CHOO CHA KISAA CHA WANAFUNZI KATIKA SHULE YA MSINGI MTAMAA MANISPAA YA SINGIDA |
MWL QUEEN MLOZI AKIJIVINJARI KATIKA VYOO VYA KISASA VYA WANAFUNZI, MWL QUEEN NDIYE MKUU WA WILAYAYA SINGIDA |
ELIMU ya usafi wa mikono hadi vyooni, mambo ya vyoo vya kisasa |
JIWE LA MSINGI UJENZI WA VYOO VYA KISASA KATIKA SHULE YA MSINGI MTAMAA |
BIDHAA ZA WAJASILIAMALI KATIKA UWANJA WA MKESHA WA MWENGE MANISPAA YA SINGIDA |
KUKU WANAUZWA BEI NAFUU |
MSHAURI WA MGAMBO WILAYA YA SINGIDA AKITOA MAELEZO YA KIKUNDI CHAKE CHA WAJASILIAMALI WALIFUZU MGAMBO KWA MKUU WA WILAYA HIYO QUEEN MLOZI |
PONGEZI kwa kuachana na mihadarati kijana wangu DC Queen Mlozi wa wilaya ya Singida |
Sitaki tena mirungnataka kusoma tu - Yusupu Saimon Shumbi akielezea ndotoyake ya kusoma mpaka basi |
WANAFUNZI MSIJIINGIZE KWA WAKUBWA SOMENI
Wananfunzi wametakiwa kuweka juhudi katika masomobadala ya kujiingiza katika mambo mengine yasiyowafaa katika umri waliokuwa naohayo yalibainishwa na kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka 2013, Juma Ali Simai katika viwanja vya kituo kipya cha mabasi mjini Singida katika Manispaa ya Singida mkoani Singida alipokuwa akiwaaga wakazi wa Manispaa hiyo waliojitokeza katika mkesha wa Mwenge Agosti 12, 2013.
Alisema hivi sasa wanafunzi wengi wasahau jukumu lao kubwa na kujiingiza katika mambo yasiyowafaa na kupoteza mwelekeo wa kimaisha na kuwaachia wazazi majanga na sononeko kubwa kwani mzazi anapokuwa na mtoto anategemea kuwa mtoto huyo atafikia umri wa kujitegemea kwa kuwa shughuli yake ya kufanya na hata baadae kumsaidia
Aliwataka kuachana na ugomvi baina yao na walimu, jamii, na hata wao kwa wao na badala yake aliwaasa kuwa na ushirikiano wa kimasomo baina yao ili waweze kusaidiana mbinu, uwezo na maarifa kwa kutumia mbinu ya majadiliano na mazoezi ili kujiweka katika mazingira mazuri hata kama walimu watakuwa hawatoshi mashuleni kwao
Alisema muda wa kufanya mambo mengine ukifika hayo mambo yatawafuata yenyewe tena bila kugomabana na wazazi au jamii lakini wakati wa masomo wazingatie sana masomo na kuepuka mambo ya wakubwa yanayowaletea matatizo katika jamii, kwa wazazi na hata kwa serikali ndiyo maana mambo hayo yanelezwa katika sheria za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni kosa kisheria kwa mwanafunzi kuyashiriki
Alisema serikali na wazazi wanatumia gharama kubwa kuwekeza katika elimu ili watoto wao wapate elimu ambayo ni ufunguo wa maisha lakini badala yake watoto wanapofikia muda wa kusoma wanashindwa kutumia fursa zilizopo mashuleni kujiendeleza kitaaluma na badala yake wanakimbilia mambo yasiyowafaa
"Wanafunzi mnapopewa nafasi ndogo sana ya kuwa na kompyuta mnakimbilia kujifunza mambo yasiyofaa badala ya kuitumia kujifunza maarifa ya kitaaluma, hilo linawaingiza katika matatizo makubwa ya nayosababisha kupata maradhi mbali mbali ukiwemo ukimwi" Alisema Simai