JUMUIYA YA WATUMIA MAJI YA BONDE DOGO LA MTO KATUMA IMEFANYA UCHAGUZI
WA VIONGOZI WAKE JANA JULAI 30, 2013
MATOKEO NI KAMA YALIVYO HAPA CHINI
JUMUIYA ya watumia maji ya bonde dogo la mto Katuma wilaya ya Mpanda
mkoa wa Katavi wametakiwa kuepuka rushwa katika utendaji kazi wao
Angalizo hilo limetolewa na Kaimu
Katibu Tawala wa wilaya ya Mpanda, Joseph Mzimya kwa wanajumuiya watumia maji
ya bonde dogo la mto Katuma kwa Kaimu jana Julai 30,2013 katika ukumbi wa shule
ya sekondari ya St. Mary’s Mpanda
kufuatia jumuiya hiyo kukamilisha mchakato wa uundaji katiba yake
amesema baada ya kujengewa uwezo
na ofisi ya bonde la ziwa Rukwa wameweza kuandaa katiba yao itakayokuwa mwongozo katika kudhibiti
matumizi holela ya maji ya mto Katuma pamoja na kulinda mazingira ya bonde dogo
la mto huo hivyo kabla ya kuanza kazi wanapaswa kujua kuwa Rushwa kwao ni mwiko
Katibu Tawala wa wilaya ya Mpanda
kuwa ofisi ya Mkuu wa wilaya inaitegemea jumuiya hiyo kumaliza migogoro iliyoko
katika bonde hilo
ambapo wakulima wanagombania maeneo ya kulima na wafugaji wanagombania maeneo
ya kufugia na kulishia wanyama hivyo kuna kila sababu kwa jumuiya hiyo kusimama
imara katika kazi zake
Alisema Miongoni mwa jukumu la
jumuiya ya watumia maji ya bonde dogo la mto Katuma ni kulinda, kusimamia,
kuhifadhi na kuendeleza rasilimali ya maji yaliyoko katika mto Katuma ambapo
jumuiya hiyo ina uwakilishi kutoka vijiji tisa vilivyoko katika bonde la mto
Katuma
Baadhi ya changamoto
walizoziainisha ni pamoja na kilimo holela, matumizi ya vizibo vya maji kwa
baadhi ya wakulima wa zao la mpunga katika bonde hilo, ufugaji usiozingatia hifadhi ya
mazingira, uvamizi wa chanzo cha mto Katuma katika mlima Waitaba kijiji cha
Bugwe unaofanywa na wafugaji pamoja na matumizi ya kemikali katika machimbo ya
madini na kutiririsha maji katika mto
Akizungumza kwa niaba ya mkuu wa
wilaya ya Mpanda, Kaimu Katibu Tawala wa wilaya hiyo, Joseph Mzimya amewataka
wanajumuiya hiyo kufanya kazi kwa uaminifu na uadilifu mkubwa kabla ya uzinduzi
ili serikali ione matunda mazuri kutoka kwenye jumuiya ambayo ni kumalizika kwa
migogoro iliyopo katika bonde hilo
Amewasihi viongozi wa jumuiya
kuepukana na vitendo vya Rushwa katika jumuiya yao
kwani serikali inataka kuona haki inatendeka kwa misingi ya usawa bila kujali
uwezo wa mtu kifedha au nafasi yake katika jamii kwani katika kazi za
uzalishaji mali
kila mmoja ana mchango wake kwa taifa na jamii nzima
Aidha mkuu wa wilaya ya Mpanda
ameziagiza halmashauri zilizopo katika bonde hilo za Nsimbo, Halmashauri ya Mji na
Halmashauri ya wilaya ya Mpanda kukamilisha haraka zoezi la mpango wa upimaji
ardhi katika vijiji na kuweka mpango wa matumizi bora ya ardhi ili kuipa nafasi
jumuiya kusimamia bonde dogo la mto Katuma kwa ufanisi