MECHI YA YANGA, AZAM YAINGIZA MIL 240/- FEB 22, 2013
Kocha wa Yanga
Kikosi cha Azamu
Mechi
namba 120 ya Ligi Kuu ya Vodacom iliyochezwa jana (Februari 23 mwaka
huu) kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na kumalizika kwa Yanga
kuibuka ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Azam imeingiza sh. 239,686,000.
Watazamaji
39,315 walikata tiketi kushuhudia mechi hiyo ambayo viingilio vilikuwa
sh. 5,000, sh. 8,000, sh. 15,000 na sh. 20,000 huku kila klabu ikipata
mgawo wa sh. 58,794,927.45 wakati Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT)
iliyolipwa ni sh. 36,562,271.19.
Kiingilio
cha sh. 5,000 ndicho kilichovutia watazamaji wengi ambapo waliokata
tiketi hizo walikuwa 33,315 na kuingiza sh. 165,655,000 wakati idadi
ndogo ya washabiki ilikuwa ya kiingilio cha sh. 20,000 kilichovutia
washabiki 485 na kuingiza sh. 9,700,000.
Mgawo
mwingine wa mapato hayo ni asilimia 15 ya uwanja sh. 29,895,725.82,
tiketi sh. 3,183,890, gharama za mechi sh. 17,937,435.49, Kamati ya Ligi
sh. 17,937,435.49, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh.
8,968,717.75 na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA)
sh. 6,975,669.36.
Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
KLABU YA SIMBA YATAJA KAMATI YA UFUNDI
Hawa ndiyo wajumbe wapya wa kamati za Simba.
KAMATI YA UFUNDI
- DAMIAN MANEMBE-MWENYEKITI
- IBRAHIM MASOUD-MAKAMU MWENYEKITI
- CRESCENCIUS MAGORI
- KHALID ABEID
- SAID TULLY
- DR. KATEGILE
- ZAMOYONI MOGELA
- JOHN WILLIAM (DEL PIERO)
- YUSUFU MACHO
- JEFF LEA
- BITA JOHN
- SHABAAN BARAZA
KAMATI YA FEDHA
- GEOFREY IRICK NYANGE (MWENYEKITI)
- RAHMA AL KHALOOS-MAKAMU MWENYEKITI
- FRANCIS WAYA
- ZITTO KABWE
- JUMA NKAMIA
- RUGE MUTAHABA
KAMATI YA MASHINDANO
- SWEDY MKWABI-MWENYEKITI
- SAID PAMBA-MAKAMU MWENYEKITI
- SELEMANI ZEDDY. (MB)
- JERRY YAMBI
- IDDI KAJUNA
- CHAUREMBO
- GERLAD LUKUMAY
- HABBIB NASSA
- BUNDALA KABULWA
- CHARLES HAMKAH
- SAID RUBEYA
- ABDULFATAH SALUM (SAPHIRE)
- HATIBU MWINYI (BUSTA)
- ABDUL MSHANGAMA
- HUMPHREY ZEBEDAYO
- MAJALIWA MBASSA
- SULEIMAN ZAKAZAKA
- KESI MOHAMED RASHID
- MOHAMED ISSA MBENA
KAMATI YA PROGRAMU ZA VIJANA
- IBARHIM MASOUD –MWENYEKITI
- RUGE MUTAHABA-MAKAMU MWENYEKITI
- JOSEPH ITANG’ARE-MJUMBE/MLEZI
- WILFRED KIDAU
- MOHAMED ABDALLAH
- SAID TULLY
- CANISIUS MASOMBOLA
- HAMIS MRISHO
- DAMAS NDUMBARO
- TALIB HILAL
Imetolewa na,
Ezekiel Kamwaga
Ofisa Habari
Simba SCMZUNGUKO WA PILI VPL JUMAMOSI FEB 2, 2013, DARAJA LA KWANZA TANZANIA
Wakati
mzunguko wa pili wa Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kuwania ubingwa wa
Tanzania Bara unaanza Jumamosi (Januari 22 mwaka huu), mzunguko wa pili
wa Ligi Daraja la Kwanza (FDL) umesogezwa mbele kwa wiki moja ambapo
sasa utaanza Februari 2 mwaka huu.
