MWANZA SI SHWARI
JIJI LA MWANZA
Hali ya jiji la Mwanza kwa sasa ni tete baada ya kuzuka kwa
vurugu kubwa kati ya jeshi la polisi na waendesha boda boda katika
jiji hilo ambapo kwa sasa kila kona ya jiji wananchi wametaharuki
na kukimbizana kuhofia usalama wao.
Mwandishi wa
mtandao huu wa www.sumiampanda.blogspot.com kutoka Jijini Mwanza
ameripoti kuwa vurugu hizo zimesababishwa na polisi ambao wamekuwa
wakiwafukuza vijana hao katika vijiwe vyao .
Hivyo
kutokana na mvutano huo jeshi la polisi limelazimika kutumia
risasi za moto kuwafukuza waendesha boda boda hao ni kuna taarifa
kuwa baadhi yao wamejeruhiwa vibaya katika vurugu hizo .
Kutokana na vurugu hizo kwa sasa jiji la Mwanza huduma za usafiri zimesimama kwa muda ili kuepuka madhara zaidi .
Habari zaidi zitakujia hivi punde
Habari tulizozipata toka ofisi ya IGP Said Mwema ni kuwa kuanzia jana jeshi la polisi nchini limeanza operesheni maalumu ya kukagua vyombo vyote vya moto ili kubaini mapungufu na kuhakikisha yanarekebishwa ikiwa ni juhudi za kukabiliana na wimbi la ajali nchini.
MIMBA SHULENI ZIKOMESHWE- MWANRI
UMENIKOSHA POKEA ZAWADI; Mkuu wa wilaya ya Mpanda, Paza Mwamlima akimpa zawadi kijana aliyekuwa akicheza ngoma ya kisukuma katika mkutano wa hadhara kijiji cha Kilida wilaya ya Mlele
SERIKALI YABADILI UTARATIBU WA MICHANGO MASHULENI, YAPIGA MARUFUKU KURUDISHA WANAFUNZI KUFUATA MICHANGO NYUMBANI
Naibu Waziri akikwa ameketi katika kiti akipokea taarifa ya mradi wa Maji ya kutega mlimani katika kijiji cha Kilida wilaya ya Mlele mkoani Katavi
MWENYEKITI wa kijiji cha Kilida akifungua mkutano wa hadhara ambao mgeni rasmi ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu TAMISEMI , Aggrey Mwanri
TUNASIKILIZA KWA MAKINI
BURUDANI TAMU KABISA
MBINU MBADALA KATIKA KUSHIRIKI MIKUTANO
NAWASALIMIA NDUGU ZANGU
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu TAMISEMI, Aggrey Mwanri akiweka jiwe la msingi katika mradi wa Maji ya kutega katika kijiji cha Kilida wilaya ya Mlele mkoani Katavi,
Mhe. Mwanri akifungua maji baada ya kufungua mradi wa Maji wilaya ya mlele mkoani Katavi
POKEA TAARIFA MKUU.
MKAO WA KUSIKILIZA TAARIFA YA WANANCHI
BURUDANI; Hii unaweza kuiita Sabuwufa ya Kifipa, wananchi wakitumbuiza katika mkutano wa hadhara katika kijiji cha Kilida
Na Willy Sumia, Mpanda
SERIKALI imepiga marufuku tabia ya baadhi ya walimu kuwarudisha
wanafunzi nyumbani kwa sababu ya kutolipia michango mbali mbali ya
shule na kwa kukosa sare za masomo.
Hayo yalibainishwa jana na Naibu Waziri kutoka ofisi ya Waziri Mkuu
Tawala za Mikoa Serikali za Mitaa, Mhe Aggrey Mwanri alipokuwa
akihutubia mamia ya wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika
katika uwanja wa Kashaulili mjini Mpanda akihitimisha ziara yake
katika halmashauri ya mji wa Mpanda.
Alisema kumekuwa na mtindo kwa baadhi ya shule kuwarudisha wanafunzi
nyumbani kwa kisingizio cha kukusanya michango lakini wanasahau kuwa
muda ule ni muda wa masomo kwani siku na saa za masomo zimehesabiwa na
inapopotea dakika moja kwa mwanafunzi kukaa bila kusoma haiwezi
kufidiwa tena hivyo serikali imeliona na kuamua kuchukua hatua.
