RAIS JOSEPH KABILA WA DRC ATUA DAR KWA ZIARA YA SIKU MOJA
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimjpokea Rais Joseph Kabila wa Jamhuri ya
Kidemokrasia ya Kongo (DRC) alipowasili uwanja wa ndege wa kimataifa wa
Julius Nyerere jijini Dar es salaam mchana wa Januari 30, 2013
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimtambulisha maafisa mbalimbali Rais Joseph
Kabila wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) alipowasili uwanja wa
ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam mchana
Januari 30, 2013
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na mgteni wake Rais Joseph Kabila wa
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) wakmiangalia ngoma za utamaduni
alipowasili uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijijni Dar
es salaam mchana Januari 30, 2013
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Rais Joseph Kabila wa Jamhuri ya
Kidemokrasia ya Kongo (DRC) wakiingia hoteli ya Hyatt Kilimanjaro
jijini mchana Januari 30, 2013
PICHA NA IKULU YA TZ.
Kimbunga Felleng Kutua Afrika Mashariki
Taarifa kwa umma: Uwezekano wa matukio ya mvua kubwa
Taarifa Na. 20130129-02
Muda wa Kutolewa Saa za Afrika Mashariki Saa 12:00 Jioni
Daraja la Taarifa:
1:Taarifa 2:Ushauri 3:Tahadhari 4:Tahadhari Kubwa:
Ushauri
Kuanzia:
Tarehe 30 Januari, 2013 Mpaka: Tarehe 01 Februari, 2013
Aina ya Tukio Linalotarajiwa
Mvua kubwa (zaidi ya milimita 50 katika kipindi cha saa 24 kilasiku)
Kiwango cha uhakika: Wastani
Maeneo yatakayoathirika Baadhi ya maeneo ya mikoa ya Rukwa, Iringa, Mbeya, Njombe,Ruvuma, Morogoro, Lindi, Pwani, Mtwara na maeneo jirani na mikoa hiyo.
Maelezo:
Kuwepo kwa kimbunga “FELLENG” kaskazini-mashariki mwa,Madagascar ambacho kinavuta upepo wenye unyevunyevu.kutoka Congo kupitia maeneo tajwa hapo juu.
Angalizo:
Wakazi wa maeneo hatarishi, watumiaji wa Bahari na nchi kavuwanashauriwa kuchukua tahadhari. Aidha taasisi zinazohusika na Maafa zinashauriwa kuchukua hatua stahiki.
Maelezo ya Ziada
Mamlaka inaendelea kufuatilia mwenendo wa kimbunga hicho,na kutoa mrejeo (updates) kila itakapobidi.
IMETOLEWA NA MAMLAKA YA HALI YA HEWA TANZANIA