Uamuzi
wa VPL kuendelea Januari 26 mwaka huu ulifikiwa katika kikao cha Kamati
ya Ligi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) na klabu za ligi
hiyo kilichofanyika jana (Januari 21 mwaka huu) jijini Dar es Salaam.
Hata
hivyo, uamuzi huo umefikiwa huku yakiwepo masharti kadhaa kutokana na
uamuzi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kukamata sh. milioni 157
kwenye akaunti za TFF, fedha ambazo zilitoka kwa mdhamini wa VPL
(Kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom) kwa ajili ya timu zinazoshiriki
ligi hiyo.
Masharti
hayo yatawasilishwa na Kamati ya Ligi kwa maandishi kwa Katibu Mkuu wa
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), nakala kwa Waziri wa
Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo. Awali klabu kupitia Kamati ya Ligi
zilisisitiza zisingecheza ligi hadi fedha hizo zitakaporejeshwa.
Kwa
upande wa FDL itaanza bila timu ya Small Kids ya Rukwa ambayo
imeshushwa daraja kwa mujibu wa kanuni baada ya kushindwa kucheza mechi
mbili katika mzunguko wa kwanza.
Kwa mujibu wa kanuni za ligi hiyo, matokeo yote ya mechi ambazo Small Kids ilicheza katika mzunguko huo wa kwanza yamefutwa. (Ratiba ya VPL imeambatanishwa).
OCHIENG, AKUFFO WAFIKIA MUAFAKA SIMBA
Kamati
ya Sheria, Maadili na Hadhi za Wachezaji iliyokutana Januari 19 mwaka
huu chini ya Mwenyekiti wake Alex Mgongolwa imeliondoa shauri lililokuwa
mbele yake dhidi ya klabu ya Simba lililowasilishwa na wachezaji Pascal
Ochieng na Daniel Akuffo baada ya pande hizo kufikia makubaliano.
Wachezaji
hao kutoka Kenya na Uganda waliwasilisha malalamiko mbele ya kamati
wakipinga kukatizwa mikataba yao bila kulipwa stahili zao. Hata hivyo,
pande zimefikia makubaliano ya kuvunja mikataba nje ya kamati, na
wachezaji hao kulipwa stahili zao.
Pia
Simba imekiri kudaiwa na wachezaji Shija Mkina, Swalehe Kabali, Victor
Costa na Rajab Isiaka na kuahidi kuwalipa wachezaji hao wakati Coastal
Union na mchezaji wake Mohamed Issa wamefikia makubaliano ya malipo,
hivyo kuvunja mkataba kati ya pande hizo mbili.
SHABANI KADO AIDHINISHWA COASTAL UNION
Kamati
ya Sheria, Maadili na Hadhi za Wachezaji ilikutana Januari 19 mwaka huu
kupitia maombi ya usajili wa dirisha dogo kwa klabu za Ligi Kuu ya
Vodacom (VPL) na Ligi Daraja la Kwanza (FDL) ambapo kipa Shabani Kado
ameidhinishwa kuidakia timu ya Coastal Union ya Tanga.
Wachezaji
wengine waliodhinishwa kwenye dirisha dogo na klabu zao kwenye mabano
ni Humphrey Mieno, Brian Umony, Jockins Atudo, David Mwantika, Abdallah
Seif, Malika Ndeule na Uhuru Selemani- kwa mkopo (Azam), Juma Mdindi,
Njaidi Mohamed na Mahmoud Mbulu (Ruvu Shooting), Mohamed kayi na
Emmanuel Gabriel (Tanzania Prisons).
Nurdin
Selemani, Shaibu Nayopa, Hamidu Hassan, Paul Malipesa, Josephat Moses,
Muharami Mnyangamala, Majaliwa Mbaga na Alphonce Peter (Oljoro JKT),
Shukuru Kassim, Chacha Marwa, Salum Machaku, Mzamiru Said, Victor
Bundala, Delta Thomas, Edward Mzeru na Tizzo Chomba (Polisi Morogoro),
Edmund Kashamila na Julius Mrope (Kagera Sugar).
Rajab
Mohamed, Zakayo Joseph, Baraka Anthony na Mussa Chambo (Mtibwa Sugar),
Zahoro Pazi- kwa mkopo, Emmanuel Linjechele, Kisimba Luambano na Nashon
Naftali (JKT Ruvu), Moaka Shabani, Ismail Mkaima na Damas Milanzi
(Mgambo Shooting), Donald Obimma, Exavery Muhollery, Mohamed Hussein na
Ulugbe Odia (Toto Africans).
