MATAPELI WA NDUMBA MBARONI
Na Geofrey Chaka, Katavi
JESHI la polisi mkoani Katavi
linawashikilia watu wanne kwa tuhuma za utapeli wa kutumia dawa za kienyeji
Kwa mujibu wa taarifa ya Kamanda wa jeshi
la polisi mkoani Katavi, Dhahir Kidavashari wanaoshikiliwa na jeshi hilo ni Charles
Mwelela (38),mkulima mkazi wa Edeni katika Manispa ya Sumbawanga Mkoa wa Rukwa,
Issa Hasan maarufu kwa jina la Senga
(42), mklima mkazi wa Kona ya Bwiru jijini Mwanza, Hussein Hassan, (38), mkulima mkazi wa jijini
Mwanza na Magreth Bakari,(45), mkulima mkazi wa Nsemulwa mjini Mpanda
Akitoa
taarifa kwa wananhabari ofisini kwake jana Kamanda Kidavashari alisema kuwa tukio hilo
lilitokea tarehe Agosti 26, 2013 majira ya saa tano usku katika mtaa wa mji
Mwema katika nyumba ya kulala wageni ya Vatcan iliyopo kata ya Kashaulili,
Wilaya ya Mpanda, Mkoa wa Katavi ambapo watuhumiwa hao walikamatwa kwa tuhuma
za kujifanya waganga wa jadi kwa kuwatapeli wananchi mbalimbali mjini hapo.
Alisema watu hao walikutwa na vifaa vinavyoashiria
kuwa wao ni waganga wa jadi pamoja na pasi ya kijerumani feki ambayo huitumia
katika shughuli za kuwatapeli wananchi baada ya kuwahadaa kuwa watapata dawa za
kienyeji za kuwasaidia katika matatizo waliyonayo licha ya kuwa siyo kweli na
wala watuhumiwa hao hawana vyeti vya kuonesha kuwa ni waganga wa jadi.
Kamanda wa polisi Mkoa wa Katavi alisema
kuwa, Agosti 26, 2013 saa tano usiku jeshi la polisi lilipata taarifa toka kwa
raia wema kwamba katika nyumba ya kulala
wageni ya VATCAN iliyoko mji mwema mjini Mpanda kuna watu katika chumba namba 8
na namba 11 wanajifanya waganga wa jadi
na kutoa tiba ya asili pasipo na kibali cha kazi hiyo.
Kamanda alisema kuwa uchunguzi wa
awali umebaini kuwa watu hao ni matapeli na huwatapeli watu kwa mtindo wa
kuwapa madawa ya kienyeji kwa lengo la kuwalevya na muda mwingine huwatapeli
watu kwa kuwadanganya watu kuwa wanapasi
ambayo wakipewa huwa na mvuto wa pesa daima na hivyo kuwataka watu hao kutoa
pesa ili wapewe pasi hiyo bila wao kujua kuwa wanatapeliwa.
Kamanda wa polisi alisema kwamba tukio
hilo lilikuwa likifanikishwa na watu hao kwa kumtumia mwanamke aitwaye MAGRETH
BAKARI kwa kuwatafuta wateje sehemu mbalimbali za mji na kuwapeleka katika
nyumba hiyo ya kulala wageni na kuwatapeli kwa mtindo huo, kwani mwanamke huaminika
kuwa hawezi kuwatapeli kwa vile ni mwanamke.
Kamanda wa polisi mkoa wa Katavi ametoa rai kwa wananchi kwamba wananchi
wawe makini na waangalifu sana wanapokuta na watu kama hao,na kutoa taarifa
kama kuna shaka na watu kama hao katika kituo cha polisi kilichopo karibu.
MKE WA MTU SUMU
WIVU wa mapenzi umepoteza maisha ya ndugu Juma Moshi mkazi wa kijiji
cha Kamsanga kata ya Kabungu wilaya ya Mpanda mkoani Katavi baada ya kupigwa na
kufariki dunia kwa fimbo katika sehemu za mwili na watu wasiofahamika
Tukio hilo lilitokea Agosti 16, 2013 majira ya saa
nane mchana katika kijiji anachoishi marehemu ambapo marehemu Juma Moshi (30)
alikamatwa na watu wasiofahamika alipokuwa katika kilabu cha pombe za kienyeji
kilichopo kijijini hapo wakimtuhumu kuwa anatembea na mke wa mtu aliyefahamika
kwa jina la Peter Makenzi
Taarifa toka eneo la tukio na
kuthibitishwa na jeshi la polisi zilidai kuwa marehemu baada ya kukamatwa na
watu hao walimuhoji maswali kuhusiana na tuhuma hizo ambapo iansemekana
marehemu alikiri na mbele yao
na kuanza kumuadhibu marehemu kwa kumchapa
viboko kuanza saa tano asubuhi hadi saa nane mchana marehemu aliweza
kupoteza maisha akila kichapo
Kamanda wa jeshi la polisi mkoa
wa Katavi, Dhahir Kidavashari alisema uchunguzi wa awali umebaini chanzo cha
mgogoro huu uliopelekea mauaji umetokana na wivu wa kimapenzi kati ya marehemu
dhidi ya Peter Makenzi ambaye inasemekana ni mume wa mwanamke aliyesemekana kutembea
na marehemu
Alisema baada ya kutokea mauaji
hayo ndugu Peter Makenzi aliweza kutoweka hajulikani aliko ambapo jeshi la
polisi linaendelea na juhudi za kumtafuta ili aweze kupatikana na kufikishwa
kwenye mahakamani kujibu tuhuma za kupanga mauaji hayo pamoja na kuwasaka
aliowapa ujira wa kufanya mauaji ya marehemu kwa tuhuma za kutembea na mke wake
Katika tukio lingine Sele Njija
mwanamke mwenye umri wa miaka 60 aliuwawa kwa kukatwa katwa kichwani na kitu
kinachosadikiwa kuwa ni shoka na watu wasiofahamika Agosti 14, 2013 majira ya
saa moja jioni katika kitongoji cha Mboge-Kalila kata ya Kabungu wilaya ya Mpanda
mkoani Katavi
Kamanda wa polisi mkoani Katavi,
Dhahir Kidavashari alisema jana ofisini kwake alisema katika tukio hilo watu watatu
wasiofahamika walifika nyumbani kwa marehemu na kumkuta akiwa na mwanae
aliyetajwa kwa jina la Ng’walu Lukulaga na kuomba maji ya kunywa ndipo motto huyo
alipoinuka na kwenda ndani kuwachukulia maji ya kunywa
Alisema motto huyo akiwa ndani
kuchota maji mtungini watu hao walimvamia mama yake na kumkatakata kwa shoka
kichwani hadi kufariki dunia papo hapo kisha watu hao wakatokomea
kusikojulikana
Alisema uchunguzi wa awali
umebaini kuwa chanzo cha mauaji hayo ni migogoro ya kifamilia na kiukoo kwani
takribani miaka miwili iliyopita mume wa marehemu aliuwawa kwa kukatwa katwa
kwa mapanga na watu wasiojulikana katika kijiji cha Kasisi eneo la Mpanda ndogo
Alisema hakuna mtu yeyote
aliyekamatwa kwa tuhuma za mauaji hayo ambapo kamanda huyo aliwasihi wananchi
kuacha kujichukulia sheria mkononi badala yake watoe taarifa katika vyombo vya
dola ili hatua ziweze kuchukuliwa kwa kufuata utaratibu wa kisheria.