Wednesday, May 22, 2013

IRINGA WAMPONGEZA JK KWA KUJALI MIUNDOMBINU YA BARABARA

Rais Jakaya  Kikwete (kushoto) akiteta  jambo na mbunge wa  jimbo la Isimani Wiliam Lukuvi  leo


 watumishi  wa mahakama kuu kanda ya  Iringa  pia wamepata  kushiriki
.............................................................................. 

FRANCIS GODWIN - IRINGA
MBUNGE  wa  jimbo la Isimani wilayani  Iringa mkoani Iringa  Bw. Wiliam Lukuvi amempongeza  Rais Jakaya  Kikwete  kwa  kuwawezesha  wakazi  wa tarafa  ya Isimani kuweza  kuanza  kushuhudia mapinduzi makubwa ya  kimaendeleo kupitia mradi mkubwa  wa barabara  ya  kiwango  cha lami kutoka Iringa - Dodoma  inayopita katika   tarafa  hiyo .
 
Lukuvi  ambae ni  waziri  wa nchi  ofisi  ya  waziri  mkuu (sera na uratibu  wa  bunge) alisema  kuwa  barabara  hiyo ambayo ni ukombozi mkubwa kwa nchi  za  kusini mwa  Tanzania  ilikuwemo katika mkakati  wa kujengwa kwa kiwango  cha lami kwa kitambo  kirefu na  kila awamu  wananchi  walikuwa  wakiulizana  juu ya kuanza  kwa mradi huo.
 
Hata  hivyo  alisema  baada ya awamu  hii ya nne  chini ya  Rais Kikwete  wananchi hao  wameweza kushuhudia  majibu ya maswali yao  kwa  kuanza  kwa ujenzi huo ambao  kila mmoja anatambua  kama ni ukombozi katika  sekta ya maendeleo.
 
Waziri  Lukuvi alitoa  pongezi  hizo kwa Rais Kikwete  leo wakati akiwasalimia  wananchi  wa  jimbo  la Isimani ambao  walishiriki hafla  fupi ya Rais Kikwete  kuweka jiwe 
 
Kwa  upande  wake  Rais Jakaya  Kikwete  alisema  kuwa  mbali ya  serikali  kujipanga kwa  ujenzi  wa barabara bado lengo la  serikali ni  kuhakikisha nchi  nzima inaunganishwa kwa mtandao  wa barabara  ya lami na kuwa kazi hiyo tayari  imeanza.
 
Alisema  kuwa serikali  yake  toka  imeingia madarakani  imeendelea  kuongeza  fedha  katika mfuko  wa barabara  na kuwa lengo ni kuendelea  kuongeza  zaidi fedha katika mfuko  huo ili  kuwezesha  ujenzi  wa barabara nchini kuweza  kukamilika 
 
 Rais  Kikwete  pia amewapongeza  viongozi wa TANROADS kwa kazi nzuri  wanayoendelea  kuifanya na kwa  mbali ya kupongezwa bado hawapaswi kulewa  sifa na badala  yake  kuendeleza  jitihada za  kusimamia  kazi  hiyo kwani upo usemi unao sema kuwa mgema akisifiwa pombe huweka maji .
 
Pia  Rais Kikwete alimpompongeza  waziri wa fedha Dkt Wiliam Mgimwa kwa kuendelea  kuidhinisha  fedha kwa ajili ya miradi ya barabara hapa nchini na kuwa  bila  wizara  hiyo  kutenga bajeti  kazi hiyo ingeendelea  kuwa ngumu

SEHEMU YA BARABARA YA IRINGA - DODOMA  ITAGHARIMU BILIONI 222


Hapa  ni eneo la simani  wilaya ya Iringa vijijini  ujenzi  uliendelea na hii ni kazi nzuri a  Tanroads mkoa  wa Iringa katika  usimamizi barabara hii itakayofungua  fursa  kwa  mikoa ya  kusini itagharimu zaidi ya Tsh bilioni 222 na  leo majira ya saa 3 asubuhi  imewekwa jiwe la msingi na Rais Jakaya  Kikwete 

WAKULIMA SUMBAWANGA WAPEWA SOMO .............

Wakulima  wa zao la mahindi mkoani Rukwa  wakipata  elimu ya shamba  darasa (picha na maktaba yetu)
...................................................................................
Na Elizabeth Ntambala
Sumbawanga
WAKAZI wa wametakiwa kulima kilimo cha kisasa na kufuata ushauri wa wataalamu wa kilimo ili waweze kuvuna mazao mengi zaidi ambayo yatawasaidia kupata chakula cha ziada ambacho kitawafaa wao na kuwasaidia mikoa ya jirani.

Wito huo umetolewa jana nakamati ya ulinzi na usalama ya wilaya ilipokuwa ikizungumza na wananchi wakati waliokusanyika katika vijiji vya kaengesa ,miangalua na lusaka .

Moja ya mikoa inayotegemewa kwa uzalishaji chakula hapa nchini hivyo basi kama wakulima watalima kilimo cha kisasa wataweza kuzalisha chakula kingi na kupata ziada ya kutosha na hivyo kuisaidia mikoa mingine yenye upungufu wa chakula.

Pia kamati hiyo iliyokuwa ikiongozwa na mkuu wa wilaya methwes sedoyeka aliwataka wazazi wa Mkoa huo kusimamia elimu ya watoto wao kwa kuhakikisha kuwa watoto wanaenda shule na kukagua madaftari yao ili pale walipokosea waweze kuwarekebisha.

Kwa upande wa wanafunzi aliwataka kusoma kwa bidii na kufanya vizuri katika masomo yao hadi kufika elimu ya juu kwa kufanya hivyo itawawezesha kushika nafasi za juu za uongozi siku za mbeleni.

“Mkisoma kwa bidii, maarifa na kujituma hakika mtafika mbali, sisi hapa tuliopo mbele yenu ni viongozi jitahidini hizi nafasi mje kuzishika ninyi miaka ijayo ili muongoze kuongoza na ninaamini kati yenu kuna viongozi wazuri”,