Obadi
Mungusa, Juma Seif, Yusuf Mgwao, Ibrahim Job- kwa mkopo, Shamte Ally-
kwa mkopo, Buya Jamwaka, Takang Valentine, Nurdin Mussa, Salvatory
Jackson, Mohamed Athuman, Athuman Kajembe na Jarufu Kizombi (African
Lyon), Mussa Mudde na Abel Dhaila (Simba).
Rashid Simba, Zuberi Hamisi, Shaongwe Ramadhan, Castory Mumbara, Tinashe Machemedze na Shabani Kado (Coastal Union).
Mchezaji
Martin Mlolere aliyeombewa usajili Mgambo Shooting kutoka Majimaji
amekataliwa kwa vile taratibu za uhamisho hazijakamilika, hivyo anabaki
kwenye timu yake ya Majimaji.
Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
WADAU WAONGEZEKA UCHAGUZI WA TFF
Idadi
ya wadau waliojitokeza kuchukua fomu za kuwania uongozi katika
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imeongezeka ambapo wengine
saba wamechukua leo (Januari 15 mwaka huu) na kufanya idadi yao kufikia
26.
Hata
hivyo, idadi hiyo ni kwa wale wanaochukua fomu hizo katika ofisi za
TFF, kwani vilevile zinapatikana kupitia tovuti ya TFF ya www.tff.or.tz ambapo mwisho wa kuchukua na kurejesha ni saa 10 kamili alasiri Januari 18 mwaka huu.
Waliochukua
leo ni Michael Wambura anayewania umakamu wa rais wakati kwa wajumbe wa
Kamati ya Utendaji ni Mbasha Matutu, Muhsin Balhabou, Salum Chama,
Titus Osoro na Zafarani Damoder.
Idadi
kamili ya waliochukua Michael Wambura, Ramadhan Nassib na Wallace Karia
(Makamu wa Rais). Kwa upande wa wajumbe na kanda zao kwenye mabano ni
Salum Chama (Kagera na Geita), Mugisha Galibona, Samuel Nyalla, Titus
Osoro na Vedastus Lufano (Mara na Mwanza).
Epaphra
Swai na Mbasha Matutu (Shinyanga na Simiyu), Charles Mugondo, Elly
Mbise na Twahili Njoki (Arusha na Manyara), Yusuph Kitumbo (Kigoma na
Tabora), Ayubu Nyaulingo, Nazarius Kilungeja na Selemani Kameya (Katavi
na Rukwa) na James Mhagama (Njombe na Ruvuma).
Athuman
Kambi (Lindi na Mtwara), Hussein Mwamba na Stewart Masima (Dodoma na
Singida), Farid Nahdi (Morogoro na Pwani), Khalid Mohamed (Kilimanjaro
na Tanga) na Muhsin Balhabou, Shaffih Dauda na Zafarani Damoder (Dar es
Salaam).
Naye Said Mohamed amechukua fomu ya kuwania umakamu mwenyekiti wa Bodi ya Ligi Kuu (TPL Board).
UCHAGUZI TAIFA KUFANYIKA DAR ES SALAAM
Uchaguzi
wa viongozi wa Chama cha Makocha wa Mpira wa Miguu Tanzania (TAFCA)
utafanyika Jumamosi (Januari 19 mwaka huu) kwenye ukumbi wa mikutano wa
Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.
Kwa
mujibu wa Katibu Mkuu wa TAFCA, Eugene Mwasamaki, mikoa ambayo tayari
imefanya uchaguzi wa viongozi inatakiwa kuwasilisha muhtasari wa mkutano
uliowaingiza madarakani. Muhtasari huo uwasilishwe TAFCA kabla ya
keshokutwa (Januari 17 mwaka huu).
Mkoa
utakaoshindwa kutuma muhtasari ndani ya muda uliotolewa utakosa haki ya
kushiriki katika uchaguzi huo uliovutia wagombea watano. Wagombea hao
ni Oscar Korosso (Mwenyekiti), Lister Manyara (Makamu Mwenyekiti),
Michael Bundala (Katibu Mkuu) na Magoma Rugora na Wilfred Kidao
wanaowania ujumbe wa Mkutano Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu
Tanzania (TFF).
Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)