiano yaliyofanyika ofisini kwake Iringa juu ya vitendo vinanyoendelea
kutokea nchini vikiwemo vya kuchomwa makanisa na kuuawa wachungaji wa kiroho
huku vikihusishwa na imani za kidini.
Amesema kama ilivyoutamaduni wa
Kikristo, yanapotukia matukio ya kusikitisha kama hayo silaha iliyo kubwa ni
sala kumuomba Mungu atoe jibu kwa wanaohusika na mateso kama
hayo.
“Kasi ya sala iendelee, ili Mungu
wetu wa Amani ajenge fikira za upendo na haki katika mioyo yetu” alisema.
Amesema waamini wasikate tamaa na
kuacha kusali kwa kuwa Mungu ndiye mwenye jibu na atatoa majibu kadiri atakavyo
kwa wale wote wanaowatesa wenzao kwa sababu zao binafsi.
Hata hivyo alisema licha ya kuwa
kila mtu amepokea kwa mshituko na maumivu makubwa, roho za watu zinazoteswa na
wengine Mungu atazifariji na kuziponya lakini mtesaji atapata majibu yake.
Alisema waliopoteza maisha katika
mlipuko huo Mungu atawarehemu na kuwafariji majeruhi wote.
“Waliopoteza maisha wapokee Rehema
ya Mungu na waliojeruhiwa wafarijiwe na uwezo wa Mungu” alisema.
Hali kadhalika amesema upendo na haki
ni zawadi kutoka kwa Mungu na hivyo, anayedhurumu wengine zawadi hiyo atapata pigo
kubwa.
Aidha amesema wakati uliopo sasa ni
wakutafakari na kumkabidhi Mungu yale yote yanayowasumbua wanadamu na kuongeza nguvu
ya sala ili majibu ya Mungu yapatikane kwao.
“Tulieni na kufanya tafakari kasha
mwambie Mungu hayo yote ayafanyie kazi kwa uweza wake. Sisi binadamu tunategemea
nguvu kutoka kwake” alisema.
TAARIFA
KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amepokea kwa mshtuko na
masikitiko makubwa taarifa ya tukio la leo, Jumapili, Mei 5, 2013 la mlipuko
kwenye Kanisa Katoliki la Mt. Joseph Mfanyakazi la Olasiti Jijini Arusha.
Tukio hilo la kigaidi limesababisha mtu mmoja
kupoteza maisha na wengine 40 kujeruhiwa.
Rais Kikwete analaani vikali shambulio hilo lililofanywa na mtu au watu
katili, waovu na wenye dhamira mbaya na nia mbaya kwa Tanzania na watu
wake.
Rais Kikwete ameagiza
vyombo vya usalama nchini kumsaka mtu au watu waliohusika na kitendo hicho
kiovu na kuwafikisha kwenye vyombo vya sheria.
Vile vile Rais Kikwete amewataka wananchi wote
kuwa watulivu wakati Serikali na vyombo vyake inaendelea kufuatilia tukio
hili. Tutawasaka popote walipo na kupambana
nao bila huruma.
Aidha, tutakabiliana na
aina yoyote ya uhalifu nchini iwe ni ugaidi au aina yoyote ya uhalifu wa namna
hiyo au wa namna nyingine, uwe na chimbuko lake ndani ya nchi ama nje ya nchi
yetu.
Kamwe hatutakubali kuwaacha
wavuruge amani na usalama wa Tanzania na watu wake. Rais anaamini kuwa Serikali,
kwa msaada na ushirikiano wa wananchi, watu hao watapatikana na kuadabishwa
ipasavyo.
Aidha, Rais Kikwete
anatoa rambirambi za dhati ya moyo wake kwa wafiwa na wale wote ambao
wamejeruhiwa katika tukio hilo.
Anaungana nao katika machungu na msiba. Rais pia
anawaombea wote walioumia katika tukio hili wapate nafuu ya haraka na waendelee
na shughuli zao za ujenzi wa taifa.
Rais Kikwete vilevile
anatoa pole nyingi kwa viongozi na waumini wa Kanisa Katoliki kwa tukio hili la
kusikitisha na kuvurugika kwa ibada na shughuli yao muhimu ya uzinduzi wa
Kanisa lao.
Imetolewa na:
Kurugenzi
ya Mawasiliano ya Rais,
IKULU,
DAR ES SALAAM
5 Mei, 2013
KANISA KULIPULIWA ARUSHA ,ASKOFU DKT MDEGELLA ATAKA MAKANISA KULINDWA
Askofu Dkt Mdegella ametoa kauli hiyo leo wakati akizungumza katika mahojiaono maalum na mtandao huu wa www.francisgodwin.blogspot.com kuhusiana na tukio la kulipuliwa kwa kanisa mkoani Arusha.
Kwani alisema alishapata kukutana na vyombo vya habari kufuatia tukio la kuchomwa kwa kanisa Zanzibar na tukio la kuuwawa kwa Paroko kwa risasi huko huko Zanzibar ila ushauri wake alioutoa kwa serikali kuwa hivi sasa nchi inakundi la watu wanaoendesha ugaidi ,na kutaka vyombo vya usalama kusaidia kupambana na kundi hilo.
Kwani amesema kuwa hivi sasa amani ya Taifa inazidi kuwa hatarini zaidi kutokana na watu hao wanaoendesha vitendo vya kigaidi kuingia kwa kasi kubwa kushambulia makanisa na kuwa ni vema vyombo vya ulinzi na usalama kusaidia kulinda nyumba za ibada ili kunusuru njama hizo za kigaidi.
Mbali ya kuvitaka vyombo vya usalama kusaidia kulinda makanisa bado alishauri waumini wa makanisa hapa nchi kuwa makini zaidi na ikiwezekana kuongeza ulinzi zaidi katika makanisa yao hasa siku za ibada .
Askofu Dkt Mdegella alisema kuwa yawezekana ni kundi la watu wanaotumia ugaidi kuhatarisha amani ya Tanzania ila pia yawezekana mambo haya ya machafuko yanafanywa na kundi furani la kisiasa kwa lengo la kuichafua serikali ya CCM iliyopo madarakani kama njia ya kuchinganisha umma kuona kama Rais Jakaya Kikwete na chama chake nchi imemshindwa jambo ambalo halipaswi kuungwa mkono na mtanzania yeyeto kwa watu kuchafua amani ili wapate kuingia Ikulu.
Bila kutaja jina la chama cha siasa kinachofanya hivyo wala mtu anayefadhili vitendo hivyo vya kigaidi askofu Dkt Mdegella aliwataka wana siasa na wananchi kuwa kitu kimoja katika kulinda amani ya Taifa hili.
Pia aliulaumu uongozi wa kanisa Katoliki Arusha kwa kushindwa kuimarisha ulinzi kwa siku ya leo ambapo walitambua wazi wana tukio kubwa na tayari kumekuwepo na vitisho mbali mbali na kuwa iwapo ulinzi ungewekwa eneo hilo yaliyotokea huenda yasingetokea.