Tuesday, August 20, 2013

POLISI KATAVI INFO

MATAPELI WA NDUMBA MBARONI




 

Na Geofrey Chaka, Katavi
JESHI la polisi mkoani Katavi linawashikilia watu wanne kwa tuhuma za utapeli wa kutumia dawa za kienyeji

    Kwa mujibu wa taarifa ya Kamanda wa jeshi la polisi mkoani Katavi, Dhahir Kidavashari wanaoshikiliwa na jeshi hilo ni Charles Mwelela (38),mkulima mkazi wa Edeni katika Manispa ya Sumbawanga Mkoa wa Rukwa, Issa Hasan maarufu kwa jina la  Senga (42), mklima mkazi wa Kona ya Bwiru jijini Mwanza,  Hussein Hassan, (38), mkulima mkazi wa jijini Mwanza na Magreth Bakari,(45), mkulima mkazi wa Nsemulwa mjini Mpanda

  Akitoa taarifa kwa wananhabari ofisini kwake jana  Kamanda Kidavashari alisema kuwa tukio hilo lilitokea tarehe Agosti 26, 2013 majira ya saa tano usku katika mtaa wa mji Mwema katika nyumba ya kulala wageni ya Vatcan iliyopo kata ya Kashaulili, Wilaya ya Mpanda, Mkoa wa Katavi ambapo watuhumiwa hao walikamatwa kwa tuhuma za kujifanya waganga wa jadi kwa kuwatapeli wananchi mbalimbali mjini hapo.

      Alisema  watu hao walikutwa na vifaa vinavyoashiria kuwa wao ni waganga wa jadi pamoja na pasi ya kijerumani feki ambayo huitumia katika shughuli za kuwatapeli wananchi baada ya kuwahadaa kuwa watapata dawa za kienyeji za kuwasaidia katika matatizo waliyonayo licha ya kuwa siyo kweli na wala watuhumiwa hao hawana vyeti vya kuonesha kuwa ni waganga wa jadi.

       Kamanda wa polisi Mkoa wa Katavi alisema kuwa, Agosti 26, 2013 saa tano usiku jeshi la polisi lilipata taarifa toka kwa raia wema kwamba katika nyumba ya  kulala wageni ya VATCAN iliyoko mji mwema mjini Mpanda kuna watu katika chumba namba 8 na namba 11  wanajifanya waganga wa jadi na kutoa tiba ya asili pasipo na kibali cha kazi hiyo.

       Kamanda  alisema kuwa uchunguzi wa awali umebaini kuwa watu hao ni matapeli na huwatapeli watu kwa mtindo wa kuwapa madawa ya kienyeji kwa lengo la kuwalevya na muda mwingine huwatapeli watu kwa kuwadanganya watu kuwa  wanapasi ambayo wakipewa huwa na mvuto wa pesa daima na hivyo kuwataka watu hao kutoa pesa ili wapewe pasi hiyo bila wao kujua kuwa  wanatapeliwa.

      Kamanda wa polisi alisema kwamba tukio hilo lilikuwa likifanikishwa na watu hao kwa kumtumia mwanamke aitwaye MAGRETH BAKARI kwa kuwatafuta wateje sehemu mbalimbali za mji na kuwapeleka katika nyumba hiyo ya kulala wageni na kuwatapeli kwa mtindo huo, kwani mwanamke huaminika kuwa hawezi kuwatapeli kwa vile ni mwanamke.

   Kamanda wa polisi mkoa wa Katavi ametoa rai kwa wananchi kwamba wananchi wawe makini na waangalifu sana wanapokuta na watu kama hao,na kutoa taarifa kama kuna shaka na watu kama hao katika kituo cha polisi kilichopo karibu.

MKE WA MTU SUMU

WIVU wa mapenzi umepoteza maisha ya ndugu Juma Moshi mkazi wa kijiji cha Kamsanga kata ya Kabungu wilaya ya Mpanda mkoani Katavi baada ya kupigwa na kufariki dunia kwa fimbo katika sehemu za mwili na watu wasiofahamika

Tukio hilo lilitokea Agosti 16, 2013 majira ya saa nane mchana katika kijiji anachoishi marehemu ambapo marehemu Juma Moshi (30) alikamatwa na watu wasiofahamika alipokuwa katika kilabu cha pombe za kienyeji kilichopo kijijini hapo wakimtuhumu kuwa anatembea na mke wa mtu aliyefahamika kwa jina la Peter Makenzi

Taarifa toka eneo la tukio na kuthibitishwa na jeshi la polisi zilidai kuwa marehemu baada ya kukamatwa na watu hao walimuhoji maswali kuhusiana na tuhuma hizo ambapo iansemekana marehemu alikiri na mbele yao na kuanza kumuadhibu marehemu kwa kumchapa  viboko kuanza saa tano asubuhi hadi saa nane mchana marehemu aliweza kupoteza maisha akila kichapo

Kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Katavi, Dhahir Kidavashari alisema uchunguzi wa awali umebaini chanzo cha mgogoro huu uliopelekea mauaji umetokana na wivu wa kimapenzi kati ya marehemu dhidi ya Peter Makenzi ambaye inasemekana ni mume wa mwanamke aliyesemekana kutembea na marehemu

Alisema baada ya kutokea mauaji hayo ndugu Peter Makenzi aliweza kutoweka hajulikani aliko ambapo jeshi la polisi linaendelea na juhudi za kumtafuta ili aweze kupatikana na kufikishwa kwenye mahakamani kujibu tuhuma za kupanga mauaji hayo pamoja na kuwasaka aliowapa ujira wa kufanya mauaji ya marehemu kwa tuhuma za kutembea na mke wake

Katika tukio lingine Sele Njija mwanamke mwenye umri wa miaka 60 aliuwawa kwa kukatwa katwa kichwani na kitu kinachosadikiwa kuwa ni shoka na watu wasiofahamika Agosti 14, 2013 majira ya saa moja jioni katika kitongoji cha Mboge-Kalila kata ya Kabungu wilaya ya Mpanda mkoani Katavi

Kamanda wa polisi mkoani Katavi, Dhahir Kidavashari alisema jana ofisini kwake alisema katika tukio hilo watu watatu wasiofahamika walifika nyumbani kwa marehemu na kumkuta akiwa na mwanae aliyetajwa kwa jina la Ng’walu Lukulaga na kuomba maji ya kunywa ndipo motto huyo alipoinuka na kwenda ndani kuwachukulia maji ya kunywa

Alisema motto huyo akiwa ndani kuchota maji mtungini watu hao walimvamia mama yake na kumkatakata kwa shoka kichwani hadi kufariki dunia papo hapo kisha watu hao wakatokomea kusikojulikana

Alisema uchunguzi wa awali umebaini kuwa chanzo cha mauaji hayo ni migogoro ya kifamilia na kiukoo kwani takribani miaka miwili iliyopita mume wa marehemu aliuwawa kwa kukatwa katwa kwa mapanga na watu wasiojulikana katika kijiji cha Kasisi eneo la Mpanda ndogo

Alisema hakuna mtu yeyote aliyekamatwa kwa tuhuma za mauaji hayo ambapo kamanda huyo aliwasihi wananchi kuacha kujichukulia sheria mkononi badala yake watoe taarifa katika vyombo vya dola ili hatua ziweze kuchukuliwa kwa kufuata utaratibu wa kisheria.