KAMANDA WA JESHI LA POLISI MKOA WA KATAVI, DHAHIR KIDAVASHARI |
MASAGA
Charles Chinga (36) mkazi wa kijiji cha Chilalo wilaya ya Misungwi mkoani
Mwanza anashikiliwa na jeshi la polisi mkoa wa Katavi kwa tuhuma za mauaji ya
Moshi Bella (44) mkazi wa Karema Katika tukio lililotekea Julai 22, 2013 katika
kijiji cha Kabage wilaya ya Mpanda mkoa wa Katavi
Kamanda wa Polisi mkoa wa Katavi,
Dhahir Kidavashari alisema jana ofisini kwake kuwa kukamatwa kwa Masaga Charles
kwa tuhuma za maujai yaliyotokea Julai 22, 2013 majira ya saa tisa alasiri
Katika kijiji cha Kabage, Kakese ambapo Moshi Bella mhutu mkazi wa Karema
alikutwa akiwa ameuawa kwa kukatwa na kitu chenye ncha kali kichwani na
shingoni kwa nyuma
Alisema uchunguzi uliofanywa ulibaini
kuwa marehemu alikuwa na kesi ya shamba Katika mahakamani wakigombania shamba
sehemu ya Iloba na ndugu Ndegesela ambapo kutokana na kuona mwenendo wa kesi
hiyo aliamua kumtafuta mtuhumiwa na kuongea nae ili amuue marehemu kwa malipo
ya shilingi mil 2, mtuhumiwa alikataa
Baadae Ndegesela aliongeza pesa hadi
shilingi mil 5 ndipo mtuhumiwa alikubali kwenda kumuua marehemu ambapo awali
alijifanya anahitaji shamba la kulima kiasi cha ekari mbili na kukubaliana
kuuziana shamba hilo
la marehemu kwa malipo ya shilingi laki tatu kila ekari makubaliano
waliyoafikiana wakiwa Katika nyumba ya Salum Kajimba (44)
Taarifa za polisi zinadai mtuhumiwa
alifika nyumbani kwa Salum Kajimba kuongea na marehemu Julai 20, 2013 na
kuondoka kwa ahadi ya kufika kulipa pesa kesho yake na kuoneshwa shamba lenyewe
Kamanda wa Polisi mkoa wa Katavi
alisema Julai 21, 2013 mtuhumiwa alifika nyumbani kwa Salumu na kuelezwa kuwa
Moshi Bella alikuwa amekwenda kisimani kuteka maji ya kuoga ambapo mtuhumiwa
aliaga kuwa anamfuata huko huko katika visima vya maji ya kuoga ambako
hawakurudi wote hadi siku ya pili mwili wa Moshi Bella ulipokutwa umekatwa
katwa kwa mapanga akiwa ameshafariki majira ya saa tisa alasiri
Alisema jeshi la polisi lilipata
taarifa ya mauaji hayo na kuanza upelelezi na kufanikiwa kumkamata mtuhumiwa
akiwa Katika eneo la Makanyagio mjini Mpanda wilaya ya Mpanda na kuanza kumhoji
kuhusiana na mauaji hayo yaliyotokea Kabage.
Alisema Katika mahojiano hayo
mtuhumiwa alikiri kuwa alimuua marehemu kwa malipo aliyokuwa amekubaliana na
mtu mmoja aliyemtaja kwa jina moja la Ngedesela ambaye anadaiana shamba na
marehemu mahakamani na alikuwa amemlipa kiasi cha shilingi milioni moja
Alisema mtuhumiwa aliwaeleza kuwa
Ndegesela alimuita akamuomba amsaidie kumuua marehemu kwa gharama ya shilingi
mil. 2 akakataa lakini baadae alimuita akamueleza kuwa ameongeza malipo
atamlipa shilingi mil 5 endapo ataweza kumuua marehemu ndipo akakubali kufanya
mauaji ambapo alipewa malipo ya awali ya shilingi mil 1.
Alisema mtuhumiwa aliwaeleza Katika
mahojiano kuwa alifika shambani kwa marehemu akijifanya anataka kununua shamba
la ekari mbili ili aweze kupata nafasi ya kumuua kirahisi marehemu ndipo
alipoweza kumpata marehemu akiwa kisimani na kumkatakata mapanga na kuondoka
kwa baiskeli hadi Mpanda mjini akimsubiri Ndegesela amlipe pesa yake aondoke
kwao Mwanza
Akizungumza na waandishi wa habari
Katika ofisi ya Kamanda wa Polisi mkoa wa Katavi mtuhumiwa alisema yeye
alitumwa kumuua marehemu kwa malipo ya shilingi milioni 5 na ekari mbili za
shamba kwa sababu marehemu alikuwa ameshitakiana na Ndegesela aliyempa kazi
mahakamani
Akizungumzia maisha yake mtuhumiwa
alisema yeye amewahi kushiriki mashindano ya baiskeli Katika mikoa mbali mbali Tanzania
kwa kipindi cha miaka 15 sasa Katika mikao ya Tabora, Mwanza, Shinyanga na
Arusha ambako aliweza kupata ushindi na kupewa fedha taslimu kiasi cha shilingi
laki nane (800,000/=)
Alisema Katika mkoa wa Katavi alikuwa
mwezi Oktoba alipoitwa na Ndegesela kwa ajili ya kazi ya kumuua marehemu lakini
alipofika wakaongea na Ndegesela hawakufikia muafaka akaamua kuendelea kuishi
Katavi baada ya kufurahiwa na maisha ya Katavi ndipo alipomuomba tena baada ya
kuongeza pesa akamuomba amfanyie kazi hiyo
Kwa mujibu wa Kamanda wa polisi mkoa
wa Katavi, mtuhumiwa Ndegesela anatafutwa ili akamatwe kwa baada ya mauaji
aliweza kukimbilia kusikojulikana hivyo alitoa rai kwa wananchi watakaomuona
sehemu yoyote Ndegesela mkazi wa Iloba wilaya ya Mpanda watoe taarifa Katika
kituo chochote cha polisi ili aweze kukamatwa