Friday, July 26, 2013

RC KATAVI AKABIDHI PIKIPIKI

TUTAZITUMIA PIKIPIKI KUFIKA MAENEO MAGUMU KWA URAHISI ZAIDI - MAAFISA TARAFA












Nakukabidhi usafiri kijana wangu


Mkuu wa Mkoa wa Katavi, Dr Rajabu Rutengwe akiangalia jambo kwa makini

WAKATI MWINGINE FURAHA NI DAWA YA KICHWA; Baada ya kutafakari mambo magumu kwa makini Mkuu wa Mkoa wa Katavi Dr Rutengwe huwa anatengeneza mazingira ya kutabasamu na hata kucheka ili kupata Brain Ventillation kama alivyonaswa na kamera yetu


MKOA wa Katavi umekabidhi pikipiki 11 na magari matatu kwa maafisa Tarafa na watendaji wa sekretarieti ya mkoa huo ili kukabiliana na changamoto ya ukubwa wa eneo la kuhudumia na uhaba wa vyombo vya usafiri katika kuwahudumia wananchi wa mkoa huo.

 Pikipiki hizo aina ya YAMAHA 125 CC na magari yamekabidhiwa na mkuu wa mkoa hu Dr. Rajabu Rutengwe jana Julai 26, 2013 katika hafla fupi ya makabidhiano iliyofanyikia katika viwanja vya ofisi ya mkuu wa Mkoa wa Katavi hafla iliyohudhuriwa na watumishi wa ofisi ya Mkuu wa mkoa na sekretarieti ya CCM ya mkoa huo

 Akikabidhi piki piki hizo kumi na moja mkuu wa mkoa amesema katika makabidhiano ya mkoa wa Katavi na mkoa mama wa Rukwa, ofisi yake ilikabidhiwa gari moja kuu kuu STK 1615 ambalo hivi sasa halitembei na hivyo ofisi yake kuwa na mtihani mkubwa wa changamoto ya ukosefu wa usafiri hasa magari kwa watendaji wake.

Amesema kwa sasa mkoa umeweza kupata magari 15 kati ya hayo magari 8 yameletwa kutoka Serikali kuu kwa ajili ya miradi na viongozi yaani Mkuu wa mkoa, Katibu Tawala na wakuu wa wilaya, mengine ofisi yake ilipewa na shirika la kuhudumia wakimbizi UNHCR magari matatu yaliyosalia yalinunuliwa na ofisi yake kwa gharama ya shilingi 460,088,740/=

Mkuu wa Mkoa ameyataja magari hayo kuwa ni basi la watumishi lililonunuliwa kwa shilingi 179,960,000/=, gari la utawala aina ya Toyota Hard Top shilingi 140,064,370/= na gali la idara ya Elimu aina ya Toyota Hard Top bei hiyo hiyo ya shilingi 140,064,370/=

 Amesema kwa namna ya pekee ofisi yake inaishukuru Serikali kwa kuiwezesha ofisi yake kuajiri Maafisa Tarafa wapya watano na kuufanya mkoa huo kuwa na jumla ya Maafisa Tarafa saba kwani mkoa huo ulikuwa na maafisa Tarafa wawili tu kati ya tarafa kumi zilizopo katika mkoa huo

 Amesema katika kuwajengea mazingira mazuri ya kiutendaji maafisa Tarafa waliopo ofisi yake iliamua kuwanunulia usafiri wa pikipiki ili waweze kumudu kuhudumia tarafa zao ambazo kimsingi zina eneo kubwa lenye wananchi wengi

Amewataka maafisa tarafa hao kuwa mfano bora kwa waendesha pikipiki wengine kwa kufuata sheria za usalama barabarani ili kuepusha ajali zisizotarajiwa kwao na kwa watumia barabara wengine pindi wanapokuwa barabarani pamoja na kuzitunza pikipiki hizo

 Amrsema ofisi yake imetumia kiasi cha shilingi 3,998,000/= kununulia pikipiki moja sawa na jumla ya shilingi 43,978,000/= kununulia pikipiki zote kumi na moja zilizonunuliwa na ofisi ya mkuu wa mkoa wa Katavi

Akizungumzia makazi ya Maafisa Tarafa waliko  mkoani kwake, Dr Rajabu Rutengwe amesema ofisi yake haina nyumba ya Afisa Tarafa hata mmoja, zipo ofisi sita tu hivyo aliahidi kufanya mazungumzo na Wizara ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) ili kujenga nyumba bora za kuishi maafisa Tarafa na ofisi katika tarafa mbali mbali mkoani humo.

 Aidha Dr Rutengwe amewaagiza makatibu tawala wa wilaya kuhakikisha wakurugenzi watendaji wa Halmashauri wanatoa huduma ya mafuta na matengenezo kwa pikipiki hizo ili ziweze kufanya kazi zilizokusudiwa na kuleta maendeleo kwa wananchi wa mkoa wa Katavi
Nakukabidhi kifaa cha kazi mama ukawajibike kwenye Tarafa yako, Mkuu wa Mkoa wa Katavi, Dr Rajabu Rutengwe akikabidhi pikipiki kwa maafisa tarafa







Dr Rajabu Rutengwe akiwasha pikipiki ikiwa ni kuzindua matumizi ya pikipiki hizo baada ya kuwakabidhi maafisa tarafa na mwangalizi wa ofisi yake.