Tuesday, January 22, 2013

POLISI JAMII MKOA WA KATAVI

 KAMANDA WA JESHI LA POLISI MKOA WA KATAVI, ACSP DHAHIR KIDAVASHARI AKIFUNDISHA ELIMU YA POLISI JAMII, ULINZI SHIRIKISHI NA ULINZI JIRANI KATIKA MKUTANO WA HADHARA KATIKA ENEO LA SHULE YA NYERERE KATIKA KATA YA KAWAJENSE MJINI MPANDA JANUARI 21, 2013

 Dhahiri Kidavashari, Kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Katavi akifafanua maana ya usiri kwa askari wanapopewa taarifa za kiuhalifu kutoka kwa wananchi baada ya kulalamikiwa kuwa wapo baadhi ya askari wake wanavujisha siri za raia wema wanapotoa taarifa za kiuhalifu na kuhatarisha usalama wa raia hao.




Umati wa wananchi, vijana, watoto na watu wazima walishiriki jana katika mkutano wa polisi jamii Mkoa wa Katavi




TUKO MAKINI TUNASIKILIZA POLISI JAMII; WAKAZI WA KAWAJENSE MJINI MPANDA


RCO KATAVI AKIDADAVUA DHANA YA ULINZI SHIRIKISHI KAWAJENSE MJINI MPANDA
Kamanda wa jeshi la polisi Katavi, Dhahir Kidavashari akiteta jambo na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Mpanda katika mkutano wa Polisi Jamii uliofanyika katika uwanja wa Web Site Kawajense mjini Mpanda jana



Dawati la jinsia na wanawake katika jeshi la polisi mkoani Katavi nalo limeshiriki katika mkutano wa polisi jamii kuhamasisha wanawake na jamii kupinga ukatili wa kijinsia na vitendo vya unyanyasaji kwa wanawake na watoto katika jamii.
 MWENYEKITI wa Halmashauri ya Mji Mpanda alikuwepo mkutanoni pembezoni mwa RPC Katavi
 TUKIAMUA UHALIFU UTAISHA, Ndivyo anavyosema Mhe Enock Gwambasa Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Mpanda katika mkutano wa Polisi Jamii.

 Diwani wa Kata ya Kawajense, Mhe Ngasa akifafanua anavyofurahia mkutano wa polisi jamii katika kata yake
 MKUU WA POLISI WA WILAYA YA MPANDA


 STAFF ONE, JOSEPH MYOVELA AKIMWAGA SERA ZA ULINZI SHIRIKISHI KWAJENSE

POLISI JAMII, ULINZI SHIRIKISHI NA ULINZI JIRANI NI SUMU KWA WAHALIFU

JESHI la polisi mkoani Katavi limetakiwa kubadili utendaji kazi wake ili kujenga imani ya ushirikiano baina ya jeshi hilo na wananchi katika juhudi za kuutokomeza uhalifu mkoani humo

Hayo yalibainishwa jana na wananchi wa kata ya Kawajense katika mkutano wa hadhara wa polisi jamii uliofanyika katika eneo la Bar ya Web Site iliyoko jirani na shule ya msingi Nyerere katika kata hiyo mjini Mpanda ambapo Kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Katavi alikuwa akitoa elimu ya polisi jamii kwa wananchi

Wananchi hao walilalamikia vitendo vya baadhi ya askari wa jeshi hilo kutoa siri ya watoa taarifa kwa wahalifu na hivyo kujenga chuki na kuhatarisha usalama wa watoa taarifa na hivyo kudhoofisha juhudi za kupambana na uhalifu mkoani humo.

Wakizungumza wananchi hao waliwasihi viongozi wa jeshi hilo ngazi ya wilaya kuiga utendaji kazi wa aliyekuwa mkuu wa polisi wa wilaya hiyo na baadaye kupelekwa mkoani kuwa aliweza kupambana na uhalifu hadi akafanikiwa kuondoa wimbi la ujambazi lililokuwa limeota mizizi wilayani Mpanda.

Akizungumza katika mkutano huo kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Katavi, Dhahiri Kidavashari aliwasihi wananchi kutokukata tamaa kwa changamoto ndogo ambazo zinaweza kutatuliwa na yeye mwenyewe tena kwa muda mfupi sana, wanachopaswa kufanya kuanzia sasa ni kumpa taarifa ni askari gani anafanya huo mchezo mchafu wa kiuaji.

Alisema anachoomba kwa wananchi ni kumpa taarifa kwa njia ya simu kwa namba alizozitoa au kumuona popote watakapokutana naye kuhusu matukio ya kuvujisha siri wanazotoa kwa jeshi la polisi ili aweze kuchukua hatua haraka na kwa wakati ili Katavi iendelee kuwa salama bila majambazi.