watumishi wa mahakama kuu kanda ya Iringa pia wamepata kushiriki
..............................................................................
FRANCIS GODWIN - IRINGA
MBUNGE wa jimbo la Isimani wilayani Iringa mkoani Iringa Bw. Wiliam
Lukuvi amempongeza Rais Jakaya Kikwete kwa kuwawezesha wakazi wa tarafa
ya Isimani kuweza kuanza kushuhudia mapinduzi makubwa ya kimaendeleo kupitia
mradi mkubwa wa barabara ya kiwango cha lami kutoka Iringa - Dodoma
inayopita katika tarafa hiyo .
Lukuvi ambae ni waziri wa nchi ofisi ya waziri mkuu (sera na
uratibu wa bunge) alisema kuwa barabara hiyo ambayo ni ukombozi mkubwa kwa
nchi za kusini mwa Tanzania ilikuwemo katika mkakati wa kujengwa kwa
kiwango cha lami kwa kitambo kirefu na kila awamu wananchi walikuwa
wakiulizana juu ya kuanza kwa mradi huo.
Hata hivyo alisema baada ya awamu hii ya nne chini ya Rais Kikwete
wananchi hao wameweza kushuhudia majibu ya maswali yao kwa kuanza kwa
ujenzi huo ambao kila mmoja anatambua kama ni ukombozi katika sekta ya
maendeleo.
Waziri Lukuvi alitoa pongezi hizo kwa Rais Kikwete leo wakati
akiwasalimia wananchi wa jimbo la Isimani ambao walishiriki hafla fupi ya
Rais Kikwete kuweka jiwe
Kwa upande wake Rais Jakaya Kikwete
alisema kuwa mbali ya serikali kujipanga kwa ujenzi wa barabara
bado lengo la serikali ni kuhakikisha nchi nzima inaunganishwa kwa
mtandao wa barabara ya lami na kuwa kazi hiyo tayari imeanza.
Alisema kuwa serikali yake toka
imeingia madarakani imeendelea kuongeza fedha katika mfuko wa
barabara na kuwa lengo ni kuendelea kuongeza zaidi fedha katika
mfuko huo ili kuwezesha ujenzi wa barabara nchini kuweza
kukamilika
Rais Kikwete pia amewapongeza
viongozi wa TANROADS kwa kazi nzuri wanayoendelea kuifanya na kwa
mbali ya kupongezwa bado hawapaswi kulewa sifa na badala yake
kuendeleza jitihada za kusimamia kazi hiyo kwani upo usemi unao sema
kuwa mgema akisifiwa pombe huweka maji .
SEHEMU YA BARABARA YA IRINGA - DODOMA ITAGHARIMU BILIONI 222
Hapa ni eneo la simani wilaya ya Iringa vijijini ujenzi uliendelea na hii ni kazi nzuri a Tanroads mkoa wa Iringa katika usimamizi barabara hii itakayofungua fursa kwa mikoa ya kusini itagharimu zaidi ya Tsh bilioni 222 na leo majira ya saa 3 asubuhi imewekwa jiwe la msingi na Rais Jakaya Kikwete
WAKULIMA SUMBAWANGA WAPEWA SOMO .............
Wakulima wa zao la mahindi mkoani Rukwa wakipata elimu ya shamba darasa (picha na maktaba yetu)
...................................................................................
Na Elizabeth
NtambalaSumbawanga
WAKAZI wa wametakiwa kulima kilimo cha kisasa na kufuata ushauri wa wataalamu wa kilimo ili waweze kuvuna mazao mengi zaidi ambayo yatawasaidia kupata chakula cha ziada ambacho kitawafaa wao na kuwasaidia mikoa ya jirani.
Wito huo umetolewa jana nakamati ya ulinzi na usalama ya wilaya ilipokuwa ikizungumza na wananchi wakati waliokusanyika katika vijiji vya kaengesa ,miangalua na lusaka .
Moja ya mikoa inayotegemewa kwa uzalishaji chakula hapa nchini hivyo basi kama wakulima watalima kilimo cha kisasa wataweza kuzalisha chakula kingi na kupata ziada ya kutosha na hivyo kuisaidia mikoa mingine yenye upungufu wa chakula.
Pia kamati hiyo iliyokuwa ikiongozwa na mkuu wa wilaya methwes sedoyeka aliwataka wazazi wa Mkoa huo kusimamia elimu ya watoto wao kwa kuhakikisha kuwa watoto wanaenda shule na kukagua madaftari yao ili pale walipokosea waweze kuwarekebisha.
Kwa upande wa wanafunzi aliwataka kusoma kwa bidii na kufanya vizuri katika masomo yao hadi kufika elimu ya juu kwa kufanya hivyo itawawezesha kushika nafasi za juu za uongozi siku za mbeleni.
“Mkisoma kwa bidii, maarifa na kujituma hakika mtafika mbali, sisi hapa tuliopo mbele yenu ni viongozi jitahidini hizi nafasi mje kuzishika ninyi miaka ijayo ili muongoze kuongoza na ninaamini kati yenu kuna viongozi wazuri”,