KUANZIA TAREHE 1, DESEMBA 2013 TUTAKUWA TUNAPATIKANA KATIKA MTANDAO MPYA KUTOKANA NA MABORESHO YANAYOENDANA NA MABADILIKO YA KITEKNOLOJIA NA KULINDA USALAMA NA MAADILI YA KAZI TUNAZOZIWEKA KATIKA MEDIA HII. .....
MTANDAO MPYA WA KUPATA HABARI ZA UHAKIKA ZILIZOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA NI www.habarikatavi.wordpress.com
KATIKA MEDIA HII MPYA UTAPATA NAFASI YA KUTOA MAONI YAKO KWENYE UWANJA TULIOKUWEKEA TUNACHOOMBA NI KUZINGATIA MAADILI NA KUEPUKA USHABIKI WA AINA YOYOTE ILE
KAZI ZOTE ULIZOKUWA UNAZIPATA KATIKA MEDIA HII UTAZIPATA KATIKA MEDIA MPYA
MMILIKI WA MEDIA ANAOMBA RADHI KWA USUMBUFU UTAKAOJITOKEZA
Blogger
Sumia W.
For SMS
0767 51 99 89
Email: willysumia@gmail.com
Friday, November 29, 2013
Sunday, November 17, 2013
TMF YAANZA KUTOA MAFUNZO YA UBORESHAJI WA UANDISHI WA MITANDAO YA KIJAMII NCHINI TANZANIA
ukumbi wa Mvumi
BEDA MSIMBE AKIFAFANUA NAMNA MITANDAO INAVYOWEZA KULETA MATATIZO KWA BLOGGER
MR SAIMON M. MKINA LECTURING BLOGGERS AT DODOMA HOTEL
on progress class |
Leading Crue at Mvumi Hall Dodoma Hotel |
Ma bloga kutoka mikoa mbali mbali wakiwa katika darasa la mafunzo ya uboreshaji uandishi wa mitandao ya kijamii chini ya ufadhili wa TMF
WEKEZA KATIKA SHULE HII
Posted by
SUMIA
TITTLE No. 37755 Registered Mwanza
LAND plot No. 122
BLOCK 'P' low Density
Mbulu Kahama Urban Area
GURANTEE ; 33 yrs
MMILIKI; BERTHA MABULA KINUNGU
SIMU: +255756 01 83 36
KAMA UNAHITAJI WASILIANA NA MMILIKI WA SHULE: Bertha Mabula Kinungu wa S. L. P 34 Kahama; simu No. +255756 01 83 36
Email: willysumia@gmail.com
BEI NI NAFUU SANA
HALMASHAURI ZAAGIZWA KUJENGA MAKTABA ZAO
WAZIRI MKUU Mizengo Pinda amesema
kila Halmashauri hapa nchini inapaswa kuweka kwenye mpango wake wa maendeleo kifungu
cha ujenzi wa maktaba ya wilaya ili watu waweze kusoma na kujiendeleza kwa
urahisi.
Ametoa kauli hiyo jana jioni (Jumamosi, Novemba 16, 2013) wakati
akiwahutubia washiriki wa mahafali ya 19 ya Chuo cha Ukutubi
na Uhifadhi wa Nyaraka cha Bagamoyo yaliyofanyika
kwenye viwanja vya chuo hicho nje kidogo ya mji wa Bagamoyo.
Jumla ya wahitimu 749 walitunukiwa
vyeti kati yao 244 vikiwa ni vya stashahada na 505 ni vya astahada katika fani
za ukutubi na utunzaji nyaraka.
Alisema ukutubi ni mojawapo ya fani kongwe hapa duniani japo haiongelewi sana
hapa nchini. “Hili ni eneo linalomgusa kila mmoja wetu, kuanzia mtu wa kawaida
awe mkulima, mvuvi, seremala, mjasiriamali ama yeyote ambaye anahitaji taarifa
mbalimbali zimsaidie katika maendeleo yake. Hali kadhalika, mwanafunzi, msomi
na mwanataaluma yeyote hawezi kufikia upeo wa masomi na taaluma yake kama hakusoma
vitabu na machapisho yaliyoko katika maktaba ambavyo vinatunzwa mkutubi.
