CHAMA CHA MAPINDUZI CHAELEZA MAFANIKIO KATIKA ZIARA ZAKE KANDA NYANDA ZA JUU KUSINI
CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimesema ziara ambazo zimekuwa zikifanywa na Katibu
Mkuu wake, Abdulrahman Kinana, zimeanza kuzaa matunda hasa upande wa utatuzi wa
kero zinazowakabili wananchi.
Hayo
yamesemwa na Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye wakati akitangaza
kuanza kwa ziara ya Kinana ya siku 22, katika mikoa ya mikoa ya Ruvuma na Mbeya
itakayoanza, Novemba 15, 2013, ambayo ni mwendelezo wa ziara za kuimarisha
chama, kukagua utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 2010,
kusikiliza kero za wananchi na kushirikiana nao kuzitafutia ufumbuzi.
Nape
alisema miongoni mwa mafanikio yanayoonekana kutokea ni mwitikio ulionyeshwa na
serikali katika kutekeleza maagizo yaliyotolewa kupitia ziara zilizopita za
Kinana, na vikao vya Chama kuhusu kushughulikiwa kwa kero au hoja mbalimbali.
Alisema,
baadhi ya kero ambazo zimeshuhudiwa zikichukuliwa hatua na serikali ni pamoja na
kufufua viwanda nchini.
Nape
alisema baada ya ziara kadhaa za Katibu Mkuu, uchambuzi na vikao kadhaa vya
CCM, Chama kiligundua kuwa viwanda vingi vilivyo binafsishwa havifanyi kazi
kama ilivyokusudiwa na vingine kufungwa kabisa na kugeuzwamagodauni.
Alisema
pamoja na athari kubwa kwa uchumi wa nch, kufungwa na kutofanya vizuri kwa
viwanda hivyo kumechangia sana tatizo la ajira kuwa kubwa, hivyo Chama
kiliagiza serikali kufanya tathimini ya viwanda vyote vilivyo binafsishwa na
hali yake kwasasa na vile visivyofanya kazi kama ilivyokusudiwa vichukuliwe na
serikali na kutafuta njia sahihi ya kuvifufua upya.
Nape
alisema, baada ya chama kuagiza kupitia ziara za Kinana na vikao vya Chama,
serikali imechukua hatua kadhaa katika hili, ikiwemo kufanya tathimini na
mapendekezo kadhaa yamewasilishwa na timu iliyoundwa na serikali kwa serikali
kwa ajili ya kufanyia uamuzi na kuchukua hatua.
Alisema,
CCM inatambua kwamba zipo hatua kadhaa ambazo imechukuliwa na serikali katika
jitihada za kufufua viwanda vya kubangua korosho kama sehemu ya utatuzi wa
tatizo la soko na zao la korosho na kwamba na sasa serikali ipo katika
hatua kadhaa za kushughulikia viwanda vingine nchini.
Nape
alisema, kutokana na mwitikio huo, CCM inaipongeza serikali kwa hatua hizo
muhimu za kutekeleza agizo la Chama, ingawa pamoja na pongezi hizo CCM imeitaka
serikali ikamilishe kazi hiyo mapema iwezekanavyo ili nchi ifaidike na ufufuaji
huo wa viwanda nchini.
Changamoto
kwa wakulima wa pamba
Nape
alisema, katika ziara ya Katibu Mkuu mikoa kadhaa ya kanda ya ziwa, alitumia
muda mrefu kujifunza na kuzungumza na wakulima wa zao la pamba wa mikoa hiyo.
Pamoja na tatizo kubwa la soko na bei ya pamba, pamekuwa na changamoto kubwa ya mfumo unaosimamia zao la pamba ikiwemo upatikanaji wa pembejeo.
Pamoja na tatizo kubwa la soko na bei ya pamba, pamekuwa na changamoto kubwa ya mfumo unaosimamia zao la pamba ikiwemo upatikanaji wa pembejeo.
Alisema,
kufuatia ziara hiyo, hatua kadhaa zimeanza kuchukuliwa na serikali ikiwa ni
pamoja na kuvutia uwekezaji kwenye viwanda vya kutengeneza nyuzi, nguo na
kukamua mafuta ya pamba. Tulishuhudia ujenzi wa viwanda kadhaa mjini Shinyanga,
vingi vikijengwa na wawekezaji kutoka China.
"Lakini
wakati wa bunge la juzi, serikali imeamua kutoa ruzuku ya asilimia hamsini kwa
mbegu bora za pamba ili kuwawezesha wakulima kumudu bei ya mbegu hizo na hivyo
kuboresha zao la pamba nchini na maisha ya wakulima kuwa bora zaidi",
alisema Nape
Alisema
Katika suala hilo la mbegu bora na kilimo cha mkataba CCM inaitaka serikali na
hasa wakuu wa wilaya na mkoa kuacha mara moja kutumia nguvu kuwalazimisha
wakulima kulima kwa mkataba na kutumia mbegu bora badala yake wawaelimishe na
kuwashawishi badala ya kutumia nguvu.
"Tunaipongeza
serikali kwa kuanza kuchukua hatua za kutekeleza baadhi ya mapendekezo ya CCM
ya namna ya kutatua matatizo yanayowakabili wakulima wa pamba nchini. Tunaitaka
serikali kuongeza kasi ya utatuaji wa changamoto hizo ili wakulima wa pamba
wafaidike na uchumi wa nchi kukua kwa kasi nzuri", alisema Nape.
Migogoro
ya wakulima na wafugaji na hifadhi juu ya matumizi ya aridhi.
Kuhusu
suala la migogoro ya wakulima na wafugaji na hifadhi juu ya matumizi ya ardhi,
Nape alisema katika ziara mbalimbali za katibu mkuu kwenye mikoa kama ya
Morogoro, Njombe, Simiyu, Mara alishuhudia migogoro mingi sana juu ya wakulima,
wafugaji na hifadhi mbalimbali nchini ambavyo vimegharimu sana maisha ya
watu na mali zao na hata uchumi wa nchi.
Nape
alisema baada ya Kinana kutoa maagizi migogoro hiyo kushughulikiwa mapema na
kupata ufumbuzi wa kudumu, Chama kinalipongeza bunge na hasa wabunge wa CCM na
serikali yake kwa uamuzi wa kuunda Kamati teule ya bunge kuchunguza na kutoa
mapendekezo ya hatua kadhaa za kuchukuliwa katika kufikia suluhisho la kudumu
kwa migogoro hiyo.
Nape
alisema CCM inawaomba wananchi watoe ushirikiano wa kutosha kwa kamati teule ya
bunge ili kazi hii ya kamati iwe na matokeo mazuri yatakayosaidia kumaliza
tatizo hilo nchini.
No comments:
Post a Comment