Thursday, January 31, 2013

ZIARA YA NAPE KIGOMA

4. Makamu Mwenyekiti wa CCM-Bara, Ndugu philip Mangula akiteremka kutoka kwenye ndege ya shirika la ndege la Tanzania (Air Tanzania) ,kwenye uwanja wa ndege wa Kigoma  asubuhi tarehe 1/2/2013.

5. Makamu Mwenyekiti CCM Bara Philip Mangula  akipokelewa na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Moses Nnauye mara baada ya kuwasili Kigoma asubuhi ya leo kwa ndege ya shirika la ndege la Tanzania (Air Tanzania)

14. Makamu Mwenyekiti wa CCM-Bara,Ndugu Philip Mangula akisalimiana na baadhi ya viongozi wa CCM mkoani Kigoma mara tu alipowasili katika uwanja wa ndege wa Kigoma, uwanja ambao umefanyiwa maboresh makubwa ikiwa na kuongezwa sehemu ya kurushia ndege.


18.Makamu Mwenyekiti wa CCM-Bara ,Ndugu Philip Mangulaakitoa salaam za shukrani kwa mapokezi mazuri pia alitoa pongezi kwa maboresho ya uwanja wa ndege ambao alisema ni mzuri kulinganisha na miaka ya nyuma na amekiri kumekuwa na mabadiliko makubwa ya kimaendeleo katika mji wa Kigoma. Makamu Mwenyekiti amewasili rasmi kwa ajili ya sherehe za miaka 36 ya kuzaliwa kwa Chama Cha Mapinduzi ambazo kitaifa mwaka huu zitafanyika tarehe 3/2/2013 mkoani kigoma kwenye Uwanja wa Lake Tanganyika.
Picha na Adam H. Mzee
Kigoma ,Tanzania.



 Katibu waItikadi na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi Nape Nnauye ametembelea Kijiji chaRungwe Mpya kilichopo kata ya Rungwe Mpya Wilayani Kasulu Mkoani Kigoma na kufanya shughuli mbalimbali za Chama ikiwa ni pamoja na Kuweka jiwe la Msingila Ofisi ya CCM kijijini hapo na kuhutubia mkutano wa hadhara wa wananchi wa Kata hiyo pamoja na Kata ya Asante Nyerere.
 Baada yakuweka Jiwe hilo la Msingi, Nnauye alikabidhi kadi kwa wanachama wapya wa Chama hicho kutoka katika kata za Asante Nyerere pamoja na Rugwe Mpya, wanachama ambao wamerejea CCM kutoka vyama vya upinzani hasa NCCR Mageuzi na Chadema kabla ya kuzungumza na Wajumbe wa Nyumba Kumi wa chama hicho, Wazee pamoja na Vijana waendesha Bodaboda mjini Kasulu.

 Nape akikabidhi kadi kwa wanachama wapya.
 Baadhi ya Kadi zilizorejeshwa katika mkutano wa hadhara.
Mkuu wa Wilaya Kasulu, Danny Makanga akicheza ngoma wakati wa mapokezi hayo ya Nape Kijijini hapo.
 Katibu
wa Itikadi na Uenezi wa CCM Taifa, Nape Nnauye akiweka jiwe la Msingi la
Ujenzi wa Ofisi ya CCM ikiwa ni moja kati ya miradi aliyoitembelea wilayani Kasulu.

NAPE KIJIJINI  RUNGWE MPYA


.  Katibu waItikadi na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi Nape Nnauye ametembelea Kijiji cha Rungwe Mpya kilichopo kata ya Rungwe Mpya Wilayani Kasulu Mkoani Kigoma na kufanya shughuli mbalimbali za Chama ikiwa ni pamoja na Kuweka jiwe la Msingila Ofisi ya CCM kijijini hapo na kuhutubia mkutano wa hadhara wa wananchi wa Kata  hiyo pamoja na Kata ya Asante Nyerere. Baada yakuweka Jiwe hilo la Msingi, Nnauye alikabidhi kadi kwa wanachama wapya wa Chama hicho kutyoka katika kata za Asante Nyerere pamoja na Rugwe Mpya,...