Alisema kati ya wilaya 133 zilizopo
hapa nchini, ni wilaya 19 tu ambazo zimejenga maktaba katika ngazi ya wilaya. “Hii
ni sawa na asilimia 14.2 tu ya wilaya zote. Upungufu huu unasababishwa na tatizo
la watu kutotambua umuhimu wa kuwa na maktaba na katika hili lawama ni lazima
wabebeshwe Wakurugenzi wa Halmashauri,” alisema.
Waziri Mkuu alisema katika ngazi ya
mikoa hali si mbaya kwani mikoa 22 kati ya 25 ya Tanzania Bara ina maktaba za
mkoa.
“Tunazo Halmashauri 167 lakini ni Halmashauri
19 tu ambazo zina maktaba... nitoe wito kwa wilaya
zote ambazo hazina maktaba zione umuhimu wa kuwa na maktaba zake. Tukifanikiwa kuwa
na maktaba katika kila mkoa na kila wilaya itatuwia rahisi kuisogeza huduma
hiyo katika ngazi ya kata ili iwe karibu zaidi na wananchi,” alisema.
Akisisitiza
umuhimu wa fani hiyo Waziri Mkuu alisema mahitaji ya wakutubi hapa nchini ni
makubwa kwani hapa nchini kuna shule za msingi zaidi ya 16,300 na shule za
sekondari zaidi ya 4,500 za Serikali na za binafsi.
“Tunawahitaji
zaidi hawa wakutubi katika shule zetu kwani wakiwepo kwenye shule zetu watakuwa
karibu na wanafunzi na wataweza kuwasaidia wanafunzi kupanua uelewa wao,”
alisisitiza.
Aliahidi
kufuatilia maombi ya bajeti ya maendeleo ya chuo ili kukisaidia chuo hicho kiwe
bora zaidi.
Mapema akitoa taarifa
ya chuo hicho, Mkuu wa Chuo hicho, Bw. Zuberi Khatibu alisema chuo hicho
kinakabiliwa na changamoto ya uhaba wa madarasa licha ya kuwa udahili umekuwa
ukiongezeka mwaka hadi mwaka.
“Mwaka 2007/2008
chuo kilidahili wanafunzi 100 lakini katika mwaka 2012/2013 tulidahili
wanafunzi 708 na mwaka huu wa masomo (2013/2014) tumedahili wanafunzi 821,”
alisema.
Naye Mwenyekiti
wa Baraza la Chuo hicho, Dk. Alli Mcharazo, alisema kabla chuo hicho
hakijaanzishwa hapa nchini, wanafunzi waliokuwa wakitaka kusomea masomo ya
ukutubi na uhifadhi nyaraka walilazimika kwenda Makerere, Uganda.
Alisema mbali ya
uwepo wa chuo hicho, changamoto kubwa inayowakabili ni ufinyu wa bajeti, uhaba
wa miundombinu hasa upungufu wa mabweni na madarasa kiasi kwamba wanalazimika
kuwa na shift mbili za masomo (asubuhi na jioni) hali ambayo inaathiri utoaji
wa elimu chuoni hapo.
Katika risala yao, wanafunzi wanaohitimu waliomba wapatiwe
ajira za moja kwa moja kama ilivyo kwa walimu au askari, pia waliomba maktaba
ya chuo hicho ipanuliwe kwa sababu ni ndogo na ikiwezekana chuo kiongezewe
kompyuta kwa sababu zilizopo hazitoshi wanafunzi wote kufanya mazoezi kwa
vitendo.
(mwisho)
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
S. L. P. 3021,
DAR ES SALAAM.