Alisema kuanzia jana (Januari 20,2013) hakuna kumrudisha mwanafunzi wa
shule ya msingi na sekondari kwa sababu hajamalizia michango ya shule
na wala eti kwa sababu hana sare za shule husika, badala yake walimu
washirikiane na uongozi wa kata kuwawajibisha wazazi wasiokamilisha
michango shuleni na kuwanunulia wanafunzi sare za masomo.
'' Walimu nisikilizeni, kuanzia leo hakuna ruhusa kwa mwalimu
kumrudisha mwanafunzi nyumbani eti kutafuta michango, mnataka
wakafanye vibarua huko? Mzigo wa michango ya shule na sare ni wa
wazazi na walezi wao siyo wa mtoto tena msiwape barua watoto
kuwapelekea wazazi wao, pelekeni katika ofisi za kata kuna kamati ya
maendeleo ya Kata WDC" alisema Mhe. Mwanri
Alisema unapomrudisha mwanafunzi nyumbani akachukue mchango wa shule
maana yake ni kwamba asirudi shule kama hajapewa mchango na hapo ndipo
unadhoofisha maendeleo ya mwanafunzi kitaaluma hivyo kama umeajiriwa
na serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania huruhusiwi kuwarudisha
wanafunzi wakatafute michango
Akizungumzia michango mingi mashuleni Mwanri alisema hivi sasa
serikali imebadili utaratibu wa kurasimisha michango kwa kupitia ofisi
ya Katibu Tawala wa Mkoa husika na hivyo kila shule itakayokaa na
wazazi na kupanga michango yao ya shule kwa maendeleo ya shule yao
lazima kwanza mapendekezo hayo yapelekwe kwa Katibu Tawala wa Mkoa huo
ili ayapitie mapendekezo hayo na kujiridhisha ndipo atoe kibali cha
kuanza kutoza michango hiyo
Alisema hivi sasa kila shule ianze utaratibu wa kuita wazazi na
kuangalia ichakavu wa madawati yaliyopo na kutolea mapendekezo ya
ukarabati wake ili yaweze kutumika badala ya kuendelea na mtindo wa
kila mwaka wanafunzi kudaiwa kwenda na madawati shuleni kwani kila mtu
anajiuliza madawati hayo hayajai shuleni huko, ni bora uwepo utaratibu
wa kuangalia mapungufu ndiyo yachangiwe na wazazi
Aliwaagiza wakurugenzi watendaji katika halmashauri kukagua na
kujiridhisha namna majembe, mapanga na madawati yanavyotumika
mashuleni kwani kuna baadhi ya sehemu wanafunzi wanaagizwa kuwenda na
majembe mapya yenye mpini lakini wakifika shuleni majembe mapya
yanakusanywa na kuwekwa badala yake siku ya kulima ikifika wanafunzi
wanagawiwa majembe ya zamani.
Naibu Waziri Mwanri anatarajia kukamilisha ziara yake katika mkoa wa
Katavi Jumatano na kurejea mjini Dodoma kwa ajili ya kikao kijacho cha
bunge.
Baadhi ya wataalamu wa mkoa wa Katavi wakijipatia picha za ukumbusho katika hoteli ya kitalii ya Katuma Lodge iliyopo katika Hifadhi ya Wanyama ya Taifa ya Katavi mkoani Katavi kabla ya kuwasilisha taarifa ya serikali ya mkoa na wilaya kwa Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali na Mitaa, Mhe Aggrey Mwanri kabla kuanza ziara.
Kaimu Katibu Tawala mkoa wa Katavi, Lauteri Kanoni akiwasilisha Taarifa ya mkoa kwa Naibu Waziri TAMISEMI, Mhe Aggrey Mwanri
Baadhi ya wataalamu wa mkoa wa Katavi wakipokea maelekezo kutoka kwa Mhe Mwanri
Mhe Mwanri akipokea taarifa ya wilaya ya Mpanda kutoka kwa Kaimu Katibu Tawala wa wilaya hiyo, Kenneth Simuyemba
Mhe Mwanri akipokea taarifa kutoka kwa Kaimu Katibu tawala mkoa wa Katavi, Lauteri Kanoni, kushoto kwake ni mke wake, Grace Mwanri
Mhe Mwanri akipokea taarifa ya wilaya ya Mlele kutoka kwa Kaimu Katibu tawala wa wilaya hiyo, Epafrace Tenganamba. waliosimama meza kuu ni Mkuu wa wilaya ya Mpanda (suti ya bluu), Paza Mwamlima, mwenyekiti wa halmashauri ya mji Mpanda, Enock Gwambasa, mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Mpanda, Wilbroad Mayala na Kaimu katibu Tawala wa mkoa wa Katavi, Lauteri Kanoni
Kaimu Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Mpanda, Patrick Mwakyusa akikabidhi taarifa ya halmashauri yake kwa naibu waziri
Naibu Waziri OW-TAMISEMI Mhe. Aggrey Mwanri akitoa nasaha kwa watendaji wa mkoa wa Katavi baada ya kupokea taarifa ya mkoa huo.
