Sunday, July 14, 2013

SUMRY YAPINDUKA TENA KATAVI, 7 WAJERUHIWA




SEVEN people sustained injuries and were rushed to Mpanda and Namanyere hospitals after a Sumry Bus in which they were travelling from Mpanda to Sumbawanga overturned at Bwawani area in Katavi Region on Friday.
Confirming the road traffic accident, the Katavi Acting Regional Police Commander (RPC), Emmanuel Mlay, told the ‘Sunday News’ through telephone from Mpanda that the bus overturned after its front tyre burst.
He said the accident occurred at around 3 am after the driver failed to control the bus. Explaining further, he said that among the injured, four are females and two are male, one of them a five year old boy.
“Bus owners should consider purchasing high quality tyres which are durable and can sustain various conditions, “advised ACP Mlay. However, some of them flout regulations and cause such accidents that claim lives,” he said, warning that the government would continue to deal with such offenders and punish them.
Commander Mlay said investigations were underway and the police are holding the bus driver identified as Sefu Mbaruki (30).
A source that preferred anonymity called upon the government to take action against owners and drivers of Sumry buses, as only last week another bus that belongs to the same company overturned and plunged into a river, claiming nine lives and leaving 53 passengers injured.


 
WATU sita wamejeruhiwa na wengine 50 wamenusurika katika ajali ya basi la kampuni ya Sumry baada ya basi hilo kupasuka gurudumu la mbele na kupinduka katika hifadhi ya wanyama ya Katavi Katika wilaya ya Mlele mkoa wa Katavi.
Kaimu Kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Katavi, Emanuely Nnley alithibitisha Julai 13, 2013 ofisini kwake mjini Mpanda kutokea kwa ajali hiyo na kueleza kuwa  ilitokea Julai 12, 2013 majira ya saa sita mchana ikilihusisha basi la kampuni ya Sumry lenye namba T 939 BJL  aina ya Nisani diesel lililoondoka mjini Mpanda  mkoa wa Katavi saa nne asubuhi kuelekea mjini Sumbawanga mkoani  Rukwa  likiwa na abiria zaidi ya hamsini
Alisema basi hilo lilipofika ndani ya hifadhi ya wanyama ya katavi kilometa nane kutoka kijiji cha Sitalike gurudumu la mbele upande wa dereva lilipasuka na kusababisha basi hilo kuserereka na hatimaye kupinduka ambapo watu saba akiwamo mtoto mmoja walijeruhiwa na kukimbizwa katika hospitali ya wilaya ya Mpanda mkoani Katavi  na hospitali Teule ya Namanyere wilaya ya Nkasi mkoani Rukwa
Kwa mujibu wa Kaimu kamanda wa polisi mkoani Katavi dereva wa basi hilo, Seif Mabrouk anashikiliwa na jeshi la polisi mkoani humo wakati upelelezi unaendelea kabla ya kuchukuliwa hatua zaidi za kisheria kutokana na makosa yatakayobainika katika uchunguzi wa jeshi la polisi, SUMATRA na vyombo vingine vya usalama
Katika kipindi cha wiki moja ajali mbili za mabasi ya kampuni ya Sumry zimetokea katika mkoa wa katavi na kusababisha vifo vya watu kumi na mbili na kujeruhi zaidi ya watu sitini katika mkoa wa Katavi ambapo julai 5, 2013 basi la kampuni ya Sumry lenye namba T909 AZT Nissan Diesel lilipinduka na kutumbukia mtoni ambapo watu tisa walifariki papo hapo na wengine watatu walifariki walipokuwa katika matibabu hospitali
Akitoa taarifa ya ajali iliyotokea mwishoni mwa wiki Afisa Mwandamizi wa SUMATRA mikoa ya Rukwa na katavi, David Chiragi alisema kuwa miongoni mwa sababu za kuibuka kwa ajali katika kampuni ya Sumry kunatokana na sababu mbali mbali za miundombinu, ugeni na uzoefu duni wa madereva na ubovu wa mabasi  na hivyo kushauri ufanyike ukaguzi wa mabasi ya kampuni ya Sumry chini ya usimamizi mkali wa jeshi la polisi kitengo cha usalama barabarani.
Aidha Chiragi alisema SUMATRA imeanzisha utaratibu wa kufuta leseni (Black List)  za udereva kwa madereva wanaosababisha ajali wanapokuwa barabarani ili kuwaondoa madaereva wazembe Katika tasnia ya udereva hapa nchini ikiwa ni sehemu ya kupunguza ajali nchini
Baadhi ya wananchi waliozungumza na waandishi wa habari mjini Mpanda walielezea namna serikali inavyokuwa bubu Katika kuishughulikia kampuni ya Sumry inayofanya biashara ya usafirishaji wa abiria Katika mikoa mbali mbali hapa nchini licha ya kupotea kwa maisha ya wananchi kila kukicha kutokana na ajali zinazojitokeza mara kwa mara.