JUMAPILI, NOVEMBA 17, 2013Friday, November 15, 2013
HABARI YA KIMATAIFA
RAIS DKT KIKWETE NCHINI SRI LANKA NOVEMBER 14, 2013
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Rais wa Sri Lanka Mhe. Mahinda Rajapaksa alipomtembelea kwa mazungumzo kwenye jengo la Temple Trees jijijini Colombo leo Novemba 14, 2013 kabla ya ufunguzi rasmi wa mkutano wa wakuu wa nchi za jumuiya ya madola mwaka huu (CHOGM 2013)
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Rais wa Sri Lanka Mhe. Mahinda Rajapaksa
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisaini kitabu cha wageni nchini sri Lanka
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Rais wa Sri Lanka Mhe. Mahinda Rajapaksa pamoja na viongozi mbali mbali
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Rais wa Sri Lanka Mhe. Mahinda Rajapaksa katika mazungumzo yao leo (picha zote na Ikulu)
Thursday, November 14, 2013
MIUNDOMBINU MASHULENI SIYO RAFIKI KWA WALEMAVU
Katavi
KAMPUNI ya uwindaji ya Tanzania Big Game Safaries Ltd imekabidhi baiskeli ya walemavu kwa walemavu 150 walioko katika mkoa wa Katavi zenye thamani ya shilingi million 52.5 ikiwa ni mchango wao katika jamii kutokana na faida wanayopata katika shughuli za uwindaji na utalii mkoani KataviAkikabidhi vifaa hivyo kwa Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Mpanda, mwakilishi wa kampuni hiyo, Rose Bekker alisema Kampuni ya Big Game imekuwa ikitoa msaada kwa wana jamii mbali katika maeneo
wanayofanyia kazi za uwindaji kila mwaka tangu 2005 ambapo mpaka sasa kampuni hiyo imeshakabidhi baiskeli za walemavu za kisasa zipatazo elfu tatu katika maeneo mbali mbali hapa nchini
Alisema kampuni yake pia imekuwa ikiwekeza katika ujenzi wa madarasa, ujenzi wa makanisa, vifaa vya shule na misaada kwa walemavu kwa kushirikiana na asasi isiyo ya kiserikali ya Conservation Foundation
Trust Fund (CFT) ya jijini Arusha
Alisema taasisinyake inawasiliana na asasi ya Kimarekani ya Wheel Chair Foundation katika matengenezo ya baiskeli kwa ajili ya walemavu kwa gharama ya shilingi laki tatu na nusu (350,000/=)
Katika hotuba yake mgeni rasmi wa hafla hiyo fupi, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Mpanda, Enock Gwambasa alisema kuwa hivi sasa kumekuwa na tabia mbaya ya unyanyapaa kwa walemavu katika jamii hali inayosababisha baadhi ya walemavu kuishi kwa sononi kubwa
Aliwataka walemavu kujiona kuwa nao ni sehemu ya jamii na hivyo wana uwezo wa kuzalisha mali ndani ya jamii ikiwa watajengewa uwezo wa kufanya kazi hizo, wasibweteke washiriki kikamilifu katika shughuli za
kijamii kama vile kupiga vita ujangiri kwa kutoa taarifa serikalini za uwepo wa majangiri katika maeneo yao
Jumla ya walemavu 150 walikabidhiwa baiskeli zenye thamani ya shilingi laki tatu na nusu sawa gharama yote kufikia shilingi milioni 52.5 zote zikiwa zimetolewa na Tanzania Big Game Safaries kama mrejesho wa
faida kwa jamii inayozunguka maeneo wanayofanyia kazi zake.
Katika hali ya kusikitisha Mmoja wa waliopata msaada huo ambaye amemaliza kidato cha nne mwaka huu katika shule ya Sekondari ya Mwangaza, Kashindie Kisamvu licha ya kushukuru kwa msaada huo aliiomba serikali kuangali suala la miundombinu katika maeneo ya maofisini na madarasani kwani hakuna sehemu ya mlemavu kuingia
Alisema vyoo vya shule havimfai kabisa mwanafunzi mwenye ulemavu wa viungo alipokuwa akisoma shuleni Mwangaza alipobanwa na haja alikuwa akilazimika kuomba ruhusa kwenda nyumbani kwao kwa lengo la kujisaidia na kurudi tena shuleni hali iliyokuwa ikimsababishia kupoteza muda mwingi na vipindi vya masomo
“Nilikuwa Napata shida sana shuleni kwani madarasani hakuna sehemu ya kuingia kwa baiskeli, ofisini hakuna na vyooni nako hakuna pia sehemu ya kupita mlemavu, nilikuwa nikibanwa na haja nalazimika kuomba ruhusa kwenda nyumbani kujisaidia ndipo nirudi tena shuleni, nikuwa nachelewa vipindi vingi sana na nilikuwa naathirika sana kitaaluma” alisema
Kashindie
Subscribe to:
Posts (Atom)