TUKO MAKINI MKUU; Baadhi ya wataalamu wa mkoa wa Katavi wakisikiliza maagizo na maelekezo ya wizara katika hoteli ya Katuma iliyopo Katavi National Park
Naibu Waziri akiwasili kijiji cha Mirumba kuweka jiwe la msingi mradi wa ghala la Mazao
Taarifa ya Mradi wa Ghala Mirumba
Naibu Waziri akipokea taarifa ya mradi wa ghala Mirumba
Hakuna Mzaha; Naibu Waziri, Mhe Mwanri akikagua bati la kuezekea ghala kama kweli ni vipimo vinavyotakiwa kwa ajili ya majengo ya serikali geji 28.
Naibu Waziri akibadilishana mawazo na mwenyekiti wa kijiji cha Mirumba wilaya ya Mlele
Mhandisi kitimoto, kwa nini hamjaweka conduit pipe katika ukuta huu?
Mhandisi na mkandarasi mmmefanya kazi nzuri katika jengo hili, pongezi sana, ndivyo anavyosema Naibu Waziri wa TAMISEMI, Aggrey Mwanri
Mhe Mwanri ni mwanamazingira mzuri, anapanda mti wa kumbu kumbu katika kijiji cha Mirumba
kazi inaendelea
Na Willy Sumia,
Katavi
Naibu Waziri wa nchi Ofisi ya waziri mkuu Tawala za Mikoa na
Serikali za Mitaa (Tamisemi) Mhe Aggrey
Mwanri amewaagiza viongozi na Watendaji wa serikali kuhakikisha wanakomesha
suala la mimba mashuleni.
Waziri Mwanri ametoa
agizo hilo katika mkutano wa hadhara katika vijiji vya Kilida Kata ya Mamba na Inyonga wilayani
Mlele Mkoani Katavi katika ziara yake ya kukagua na kuhimiza shughuli za
maendeleo katika mkoa wa ikiwa ni pamoja na kuangalia Halmashauri zinavyosimamia
fedha za serikali zinazoletwa kwa ajili
ya shughuli za miradi mbali mbali ya maendeleo
Amesema
katika taarifa ya mkoa imeelezwa kuwa asilimia ya wanafunzi wanaopata
mimba imepungua kutoka asilimia sitini na tisa hadi sitini na saba hali
inayoashiria kuwa tatizo linaendelea kwa kasi sana na kuwa endapo hatua za
makusudi hazitachukuliwa suala la elimu kwa watoto wa kike itaendelea kudumazwa
Amesema kila mkoa
na wilaya nchini zipo taarifa za tatizo la mimba kwa wanafunzi hivyo ipo haja
ya watu kuwajibika katika kuhakikishani tatizo hili linaondoka kabisa na ni wajibu
wa viongozi kuhakikisha suala la mimba linakomeshwa kabisa mashuleni na
haitoshi kila mara viongozi kuripoti tu suala la mimba mashuleni bila kuchukua hatua
kuchukuliwa kwa wale wahusika wanaofanya vitendo hivyo vya kuwapa mimba watoto
wa kike.
“Haitakiwi kuripoti
tu, pia inatakiwa kueleza ni hatua gani zimechukuliwa kuhakikisha hao wanofanya vitendo hivyo
wamechukuliwa hatua zipi za kisheria ili kukomesha vitendo hivyo, ukisikia
mimba, kamata binti mwenye mimba, kamata wazazi wake weka msukosuko watakueleza
mwenye mimba” Alisema Mhe. Mwanri.
Aidha katika
taarifa ya mkoa wa Katavi kwa Mhe. Mwanri imeelezwa kuwa mimba kwa mkoa wa katavi
zimepungua kutoa wasichana waliopata ujauzito mwaka 2011 walikua 63 na mwaka 2012 mimba zilikuwa
61 sawa na upungufu wa asilimia tano taarifa
ambayo haikueleza namna wanavyolishughulikia tatizo la mimba na kueleza wangapi
walichukuliwa hatua za kisheria kulingana na makosa hayo.
