OMBA OMBA ALIYEIGIZA MLEMAVU WA MIGUU NA MIKONO ATIMUA MBIO
MTI WAANGUKA MLIMA IPOGOLO MAGARI YAKWAMA KUPITA
Hapa wananchi wakihangaika kukata mti huo kwa shoka ili kupata nafasi ya kupita
Tukio hilo limetokea mida ya saa 8 mchana katika eneo hilo ambapo moja kati ya daladala lililokuwa likipandisha eneo hilo likiwa na abiria zaidi ya 50 limenusurika kufunikwa na mti huo.
Baadhi ya abiria na mashuhuda wa tukio hilo waliozungumza na mtandao wa www.francisgodwin.blogspot.com eneo la tukio wamedai kuwa hakuna mtu aliyejeruhiwa japo wameomba wasimamizi wa barabara hiyo wakala wa barabara mkoa wa Iringa (TANROADS) kuangalia uwezekano wa kukata miti mikubwa iliyopo eneo hilo ili kuepusha maafa makubwa zaidi ya hayo.
Kwani wamesema tatizo la mti huo na mawe kuanza kuporomoka katika mlima huo limetokana na baruti ambazo zilikuwa zikitumika kupasua mawe katika mlima huo wakati wa upanuzi wa barabara hiyo hivyo sasa maji yanapoingia ndani ya ardhi hiyo ndio husababisha matatizo hayo .
Baadhi ya wananchi wamempongeza meneja wa TANROADS mkoa wa Iringa Paul Lwakurwa kwa kufika mapema eneo hilo na kufanikisha kutatua tatizo hilo vinginevyo hadi kesho barabara hiyo ingefungwa rasmi. KALI YA 2013
OMBA OMBA ALIYEIGIZA MLEMAVU WA MIGUU NA MIKONO ATIMUA MBIO
Hapa akisubiri msaada kutoka kwa wasamaria wema leo
Hapa akitimua mbio kukwepa kamera ya PAPARAZ mjini Iringa leo
Ule usemi wa wahenga kuwa ukistaajabu ya mussa utayaona ya filauni leo umetimia katika eneo la M.R mjini Iringa baada ya wananchi waliokuwepo eneo hilo kupigwa na butwaa baada ya mzee janja ambaye amekuwa akishindwa eneo hilo na kujifanya mlemavu asiyekuwa na mkono mmoja na mguu mmoja kutimua mboni kukwepa kamera ya mtandao huu.
Tukio hilo limetokea majira ya saa 8 mchana baada ya camera ya mwandishi kufika eneo hilo kushuhudia umati wa wananchi wakiendelea kumpa fedha mzee janja huyo ambae alijifanya mlemavu wa viongo na kuongea kwa shida .
Hata hivyo baada ya mmoja kati ya wananchi kufika eneo hilo alionyesha kufichua mbinu hiyo chafu ya mzee huyo kujifanya ni mlemavu wakati asubuhi alikutana maeneo akiwa mzima wa afya njema na katika kumhoji zaidi ndipo kamera ya mtandao huu ilipoamua kufanya kazi yake ya kunasa kituko hicho na ndipo mzee huyo alipoanza kuongea kwa sauti vizuri tofauti na alivyokuwa akijifanya kuwa hawezi kuongea kabisa (bubu)
Wakati mabishano yakiendelea eneo hilo ghafla mzee huyo alisimama kwa miguu yake yote miwili pamoja na awali kujifanya ni mlemavu asiye na mguu mmoja ila baada ya watu kutaka apigwe picha ndipo mzee huyo alipoanza kutimua mbio huku ulemavu aliokuwa nao akiusahau hapo pamoja na kandambili zake na hakuna mtu aliyeweza kumfukuza na kufanikiwa kumkuta.
Baadhi ya wananchi wameuomba uongozi wa Manispaa ya Iringa na miji mingine kuwabana omba omba hao ambao wamekuwa wakidanganya watu kuwa wao ni walemavu kumbe ni wazima na kutaka kuwepo kwa utaratibu maalum wa watu kuomba misaada.Habari hii ni kwa mujibu wa Francis Gowin