Akiwasilisha taarifa
hiyo Kaimu Katibu Tawala wa mkoa huo, Lauteri Kanoni amesema kuwa juhudi za
kuwabana wanaotenda vitendo vya kuwapa ujauzito wanafunzi zinakwama kutokana na
changamoto ya baadhi ya wazazi wa mwanafunzi mwenye ujauzito kushiriki katika mikakati
ya kuficha ushahidi wakati wa kumtafuta mhalifu
WANAFUNZI LAZIMA WAPATE CHAKULA CHA MCHANA SHULENI - MWANRI
Na Kibada Kibada –Katavi
Viongozi wa Serikali wa Mkoa wa Katavi
wametakitakiwa kuhakikisha wanaweka
utaratibu wa wanafunzi wote wa shule za
sekondari wanapatiwa chakula cha mchana kwenye shule zao.
Agizo hilo limelitolewaa leo(jana)
na Naibu Waziri wa TAMISEMI Aggri Mwanri wakati
akiongea na viongozi wa serikali mkoani humo kwenye hoteli ya Katuma
iliyoko katika hifadhi ya Taifa ya Katavi mara baada ya kusomewa Taarifa ya
utekelezaji wa shughuli za maendeleo za Mkoa huo.
Mwaniri alisema kuwa ni vizuri
viongozi washirikiane na bodi za
shule zasekonari kukaa na wazazi wa
wanafunzi wanaosoma kwenye shule za sekondari katika mkoa huo kupanga namna
ya kuhakikisha wanafunzi wanapata
chakula cha mchana hapohapo shuleni kwao.
Kauli hiyo aliitoa kufuatia taarifa
iliyosomwa mbele yake na Kaimu Katibu tawala wa Mkoa wa Katavi Lauteri Kanoni
ambayo ilieleza kuwa ni wanafunzi asilimia 60 tu wanaosoma katika shule za
sekondari za kata ndio wanaopata chakula katika mkoa wa katavi.
Alieleza kuwa ameshitushwa na taarifa
hiyo ya baadhi ya shule wanafunzi kutopata chakula cha mchana ukizingatia mkoa
wa katavi ni miongoni mwa mikoa inayozalisha chakula kwa wingi hapa nchini
likiwemo na zao la mahindi
“Inawezekana kabisa wazazi wakawa
hawajapewa elimu ya kutosha juu ya namna ya uchangia wa chakula cha wanafunzi
mashuleni sasa ni juu yenu viongozi kuwaelimisha”alisema Mwaniri.
Akifafanua zaidi alieleza kuwa
endapo mzazi wa mwanafunzi akishakuwa na elimu ya uelewa wa kuchangia chakula
tatizo hilo halitakuwapo tena.
Naibu Waziri Mwanri ameanza ziara
ya siku saba mkoani katavi yenye lengo la kukagua shughuli za Miradi ya
maendeleo ili kuona fedha inayotolewa na serikali kama zinatumika ipasavyo kwa
lengo lililokusudiwa na miradi inayotekelezwa
inalingana na thamani ya fedha iliyotolewa na serikali
Lengo linguine la ziara hiyo ni
kuangalia namna halmashauri za mkoa huo zinavyoweza kukusanya mapato ya ndani
na jinsi zinavyotumia kwa ajili ya kuwaletea maendeleo.
Miradi aliyoikagua kwa siku ya
kwanza ya ziara yake hapo jana aliweka jiwe la msingi katika la kuhifadhia mazo
ya chakula mbalimbali katika kijiji cha mirumba Kata ya Kibaoni Wilayani
Mlele,kutembele a mradi wa ghala, mashine ya kusindika mpunga na kituo cha
Habari cha Kilimo katika ya Mwamapuli.
Miradi mingine atakayotembelea
katika ziara yake hiyo ni kuweka jiwe la msingi katika jingo la utawala Nsimbo
Kata ya Nsimbo,kutembelea shamba darasa la miembe Nsimbo pamoja na kuangalia ujenzi wa kituo cha Afya
cha Inyonga ambacho kiombwa kigezwa kuwa hospitali ya wilaya ya Mlele pindi
kitakapokamilika na huo utakuwa mradi wake wa mwisho katika wilaya ya Mlele.